Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

MPAMBANO WA MISS TALENT 2016 JINSI ULIVYOFANA, MSHIRIKI WA MISS TANZANIA, 2016 NO. 20 AIBUKA KIDEDE.

$
0
0
Miss Talent 2016 ambaye ni Mshiriki wa Miss Tanzania 2016 namba 20 ameshika nafasi ya Kwanza katika mpambano wa Kusaka Vipaji kwa washiriki wa Miss Tanzania 2016 uliofanyika Jembe Beach jijini Mwanza leo. Mshindi huyo wa Miss Talent 2016 amecheza ngoma ya asili.
Top 5 Miss Talent 2016 wakiwa wamepozi mara baada ya kushinda nafasi tano Bora ya Miss Talent 2016.


Mamiss Tanzania 2016 wakionesha Vipaji vyao wakicheza  katika hafla ya Kutafuta Miss Talent 2016 leo jijini Mwanza.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii Mwanza.




VICHWA VYA HABARI YA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 23,2016

WAZIRI MAKAMBA AKATAZA UCHEPUSHAJI WA VYANZA VYA MAJI

$
0
0

Na Lulu Mussa-Songwe

Wakazi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira nchini.

Akiwa katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, na haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha wanambaini mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya Sheria.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa na uvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi za kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia kutumika mamlaka ya Dola. “Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya Maji na kuwabembeleza watoke” Makamba alilisitiza.

Waziri Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka zilizopo, ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo waondolewe kwa nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha ainishwa. Pia Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo za Mazingira za Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi ya Mazingira Nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata ya Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na kuwasisitizia, kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa Vyanzo vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.

Pia Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima kilimo cha Matuta ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika miinuko. Aidha Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo za ujenzi wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.

Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na binadamu, pichani ni Mto Kalembo uliopo katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje uliochepushwa kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kutafuta wahusika na kuwafikishwa kwenye Vyombo vya dola.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwa wananchi mara baada ya kuwapa fursa ya kuuliza maswali katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Lubada Wilayani Ileje. Kushoto ni Bw. Stanford Kibona aliyeuliza swali.

DC WA KILWA,MH.NGUBIAGAI AWAPA SIKU 14 WAVUVI HARAMU WAJISALIMISHE.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Chistopher Ngubiagai, ametoa siku 14 kwa wavuvi haramu katika wilaya hiyo wajisalimishe na kukabidhi dhana wanazotumia.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la uchomaji wa zana za uvuvi haramu lililofanyika mjini Kilwa Masoko.

Ngubiagai alisema uvuvi haramu nitatizo linalohitaji nguvu na jitihada zinazotokana na uzalendo ili kulikabili. Kwasababu ya mbinu zinazotumiwa na wahalifu katika kuhakikisha hawakamatwi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema mapambano hayo ni makali na magumu, kwa sababu baadhi ya wahalifu hao kuwa na mtandao mkubwa unaowahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa umma wasiowaadilifu. Hivyo wilaya hiyo imetengeneza mikakati madhubuti itakayotokomeza tatizo hilo linalotishia uwepo wa viumbe hai wa baharini. 

Ngubiagai aliitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kuhakiki wavuvi wote waliopo katika wilaya hiyo na maeneo wanayofanyia shugulizao, kusajili vyombo vyote vya uvuvi na kuvipa namba za utambuzi na kujua kila chombo mahali kilipo, kuwasajili wavuvi wote walio kwenye kambi za uvuvi na kuainisha bandari maalumu zinazoshushia mazao ya uvuvi ya maeneo mbalimbali.

"Napenda kuwatahadharisha wasalimishe zana zao za uvuvi haramu haraka iwezekanavyo ndani ya wiki mbili kwani zama zao zimekwisha. Vita hii niliyoianza haitasimama nitahakikisha uvuvi haramu unatokomea kabisa katika wilaya hii,lengo ni kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinavinufaisha hata vizazi vijavyo," alisisitiza Ngubiagai.

Alibainisha kuwa kupitia hatua za awali za mapambano hayo ambayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli aliyotoa hivi karibuni jijini Mwanza, naya waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliyotoa wilayani Mafia mkoa wa Pwani.

Wamefanikiwa kukamata kilo 281 za unga wa kutengenezea mabomu tambi 7, vibati 7 na chupa za mabomu ambazo zilikamatwa kutokana na ushiriano mkubwa wa raia wema kwenye kambi za uvuvi za Nyuni, Ukuza na Simaya.
"Unga uliokamatwa ulikuwa na uwezo wa kutengeneza chupa za mabomu 188,kila chupa ingeweza kuharibu eneo lenye ukubwa wa zaidi ya mita hamsini,maana yake nikwamba zisingekamatwa basi eneo la bahari lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 9400 zingeharibiwa kabisa," alisema.

Mkuu huyo wawilaya alitoa wito kwa serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kwa kusema "Kuna umuhimu wakuangalia na kutafuta uwezekano wa kuunda kikosi maalum cha kwa ajili ya kupambana na wavuvi haramu katika bahari na maziwa,kwa sababu hawa askari ingawa wanajitihidi sana na juhudi zao zinazaa matunda,lakini hawana uelewa mkubwa wa mambo ya bahari na sheria zake," alisema.

Kwa upande wake ofisa uvuvi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Ahmad Mkali. Alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazosababisha kupunguza kasi ya kupambana na uvuvi huo ni uchache wa boti za kufanyia  doria.Akibainisha kuwa halmashauri hiyo inaboti moja tu. Wakati mahitaji halisi ni angalau boti nne."Wavuvi haramu wanavua bahari kuu ni mbali,na eneo la bahari nikubwa sana kwa boti moja inakuwa vigumu kuyafikia maeneo yote kwa wakati mmoja," alisema Mkali.
Baadhi ya zana haramu za uvuvi zilizokamatwa, Pichani ni Mabomu yanayotumika kulipulia Samakina viumbe vingine Baharini.

Zana Haramu za vuvi zikiteketea kwa moto. (Picha na :Bernad Mpangala Mchambuzi wa Mifumo Kilwa.)
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndg; Christopher Ngubiagai akizungumza na wavuvi.

BALOZI WA AUSTRALIA NCHINI ATEMBELEA KIJIJI CHA DONGOBESH,MANYARA

$
0
0


Balozi wa Austraia nchini John Feakes akizungumza alipotembelea kijiji cha Dongobesh Mkoani Manyara, katika mradi wa FREO2 wa kuanzisha kituo cha kufua hewa ya oxygen kwa ajili ya kituo cha afya Dongobesh, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga.

MANGULA AFURAHISHWA 100 KUFUKUZWA UANACHAMA WA CCM MWANZA

$
0
0
Mzee Philip Mangula
Na Bashir Nkoromo, Mkuranga
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula ameelezea kufurahishwa kwake kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza kwa kubainika kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

"Haiwezekani, unajiita mwanachama, halafu badala ya kujitolea kwa nguvu zako zote chama kishinde vita ya kushika dola, wewe unakisaliti,  hapo unakuwa si mwanachama bali jeshi la kukodiwa",  Mangula alisema, hayo jana, wakati akizungumza na Vijana wanaosoma na waliohitimu vyuo vikuu 20, ambao wameweka kambi ya kufyatua matofali kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Nasabagani, Mkuranga mkoa wa Pwani.

 "Taarifa ya Chama kuwafukuza uanachama wale 100 kule Mwanza imenifurahisha sana, ni matumaini yangu kwamba hatua kama hizi zitaendelea kuchukuliwa  kila mahala nchini kote kwa waliokisaliti chama. hivi ni mchezaji gani anayempiga ngwara mchezaji wa timu yake wakati wa mechi ya kutafuta ubingwa halafu akaachwa kuendelea kuwa katika timu?" Mangula alisema na kuhoji kwa mshangao.

Mangua alisema, wakati mikoa itaendelea kuchukua hatua, lakini pia kwa ngazi ya taifa hatua dhidi ya waliokisaliti chama zitaendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwatupilia mbali watakaojaribu kuomba nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi wa Chama mwakani, huku wakiwa wameshabainika kuwa walikisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu ulipita.

Mangula aliwataka vijana nchini kote hasa wasomi, kuepuka kutumiwa vibaya na wanachama watakaokuwa wanasaka uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwakani, kwa kuwa kijana yeyote atakayekubali kutumiwa vibaya atakuwa amekisaliti na kuchangia kunyong'onyesha nguvu na uhai wa Chama.

"Hili la kutumiwa vibaya hasa ninyi vijana, nawaasa sana kuepuka nalo, jambo hili ni baya sana, na si kwa Chama tu lakini hata kwa wewe uliyekubali kutumika, maana utatumiwa kama ngazi, halafu akishapita hatakuwa na manufaa kwako na hata kwa taifa maana atakuwa mvurugaji tu, badala ya kushiriki kuleta maendeleo ya chama na taifa", Alisisitiza mangula.

MALKIA WA SHINDANO LA UREMBO KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI ‘ALBINO’ KENYA APATIKANA

$
0
0

Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Mamia walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. Kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.Chanzo-BBC SWAHILI
Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama  jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.

Kutoka kulia, naibu rais wa Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia walikuwemo.

TANZIA: DADA WA MDAU FATMA SALUM AFARIKI DUNIA MSUMBIJI

$
0
0
Mpendwa wetu Fatuma  Salum (pichani, enzi za uhai wake) akiwa huko Mozambiki katika kutafuta maisha, ametutoka Duniani akiwa katika maandalizi ya kurudi nyumbani kwao kuiona familia yake na Mzazi wake na ndugu zake waishio Kinondoni maeneo ya Mkwajuni  Jijini Dar es Salaam.
Siku mbili nyuma Marehemu Fatma aliugua ugonjwa wa kuishiwa nguvu mkono na mguu upande mmoja na kukimbizwa Hospitali ambako alipata bahati ya kuongea na mama yake Mzazi na kumweleza hali yake. 
Baada ya hapo tulipata taarifa ya kuwa amefariki akiwa katika maandalizi ambapo Ijumaa hii iliyopita alitarajia  aanze safari, na Ijumaa hiyo hiyo mchana akaaga Dunia.

Hadi sasa wafanya biashara wenzake kwa kushirikiana na familia ya mpendwa wetu mwili utalala Boda na asubuhi safari itaanza.
Familia ya mpendwa wetu inatoa asante kwa wote walioshiriki kufanikisha michango yao na kujinyima ili kufanikisha safari ya mpendwa kurudishwa nyumbani na wote wanao endelea kutoa misaada ya hali na mali. Shukrani za kipekee ziwafikie wafanya biasha wenzake pamoja na Madaktari wote na ndugu na jamaa kwa kufanikisha taratibu za maandalizi ya safari yake ya mwisho
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un 
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعون

Jaji Lubuva aitaka Tume ya Haki za Binadamu kujifunza kwa Tume ya Uchunguzi kuimarisha Utawala Bora

$
0
0
Hussein Makame, NEC .

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa tendaji wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.

Jaji Mst. Lubuva ametoa wito huo wakati akeleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Tume hiyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi katika inatekeleza majukumu yake wakati huo lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.

“Katika hali na mazingira ya Tume ya wakati huo, bila kusita nashawishika kusema kuwa Tume ya Kudumu ilianzishwa wakati ambapo si watu wengi kwa bahati mbaya Afrka ambao walijali haki za binadamu na utawala bora” alisema Jaji Mst. Lubuva.

Aliongeza kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambapo Tanzania ndio ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo alisisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha TKU ili kunusuru wananchi kutakona na madhila ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.

“Kwa upande mwingine Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina kibarua kizito katika kutekeleza majukumu yake katika mazingira ya sasa ambapo tume hii si rahisi kuelezea kwa wananchi kwa nini isifanikiwe zaidi ya TKU” 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa akipokea tuzo ya Heshima ya Utawala Bora kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (katikati) akiwa amepokea Cheti cha Utambuzi wa Utumishi wake kwenye Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kutambua mchango wake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga na kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay.
1. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akibadilisha mawazo na Wanasheria Wakuu wa Serikali Wastaafu wenzake Jaji Mst. Mark Bomani 1965-1976 na Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba 1976 -1985.Jaji Mst. Warioba alitumikia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1985 hadi 1993.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (wa tatu kulia) akiungana na kwenye picha ya pamoja na na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wengine wa Serikali Wastaafu waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

DC LONGIDO,DANIEL CHONGOLO AMSWEKA NDANI MKANDARASI WA BARABARA

$
0
0
DC-Longido,Mh Chongolo.
Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Godfrey Chongolo amemtia ndani Mkandarasi anayejenga barabara ya Longido-Kitumbeine-Oldonyolengai Bw. Loserian Sokonei Mollel kutokana na uzembe na kutotimiza matakwa ya mkataba na kuwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo pamoja  na wananchi kwa ujumla. 

Mkandarasi huyo anayemiliki kampuni ya Genuine Company Limited amekuwa akiendesha shughuli za ujenzi wa drift katika barabara hiyo bila kutengeneza barabara mchepuko (diversion) katika maeneo hayo na kusababisha mara kwa mara wasafiri kukwama na kulala porini. 

Wakizungumza na mtandao huu, wananchi wa kijiji cha Gelai Lumbwa wamepongeza uamuzi wa DC Chongolo kwa sababu unasaidia kuondosha na kutatua kero zanazowasumbua na kuwakwaza kwenye maisha yao ya kila siku. "Tulichoshwa na watu waliokuwa wakifanya mambo vile wanavyotaka wao. Kwa hakika hii ni awamu ya Kazi Tu, tunamshukuru DC na OCD na tunamuunga mkono" alisema Mesiaki Laizer.

TIMU YA GOLF YA LUGALO YATESA MASHINDANO YA PWC TROPHY

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

Mchezaji wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Nicholous Chitanda imeibuka washindi wa Jumla katika mashindano ya wazi ya PWC Trophy yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Chitanda aliibuka na ushindi huo nakuwashinda wachezaji wengine zaidi ya 100 waliojitokeza kutoka Klabu zote Nchini baada ya kupata Mikwaju au Gross 74 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na hivyo kuibuka na Mikwaju ya Jumla Net ya 65.

Katika Division A ushindi ulinyakuliwa na Isack wanyenche kutoka Klabu ya Arusha baada kupiga mikwaju 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni Tatu na hivyo kuibuka na ushindi kwa kupiga mikwaju ya jumla 66 na kufuatiwa na Juma Likuli wa Lugalo baada ya kupiga mikwaju ya jumla 68.
Kwa upande wa Division B mshindi ni Dk James Legg wa Lugalo baada ya kupiga mikwaju 84 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 13 na hivyo kuwa na mikwaju ya jumla 71 na kufuatiwa na Salum Mvita wa Dar es Salaam Gymkhana kwa mikwaju ya Jumla 71.

Division C kwa upande wake Mpiga Golf Reneir Kuhcmanu wa Lugalo aliibuka na ushindi katika kundi hilo baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 68 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 24 akifuatiwa na Kapten Amanzi Mandengule wa Lugalo pia baada ya kupata mikwaju ya Jumla 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 19..
Mshindi wa Jumla wa mashindano ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 Jijini Dar es Salaam Nicholous Chitanda wa Lugalo aliyeshika Vikombe akiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa Kushoto ni mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo , wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa TGU Joseph Tango na wa pili kulia ni Msuya Mkurugenzi PWC .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Wachezaji wa Golf kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima, Dk Edmund Mndolwa aliyekuwa Mkuu wa majeshi Jenerali Mstaafu George Waitara na Balozi Clemence Sanga wakibadilshana mawazo kabla ya kuanza mashindando ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam.

USIKOSE KUTAZAMA KIPINDI CHA MUSWADA WA HABARI NA TANZANIA IJAYO

CHAWABATA CHAIOMBA SERIKALI KURUDISHA MUDA WA ZAMANI WA KUFUNGUA BAA NCHINI

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimeiangukia serikali kwa kuiomba iruhusu wenye mabaa kufanya biashara zao wakati wote ili kusaidia kupata fedha za kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ali Huseein wakati akizungumza na mtandao wa www.habarizajamii.com Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu changamoto waliyonao wenye mabaa katika kufanya biashara yao hiyo ya uuzaji wa vileo na vinywaji baridi."Tunaiomba serikali kuangalia kwa karibu kuhusu muda wa kufungua baa kwani muda huu wa sasa wa kufungua saa 10 jioni na kufunga saa tano ni mdogo ukilinganisha na ilipokuwa awali wa kufungua wakati wote" alisema Hussein.

Hussein alisema nia ya serikali haikuwa mbaya ya kufungua baa saa 10 lakini hawakuangalia upande wa pili wa wamiliki wa baa hizo kwani wengi wao katika muda huo wengi wao hawafanyi kabisa biashara.aliongeza kuwa wafanyabiashara hao wanahitaji kupata muda wa siku nzima wa kufanya biashara zao ili waweze kumudu kupata fedha za kulipa kodi ya serikali na mishahara ya wafanyakazi na wahudumu wa baa ambao ni wengi,hivi sasa wanashindwa kufikia malengo.

Alisema baadhi ya baa zimepunguza wahudumu wake kutokana na kubanwa na muda huo ambapo wahudumu wamekuwa wakiingia jioni tu baada ya muda wa asubuhi kupigwa marufuku na serikali."Wenye mabaa hivi sasa wapo katika changamoto kubwa ya biashara zao tunaiomba serikali kuangalia jambo hilo kwa sura nyingine ili kuinusuru biashara hiyo kuanzia mmiliki wa baa na viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo na serikali yenyewe kupata kodi yake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa ombi kwa serikali la kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.
Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck. akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Wabunifu mitindo waonesha mavazi uzinduzi duka la maharusi

$
0
0
Wabunifu mitindo waonesha mavazi uzinduzi duka la maharusi Na Mwandishi Wetu WABUNIFU wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi wamejitokeza kufanya maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi katika uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaa. Uzinduzi huo uliofanyika jana eneo la Sinza Madukani ulipambwa na mbunifu wa mitindo kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kwa jina la Femi, mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa ambao ni waandaaji wa onesho alisema waliamua kufanya onesho hilo ili kutoa fursa kwa wananchi hasa wanaoelekea kufanya harusi kujua mitindo mbalimbali ya mavazi ambayo wanaweza wakaitumia katika shughuli zao za harusi na kuonekana tofauti kimuonekano.

Alisema wabunifu walifanya maonesho ya mavazi katika mitindo mbalimbali kutumia mavazi ya hali zote ikiwa ni kuonesha jamii harusi si lazima muhusika au maharusi kutumia gharama kubwa bali wanaweza kutumia gharama za chini na kuonekana wenye mvuto kama watapata ushauri kutoka kwa wabunifu na wanamitindo. 

Alisema duka lao pamoja na kuuza nguo za maharusi watakuwa wakitoa ushauri bure kwa maharusi endapo watafika katika duka hilo ambalo limekuja kuleta mabadiliko katika mitindo ya maharusi. Alisema duka hilo litahudumia watu wenye kipato cha chini, cha kati na hata cha juu kulingana na mahitaji ya wahusika huku wakinufaika kwa ushauri bure kila atakaetembelea na kuomba ushauri kwa wataalamu wa mitindo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo pamoja na Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa (kulia). Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania.
Mmiliki wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria.
Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimlisha keki Mwendeshaji wa duka hilo, Victoria Chuwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Mbunifu maarufu wa mitindo kutoka nchini Nigeria, Femi (wa pili kushoto), pamoja na mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano (wa kwanza kulia) wakiwa katika pozi pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania, kwenye maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanyika katika duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. 

SERIKALI YAKABIDHI HATI ZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NYAKATO

$
0
0
Serikali imeyakabidhi makampuni ya mafuta ya OILCOM, GBP na MOIL hati za Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera lilitokea mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano wa hati hizo jijini Dar es Salaam leo Tarehe 23 Oktoba, 2016, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dkt. Hamisi Mwinyimvua ameyashukuru makampuni hayo kwa ahadi ya kujenga shule mbili zilizobomoka kutokana na tetemeko hilo.
“Shule ya sekondari ya Ihungo na Shule ya Sekondari ya Nyakato zilibomoka kutokana na tetemeko hilo, Kwa kuwa serikali imeanza kujenga shule ya sekondari ya Ihungo ninawakabidhi nyaraka za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato na ninaamini mtakamilisha ujenzi kwa wakati ili wanafunzi waweze kurejea shuleni hapo”amesema Mwinyimvua
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor amesema makampuni yao yataendelea kuziunga mkono juhudi za serikali za kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea nchini.
“Sisi tunaamini nchi yetu ya Tanzania lazima ijengwe na watanzania wenyewe na sisi hatunabudi kuwasaidia ndugu zetu wa Kagera kwa athari walizozipata za tetemeko kwa kujenga shule hiyo kwa ramani ambayo mmetukabidhi” amesema Mansoor
Naye, Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Maimuna Tarish amesema kuwa jukumu la wizara hiyo ni kutoa elimu bora na ili elimu iwe bora ni lazima iwepo miundo mbinu ya majengo ya shule ambayo ni bora kama itakayojengwa na makampuni hayo ya mafuta.
“Tutawakabidhi michoro ya shule hiyo ambayo ujenzi wake umezingatia ushauri wa wataalamu wakiwemo wa Jiolojia, aidha katika ujenzi  mtakao kuwa mnaufanya Wakala wa majengo ya serikali (TBA), itasimsmia kazi ya ujenzi ili kuhakikisha ubora unaotakuiwa unafikiwa” amesema Tarish
Itakumbukwa kuwa nchi yetu ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika Kanda ya Ziwa na Hasa Mkoa wa Kagera , Mwezi Septemba mwaka huu. Tetemeko hilo lilikuwa na athari kubwa kwa miundombinu na majengo ya taasisi mbalimbali za serikali na makazi ya wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, OKTOBA 23, 2016

h1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato,  kutokana na hiyo na  makumpuni ya mafuta mengine ya OILCOM na GBP waliahidi kuijenga shule hiyo iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardh mkoani Kagera, Septemba, 2016, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.
h2
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba , 2016, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu GBP Badal Sood, Mkurugenzi MOIL, Altaf Mansoor, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Maimuna Tarish, tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam. 

'NILIAHIDI, NIMETIMIZA, NITAENDELEA KUTIMIZA' - RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

RATIBA YA MAZISHI YA JACOB ELINAZA

$
0
0
Ratiba ya mazishi Jacob Elinaza yatakayo fanyika Oktoba 24,2016 nyumbani kwao Segerea jijini Dar es Salaam.

1. Mwili wa marehemu utafika saa 11:30 am 
2. Chakula cha mchana kuanzia 12:00pm 
3. Kuaga mwili wa marehemu kuanzia saa 2:30pm 
4. Ibada ya mazishi itaanza kuanzia 4:00pm 
Kila kitu kitakuwa nyumbani kwetu segerea kwa mama 
*Maelekezo* ya kufika

Unashuka kituo  cha Oil com segerea anachukua pikipiki unasema wakupeleke kwa msoji mwanajeshi au kwenye msiba kwa Elinaza 
    
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

TOYOTA TANZANIA YAZINDUA JUMBA LA MAONYESHO JIJINI DAR

$
0
0
Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Bw. Mahmood Karimjee alisema “Uzinduzi wa jumba hilo la maonyesho unaleta zama mpya katika safari ya Toyota Tanzania, inadhiirisha azma ya Karimjee Group katika kutoa huduma bora kwa wateja. Wateja sasa watafaidika na huduma zilizoboreshwa na bora zaidi kimataifa na tunatarajia watafurahia huduma hii kwa miaka mingi ijayo”. 

Jumba hilo kubwa la magari ya Toyota yanayotumika zaidi hapa nchini limeboreshwa kwa kuwekewa huduma nyingi za kisasa kama kumbi za mikutano zenye vifaa vya kisasa ili kuendana na viwango vya kimataifa na litatumika kama maonyesho ya magari ya Toyota hususani aina mpya za magari hayo yakiwemo yale yaliyozinduliwa hivi karibuni kama Hilux pick mpya, Fortuner SUV na Landcruiser VXR. 

Kutokana na uwekezaji huu, Toyota Tanzania imelenga kuwapatia huduma mpya na bora wanunuzi wa magari hayo na watu wengine watakaotembelea jumba hilo kujionea huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo. “Kununua gari ni maamuzi muhimu na sio jambo unaloweza kulifanya kila siku. Hivyo basi Toyota imeamua kuhakikisha kila mnunuzi wa gari anaweza kufurahia huduma za kisasa,” alisema Karimjee. 

Kufuatia ufunguzi huo, mwakani kampuni hiyo pia itazindua kituo cha huduma baada ya mauzo kwa lengo la kuhakikisha watumiaji wa magari hayo wanaendelea kupata huduma zitakazofanya magari hayo yadumu katika hali nzuri kwa muda mrefu. Vilevile kampuni hiyo itazindua kituo cha kutoa huduma za kuzuia magari yasiharibike na pia itatoa huduma za kukodisha magari kupitia kampuni yake ya Salute Finance Ltd. 

Karimjee alisema uzinduzi huu ni historia muhimu katika miaka 191 familia ya Karimjee na miaka 50 ya Toyota hapa nchini kwani jumba la mwisho la maonyesho lilizinduliwa miaka 26 iliyopita. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, mabalozi mbalimbali, wapenzi wa magari ya Toyota na Meneja Mkuu wa Toyota Motor Corporation, Bw. Yu Asano. Ambaye aliipongeza Toyota Tanzania kwa kupiga hatua hii muhimu. 

Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida akiangalia gari jipya aina ya Land Cruiser VXR wakati wa uzinduzi wa jumba la maonyesho ya magari la Kampuni ya Toyota Tanzania jijini Dar es Salaam juzi 
Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Mahmood Karimjee wakati wa uzinduzi wa jumba la maonyesho ya magari la kampuni hiyo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kushoto) pamoja na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (kulia) wakifatilia uzinduzi wa jumba jipya la maonyesho ya magari ya Toyota --- Kampuni ya magari ya Toyota Tanzania Limited imezindua jumba la maonyesho la kisasa kwenye makao makuu yake jijini Dar es salam ikiwa ni jitihada za kuboresha  huduma kwa wateja. 

MAKALA YA SHERIA: NANI ANASTAHILI KIPAUMBELE KUSIMAMIA MIRATHI KATI YA WARITHI WA MAREHEMU

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Ni vema  kujua nani  anapaswa  kupewa  kipaumbele  cha  kusimamia  mirathi  pale   mwenye  mali  anapokuwa  ameaga  dunia. Mara  kadhaa  mjadala  huibuka   baina  ya  wanafamilia  hasa  pale  inapotokea  kuwa  marehemu  alikuwa  na  mke  zaidi  ya  mmoja  na  kila  upande  kuna  watoto. 

Lakini  pia  hata  pale  marehemu  anapokuwa  na  mke  mmoja  mjadala  huu  napo  waweza  kuibuka  kati  ya  wanaotegemewa  kurithi  juu  ya  nani  awe  msimamia  mirathi. Hii  si  pale  tu  anapokufa  baba  lakini  pia  hata  panapo mswiba wa mama  mjadala huu huibuka.

1.WOSIA  KUTAJA  MSIMAMIA  MIRATHI.
Ikiwa  marehemu  ameacha  wosia  na  katika  wosia  huo  imeelezwa  wazi  nani  atakuwa  msimamizi wa  mirathi  basi  huyo  aliyetajwa  ndiye  atakuwa  msimamizi  wa  mirathi . Wosia  unaweza kumtaja  mtu  mmoja kusimamia  mirathi  au  zaidi  ya  mtu  mmoja. Kwa  vyovyote  utakavyotaja   hao  waliotajwa  ndio  watasimamia  mirathi.

2.  WOSIA  KUTOTAJA  MSIMAMIA  MIRATHI.
Si  wakati  wote  wosia hutaja  msimamia  mirathi.  Hii  yaweza  kutokea  kwa  kutokujua  kwa  aliyeandika wosia   au  kujua  lakini  kuacha  makusudi  kwasababu  nzuri  anazozijua  mwenyewe.  Kwa  namna  yoyote  itakavyokuwa  wosia  usipotaja nani   asimamie  mirathi  basi   ni  wajibu  wa  wanafamilia  kuhakikisha  anapatikana    msimamizi ili  agawe  mali kutokana  na  wosia  unavyoeleza.

Muhimu  ni  kuwa  ni  lazima  apatikane  msimamizi   wa  mirathi.  Aweza  kuwa  mmoja  au  zaidi. Swali  kwetu  ni  ikiwa  kumetokea mgogoro  kuhusu  nani  asimamie  mirathi  je  nani  afaa zaidi  kuliko wenzake  kupewa  kipaumbele  kwa  mujibu  wa  sheria.

3.NANI APEWE KIPAUMBELE  CHA KUSIMAMIA  MIRATHI  KATI  YA  WARITHI   WA  MAREHEMU.
Sura  ya  352  ya  sheria  ya  usimamizi  mirathi  ndiyo  huongoza  jambo  hili.  Ikumbukwe  tumesema  hapo  juu  kuwa  suala  la  nani apewe  kipaumbele  cha  kusimamia  mirathi  linaibuka  pale  tu  ambapo  marehemu  hakuacha  wosia  kabisa  au  ameacha  wosia  lakini  ndani  mwake  hakumtaja  msimamizi  wa  mirathi.

RC Gambo aongoza Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa wa Arusha leo

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania ipate uhuru na kuelekea kutimize mwaka 1 madarakani kwa kuipatia Wilaya ya Ngorongoro  barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 60 tangu Wilaya hiyo ianzishwe.

Haya yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.
Gambo alisema  barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami  na itaunganisha  mji wa Wasso hadi Sale kilomita 60 imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.

Gambo ameeleza katika Kikao  hicho kwamba  Rais Magufuli ameagiza kuanza kujengwa kwa barabara hiyo mara moja  kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.

Amesema barabara hiyo  inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha ( TANROADS).

Mkuu huyo wa Mkoa amesema  hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ,Wilaya  haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.

Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema  fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya dunia  sio msaada  bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo  Tanzania italazimika kuzilipa hapo baadaye.

Akitoa shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha alisema kwa mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha lami, kweli itakuwa furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.

Wilaya ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha  ambapo Wilaya hii inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa barabara za uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda maeneo ya vijijini.

Hivi sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya   za Mkoa wa Arusha zikiwemo  barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja wa Mkoa Mhandisi  John Kalupale.
Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha 38 cha bodi hio,jijini Arusha.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images