Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110115 articles
Browse latest View live

KINGATIBA ZA MATENDE, MABUSHA NA MINYOO KUANZA KUTOLEWA OKTOBA 25

$
0
0
Na Ally Daud- MAELEZO

SERIKALI kupitia mpango wa Taifa Wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele itaanza kugawa kingatiba za ugonjwa Wa matende, mabusha na Minyoo Oktoba 25 mwaka huu ili kuondoa kabisa magonjwa hayo mpaka ifikapo 2020.

Akizungumza hayo katika semina na waandishi Wa habari kuhusu magonjwa hayo Afisa Mpango wa huduma hiyo Bw. Oscar Kaitaba  amesema kuwa zoezi hilo litaanza Oktoba 25 hadi Oktoba 30 mwaka huu katika maeneo yote ya Dar es salaam.

"Zoezi la kugawa kingatiba kwa wananchi Wa Dar es salaam litaanza Oktoba 25 na kumalizika Oktoba 30 ili kuweza kupambana na vimelea vya magonjwa hayo na kuendelea na mikoa mingine" alisema Kaitaba.
Aidha Bw.Kaitaba amesema kuwa kingatiba ambazo zitatolewa ni Ivermectin na Albendazole ili kuondoa magonjwa ya Matende,Mabusha, na Minyoo kwa wakazi wa Dar es salaam na vitongoji vyake.

Bw.Kaitaba amesema kuwa kingatiba hizo zitatolewa kwa wananchi wote wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea katika maeneo yote ya Dar es salaam katika stendi za mabasi, Masoko,Hospitalini, Ofisi za Serikali za Mitaa, Ofisi za Wizara, Kambi za majeshi ns Magereza.

Aidha Bw.Kaitaba ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kwa wingi kupata kingatiba hizo wakiwa wameshakula vizuri chakula na kuondokewa na imani potofu kwamba zinachangia kuzuia mimba ama kwa wanaume kupungukiwa nguvu za kiume.

Kwa upande wake Muhamasishaji Wa Mpango huo kutoka Wizara ya Afya Bw. Makora Said amesema kuwa Semina hiyo inahusu kuwahamasisha waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Mpango Wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini kama vile Matende, Mabusha, Minyoo, Usubi, Trakoma na Kichocho.

Aidha Bw. Makora amesema kuwa kama waandishi watakavyoielimisha jamii kwa elimu ya kutosha na wananchi wakakubali wito Wa kutumia kinga tiba hizo Serikali itafanikiwa kuepusha ulemavu na udumavu kwa watanzania.

Aidha Bw. Makora amesema kuwa waandishi wanatakiwa wawe kipaumbele katika kuandika habari za afya ya Binadamu ili kuwapa ufahamu  wananchi na uwezo Wa wa kufanya maamuzi sahihi juu ya afya zao kwa ujumla.                  
      
Semina hiyo ya siku moja imelenga kuwaelimisha waandishi Wa habari kuhusiana na Mpango Wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili elimu ya kutosha ikatolewe kwa wananchi ili kufanikisha lengo la Sera ya Afya ya mwaka 2007 hadi kufikia 2020.

DK. SHEIN AWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOFAULU DARAJA LA KWANZA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Walimu na Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016,sherehe ya kuwazawadia wanafunzi hao iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao  katika sherehe maalum ya kuwazawadia iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Mahira Baraka Hamadi wa kidato cha sita Skuli ya Biashara Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri katika Mtihani wa Taifa Mei mwaka 2016,hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.

TANZANIA KUNUFAIKA KIBIASHARA NA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA KUPITIA NEMBO YA HALAL

$
0
0
Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila amesema Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa na mtanzania mmoja mmoja ifikapo mwakani kwa sababu wapo mbioni kuingia kwenye orodha ya nchi ambazo biadhaa zake za chakula zitawekewa nembo ya Halal ambapo bidhaa hizo zitauzwa kwa nchi 33 kimataifa ikiwemo Malaysia inayotoa nembo ya JAKIM.

Halal ni nembo ambayo inawekwa katika bidhaa inapoazalishwa hadi kumfikia mlaji kwa kuzingatia viwango maalum vilivyowekwa na kampuni ya JAKIM nembo ya halali.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Lolila amesema nembo ya Halal itaweza kumhakikishia mlaji muislamu na wasiokuwa waislamu uhakika wa chakula tokea kilipoanzishwa hadi kuuzwa kuwa kimepitia njia inayotakiwa kwa misingi ya dini ya kiislamu.

"Katika kitabu cha Qur an kinatueleza kuwa tuchinje na tule vyakula vya halal lakini kwa sababu mbali mbali tumekuwa tukila chakula bila kujua kimeanzia wapi na kimepita katika njia gani" Kwa kutambua mchango wa dini yetu tumepata mafunzoambao ndio wamiliki wa nembo ya Halal baada ya mwaka mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa kile walichotuachia ili kueza kupata nembo hiyo itakayotusaidia kuuza bidhaa zetu katika nchi za Asia na nyenginezo, "alisema Lolila.

Ameongeza kuwa nchi nyingi za kiarabu hawali chakula mpaka waone nembo ya Halal ambapo wanaamini chakula hicho kimepita katika njia sashihi inayotakiwa kwa waumini wa kiislamu na wasiokuwa waislmu.

Huku akieleza kuwa Tanzania zipo bidhaa nyingi zitakazo weza kuingizia pato la Taifa kwa nchi hizo ikiwemo Malaysia endapo kama zitauzwa katika nchi za kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halal Tanzania Certification (HTC) Muhsin Hussein amesema wamejifunza mengi kutoka kwa ugeni huo kutoka Malaysia na watayafanyia kazi mafunzo hayo yaliyowapa weledi wa kutambua bidhaa Halali kuanzia kwenye hatua za awali, na kuongeza kuwa wataitisha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari ili waweze kutoa elimu kwa Umma nao ujue kwa undani bidhaa Halal.

Mkurugenzi huyo amewatoa hofu a kwa kuwaeleza kuwa zile nembo za Serikali zinazotumika katika usimamizi wa bidhaa na chakula ikiwemo TBD na TFDA zitaendelea kuwepo ila nembo hiyo ya Halal itakuwepo ili kuweka Imani kwa waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa na hofio ya kutumia bidhaa zisizo Halal, zinazokwenda kinyume na mafundisho ya Dini hiyo Tukufu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa na mtanzania mmoja mmoja ifikapo mwakani leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Msaidi JAKIM kutoka nchini Malaysia Mohd Amri Bin Abdullah.
Mkurugenzi Msaidi wa kampuni ya JAKIM kutoka nchini Malaysia,Mohd Amri Bin Abdullah akizungumza na waandi wa habari (hawapo pichani) juu kuzingatia viwango maalum vilivyowekwa na kampuni ya JAKIM nembo ya halali leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila Mkurugenzi wa Halal Tanzania Certification (HTC),Muhsin Hussein akifafanua jamb leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila.

WAZIRI KAIRUKI AMALIZA ZIARA YA SIKU 2, KUWATEMBELEA, KUWASIKILIZA NA KUZUNGUMZA NA WANUFAIKA TASAF WA MANISPAA ZA KINONDONI NA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi wa Kata ya Sandali, ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika mpango huo. 

Diwani wa Kata ya Sandali, Temeke jijini, Abel Tarimo, akitoa maelezo kuhusu masuala mbalimbali kwenye mtaa wake huo, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alipokuwa na mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na wakazi wa maeneo hayo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kulia), kuzungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao kaya zao hazijaingizwa katika mpango huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Nasib Mbaga.
Baadhi ya wanufaika wa Tasaf katika mpango wa Serikali wa kuzinusuru kaya masikini pamoja na wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo wa maeneo ya Kata ya Mtoni, Temeke jijini Dar es Salaam jana, wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa katika mkutano huo.

Rais Mstaafu BENJAMINI MKAPA azindua Filamu ya Utalii NshabaOntwale Nyakijoga "Nipeleke Nyakijoga"

$
0
0


Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa, akitoa neno kwa Wageni waalikwa kwenye Jioni ya Bwanjai, kabla ya kuzindua rasmi filamu ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' Uzinduzi wa filamu hiyo ya utalii ulifanyika, katika Ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wa Jioni ya Bwanjai Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa, akikabidhiwa filamu ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' na Mrs Dorina Kilama tayari kwa ajili ya Uzinduzi huo, anayeshuhudia katikati ni Profesa Wenceslaus Kilama, uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa, akikabidhi CD yenye filamu hiyo ' Nipeleke Nyakijoga ' ndugu Salum Salum ambae ni mwakilishi wa DSTV, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo ambayo ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa Usiku wa Bwanjai, Uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waalikwa katika Uzinduzi wa filamu hiyo ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' Uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Ngoma kutoka Kantare, Bwanjai kikitoa Burudani maridhawa wakati wa Uzinduzi wa filamu ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' Uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.kwa hisani ya www.habari360.com

MAPOKEZI YA B.G MALISA MKOANI ARUSHA LEO OKTOBA 22,2016

$
0
0
Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa akizungumza na waandishi wa habari mara baada tu ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha.
Nabii B.G Malisa akipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 jijini Arusha katika viwanja vya reli.
Umati wa wakazi wa mkoa wa Arusha waliofurika katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Kilimanjaro(KIA) kumpokea Nabii B.G Malisa ambaye atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWATAKA WANAWAKE KUWAFICHUA WAPENDA RUSHWA WANAOKWAMISHA HARAKATI ZAO ZA KUJIKOMBOA KIUCHUMI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wajasiriamali kuwafichua watendaji wa mamlaka za kurasimisha biashara watakaowadai rushwa wakati wa kupatiwa huduma ya kurasimisha biashira zao.

Makamu wa Rais alitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati kufungua Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasirimali Tanzania (VoWET).Alisema wanawake hawapaswi kuogopa kuwafichua watendaji wanaowaomba rushwa kwani wanawakwamisha katika harakati zao (wanawake) za kujiendeleza kibiashara,kiuchumi na pia kukwamisha juhudi za serikali katika kuinua maendeleo ya Wanawake nchini.
Rais wa VoWET Bi. Maida Waziri (kulia) akihutubia wakati wa Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania ambapo licha ya kupongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika masuala mbali mbali ya kumuwezesha mwanamke pia alielezea changamoto ambazo wanawake wanakutana nazo katika shughuli zao za kuwainua kiuchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya kazi za ubunifu zilizofanywa na Wanawake Wajasiriamali kabla ya ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.


RC GAMBO APOKEA MSAADA WA BATI 500 NA MIFUKO YA SARUFI 500

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah – Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.

Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.

Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil – Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina – Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.

“Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii “.


Meneja Mradi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia mbele) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto) mfuko wa saruji na bati kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya saruji 500 waliyoitoa kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za Maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshukuru Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(mbele kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha mifuko ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet. 

Mhandisi wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia) akiwatambulisha wawakilishi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd walipokuja kukabidhi msaada wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. 


BAMIZA TOP CHARTS OCTOBER 22, 2016

TANESCO YASEMA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha ujenzi wa  mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.

Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa  mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmision Lines),  kwa msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre pia umekamilika.
 Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondaru ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.

 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,  Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
 Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli ya Kitalii katika Kijiji cha Matemwe Zanzibar Inayojengwa na Pennyroyal (Gibraltar) Ltd Zanzibar.

$
0
0
 
 
Mmiliki wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkurugenzi wa Mradi huo Brain Thomson, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofika kutembelea mradi huo kujionea maendeleo ya matayarisho yake na kuwaonesha michoro ya picha za majengo ya Mradi huo mkubwa utakaokuwa na uwanja vya ndege. na kutengeneza visiwa kwa ajili ya wageni wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar. 
Mmiliki wa Mradi wa Mkubwa wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson, akitowa maelezo ya mradi huo kwa kuwaonesha jinsi ya majengo yatakuwa katika eneo hilo na kutoa ajira kwa Wananchi wa Matemwe na vijiji jirani kupitia mradi huo. 
Mmiliki wa Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson akizungumza na waandishi wa habari walipofika kuangalia ujenzi wa mradi huo na kusema kukamilika kwakev kutachukua miaka minane kukamilika kwake na kutowa fursa za ajira kwa vijana wa kijiji hicho na kutowa maendeleo katika sekta za jamii kunufaika na mradi huo.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MANGULA ASHIRIKI KUFYATUA MATOFALI KUUNGA MKONO VIJANA WANAOSOMA NA WALIOHITIMU VYUO VIKUU 20

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Mabweni ni kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha tano na cha sita, ambao kwa sasa wanalala chini katika chumba cha maabara ya shule hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akisaidiana kubeba tofali na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga, baada ya kufyatua tofali hilo, wakati akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani humo mkoa wa Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, Filbarto Sanga akimweleza jambo, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula aliyetembelea eneo la ufyatuaji matofali kabla ya kushiriki ufyatuaji huo leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Kulia ni Mwenyekiti wa Kambi ya Vijana hao, Mwita Myamkururu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula, akikagua matofali yaliyokwishafyatuliwa na vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, alipofika kuwaunga mkono vijana hao leo. Nyuma yake ni Mkuuwa wilaya ya Mkuranga, Filbarto Sanga na katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Pwani, Abiudi Shilla. Picha zote na Bashir Nkoromo-Official CCM Blog. PICHA ZINGINE KEM KEM ZA TUKIO HILI/>>BOFYA HAPA

YANGA WAIADHIBU KAGERA SUGAR BAO 6-2 KWENYE UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA LEO

$
0
0
Yanga leo wameichakaza Kagera Sugar kwa idadi ya mabao 6-2 kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara, iliyochezwa katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na kuchupa hadi Nafasi ya Pili.

Kagera Sugar ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 3 Mfungaji akiwa Mbaraka Yusuf na Yanga kusawazisha Dakika ya 4 kupitia Straika wao kutoka Zimbabwe Donald Ngoma.

Yanga walipa Bao la Pili Dakika 21 kupitia Simon Msuva na Straika wa Zambia, Obrey Chirwa, kuipa Bao la 3 Dakika ya 26.
Yanga waliongoza kwa Bao hizo 3 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 49, Mbaraka Yusuf, kwa mara ya pili, akaipa Kagera Sugar Bao lao la Pili lakini Yanga wakaja juu na kupiga Bao 3 nyingine katika Dakika za 58, 63 na 64 kupitia Deus Kaseke, Chirwa na Ngoma.

Timu ya Pili ni Yanga yenye Pointi 21 kwa Mechi 10 wakifungana na Stand United, waliocheza Mechi 12, lakini wana udhaifu wa Magoli na hivyo kushika Nafasi ya 3.

Jumapili Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Mbao FC.
Mchezo huo umezalisha mabao nane ambapo Casillas alifungwa mabao matatu mepesi katika dakika 27 pekee alizokuwa langoni kabla ya Kocha Mecky Mexime kumtoa na kumuingiza David Burhan ambaye nae alifungwa matatu.

Cassilas alishindwa kujiamini langoni ambapo alifanya makosa kadhaa katika dakika chache alizodumu uwanjani ambapo kama washambuliaji wa Yanga wangeongeza umakini kabla ya mlinda mlango huyo kufanyiwa mabadiliko basi wangeweza kufunga zaidi ya mabao hayo kipindi cha kwanza.
Washambuliaji Obrey Chirwa na Donald Ngoma walifunga mabao mawili kila mmoja huku Simon Msuva na Deus Kaseke wakifunga moja moja na kukamilisha karamu hiyo ya mabao.

Rais Magufuli amteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi TAA

$
0
0






  Prof. Ninatubu Mbora Lema





Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Oktoba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 20 Oktoba, 2016.

Prof. Ninatubu Mbora Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia tarehe 20 Agosti, 2015.

Prof. Ninatubu Mbora Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Associate Professor of Construction Management - University of Dar es Salaam).


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


22 Oktoba, 2016

MKUTANO WA KWANZA WA BIASHARA NA UWEKEZAJI BAINA YA TANZANIA NA MOROCCO WAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa Kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Morocco Makamu wa Rais aliainisha maeneo mbali mbali ambayo yanaweza kuwa fursa nzuri ya kuwekeza Tanzania.Baadhi ya maeneo hayo ni Kilimo,Utalii, Nishati, Mafuta na Gesi, Viwanda,Sekta ya Huduma, na Sekta ya Madini.Mbali na kuainisha baadhi ya fursa Makamu wa Rais aliwahakikishia uwepo wa amani na usalama na sheria mbalimbali zinazolinda haki za wawekezaji. 
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Morocco Bi.Miriem Bensalah-Chaqroun, akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Morocco uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Morroco.
Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Morocco wakifuatilia kwa makini mkutano huo.



Wazalendo 53: Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara mzee Philip Mangula atembelea kambi la wazalendo wasomi

$
0
0
Makamu mwenyekiti wa ccm Tanzania Bara Mzee Philip Mangula akitembelea kambi ya Vijana 53 wazalendo Wasomi wetu kutoka vyuo vikuu vya nje na ndani ya nchi walioungana kwa pamoja kufyatua matofali 45,000 kwa ajili kujenga mabweni 5 pamoja na nyumba 5 za walimu katika shule ya sekondari Nasibugani wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mh Filberto Sanga alichukua hatua ya kuandaa kambi hii ya wazalendo kusaidia adha waliyokuwa wakipata wanafunzi wa shule ya Nasibugani gani ikiwemo kukosa mahala pa malazi huku baadhi yao kidato cha tano na sita wakilala katika chumba cha maabara.
Ripoti iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wazalendo Bw Daniel Sarungi inaelezea maisha ndani ya kambi na shughuli walizofanya ikiwemo
 Kufyatua matofali, Kusomba Mchanga, Kujipikia chakula, Kufundisha wanafunzi wa kidato cha V na VI, Kutoa huduma ya afya kwa wanakambi na wanafunzi, Mijadala ya maendeo na utawala bora pamoja na Kuhamasisha wanafunzi kujiunga na vilabu vya kupinga rushwa.
Report hiyo ya wazalendo pia imeomba serikali kama ikiona inafaa wale wote wanaopenda kufanya kazi serikalini waanze kwa kujitolea miezi 6 au mwaka mmoja ndipo waajiriwe kufuatana na taaluma zao.
Kambi inaongozwa na mwenyekiti wa kambi Mwita Nyarukururu, Makamu Mwenyekiti ambae ni Helen Madole pamoja na Katibu Mkuu wa wazalendo Daniel Sarungi.
Mlezi wa kambi ya wazalendo ni kamati ya ulinzi na usalama wilaya ikiongozwa na Mh DC Filberto Sanga.

Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula katika picha ya pamoja na kambi la wazalendo wasomi
Kambi ya wazalendo ilianza tarehe 28/09/2016 na mpaka sasa zaidi ya matofali 38,235 yako tayari na yamebaki matofali 6,765 tu.
 Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula akichakarika na Wazalendo wasomi
 Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula akiendelea kufanya kazi  na Wazalendo wasomi
Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula akiongea na Wazalendo wasomi.

RC Arusha apokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo amepokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea inayojenga barabara ya Tengeru - Sakina.

Msaada huo umetolewa ofisini kwake ambapo tukio hilo limeweza kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,Wilaya na Wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Arusha.

Akipokea msaada huo, Mrisho Gambo amesema atagawa mifuko 100 ya simenti na mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati kata ya Murieti kwasababu kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wagonjwa katika hospitali ya Mkoa Mt.Meru wanaotoka maeneo hayo hivyo ujenzi huo utasaidia  kupunguza wagonjwa katika hospitali hiyo.

Pia yatakayo baki atayapeleka Wilaya ya Longido katika kusaidia ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Longido ambayo liliungua moto nakuteketeza kila kitu.

“Napenda kuishukuru na kuipotengeza kampuni ya ukandarasi ya barabara ya Tengure Sakina na ile ya njia mbadala(by path) kwakutoa msaada huu na kwakuwa tumeshaanza  mkakati wa ujenzi wa madara kwa shule za msingi na Sekondari,hivyo nitagawa hayo mifuko ya simenti 100 na mabati 100 ikajenge Zahanati kata ya Murieti na yaliyobaki yataenda Longido katika ujenzi wa bweni lililoungua”.

Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu bwana Xie Jianbao amesema kampuni yao imetoa msaada huo ikiwa ni moja ya shughuli zao zakusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Tumetoa mifuko ya simenti 500 na mabati 500 kama moja ya mchango wetu katika kusaidia jamii yetu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo”.

Aidha Mkurungezi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema  kutokana na wingi wa wananchi waliopo katika kata ya Murieti Zahanati hiyo itaenda kuwasaidia sana na kwakipindi kisichozidi miezi 2 Zahanati hiyo itakamilika na wananchi wataweza kuitumia.

Ukosefu wa kituo cha afya katika kata ya Muriet ulibainika baada ya Mkuu wa Mkoa Gambo kufanya ziara katika kata hiyo nakupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatembe umbali mrefu sana kutafuata huduma za afya.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akitoa shukrani kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kwa kutoa msaada wa mifuko ya simenti 500 na mabati ya 500 kwa shughuli za maendeleo za Mkoa wa Arusha.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

LATEST UPDATES FROM KC GLOBAL LINKS LTD

$
0
0

ILI KUBORESHA HUDUMA, SASA TUTAKUA TUNATUMA MZIGO KWA NDEGE MARA MBILI KWA WIKI.
AIR CARGO NO 1005 SASA KUONDOKA JUMATANO IJAYO IKIFUATIWA NA AIR CARGO 1006  JUMAMOSI IJAYO. 
KONTENA LA SEA CARGO NDIO LINAPAKIA SASA NA LITAONDOKA IJUMAA IJAYO. 
LETE MZIGO WAKO SASA.
AIR CARGO £3.50 inclusive clearance, 
Sea cargo £1.80 inclusive clearance
Tunafuata mzigo popote
Contact us:
KC GLOBAL LINKS LTD
SUITE 2 CLIPPER HOUSE
TILBURY PORT
TILBURY
RM18 7GS
Tel 01375 85 85 25
Mob: 07494364194

SHAMBA LA MITI LUNGUZA WAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI MUHEZA WAKABIDHI MADAWATI 200.

$
0
0


 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akikagua madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akitazama baadhi ya madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Meneja wa Shamba la Miti Lunguza,Abdallah Mchomvu akizungumza katika halfa hiyo ya kukabidhi madawati kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kushoto aliyekaa ambayo yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)
 Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza ambaye ni Afisa Tarafa ya Muheza Khatibu Omari wakati wa halfa hiyo wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Lunguza ambalo ni la serikali linalojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na ustawishaji wa miti ya misaji (Teak)
Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya MuhezaHajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo. 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

KICK BOXING BOUT IN NAIROBI: Emmanuel Shija [Tanzania] Vs Golola Moses [Uganda]

Viewing all 110115 articles
Browse latest View live




Latest Images