Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109922 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA UTAMADUNI LA NAMASTEE TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi akiwasha mshumaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vikundi vya Utaamduni wa kihindi vikitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi (kulia)akimsikiliza Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya (katikati) wakati wa onesho la uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Wageni waalikwa wakifatila burudani mbalimbali wakati wa onesho la Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM.



Asasi Ya Vijana Ya TYVA yawakutanisha vijana kujadili haki na wajibu wao katika Jamii

$
0
0
Meneja Mradi, Ushirikishwaji wa Vijana - TYVA, Alfred Kiwuyo  akiwaelezea washiriki dhima ya kongamano la vijana waliokutana kujadili haki na wajabu kwa vijana katika maendeleo ya Taifa. (Picha na Geofrey Adroph)

TYVA  ni asasi ya vijana ambayo imejikita na Kujipambanua kupigania jamii yenye haki na usawa, amani na misingi ya kidemokrasia na yenye ushiriki hai na wenye tija kwa vijana katika shughuli za maendeleo imeandaa kongamano hili kuwawezesha vijana kujadili Haki na Wajibu kwa Vijana na mstakabali wa Taifa kwa ujumla. Kongamano hili pia lilikuwa na dhima ya kupanua uelewa na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendele ya Taifa kwa ujumla.
Wakili Chikulupi Kasaka, akitoa mada ya Haki na Wajibu wa Vijana kwa vijana mbalimbali wa vyoni na mtaani waliokuta kujadili haki na wajibu wao katika jamii iliyofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es salaam iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA .

Mwenyekiti wa Bodi ya washauri ya Vijana(YAB) Femina Hip, Hassan Pukey akitoa mada kwa vijana waliofika katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA ili kujadili haki na wajibu wa vijana na katika jamii.

Makamu Mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumzia mchakato wa baraza la vijana na jinsi vijana walivyoshirikishwa katika kutoa maoni ya mchakato mzima iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA na kufanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam leo
Picha ya Pamoja.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

DC NDEJEMBI ASIMAMISHA UCHIMBAJI MADINI KATIKA KIJIJI CHA SILWA KATA YA PANDAMBILI NA KUMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI CHA SILWA.

$
0
0
Leo (jana) baada ya shuguli ya kuadhimisha miaka 17 toka Mwalimu Nyerere afariki, DC Ndejembi na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Kongwa Ndg Izengo walifanya ziara ya kushtukiza katika Kijiji Cha Silwa kata ya Pandambili Baada ya kupata taarifa kuna uchimbaji wa madini aina ya KONISUPHIRE unaofanyika na wafanyabiashara bila kua na vibali vyovyote. 

Baada ya kufika eneo la tukio wakabaini mtendaji wa kijiji Ndg Michael Boniface Magenje alitoa eneo bila kutoa nakala kwenye Kata wala Halmashauri na hakuhusisha serikali ya kijiji. Hivyo DC akachukua hatua kusimamisha uchimbaji na kumuagiza Mkurugenzi kumsimamisha kazi mtendaji huyo mara moja kwa kutokufuata taratibu.

WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI AZINDUA RASMI KAMISHENI YA TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi,Mwenyekiti,Katibu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo
Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ATEMBEA SIKU 21 KWENDA DODOMA KUMFUATA WAZIRI MKUU ILI KUFIKISHA MALALAMIKO YAKE YA KUPORWA ARDHI.

$
0
0
Mkazi wa Kilindi, Tanga Angela Basso , aliyetembea kwa miguu kwa muda wa siku 21 pamoja na Watoto wake Janeth Peter (9) na Happy Peter (7) kuja Mkoani Dodoma kuonana na Waziri mkuu ili kupeleka malalamiko yake ya kudhulumiwa mashamba yake ya hekari 30 na kuchomewa nyumba .


=====  ======  =======
MKAZI wa Kilindi mkoani Tanga, Angela Basso, akiwa na watoto wake wawili Happy(7) na Janeth Peter(9), amelazimika kutembea kwa mikuu kwa siku 21 hadi mkoani Dodoma kwa lengo la kumuona Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili amsaidie kurudishiwa hekari 30 za mashamba yake aliyozoporwa.

Basso alifika mjini Dodoma akiwa na watoto wake hao, ambapo alisema aliona ni vyema kwenda Dodoma kuonana na Waziri Mkuu kutokana na kuporwa mashamba na kuchomewa nyumba yake katika kijiji cha Kwendigole wilayani Kilindi na wanaume wawili ambao waliojitokeza kwa nyakati tofauti wakidai ni maeneo yao.

Alisema alipita hatua zote zinazotakiwa kuomba mashamba, ambapo awali alipatiwa hekari 10 na kijiji na akazifanyia shughuli za kilimo na kujenga nyumba yake ya kuishi, lakini baada ya kwenda kujifungua alikuta mazao yamefyekwa na yeye kutakiwa kuondoka kwenye eneo hilo.

Mwanamke huyo alisema baada ya kunyang’anywa alifikisha malalamiko yake kuanzia uongozi wa kijiji hadi wilayani na baadaye akapatiwa eneo jingine la hekari 20, lakini alijitokeza mtu mwingine na kudai eneo hilo ni mali ya kanisa, licha ya kumiliki kihalali eneo la Hembekali.

“Nilikwenda kushtaki kwa serikali ya kijiji, kata na baadaye kwenda kwa mkuu wa wilaya ambako iliamuliwa nirudishiwe mashamba yangu, lakini hawakufanya hivyo mwisho wa siku nikafukuzwa kabisa kuishi kwenye eneo hilo,” alisema Basso

Mwanamke huyo alisema baada ya kutimuliwa alianza kuishi maisha yake kituo cha mabasi Muheza na baadaye alifukuzwa kituoni hapo kwa madai watu hawaruhusu kulala ama kuishi hapo na ndipo akaamua kuanza safari ya Dodoma baada ya kusikia Waziri Mkuu amehamia Dodoma.

Akisimulia machungu ya safari yake, Basso alisema akiwa njiani walikuwa wakila mahindi ya kukaanga na maji ya kunywa na kulala porini muda mwingine giza linapowakuta katikati ya pori.“Naomba kusaidiwa jamani nimeanza kufuatilia tangu mwaka 2012 lakini bila mafanikio jambo ambalo limechangia familia yake kusambaratika kutokana na kukosa pa kuishi huku watoto wangu hawa wakikosa elimu kwa kutangatanga,”alisema Mwanamke huyo

Basso aliomba Serikali itende haki ili yeye aweze kupata haki yake ya kurejeshewa mashamba yake na kurudi katika eneo hilo ili watoto wake wawili wapate nafasi ya kusoma. Mwanamke huyo alisema kwa sasa amekuwa kama mkimbizi kutokana na kukosa hana mahali pa kuishi huku mumewe naye akiikimbia familia yake baada ya kuporwa ardhi hiyo ambayo ilikuwa kama kitega uchumi chao.

WAZIRI MUHONGO AKAGUA NYUMBA ZILIZOATHIRIWA NA UPEPO MKALI ,MUSOMA MKOANI MARA

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter M. Muhongo akiongea na baadhi ya Wananchi ambao Nyumba zao ziliathirika na Upepo Mkali katika kijiji Cha Kiemba Kata ya Ifulifu. Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 Usiku upepo mkali ukiandana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44 na kusababisha madhara makubwa
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Vijijini akikagua baadhi ya nyumba zilizoathirika na upepo mkali katika kijiji cha Kiembe Kata ya Ifulifu Wilaya ya Musoma. Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 usiku upepo mkali ukiandamana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter M. Muhongo na Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini akiwa amekaa kwenye moja ya nyumba akikagua baadhi ya Nyumba zilizoathirika na Upepo Mkali katika kijiji Cha Kiemba Kata ya Ifulifu Wilaya ya Musoma Mkoani Mara. 

Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 Usiku upepo mkali ukiendana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44. Nyumba Nyingi zilizoathirika ni zile za mgongo wa Tembo. Katika kukagua athari za uharibifu ilibainika myumba Tano ziliathirika vibaya kiasi cha kusababisha wamiliki wake kulala Nje.

Hata, hivyo ilielezwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Viongozi wa Halmashauri walitembelea eneo hilo baada ya kupata taarifa za athari za kuezuliwa paa na kuahidi kuagiza tathmini ifanyike ili Serikali iweze kutoa masaada kwa Wananchi hao.

kuongea na Wananchi hao, Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo hilo la Musoma Vijijini aliiwaambia Wananchi hao kuwa Serikali ya Rais Magufuli ipo pamoja nao na ametumwa kuwapa pole kutoka kwa Viongozi wa juu wa Serikali. "Ndugu wananchi, nimetumwa na Rais wetu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli niwape pole sana kwa kukutwa na kadhia hii ya kuenguliwa Nyumba Zenu na upepo, aidha, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanawapa pole pia na wanawatakia heri wale wote walioathirika"

Prof. Muhongo aliwaelekeza Viongozi wa kijiji hicho kuwa wahakikishe wanafanya tathmini ya kweli kwa kupita kila Nyumba iliyoathirika na yoyote atakaegundulika Amedanganya ili alipwe zoezi zima litaahirishwa na kurudiwa upya, pia wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha, aliwaahidi Wananchi hao kuanza kupewa misaada Baada ya kikao Cha Halmashauri kupitia taarifa ya tathmini jumatatu tarehe 17/10/2016 na kuwaelekeza Viongozi wa Halmashauri kufanya kazi hiyo kwa haraka.

Prof. Muhongo alikuwa Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya kukagua umeme Sambamba na kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere iliyofanyika nyumbani kwake Butiama tarehe 14/10/2016

HABARI PICHA KWA HISANI YA ANNA NKINDA 

VIJANA WATAKIWA KUFUATA MAFUNDISHO YA BABA WA TAIFA MWALIMU J.K NYERERE

$
0
0
Na Emmanuel Matinde-Kigoma

VIJANA wametakiwa kufuata mafundisho ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, juu ya uwajibikaji katika kazi,kuwa wazalendo, kudumisha amani na kuwa walinzi wa amani ya nchi yao.

Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba, metoa wito huo juzi katika kijiji cha Katanga wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani humo katika siku ya kumbukumbu ya miaka 17 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema wakati wa uhai wake Mwalimu alihubiri uwajibikaji, uzalendo, amani na upendo na kupinga rushwa, hivyo vijana wana wajibu wa kuyazingatia yote hayo kwa manufaa ya taifa.“Tuendelee kufanya kazi ili kumuenzi mwalimu kama vile rais wetu Magufuli anavyofanya kwa vitendo,”alisea Mh.Zainabu.

Kuhusu suala la amani Mh.Zainabu, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Chipukizi Sekondari na vyuo vikuu, alisema vijana hasa waishio mpakani na nchi jirani wanalo jukumu kubwa la usalama wan chi yao kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na kutoa taarifa pindi wanapoona watu wanaowatilia mashaka.

Kauli ya mbunge huyo inakuja siku moja tu baada ya askari polisi wakishirikiana na askari wa jeshi la wananchi kuwaua majambazi wawili waliokuwa wanajiandaa kufanya uhalifu katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko baada ya kukabiliana nao kwa risasi.Nao baadhi ya vijana katika kijiji cha Katanga wakiwemo Nestory John na Honorata Petro, walieleza utayari wao katika kuhakikisha kwamba wanafichua mtu yeyote mwenye nia ya kuhatarisha usalama katika maeneo yao.

Katika ziara yake Mh.Zainabu Katimba, alilenga kukutana na vijana, kusikiliza changamoto zao na kuhamasisha vijana kuanzisha na kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na yeye kuahidi kushirikiana nao ili kupata fedha za kuanzisha miradi ya ujasiriamali ikiwemo asilimia 5% ya fedha zitolewazo na halmashauri kwa ajili ya vijana.

Vile vile alitoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuwezesha usajili wa vikundi 18 vya vijana katika wilaya za Kigoma vijijini, Buhigwe, Kasulu, Kibondo na Kakonko.
Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba.

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA AKUTANA NA MAKUNDI YA MBALI MBALI YA WAKAZI WA MJI WA DODOMA WANAOENDESHA SHUGHULI ZENYE MAHUSIANO NA MAZINGIRA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma ambapo alisisitiza dhambi ya kuharibu mazingira haisameheki hivyo kuwataka kila mmoja awe mstari wa mbele katika kutunza mazingira.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma.
 Vijana wa DOYODO ni sehemu ya makundi yaliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais mjini Dodoma.
 Wazee Mashuhuri wa mji wa Dodoma ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Dampo la kisasa lililopo Chidaye ambalo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo.
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Mazingira na Taka ngumu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Barnabas Faida (kushoto) akielezea utaratibu utakaotumika wa kutupa taka katika dampo la kisasa la Chidaye kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumia mwezi novemba.
Mhandisi wa Majengo Bi. Gladness Pesha akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan mgawanyo wa ofisi katika jengo la Mkuu wa mkoa wa Dodoma.
  Jengo la Ofisi ya Mkoa wa Dodoma lililopo eneo la Makulu ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika.

                                      .................................................................

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ametaja vigezo vinavyokwamisha Dodoma kuwa Jiji ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na uzembe wa ukusanyaji mapato.

Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na wazee, wafanyabiashara, vikundi vya usafi wa mazingira na viongozi mbalimbali wa serikali, mjini hapa.

Alisema serikali inapohamia Dodoma lazima kuwe Jiji na ili kupata hadhi hiyo mambo mengi yanahitajika ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira.

Samia alisema mkoa huo umeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa asilimia kubwa yamesababishwa na shughuli za kibinadamu kwa kukata miti ovyo na kuifanya Dodoma kubadilika tofauti na ilivyokuwa awali.

“Wakati nakuja Dodoma mwaka 2002 kulikuwa na baridi sana nakumbuka wakati ule kwa nyumba za zamani ambayo hata ninayoishi kwasasa hazikuwa na kiyoyozi na feni zenyewe zilipachikwa tu hazitumiki maana hali ya hewa ya Dodoma haihitaji kiyoyozi lakini kwasasa joto lipo na baridi ipo ya msimu,”alisema Samia






GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU JUU YA KUDUMISHA AMANI KATIKA FAMILIA , JUKWAA LA VIJANA JIJINI DAR

$
0
0
Kila Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na wao. Katika jukwaa la mwezi huu kulikuwa na mada inayosema: "Nafasi  ya mtoto wa kike katika jamii" ambapo majadiliano yalilenga zaidi kutambua nafasi hizo, changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike pamoja, namna ya kuzitatua na jinsi gani mtoto wa kike anavyoweza kusimamia malengo yake kufanikiwa.

Aidha katika jukwaa hilo la vijana Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation  kupitia Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini, Martha Nghambi alitoa pia elimu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha  amani ndani ya familia, ambapo alisema kuwa ili amani iweze kudumishwa na watu waishi bila kuwepo na mifarakano ni lazima kujenga mahusiano mazuri kuanzia chini yaani wanafamilia kuweza kuelewena kwa kuwahusisha wazazi na watoto ambapo hawa wakiishi vema basi hakutakuwa tena na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa kila mtu analojukumu la kulinda amani.
Mwendeshaji wa Jukwaa la Vijana lililofanyika Tandale leo Jamal Magabilo akitoa neno la utangulizi na kuwakaribisha wageni waalikwa wote katika jukwaa
Vijana, Wazazi na wadau mbalimbali wakiwa katika jukwaa hilo
 Picha ya Pamoja
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

MAHAFARI YA TISA YA SHULE YA HERITAGE ENGLISH MEDIUM SCHOOL JINSI YALIVYOFANA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
MAHAFARI ya tisa ya Wanafunzi wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) jinsi ilivyofana jijini Dar es Salaam leo.

  Wanafunzi wa Shule ya English Medium ya Heritage iliyopo Banana Ukonga jijini Dar es Salaam wa wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati wa mahafari ya wanafunzi wa shule hiyo wanaohitimu masomo yao ya Darasa la Saba katika shule hiyo.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Mahafari ya tisa ya  Darasa la Saba katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) mara baada ya kutembelea maonesho ya masomo mbalimbali ya wanafunzi hao.
Amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa kuwafundisha watoto hao hasa watoto wa darasa la awali katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) hasa katika taaluma pamoja na kuwafundisha watoto hao kuwa na hofu ya Mungu.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ikiwa na sera ya Kusimamia na Kuimarisha elimu katika shule za awali katika shule zote za msingi kuwa na madarasa ya awali ili kuwezesha kutoa watoto wakiwa na uelewa bora.

Amesema katika Manispaa ya Ilala ina shule msingi za serikali 121, Shule za Binafsi za msingi 89 na shule za awali za serikali 99 pamoja na shule za binafsi za awali 84.
 Mwalimu Mkuu wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School), Kebaso Elia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafari ya tisa ya Darasa la Saba katika shule hiyo.
Amewaomba Wizara ya elimu, sayansi na Teknologia iwapitishe waandishi wa vitabu vya kiada na ziada  ili kusitokee mkanganyiko katika ufundishaji wa watoto na kuwa na utofauti kati ya vitabu.
 Wahitimu wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) wakiingia ukumbini jijini Dar es Salaam leo katika mhafari ya tisa ya shule hiyo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

GLOBAL ILIPOWATEMBELEA WAFUNGWA GEREZA LA UKONGA DAR ES SALAAM

$
0
0

Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya tamasha la michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.

Akiongea katika tamasha hilo, Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi, Eric Shigongo, amewaambia wafungwa kuwa dhamra ya ujio wao gerezani hapo ni katika kuonyesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.

Shigongo aliwatia moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya kubadilika na kuwa raia wema.“Kila mwanadamu anao wajibu wa kubadili maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka, kwa nini wewe ushindwe?” aliuliza Shigongo.

Aliongeza: “Najua wengi wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwa kuwa mmehukumiwa, hizi ni hukumu za wanadamu, mnao uwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza."

Wadau wengine walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza hilo la Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao vikiwemo vifaa kama sabuni, soda na kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.

Katika tamasha hilo wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika kijiko, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji, kuimba kwa mtindo wa kufokafoka, ngoma za jadi na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta.

Picha zote na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza.

Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (aliyesimama), akiwasalimia wafungwa (hawapo pichani) wa gereza la Ukonga katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere (Nyerere Day) Oktoba 14, Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitia saini kitabu kitabu cha wageni gerezani Ukonga katika Tamasha la Michezo wakati wa kuadhimisha Nyerere Day. Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Stephen Mwaisabila, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Thom Nyanduga, Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo na Abdalah Mrisho ambay ni Meneja wa Global Publishers.

Johnson Nguza aka Papii Kocha (wa pili kushoto) akitumbuiza na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa tamasha hilo.
Baadhi ya wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia kwa magunia katika tamasha hilo.

HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA MARKAZ SHAAFIYATUL AZHARIYA MBEZI SALASALA, DAR ES SALAAM.

$
0
0
Asalaam alaykum warahmatullahi wabarakatu. 
Alhamdullilah siku Mpya ya Jumapili , tumeamkia Eneo la kazi 
HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA MARKAZ SHAAFIYATUL AZHARIYA
MBEZI SALASALA, DAR ES SALAAM.
Mchango wako ni Muhimu sana tuweze kuhitimisha zoezi hili la Ujenzi .
Inajulikana hali imebana kigawe kidogo chako kwa kutengeneza Akhera yako.
Tia nia katika katika mambo yako yote kupitia Ushiriki wa Jambo hili la Allah akufanyie Wepesi na atufanyie Wepesi katika Mambo yetu yote .
Tuma Mchango wako kupitia Namba 0715800772.
TUMIA NDUGU ZAKO NDUGU, MARAFIKI, JIRANI, 

WAISLAM WENZETU 
huenda na wao wakachangia.
Na Mratibu Msimamizi GHALIB N MONERO.
16/10/2016.


KILIMANJARO WAADHIMISHA MIAKA 17 YA KUMBUKUMBU CHA KIFO CHA BABA WA TAIFA KWA KUOTESHA MITI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru wakati alipowasili katika chanzo cha maji cha Shiri kwa ajili ya zoezi la kuotesha miti ikiwa ni kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa ,Hayati Mwl Julius Nyerere.
Wakuu wa wilaya za Hai na Moshi ,Gelasius Byakanwa (wa pili toka kulia) na Kippi Warioba (wa tatu toka kushoto waliungana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro katika zoezi hilo.kulia ni Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour.
Eneo lilipo jirani na chanzo cha maji cha Shiri ambalo liliandaliwa kwa ajili ya kuoteshwa miti.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la uoteshaji miti.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji la Shiri Njoro lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

RATIBA YA MAZISHI YA MWANASHERIA YUSTA MSOKA HAPA DAR ES SALAAM

$
0
0

Marehemu Advocate Yusta Msoka enzi za uhai wake.

Jumuiya ya wanafunzi kutoka Shule ya msingi Changa na Shule ya sekondari Usagara zilizopo mkoani Tanga pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam tunasikitika kutangaza kifo cha aliyewahi kuwa mwanafunzi mwenzetu Marehemu Advocate Yusta Msoka kilichotokea Majuzi hapa Dar es salaam.

Sisi kama wanajumuiya wenzake kupitia shule mbalimbali tulizopitia tunatoa pole zetu kwa pacha mwenzake Mwanasheria Felista Msoka na wana familia kwa ujumla, tunaungana nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.  
Taarifa kutoka kwa familia ya marehemu zinasema mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 17/10/2016 hapa jijini Dar es salaam katika makaburi ya Chamanzi - Mbagala ambako ni jirani na wazazi wake wanapoishi huko Mbagala kuanzia saa 5 asubuhi kwa kutanguliwa na Chakula/ Ibada kisha kuishiwa na Mazishi katika nyumba yake ya Milele.

Kwa wale wote ambao watapata taarifa hii tunaomba umjulishe na mwingine ili tuweze kuungana pamoja kumsindikiza mwenzetu. a

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA 
JINA LAKE NA LIHIMIDIWE

AMIN. 

Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wapitisha Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo ya Afrika.

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


              


 



               


Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo (The African Charter on Maritime Security, Safety and Development) umepitishwa katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Afrika (The AU Extraordinary Summit) uliofanyika tarehe 15 Oktoba, 2016 Lome, Togo. Kupitishwa kwa Mkataba huu kumefuatia makubaliano yaliyofikiwa katika Mikutano ya Kilele ya Wakuu wa Nchi za Afrika iliyofanyika Younde Juni, 2013 na Visiwa vya Shelisheli Februari,2015.
Tanzania imewakilishwa katika Mkutano huo na Mhe. Balozi. Dkt. Augustine P. Mahiga (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye hakuweza kuhudhuria Mkutano huu kwa sababu ya Majukumu mengine ya Kitaifa.
Akihutubia Mkutano huo Balozi Dkt. Mahiga alisema, Mkataba huo ni kati ya nyaraka muhimu zitakazoelimisha kuhusu kutunza amani ya Dunia, usalama na maendeleo katika karne hii ya 21. Alisisitiza kwamba Bara la Afrika liko kati ya bahari kuu mbili yaani Atlantic na Hindi ambazo ni kati ya bahari zilizo na shughuli nyingi sana za usafirishaji duniani. 
Tanzania ikiwa katika nusu ya ukanda wa pwani ya Mashariki na pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi yenye urefu wa Kilomita 1400, Mkataba huu ambao Balozi Mahiga ametia sahihi kwa niaba ya Tanzania ni muhimu sana hivyo amewasihi wanachama wengine kuhakikisha wanafanya hivyo.
Sambamba na hilo Balozi Dkt. Mahiga amesema Mkataba huu si muhimu tu kwa Afrika kulinda bahari na rasilimali zake bali ni muhimu kwa dunia nzima. Balozi. Dkt. Mahiga ameomba Nchi zote na Mashirika ya Kimataifa kuunga mkono utekelezaji wa mkataba huu. Kufuatia kupitishwa kwa mkataba huu ameiomba Sekretariati ya Umoja wa Afrika kupeleka Mkataba huu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katika Jumuiya ya Kimataifa ili kuweza kutambuliwa.
Aidha, Balozi Mahiga amesisitiza kuwa bahari ni hadhina muhimu si tu ya samaki na gesi bali rasilimali nyinine za thamani kama vile madini ambazo zimekaa tu chini ya bahari hivyo ni jukumu la kila mwana Afrika kuhakikisha analinda rasilimali muhimu tulizo nazo zikiwemo hizi ambazo zinapatikana baharini.
Akimalizia hotuba yake Balozi. Dkt. Mahiga alisisitiza “Hivi karibuni bahari hizi ( Atlantic na Hindi) zitakuwa chanzo muhimu cha nishati, hivyo kusaidia jitihada za  kuleta maendeleo kupitia rasilimali za bahari, naamini mkataba huu utakuwa ni silaha muhimu katika kulinda rasilimali hizi za bahari kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo”. Balozi. Dkt. Mahiga ameusihi Umoja wa Afrika na Wanachama wote kuendelea kuuboresha Mkataba huu na kupitisha viambasho muhimu na hatimaye kuharakisha kuuridhia Mkataba huu ili utekelezaji wake uanze bila kuchelewa.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 16 Oktoba, 2016.

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0


SIMU.TV: Diwani wa kata ya Kaloleni ambae pia ni mjumbe wa chama cha mapinduzi, amenusurika kifo baada ya kundi la wamasai wenye silaha kali kumshambulia; https://youtu.be/T47pLU43h-g

SIMU.TV: Wananchi wilayani Mkuranga wamepinga maamuzi ya halmashauri yao katika maamuzi yaliyofikiwa juu ya mgogoro wa ardhi uliosemekana kumalizika hapo awali; https://youtu.be/5tGyoSacZzI

SIMU.TV: Waumini wa dini ya kiislamu kupitia dhehebu la Bohora, wametoa msaada wa Bajaj mbili kijana Said Ally aliyetobolewa macho;https://youtu.be/xZjK1UfQa0I

SIMU.TV: Makamu wa rais mstaafu Dr Mohamed Ghalib Bilal, amesema dini ya kiislamu daima imekuwa mstari wa mbele katika kufundisha matendo yaliyo mema; https://youtu.be/m_94JaHIi1g

SIMU.TV: Mbunge wa jimbo la Monduli Julius Kalanga, amewataka jamii ya wafugaji ya Kimasai kuachana na wizi wa mifugo na kuachia sheria kufuata mkondo wake; https://youtu.be/uz_MhHMTYOU

SIMU.TV: Wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe, wamehimizwa kuendelea kupanda miti kwa wingi ili kulinda mazingira;https://youtu.be/yzaPGOF5pes

SIMU.TV: Ligi kuu Tanzania bara imeendelea kurindima hii leo katika viwanja mbalimbali, na huu hapa ni mkusanyiko wa matokeo ya michezo hiyo; https://youtu.be/I7Je7LM9sKU

Wadau wa soka mkoani Geita wameelezea kilio chao cha kukosa ligi mbalimbali ambazo zingewawezesha vijana kuachana na mambo yasiyokuwa na faida; https://youtu.be/Zy16BUn2W2E

SIMU.TV: Ili kuandaa timu bora ya taifa nchini, wadau wa michezo nchini wanatakiwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za kusaka vipaji vya soka na kuviendeleza; https://youtu.be/6ZyxtOcJCSw

SIMU.TV: Katika anga za michezo kimataifa hii leo tumebahatika kukukusanyia taarifa za soka sambamba na tenisi, karibu hapa uweze kutazama; https://youtu.be/HA6qvRRTnjs

introducing rudi by Ney lee ft Ray van

WAZIRI MKUU AAGIZA MAPATO YA HOSPITALI YA NACHINGWEA YAKUSANYWE KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

$
0
0
luw2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na watumishi wa Hospitali ya Nachingwea pamoja na wananchi waliofika katika Hospitali ya nachingwea Waziri Mkuu alifanya ziara ya kutembelea hospitalini hapo kwa ajili yakuona na kusikiliza wagonjwa wanavyo pata huduma  

WAZIRI MKUU AAGIZA MAPATO YA HOSPITALI YA NACHINGWEA  YAKUSANYWE KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumiamfumo wa kielektroniki.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Lindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma.

Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi milioni nne kwa siku.

Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.

Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Mohammed kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.“Mkurugenzi hakikisha watendaji wako wa kata na vijiji wamebaini wazee wote katika maeneo yao na kuwatengenezea vitambulisho vitakavyowawezesha kupatibiwa bure,” amesema.

Naye Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema muamko mdogo wa jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za afya.Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.

Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia wananchi kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.

Amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi. “Serikali haitaridhika kuona wananchi wakizagaa kwenye ofisi za halmashauri hiyo bila ya kusikilizwa,” amesema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 16, 2016

introducing NEW AUDIO by MSABILa - "USIUWEKE"

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Murieti mkaoni Arusha wameiomba serikali kuwajengea kituo cha polisi kutoka na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu katika maeneo hayo.https://youtu.be/vDrWN46OoYw

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaasa watumishi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. https://youtu.be/9FuYVRCTpBE

SIMU.TV: Serikali imewaagiza wakala wa hifadhi ya chakua NFRA kupeleka tani 20 za mahindi katika wilaya za Karagwe Kerwa na Misenyi zinazokabiliwa na baa la njaa.https://youtu.be/ebDna8JNtd0

SIMU.TV: Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili imeokoa zaidi ya bilioni 13 zilizokua zikitumika kupeleka wagonjwa wa moyo kupata matibabu nje ya nchi. https://youtu.be/ASzO1xEqldA

SIMU.TV: Tatizo la upungufu wa dawa lilikokua likizikabili zahanati za Vigwaza na Ruvu Darajani limemalizika baada ya kupatiwa msaada wa dawa kutoka kwa diwani.https://youtu.be/9I9vsCFRdCs

SIMU.TV: Askofu mkuu wa kanisa la Morovian Tanzania jimbo la Kusini amempongeza rais Dr John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kuwaletea watanzania maendeleo.https://youtu.be/WJXyjqSVOFg

SIMU.TV: Baadhi ya waendesha pikipiki kutoka mjini Shinyanga wameiomba jamii kuwashirikisha katika kufanya shughuli za kijamii ili kuepuka kutuhumiwa kuwa wavunja sheria. https://youtu.be/Srjc01IZSkw

SIMU.TV: Kiongozi wa madhehebu ya Bohora duniani ametoa msaada wa bajaji mbili kwa kijana Saidi Ally aliyepatwa na mkasa wa kutobolewa macho.https://youtu.be/mG3UYTvqejA

SIMU.TV: Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na Mazingira ameiitaka mamlaka ya maji safi na salama kwa kushirikiana na baraza la mazingira kuwaondoa wananchi wanaoishi kandokando ya mto Morogoro. https://youtu.be/Zks-Dl4H4fg

SIMU.TV: Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara wameshikwa shati na Azam FC na kukubali kutoka sare ya bila kufungana katika uwanja wa Uhuru. https://youtu.be/WwaVnz9TiOE

SIMU.TV: Wadau wa mchezo wa ngumi nchini wameandaa ziara ya wanamichezo wa mchezo huo kutoka Dar es Salaam kwenda kushindana na mabondia kutoka Morogoro ili kuinua mchezo huo hapa nchini. https://youtu.be/_cXXQxXcQTU

SIMU.TV: Kocha wa timu ya Zamaleki amesema bado ana matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya klabu bingwa Afrika. https://youtu.be/dXaNXRL60qc
Viewing all 109922 articles
Browse latest View live




Latest Images