Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1391 | 1392 | (Page 1393) | 1394 | 1395 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla jana jioni (Oktoba 13.2016), amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Bohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.

  Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla, Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

  Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

  Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

  Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Bohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.
  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akibusu mkono wa Sheikh Mkuu wa Bohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
  Waziri wa mambo ya ndani nchini ,Mwigulu Nchemba akiombewa baraka na kiongozi Dawood Bohora Duniani Dkt Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa mabohora Upanga.
  Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa tukio hilo.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi saba Barani Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi hivyo amewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.

  Tanzania ni nchi ya pili kwa kasi ya ukuaji wa uchumi Barani Afrika ambapo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 7 ikiongozwa na Ivory Coast inayokua kwa asilimia 8.5, Senegal ya tatu (asilimia 6.6), D’jibout ya nne (asilimia 6.5), Rwanda ya tano (asilimia 6.3), Kenya ya sita (asilimia 6.0) na Msumbiji ya saba (asilimia 6.0).

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamis, Oktoba 13, 2016) wakati akifungua kongamano la Jumuiya ya Dawoodi Bohora lililohusu fursa za uwekezaji. 

  Amewakaribisha wanajumuia hiyo kuja kuwekeza nchini. Kongamano hilo lilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere.“Tanzania ina sera nzuri za kiuchumi ambazo zimesababisha uchumi wake kuendelea kuwa imara kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Naikaribisha jumuiya ya Bohora kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania,” alisema. 

  Waziri Mkuu alisema makampuni yatakayowekeza nchini yatafaidika na uwepo wa malighafi za kutosha, sera nzuri uwekezaji pamoja na uhakika wa usalama wa mali zitakazowekezwa nchini kwa sababu ya hali ya amani na utulivu iliyoko nchini.

  Alisema licha ya Tanzania kuwa maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji pia ina soko la uhakika kwa sababu ya kuwa mwanachama wa jumuiya mbili ambazo ni Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zenye watu takriban milioni 600.

  “Tanzania ni kitovu cha biashara kwani inapakana na nchi nane ambazo kati yake nchi sita zinatumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yake. Mizigo hiyo husafirishwa kwa njia ya reli na barabara,” alisema.

  Nchi zinazopakana na Tanzania ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Zinazotumia bandari ya Dar es Salaam ni Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia. 

  Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano hilo la kidini (Ashara Mubarak) lililowakutanisha Mabohora kutoka duniani kote Bw. Murtaza Adamjee ameahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko nchini.

  Bw. Adamjee alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba Mabora dunia nzima wanakuja Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali hususan ya viwanda. “Tutafikisha ujumbe kwa Mabohora dunia kote kwamba Tanzania ni sehemu salama ya kuja kuwekeza,” 


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 - DAR ES SALAAM.
  IJUMAA, OKTOBA 14, 2016.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) hivi karibuni Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House juu ya ufafanuzi wa kuwaondoa wananchi katika maeneo yaliyohifadhiwa. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Angelina Madete na Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa TFS, Mohammed Kilongo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) Makao Makuu wa Wizara hiyo  Mpingo House hivi karibuni juu ya ufafanuzi wa kuwaondoa wananchi katika maeneo yaliyohifadhiwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara Wanyamapori, Prof. Alexander  Songorwa.
  _____________________________


  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  Wizara ya Maliasili na Utalii


  TAARIFA KWA UMMA


  UFAFANUZI KUHUSU UONDOAJI WANANCHI KATIKA MAENEO YALIYOHIFADHIWA


  Serikali inawakumbusha wananchi wote na kusisitiza kwamba ni wajibu wao kutii sheria na kuepuka kabisa vitendo viovu vinavyosababisha kupotea kwa uoto wa asili kwa kasi inayoendelea hivi sasa nchini na kutishia UHIFADHI ENDELEVU,  hali hii inapelekea nchi kuwa Jangwa kutokana na ukataji wa miti hovyo, kilimo kisichoendelevu, uchungaji holela wa mifugo, uanzishaji makazi na shughuli zingine za kibinadamu katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwa ni pamoja na Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na  Hifadhi za Taifa.


  Ikumbukwe kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kwa sasa Tanzania inapoteza takriban hekta 372,000 za uoto wa asili kila mwaka na kwamba kasi hiyo ikiachwa iendelee tishio la kutoweka kwa uoto huo ni kubwa sana. Takwimu pia zinaonyesha kuwa Tanzania ina eneo la uoto wa asili lenye ukubwa wa takriban Hekta milioni 48.1 na kwamba kasi iliyopo ya uharibifu ikiachwa iendelee itaiacha Tanzania bila uoto wa asili baada ya miaka 129.


  Takwimu hizi zitabakia hivyo ikiwa idadi ya watu haitaongezeka, ukuaji wa shughuli za kibinadamu hautaongezeka na aina ya shughuli hizo haitabadilika, jambo ambalo haliwezekani. Hivyo basi upo uwezekano wa idadi ya miaka hiyo kupungua hata kufikia nusu, sawa na umri wa kawaida kabisa wa binadamu.  0 0

  Na. Aron Msigwa –NEC, Bariadi-Simiyu.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa elimu ya mpiga kura inayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika maeneo mbalimbali nchini ni vema ikawa endelevu kwa kuwa inaongeza uelewa na kukuza Demokrasia nchini.

  Dkt. Shein ameyasema hayo leo mjini Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea banda la maonesho la Elimu ya Mpiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Vijana na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mkoani Simiyu.

  Amesema hatua ya NEC kuwa na programu endelevu za kuwapatia wananchi elimu ya mpiga katika maeneo yao ni muhimu katika kukuza Demokrasia na kuwafanya waelewe wajibu wao katika kudumisha amani na utulivu nchini kwa kupiga kura kwa uhuru kuwachagua viongozi wanaowataka.

  “Hongereni sana, mnapotoa elimu hii mapema mnafanya kazi nzuri, hii inaongeza uelewa miongoni mwa wananchi na kuwafanya muwafikie wananchi wengi zaidi kabla ya uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020” Amesisitiza Dkt. Shein.

  Kwa upande wake Afisa Habari Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Margareth Chambiri amemweleza Dkt. Shein kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani Simiyu ili kutoa Elimu kwa wananchi hususan vijana wa mkoa huo.

  “NEC tumeshiriki maadhimisho haya ili kuwaeleza wananchi namna ambavyo chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini zinaendeshwa kwa uhuru na uwazi kabisa, katika kufanikisha jambo hili Idara mbalimbali zimeshiriki ikiwemo Idara ya Elimu ya Mpiga Kura, Idara ya TEHAMA, Idara ya Daftari la Wapiga Kura, Idara ya Uchaguzi na Idara ya Sheria” Ameeleza Bi. Margareth.

  Amesema tangu kuanza kwa maonesho hayo Oktoba 8, mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanikiwa kutoa Elimu ya Mpiga kura kwa wananchi waliokuwa wakilitembelea banda la maonesho la NEC, kutoa elimu hiyo kupitia majukwaa ya wazi ya burudani pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura kwa wanafunzi wapatao 2100 wa shule za Sekondari mkoani humo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili uwanja wa sabasaba kutembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi na Vikundi mbalimbali vya maendeleo ya vijana wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya vijana mkoani humo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kuhusu Elimu ya Mpiga Kura kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Margareth Chambiri mara baada ya kutembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye viwanja vya sabasaba wilayani Bariadi uemkoani Simiyu.

  Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Takwimu waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Mkoani Simiyu. 

  0 0

  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro ambapo amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo


  Na Hassan Silayo-MAELEZO

  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amewataka watanzania kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwahudumia Wazee nchini kwa kuwapatia mahitaji ya muhimu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

  Akiongea na Wazee katika Kambi ya kulea wazee ya Chazi iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Mama Janeth amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua Wazee ni kundi muhimu kwa ustawi wa nchi kwani miongoni mwao walishiriki katika ukombozi wa taifa leo hivyo tuitumie Siku kama ya leo na nyingine kumuenzi Hayati mwalimu Julius Nyerere akiwa kama mzee aliyetangulia mbele za haki.

  "Leo ni siku muhimu sana katika taifa letu siku ambayo tunaenzi siku aliyofariki muasisi awa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hivyo ni rai yangu kwa watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kushiriki kwa pamoja katika kuwahudumia wazee na kuwapatia mahitaji yao muhimu" Alisema Mama Janeth.

  Aidha, Mama Janeth alisema kuwa amesikia changamoto zinazokabili Makazi hayo na ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau kwa kadri iwezekanavyo ili kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa changamoto hizo iwe makazi ya wazee Chazi na yote nchini yawe sehemu salama ya kuwahudumia wazee.

  Katika kutembelea kituo hicho Mamam Janeth Magufuli ametoa zawadi ya mchele, Maharagwe,unga na mafuta ya kupikia kwa ajili ya wazee na watu wasiojiwezakatika kituo hicho.

  Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli ya kuwahudumia wazee na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya wazee mkoani humo.

  Pia Dkt. Kebwe amewataka watu wote waliovamia makazi ya wazee kuondoka mara moja na kutafuta maeneo mengine na atakayekiuka agizo hilo serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.

  Akiwasilisha Risala ya Makazi ya Ya wazee ya Chazi kwa Mama Janeth Magufuli Kaimu Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bw. Richard Kamwana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa misaada aliyoitoa kwa wazee wa kituo hicho wakati wa sikukuu ya Eid.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kiombo amemuhakikishia Mama Janeth Magufuli wataendelea kushirikiana na taasisi nyingine katika kukiendeleza kituo hicho ikiwamo kuwapatia wazee wote kadi za CHF kwa ajili ya kuwasaidia wazee hao kupata huduma ya Afya popote waendapo.

  0 0

   
   
   Baadhi ya Wananchi wakiwa juu ya mgongo wa huyo samaki mkubwa ambaye mpaka sasa hakufahamika jina lake mara moja
  Sehemu ya mwili wa samaki huyo 

  0 0
  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa pole ndugu marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Bw. Deogras Didas Masaburi (Ojambi) ambaye ni mtoto wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Diwani wa  kata ya Chanika,jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi mara baada ya kukutana kwenye msiba wa Marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi wakimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kwenye kitabu cha maombelezo cha marehemu Dk. Didas Masaburi  nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam. 
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI. 

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya(DAS)David Mwakiposa.
  Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo

  Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha

  Burudani nayo ilikua sehemu ya kunogesha Nyerere Day.


  0 0

  mibi
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein akipokea mwenge kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu George Mbijima wakati wa sherehe za uzimaji wa Mwenge wa Uhuru Bariadi mkoani Simiyu leo  baada ya kukimbizwa nchi nzima huku kiongozi huo akikagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhimiza wananchi katika uwajibikaji kwa taifa ambapo sherehe hizo zimefanyika kitaifa mkoani humo.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Sinohydro Corporation anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa kilometa 43.65 kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

  Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo mkoani Dodoma na kuridhishwa na ujenzi wake Prof. Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwani ni kiungo kikuu kwa watu wanaosafiri kati ya mkoa wa Dodoma, Manyara, Arusha na nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

  “Kamilisheni kipande hiki kilichobaki haraka kwani barabara hii ni kiunganishi cha nchi za Kaskazini na Kusini mwa bara la Afrika hivyo kukamilika kwake kutasaidia kufungua fursa za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi”, amesema Waziri Mbarawa. 

  Amemtaka mkandarasi huyo kuzingatia viwango bora vya ujenzi wa barabara kama ilivyosainiwa kwenye mkataba na kuhakikisha thamani ya fedha katika ujenzi huo unaonekana.
  Muonekano wa Barabara wa Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba Mwaka huu.
  Meneja Mradi wa Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 Eng. Yusuf Karera, akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), alipokagua ujenzi wake, Mkoani Dodoma.
  Muonekano wa tabaka la kwanza la Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.


  0 0

  Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Ahmed Olotu(Mzee Chilo) mara baada ya kupokea shilingi laki sita na ishirini kutoka kwa Mtandao wa wasanii(SHIWATA) ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.Wengine pichani ni Mkurugenzi Idara ya uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Gen.Mbazi Msuya na Caasim Taalib(wa tano kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii.
  Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ndogondogo solo la kariakoo mara baada ya kupokea msaada wa nguo mchanganyiko,midoli na kanzu wenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.

  ……………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili kutoka kwa wadau mbalimbali.

  Makabidhiano ya michango hiyo yamefanyika leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

  Akiwashukuru wadau hao Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

  “Nawashukuru kwa kuamua kutumia siku ya leo ya kukumbuku ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema michango hiyo ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo baina ya Watanzania.

  Misaada hiyo imetolewa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sh. milioni 20, Mtandao wa Wasanii Tanzania sh. 620,000 na nguo mifuko miwili, Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA) sh. milioni tano.

  Wengine ni Umoja wa Wafanyabiashara Ndogondogo soko la Kariakoo ambao wametoa marobota mawili ya nguo (suruali, kanzu na nguo za akinamama na moja la wanasesere kwa ajili ya watoto waliopatwa na maafa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni mbili.

  Fedha na nguo hizo vimetolewa kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.

  Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali .

  0 0

  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akitembelea na kukagua makazi ya Wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro 
  Baadhi ya Misaada iliyokabidhiwa kwa wazee wanaoishi katiika makazi ya Chazi yaliyopo  Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro 
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe. 


  0 0

  Na Luteni Selemani Semunyu Arusha.

  Wachezaji wa timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wamewasili salama jijini Arusha na wamefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Gymkana utakaotumika kwa ajili ya michuano ya wazi inayotari wa kuanza kesho jumamosi.

  Wachezaji hao ambao wanafikia 14 wakiwemo wanawake watatu wanawake wamesema ni matumaini yao kurejea na ushindi mnono ili kuwapa faraja mashabiki wa klabu yao ambao wanamatumani makubwa nao.

  Kwa upande wake bingwa wa Moshi Open mashindano yaliyomalizika hivi karibuni kutoka Lugalo Nicholous Chitanda amesema anajivunia kuwa na mwalimu mzuri hivyo atatumia mafunzo mazuri aliyopata kutoka kwa mwalimu wake kutetea ubingwa aliopata Arusha Open katika kundi lake.

  Kwa upande wake mkuu wa msafara wa timu ya Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule amesema kikosi chote cha timu ya Lugalo kimefika salama hakuna majeruhi na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu ya Gymknana ya Arusha ambao ndio wenyeji wa michuano hii ya Arusha Open mwaka 2016 jumla ya washiriki 102 wamethibitisha kushiriki.

  Wachezaji hao kutoka klabu ya jeshi ya Lugalo ni 14,wawili toka mkoani Morogoro,16 kutoka klabu ya TPC ,nane kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es salaam, saba toka Moshi na wenyeji kutoka klabu ya Gymkhana ya Arusha 55.

  Mashindano ya wazi ya Arusha Open yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kwa kuanza na jumamosi na jumapili ambapo mara baada ya kumalizika kwa michezo sherehe ya ugawaji zawadi kwa washindi itafanyika kwa makundi yote ambayo ni A,B,C Senior,Junior,na wanawake
  WACHEZAJI WA KLABU YA GOLF YA LUGALO WAKIJADILIANA JAMBO WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA .
  MPIGA GOLF NICHOLOUS CHITANDA WA KLABU YA GOLF YA LUGALO AKIWA KATIKA MAZOEZI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 JIJINI ARUSHA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
  AFISA TAWALA WA KLABU YA LUGALO KAPTENI AMANZI MANDENGULE MWENYE FULANA NYEUPE AKIJADILIANA JAMBO NA MCHEZAJI MWENZIE WA KLABU HIYO PROSPER EMANUEL (KULIA) NA JUMA LIKULI( KUSHOTO )KATIKA MAZOEZI YA KUJIWINDA NA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN .
  WACHEZAJI WA KLABU YA GOLF YA LUGALO WAKIJADILIANA MATOKEO WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)

  0 0

  Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, imekuwa ikiwakopesha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kugharimia masomo yao. Katika utekelezaji wa jukumu hili, Serikali huandaa Sifa na Vigezo vya Utoaji Mikopo kila mwaka ili kuendana na malengo na matarajio yaliyopo katika mipango na mikakati ya kitaifa kama ilivyoainishwa  katika Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 -2020/21), Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Ilani ya Chama cha Mapinduzi. 

  Kwa kuzingatia mipango mikakati na sera hizo, pia Mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/2017 katika mwaka wa masomo 2016/17, Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo kama ifuatavyo:

  (i)    Vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na mpango wa maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele kama vile:

  ·         Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
  ·         Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
  ·         Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia
  ·         Sayansi Asilia na Mabadiliko ya Tabianchi
  ·         Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu

         (ii)  Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile Ulemavu na Uyatima

         (iii)   Ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri

  Kwa hivi sasa Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2016.   Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo.

  Imetolewa na:

  Mhandisi Stella M. Manyanya (Mb)
  NAIBU WAZIRI
  ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  Oktoba 14, 2016

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la kiraia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Gereza Karanga, Moshi, ACP. Hassan Mkwiche (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Karanga, ASP. Michael Minja(kulia) alipotembelea Kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha kisasa cha viatu leo Oktoba 14, 2016. Wengine pichani ni Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo(kulia) alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho kipya cha kutengeneza viatu.
  Eneo litakalojengwa kiwanda kipya cha kisasa cha kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi. Kiwanda hicho kitakuwa cha ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa jamii wa PPF.
  Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja akiangalia kiatu aina ya buti ndefu zinazotengenezwa kiwandani hapo kwa ajili ya Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Oktoba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Qian Keming ambapo viongozi hao wamekubaliana kuharakisha miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kati.

  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amemueleza Mhe. Qian Keming kuwa Serikali yake ya awamu ya tano inataka kuona mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda na kwamba angependa wadau wa maendeleo hasa nchi ya China ambayo ni ndugu na rafiki mkubwa wa Tanzania iende katika kasi hiyo hiyo.

  Rais Magufuli ameuzungumzia mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na kuunganisha nchi za Rwanda na Burundi ambao Tanzania imetenga Shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi katika bajeti hii, kwa kutaka China ambayo imekubali kushiriki katika ujenzi iendane na kasi ya Serikali yake.

  “Mhe. Qian Keming sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilometa 200 za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe.

  “Kazi hii tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike, nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani” amesema Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli ameongeza kuwa mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo imedharia kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Biashara wa China Mheshimiwa Qian Keming amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza uchumi wa Tanzania, kupiga vita rushwa na kwa namna ya kipekee kwa dhamira yake ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na China na ameahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kati.

  “Mheshimiwa Rais Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu waongeze kasi, na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa” amesema Mhe. Qian Keming.

  Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing, Makamu wa Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Sun Ping, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
    
  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  14 Oktoba, 2016.   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming  aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
   . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini  Dkt. Lu youqing  Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming .
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming, pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu youqing.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming watatu kutoka kulia  aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Wengine katika picha ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakwanza (kushoto) Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping wapili kutoka (kushoto) Balozi wa China hapa nchini Dkt. Dkt. Lu youqing watatu kutoka (kushoto),Pamoja na  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wapili kutoka kulia.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  2
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Ifakara
  Shirika la Plan International limezindua mradi wa miaka minne wa kuzuia ndoa za utotoni utakaogharimu jumla ya shilingi bilioni moja ukiwa na lengo la kumuinua mtoto wa kike kijinsia, kiuchumi na kijamii.
  Mradi huo umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yaliyoandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika Kijiji cha Ihenga kilichopo wilayani humo.
  Ihunyo amesema kuwa ndoa za utotoni ni changamoto moja wapo inayowakabili watoto wa kike na kuwafanya wasifikie malengo waliyojipangia hivyo, ametoa rai kwa Serikali na mashirika mbalimbali kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tatizo hilo linakomeshwa.
  “Ndugu wananchi, kwa kutambua changamoto zinazowakabili wasichana wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Shirika la Plan International limeandaa mradi maalum kwa ajili yao ambao utatekelezwa katika Kata nne za Idete, Mofu, Namwawala na Kisawasawa ambapo vijiji 13 vitafikiwa na mradi huo”, alisema Ihunyo.
  Mkuu wa Wilaya huyo amelishukuru shirika hilo kwa mchango wao katika kuhakikisha wasichana wanapata haki zao za kukua na kuendelezwa kama watu wengine kwa kuwajengea uwezo kielimu na kimtazamo utakaowasaidia kujitambua na kupinga ndoa hizo.
  Kwa upande wake Meneja wa Shirika hilo (Ifakara), Majani Rwambali amesema kuwa Shirika limeamua kuanzisha mradi huo katika Mkoa wa Morogoro kwa sababu ni mkoa mmoja wapo kati ya mikoa iliyoathirika na tatizo hilo hivyo, wanashirikiana na Serikali kuzuia ndoa hizo zinazosababisha wasichana kushindwa kufikia malengo yao.
  “Asilimia 42 ya watu wanaoolewa katika Mkoa huu wapo chini ya umri wa miaka 18, hii inaonyesha dhahiri tatizo hili ni kubwa mkoani hapa kwahiyo, mradi huu unalenga kuwawezesha wasichana kujitambua na kuweza kusema hapana pamoja na kuwa na uelewa wa kutoa taarifa mapema pindi waonapo hali hiyo, hii itasaidia kukomesha tatizo hili”, alisema Rwambali.

  Amefafanua njia zitakazotumika katika kuhakikisha wasichana wanapata elimu hiyo zikiwemo za kufungua klabu katika shule mbalimbali ili kuwapa mafunzo juu ya athari ya ndoa za utotoni, kushirikiana na Serikali katika kufanya vikao vya hadhara ili kuwaelimisha wananchi pia kuandaa mabonanza ya michezo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa kupambana na ndoa za utotoni.

  0 0


  Na Mathias Canal, Singida

  Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.

  Tatizo hilo sugu limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili nchini Kenya.

  Mhe Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.

  Sima alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.

  Sima Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.

  Alisema kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.

  Sima ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya kipimo cha ugonjwa wa Malaria
  Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara.


  0 0

  Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF)  imezindua kampeni kwa jina BINTI WA KITAA eneo la Pakacha kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni itakayodumu kwa mwaka mmoja yenye lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni  nchini Tanzania.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.

  "Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani  zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo" alisema  George.

  BINTI WA KITAA  imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.

  Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazowapelekea mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,hii ndio iliyosababisha kampeni hii kuzinduliwa mtaa wa Pakacha Tandale kwani.
  Baadhi ya waliofanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa wanaonesha #tag  Binti ya Kitaa.
  Baadhi ya akina mama wa Tandale pamoja na waendeshaji wa Kampeni ya Binti wa kitaa wakiwa katika uzinduzi
  Baadhi ya wawezeshaji, na wakazi wa Tandale wakionesha Mabango ya Binti wa Kitaa
  Picha ya pamoja  .Picha zote na Fredy Njeje/Story na Mwana Libeneke wa Funguka Live Dickson Mulashani


older | 1 | .... | 1391 | 1392 | (Page 1393) | 1394 | 1395 | .... | 3278 | newer