Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 12 | 13 | (Page 14) | 15 | 16 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Mapema leo asubuhi katika eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge Basi la abiria la 'Bunda express" lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza lilipata ajali mbaya sana kwenye eneo hilo na Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda katika eneo la tukio kuhofia usalama wa abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo kwani,basi lilipinduka kabisa na tairi zikielekea juu, lilitumbukia kwenye majaruba ya mpunga, huku likiwa limepondeka vibaya upande mmoja.chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha jijini Mwanza leo na basi hilo lilikuwa likitembea kwa mwendo wa kasi pia.
  Hali ya uokoaji iliathiriwa na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha eneo hilo na ni abiria wachache tu ndio waliweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hilo ili wapate kujisitiri.
  Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao. Picha na G Sengo Blog.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe-Mb., akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe.Vicente M. Veloso. Hafla hiyo ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Waziri Membe leo.  
  Mhe. Balozi Veloso aliye kushoto akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule huku Mhe. Membe akishuhudia.
   Mhe. Membe akifafanua jambo kwa Mhe. Balozi Veloso wakati wa mazungumzo yao mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Nakala ya Hati zake za Utambulisho  
  Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Veloso huku Afisa kutoka Ubalozi wa Msumbiji hapa nchini, Bi. Helena Sitore akinukuu mazungumzo yao.

  0 0

  Meneja Usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania, Sylvester Manyara(kushoto),Msimamizi wa Bahati na sibu Tanzania, Abdalah Hemed na Mkufunzi wa Samsung Tanzania, Joel Laizar wakionyesha zawadi za washindi mara baada ya kuchezesha droo ya Samsung ya msimu wa sikuu ya X’mass na Mwaka mpya Dar es Salaam.Zawadi zote zinathamani ya shilingi milioni 6.
  Meneja Usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania, Sylvester Manyara akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya Samsung ya msimu wa siku kuu ya X’MASS NA mwaka mpya jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Na Mwandishi wetu 

  WAWAKILISHI wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani wataendesha semina kwa wadau wa michezo hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.

  Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .

  Wakiwa nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao utangazwa hapo baadaye.

  Ziara hiyo ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na wadau wa michezo nchini na ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester United.

  Kwa kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA), wawakilsihi wa timu hiyo pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH na Chuo kijulikanacho kwa jina la Washington State University's Paul G. Allen School for Global Animal.

  "Ziara hii itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.

  Alisema kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009.

  Mpango huo una lengo la kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.

  0 0


  Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

  Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:

  1.      Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila
  2.      Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru
  3.      Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA
  4.      Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba
  5.      Majadiliano
  6.      Documentary za Regia Mtema
  7.      Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema
  8.      Chakula cha jioni
  9.      Networking  Wasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams

  Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820

  RMF inawaomba Wanahabari wote wasaidie kusambaza mwaliko huu.

  Wasalaam

  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanachama wa UVCCM wa vyuo vikuu mkoani Tabora waliomtembelea Ikulu ndogo mkoani humo usiku wa kuamkia leo. Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete aliwataka vijana hao kuzingatia masomo kwa nguvu zao zote, akisisitiza kwamba elimu ni ufunguo wa maisha hivyo wasome kwa bidii ili nchi ipate wasomi waliobobea katika kila nyanja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
   Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe, Fatma Abubakar Mwassa (mwenye kitenge, kati) na Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Mhe Suleiman Kumchaya (kulia) wakipozi na viongozi wa wanafunzi wa UVCCM vyuoni
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa UVCCM wa vyuoni Tabora
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa jumuiya hiyo vyuoni Tabora
   Juu na chini Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wana UVCCM vyuoni Tabora

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na makada hao wa UVCCCM

  0 0
 • 01/10/13--07:23: Article 24


 • 0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Valerie Msoka akikabidhi maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine toka kulia  ni Wajumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim, Bw. Simai Mohammed na Bi. Jessica Mkuchu.

  0 0

  Mwenyekiti wa asasi  ya siasa ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine ambao ni wajumbe wa asasi hiyo wakati wa mkutano wa siku moja uliofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini,Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji(Watatu kushoto),Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia) na wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dr.Tomaza Salomao. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0

   Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
   Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
   Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
   Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
   Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
   Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
   Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
   Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzindzi huo
  KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo wakati wa uzinduzi huo
   Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
   KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee,  kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani
   J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
   Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
   BAADAYE: Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
   Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini
   Kariati akionyeshwa maeneo yaliyoathirika
  Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzindizi wa Kampeni ya kilimo kwanza na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha zote na Bashir Nkoromo

  0 0
 • 01/10/13--08:51: Article 20


 • 0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akisalimiana na Mhe. Armando Emillio Guebuza, Rais wa Msumbiji mara baada ya Rais huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo. Mhe. Guebuza ni miongoni mwa Marais wanaohudhuria Mkutano Maalum wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA) unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2013.
  Mhe. Guebuza (kushoto) akifuatana na Waziri Membe mara baada ya kuwasili
  Mhe. Rais Guebuza wakati alipokuwa akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili nchini.
  Mhe. Rais Guebuza akiangalia ngoma za utamaduni (hazipo pichani) zilizokuwa zikitoa burudani kiwanjani hapo mara baada ya kuwasili.
  Moja ya kikundi cha utamaduni kilichokuwa kikitoa burudani kwa Mhe. Rais Guebuza alipowasili nchini.

  0 0

  Mmoja wa Wawakilishi wa Kundi la Wafugaji waliokutana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan. 10, 2013) Bi. Lilian Looloitai akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bw. Adam Ole Mwarabu na kushoto ni Bw. Joseph Parsambei.
  Mmoja wa Wawakilishi wa Kundi la Wafugaji waliokutana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan. 10, 2013) Bi. Esta Labani akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakifuatilia mkutano kati yao na Wawakilishi wa Wafugaji uliolenga kupata maoni ya kundi hilo kuhusu Katiba Mpya. Kutoka kushoto ni Bi. Maria Kashonda, Dkt. Senondo Mvungi na Bw. Yahya Msulwa.
  Baadhi ya Wawakilishi wa Wafugaji waliokutana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan. 10, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya wakifuatilia mkutano.

  0 0

  Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kwa ukanda wa Afrika Mashariki Stephen Isaboke ambapo amesema Wateja wa huduma za Dstv nchini Tanzania wametakiwa kutokuwa na hofu ya kupata muingiliano au kukatika kwa picha katika kipindi hichi cha kutoka analogia kwenda digitali.

  Barbara Kambogi amesema watanzania ambao wamejiunga na Dstv hawatahitaji kuhama kwa kuwa Dstv iko katika mfumo wa digital tangu awali.

  Ameoneza kuwa Dstv imekuwa ikitoa huduma za digital televisheni kwa Tanzania kwa kipindi cha miaka 17 iliyopita, ambapo wateja wake wameweza kupata channel nyingi zaidi za kuchagua zikiwa na picha safi na sauti bora.

  Kupitia vifurushi tofauti vinavyotolewa na Dstv wateja wanakuwa na maamuzi ya kuchagua kifurushi anachotaka na bei ambapo Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas inaendelea pamoja na punguzo la asilimia 10 la kufanya malipo kabla ya muda uliolipia huduma kumalizika. Kulia ni Operation Manager wa Multichoice Tanzania Bw. Ronald Baraka Shelukindo.
  Managa Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifafanua jambo kuhusu Televisheni nyingine kuingizwa katika huduma za DStv na kusema suala hilo litategemeana na makubaliano na mikataba na wamiliki pamoja na kutegemea uwezo wa Satelite.

  Kwa Tanzania DStv inamkataba na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) la kuichukua TBC katika DStv Platform ambapo itakuwa inaonekana bure hata kama hujalipia king'amuzi chako chaneli hiyo haikatwi.

  Bw. Shelukindo amewataka Watanzania kuendelea kununua ving'amuzi vya DStv kabla ya kuisha kwa Ofa ya msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mayor of Ilala Municipal Council who also is The Councilor for the Gongo La Mboto Ward His worship Jerry Silaa visited various projects in his ward amongst them being in mtaa wa Gulukakwalala whereby he visited a dispensary which he built between 2005-2010 and he personally pledged to get it equipped with various instruments to measure diabetes, blood pressure and a portable ultrasound machine.

  0 0

  Wahariri - Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa maoni ya wananchi na kuwa Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) kwa ujumbe wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
  Wahariri - Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Mohammed Khamis Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa Ujumbe wa Taasisi za Habari nchini uliotembelea ofisi za Tume leo (Januari 14, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
  Wahariri - Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Assaa Rashid (wa pili kulia), akitoa ufafanuzi uhifadhi wa maoni ya maandishi yanawasilishwa na wananchi katika Tume kwa wadau wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (Januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha  Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF). Picha na Tume ya Katiba. 

older | 1 | .... | 12 | 13 | (Page 14) | 15 | 16 | .... | 3272 | newer