Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Prof. Elisante Ole Gabriel kufungua kongamano kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa klabu za soka nchini

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel anatarajiwa kufungua kongamano kuhusu mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji katika klabu za soka nchini.
 
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuhusu mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia na limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
 
Kongamano hilo litaanza saa nne na nusu asubuhi na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam kupitia chaneli yake ya Azam Two.Dhamira kubwa ya kongamano hilo ni kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga utaratibu wa kukodishwa.
 
Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni namna ya kuendesha klabu za soka kibiashara, uwekezaji, mambo ya hisa na masuala ya uthamini kukiwa na watalaamu kutoka taasisi mbalimbali nchini.
 
Pia kutazungumzwa umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo na harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake yalivyokuwa.
 
Lengo ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka.
 
Nawasilisha,
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
21/10/2016

BALOZI WA FINLAND NCHINI AMTEMBELEA PROFESA MUHONGO

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza alipokutana na Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (kushoto). Balozi Hukka alimtembelea Waziri Muhongo Ofisini kwake, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Jijini Dar es Salaam ili kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa Sekta ya Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (katikati). Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipeana mkono na Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Muhongo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza katika kikao na Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (kushoto).

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA AFYA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya  katika  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb2
Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo   akisoma   utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mhe,Harusi Saidi Suleiman,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb3
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Afya   wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo   Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016

VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 97: Kanye West, Jay Z, Frank Ocean, Chris Rock and Taylor Swift

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 21.10.2016

Ziara ya Mfalme wa Moroco ni Fursa kwa Wafanyabiashara

$
0
0
Immaculata Makilika- MAELEZO

Moroco ni nchi iliyopo Kaskazini Magharibi mwa Afrika, ambayo imepakana na bahari za Atlantiki na Mediteraniani, na upande wa bara imepakana na nchi za Algeria, Mauritania.mpaka wa kusini unatajwa kuwa Sahara Magharibi.

Nchi ya Moroko inakadiriwa kuwa na eneo la Km2 446,550, huku sehemu kubwa ikiwa ni jangwa la Sahara na watu wengi nchini humo huishi kwenye sehemu zilizo na rutuba hasa karibu na maeneo ya pwani.

Nchi hiyo ina milima inayofunika eneo kubwa, ikiwemo milima ya Atlas ambayo ipo katikati ya nchi hiyo kutoka kusini magharibi kuelekea upande wa kaskazini mashariki na mji mkuu wake ukiwa ni Rabat wenye wakazi milioni 2, aidha mji mkubwa ni Casablanka.

Nchi ya Moroco ilipata uhuru wake mwaka 1956 kutoka kwa nchi za Ufaransa na Hispania zilizokuwa zikiitawala, na kikatiba inaongozwa na Mfalme, kwa sasa inaongozwa na mfalme anayeitwa Mohammed wa VI, na Waziri Mkuu ni Abdelilah Benkirane. Watu wa Moroko hutumia lugha rasmi za kiarabu na kiberiberi. Fedha yao inajulikana kama Dirham, zaidi ya 90% ya watu wake ni waislamu. Uchumi wa Moroco unategemea zaidi utalii, sekta ya mawasiliano, viwanda vya nguo pamoja na kilimo.

Hivi karibuni, kwa mara ya kwanza tunashuhudia ziara ya Mfalme wa Moroco Mohammed wa VI aliyewasili nchini wiki hii kwa ziara ya siku tatu hadi Oktoba 25 mwaka huu. Ujio wa Mfalme huyo wa Moroko unaidhihirishia dunia kwa kiasi gani diplomasia ya Tanzania imeendelea kukua kwa kasi, ikiwa ni sambamba na kukuza diplomasia ya uchumi.

HABARI ZAIDI SOMA HAPA

Marehemu Omari Kungubaya azikwa jijini Dar es salaam

$
0
0
 MWANAMUZIKI mkongwe ambaye alipata umaarufu kutokana na wimbo wake Salamu za Wagonjwa Marehemu Omari Kungubaya (pichani enzi zauhai wake) amezikwa leo katika makaburi ya kifamilia Njeteni Kwembe. Msiba huo ulihudhuria na watu wengi wakiwemo majirani, ndugu, wanamuziki na wapenzi wa muziki wa Mzee Kungubaya.Tatu itakuwa siku ya Jumamosi 22/10/2016.

 Mwanamuziki Mjusi Shemboza akimfariji mmoja wa watoto wa marehemu Mzee Kungubaya
Jeneza likiwa na mwili wa marehemu Omari Kungubaya likitolewa nje tayari kwenda makaburini
Kwa picha zaidi na Anko John Kitime BOFYA HAPA

Tanzania na Uswisi zasaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano wa kisheria kwenye masuala ya Jinai

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) kwa pamoja na Mhe. Florence Tinguely Mattli, Balozi wa Uswisi hapa nchini wakisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uswisi kuhusu Ushirikiano wa Kisheria kwenye masuala ya Jinai. Mkataba huu utasaidia kuzijengea uwezo mamlaka zinazohusika na masuala ya Jinai na pia kubadilishana taarifa kuhusu masuala hayo. 
Mhe. Mahiga na Mhe. Mattli wakiendelea na zoezi la kusaini huku Maafisa kutoka Wizarani na Ubalozini wakishuhudia. Kulia aliyesimama ni Bw. John Pangipita, Afisa Mambo ya Nje na Bi. Sheila Ally.  
Dkt. Mahiga pamoja na Balozi Mattli wakibadilishana Mkataba mara baada ya kumaliza kuweka saini.
 
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvanda (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Balozi Joseph Sokoine (wa pili kutoka kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu na Bw. Pangipita (wa pili kutoka kulia).

KUTOKA MAKTABA: Maquis Original katika Pasaka Show 1988 RTD

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Bunge la nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki linaendela Visiwani Zanzibar ambapo limepokea hoja binafsi kutoka kwa mbunge wa Tanzania kuhusu kutunga sheria ya kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi. https://youtu.be/QMpPY7OZYr0

SIMU.TV: Wananchi katika kata tatu wilayani Hanang wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya kansa kutokana na kuchafuliwa kwa vyanzo vya maji wanavyotumia.https://youtu.be/v7XiAirCGj8

SIMU.TV: Serikali imesema licha ya uchumi wa nchi kukua bado theluthi ya watanzania ni masikini na kiwango cha umaskini kwa watanzania kinapungua kwa kasi ndogo sana.https://youtu.be/YQ4OIwvhZz0

SIMU.TV: Kaya nne katika kijiji cha Tindigan wilayani Siha mkoani Kilimanjaro zimebomolewa nyumba zao baada ya kujenga eneo lenye mgogoro. https://youtu.be/UMytAvpNqyQ

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam kutumia fursa ya ujio wa Mfalme wa Morocco kujenga fursa za kiuchumi.https://youtu.be/R8zbU6daA4s

SIMU.TV: Waziri wa fedha na mipango ameyataka mabenki na taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali. https://youtu.be/4alMkKCTd2E

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wamelalamikia kuendelea kutozwa ushuru licha ya serikali kupiga marufuku ushuru kwa wafanyabiashara wadogo.https://youtu.be/4KCVV8nLQUY

SIMU.TV: Kampuni ya Zuku TV inayomilikiwa na Wananchi Group imefanikiwa kuboresha huduma zake na kuongeza ajira kwa mwaka 2016. https://youtu.be/2nbsT0L-bVw

SIMU.TV: Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia mwenyekiti wao Yusuph Manji umewataka wananchama kuhudhuria mkutano wao wa dharura jumapili ili kila mmoja aweze kutoa maoni yake badala ya kuongea kwenye vyombo vya habari. https://youtu.be/uzfdFaz1TOM

SIMU.TV: Timu ya Kagera Sugar Kesho inakabiliwa na kibarua kigumu katika uwanja wake wa Kaitaba kwenye mchezo dhidi ya mabingwa watetezi timu ya Yanga.https://youtu.be/IMVEsdEk5-w

SIMU.TV: Zaidi ya wachezaji mia moja kutoka maeneo mbalimbali nchini wamejitokeza kushiriki katika mashindano ya wazi ya Gofu ya PWC katika viwanja vya Lugalo.https://youtu.be/lohkcvdeszA


Hafla ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuendeleza harakati za Albino Tanzania yafanyika Uingereza

$
0
0
 Baadhi ya Watanzania waishio Uingereza wakiwa katika hafla ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuendeleza harakati za Albino Tanzania wakiwa pamoja na Rais wa Albino Society of Tanzania Bw. Josephat Tonner aliyeketi mbele.
  Baadhi ya kinamama wa Kitanzania waishio Uingereza wakiwa katika hafla ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuendeleza harakati za Albino Tanzania wakiwa pamoja na Rais wa Albino Society of Tanzania Bw. Josephat Tonner 
 Rais wa Albino Society of Tanzania Bw. Josephat Tonner akizungumzia juu ya changamoto wanazozipata watu wenye ulemavu wa ngozi

Extended Services Limited: WE SHIP ALL TYPES OF CARGO (SEA FREIGHT AND AIR FLIGHT CARGO) TO EAST AFRICA AT UNBEATABLE RATES, i.e. BOUTIQUE STUFFS AND ACCESSORIES CONTAINERS, TRUCKS, CARS, MACHINERY ETC.

$
0
0
          
WE ARE THE MOST AFFORDABLE AND RELIABLE SHIPPING AGENT IN U.K

 

      CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 850 (TILBURY/ SHERNESS PORTS)

CAR (SALOON) TO DAR OR MOMBASA £ 750 (SOUTHAMPTON/ NEWCASTLE PORT)

4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 910 (SOUTHAMPTON PORT)

4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 945 (NEWCASTLE PORT)

4X4 TO DAR OR MOMBASA £ 930 (TILBURY/ SHEERNES PORTS)
        40’ CONTAINER TO DAR £ 1750
40’ CONTAINER TO MOMBASA £ 1750 HC
40’ CONTAINER TO ZANZIBAR £ 2300
20’ CONTAINER TO DAR £ 1220
20’ CONTAINER TO MOMBASA £ 1220
20’ CONTAINER TO ZNZ FROM £ 1600
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2650(TILBURY PORT)
        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2400(SOUTHAMPTON)

        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM £ 2450(NEWCASTLE)

        TRACTOR UNITS (KICHWA) TO DAR OR MOMBASA FROM 2612.50(IMMINGHAM PORTS)
        TRACTORUNITS(KICHWA)TODARORMOMBASAFROM£2612.50(KILLINGHAM)

        ALSOWECAN      ARRANGEPRE SHIPMENTINSPECTIONFORYOUTOAVOIDINCONVINIENCES.

·       GOOD NEWS FOR AIR CARGO CUSTOMERS FOR NAIROBI,MOMBASA AND DAR ES SALAAM!!!!!.

·         WE SHIP AIR CARGO TO NAIROBI FOR ONLY £2(EXCLUDING CLEARANCE).

·         WE SHIP AIR CARGO TO MOMBASAFOR ONLY £2.50(EXCLUDING CLEARANCE)

·         WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM FOR ONLY £2.50(EXCLUDING CLEARANCE)

·         WE SHIP AIR CARGO TO DAR ES SALAAM WITH CLEARANCE ONLY FOR £ 5

 FORMOREDETAILSPLEASE  CONTACTUSONOURCONTACTSBELOW:- EXTENDED SERVICES LIMITED, CLIPPER HOUSE, TILBURY FREEPORT, TILBURY, ESSEX, RM18 7SG Tel:+441375767890, mobile:+447438145815,EMAIL:info@extendedserviceslimited.co.uk,www.extendedserviceslimited.co.uk

Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Lesotho atembelea Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (Kulia) akimkabidhi nembo ya JWTZ Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Lesotho Luteni Jenerali Tlali Kamoli, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 21 Oktoba 16, kwa ziara ya kikazi ya kuimarisha uhusiano wa majeshi ya nchi mbili hizi (picha na JWTZ).

MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA MBEYA ATIWA MBALONI KWA KUDAIWA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA

$
0
0

Na JamiiMojaBlog

Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi wa afya katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito kujifungua mtoto akiwa amekufa.

Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama na kimetia aibu sekta ya afya.

Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, mjamzito huyo akiwa ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku, wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.

Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na kushindwa msaada wowote.

Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.

Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.

Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema siku hiyo, yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake, walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa umefungwa.

Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mates ohayo mpka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa oparesheni.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni, ndani yake kulikuwa na uzembe.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya Chunya Rehema Madusa akiwa na majonzi baada ya kumsikia mama aliyepoteza mtoto wake mara baada ya kujifungua kutokana na uzembe wa muuguzi katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Baadhi ya watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya katika Mkutano na Mkuu wa Wilya y chunya mara baada ya kutokea tukio la mama mjamzito aliyepoteza mtoto wakati akijifungua kutokana na uzembe wa mmoja wa wauguzi hospitalini hapo. 

JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHERN CALIFORNIA YACHANGIA MAAFA KAGERA Tsh milioni 10,271,150/-

$
0
0
Jumuiya ya watanzania na marafiki wa Northern California wametoa mchango wao wa kiasi cha Tsh milioni kumi laki mbili sabini na moja elfu na mia moja hamsini. (Tsh milioni 10,271,150/=) kusaidia serikali katika kukabiliana na wahanga pamoja na maafa yaliyotokana na tetemeko mkoani Kagera.
Shukrani ziwaendee wote walioweka mkono wao na nguvu zao katika kufanikisha hili zoezi bila kusahau  chama cha watanzania eneo hili la ghuba (TCO) kwa kusaidia kuratibu zoezi zima na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa.
Fedha zimetumwa katika account ya bank ya CRDB kama ilivyoelekezwa na serikali ili zifike katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera ambapo ndio shughuli zote za zoezi hili zinaratibiwa.
Katibu wa mkuu wa mkoa wa Kagera Thomas James Salala amethibitisha kiasi cha pesa hiyo kuingia katika account hiyo na kutoa shukrani kwa niaba ya mkuu wa mkoa. 
Aksanteni sana.

Erick Byorwango
Katibu  Mwenezi. 

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TAMICO yawaomba wadau kujiunga na chama

$
0
0

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Chama cha wafanyakazi wa migodini na kazi za ujenzi (TAMICO), kimewataka wadau na wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika mashirika ya ujenzi kujiunga na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa TAMICO Taifa,Mhandisi Fred Kapamila,amesema kuwa matokeo ya huru na utandawazi ni ajira isiyo na staha kwasababu makampuni yanawania kupata faida zaidi kupitia kuwapunja wafanyakazi wao.

"Tarehe 18/10/2016 chama kilifanya mkutano wake mkuu na kupata safu ya viongozi wapya hivyo uongozi mpya unawaomba watu wenaofanya kazi katika makampuni ya migodi kujiunga kwa wingi katika chama hicho hili waweze kupata msaada pindi wanapopata matatizo"amesema Kapilima.

Amesema kuwa uongozi mpya umejitayarisha vya kutosha kupambana na changamoto za kuhakikisha dhamira na matarajio ya wanachama yanafikiwa katika kipindi kijacho cha  miaka mitano.

Alitoa wito kwa serikali kuangalia upya maslahi ya wafanyakazi wa migodini ambao wamekuwa wakiteseka kila kukicha.
Mwenyekiti wa wa chama cha wafanyakazi  wa Migodi,Nishati,ujenzi na kazi nyinginezo nchini,TAMICO,Mhandisi Fred Kapimila,akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni katibu wa chama hicho,  Thomas Sabai,kushoto  Afisa elimu na mafunzo Philotea Ruvumbagu,

VYUO VYA HABARI VIJIANDAE KUTOA ELIMU BORA ILI KUENDANA NA MABADILIKO YATAKAYOLETWA NA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI.

$
0
0
Mapema Septemba 2016 kwa mara ya kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Habari nchini.

Kwa sasa Muswada huu unaendelea kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Peter Serukamba na baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa ajili kuanza kujadiliwa na wabunge.

Sasa hoja yangu naielekeza katika kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu ya Tatu (c) Uthibitishwaji wa wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2) vinaelezea kuwa Mtu hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari isipokuwa kama mtu amethibitishwa na Sheria hii na (2) inasema mtu ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi wa habari ataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi utakaoainishwa katika kanuni.

Ukisoma kifungu hiki na sehemu zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo ambavyo mwandishi wa habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze kumthibitisha kuwa mwandishi wa habari kamili na baadae kumpatia Press Card.

Tukiangali kwa mifano tu ya taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka kwa Bodi zao utaona kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na kwa mfano wanasheria ili kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri wa kuwa Wakili unabidi uwe na Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya baadhi ya mitihani ya kufuzu ili kudhibitishwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MPAMBANO WA MISS TALENT 2016 JINSI ULIVYOFANA, MSHIRIKI WA MISS TANZANIA, 2016 NO. 20 AIBUKA KIDEDE.

$
0
0
Miss Talent 2016 ambaye ni Mshiriki wa Miss Tanzania 2016 namba 20 ameshika nafasi ya Kwanza katika mpambano wa Kusaka Vipaji kwa washiriki wa Miss Tanzania 2016 uliofanyika Jembe Beach jijini Mwanza leo. Mshindi huyo wa Miss Talent 2016 amecheza ngoma ya asili.
Top 5 Miss Talent 2016 wakiwa wamepozi mara baada ya kushinda nafasi tano Bora ya Miss Talent 2016.
Mamiss Tanzania 2016 wakionesha Vipaji vyao wakicheza  katika hafla ya Kutafuta Miss Talent 2016 leo jijini Mwanza.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii Mwanza.


YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO October 22, 2016

$
0
0



SIMU.tv: Mtazame bondia  Thomas Mashali akizungumzia pambano lake la kimatifa litalofanyika mwezi Disemba mwaka huu mkoani Morogoro; https://youtu.be/zjnTtNx6LZ0

SIMU.tv: Spika wa Bunge Job Ndugai awashauri wakuu wa idara mbalimbali wa halmshauri ya wilaya ya Kongwa kutumia vizuri fedha za miradi ya maedeleo; https://youtu.be/QXTF8S4V8dM

SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Mwanza aunda kamati kuchunguza tuhuma ya kughushi takwimu za idadi ya wanafunzi katika shule za msingi; https://youtu.be/0u9BU49LkZ4

SIMU.tv: Serikali inatarajia kutangaza safu ya milima ya Mbeya kuwa sehemu muhimu ili kutunza mazingira na maji yanayopatikana;https://youtu.be/8rUKD5hXaMA

SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Kagera awataka wananchi mkoani humo kuacha tabia ya kuchoma moto misitu katika harakati za kutunza mazingira; https://youtu.be/wuGtgH41IvE

SIMU.tv: Wanawake wa kabila la kimasai mkoani Mbeya wapinga zeozi la utambuzi wa mifugo kwa kupiga chapa;https://youtu.be/lbH8Edjw9KE

SIMU.tv: Taasisi ya GSM yaelezea kusikitishwa na mwitikio wa wazazi wa mkoani Tabora wa kuwapeleka watoto wenye vichwa vikubwa kupatiwa matibabu; https://youtu.be/8zWm7l1wKpA

SIMU.tv: Makamu wa Rais Samiha Suluhu akutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Iran anayemaliza muda wake nchini;https://youtu.be/Tlq_ux8Yy1I

SIMU.tv: Baadhi ya wakulima wilayani karatu waiomba serikali kuwaboreshea miundombinu ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji;https://youtu.be/khOu5eI9giI

SIMU.tv: inaelezwa kuwa hosptali ya mkoa wa Singida inakabiliwa na uhaba wa dawa pamoja na vifaa tiba;https://youtu.be/Zz2KTi6QAOM

SIMU.tv: Rais  wa Zanzibar , Dkt. Shein aipongeza wizara ya habari utalii , utamaduni na michezo kwa kutekeleza vyema majukumu yake;https://youtu.be/TqjhlDcb_Mg

SIMU.tv: Rais John Magufuli asema serikali yake ya awamu ya tano haitakuwa tayari kuona wanafunzi wa vyuo nchini wakisoma kwa shida; https://youtu.be/0PXoFgH0gME

SIMU.tv: Serikali yawataka watumishi wa umma kuwahudumia wananchi wote bila ubaguzi; https://youtu.be/LQhgmouIZEQ
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images