Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

EFM 93.7 YAENDELEA KUSAKA VIPAJI VYA SINGELI MKOANI PWANI

$
0
0
 Msaani chipukizi,Mussa  Mkumba a.k.a Dogo Jet akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka  vipaji vya waimbaji wa nyimbo za singeli katika viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.
 Msaani chipukizi,Idd Issa a.k.a Mauwezo akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka  vipaji vya waimbaji wa nyimbo za singeli katika viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.


Mashabiki wakipagawishwa na wasanii waimbaji wa nyimbo za singeli katika  viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.


Mashabiki wakipagawishwa na wasanii waimbaji wa nyimbo za singeli katika  viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

WASHINDI WA JIONGEZE NA M-PAWA YA VODACOM WAZIDI KUJINYAKULIA VITITA VYAO

$
0
0
 Mshindi wa jiongeze na M-Pawa mkazi wa Buza  temeke mkoa wa Dar es Salaam, Astride Mtewele(kushoto) akipokea fedha taslimu shilingi Milioni 20/- kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu (kulia)Anayeshuhudia katikati Mkuu wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini leo.

 Mshindi wa jiongeze na M-Pawa mkazi wa Buza  temeke mkoa wa Dar es Salaam, Astride Mtewele(kushoto)akionekana kutokuamini kama atakabidhiwa kitita chake cha shilingi Milioni 20/-alizojishindia kupitia promosheni hiyo kabla ya kukabidhiwa rasmi kitita hicho leo,Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.

 Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu(kulia) na  Mkuu wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Dar es Salaam wa kampuni hiyo,Domician Mkama wakimshuhudia Mshindi wa jiongeze na M-Pawa ambaye ni mkazi wa Buza jijini  Dar es Salaam, Astride Mtewele(kushoto)jinsi asivyoamini kama kajishindia kitita cha shilingi Milioni 20/- kupitia promosheni hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi leo jijini.

MTANDAO WA WIZI WA BAJAJI NA BODABODA WANASWA MBEYA

$
0
0
Mtuhumiwa anayehusika na matukio hayo imefahamika kwa jina la Getruda Mwakyusa Mkazi wa Mtaa wa Manga Veta jijini hapa. Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema jeshi la polisi limeendelea kufanya misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kudhibiti uhalifu . 

Amesema Octobar 13 katika misako hiyo jeshi hilo la polisi lilifanikiwa kuunasa mtandao wa wizi wa bajajai na pikipiki ambapo mtuhumiwa wa matukio hayo alifanikiwa kutoroka ambapo nyumba yake mara baada ya kufanyiwa upekuzi zilikutwa pikipiki 3,bajaji 3,bodi 7 za bajaji . 

Amesema kati ya mali hizo pikipiki mbili tayari zimekwisha tambuliwa na wamiliki wake kuwa ziliibiwa wilayani Chunya septemba25 mwaka huu katika kijiji cha Isenyela kata ya Mbugani. Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani humo ametoa wito kwa jamii husasani vijana kuacha tabia ya kutaka mali kwa njia ya mkato badala yake wafanye kazi kihalali ili kijipatia kipato sanjali na kutumia fursa zilizopo ili kujitafutia ajira.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusiana na tukio la kuunasa mtandao wa wizi wa Bajaji na Pikipiki (BodaBoda) Mkoani Mbeya.(JamiiMojaBlog) 
Mkutano wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Waandishi wa habari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akionesha baadhi ya Bjajai na Pikipiki ziizokmatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo la POLISI Mbeya. 
Askari Polisi wakiwa wamebeba moja ya bajaji iliyokamatwa mara baada ya Jeshi la Polisi Kufanya masako . 
Bajaji zilizokamatwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kufanya msako. 
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kuunasa mtandao uliokuwa ukihusika na matukio mbalimbali ya wizi wa bajaji na Pikipiki (bodaboda) katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

WAFANYAKAZI NEW HABARI CORPORATION HATARINI KUWA VIZIWI

$
0
0
Hayo yamebainika wakati wa Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo ambapo miongoni mwa mambo yaliyobainika ni pamoja na kelele hizo zisizo za kawaida ambazo zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni hiyo ambazo zinahatarisha uwezo wa wafanyakazi wa kusikia .

Ziara ya Mkurugenzi Kayombo ya kutembelea katika kampuni hiyo imekukuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hicho. Baadhi ya wananchi wanaofanya biashara jirani na eneo hilo wamesema kuwa kwa muda mrefu wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi, hivyo kuamua kufikisha kwa kiongozi shupavu mwenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi Mh. John Kayombo.

Baada ya malalamiko ya wananchi kumfikia ,bila kupepesa macho Mkurugenzi Kayombo akaenda New Habari House bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kuona hali halisi.Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanayozunguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye mashine inayochapisha magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo.

Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia au kupunguza sauti hizo.'' Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti,huu ni ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu"alisema Kayombo.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo (Kushoto) akiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Mariam Malliwadh mara baada ya kuwasili katika kampuni ya New Habari Corparation
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo akisikiliza kelele hizo ambazo zimekuwa zikiwasumbua wafanyakazi wa kampuni hiyo
Kelele ziosizo za kawaida huenda zikawasababishia wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari Corparation matatizo ya kutesikia kutokana na kutokuwa na vifaa madhubuti vya kuzuia kelele hizo.

TABATA KIMANGA JIJINI DAR ES SALAAM WAIOMBA MANISPAA YA ILALA KUWAJENGEA DARAJA LITAKALO WAUNGANISHA NA TABATA CHANG'OMBE

$
0
0


Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wanaoishi mpakani mwa Tabata Kimanga na Chang'ombe katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kujengewa daraja ili waweze kutumia muda mfupi wa kufika katika maeneo hayo badala ya kupitia Tataba Mawenzi.

Ombi hilo wamelitowa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com kuhusu changamoto mbalimbali zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya kujengewa daraja hilo lililopo Mtaa wa Amani.

Akizungumzia changamoto ya daraja hilo, mkazi wa eneo hilo Tusekelege Ambonisye alisema wamekuwa wakitumia muda mwingi wa kuzunguka na gari kupitia Tabata Bima na kwenda Tabata Chang'ombe lakini kama daraja hilo linalounganisha maeneo hayo lingejengwa lingewarahisishia" alisema Ambonisye.

Aliongeza kuwa adha kubwa waliyonayo ni pale ikinyesha mvua kwani maji yanajaa na barabara hiyo kushindwa kupitika ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha ya watu wanaojaribu kupita kaika eneo hilo.

Alisema kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa eneo hilo walikusanya nguvu na kujenga daraja la miti la muda ambalo linatumika lakini sio salama kwa watumiaji.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo wa Amani, Jonathan Mlay alisema changamoto ya daraja hilo ni ya muda mrefu kwani waliwahi kuiwasilisha kwa wabunge wa jimbo hilo waliopita na wa sasa Bonah Kaluwa lakini bado halijapatiwa ufumbuzi wowote.

"Kupitia vikao vyetu vya kamati ya maendeleo ya mtaa changamoto hii tuliipeleka kwa wabunge waliopita pamoja na huyu wa sasa tupo tunasubiri matokea yake" alisema Mlay.
 Mtoto Juma Ramadhan mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Tabata Kimanga, akiwa amembeba mdogo wake Sara Sadiki wakati wakipita katika daraja la miti linalounganisha wakazi wa Tabata Kimanga na Tabata Chang'ombe Dar es Salaam , ambapo wakazi wa eneo hilo wanaiomba Manispaa ya Ilala iwajengee daraja la kudumu.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Jonathan Mlay akimuonesha mwandishi wa mtandao huu, daraja la miti wanalolitumia lililojengwa kwa nguvu za wananchi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.

INTRODUCING NEW AUDIO BY TEA SIGWER - NYOTA NDOGO

KANDANDA DAY 2016: TEAM ISMAIL YAIBUKA NA USHINDI MNONO WA BAO 4-1 DHIDI YA TEAM DIZO MOJA

$
0
0
TIMU ya soka ‘Team Ismail’ imefanikiwa kuwagaragaza wapinzani wao wa jadi 'Team Dizo Moja' kwa kipigo cha mabao 4-1, katika tamasha la Kandanda day, lililofanyika Jumamosi katika Viwanja vya Jakaya M Kikwete Youth Park.


Kipigo hicho kwa 'Team Dizo', ni mfululizo wa matokeo mazuri ya Team Ismail,ambayo mwaka huu imeonekana kulipiza kisasi cha kuchapwa idadi hiyo ya mabao kama walivyofanya Team Dizo katika msimu wa mwaka 2014.

Mabao ya Team Ismail,yaliwekwa kimiani na Freddy Pastor aliyeweka kimiani mabao mawili,huku Gerald Bernald na Noah Katepa wakifunga bao moja moja na lile la kufutia machozi kwa timu Dizo likifungwa na mchezaji wao waliyemchukua kwa mkopo toka timu Ismail Wilfred Kadege.

Mwaka jana katika tamasha hilo, Timu Ismail,iliwatandika wapinzani wao kwa mabao 2 kwa mtungi,jambo ambalo mwaka huu liliongeza upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili.

Mbali na mtanange huo,mechi nyingine iliyovuta hisia za mashabiki waliohudhuria tamasha hilo ni mchezo wa fainali ya makundi ulizokutanisha timu za Dar City Fc na Coca Cola,ambapo katika mchezo huo, Coca waliigaragaza Dar City kwa mabo 3 kwa bila.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati,Patrick Dumulinyi,aliwashukuru wadhamini wote pamoja na timu shiriki kwa kufanikisha lengo la tamasha la mwaka huu lililobeba kauli mbiu ya Mpira na Dawati kufana kwa kiasi kikubwa.

“Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu na timu shiriki,kwa kuungana kutimiza ndoto zetu za mwaka huu za kuisaidia jamii kwa kukusanya fedha za madawati,ambayo kabla ya kuisha kwa mwezi huu tunatarajia kuyakabidhi katika shule husika,”alisema Dumulinyi.

Mshambuliaji wa 'Team Ismail', Nassor Bin Slum akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea langoni mwa 'Team Dizo Moja', katika tamasha la wapenzi wa mchezo wa soka nchini 'Kandanda Day 2016', lililofanyika Jumamosi Oktoba 15, 2016 katika Viwanja vya Jakaya M Kikwete Youth Park, Jijini Dar es salaam.

Diwani Mohsin Bharwani wa Kata ya Vigwaza amkumbuka Mwl. Nyerere kwa kugawa dawa bure

$
0
0
DIWANI wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani, amemkumbuka Mwalimu Nyerere kwa kumwaga madawa katika Zahanati ya Vigwaza na Ruvu Darajani, wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani zenye thamani zaidi ya Sh milioni 4 .

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Vigwaza diwani huyo alisema kutokana na changamoto za ukosefu wa dawa zanazozikabili zahanati ya hizo wananchi wengi wanapata shida sana ya kukosa matibabu, hivyo yeye kama Diwani wao aliliona hilo na kuwakumbuka kwa kuwatelea dawa katika zahanati hizo ili kurahisisha matibabu kwa wananchi wake.
Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani akizungumza na wananchi wake waliojitokeza katika Zahanati ya Ruvu Darajani, alipotembelea na kukabidhi msaada wa dawa. 
Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani(CCM), akimkabidhi msaada wa dawa Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ruvu Darajani, Dk. Gilbert Daniel, ikiwa ni sehemu ya kumuenzi na kukumbuka miaka 17 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 14, 2016.
Picha ya pamoja na wananchi wake hao.

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAANZISHA CLUBS MASHULENI KUONGEZA UELEWA WA WATOTO 'NJITI'

$
0
0
Ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na uelewa mpana wa masuala ya watoto njiti (prematurity babies), Taasisi ya Doris Mollel imeamua kuongeza ufahamu huo kwa kuanza kutembelea shule mbalimbali zilizopo jijini Dar es Salaam na kuunda vikundi vidogo vya kujitolea (Clubs).

Vikundi hivyo vilizinduliwa Oktoba 15, 2016 kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa anahimiza jamii kuwa na moyo wa kujitolea, hivyo basi kwa kupitia vikundi hivyo itasaidia kuongeza molari ya kujitolea kwa kizazi kijacho kuanzia wakiwa bado mashuleni.

Vilevile vikundi hivyo vitakuwa vinajadili masuala mbalimbali yanayohusu watoto njiti, maisha baada ya shule na mambo mengine mengi.

Baadhi ya shule zitakazokuwa na vikundi hivyo (Clubs) ni shule za sekondari za Al-Muntazir, Alpha, Msimbazi, Good Samaritan, Green Acres, IST, Mbezi High na Salma Kikwete.

Sherehe za uzinduzi wa clubs hizo zilifanyika katika shule ya sekondari ya Salma Kikwete, zikiwezeshwa na kampuni ya ASAS DIARES pamoja na Taasisi ya Rehema Friendship and Solidarity Trust ambao walitoa vitabu kwa ajili ya kuongeza ufahamu wa wanafunzi wa kile wanachofundishwa na walimu wao.
Mgeni rasmi alikuwa ni Bi. Anna Mgwira, waalikwa wengine ni pamoja na Bi. Doroth Kipeja, Bi.Lisa Jensen, wawakilishi kutoka shule tajwa pamoja na mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Bi. Doris Mollel akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Taasisi hiyo Bi. Rahma Amood.

JAMII ZA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYANI KILOSA ZATAKIWA KUISHI KWA AMANI - MAKAMBA

$
0
0
Na Lulu Mussa, Morogoro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameitaka jamii ya watu wa Parakuyo katika Wilaya ya Kilosa kuishi kwa amani, uvumilivu na upendo miongoni mwao kwani ndio misingi ya watanzania.

Rai hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa hadhara uliojumuisha jamii za wakulima na wafugaji ambazo zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara. Waziri Makamba alizitaka jamii hizo kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa na jamii hiyo ni kutokuwa na elimu juu ya mabadiliko ya Tabianchi na athari zake pamoja na kutokuwepo na matumizi bora ya ardhi.

Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda kamati ya 'Amani' itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za wakulima na wafugaji na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta suluhu ya kudumu baina ya pande mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara kwa mara.

"Undeni Kamati hii mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo kwa Kamati husika juu ya namna bora ya kutatua migogoro" alisisitiza Waziri Makamba.

katika jitihada za kukuza uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto zake, Waziri Makamba ameitaka Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za Mazingira ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya Mazingira na kuahidi kuipati mafunzo Kamati hizo ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazotumika kama nyenzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira ya maeneo yao.

Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu sana na kuitaka jamii ya Parakuyo na Twa twa twa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhakiki na kuhesabu mifugo yako ili kubaini ni ardhi kiasi gani inahitajika kwa wakulima na kiasi gani kwa wafugaji. "ndugu zangu niwasihi, Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na matumizi bora ya ardhi, hivyo nawashauri mmshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata uwiano wa idadi ya mifugo na ardhi iliyopo" Makamba aliongezea.

Awali katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Morogoro Waziri Makamba pia alitembelea chanzo cha maji na kujionea changamoto za kimazingira katika mto Mambogo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Waziri Makamba yuko Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba, wa tatu kutoka kulia akiangalia chanzo cha maji kilichovamiwa katika Mto Mambogo.

KUTOKA MAKTABA: MWALIMU NA WASIDIZI WAKE IKULU

$
0
0
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kati) alikuwa na wasaidizi wa karibu mahiri mbalimbali katika enzi za uongozi wake wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawa ni baadhi tu waliomsaidia kwenye nyanja ya habari. Kutoka kushoto ni Marehemu Sammy Mdee, Marehemu Paul Sozigwa, Marehemu Hashim Mbita na Benjamin William Mkapa, ambaye alikuja kuchukua nafasi yake kwenye awamu ya Tatu. 

FNB YAZINDUA MASHINE ZA MALIPO KWA NJIA YA KADI

$
0
0

Na Cathbert Kajuna. 

First National Bank Tanzania (FNB) imezindua rasmi mashine za malipo kwa njia ya kadi (POS Devices) jijini Dar es salaam kama hatua ya kuimarisha matumizi ya kadi za benki kwa ajili ya malipo ya bidhaa na huduma kwa njia salama, rahisi, na kwa gharama nafuu na zitatumika kama mbadala wa fedha taslimu. Mkuu wa bidhaa na huduma za dijitali wa benki hiyo, Silvest Arumasi alisema benki itatoa mashine za kuweka maeneo mbalimbali ya biashara kubwa na biashara ndogo au za rejareja. 

Vilevile benki hiyo itatoa mashine ndogo za kubeba kama simu ambazo zitatumika kwenye sekta ya utalii na mahoteli pamoja na biashara nyingine hasa zile zinazohama hama kwani mashine hizo zinatumia mtandao wa Intaneti kama simu. “Biashara yoyote inaweza kutumia mashine za malipo kwa njia kadi (P0S Device) kupokea malipo ya bidhaa au huduma. 

Huduma hii inatarajiwa kuongeza tija kwenye maeneo ya biashara kwa kupunguza hatari zitokanazo na utunzaji fedha taslimu na pia itapunguza safari za wafanyabiashara kwenda katika matawi ya benki kuweka fedha na sasa wataweza kutumia muda mwingi zaidi kuendesha biashara. 

Mashine za malipo kwa njia ya kadi zinaweza kuwekwa sehemu ya kudumu karibu na wateja au kubebeka kulingana na mahitaji ya mteja” alisema. Alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo kutaboresha huduma za kidijitali za benki hiyo kwani sasa wateja wataweza kuangalia na kupakua taarifa za mihamala na fedha kila siku na za kila mwezi jambo ambalo litawasaidia wafanyabiashara katika kutunza mahesabu. Uzinduzi wa mashine hizo ni sehemu ya mkakati wa FNB kuwa kiongozi katika huduma za benki na sehemu ya mpango wa benki hiyo kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuwawekea wafanyabiashara mazingira mazuri ya kuendesha shughuli zao. 

Arumasi alisema kuwa sambamba na uzinduzi huo, benki hiyo imepokea tuzo ya ufanisi wa kadi za fedha na malipo za VISA kwa mwaka 2016 baada ya kuwa imekidhi viwango vya ubora kimataifa na kuwa benki bora nchini katika utoaji wa huduma kupitia kadi hizo. Hii ni kutokana na huduma bora kwa wateja, ufanisi, na mfumo wa kuaminika katika kuendesha shughuli za kibenki. 

Programu ya tuzo za viwango vya ubora za VISA kimataifa ilianzishwa mwaka 1992 ili kutambua taasisi za kifedha dunia nzima zinazotoa huduma bora kwa watumiaji wa kadi za VISA kwenye maeneo mbalimbali. Kila mwaka tuzo hizo utolewa kwa taasisi hizo kutokana na kukidhi viwango vya ubora katika utendaji, ufanisi na mifumo madhubuti ya kudhibiti udanganyifu. 

Meneja Masoko wa First National Bank Tanzania, Bi. Blandina Mwachang’a (Kushoto), na Mkuu wa kitengo cha bidhaa na huduma za kimtandao, Bw. Silvest Arumasi ( kulia) wakionyesha Mashine za malipo kwa njia ya kadi ambazo benki hiyo imezindua ili kuimarisha matumizi kadi za benki kama mbadala wa fedha taslimu Katikati ni Meneja wa Huduma za Kadi, Bi. Emma Kilimba akiwa ameshikilia tuzo ya ufanisi wa mashine hizo za malipo kwa mwaka 2016. 

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA MJINI DODOMA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma
 Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya  uliofanyika kwenye Chuo Cha Mipango mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma .

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA ARDHI,MAJI,NISHATI NA MAZINGIRA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiongoza kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
ari2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
ari3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
ari4
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
ari5
Baadhi ya Viongozi wa   Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
ari6

Baadhi ya Maafisa wa Idara mbali mbali katika  Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 17/10 /2016.

OMEGA MINISTRY CHURCH OF ALL NATIONS YAANDAA SEMINA YAKUOMBEA TAIFA

$
0
0
Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa.
Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry.

…………………………………………………………..

Lilian Lundo, MAELEZO.

KANISA la Omega Ministry of All Nations lenye makao yake Makuu Mbezi Afrikana, Jijini Dar es Salaam limeandaa Semina ya Injili ya Neno la Mungu la kuiombea Taifa na Viongozi wa Nchi, inayotarajiwa kufanyika Urafiki Nyangumi Jijini Dar es Salam Octoba 21 mpaka 23 mwaka huu.

Nabii Samson Rolinga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Semina hiyo yenye lengo la kuiombea Taifa, Viongozi wa Nchi na kuwafungua watu katika vifungo mbalimbali.

“TutaliombeaTaifa lirudi katika misingi ya Mungu, vile vile tutawaombea watu waliofungwa na nguvu za giza na magonjwa kama vile kanda, ukimwi na utasa,” alifafanua Nabii Rolinga.Amesema magonjwa yapo lakini pia yapo magonjwa ambayo yanatengenezwa na watu ilikumdhoofisha mtu, hivyo katika semina hiyo kutafanyika maombi ya kuombea magonjwa hayo pamoja na matatizo yote yanayotokonana roho za kurithi.

Vile vile amesema kuwa kumekuwa na matatizo mengi sana ambayo watu hawana majibu ya matatizo hayo mfano vijana wengi kutokuwa na kazi na kukata tama huku wakijraribu kupambana na matatizo hayo kwa njia ya mwili.Nabii Rolinga amesema kuwa lengo lake nikuonyesha chanzo cha matatizo na kuyatatua kwa njia ya maombi pamoja na kueleza namna ufalme wa giza unavyofanya kazi.

Kwa upande wake Nabii Donald kutoka Mwanza amesema kuwa atakuwepo katika semina hiyo ambayo itashughulikia matatizo ya Roho, kuvunja yanayoonekana katika ulimwengu wa Roho pamoja na kuombea nchi na Utawala wa nchi.

Aidha amesema kuwa watumishi wa Mungu wana jukumu kubwa la kuwaombea Viongozi wa Nchi na Rais ili Mungu awasimamie katika majukumu yao ya kila siku ya kuliongozaTaifa.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA PROFESA MUHONGO

$
0
0

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili namna Serikali ya Uingereza inavyoweza kufanya kazi na Tanzania kwenye uboreshaji wa sekta za Nishati na Madini.

Balozi Cooke alifanya mazungumzo na Profesa Muhongo pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA)

Akielezea kuhusu Sekta ya Nishati nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme kama vile gesi, maji, jotoardhi, makaa ya mawe, upepo, jua na kukaribisha wawekezaji kutoka Uingereza kushirikiana na Serikali kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini hususan katika maeneo ya vijijini.

Aliongeza kuwa, Serikali imeanza kutumia gesi yake iliyogunduliwa kwa wingi kwa kiwango cha futi za ujazo trilioni 57.2 kwa kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam na kuendelea kusema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kusambaza gesi mikoani pamoja na nyingine kuuzwa nje ya nchi.

“Kuna nchi zilizopo Ukanda wa Afrika Mashariki zimeomba bomba la gesi liende kwao; hii itatuwezesha sisi kufanya biashara pamoja nao na kuingiza fedha za kigeni,” alisema Profesa Muhongo

Aliongeza kuwa, mikakati mingine inayofanywa na Serikali ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi kimiminika ( Liquefied Natural Gas Plant) na kiwanda cha mbolea katika eneo la Kilwa mkoani Lindi na kiwanda kingine cha mbolea katika mkoa wa Mtwara.

Alisisitiza kuwa, bado Serikali inaendelea na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali nchini na kuomba kampuni za Uingereza zenye uzoefu kujitokeza na kuwekeza nchini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nishati kwa Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke (kushoto). 
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akielezea mikakati ya nchi yake katika kuisaidia Tanzania katika uboreshaji wa sekta ya nishati nchini. 
Watendaji kutoka kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). 

MASAUNI ATAKA IFUTWE G.N.U NDANI YA KATIBA YA Z'BAR.

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameshauriwa kuondosha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka mwaka 1984.

Ushauri huo umetolewa na Katibu  wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar,  Hamad Yussuf Masauni katika Majumuisho ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama huko katika Ukumbi wa Amani Mkoa wa Mjini, Unguja.

Alisema huu ndio wakati mwafaka wa kuondosha mfumo huo kwani hauna tija katika maendeleo ya nchi badala yake ukiachwa itakuwa ni fursa kwa wapinzani kurudi tena katika serikali baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Alieleza kwamba nia ya CCM kukubali kuingia katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (SUK) ni kushirikiana na vyama vya upinzani katika mipango ya maendeleo ya nchi pamoja na kumaliza siasa za chuki, hali ambayo CUF haikutaka kubadilika hivyo hakuna haja ya kubakisha mfumo huo katika Katiba ya Zanzibar.

Masauni aliwasihi Wawakilishi wa CCM kuhakikisha wanalinda kwa vitendo  maslahi ya Chama kwa kuandaa taratibu zote za kisheria kwa kufuta kipengele ndani ya Katiba kinachoeleza uwepo wa mfumo huo.

Alisema hatua ya mwisho itakuwa kurudi kwa wananchi kupiga kura ya maoni ya kukubali ama kukataa kuendelea na SUK, jambo ambalo kwa sasa ni rahisi kwani wananchi wengi hasa wafuasi wa CCM hawataki kuendelea na serikali hiyo.

“ Huu ni wakati mwafaka wa kuifuta CUF katika siasa za Zanzibar kwani hatuwezi kuendelea kuwa na ushirikiano na Chama kinachojali maslahi binafsi pamoja sera za utengano badala ya kuwaunganisha wananchi.
 Akizungumza Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar,  Hamad Yussuf Masauni , na wafusi wa CCM katika mkutano wa majumuisho katika ziara yake aliyofanya Wilaya za Amani na Mjini Kichama Zanzibar.
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakifuatilia kwa makini mkutano wa majukuisho ya Ziara ya Masauni uko katika ukumbi wa Mkoa wa Mjini kichama uliopo Amani Zanzibar.

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa UN Ukanda wa Maziwa Makuu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe.Said Djinnit. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Oktoba, 2016 .
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Omary Mjenga (wa kwanza kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ally Ubwa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bw. Djinnit (hawapo pichani). 
Mkutano ukiendelea. 
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASIKITISHWA NA MWEKEZAJI KUBADILI MATUMIZI YA KIWANDA NA KUKITELEKEZA

$
0
0
koro1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda  cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji amekifanya kuwa Ghala nakukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa Kiwanda hicho kipo wilaya ya Rungwe Mkoani Lindi Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Rungwe Mkoani Lindi(Picha na Chris Mfinanga)
koro2

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyo haribika ambayo yalikuwa yanamilikiwa nakiwanda cha kukamua ufuta  ILULU kiwanda hicho kipo wilani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliye kichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala lakuhifadhia bidhaa kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi    picha na Chris Mfinanga

DKT. CHARLES MWIJAGE AITAKA NBS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA TAFITI YA VIWANDA VIDOGO NCHINI

$
0
0
Na Beatrice Lyimo -MAELEZO-Dar es Salaam 

SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.

Dkt Mwijage alisema kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.

Alisema katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua uchumi wan chi.

“Asilimia 25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.
Wazi wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu mbalimnbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
 (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO) 


Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images