Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1396 | 1397 | (Page 1398) | 1399 | 1400 | .... | 3270 | newer

  0 0  VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

  Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

  Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).

  Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .
  Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru Broun
  Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi, Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu, wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Robi Bwiru. 
  Kaimu Mkurugenzi, Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Bernard Haule akiongea na waandishi

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

   


  Simu:255-22-2114615, 211906-12
  Barua pepe: nje@nje.go.tz
  Barua pepe: gcu@nje.go.tz

  Nukushi: 255-22-2116600

                

   

                  20 KIVUKONI FRONT,
                             P.O. BOX 9000,
                    11466 DAR ES SALAAM, 
                                      Tanzania.

   

  Mchakato wa kuanzisha Viza ya Pamoja ya Utalii katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Ndugu wanahabari:

  Wiki iliyopita baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii ya hapa nchini na nje ya nchi iliandika taarifa kuhusu Tanzania kujitoa au kugomea utaratibu wa visa ya pamoja ya utalii (Single Tourist Visa) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

  Kufuatia taarifa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekuwa ikipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kutaka kufahamu ukweli wa jambo hilo. Hivyo, Wizara imeona leo itoe taarifa rasmi kufafanua namna ya mchakato wa uanzishwaji wa viza ya pamoja ya utalii ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unavyoendelea.


  Suala la Uanzishwaji wa Viza ya Pamoja ya Utalii kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki bado liko katika majadiliano ya Nchi Wanachama kupitia Vikao vya Sekta ya Utalii na Wanyamapori. Katika kufanikisha azma hii,  Baraza la Kisekta la Mawaziri wa  Maliasili na Usimamizi wa Wanyamapori uliofanyika  tarehe 1 Novemba 2008 liliunda Kikosi Kazi kwa ajili ya kufanya  utafiti kwa lengo la kubainisha mahitaji na utayari wa Nchi wanachama juu ya kuanzisha  Viza ya Pamoja ya Utalii.  Utafiti uliofanyika mwaka 2010, ulibainisha masuala muhimu yafuatayo ya kuzingatiwa kabla ya kuanzishwa kwa Viza ya Pamoja ya Utalii:


  a)    Kurazinisha  (harmonization) sheria za Viza za Nchi Wanachama;

  b)     Idara ya Uhamiaji  kuanzisha Mfumo  wa  kudhibiti Usalama;

  c)     Utoaji wa Viza kuwa wa kielektroniki;

  d)   Kuwepo kwa mfumo wa ukusanyaji na ugawanyaji wa mapato pamoja na namna ya kulipa;

  e)     Kuwepo kwa maafisa uhamiaji katika kila ofisi za ubalozi;

  f)      Kujenga uwezo wa watumishi kwenye suala la  mfumo wa kieletroniki  wa utoaji wa viza ya pamoja ya Utalii.


  Kufuatia matokeo ya utafiti huo, Mkutano wa 5 wa Baraza  la Kisekta la Mawaziri wa Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori  uliofanyika  mwezi Julai 2013  jijini Bujumbura, Burundi pamoja na mambo mengine uliagiza kuundwa kwa kikosi kazi ambacho kitajumuisha wataalamu kutoka Taasisi za Uhamiaji, Utalii, Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tehama, Usalama, na Sheria katika nchi wanachama ili  kuandaa mpango kazi  na  kushughulikia masuala yote ambayo  yatajitokeza kuhusiana  na uanzishwaji wa  Viza ya Pamoja ya Utalii. Hata hivyo, kabla ya utekelezaji wa maagizo hayo, Nchi za Uganda, Kenya na Rwanda zilianzisha  Viza ya Pamoja ya Utalii baina yao nje ya vikao vya Jumuiya.


  Ni vema ikaeleweka kwa umma wa Watanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla kuwa kwa kuzingatia Mfumo wa Maamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao ni wa kukubaliana kwa pamoja (consensus) hakuna Mfumo wowote wa uanzishwaji wa Visa ya Pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanzishwa. Hii inamaanisha kuwa hakuna Visa ya Pamoja ya Utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokubalika. Kwa mantiki hiyo, taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari hazina ukweli wowote na zilikuwa na lengo la kuichafua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


   Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawawahakikishia umma wa Tanzania kuwa itaendelea kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya Jumuiya na kushiriki katika majadiliano ya kuanzisha visa ya pamoja ya utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

  Dar es Salaam, 18 Oktoba  2016.


  0 0  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

  Wanamuziki mahiri wa Muziki wa Taarab, Khadija Kopa,Mwanahawa Ally na Kahadija Yusufu, wanatarajia kuwaburudisha wakazi wa  mji kasoro bahari (Morogoro)  katika tamasha la Muziki litakalokwenda sambamba na zoezi zima la uchangiaji damu.

  Akiwatambulisha wasanii hao mapema jijini Dar es Salaam leo Mratibu wa Tamasha hilo ,Hamis Mkongowale(Kajumulo), amesema kuwa tamasha hilo linalenga la kuihamasisha jamii katika suala zima la uchangiaji damu,ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu, hasa wakina Mama na watoto ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

  "Pamoja na yote haya kutakuwa na maonesho ya uuzaji wa bidhaa mbalimbali kutoka kwa wadau na wajasilimali, hivyo zoezi hili la uhamasishaji litaanza siku tano kabla ya Tamasha husika,ili wananchi wapate huduma husika kwa kukusanya damu kwa wingi kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu"amesema Kajumulo.

  Aliongeza kuwa tatizo la kuona jamii inapoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu ni aibu kwa nchi kama hii yenye wakazi zaidi ya milioni 25.

  Kwa upande wake gwijinwa muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa aliwaomba wakinamama na wakzi wa morogoro wajitokeze kwa wingi siku ya Tamasha hilo hili waweze kufanikishamkuokoa maisha ya wanawake wenzao.
  Mwanamuziki mkongwe wa Muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uwepo wake katika Tamasha la muziki na uchangiaji damu Desemba 25 Mkoani Morogoro.
  Mwenyekiti wa Asasi ya Tegemeo Arts na mratibu wa Tamasha hilo Hamis Mkongowale (Kajumulo) Katikati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna tamasha hilo litakavyofanyika.


  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi kufuatia vifo vya watu 11 vilivyosababishwa na ajali ya basi la kampuni ya Barcelona iliyotokea jana tarehe 17 Oktoba, 2016 katika eneo la Miteja Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

  Basi hilo lenye namba T 101 CUU lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kijiji cha Mahuta katika Wilaya ya Newala Mkoani Lindi, lilipinduka baada ya gurudumu lake la kushoto kupasuka na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na mwingine 1 kufariki dunia baadaye akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Lindi, huku watu wengine 43 wakiwa wamejeruhiwa.

  Katika salamu zake, Rais Magufuli amesema amepokea taarifa za vifo vya watu hao kwa mshituko na huzuni kwa kuwa kwa mara nyingine Taifa limepoteza watu wake na familia zimepoteza wapendwa wao na watu ambao ziliwapenda na kuwategemea.

  "Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa wote waliopoteza jamaa na ndugu zao katika ajali hii, kwa hakika nimeguswa sana na vifo hivi na naungana na familia za marehemu wote katika maombolezo na sala"amesema Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli amewasihi wote walioguswa na vifo hivyo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi na amewaombea Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

  Pia Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa,
    
  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  18 Oktoba, 2016. 

  0 0


  Na Lulu Mussa-Kilombero

  Wananchi wa Kijiji cha Katurulika, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro wameahidiwa Mifuko mia moja ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa zahanati katika tarafa yao inayohudumia wakazi wa vijiji sita.

  Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kutoa mifuko hiyo ndani ya wiki moja ikiwa ni pongezi kwa Kijiji hicho kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira na msitu wa Magombera.

  Awali, Bwana Dandidius Songela alimfamisha Waziri Makamba changamoto wanazokutana nazo katika Kijiji chao kuwa, ni pamoja na mgogoro baina ya Kijiji cha Katarukila na mwekezaji anayehodhi sehemu ya eneo la Kijiji na kusababisha uharibifu wa mazingira. Waziri Makamba aliwasihi wanachi wa Kijiji cha Katarulika kuwa ni jukumu lao msingi kulinda msitu huo kwa nguvu zao zote na kubainisha kuwa Hifadhi endelevu ya mazingira ndio mustakabali wa maisha yao.

  Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kumpa mwekezaji huyo “Restoration Order” kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa kumtaka arejesha mazingira katika hali yake ya asili, kwakuwa ni eneo tengefu.

  kwa upande mwingine Waziri Makamba amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilombero Bw. Dennis Londo kuhakikisha wanasheria wa Manispaa wanahudhuria kesi baina yao na mwekezaji huyo bila kukosa kila inapotajwa na baada ya kuhumu kutolewa Waziri Makamba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kwa kina endapo kulikua na mianya yoyote ya rushwa katika mchakato wa kumilikisha ardhi ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara.

  Waziri Makamba yuko ziarani Kilombero kuangalia changamoto za mazingira na awali alitembelea Mto Mkondoa Wilayani Kilosa.

  Sehemu ya kingo za Mto Mkondoo zilizoharibiwa na uharibifu wa mazingira Wilayani Kilosa 
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba katika mkutano na wananchi katika Kijiji cha Katarukila akiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Katurukila na kuwapongeza kwa kuwa Kijiji cha mfano kwa kuonyesha jitihada za dhati za kuhifadhi mazingira. 
  Bwana Candidius Songela akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akingalia ramani inayo onyesha eneo lenye mgogoro baina ya wanakijiji wa Katarukila na mwekezaji. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo

  0 0


  KICHUNYA MCHEZAJI BORA SEPTEMBA VPL 

  Mshambuliaji Shiza Kichuya wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa 2016/2017.

  Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.
  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


  LIGI DARAJA LA PILI KUANZA OKTOBA 29, 2016

  Timu 24, zinatarajiwa kupambana katika michuano ya Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 kuanzia Oktoba 29, mwaka huu, imefahamika.

  Timu hizo zimepangwa katika makundi manne yenye timu sita kwa kuangalia zaidi jiografia au kanda ambako timu imetoka – lengo likiwa kupunguza gharama kwa timu shiriki hasa ikizingatiwa kuwa michuano hiyo haijapata mdhamini hadi sasa.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini  VPL: TIMU 12 UWANJANI KESHO, AZAM NA MTIBWA SAA 1.00 USIKU

  Wakati leo Jumanne Oktoba 18, 2016 timu ya JKT Ruvu ya Pwani na Kagera Sugar zinafungua rasmi mzunguko wa 11 wa Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), michezo mingine sita itafanyika kesho Jumatano Oktoba 19, mwaka huu wakati keshokutwa Alhamisi Oktoba 20, kutakuwa na mchezo mmoja tu.

  Mchezo wa leo Na. 86 wa VPL utafanyika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani kabla ya kesho Oktoba 19, mwaka huu kuendelea kwa mechi sita pia za mzunguko 11 wa kukamilisha raundi ya kwanza kwa msimu 2016/17.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


  0 0

  WAFANYABISHARA Mkoani Shinyanga, wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kusajili majina ya biashara zao katika zoezi linaloratibiwa na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kutambulika kisheria na kuchangia mapato ya Serikali.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Bi. Zainabu Telack, amewahamasisha wafanyabiashara mkoani humo kutumia fursa ya kuwepo maofisa wa BRELA kutoka makao makuu ya BRELA kurasimisha biashara zao na kujifunza umuhimu wa kusajili majina ya biashara.

  “Tumepata bahati kubwa kutembelewa na maofisa wa BRELA ambao wanaendesha semina kwa wafanyabiashara na wakati huo huo kusajili majina ya biashara,” Bi.Telack alisema hayo mkoani hapa jana wakati wa semina ya wiki moja ya uhamasishaji wa usajili majina ya biashara inayoratibiwa na BRELA.

  Alisema azima ya serikali ya Awamu ya Tano ni kuwekeza katika biashara na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa lengo kubwa kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira na kukuza kipato cha watanzania.

  “Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwashukuru na kuwapongeza BRELA kwa zoezi ili la uhamasishaji kwani ni matumaini yangu mwitikio utakuwa mkubwa sana,” alisema na kuongeza kuwa Shinyanga itakuwa mfano wa kuigwa katika urasimishaji biashara.

  Afisa mtendaji mkuu wa BRELA, Frank Kanyus, akiainisha faida za usajili wa biashara, amesema pamoja na mambo mengine kutasaidia serikali kupata mapato ili iweze kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi, alisema Wakala umejipanga na zoezi la kuzunguka nchi nzima kutoa elimu na faida za kusajili majina ya biashara nchi nzima.

  “Mikoa ambayo tumeshafanya semina tulipata mwitikio mkubwa na pia watu wengi walijitokeza kusajili majina ya biashara zao,” alisema na kuongeza kuwa wakala ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kurasimisha shughuli zao.Alisema tayari BRELA imeshatoa semina katika mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu na Geita ambapo wiki ijayo semina za uhamasishaji zitafanyika mkoani Tabora.

  Naye, Afisa Mtendaji wa Chama cha wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mkoani Shinyanga, Bi.Malicelina Saulo,alisema jumuiya ya wafanyabiashara imefuruhishwa na semina yenye lengo la kuwajengea uelewa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kusajili majina ya biashara zao.

  “Hii ni fursa pekee kwa wafanyabishara mkoani Shinyanga kujisajili majina ya biashara zao na kuwaondolea usumbufu wa kusafiri umbali mrefu hadi Dar es salaam,” alisisitiza.

  0 0

  Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC) imejipanga kuwekeza katika sekta ya viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ili kuchangia kukuza uchumi wa taifa na ajira.

  Akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa kampuni hiyo jijiji Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Aloys Mwamanga, imejipanga kuanzaisha viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo, lakini hakutaja idadi ya viwanda na kiasi kitakachotumika. 

  Alipoulizwa nje ya mkutano sababu za kuwekeza katika viwanda hivyo, alisema kampuni inaunga mkono kwa dhati dhamira ya serikali ya kuwekeza katika sekta ya viwanda na hasa viwanda vya kusindika mazao. Kampuni imepata faida ya shilingi 564.18 milioni kabla ya kodi.

  Bw. Mwamanga amefafanua kuwa kampuni yao ni Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja ambayo imejitokeza kuwa mfano wa kuigwa nchini, na kuongeza kwamba pamoja na ongezeko la gharama za uendeshaji kwa sababu ya kupanuka kwa shughuli za kampuni bado ina uwezo wa kuwekeza. Mwaka 2014 kampuni ilipata faida ya shilingi 784.23 milioni.

  Mwenyekiti huyo amesema kwa uwezo iliyonao, kampuni imepanga kuwekeza pia katika dhamana za serekali na makampuni, amana katika mabenki, uanzishaji wa microfinance, ujenzi wa jingo la ofisi na maghala ya kuhifadhi bidhaa.

  Alisema uwekezaji huu utakapo kamilika utawezesha wanahisa kupata fedha nyingi zitakazo tokana na gawio la kila mwaka.Amefafanua kuwa kutokana na kushuka kwa thamani ya hisa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam, mtaji wa kampuni uliathirika kidogo na kupungua kutoka. bilioni 34.56 Desemba 31 mwaka 2014 kufikia bilioni 31.95 Desemba 31, mwaka 2015. 

  Kampuni ilipoanza shughuli za biashara Octoba,Mosi, 2005 mtaji wake ulikuwa sawa na bilioni 1.97, alieza Bw. Mwamanga.Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori alisema kampuni inakusudia kujiorodhesha katika Soko la Hisa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata mtaji na kufanya uwekezaji zaidi kwa manufaa ya wanahisa na nchi.

  “Lengo letu ni kuuza jumla ya hisa 112,500,000 kwa bei ya shilingi 400 kwa kila hisa moja,” na aliongeza kusema kuwa kama hisa zote zitauzwa, watapata bilioni 45.Mmoja wa Wanahisa, Dkt. Tom Maeda, kutoka Hanang, Mkoa wa Manyara ameunga mkono dhamira ya kampuni ya kupanua uwekezaji ili kuongeza mtaji utakao fungua fursa zaidi.

  Aliwataka wanahisa wenzake na Watanzania kununua hisa zitakapotangazwa sababu hisa ni uwekezaji ni ukombozi wa mtu anayenunua hisa.Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA ina wanahisa wake 2,443 na ina rekodi ya kufanya mkutano mkuu kila mwaka.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment Plc),Mhandisi Aloys Mwamanga (katikati) akifungua Mkutano Mkuu wa Kumi na Moja (11) wa wanahisa wa kapuni hiyo. (Kulia) ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori na kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Bi. Hanim Babiker. (Picha na mpiga picha wetu, Dr es Salaam).

  Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC), Bw. Donald Kamori (kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji kwa mkutano mkuu wa kumi na moja (11) wa kampuni hiyo, ambapo wanahisa walikutana kujadili maendeleo ya kampuni yao, (katikati)ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo,Mhandisi Aloys Mwamanga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti,Bi. Hanim Babiker.

  Wanahisa wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC), Bw. Donald Kamori hayupo pichani wakati wa mkutano mkuu wa kumi na moja (11) wa kampuni hiyo. (Picha na mpiga picha wetu, Dr es Salaam

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mkoa wa Lindi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaoharibu mazingira kwa kufyeka na kuchoma moto misitu kwa sababu wanaharibu mazingira na kusababisha ukame.

  Amesema mkoa huo upo hatarini kugeuka jangwa na tayari vyanzo vingi vya maji vimeanza kukauka kwa sababu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na watu kufanya shughuli za kijamii kwenye vyanzo vya maji.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 18, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Nanjaru, Nachinyimba, Nambiranje, Mkaranga, Nandenje, Nachinyimba na Mandarawe.

  Amesema wakulima wa ufuta wanatakiwa kuendelea kutumia mashamba yao ya zamani na kuacha tabia ya kufyeka misitu kila mwaka na badala yake waanzishe mpango wa upandaji miti ili kuepusha taifa kugeuka kuwa jangwa.

  “Vyanzo vya maji vimekauka kwa sababu tumekata miti mingi. Mito yote iliyokuwa inatiririsha maji imekauka. Viongozi wa mkoa hakikisheni misitu inalindwa na atakayekutwa analima kwenye vyanzo vya maji akamatwe,” amesema.

  Waziri mkuu aliongeza kuwa “Ukataji miti huu unaoendelea katika maeneo yetu  hakutosababisha kukosekana kwa maji tu, bali  hata mazao yatapungua. Jambo hili  itasababisha njaa katika vijiji vyetu, hivyo tuache kukata miti.

  Waziri Mkuu amesema kwa sasa Serikari inatumia gharama kubwa kuchimba visima virefu kutafuta maji. Amesema zamani walikuwa wanachimba mita 20 au 30 wanakuta maji na gharama yake ilikuwa sh. milioni 35, ambako kwa sasa wanalazimika kuchimba mita zaidi ya 150 kwa gharama y ash milioni 75 kwa kisima kimoja.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi,amewataka watendaji wa kata na vijiji kuimalisha ulinzi wa maeneo ya misitu na maji, na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  “Hatuko tayari kutengeneza jangwa hivyo tutapamba na wale wote wenye tabia za kuchoma moto misitu au kulima kwenye vyanzo vya maji,” amesema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMNNE, OKTOBA 18, 2016

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi akizungumza na wakazi wa Magomeni Suna, Jijini Dar es Salaam leo, baada ya kusikiliza kero zao.

  Na Humphrey Shao,
  Globu ya Jamii.

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi, amemwagiza Mkuu wa Polisi Kanda ya Magomeni Salum Morcase, kufanya uchunguzi wa kina katika nyumba zinazo sadikiwa kuwa zinahifadhi katika kata ya Magomeni Makuti.

  Hapi alitoa agizo hilo, baada ya kusikiliza kero ya wanachi wa kata ya Magomeni Suna, waliolalamika kuna nyumba inayotunza wahalifu imekuwa tishio katika mtaa wa Makuti.Hapi alimwagiza Mkuu wa Polisi kufanya doria katika eneo hilo, kwani nyumba hiyo imekuwa kero kwa wananchi.

  Mbali na kuwakamata wahalifu hao, DC Hapi aliagiza mmiliki wa nyumba hiyo kukamatwa ili aweze kuisaidia Polisi kukamatwan kwa wahalifu hao. Naye Mkazi wa eneo hilo Sabrina Ibrahimu alisema kuwa  nyumba hiyo inatunza vibaka, wavuta bangi, ambao wamekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwaibia fedha na mali zao.
  Ibrahim alisema kuwa, vijana wanaoishi katika nyumba hiyo wamekuwa wakivuta bangi nje ya adhara, huku wakiwahalaso hata watoto wa shule wanaopita nje yanyumba hiyo wakielekea shule.Aidha mkazi huyo alidai kuwa, nyumba hiyo imekuwa tishio katika maeneo hayo, huku Polis wakionekana kutochukua hatua yoyote licha ya kuwa jershi hilo linataarifa za uhalifu huo.

  0 0

  Na Editha Karlo, wa blog ya jamii,Missenyi

  SHULE ya msingi Byamutemba iliyopo katika kata ya Nsunga Wilayani Misenyi imefungwa kwa muda wa wiki tatu,kufuatia shule hiyo mapaa yake kuezuliwa na upepo mkali.

  Tukio  hilo limetokea leo majira ya mchana wakati wanafunzi wakiendelea na masomo darasani na kusababisha baadhi ya wanafunzi kujeruhiwa.Upepo huo umeezua mapaa ya shule hiyo nyumba moja ya mwalimu pamoja na nyumba tatu za wakazi wa kijiji cha Byamutemba.

  Mganga msaidizi wa Wilaya ya Missenyi Godon amekiri kupokea wanafunzi hao waliojeruhiwa 14 na wanafunzi 7 wakirudishwa nyumbani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Zahanati ya Igayaza.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denis Mwila alisema kuwa wameifunga shule hiyo kwa miezi mitatu wakati wanafanya utaratibu wa kuijenga shule hiyo kwa haraka.

  Alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 903.
  Shule ya msingi Byamutemba iliyoko kata Nsunga Wilayani Missenyi imeezuliwa na upepo mkali na kupelekea Wanafunzi saba kujeruhiwa,kufuatia tukio hilo, shule hiyo kwa sasa imefungwa kwa muda.
  Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wamelazwa baada ya kujeruhiwa na tukio hilo
  Baadhi ya wananchi wakijadiliana jambo kufutia shule hiyo kuezuliwa na upepo mkali .
   

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto) na Nirina Kiplagat, walipofika kwa ajili ya kujadiliana juu ya masuala ya amani na maendeleo.Kulia ni Katibu wa naibu waziri, George Mwansasu.Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam. 
  Meneja Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Katikati ni Mshauri wa Mradi kutoka UNDP, Lawrence Lachmansingh. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Mshauri wa Mradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto), akizungumza na Naibu Waziri waWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Watatu kushoto ni Meneja Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba hujulikana kama wiki ya huduma kwa mteja na huadhimishwa duniani kote. Benki ya NMB imeamua kuendelea kusherehekea huduma kwa mteja kwa mwezi mzima ili kuonyesha jinsi inavyomjali mteja kibiashara, kimaendeleo pamoja na amani kwa ujumla. NMB imejikita kwenye kutoa huduma bora zinazofikia malengo ya wateja wa ndani na nje.

  Kutana na Meneja Mwandamizi  wa huduma kwa wateja wa NMB, Amanda Feruzi anayetuelezea maoni binafsi na ya kampuni kuhusu huduma kwa mteja na kwanini ni muhimu kuadhimisha huduma kwa mteja.

  Mimi: Karibu sana Amanda, tuanze kwa kufahamu jukumu lako ni nini?
  Amanda: Jukumu langu ni kutengeneza, kuratibu, kufuatilia na kupima ubora wa huduma kwenye benki


  Mimi: Huduma kwa mteja inamaanisha nini kwako na kwenye benki kwa ujumla?

  Amanda: Binafsi, naamini kwamba huduma kwa mteja ni kuwaheshimu na kuwajali wateja kwa kutumia weledi kufanikisha mahitaji yao. Kama shirika – huduma kwa wateja ni jambo la msingi sana hapa NMB na ndio maana kila siku tunaboresha huduma na bidhaa zetu ili kufanikisha malendo ya wateja wetu.


  Mimi: Kwanini ni muhimu kuwa na wiki ya huduma kwa mteja?

  Amanda: Wateja wetu (wa ndani na nje) ndiyo sababu ya sisi kuwa na mafanikio. Kwahiyo, tunasherehekea mchango wao na kuwaahidi kwamba TUNAWAJALI kwa kuwa sehemu ya mafanikio yetu.

    
  Mimi: Ni kitu gani cha muhimu sana cha kufuata unapokuwa unamhudumia mteja?

  Amanda: Kitu cha msingi sana wakati wa kumhudumia mteja ni kuhakikisha mahitaji na matarajio yake yanafikiwa. Inapotokea kwamba kwa namna moja au nyingine hatujafikia matarajio ya mteja wetu, tunachukua mrejesho na kulifanyia kazi suala hilo.


  Mimi: Msemo wa “mteja ni mfalme” una ukweli kiasi gani?

  Amanda: Tunaposema mteja ni mfalme, tunarudi palepale kwenye kutilia msisitizo wa kusherehekea wiki ya huduma kwa mteja. Mteja ni mfalme kwa sababu ndiye sababu ya sisi kufanikiwa na kuongeza jitihada ili kufanikisha malengo yake. Mteja anahitaji huduma bora kwenye pesa zake hivyo, ni wajibu wetu kumsikiliza kwa makini, kumwelewa na kufanikisha mahitaji yake.


  Mimi: Kama huduma kwa mteja ingekuwa ni mnyama, unafikiri angekuwa ni mnyama gani na kwanini?

  Amanda: Hilo ni swali zuri lakini gumu pia. Mi nafikiri ningefananisha wiki ya mteja na tembo. Tembo ni wapole na viongozi wasiotumia mabavu. Hiyo ndio sababu tembo wenzao huwaheshimu kutokana na uwezo wao wa kutatua matatizo. Hiyo ni sawa na hhuduma kwa mteja.


  Mimi: Ahsante sana kwa kuzungumza nasi kuhusu huduma kwa mteja na namna mlivyojipanga kuhakikisha kwamba mnatimiza matarajio ya wateja wenu.

  Amanda: Shukrani sana.
  0 0

  Meneja masoko huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)baada ya kumpata mshindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa,ampapo mkazi wa Kiloleli mkoani Mwanza Bi. Paulina Kulwa,aliipuka na ushindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/- hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini,Emannuel Ndaki na Meneja wa Huduma za M-pawa wa benki ya CBA, Eric Luyangi.
  Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Emannuel Ndaki(kushoto)akihakiki namba ya mshindi wa promosheni ya Jiongeze na M-Pawa wakati alipokuwa akionyeshwa na Meneja wa Huduma za M-pawa wa benki ya CBA, Eric Luyangi(katikati)kabla ya kupigiwa simu na Meneja masoko huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (kulia) ambapo mkazi wa Kiloleli mkoani Mwanza Bi. Paulina Kulwa, aliipuka na ushindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/- hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Promosheni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na benki hiyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali katika droo kubwa ya mwisho ya Jiongeze na M-Pawa,ambapo Bi. Paulina Kulwa mkazi wa Kiloleli mkoani Mwanza aliipuka na ushindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/- hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

       Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifungua Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha. Mkutano huo umeandaliwa na Africa Group for Justice and Accountability.  
  1.       Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye Majadiliano leo jijini Arusha. Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wamewakilisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini, Sierra Leone, Uganda, Tanzania, Kenya, na Botswana.      
  1   Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akishiriki kwenye Mjadala kuhusu masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha.

   Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Hayupo Pichani) wakati akifungua mkutano huo leo jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability Mheshimiwa Catherine Samba-Panza.
     Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability na aliyekuwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Mheshimiwa Hassan Bubacar Jallow kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha. 

  PICHA NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA.

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya katiba na Sheria Bw Amon Mpanyu akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wadau kutoka Nchini Ghana, Marekani na mashirika ya Kimataifa ya maendeleo waliokutana hii leo Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani kwa lengo la kujadili Mifumo mbalimbali ya kisheria inayosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya Binadamu na Ukusanyaji wa takwimu,kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson na kushoto kwake ni Msajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu kutoka Marekani state ya Hawaii Bw Alvin Onaka,pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi Erica Yegela.
  Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kwa umakini majadiliano kuhusu maboresho ya mifumo ya sheria zinazosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya maisha ya binadamu katika Hoteli ya Stella Maris Mjini Bagamoya Mkoani Pwani.
  Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ambaye ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju katika Hoteli ya Stella Maris Mjini Bagamoya Mkoani Pwani.

  0 0


  0 0


  Na Chalila Kibuda,
  Globu ya Jamii
  MAHAKAMA Kuu Tanzania, Divisheni ya Ardhi, jijini Dar es salaam imetupilia mbali maombi ya Kampuni ya Mbowe Hotels Limited inayomilikiwa na Mwenyekiti Taifa wa Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe ya kutaka kurudishwa kwenye jengo la Billicanas kwa sababu waliondolewa katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

  Jaji Sivangilwa Mwangesi alisema shirika hilo lilifuata taratibu zote kumwondoa mlalamikaji katika jengo hilo na kwamba inashikilia mali zake kihalali hadi atakapolipa kodi ya Sh.Bilioni 1.3  anavyodaiwa na NHC.
  Akisoma uamuzi huo mapema leo Jaji Mwangesi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama yake iliamua kutupilia mbali maombi hayo yaliyofunguliwa chini ya hati ya dharula bila kulipwa gharama.

  Jaji alisema madai ya mlalamikaji kwamba aliondolewa kinyume cha sheria katika jengo hilo na kampuni ya udalali isiyosajiliwa hayana mashiko kisheria na kwamba mahakama inafutilia mbali kesi hiyo.

  “Mahakama hii baada ya kupitia hoja za pande zote mbili imeona kwamba mlalamikiwa wa kwanza NHC alifuata taratibu zote kumtoa mlalamikaji katika jengo hilo.  Pia imeona kwamba kampuni ya udalali  ya Foster Auctioneers and General Traders ilifanya kazi ya kuondoa mali zake kihali, hivyo mahakama inatupilia maombi haya bila kulipwa gharama ya kesi hii” alisema Jaji Mwangesi.
  Akifafanua zaidi Jaji  Mwangesi alisema pamoja na madai ya kuwepo kwa mkataba kati ya NHC na Mbowe, mkataba huo haukuwahi kutekelezwa kwa hiyo ni sawa na kwamba haupo. 
  Upande wa mlalamikaji uliongozwa na Mawakili Peter Kibatala akisaidiana na John Mallya. Upande wa walalamikaji uliongozwa na Mawakili Aloyce Sekule, Aliko Mwamanenge na Mariam Mungula.
  Wakili Mwamanenge akizungumza na Globu  ya Jamii nje ya viunga vya mahakama hiyo, alisema mlalamikaji alisema mahakama imetenda haki na kwamba mlalamikaji alidai kuwa na mkataba kati yake na NHC, lakini mahakama hiyo imeona mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

  “Mahakama imeona dalali alifanya kazi yake kwa kufuata taratibu za kisheria na hata hizo mali zinashikiliwa na mteja kihalali hadi atakapolipa deni la Sh. Bilini 1.3 ndipo atarejeshewa mali hizo” alisema wakili Mwamanenge.
  Kwa upande wake Wakili Mallya alisema wamewasilisha maombi ya kuomba nakala ya uamuzi ili waombe marejeo Mahakama ya Rufani Tanzania.

  Wakili wa NHC Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi habari baada ya kutoka katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikihusu maombi ya Mbowe hotels kurejea katika ofisi zake,ambapo hukumu yake imetolewa leo katika  mahakama kuu kitengo cha Ardhi,jijini Dar.
   Wakili wa Mbowe Hotels, John Mallya, akizungumza na waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotelewa na Mahakama kuhusiana na maombi ya kurejea Mbowe hotels na Mali zake,  katika mahakama kuu kitengo cha ardhi leo jijini Dar es salaam.
   Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa. 
  Mawakili wa Mbowe Hotels John Mallya (kushoto) na Peter Kibatala (kulia) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga,  ajulikanae kwa jina la Emmanuel Mkumbo.


  Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Emmanuel Mkumbo kuanzia leo tarehe 18 Oktoba, 2016. Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya Emmanuel Mkumbo utafanywa baadaye.

  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam
  18 Oktoba, 2016


  0 0


older | 1 | .... | 1396 | 1397 | (Page 1398) | 1399 | 1400 | .... | 3270 | newer