Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASIKITISHWA NA MWEKEZAJI KUBADILI MATUMIZI YA KIWANDA NA KUKITELEKEZA

$
0
0



DHIBITINI BIASHARA ZA MAGENDO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi kuhakikisha anadhibiti wafanyabiashara wanaonunua korosho kwa njia ya magendo na atakayekamatwa achukuliwe hatua.

Pia amewataka wananchi wa mkoa huo kutouza korosho zao kwa walanguzi maarufu kangomba na badala yake wazipeleke kwenye masoko rasmi ili waweze kupata tija. “biashara ya kangomba ni mwiko atakayekamatwa amebeba korosho za kangomba atachukuliwa hatua za kisheria na chombo chake cha usafiri kitataifishwa” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Oktoba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Mibure, Namakuku, Ng’imbwa, Chienjele, Mkata, Mitope na Kitandi

“Marufuku kuuza korosho kwa kangomba kwani mnapata hasara kipimo kinachotumika si rasmi. Mkoa kamateni na taifisheni korosho na chombo cha usafiri kitakachotumika kubeba korosho za magendo,” amesema.Amesema ni vema wakulima wakaachana na biashara ya kangomba kwa sababu haina tija na badala yake wasubiri na kwenda kuuza korosho zao katika minada kwa bei nzuri.

“Mwaka huu korosho itauzika kwa bei ya juu zaidi isiyopungua sh.3500, msikubali kuuza korosho mlizizitolea jasho kwa walanguzi wanaotumia kangomba kwa sh. 1000 huu ni wizi, kwani kile kipimo cha wanachotumia ni sawa na kilo mbili, hivyo unapoteza zaidi ya sh. 6000”. amesema

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao kuongeza idadi ya mazao ya biashara na kuanza kulima alizeti ambapo wataweza kupata faida ya zaidi ya sh. milioni moja kwenye shamba la ukubwa wa ekari moja. Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa miezi miwili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue kuhakikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mibure unakamilika. “Ndani ya miezi miwili Zahanati iwe imekamilika, tuache kuzungumza sasa ni vitendo tu”amesema.

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya ufuta na karanga cha Ilulu kilichoko wilayani Nachingwea na kukuta kimetelekezwa. Ameagiza uongozi wa kiwanda kumpelekea nyaraka zote za umiliki. Kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa marehemu Abbas Gulamali na sasa kinasimamiwa na familia yake. “Nawahitaji Dodoma Oktoba 22 waje na nyaraka zao ili nijue walipokabidhiwa kiwanda hiki walitaka kufanya nini,” alimuagiza Msimamizi wa Kiwanda hicho Dinna Mavumbi kuwajulisha wahusika.

Waziri Mkuu alisema haiwezekani kiwanda hicho kilichojengwa kwa fedha za umma kikatelekezwa bila ya kuendelezwa. Alisema baada ya kupitia nyaraka zao ataangalia namna ya kurudisha majengo hayo ya kiwanda kwa Serikali. “Hatuwezi kuacha raslimali hii ikiwa imetelekezwa msituni inaharibika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 17, 2016
koro1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda  cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji amekifanya kuwa Ghala nakukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa Kiwanda hicho kipo wilaya ya Rungwe Mkoani Lindi Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Rungwe Mkoani Lindi(Picha na Chris Mfinanga)
koro2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyo haribika ambayo yalikuwa yanamilikiwa nakiwanda cha kukamua ufuta  ILULU kiwanda hicho kipo wilani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliye kichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala lakuhifadhia bidhaa kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi    picha na Chris Mfinanga.


WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA MABARAZA YA ARDHI

$
0
0


Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Bibi. Amina Rashid Ntibampemba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mabaraza hayo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mboza Lwandiko.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mboza Lwandiko akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya leo Jijini Dar es Salaam.

………………………………………………………..

Na Georgina Misama – MAELEZO

Wizara ya Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi imewataka watanzania kutumia Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya katika kutatua matatizo mbalimbali yanayohusu Nyumba na Makazi.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Msajili Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Bi Amina Rashidi wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.“Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ndiyo chombo pekee kilichoundwa kwa ajili ya kutatua matatizo yote yanayohusu ardhi na nyumba” alisema Amina.

Akitaja baadhi ya mashauri yanayosikilizwa kwenye Mabaraza hayo Amina alisema mashauri yanayotokana na milki pandikizi (double allocation) au mashauri ya wananchi wanaopakana kwa mmoja wao kutaka kujipanulia eneo. Yapo pia mashauri ya wenye nyumba na wapangaji yanayofunguliwa kwa kukiukwa kwa mikataba.

Aidha, Amina alifafanua kwamba uendeshaji wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ni wakirafiki nasio unaofuata taratibu za Mahakama za kawaida. Wajumbe wa Baraza wanatoka miongoni mwa wanajamii wa eneo ambalo Baraza limeundwa.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Bi. Mboza Lwandiko alitolea ufafanuzi wa dhamira ya wizara yake katika kuhakikisha inapambana na ongezeko la mashauri kwa kuunda Mabaraza mapya yapatayo 20 kila mwaka.

“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Wizara itakamilisha taratibu za kuunda Mabaraza(44) kati ya Mabaraza mapya 47 yaliyoundwa na tangazo la serikali la mwezi Aprili, 2016” alisema Mboza.Tayari takribani mashauri elfu 43 yamesikilizwa kati ya mashauri elfu 59 yaliyofunguliwa kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2004 na Septemba 2016.

BODI YA MFUKO WA BARABARA YASITISHA UFADHILI WA UJENZI WA BARABARA KWA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.
uje2
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Meneja wa Mfuko huo Bw. Eliud Nyauhenga.
uje3

Baadhi ya Watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bw. Joseph Haule (hayupo pichani), wakati alipotoa ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni.Jijini Dar es Salaam


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Bodi ya Mfuko wa Barabara umesitisha ufadhili miradi ya barabara kwa Manispaa ya Kinondoni baada kubainika kutengeneza barabara chini ya kiwango pamoja na ukiukaji sheria za manunuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Joseph Haule amesema kusitisha ufadhili kwa barabara kwa Manispaa ya Kinondoni kumetokana manispaa hiyo kujenga barabara chini ya kiwango ikiwemo Barabara ya Masjid-Quba iliyopo Sinza.

Haule amesema barabara barabara hiyo mkandarasi anafanya kazi huku Bodi ikiwa imetoa Sh.Bilioni 3.3 lakini Manispaa imemlipa Mkandarasi sh.milioni 200 ambapo ni kinyume na sheria ya manunuzi ya kulipwa sh.milioni 801 kwa mkupuo wa kwanza.

Amesema barabara hiyo ilitakiwa kuisha mwaka jana lakini bado wanaendelea kujenga ambapo ni kinyume cha mkataba na kuhoji kuwa mkandarasi huyo anaendelea kujenga kwa mkataba gani wakati muda wake wa ujenzi ulikuwa umeisha.

Bodi imeuagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi kuwachukulia hatua wote waliohusika na mkataba wa barabara ya Masjid Kuba pamoja kubadili mfumo manispaa jinsi kuweza kufanya fedha ya serikali inayotengwa na Barabar inakuwa salama.

Aidha bodi hiyo imetaka Halmashauri zote kuhakikisha zinasimamia fedha za barabara ipasavyo na pamoja na barababaea kujengwa kwa ubora unaotakiwa..

BODI YA MFUKO WA BARABARA YASITISHA UFADHILI WA UJENZI WA BARABARA KWA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.
uje2
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Meneja wa Mfuko huo Bw. Eliud Nyauhenga.
uje3

Baadhi ya Watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bw. Joseph Haule (hayupo pichani), wakati alipotoa ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni.Jijini Dar es Salaam


Na Chalila Kibuda, 
Globu ya Jamii
Bodi ya Mfuko wa Barabara umesitisha ufadhili miradi ya barabara kwa Manispaa ya Kinondoni baada kubainika kutengeneza barabara chini ya kiwango pamoja na ukiukaji sheria za manunuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Joseph Haule amesema kusitisha ufadhili kwa barabara kwa Manispaa ya Kinondoni kumetokana manispaa hiyo kujenga barabara chini ya kiwango ikiwemo Barabara ya Masjid-Quba iliyopo Sinza.
Haule amesema barabara barabara hiyo mkandarasi anafanya kazi huku Bodi ikiwa imetoa Sh.Bilioni 3.3 lakini Manispaa imemlipa Mkandarasi sh.milioni 200 ambapo ni kinyume na sheria ya manunuzi ya kulipwa sh.milioni 801 kwa mkupuo wa kwanza.
Amesema barabara hiyo ilitakiwa kuisha mwaka jana lakini bado wanaendelea kujenga ambapo ni kinyume cha mkataba na kuhoji kuwa mkandarasi huyo anaendelea kujenga kwa mkataba gani wakati muda wake wa ujenzi ulikuwa umeisha.
Bodi imeuagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi kuwachukulia hatua wote waliohusika na mkataba wa barabara ya Masjid Kuba pamoja kubadili mfumo manispaa jinsi kuweza kufanya fedha ya serikali inayotengwa na Barabar inakuwa salama.
Aidha bodi hiyo imetaka Halmashauri zote kuhakikisha zinasimamia fedha za barabara ipasavyo na pamoja na barababaea kujengwa kwa ubora unaotakiwa..

LUKUVI ATOA HATI KWA WANANCHI WA MAKAZI HOLELA MOROGORO.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi katika ziara yake ya mkoani Morogoro (17-10-2016) ameendelea kutekeleza program ya kurasimisha makazi holela kwa wananchi 116, ambapo amegawa hati 60 za awali na kumuagiza Afisa ardhi kuhakikisha anatoa hati zilizobakia ndani ya mwezi mmoja.

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mpango wake wa kuboresha maendeleo ya wananchi na makazi yao, imeanzisha program ya kurasimisha makazi holela kwa wananchi. Mpango huu ni wakupima, kupanga na kuwapatia hati wananchi waliojenga katika makazi yasio na mpangilio rasmi.

Akiwa mkoani morogoro Mhe. Waziri alitembelea baadhi ya makazi ya wananchi hao katika kata ya Bigwa na kujionea jinsi wananchi wanavyounga mkono juhudi za serikali katika kurasimisha makazi holela.Wananchi hao wa Bigwa kwa umoja wao walipima ardhi zao na kufuata utaratibu wa mipango miji kwa mujibu wa taratibu za serikali.

Aidha, Lukuvi alifanya ziara ya kushtukiza katika Masijara ya Ardhi ya Manispaa ya Morogoro, na kukuta idadi kubwa ya hati za wananchi zimekaa zaidi ya mwaka mzima bila ya kuwafikia wahusika. Alihoji juu ya suala hilo, na kutoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa hati hizo kuwafikia walengwa ndani ya mwezi mmoja.

Baada ya ziara hiyo Mheshimiwa Waziri aliongea na wananchi wa Morogoro katika ofisi za Manispaa ya Morogoro na kusikiliza kero zao mbalimbali za ardhi na kuzitatua papohapo. Katika mazungumzo yake aliwataka wananchi waunge mkono juhudi za serikali kurasimisha makazi yao ili waweze kuishi katika makazi salama yanayotambulika na pia waweze kufaidika na ardhi yao kama kupata mikopo Benki au katika mambo mengine ya maendeleo yao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimuhoji Afisa ardhi Manispaa ya Morogoro Bw. Abenance Kanomoga (wa kwanza kushoto), kwanini amekaa na hati za wananchi kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kuwajulisha wahusika kuja kuzichukua.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akigawa hati kwa wakazi wa Bigwa mkoani Morogoro..


 Baadhi ya wananchi wa mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.

1.       Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajiongea na wananchi wa mkoani Morogoro. 

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KOMORO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KOMORO,

$
0
0
Balozi Chabaka Kilumanga akipokea zawadi kutoka kwa Rais. Azzali Ousman
Kutoka Kushoto Rais Azali Ousman, Balozi wat Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka Kilimunga, Bw. Mudrick Soragha Mkuu wa Afisa Ubalozi na Bi. Sheehat Kassim Mkalimani .
Mhe. Chabaka Kilumanga Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro leo tarehe 17 Oktoba, 2016 alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Col. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro katika Ikulu ya Bait Salam. Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais Azzali kufanya mazungumzo na Balozi huyo kutoka Tanzania tangu kuingia kwake madarakani Tarehe 25 Mei, 2016. 

Katika mazungumzo yao Mhe. Chabaka Kilumanga alichukua fursa hiyo kumpongeza Rais Azzali kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuongoza Wanakomoro na kuelezea kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Komoro hasa kwa kuzingatia mahusiano yakaribu yaliyopo baina ya hizo mbili. 

Kwa upande wake Mhe. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Visiwa vya Komoro alimshukuru Mhe. Balozi kwa ushirikiano ambao amekuwa akiupata kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Komoro na kueleza kuwa Komoro inajifunza mambo mengi kutoka kwa ndugu zao wa Tanzania. 

Aidha aliezea kuwa uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Komoro ni wa Kihistoria na ni matarajio yake kuwa uhasiano huo utaendelea kukuzwa na kudumishwa kwa manufaa ya nchi zote mbili. Wakati wakimaliza mazungumzo yao, Mhe. Azzali alieleza dhamira yake ya kutaka kufanya ziara nchini Tanzania na kwamba ni matarajio yake kuwa ziara hiyo itafanyika mapema iwezekanavyo.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Akutana na wamiliki wa Daladala

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiongea leo na  umoja wa wamiliki wa Daladala Wilayani Iringa katika ukumbi wa Siasa na kilimo kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri.




Na Mathias Canal
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekutana na umoja wa wamiliki wa Daladala Wilayani Iringa katika ukumbi wa Siasa na kilimo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Baadhi ya madereva na Makondakta wameomba kurudishwa katika Stendi ya Miyomboni kama ilivyokuwa hapo awali wakidai kuwa eneo la walilohamishiwa kwa sasa la Mashine tatu ni finyu na lina msongamano mkubwa wa watu jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wananchi.
Dc Kasesela amesema kuwa kurudi katika standi ya Miyomboni ni jambo lisilowezekana kutokana na eneo hilo kuwa dogo na limezungukwa na makazi ya watu pamoja na majengo makubwa ya biashara jambo ambalo linafanya eneo hilo kuwa hatarishi zaidi kama iwapo kunaweza kutokea janga la moto.
"Unajua Miyomboni ni padogo sana pia pamejibana sasa kama ikitokea moto umewaka pale ni ngumu sana kupafikia kwa wepesi lakini pia Watu wa zima moto ndio waliopendekeza kuwa kituo kile kihamishwe sasa nadhani mnafahamu kuwa sheria ya zimamoto huwa ni ngumu kuipinga", alisema Mhe. Kasesera.
Lakini pia amewataka madereva kuacha kutumika kisiasa kwani wanaofanya hivo wanafanya kwa maslahi yao binafsi.

MKUTANO WA TATU WA UMOJA WA MATAIFA WA MAKAZI NA MAENDELEO ENDELEVU YA MIJI.(UN HABITAT III)

$
0
0
Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji umeanza leo tarehe 17 Oktoba 2016, katika ukumbi wa Casa De La Cultura Ecuatoriana Mjini Quito ,mji mkuu wa Ecuador. 


Mkutano huo wa siku tano unaowakutanisha viongozi wa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa na wadau mbalimbali umefunguliwa rasmi  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon. 
Tanzania imewakilishwa na wajumbe saba wakiongozwa na Dkt. Yamungu Kayandabila Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Wengine ni Mhe. Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini, Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango miji na Vijiji  kutoka Wizara ya Ardhi, Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sada Sekiete Afisa Mipangomiji Mkuu kutoka Wizara ya Ardhi, Abdillahi Namwambe Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Fatuma Chillo Mkurugenzi wa Sheria kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
 Ujumbe wa Tanzania  kutoka kushoto ni Dkt. Yamungu Kayandabila Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa mkutanoni hapo pamoja na Mhe. Profesa Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini na Mama  Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango miji na Vijiji  kutoka Wizara ya Ardhi.


Inatarjiwa kuwa matokea ya mkutano huo ni kupatikana kwa  Ajenda Mpya ya tatu  ya Makazi na maendeleo endelevu ya miji,(habitat iii) kwa miaka ishirini ijayo ambayo utekelezaji wake unaenda sawa na utekelezaji wa malengo ya Ajenda 2030 ya Maendeleo endelevu.(SDGs)

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASIKITISHWA NA MWEKEZAJI KUBADILI MATUMIZI YA KIWANDA NA KUKITELEKEZA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda  cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho mwuekezaji amekifanya kuwa ghala na kukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa. Kiwanda hicho kipo Nachingwea  Mkoani Lindi ambako Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyoharibika ambayo yalikuwa yanamilikiwa na kiwanda cha kukamua ufuta  ILULU  wilayani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliyekichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala la kuhifadhia bidhaa kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi. 
Picha na Chris Mfinanga

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAELFU KUAGA MWILI WA MEYA WA ZAMANI WA DAR ES SALAAM DKT. DIDAS MASABURI

$
0
0
 VIONGOZI MBALIMBALI WAMEJITOKEZA KUAGA MWILI WA DKT DIDAS MASABURI,VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR LEO .
SANDUKU LENYE  MWILI WA MAREHEMU DKT DIDAS MASABURI LIKIWASILI VIWANJA VYA KARIMJEE,JIJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI HII KWA AJILI YA KUTOLEWA HESHIMA ZA MWISHO,AMBAPO RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ALIWAONGOZA WANANCHI WALIOFIKA KUSHIRIKI KUAGA MWILI WA DKT DIDAS MASABURI.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.
 Sehemu ya wafiwa kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016..

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

UNAKARIBISHWA Jioni Ya Bwanjai ukumbi wa Kardinali Rugambwa IJUMAA OKTOBA 21, 2016 katika kanisa la Mt. Petro Oysterbay, Dar es salaam

WAZIRI WA FEDHA AITAKA BENKI YA MAENDELEO TIB KUJIKITA KATIKA UWEKEZAJI WA VIWANDA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amezindua rasmi bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo TIB kwa kuiagaiza iweke mikakati yakutaua changamoto mbalimbali zitakozoiwezesha kushiriki kikamilifu katika utelezaji wa Mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano. Bodi hiyo imeundwa kufuatia uteuzi wa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika mwezi  Julai 2016.

Akizindua bodi hiyo, Dkt. Mpango aliwakumbusha wajumbe kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuweza kufanikisha azma ya Rais ya kujenga Tanzania ya Viwanda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango (wanne kutokea kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wakurugenzi ya TIB baada ya uzinduzi wa bodi hiyo. Kutokea kulia ni Bw. Maduka Kessy, Bi. Rose Aiko, Bw. Charles Singili, Professa Palamagamba Kabudi, Dkt Said Seif Mzee, Profesa Joseph Buchweishaija na Dkt. Anorld Kihaule. 

“Serikali ya awamu ya tano imejikita kwenye kuhakikisha kuwa uchumi wetu unakuwa ni uchumi wa viwanda. Benki hii ikiwa ni benki ya kisera inawajibu wa kuhakikisha hili linatekelezwa. Kwa mantiki hiyo ni matarajio ya serikali kuona kuwa benki inachochea maendeleo katika nyanja zote muhimu za uendelezaji wa viwanda  vya kuzalisha umeme na miundombinu yake, maji, barabara/usafirishaji na mawasiliano ili  kufikia malengo tarajiwa hususan kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa ni nchi ya uchumi wa kati unaotegemea viwanda ” alisema Dkt. Mpango.

Kwenye maelezo yake ya awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Charles Singili mbali na kuainisha juhudi zinazofanywa na benki hiyo katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya Taifa alielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili benki hiyo. Changamoto hizo ni pamoja na udogo wa mtaji, uhitaji wa kuwepo kwa fedha za kuandaa miradi, taratibu ndefu za upatikanaji wa vibali vya kukopa kwa taasisi za Serikali na uwepo wa mikopo chechefu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugezi wa Benki ya Maendeleo ya TIB (Profesa Paramagamba Kabudi). wengine katika picha kutokea kushoto ni Mkurugezi Mtendaji Msaidizi Bw.Jaffer Machano, Mkurugezi Idara ya Tecknohama Bw.Robert Ndaki na Mkurugenzi wa usimamizi wa Mikopo Bw. Erick Hamisi.

Waziri Mpango pia aliongelea changamoto zinazo ikabili benki hiyo ikiwemo suala la mtaji ambapo alisema, “Serikali ya awamu ya tano inalifanyia kazi suala hili ili kuleta suluhisho endelevu na kuiwezesha benki hii kutimiza malengo ya kuundwa kwake”.
 
Pia aliisisitizia bodi kuweka mikakati madhubuti katika  kukusanya madeni, kusimamia mikopo inayotolewa  na kuhakikisha kuwa mikopo inayoidhinishwa ni kwa miradi inayo stahili na yenye uwezo wa kurejesha mikopo hiyo. Aidha, aliitaka benki hiyo kutokufanya kazi kwa mashinikizo yoyote kutoka kwa watu, wanasiasa, idara au taasisi yoyote; bali wazingatie sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza tasnia ya mabenki kama zinavyoelekezwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango akihutubia bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya Benki ya Maendeleo TIB wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mjini Dododma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya ya bodi hiyo ilioteuliwa Profesa Palamagamba John Kabudi alimuahidi Waziri kuwa watafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na kutekekeleza maelekezo aliyoyatoa ili kutimiza matarajio ya Serikali na waliowateua. Aidha, Mwenyekiti Profesa Kabudi alisema “Tutafanya jitihada ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazo ikabili benki yetu, Kwa yale yanayohitaji maelekezo ya ofisi yako hatutasita kuwasiliana na ofisi yako na yale yaliyoko ndani ya mamlaka yetu tutayashughulikia kulingana na taratibu za kiutendaji katika sekta husika.”

Bodi hiyo iliyozinduliwa rasmi mjini Dodoma sasa itaanza kazi zake rasmi kuhakikisha inaiendeleza na kuiimarisha Benki hiyo ya Maendeleo TIB.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB akipeana mikono na Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt Philip Mpango baada ya Uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara TIB Frank Nyabundege. 

RAIS DKT MAGUFULI AUNGANISHA FAMILIA YA MAREHEMU DKT DIDAS MASABURI, WANAFAMILIA NA WANANCHI WAFURAHIA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 17.10.2016


New MUHAS academic medical centre Mloganzila Campus

Klabu ya Rotary ya Oyster Bay Yajenga Ukuta katika Shule ya Msingi Msasani A na Msasani B

$
0
0
Klabu ya Rotary ya Oyster Bay ya jijini Dar es Salaam imekabidhi rasmi ukuta uliojengwa na klabu hiyo katika Shule ya Msingi ya Msasani A na Msasani B. Ukuta huo umejengwa ili kuimarisha usalama kwa wanafunzi wa shule hizo pamoja na kulinda mali za shule. Kabla ya ujenzi wa ukuta huo, mazingira ya shule hizo yalikuwa hatarishi kwa wanafunzi kutokana na watu wasiohusika kupita katika eneo la shule bila udhibiti.

Ujenzi wa ukuta huo wenye thamani ya takribani Tshs Milioni 35 umewezeshwa na fedha zilizopatikana kutoka kwenye mojawapo ya shughuli za uchangishaji fedha zinazofanywa na klabu hiyo ambapo wadau mbalimbali walichangia ili kufanikisha zoezi hilo.

Ukuta huo ni muendelezo wa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Klabu ya Rotary ya Oyster Bay katika kuboresha mazingira ya shule hiyo. Jitihada nyingine zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa maktaba mbili pamoja na kuweka vitabu vya aina mbalimbali, maji safi na salama ya kunywa, kambi ya siku moja ya huduma za bure za upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali, mafunzo kwa walimu pamoja na upandaji wa miti.

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na wanachama wa klabu ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa Muunganiko wa Klabu za Rotary katika nchi za Tanzania na Uganda. Kiongozi Mkuu wa mkusanyiko wa klabu za Rotary Tanzania na Uganda, bwana Jayesh Asher alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo na alipongeza juhudi za klabu ya Oyster Bay katika kusaidia shule hizo.




RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,
Makamo Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar SUZA Prof.Idrissa Rai (kulia) akiwa na Viongozi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Viongozi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi.Khadija Bakari Juma (kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 18/10 /2016.

WAZIRI NAPE AKIWASILISHA MUSWADA WA HABARI KUIBADILI TAALUMA

$
0
0

SERIKALI imewasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Muswada wa Huduma za Habari ikieleza kuwa ni sheria itakayoleta mageuzi makubwa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akiwasilisha muswada wa sheria hiyo leo mjini Dodoma ambapo amesema sasa sekta ya habari inakwenda kuwa taaluma kamili.

Waziri Nnauye amesema Sheria hii italeta mifumo ya kisasa ya usimamizi wa sekta ya habari na mifumo ambayo inaweza kugusa au kubadili namna wanahabari walivyozoea kutenda au kufikirika kwa sasa lakini akasema sekta hiyo iwe tayari kwa mabadiliko.

“Niwaombe wanatasnia wenzangu tuwe tayari kwa mabadiliko haya ili taaluma yetu iheshimike na sisi wenyewe tuheshimike zaidi” alisisitiza Mhe. Nnauye.Aidha Mhe. Nnauye ametoa wito kwa wadau wote kuunga mkono muswada huo utakaojadiliwa katika Bunge lijalo la Novemba mwaka huu. 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mswada wa Sheria ya Huduma za Habari 2016 leo Mjini Dodoma Oktoba 18,2016.

HABARI ZAIDI BOFYA 

MKE WA WAZIRI MKUU MARY MAJALIWA AIOMBA JAMII,MASHIRIKA NA MAKAMPUNI KUWASAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI HAPA NCHINI (ALBINO)

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa kwa niaba ya familia yake ametoa mchango wa fedha zaidi ya shilingi laki sita kwa Mama Hakika Swalehe kwa ajili ya kuwasidia watoto wake wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) Rashidi Juma (5)na Iklamu Juma (miezi 9) Mama Majaliwa ameahidi kuwasidia watoto hao vifaa vingine vya kutunza ngozi kwa ajili ya Watoto hao wanaoishi katika kijiji cha Mtope wilaya ya Ruwangwa Mkoani Lindi .Picha na Chris Mfinanga
Mama Majaliwa akimsalimia mtoto Iklamu Juma mwenye ulemavu wa ngozi Kushoto ni Rashidi Juma (5)kaka wa Iklamu
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akiagana na Mama Hakika Swalehe mara baada ya kuzungumza naye
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images