Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

KONGAMANO LA KUMUENZI MWALIMU J.K NYERERE LAFANYIKA WILAYANI IKUNGI

$
0
0
Na Mathias Canal, Singida

Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeungana na Watanzania kote ulimwenguni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Mwasisi wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Octoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.

Katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi limejumuisha Viongozi wa kada tofauti wakiwemo viongozi wa serikali, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vitongoji na vijiji, Viongozi wa siasa, Wazee wa mji wa Ikungi, Maafisa Tarafa na Watendaji, Madiwani, Walimu na wanafunzi ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuchangia mada na kupitisha maadhimio zaidi ya kumi na tano yatakayotoa taswira ya namna ya kumuenzi Mwalimu Nyerere mwakani.

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewasihi wananchi kwa umoja wao  kumuenzi Mwalimu Nyerere katika matendo makubwa na muhimu aliyokuwa anayafanya hususani misingi ya Haki, Ukweli na uwajibikaji.

Amewataka watanzania kuishi katika matakwa ya Mwalimu Nyerere ikiwa ni pamoja na kutokubali kutoa na kupokea Rushwa kwani hayo ni miongoni mwa mambo mengi aliyoyahubiri wakati akiwa waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo na hatimaye kuyahubiri na kuyaishi kipindi akiwa Rais wa kwanza wa Tanzania.

Dc Mtaturu alisema kuwa Tanganyika wakati wa uhuru ilikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi yatokanayo na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, Pia kulikuwa na ujinga uliosababishwa na ukosefu wa elimu bora kwa kiasikikubwa kwani watanganyika wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu walikuwa ni zaidi ya asilimia 90.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsalimu Bi Fumbo Shishiwa aliyejifungua salama mtoto wa kiume na kumuita Magufuli
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Bi Faidha Athumani mara baada ya kumkuta akisubiri matibabu katika Kituo cha afya Ikungi
 Baadhi ya washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano.


BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YAMALIZA TATIZO LA UHABA WA VYOO KWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI IPINDA KYELA

$
0
0
Meneja Mahusiano kwa Umma benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambavyo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 8kwa msaada wa benki hiyo ya Posta Tanzania. 
Baadhi ya wananchi,walimu na wazazi pamoja na wanafunzi shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vilivyo jengwa kwa msaada wa benki ya Posta Tanzania TPB. 
Vyoo vilivyokuwa vikitumiwa na walimu wa shule ya Msingi Ipinda kabla ya kujengewa vyoo vipya na benki ya Posta Tanzania (TPB). 
Muonekano wa jengo la vyoo vya walimu katika shule ya Msingi Ipinda lenye matundu matano ambalo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni8. 

JAFO AWAFAGILIA WATENDAJI NA VIONGOZI TEMEKE KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA SERIKALI.

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya ya Temeke kwa kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa mwezi mmoja aliopita ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye madawati na kuongezwa vyumba vya madarasa.

Mnamo mwezi Septemba mwaka huu, Jafo alizitembelea shule nne za wilaya ya Temeke zilizopo eneo la mbagala na kukutana na changamoto lukuki, zikiwemo kutotembelewa shule hizo na Afisa elimu wilaya toka mwaka huu uanze kitendo kilicho sababisha kutobainika kwa changamoto ili zipatiwe ufumbuzi.

Shule alizozitembelea ni pamoja na shule za msingi Chemchem, Nzasa, Charambe, na Kilamba ambapo Jafo alikuwakuta watoto wa darasa la saba pekee kwa shule ya Chemchem ndio waliokuwa wakikalia madawati.Katika shule ya nzasa, Naibu Waziri huyo aliwakuta watoto wamejazana huku kukiwa hakuna mpango wowote wa ujenzi wa madarasa.

Aidha aliwakuta walimu wakiwa hawana ofisi ya walimu licha ya shule hizo kuwa katika jiji la biashara lenye mapato mengi.Hata hivyo, Shule ya Kilamba pekee ndiyo ilikuwa katika hali ya kuridhisha, na baada ya ziara hiyo alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa Temeke kuzifanyia kazi changamoto alizo zibaini kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Jafo alifanya tena ziara kwenye eneo hilo ili kubaini utekelezaji wa maagizo yake na katika safari hiyo ya pili alifanikiwa kuzitembelea shule alizozitembelea awali pamoja na shule mbili nyingine za Kiburugwa na Kingugi.Alipofika alikuta watoto wote wakiwa katika madawati pamoja na kuanza kwa harakati za kuongeza madarasa na ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule hizo ambazo baadhi zilikuwa hazina.

Kadhalika, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, alimpa taarifa Jafo kuwa shule ya Nzasa itapata jumla ya vyumba saba, Chemchem vyumba vitano, chalambe vyumba vinne na ofisi ya walimu na kilamba kujengewa fensi ya shule.Naibu Waziri huyo aliwashukuru na kuwapongeza viongozi wote wa temeke kwa kujali matatizo ya jamii.

Katika ziara hiyo Jafo aliongozana na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mbunge wa jimbo la Mbagala Issa Mangungu, Meya ya Temeke Chaurembo, Mkurungenzi wa Manispaa ya temeke na wakuu wake wa idara huku akisema viongozi hao ni mfano wa kuigwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilamba, kushoto ni Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu.

MIGOGORO YA ARDHI JIJINI MWANZA MBIONI KUMALIZIKA

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanza zoezi la kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela ili kuyafanyia urasimishaji.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema zoezi hilo limelenga kuondoa migogoro yote ya ardhi na kutoa hati ya makazi kwa wananchi ambao makazi yao yaliyojengwa kiholela yatarasimishwa.

Amesema wale waliojenga katika maeneo hatarishi ikiwemo milimani, hawatahusika katika zoezi hilo hivyo wasiendelee na ujenzi wa makazi hayo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Buhongwa na Luchelele, wameomba migogoro yote ya ardhi inayowakabili ikiwemo kulipwa fidia katika maeneo yao, itatuliwe kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanya tathmini upya na katika maeneo yenye migogoro na kutoa hati za umiliki.

Zoezi hili limejili ikiwa siku chache baada ya Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi, kufanya ziara Jijini Mwanza na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kutembelea maeneo yote yenye migogoro na makazi holela kabla ya zoezi za usaminishaji kufanyika.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa jijini humo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela kabla ya kuyafanyia urasimishaji na kutoa hati ya makazi kwa wamiliki wake.

Kiomoni alifanya ziara ya kutembelea Kata za Buhongwa na Luchelele na kuzungumza na wakazi wa kata hizo juu ya maeneo yenye migogoro na ambayo bado wananchi wanadai fidia ili kutatua changamoto hizo.
Na BMG
Diwani wa Kata ya Buhongwa, Joseph Kabadi (mwenye suti) akizungumza kwenye ziara hiyo na kuelezea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Kata yake kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi kabla ya urasmishaji wa makazi yaliyojengwa kiholela kufanyika katika kata hiyo. 
Wengine ni viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo watendaji wa idara ya ardhi.
Wakazi wa Kata ya Buhongwa Magharibi Kata ya Buhongwa wakiwa kwenye kikao baina yao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kilicholenga kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA MELI MPYA NA YA KISASA YA MV NYEHUNGE II.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa (Kivuko) ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
 
“Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini  kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe”. Alisema Mongella na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
Mama  Gertrude Mongella (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha (kulia), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonard Masale (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo.
“Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini  kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe”. Alisema John Mongella (katikati) na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.

Wasanii wa Muziki wa Singeli waaswa kuzingatia mafunzo ya sanaa ya ujasiliamali

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM 

Wasanii wa Muziki wa Singeli wameaswa kuzingatia mafunzo ya sanaa ya ujasiliamali yatakayowasaidia kuongeza weledi na mbinu za kukuza kazi zao na hatimaye kuwa na sanaa bora kwa ukanda wa Afrika Mashariki. 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam. 

Bi Joyce aliongeza kwa kusema kuwa sanaa ya muziki ni kazi kama kazi nyingine hivyo ni budi kusimamia misingi iliyo bora inayoendana na utamaduni wa kitanzania katika utunzi wa tungo za singeli. 

“Utamaduni ni mali ya jamii hivyo ni jukumu letu sote kupenda,kuthamini na kuendeleza utamaduni wetu kupitia kazi za sanaa na hii itasaidia kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni” alisema Bi.Joyce. 

Aidha aliupongeza uongozi wa EFM kwa kuandaa semina hiyo ambayo imewapa fursa wasanii kupata elimu ya msingi kuhusu muziki na kuifanya kazi ya sanaa kuwa ya thamani kwa jamii. 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mkuu wa EFM Bw.Denis Ssebo na kushoto ni Mkurugenzi wa EFM Bw. Francis Ciza. 
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi akiwasisitiza wasanii (hawapo katika picha) matumizi sahii ya mitandao ya kijamii wakati wa semina ya wanamuziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es Salaam.  
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu(wa tano kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa muziki wa singeli baada ya semina iliyokuwa imeandaliwa na uongozi wa Radio EFM jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence .


MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AELEKEA MKOANI DODOMA KWA ZIARA YA SIKU TATU

$
0
0
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Chalinze Mkoani Pwani leo Octoba 15,2016 alipokua njiani kuelekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa MlandiziMkoa wq Pwani leo Octoba 15,2016 alipokua njiani kuelekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya  kikazi ya siku 3. 
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia,maeneneo ya Mlandizi Mkoa wa Pwani leo Octoba 15,2016 alipokua njiani kuelekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya  kikazi ya siku 3

TANGAZO


Viongozi wa Umma watakiwa kuwa na maadili mema ili kumuenzi Mwali Julius Kambarage Nyerere

$
0
0
kig3
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig1
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA).Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila, Mwenyekiti wa Kongamano hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri msaafu Mhe. Anne Makinda.
kig5
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere wakifuatilia mada kutoka kwa wawasilishaji ambao ni Mhe. Phillip Mangula, Joseph Butiku, Ibrahim Kaduma na Dkt. Harun Kondo, mada zilizowasilisha ni pamoja na Miiko ya Uongozi, Azimio la Arusha na Maadili ya Viongozi.
kig7
Mchumi Mwandamizi Profesa Ibrahim Lipumba akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig13
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) akiagana na washiriki.Picha na. Frank Shija, MAELEZO.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Video: Kagera All Star Ft Baghdad - Inaanza Na Wewe (Tetemeko Kagera)

Shule ya ATLAS yafanya Mahafali ya Darasa la Saba, Wazazi na Walezi Watakiwa kutowakatishaTamaa Watoto

$
0
0

Shule ya Atlas Madale iliyopo Jijini Dar es Salaam imefanya mahafali ya Darasa la saba, ambapo Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alikuwa ni ndugu Rogers Shemwelekwa, ambae ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni.

Mkuu wa Shule ya Atlas Madale Justus Kagya akizungumza katika Mahafali hayo ameeleza kuwa kila mwaka ifikapo Oktoba 14 shule hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya mahafali ili Kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE.

Makamu mkuu upande wa Taaluma kwenye shule hiyo Joseph Mjingo amewataka Wazazi kuacha kuwakatisha tamaa Watoto, hususani kwenye Somo la Hesabu, ambalo limekuwa likionekana kuwa ni gumu tofauti na masomo mengine

Aidha Mahafali hayo yamehudhuriwa na Wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi hao.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo ya kina kutoka kwa mkuu wa Shule ya Atlas madale, ndugu Justus Kagya wakati wa mahafali ya wahitimu wa Darasa la saba kwenye shule, ambayo pia yalihudhuriwa na wazazi na walezi wa wanafunzi hao. 
Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi katika Shule ya Atlas madale ya Jijini Da es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye Shughuli hiyo.
Sehemu ya Wanafunzi wa Atlas madale waliohudhuria Mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba kwenye Shule hiyo.




DAWASCO NA DAWASA SHIRIKIANENI KUONDOA KERO YA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM-MHADISI MBOGO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati amezindua Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) iliyofanyika mjini Bagamoyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Mfutakamba amezitaka taasisi hizo kuongeza ushirikiano,haswa kwa wafanyakazi kwa kuwaandalia semina za mafunzo kwa pamoja ili waweze kufahamiana na kushirikiana kwa pamoja katika kuondoa kero ya Maji iliyopo jijini Dar es salaam.

“Mimi faraja yangu ni kuona DAWASCO na DAWASA mnashirikiana haswa wafanyakazi kwa kuwa kitu kimoja katika kutimiza majukumu yao, muone tatizo la Maji ni lenu wote ,naamini mkipendana na kuwa wamoja mtasaidia sana kuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam” alisema Mfutakamba.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu amemshukuru katibu mkuu kwa kufika na kuzindua semina hiyo na pia amewataka washiriki hao kutumia elimu watakayopata kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na kutatua kero ya Maji kwa jiji la Dar es salaam.

“Kwa niaba ya DAWASCO na DAWASA tunakushukuru katibu mkuu kwa kuweza kushiriki nasi kuzindua semina hii ya mafunzo kwa wafanyakazi wa taasisi hizi mbili tunaona upo pamoja nasi hivyo na mimi napenda kuwa sisitizia washiriki wa semina hii kutumia elimu na ujuzi watakaopata kuboresha huduma ya Maji kwa kuwa wabunifu kwenye maeneo yao ya kazi nakuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa pwani” alisema Kitundu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza katika uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani 
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu akizungumz machche kwenye uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu wakiwa kwenye picha ya pamoja na DAWASCO na DAWASA Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Serikali yatangaza vigezo mikopo elimu ya juu 2016/2017

$
0
0
·          *Vitatumika kwa wanaonza masomo na wanaoendelea

Serikali imetangaza vigezo vitakavyotumika katika kupanga na kugawa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2016/2017 vitakavyotumika kwa wanafunzi wa mwaka wa kwaza na wale wanaoendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) katika Ofisi za Bodi ya Mikopo (HESLB) zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amesema vigezo hivyo vinazingatia mahitaji ya kitaifa, uhitaji wa waombaji na ufaulu katika kozi za kipaumbele.

“Kozi za kipaumbele ni kama fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa kilimo, gesi na mafuta na nyinginezo,” amesema Naibu Waziri Manyanya.

Kwa mujibu wa Mhandisi Manyanya, fani hizi zinatokana na mahitaji ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 ambazo zinasisitiza umuhimu wa kuzalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani hizo.

Naibu Waziri huyo ametaja vigezo vingine kuwa ni uhitaji wa waombaji hususani wale wenye mahitaji maalum kama wenye ulemavu na yatima.

Aidha, waombaji wenye ufaulu wa juu na wanachukua kozi za kipaumbele nao watafikiriwa, amesema Naibu Waziri Manyanya katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru.  

Kuhusu kutolewa kwa orodha ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kwa 2016/2017, Naibu Waziri huyo amesema Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2016.

Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo.

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO October 15, 2016

$
0
0

SIMU.tv: Watoto wa jamii ya kifugaji ya  kisukuma wilayani Morogoro wanasoma katika vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa mabua;https://youtu.be/ORv3NpWBxac

SIMU.tv: Katika hali isiyo ya kawaida mkazi mmoja mjini Dodoma ajenga ukuta katika eneo la  hifadhi ya barabara;https://youtu.be/gprtO1fUwNY

SIMU.tv: Jeshi la mkoani Rukwa linamshikilia diwani mmoja kwa kosa la kukutwa silaha pamoja na madawa ya kulevya aina ya bangi;https://youtu.be/fj4rQbfGzVI

SIMU.tv: Mwanamke mmoja mkazi wa kikiji cha Igoji  wilayani Mpwapwa atishiwa kuawa kwa kosa la kuelezea kero wanazopata wananchi wakati wa kikao cha hadhara; https://youtu.be/9bDFxmzWdbg

SIMU.tv: Waziri mkuu Kassm Majaliwa apokea msaada wa zaidi ya shilingi milioni 27 kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera; https://youtu.be/UhdwIIOS6wE

SIMU.tv: Baraza la taifa la hifadhi wa mazingira NEMC yaitoza faini ya shilingi million 12 halmashauri ya manispaa ya Tabora kwa kushindwa kutunza mazingira; https://youtu.be/8ZJRX4pKvqU

SIMU.tv: Mgogoro wa kugombania eneo la makaburi yaliopoa Karume  wilaya ya Ilala jiji Dar es Salaam  waibuka upya tena;https://youtu.be/tCb3_mMSS64

SIMU.tv: Mwili wa aliyekuwa mjumbe wa baraza kuu wa CUF marehemu Ashura Mustapha azikwa jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/4jC8aOYPNYg

SIMU.tv: Rais John Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na  naibu waziri wa biashara wa jamhuri ya watu wa China;https://youtu.be/AIzUuQ846OE

SIMU.tv: Serikali ya Zanzibar yasema haitasita kumfukuza mwekezaji yeyote atakayekiuka sheria na taratibu za uwekezaji;https://youtu.be/SnSN29pO5E0

DC Makete Atoa Maagizo Mazito kwa Walimu wanaotembea na Wanafunzi

$
0
0
Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, wanafunzi wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kusoma kwa bidii kwa kuwa taifa linawategemea ikiwemo kuja kushika nyadhifa mbalimbali baada ya kuhitimu masomo yao

Kauli hiyo imetolewa jana na Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi yaliyoadhimishwa kiwilaya katika shule ya Sekondari Lupalilo

Aidha Mkuu huyo ametoa Onyo kali kwa walimu wote wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi na kusema sheria zipo wazi kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua, huku akiwataka wanaofanya hivyo kama wapo kuacha vitendo hivyo mara moja

Naye diwani wa kata ya Tandala Mh Egnatio Mtawa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete akishukuru kwa hotuba ya mgeni rasmi amesisitiza maagizo hayo wahusika wayafanyie kazi ili kuepusha madahara yatakayoweza kujitokeza endapo maagizo hayo yatapuuzwa

Awali katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo wamepatiwa elimu ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI kazi iliyofanywa na Mratibu wa Ukimwi sekta zote Wilaya ya Makete Bi Ester Lamosai ambapo pamoja na mambo mengine amemueleza mgeni rasmi jinsi ambavyo shule nyingi hazipo salama kwa sasa

Na Edwin Moshi

Undergraduate scholarships

WANAUME WA KATOLIKI JIMBO LA DAR ES SALAAM WATEMBELEA MASISTA WA DADA WADOGO WA MTAKATIFU FRANSISKO MBAGALA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.Hayo yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista wa Shirika la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini, Dares Salaam.

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi iwe ya halali.“Tusidharau tufanye kazi na asiye fanya kazi hastahili kula. Hata familia yaYesu ililala njaa…hata ukilala njaa usidharau kazi,”alisema.Akimzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, PadriMbiku alisemaalikuwa mtu wa kwanza kuwaomba masista kuombea nchi ilipovamiwa na majeshi yaIdd Amin wa Uganda.

“Nyerere aliwashukuru sana watawa masista kwa kushinda vita ile dhidi ya Idd Amin. Tanzania haikuzoea vita.“Hivyo aliomba masista wasali sana. Tanzania ikashinda. Nyerere alisema waziwazi na washukuru masista kwa kushinda vita,” alisemaMbiku.Vita kati ya Tanzania na Uganda iliibukamwaka 1978 nakufikia tamati mwaka 1979 baadayamajeshi ya Amin kuchakazwa vibaya na Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).Kutokana na umuhimu wa sala za masista hao, Padri Mbiku aliwaomba Uwaka kuhakikisha wanawasaidia masista kwani wanamchango mkubwa kwa taifa na kanisa.

“Masista wanajitoleakuombea kanisa na watu wote wapate wokovu pasipo kubagua dini zao. Sala yao nimuhimu, ina nguvu na Mungu anaisikiliza kwa kujitoa kwao,” alisema.Kwa msingi huoaliwaomba Uwaka ambao kaulimbiu yao “Nguzo Imara Hekalu la Bwana” 

Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia), akishiriki sakramenti takatifu wakati wa ibada hiyo. 

AFANDE SELE AIBUKIA MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSANI MKOANI MOROGORO LEO.

$
0
0
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Morogoro mjini.kijiji cha Msamvu alipokua njiani akielekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Octoba 15,2016
 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Afande Sele akizungumza jambo mbele ya Makamu wa Raisi na wananchi,mara baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kusalimiana na wananchi wa Morogoro mjini kijiji cha Msamvu alipokua njiani akielekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Octoba 15,2016. Pichani kulia ni MKuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Morogoro katika kijiji cha Msamvu leo Octoba 15,2016. 
MKuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt Kebwe Stephen akizungumza jambo na Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Afande Sele mapema leo mchana,Mara baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kusalimiana na wananchi wa Morogoro mjini kijiji cha Msamvu alipokua njiani akielekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Octoba 15,2016. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA HAPA NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la uwekezaji lilo andaliwa na jumuiya ya Dowoodi Bohora lililo fanyika hapa nchini katika ukumbi wa mwalimu Nyere jijini Dar ess salam linalo lenga kutangaza fursa za uwekezaji Tanzania kongamano hilo liliuhudhuriwa na wafanya biashara sekta mbali mbali kutoka zaidi ya nchi 40 duniani.
Picha na Chris Mfinanga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea shukurani kutoka kwa mwakilishi wa Shehe mkuu wa Bohara kutoka Mumbai Shehe Badrul Jamali baada ya kufungua kongamano la uwekezaji lililo andaliwa na Jumuiya ya Dawoodi Bohora linalo elezea furusa za uwekezaji nchini Tanzania kushoto ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Chales Mwijage Kongamano hilo lilihudhiriwa na Bohara zaidi ya mianne wasekta mbalimbali kutoka zaidi ya Nnchi 40 kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mwakilishi wa Shehe mkuu wa Bohora kutoka Mumbai Shehe Badrul Jamal katikati ni muandaaji wa kongamano la wafanya biashara wa Dhehebu la Dawood Bohora Bwana Mustafa Hassanali kongamano hilo lilikuwa likielezea furusa za uwekezaji zilizopo Tanzania.

KONGAMANO HILO LIMEFANYIKA MWISHONI MWAWIKI HII

SAFARI ZA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER JIJINI ARUSHA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHINI

$
0
0
Moja ya Ndege mpya ya serikali iliyokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier  Dash 8 Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakati maafisa wa Mamlaka ya Anga(TCAA) walipokua wakifanya ukaguzi kabla ya kuanza rasmi safari za kibiashara nchini.
Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)wakilakiwa katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya ukaguzi kabla ya safari kwa ndege hizo kuanza.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ,Ibrahim Mussa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)akizungumza na waandishi wa habari juu ya faida za utalii zitakazotokana na kukua usafiri wa anga nchini.

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images