Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1403 | 1404 | (Page 1405) | 1406 | 1407 | .... | 3278 | newer

  0 0
 • 10/23/16--14:03: Mzungu Kichaa acharuka!
 • Mzungu Kichaa is currently doing a tour in Europe with his Tanzanian band Bongo Beat. Today he is releasing Akili Mwili Roho as audio and video. The video was shot on location in Dar es Salaam at the SOS children’s villages. Mzungu Kichaa has been appointed goodwill ambassador for the organisation.
  Mzungu Kichaa produced the song and plays the bass and guitar on the track. Tanzanias very own heavyweight producer P Funk Majani did the vocal production and mix.The song is also being released in English and Danish.
  Download (MP3) via mkitohttp://bit.ly/AkiliMwiliRoho 
  For more information
  Mzungu Kichaa

  Twitter: @mzungukichaa
  Instagram: @mzungukichaa
  Snapchat: KichaaMusic


  0 0


  SIMU.TV: Halmashauri ya Manspaa ya Morogoro imeendesha zoezi la kubomoa vibanda vya wafanyabiashara katika soko la Manzese huku wafanyabiashara wakilalamikia zoezi hilo. https://youtu.be/j7MWjr4bPeM

  SIMU.TV: Rushwa ,viwango vya kodi na usimamizi wa kodi vimeonekana kuwa changamoto inayokwamisha mazingira ya uwekezaji nchini. https://youtu.be/P--psebW9Do

  SIMU.TV: Waziri wa maliasili na utalii Prof Jumanne Magembe amesema serikali bado inaongeza juhudi katika kupambana na vitendo vya ujangili nchini.https://youtu.be/FGS4T460Dqg

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Tabora ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo kuwasaka na kuwakamata wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya mkoani humo.https://youtu.be/eycYTTVXOtM

  SIMU.TV: Wadau wa maji katika mji mdogo wa Utete mkoani Pwani wamekutana  kujadili na kupitisha gharama mpya za huduma ya maji kwa wakazi wa Utete.https://youtu.be/__RQml9h-fU

  SIMU.TV: Hospitali ya taasisi ya saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam imepata msaada wa vifaa vya usafi  na vifaa tiba kutoka kwa wakadiariaji majenzi nchini.https://youtu.be/VJu_pYu28oc

  SIMU.TV: Idara ya makumbusho ya taifa imeanza jitihada za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo kandokando ya bahari ya Hindi wilayani Kilwa. https://youtu.be/SJY81aCLhlQ

  SIMU.TV: Timu ya Simba imeendela kuukimbiza ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Toto African mabao matatu kwa bila leo. https://youtu.be/_I9UHFDhTwI

  SIMU.TV: Mashabiki wa mpira wa miguu mkoani Mbeya wameaswa kuziunga mkono timu za jiji hilo ili ziweze kufanya vizuri. https://youtu.be/oCZS8bMJ07o

  SIMU.TV: Mbio za ubingwa kwa timu ya Manchester City zimeonekana kupungua kasi baada ya kutoshana nguvu na Southampton leo kwa bao moja kwa moja.https://youtu.be/qEfE5ZC_kvQ

  Timu ya Simba imeendelea kujichimbia kileleni katika kuutafuta ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuichapa Toto African Mabao matatu kwa bila.https://youtu.be/_cfoWwy6RXk  

  SIMU.TV: Klabu ya Gofu ya jeshi la wananchi wa Tanzania imetamba kwa kuibuka na ushindi katika mashindano ya PWC yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.https://youtu.be/wZo4YZ02Lf0

  SIMU.TV: Mkuu wa shule ya sekondari ya White lake amesema wamejipanga kujenga viwanja vya michezo yote shuleni hapo  ili kukuza michezo kwa wanafunzi.https://youtu.be/amGr0kiFmcI
  SIMU.TV: Klabu ya Chelsea imeibuka na ushindi mnono wa magoli manne kwa bila dhidi ya klabu ya Manchester United. https://youtu.be/xW0iqFjcOS4

  SIMU.TV: Waziri January Makamba, amewataka wananchi kupanda kwa ajili ya kuni na biashara ili kupunguza ongezeko la ukataji hovyo misitu; https://youtu.be/nLmV9AdXlbw

  SIMU.TV: Watendaji wa serikali wilayani Simanjiro wameagizwa kukamata mifugo ya wafugaji wasiotaka kushiriki katika shughuli za maendeleo; https://youtu.be/1PRrGLI29WA

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amepokea msaada wa mabati 500 na mifuko 500 ya saruji kwa ajili kufanyia ukarabati wa miundombinu ya Elimu na Afya;https://youtu.be/vausceJbByw

  SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga, amewataka watumishi wilayani humo kuwatumikia wananchi wao kwa kuzingatia sheria zilizopo;https://youtu.be/PpQC1c_nb74

  SIMU.TV: Fuatilia mkasa wa Emmaculate Charles aliyepatwa na mkasa wa kupooza miguu na kushindwa kutimiza ndoto yake ya kuwa Daktari; https://youtu.be/XqFwdTAs5Mc


  0 0  Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohammed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
  Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohammed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake,Mfalme Mohammed VI kutoka Taifa la Morocco wakisimama pamoja wakati wa nyimbo za Taifa na mizinga 21 ikipigwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar jioni hii.Mfalme huyo amewasili jioni ya leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,aidha imeelezwa kuwa Mfalme huyo aliyekuja na ujumbe wa watu takribani 1000,mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu,atakuwa na siku nyingine tano za mapumziko hapa nchini ambapo atatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio na utalii nchini Tanzania.
  Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara waliotangulia kabla ya kutua kwa Mfalme Mohammed VI wa Morocco,aliyewasili jioni ya leo na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli na mamia ya wananchi.

  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Margareth Lwekama katika ibada ya kumuombea marehemu iyoyofanyia kwenye Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Oktoba 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Usisahau kuhusu Show ya Usiku wa Mshike Mshike na Malkia  wa taarabu Afrika Mashariki na Kati Khadija Omar kopa iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.
  Ni Alhamisi wiki hii tarehe 27.10.2016 ndani ya kiwanja cha nyumbani, Villa Park Resort, kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa tano usiku na shilingi 10,000 baada ya saa tano usiku.
  Pia watatambulishwa watangazaji wa Lake Fm wakiongozwa na Aisha BBM anayetangaza kipindi cha Mshike Mshike jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa saba mchana, Ma'Djz wa Lake Fm pamoja na wananzengo wengine wanaoendelea kuhakikisha redio hiyo inazidi kupenya Jijini Mwanza.
  Bonyeza HAPA Kujua Zaidi
  Malikia wa taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Kopa.

  0 0

  Balozi wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni amemhakikishia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa nchi yake itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri na ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

  Balozi huyo wa Italia hapa nchini ametoa kauli hiyo leo 24-Okt-2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es Salaam.Balozi huyo Roberto Mengoni ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini.

  Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati ya Italia na Tanzania.

  Amesisitiza kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kupokea mawazo mazuri ya kimaendeleo kutoka kwa Serikali ya Italia yatakayosaidia kujenga na kuimarisha ustawi mzuri katika jamii hapa nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (Watatu kushoto) akishikana mikono kuonyesha mshikamano na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Song Tao (wanne kushoto), baada ya kuwawakilisha Makatibu Wakuu hao katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya CPC, Liu Yunshan. Kutoka kushoto ni Pedro Sebastiao wa MPLA (Angola, Elisau Joaquim wa FRELIMO (Msumbiji), Waziri wa Mambo ya Nje katika Chama cha Kikomunisti cha China, Song Tao, Gwede Manlashe wa ANC (Afrika Kusini), Nangolo Mbumba wa SWAPO (Namibia), Ignatius Chembo wa ZANU-PF (Zimbabwe). PICHA ZOTE NA OFISIYA KATIBU MKUU WA CCM .

  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Chama Cha kikomunisti cha China (CPC) Ndugu Liu Yunshan, mjini Chongqing, nchini China hivi karibuni. Katika Mazungumzo hayo, Ndugu Kinana aliwawakilisha Makatibu Wakuu kutoka vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambao alifuatana nao nchini China. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (Watatu kushoto) akiwa katika kikao na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Song Tao (wanne kushoto), baada ya kuwawakilisha Makatibu Wakuu hao katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya CPC, Liu Yunshan. Kutoka kushoto ni Pedro Sebastiao wa MPLA (Angola, Elisau Joaquim wa FRELIMO (Msumbiji), Waziri wa Mambo ya Nje katika Chama cha Kikomunisti cha China, Song Tao, Gwede Manlashe wa ANC (Afrika Kusini), Nangolo Mbumba wa SWAPO (Namibia), Ignatius Chembo wa ZANU-PF (Zimbabwe).

  0 0

  Mwenyekiti wa Kampuni ya S & E GROUP LTD, Elihuruma Ngowi akitoa maelezo kwa Mchungaji Kiongozi wa K.K.K.T. Usharika wa Mbezi Beach, Allen Mbiso wakati wa ufunguzi wa kampuni za S & E GROUP LTD pamoja na S & E PHOTOS & VIDEO SERVICES LTD hivi karibuni.
  Mchungaji Kiongozi wa K.K.K.T. Usharika wa Mbezi Beach, Mch. Allen A. Mbiso (kulia) akifanya maombi na hatimaye kufungua rasmi ofisi za Kampuni ya S & E GROUP LTD pamoja na Kampuni ya S & E PHOTOS & VIDEO SERVICES LTD hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni hizo, Elihuruma Ngowi.


  0 0
 • 10/24/16--05:55: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

  Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera.

  MARADHI ya vichwa vikubwa na migongo wazi kwa watoto yanatibika endapo wazazi watachukua tahadhali mapema ya kumpeleka mtoto hospitali kwaajili ya matibabu.

  Dk Hamis Shaabani daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu kutoka Taasisi ya mifupa(MOI) ameyasema hayo leo wakati wa zoezi la ufungaji upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi katika hospital ya Mkoa wa Kagera.Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

  Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa."Kwa wale wanao zaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba virutubisho hivo vinapatikana kwenye matunda,mboga za majani,mayai na vyakula vyote vyenye protini,pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao,"alisema

  Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kagera wameshawafanyia upasuaji jumla ya watoto saba wenye vichwa vikubwa na mmoja wa mgongo wazi.Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.

  Joviti Mchuruza akiongea kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji aliwashukuru timu nzima ya madaktari hao pamoja na Taasisi ya GSM kwa msaada huo wa matibabu waliowapatia wa watoto wao bure.Aliiomba jamii kuacha kuhusisha maradhi hayo na mila potofu za imani za kishirikina au mikosi kwenye familia hali inayofanya akina mama au baba kutelekezewa watoto.

  Aliwaomba pia wataalam hao wasogeze huduma hiyo karibu na jamii hasa maeneo ya vijijini ambapo wapo watoto wengi wenye maradhi hayo wanateseka na hawana msaada."Nawaomba wazazi wenzangu hasa akinamama sababu sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaoweza kugundua mabadiliko ya mtoto pia tusisikilize maneno ya dhihaka ya watu wa pembeni maradha haya yanatibika kabisa"alisema mzazi huyo

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu aliwashukuru madaktari pamoja na shirika la GSM Foundation kwa udhamini huo wa matibabu bure kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.Pia aliwataka wazazi wenye watoto wenye maradhi hayo wasione aibu kuwapeleka hospitali ili waweze kupatiwa matibabu bure.

  Jovita Mchuruza akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)baada ya kutelekezewa watoto watano na mkewe wenye vichwa vikubwa,wanaondelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kagera.

  Timu ya madaktari kutoka Taasisi ya mifupa(MOI)pamoja na wafadhili wao GSM Foundition wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakimpa taarifa juu ya upasuaji wa vichwa vikubwa na mgongo wazi jwa watoto walioufanya katika Mkoa huo kwa muda wa siku tatu.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimpa pole mmoja wa  watoto wenye maradhi ya kichwa kikubwa aliyelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari toka MOI kwa ufadhili wa Taasisi ya GSM Foundation 
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimpa pole mmoja wa  watoto wenye maradhi ya kichwa kikubwa aliyelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari toka MOI kwa ufadhili wa Taasisi ya GSM Foundation.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo.

  SERIKALI imevitaka wadau wa vyombo vya habari nchini kuacha kulalamika na badala yake waendelee kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria kwa vyombo vya habari ambao unatarajiwa kuwasilishwaa katika Bunge lijalo mjini Dodoma.

  Akizungumza katika wakati tofauti wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi za Vyombo vya habari nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO), Hassan Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa na Bunge ili uweze kuwa sheria kamili na hatimaye kuifanya tansia ya habari kuzidi kuheshimika.

  Mkurugenzi Abbas alisema tangu muswada huo uliposomwa kwa mara ya kwanza Bungeni, mwezi Septemba mwaka huu, wadau wa tasnia ya habari nchini ikiwemo Wahariri na waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele kupingana katika mitandao ya kijamii badala ya kutoa maoni yao katika mamlaka zinazohusika.

  “Ni aibu kwa maoni ya muswada huu yanayohusu tasnia ya habari kutolewa na watu ambao hawana taaluma ya habari, hivyo tukiwa kama wanataaluma ni vyema tujitokeze kwa wingi kutoa maoni kifungu kwa kifungu ili kuweza kuboresha muswada” alisema Mkurugenzi Abbas.

  Aliongeza kuwa haitopendeza kwa muswada huo kuendelea kutolewa maoni na wananchi wengine na wadau wa muswada kukacha kutoa maoni yao, na hivyo kusababisha muswada huo kuandikwa na watu walio nje ya tasnia ya habari.

  Abbas alisema, muswada huo utakusudia kuiongezea nguvu tasnia ya habari kwa kuweka ikiwemo suala zima la kuzingatia sheria na mipaka ya nchi katika utoaji wa habari na taarifa maalum za Serikali kwa umma kwa kuzingatia ukomo wa kimataifa.

  “Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1948, pamoja na kuzungumzia kuhusu haki ya kupata taarifa lakini pia limeanisha sheria mbalimbali ambazo hazina budi kuheshimiwa, na sheria hizo ni pamoja na sheria za ulinzi na usalama” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

  Akifafanua zaidi alisema taaluma ya habari ni tasnia muhimu katika maendeleo ya taifa ila kwa upande mwingine inaweza kuharibu maendeleo kwa njia moja au nyingine na hivyo kuwataka wadau wa habari kujitokeza kutoa maoni kwa kujenga hoja za msingi ili kuboresha muswada badala ya kulalamika.

  Aidha kwa upande mwingine, Abbas alisema Ofisi yake ni mlezi na mratibu wa vyombo vya habari na hawana budi kuwasiliana naye pindi wanapopata changamoto mbalimbali ikiwemo utoaji na upatikanaji wa taarifa za Serikali katika Wizara, Taasisi, Idara, Mikoa na halmashauri nchini.

  Pia alisema zipo taarifa ambazo zinahitaji kufanyiwa uhakiki ikiwemo ufundi na takwimu, na hivyo aliwataka waandishi wa habari kuwa wavumilivu pale wanapohitaji taarifa hizo kutoka kwa maafisa habari wa Wizara au Taasisi husika.

  Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Majira, Imma Mbughuni alisema chombo hicho kimejipanga kutoa maoni yao kuhusu muswada huo na mara baada ya kumaliza wanatarajia kuwasilisha katika kamati ya kudumu ya Bunge.

  Naye Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa alisema chombo chao pia kimekusudia kuupitia muswada huo ili kutoa maoni yao na baadae kuyawasilisha katika kamati husika.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kulia) akizungumza jambo na Mwandishi Mwadamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Mashaka Mgeta (kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhariri Mtendaji Anicetus Mwesa.

  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kushoto), akizungumza na Wahariri Waandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa (katikati), Exuper Kachenje na Kizito Noya wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kushoto), akizungumza na Wahariri Waandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Joseph Lugendo (kushoto), na Joseph Kulngwa wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Huenda ukiambiwa utaje wanyama hatari sana duniani utakimbilia kwa simba ama chui kwa haraka......
   Nyegere ama Honey badger ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi duniani, kwa tarifa yako tu hata nyoka, chui na simba huufyata kwa Nyegere ..............Nyegere ndio mmoja kati ya wanyama wasioogopa kitu chochote duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda. Na yeye hategemei mob/kuchangia mande kwani ni mmoja wa wanyama wanaotembea kivyake wakati wote isipokuwa wakati wa kupandana tu.

  1. Nyegere ana gozi gumu zaidi kuliko haywani wte wa mwituni kiasi ambacho ni ngumu sana kumuua kwa mshale au hata panga, gozi la mnyama huyu linafanua sindano ya nyuki kudunda tu....anasaidiwa kucha zake, ndefu na ngumu awapo katika hatari ya kushambuliwa ngozi yake huwa ngumu na kukakamaa zaidi ("defensive mechanism).
  2. Nyegere hula vyote iwe nyama iwe majani na hii imemfanya kustahili shuruba za mazingira yote iwe nyikani ama mwituni. Chakula chake kikubwa ni asali, yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula.

  Nyegere hula nyoka wa aina yoyote, ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi ingawa wapo nyoka wenye sumu ambao Nyegere akiwala anaweza kuzimia kwa msaa kadhaa kutokana na ukali wa sumu ambayo inakuua wewe kwa dakika tu.

  3.Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa dunianikwani ana wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari, maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.......Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume, mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike, hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
  4. Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere, anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke, mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii
  Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...

  Yasemekana huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.

  Geofrey Chambua kutoka vyanzo mbalimbali 

  0 0

  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, ameiagiza Kampuni ya Serengeti Limited kukamilisha mradi wa uchimbaji visima 20 vya maji vya Kimbiji na Mpera kwa muda waliokubaliana, vinginevyo itabidi ilipe gharama za ucheleweshaji kama itashindwa. 


  Alisema serikali haitavumilia kuona mradi huo wenye manufaa makubwa kwa Jiji la Dar es Salaam unachelewa kukamilika, kwa sababu unahitajika kuhudumia wananchi kwa kuwapatia huduma ya majisafi na salama. 

  Waziri Lwenge alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki, baada ya kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo mkubwa uliopo Kigamboni, Dar es Salaam ulioanza kutekelezwa tangu mwezi Machi, 2013. 

  Alisema mradi huo utagaharimu zaidi ya Sh. bilioni 18, na serikali imeshalipa kwa mkandarasi zaidi ya Sh. bilioni 13, na ulitegemewa kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu, lakini utachelewa kutokana na changamoto mbalimbali alizotaja mkandarasi huyo. 

  “Pamoja na changamoto alizozitaja mkandarasi, hatutakubali utekelezaji wa mradi huu uendelee kuchelewa, mkandarasi inabidi aongeze kasi ili tumalize kero ya wananchi wa Kigamboni, Mkuranga na Dar es Salaam yote, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri mradi huu, hatutavumilia uchelewaji zaidi na itabidi walipie gharama endapo watashindwa”, alisema Inj. Lwenge. 

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akipokea maelezo ya ramani ya mradi wa uchimbaji visima vya Kimbiji na Mpera kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa mradi, Injinia Charles Kaaya. 
  Mashine ikiendelea na kazi ya uchimbaji kisima Kimbiji. 

  Baadhi ya mafundi wakiwa eneo la kazi Kimbiji. 
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Serengeti, Mehrdad Talebi (kushoto), Mhandisi Mkazi wa mradi, Charles Kaaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Archad Mutalemwa na Mkurugenzi wa Maji Mijini, Mhandisi Dkt. Justus Rwetabula.


  0 0

  1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakati wa  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja
  2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakati wa  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja
  3
  Waziri wa Wizara wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid  Mohamed (katikati) akisoma taarifa ya  utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao  cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo   Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Lulu Msham Abdalla.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda amezindua mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi ambayo yalianza tarehe 17 Oktoba mwaka huu chuoni Changanyikeni jijini Dar es Salaam. 

   Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Prof. Ngalinda amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa nia ya kumpatia mshiriki ujuzi katika ukusanyaji takwimu kwa ajili ya kuzichakata na kuwa takwimu rasmi.

  “Washiriki hawa watafundishwa mbinu shirikishi, utatuzi wa matatizo mbalimbali wakati wa ukusanyaji takwimu, sensa na viwango vya tafiti mbalimbali, utunzaji wa Vifaa vya ukusanyaji takwimu kama vile simu za mkononi na kumpyuta mpakato pamoja na kubadilisha madodoso ya kawaida na kuwa ya kisasa”, amesema Prof. Ngalinda.

  Akizungumzia malengo ya mafunzo hayo Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa chuoni hapo Dkt. Frank Mkumbo amesema lengo ni kuwawezesha wakusanyaji takwimu kukusanya takwimu halisi na zenye ubora kwa ajili ya kupanga mipango mbalimbali ya Maendeleo.

  “Lengo kuu la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa wakusanyaji takwimu rasmi wanakuwa na weledi wa kutosha katika kukusanya takwimu bora na zenye tija kwa taifa” amefafanua Dkt. Mkumbo.

  Jumla ya washiriki 110 wamejiunga na mafunzo hayo maalumu ya muda wa miezi miwili kwa awamu ya kwanza ambayo yatamalizika mwezi Disemba, 2016 na watakaomaliza na kufaulu watapatiwa cheti cha Ukusanyaji Takwimu. Awamu ya pili ya mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu na kumalizika Januari, 2017.
  Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Frank Mkumbo akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0

  Pamela Mollel,Arusha


  Watanzania wametakiwa kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya machafuko. 

  Wito huo umetolewa jana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Ukombozi hapa nchini, Nabii B. G Malisa wakati alipokuwa akihubiri neno la Mungu katika viwanja vya reli jijini Arusha na kuhudhuriwa na maelfu ya watu

  Nabii Malisa alisema kwamba watanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanaombea amani ya nchi iendelee kutawala kwa kuwa bila amani hakuna kitu kitakachoweza kuendelea katika nchi hii.

  Aidha alisema kuwa amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika nchi mbalimbali duniani na kushuhudia hali ya usalama ikiwa tete ambapo askari wamekuwa wakitembea mitaani huku wameshika silaha za moto. 

  "Hivi karibuni nilikuwa Nigeria wakati nashuka uwanja wa ndege nilipokelewa na askari wenye silaha za moto nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu amani tuliyonayo hapa Tanzania "alisema Malisa 

  Hatahivyo, alitoa wito kwa serikali kuunga mkono juhudi za viongozi mbalimbali wa dini hapa nchini katika kuwasaidia vijana na kusema viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa katika kuwainua watu kiuchumi na kuwaepusha na vitendo viovu. 

  Awali akizungumza na waandishi wa habari mchungaji wa kanisa la Ukombozi tawi la Arusha Mchungaji Ushindi alisema kwamba mhubiri huyo atakwenda kufanya huduma ya maombezi mkoani Arusha kwa siku nane na kuwataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi. 

  Mchungaji Ushindi alisema kuwa wakazi wa jiji la Arusha wamepata neema kubwa ya kupata neno la Mungu kupitia mkutano huo wa maombezi .
  Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa akihubiri katika mkutano mkubwa wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha ambapo amewatakaWatanzaniakudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya machafuko. (Picha na Pamela Mollel).
  Kulia ni mama mchungaji Grace Mshindi wa kanisa la ukombozi tawi la Arusha akiwa anazungumza na watu waliojitokeza katika mkutano huo wa maombezi na kupokea uponyaji.
  .Watu mbalimbali waliojitokeza katika mkutano wa Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa unaofanyika katika viwanja vya reli jijini Arusha. 
  Taswira ya watu waliojitokeza katika mkutano huo .


  0 0

  Na: Frank Shija, MAELEZO. 

  UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) takiwa kuhakikisha Chuo hicho kinaendelea kuwa kiongozi miongoni mwa Vyuo Vikuu nchini. 

  Ushauri huo umetolewa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akifungua maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. 

  “Hiki ndicho Chuo kiongozi kati ya Vyuo Vikuu vyote hapa nchini, mnatakiwa kuhakikisha kinaendelea kuwa kiongozi huku Vyuo vingine vikifuatia”. Alisema Dkt. Kikwete 

  Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Lwekaza Mukandara amesema kuwa pamoja na changamoto zinazo kikabili chuo hicho wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kusaidia katika kuleta maendeleo ya chuo hicho. 

  Alisema kuwa baadhi ya changamoto zimetatuliwa kwa pamoja kati ya Serikali na wahisani ambapo alisema kuwa ujenzi wa kumbi mpya za mihadhara, Maabara za Kisasa na jengo la malazi,pamoja na ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea katika Kampasi ya Julius K. Nyerere ambayo itakuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 4000 mara itakapo kamilika. 

  Akiwasilisha mada juu ya “hali ya Taaluma Barani Afrika katika Muktadha wa Kimataifa” Mhadhiri wa Heshima kutoka nchini Nigeria, Profesa Tade Aina amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja kati ya Vyuo Vikuu mahiri barani Afrika ambapo kimetoa mchango mkubwa kwa ukombozi wa nchi nyingi za bara hili. 
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na washiriki wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam. 
  Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika muktadha wa Kimataifa wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya washiriki wa kongamano maalum la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria wakati akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika muktadha wa Kimataifa mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam. 
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) wakati wa kongamano la  kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema hii leo Chuoni hapo, katikati ni Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria. 
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wakuu wa Vitivo wa Chuo hicho wakati wa kongamano la kusherehekea kutimiza miaka 55 toka kuanzishwa kwa chuo hicho. 

  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo .

  0 0

  MKUTANO wa Tano wa Ushirikiano kati ya Nchi za Kiafrika na Korea Kusini (Korea-Africa Economic Cooperation (KOAFEC), Umefunguliwa leo Jijini Seoul, Korea Kusini, huku agenda kubwa ikiwa ni kuzungumzia namna nchi za Kiafrika zinavyoweza kutumia kilimo katika muktadha wa maendeleo ya viwanda ili ziweze kujikwamua haraka kiuchumi.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, anawakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) katika mkutano huo unahusisha nchi 54 za kiafrika na nchi ya Korea Kusini.

  Dkt. Mpango ameuelezea mkutano huo ulioandaliwa na Serikali ya Korea Kusini kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya EXIM ya nchini humo, kwamba utaleta mapinduzi makubwa katika nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kilimo, rasilimali watu na teknolojia ya habari na Mawasiliano-TEHAMA.

  Amesema kuwa nchi ya Korea Kusini ilipata uhuru mwaka mmoja na nchi ya Ghana, Mwaka 1954 miaka michache kabla ya Tanzania Bara kupata uhuru wake, lakini imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kuwa moja kati ya nchi za ulimwengu wa kwanza kiuchumi, lakini Ghana na Tanzania bado ni nchi masikini.“Ni jambo zuri kwamba tuimarishe ushirikiano na Korea Kusini ili njia walizotumia kupiga hatua kubwa kimaendeleo, na sisi tuweze kujifunza kwa haraka” alifafanua Dkt. Mpango

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.


  Na George Binagi-GB Pazzo

  "Hii mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni dili, hivyo haitambuliki kwa sasa, kwanza imesababisha migogoro mingi kwa wananchi ikiwemo uuzaji wa viwanja kiholela". Amesisitiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.Ameshikilia msimamo wake kwamba mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza haitambuliki kama awali alivyosema kwamba waikabidhi ofisini kwake.

  Leo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutorudisha mihuri hiyo huku wakitishia kutoshirikiana na Watendaji Jijini Mwanza.Juzi jumamosi Wenyeviti 174 wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza, walivunja kikao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, baada ya Mkurugenzi huyo kuwataka kukabidhi mihuri yao.

  #Lakefm #BinagiBlog #BMG #Mwanza

older | 1 | .... | 1403 | 1404 | (Page 1405) | 1406 | 1407 | .... | 3278 | newer