Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

KONGAMANO LA HAKI YA AFYA YA UZAZI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
1
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Bw. Justus Mulokozi akifungua kongamano la Kitaifa la Haki ya Afya ya Uzazi katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam ambapo wadau mbalimbali wamehudhuria katika kongamano hilo wakiwemo Wanasheria , Wanasiasa, Wanafunzi Waandishi wa habari pamoja na waalikwa mbalimbali.
002
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile akizungumza katika kongamano hilo wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Haki ya Afya ya Uzazi.
02
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Anne Makinda akiwa katika kongamano hilo pamoja na washiriki wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Bw. Justus Mulokozi, Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Attanasia Soka na Jaji Winnie Korosso.
6
Baadhi ya wadau mbalimbali katika picha tofauti wakionekana kufuatilia na kuandika mambo muhimu yanayojadiliwa katika kongamano hilo.


JAFO AWAAGIZA WAHANDISI WA MAJI KUSIMAMIA VYEMA MIRADI YA MAJI

0
0
Halmashauri alizofanya ziara yake ni pamoja na halmashauri ya wilaya ya kilindi Kiteto, Babati Mji, Babati, Mji Mbulu na Halmashauri ya Mbulu vijijini.Katika ziara hiyo pia alifanikiwa kuzungumza na watumishi na kutembelea miradi ya Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya barabara.

Akizungumza na watumishi, Jafo aliwaagiza wahandisi wa maji kusimama imara katika kusimamia miradi ya maji inayo endelea kujengwa ili miradi hiyo iweze kuwa na ubora unaokusudiwa ili kuondoa changamoto za upatikanaji wa maji katika jamii.

“Kila mradi wa Maji lazima uwe chini ya usimamizi wa chombo cha watumia maji ili miradi hii iwe endelevu,”amesema Jafo.
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akiwa katika Ukaguzi wa ujenzi wa Lambo la kuvuna maji ya mvua wilayani kilindi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akikagua ujenzi wa barabara za halmashauri na ujenzi wa madaraja Katika halmashauri ya wilaya ya kilindi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi)akisaini kitabu cha wageni alipokuwa akikagua hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo, amefanya ziara katika Halmashauri 6 za mikoa ya Tanga na Manyara huku akiwaagiza Wahandisi wa maji wa Halmashauri hizo kusimamia vyema miradi ya maji inayoendelea kujengwa katika halmashauri hizo.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA UONI DUNIANI

0
0
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amewataka wananchi kuendelea kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao vinavyotoa huduma za macho katika jamii ili kupambana na upofu usiowalazima.

Amesema vituo vingi vya Afya hivi sasa vimewekewa huduma muhimu za uchunguzi wa maradhi mbali mbali, ikiwemo uchunguzi wa macho, na hakuna haja ya wananchi kukimbilia Hospitali Kuu ya Mnazimmoja. Waziri Mahmoud ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya uoni Dunini yaliyofanyika Kitaifa kituo cha Afya Magogoni Wilaya ya Magharibi B.

Amesema madaktari wanapohisi tatizo ni kubwa na haiwezekani kupata matibabu katika vituo vidogo wanaamua kumpeleka mgonjwa Hospitali Kuu hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na viituo hivyo. Amesema tatizo la uoni limekuwa kubwa duniani kote na inakisiwa hivi sasa kuna watu wasioona wapatao milioni 285 na asilimia 37 kati yao hawaoni kabisa.

Kwa upande wa Zanzibar amesema inakisiwa kuwa na watu 10,000 ambao wanamatatizo ya uoni na asilimia 50 kati ya hao hawaoni kabisa kutokana na sababu mbali mbali. Waziri wa Afya ameongeza kuwa wataalamu wa maradhi ya tiba ya macho nchini kwa kushirikiana na Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) pamoja na taasisi mbali mbali duniiani wako katika mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maradhi ya macho.

Hata hivyo amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inajitahidi kuendeleza huduma za matibabu ya macho katika nyanja zote katika vijiji mbali mbali Unguja na Pemba kupitia Kitengo chake cha Afya ya msingi ya matibabu ya macho vijijini. Amewataka wananchi kufanya juhudi kuepuka maradhi ambayo yanapelekea matatizo ya macho na kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwani ni moja ya tiba ya kujiepusha na maradhi mengi.

Aidha alilishukuru Shirika la Kimataifa la Sightsaver kwa ushirikiano wake wa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na misaada ya kitaalamu na dawa wanazosaidia kitengo cha matibabu ya macho. Katika risala ya wafanyakazi wa Kitengo cha matibabu ya macho iliyosomwa na Mratibu wa Kitengo hicho Dkt. Rajab Mohammed Hilal wamesema wanakabiliwa na udogo wa nafasi ya kutekeleza katika kitengo hicho. 

Mtaalamu wa macho kutoka China Dkt. Zhao Wei akimpima macho Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika kitaifa kituo cha Afya cha Magogoni, Mjini Zanzibar. 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima macho kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Magogoni wakiendelea kuangaliwa macho. 
Mratibu wa huduma za macho Zanzibar Dkt. Rajab Mohammed Hilal akisoma risala ya kitego cha matibabu ya macho kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Magogoni, Mjini Zanzibar. 
Mwakilishi wa Shirika la Sightsaver Tanzania Andrew Kilewela akibadiliishana mawazo na Mratibu wa Mradi wa Afya ya macho Zanzibar Dkt. Fatma Juma Omar wakati wa maadhimisho ya siku ya uoni Duniani katika Kituo cha Afya Magogoni. 
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Kituo cha Afya Magogoni kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika katika Kituo hicho. 

TWANGA, PAPII, BABU SEYA KUTUMBUIZA TAMASHA LA WAFUNGWA UKONGA KESHO

0
0
papii
Wanamuziki wakongwe wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

TAMASHA kubwa la wafungwa linatarajiwa kuunguruma kesho kuanzia saa 2 asubuhi na habari njema ni kwamba, Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ itatumbuiza sambamba na wanamuziki wakongwe wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.Pia msanii wa Singeli, Msaga Sumu ataporomosha burudani.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwatia moyo wafungwa na kuwaonesha kwamba wapo pamoja na Watanzania wenzao ambao wanaishi huru litakuwa la aina yake kwani mbali na burudani kamambe kutoka kwa Twanga Pepeta, mhamasishaji mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo atakuwepo kuwatia moyo wafungwa.
twanga
Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ 

Shigongo ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Wachapishaji wa Magazeti ya Ijumaa Wikienhemda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, amesema anatambua wafungwa waliopo gerezani nao wanahitaji faraja na kutiwa moyo kwa namna moja au nyingine, kwani nao walikuwa na ndoto zao hivyo kuwatia moyo ni jambo jema.

“Hii si mara ya kwanza kwa Global kuandaa tamasha la namna hii, mwaka 2008 tuliandaa, tunapozungumza pamoja na ndugu zetu waliopo gerezani huwa nao wanafarijika.

“Wanaona tuko nao pamoja. Mtu kufungwa haimaanishi kwamba hana maisha tena, haimaanishi kwamba hawezi kutimiza ndoto zake, haimaanishi kwamba alikuwa mkosaji sana asiyefaa katika jamii.“Bado mfungwa ana nafasi ya kujitunza, kuwa na malengo, kujiandaa na kutimiza ndoto zake pindi wakitoka gerezani. Mifano ninayo mingi tu, kuna wafungwa ambao tulizungumza nao mwaka 2008, kesho hii wameshatoka na wanakuja ofisini kwetu kutushukuru.
live3
Msanii wa Singeli, Msaga Sumu.
“Wanasema kupitia tamasha lile tuliwatia moyo na walibadilika na sasa wanaishi vizuri katika jamii zinazowazunguka na wanafanya biashara mbalimbali na wana mafanikio makubwa tu,” alisema Shigongo.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga, kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na mingineyo ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi.

“Kama unavyojua Ijumaa itakuwa ni Nyerere Day, hivyo tutamkumbuka muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuimba, kucheza pamoja na wafungwa.“Twanga wataporomosha nyimbo zao kali. Wanamuziki wote wakali wa Twanga watakuwepo, wataimba pamoja na wanamuziki waliopo gerezani.

“Kuna wanamuziki maarufu waliotamba enzi hizo kama Papii Kocha na Babu Seya ambao wanatumikia kifungo chao cha maisha, nao watatumbuiza siku hiyo, tutapata fursa ya kuwaona live ndani ya Gereza la Ukonga,” alisema Mbizo.

Pamoja na maneno mazuri ya kutia moyo yatakayotolewa na Shigongo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen Mwaisabila naye anatarajiwa kutoa neno katika tamasha hilo sanjari na viongozi wengine wa magereza.

TRA WAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO ARUSHA

0
0
Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku.


Mamalaka ya mapato mkoa wa Arusha (TRA) imekusanya shilingi bilioni 64.6, ikiwa imevuka malengo yake iliyojiwekea awali ya kuweza kukusanya shilingi bilioni 63.1. Ongezeko hilo, ni sawa na asilimia 102, kulingana na meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku. 

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Globu ya Jamiii mapema leo,Meneja wa mamlaka hiyo mkoa wa Arusha Apili Mbaruku alielezea kuwa ongezeko hilo linatokana na majumuisho ya makusanyo ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu. 

“Ni kweli tumeweza kukusanya kiasi hiki cha fedha, na hii inatokana na
kukua kwa mwamko wa ulipaji kodi mkoani hapa japokuwa bado zipo
changamoto kadhaa za baadhi ya wafanyabisahara kutokuelewa umuhimu wa kulipa kodi,” alisema meneja huyo. 

Apili ametaja sekta ya utalii kuongoza katika ulipaji huo wa kodi. 
“Tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na kukwepa usumbufu usio na lazima,” alishauri meneja
huyo. 

Hata hivyo, Mbaruku aliweka wazi kuwa ofisi yake ilishindwa kufikia
malengo ya ukusanyi wa mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16. 
“Kwa mwaka uliopita malengo yetu yalikuwa kukusanya shilingi 329.5
lakini kwa bahati mbaya tulipata shilingi bilioni 324.6 tu”. 
Na Woinde Shizza,Arusha.

Akifanunua zaidi kuhusu makusanyo ya mwaka huu, Mbaruku alisema kuwa
kiasi cha bilioni 30.3 zilitokana na makusanyo ya ndani wakati
shilingi bilioni sita zilitokana na malipo ya ushuru. Aidha, Mbaruku ameongeza kuwa ofisi yake inatarajia kukutana na
maofisa wa jiji la Arusha kuanza kukusanya makusanyo ya kodi za
majengo. 

Kulingana na meneja huyo wa TRA, ofisi yake inalenga kukusanya kodi
kutoka kwenye majengo 20, 536 mkoani hapa. Mamlaka ya mapato mkoni
Arusha(TRA) imevuka lengo la makusanyo yake kwa mwaka wa fedha
2016/17. 

“Nia yetu ni kuanza kukusanya kodi kutoka kwenye majengo hayo, na
tayari tumeshafanya mawasiliano na maofisa wa jiji na kuweza
kubainisha majengo hayo,” aliongeza meneja huyo wa TRA mkoani Arusha.

Waziri Mkuu awataka Jumuiya ya Bohora kuwekeza katika Viwanda nchini

0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

Waziri mkuu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Kassim Majaliwa ameiasa Jumuiya  ya Bohora kuja kuwekeza katika nyanja ya viwanda kutokana na Sera nzuri zilizowekwa za uwekezaji na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya jamii ya mabohora Duniani kote na tangu kuanzishwa kwa Taifa hili.

Waziri  Mkuu amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifunga Kongamano la Biashara lililoandaliwa na jumuiya ya Bohora nchini na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu nyerere, Dar es Salaam.

"Mazingira ya nchi ya Tanzania ni rafiki kwa biashara na uhakika wa soko kutokana na eneo ilililopo kijiografia, kwani nchi yetu inahudumia nchi zaidi ya nane kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuwa sehemu ya kipekee yenye uhakika wa biashara katika ukanda wa Afrika ya Mashariki" amesema Waziri mkuu Majaliwa.

Amesema kwa sasa serikali yake imejipanga kuziwezsha sekta binafsi zote zinazo hitaji kuwekeza Tanzania hasa katika upande wa Viwanda, hivyo kuwaalika wote ambao wana nia ya kuwekeza kuja hapa nchini na watapata msaada wa kutosha.

Kwa upande wake muwakilishi wa Bohora nchini ,Murtza Adam Jee alimuhakikishia Waziri mkuu kuwa kwa maneno waliyoambiwa na Rais pamoja na yeye sasa viwanda vitakuja, kwani wamejua kuwa hapa ni mahali salama pa kufanya biashara na kujenga Viwanda.

Amesema kuwa kila mfanyabiashara aliyefika hapa nchini amejionea mwenyewe kwa namna gani nchi hii ilivyojiandaa katika uchumi wa viwanda .
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana kiongozi wa Jumuiya ya Bohora Badrul Jamal Bhausaad wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar Es Salaam.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa jumuiya wa Bohora kutoka nchi mbalimbali.
Wafanyabiashara wa Jumiya ya Bohora wakimsikiliza Waziri mkuu katika kongamano la Wafanyabiashara.

WAZIRI DK. POSSI: UELEMAVU NA UZEE SIO LAANA

0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO 

Watafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii nchini wametakiwa kuhakikisha wanafanya tafiti ambazo zitawasaidia watu wenye ulemavu kupata vifaa saidizi ili waweze kumudu kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Possi Abdallah alipokuwa akizindua taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.

“Serikali inafarijika inapoona watu wanafanya utafiti ili kuwasaidia watu wenye ulemavu waweze kupata vifaa saidizi na ni kitu gani kifanyike ili NGOs ziweze kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia wenye mahitaji” alisema Dkt. Possi.

Kuhusu suala la unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu hapo tayari kuona wananchi wananyanyapaliwa huku akisisitiza kuwa watu wote ni sawa na ofisi hiyo ina “zero tolerance” kwa watu wanaowanyayapaa mlemavu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi akiongea na wageni waalikwa hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam. 

Vijana jitokezeni kupima ukimwi kujenga taifa lililo na afya bora – Mkwinda

0
0
Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Vijana nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili waweze kujitambua na kupata mbinu mbadala zitakazowazesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kujenga taifa lililo na afya bora.

Hayo yamesemwa na Mwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Hamidu Mkwinda alipokua akizungumza na vijana waliojitokeza kupata elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa wiki ya vijana kitaifa na kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru leo katika Viwanja vya Sabasaba Mkoani Simiyu.

“Vijana wanatakiwa kujitambua na kujua haki zao ili wasije wakaangukia katika wimbi la ulaghai na anasa ambazo zitawapelekea kutokufikia malengo yao na wakati mwingine kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi bila kutarajia” amesema Bw. Mkwinda.

Aidha Bibi. Happiness Malamala kutoka NACOPHA amewataka vijana kutokukata tamaa pale wanapojitambua kuwa wamepata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani kuwa na virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha bali watambue kwamba virusi vya ukimwi ni kama magonjwa mengine yasiyotibika kama vile kisukari, kansa na presha.
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja (kulia) akizungumza na vijana wenye umri chini ya miaka 18 kuhusu namna kijana anavyopaswa kujitambua na maambukizi ya virusi vya ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Baadhi ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 wakifuatilia mada iliyokua ikitolewa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mjumbe kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bibi. Happiness Malamala (kulia) akitoa elimu ya namna ya kutumia kinga kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana waliotembelea banda la NACOPHA leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.


MAJAMBAZI WA TUKIO LA MAUAJI MBANDE WAUAWA KATIKA MSITU WA DONDWE

MHE ANASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA JAKAYA MRISHO KIKWETE YOUTH PARK NA KUBARIKI MASHINDANO YA YOUTH DEVELOPMENT CUP 2016

0
0
yuo8
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipiga mpira ikiwa ni ishara ya kubariki fainali za mashindano ya Youth Development Cup yaliyofanyika katika viwanaja vya kituo cha michezo Jakaya Mrisho Kikwete leo Oktoba 13, 2016.
yuo4
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitembelea na kujionea viwanja mbalimbali vya michezo katika kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park  kilichopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam huku akipata  maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa Ufundi wa kituo hicho Bw. Ray Power leo Oktoba 13,2016.
yuo6
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na wachezaji wa timu ya vijana ya Home Team Academy kutoka Temeke kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya Youth Development Cup 2016 leo Oktoba 13, 2016.
yuo7
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na wachezaji wa timu ya vijana ya Bom Bom kutoka Ilala kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya Youth Development Cup 2016 leo Oktoba 13, 2016.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA UMMA KUTOKA MKOA WA MWANZA

0
0
msangii

Tarehe 12.10.2016 majira ya saa 16:35 katika eneo la busenga “a” kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, askari walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la juma biria miaka 42, mfanya biashara na mkazi wa mtaa wa Busenga akiwa na vifaa vya kutengeneza noti bandia ambavyo ni kemikali ikiwa ndani chupa kubwa, sabuni ya maji iliyowekwa ndani ya chupa ndogo, karatasi zilizokatwa mfano wa noti ya shilingi elfu kumi pamoja na unga ambao bado haujafahamika ni wa kitu gani, kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi .


Inadaiwa kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu akishirikiana na wenzake amekuwa akifanya shughuli hiyo ya uhalifu, ndipo zilipatikana taarifa za kiintelejensia kuhusiana na uhalifu huo, ndipo askari waliweza kufuatilia na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.

Aidha kwa sasa jeshi la polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua za stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. aidha jitihada za kuwasaka wenzake wanaodaiwa kushirikiana na mtuhumiwa huyu katika uhalifu huo bado zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza, akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu wa aina kama hii, ili waweze kufikshwa katika vyombo vya sheria, kwani jeshi la polisi linaamini endapo wananchi wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lao, tutaweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.

imetolewa na:

DCP: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) Mwanza

WAKAZI WA WILAYA YA CHEMBA KUADHIMISHA MIAKA 17 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA KWA KUSHIRIKI KUFANYA KAZI ZA KIJAMII KWA PAMOJA

0
0
Katibu tawala wilaya ya Chemba,Ndugu Nyakia Ally
Katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere, Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Vijana pamoja na Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru hapo kesho tarehe 14/10/2016. 

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally,alipokuwa akizungumza na Globu ya Jamii kwa njia ya Simu,leo.

Nyakia amesema kuwa Wilaya ya Chemba imepanga kufanya yafuatayo katika kuenzi harakati na juhudi za Muasisi huyu wa Taifa letu.

Ikumbukwe Mwl Nyerere katika maisha yake alipigania ukombozi wa Tanzania katika 1.  Kupambana na adui ujinga. 2. Adui Maradhi. 3. Adui Umasikini na 4. Adui njaa.

"Hivyo Wilaya yetu itaadhimisha siku hii kwa kushiriki kwa kusafisha eneo itakapojengwa Zahanati ya Wilaya ya Chemba na wananchi watachangia matofali ya ujenzi wa Zahanati hiyo. Vile vile zoezi hilo litaendana na uchangiaji wa damu katika benki ya damu hapa Wilayani Chemba",alisema Nyakia

Amesema kuwa baada ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kijamii,baadae Kutakuwepo na Michezo mbalimbali ya kuvuta kamba  baina ya Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Kijiji cha Chemba,Kukimbiza kuku na mwisho kutakuwa na mchezo wa bao kati ya Wazee wa hapa Chemba katika kumuenzi Mwl Nyerere ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo huu.

Amesema kuwa Washindi katika mchezo wa kuvuta kamba na nao watajinyakulia zawadi ya Mbuzi na ule wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake na wanaume watajinyakulia kuku watakaye mkamata.

Katibu Tawala wamewaomba wananchi wa Chemba na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi bila kukosa katika tukio hili la kipekee la kuenzi juhudi za Baba wa Taifa katika kuwaletea wananchi maendeleo majira ya saa 2:00 asubuhi ya kesho katika viwanja vya michezo shule ya Msingi Chemba.

MAMA JANETH MAGUFULI:JITOKEZENI KUSAIDIA WAZEE.

0
0
Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.

Hayo yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.

“Kundi hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.

Pia Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu.

Aidha, Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari Kilo 175, Maharage Kilo 350 na Mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa..
Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki. Akimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa msaada wa chakula na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo kwani kusaidia wazee ni kulisaidia taifa pia.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwaaga baadhi ya Wazee na watu wenye mahitaji maalum katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli hotuba.

RAIS MAGUFULI ALIVYOAGANA NA KIONGOZI MKUU WA BOHORA DUNIANI,IKULU JIJINI DAR LEO

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAGANA NA KIONGOZI MKUU WA MADHEHEBU YA BOHORA DUNIANI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0


Jumuiya ya Madhehebu ya Dawoodi Bohra imetoa mchango wa Dola za Marekani laki mbili na nusu (Usd. 250,000) sawa na Shilingi Milioni Mia Tano Arobaini na Tano za Kitanzania (Ths. 545,000,000) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.

Kiongozi Mkuu  wa Madhehebu ya Bohra Duniani Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin amekabidhi mchango huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, walipokutana na kufanya Mazungumzo leo tarehe 13 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kati ya fedha hizo Dola za Marekani laki moja (Usd. 100,000) zimetolewa na Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mwenyewe, Dola za Marekani laki moja (Usd. 100,000) zimetolewa na Viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohra na Dola za Marekani Elfu Hamsini (Usd. 50,000) zimetolewa na wana Jumuiya ya Bohra wa Tanzania.

Pamoja na kutoa mchango huo, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin ameahidi kuwa Jumuiya hiyo ambayo inamiliki hospitali kubwa zilizopo maeneo mbalimbali duniani ikiwemo India, itajenga hospitali hapa nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu.

Pia Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin ameahidi kuwa Jumuiya ya Bohra itatoa udhamini wa masomo ya udaktari kwa vijana wa Tanzania na pia itadhamini matibabu kwa wagonjwa 20 watakaopelekwa nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa Upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemshukuru Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na Jumuiya nzima ya Dawoodi Bohra kwa mchango walioutoa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera na pia kwa kufanyia mkutano wao wa mwaka hapa nchini uliowaleta wageni takribani 31,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

“Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin nakushukuru sana kwa kuja hapa nchini kwetu na kutuletea mkutano huu mkubwa, ujio wenu umeimarisha uhusiano kati ya Bohra na Tanzania na pia umechangia uchumi wa nchi yetu.

“Nakushukuru pia kwa nia yenu ya kujenga hospitali hapa nchini, kuwasomesha madaktari na kudhamini matibabu ya wagonjwa huko India, naomba nikuhakikishie kuwa mchango mlioutoa utatusaidia sana na pia mkijenga hospitali na kufundisha madaktari mtakuwa mmesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo Serikali ingetumia”amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewaalika wanajumuiya ya Dawoodi Bohra kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, kilimo, usafirishaji, madini na uvuvi na amewahakikishia kuwa Serikali itawaunga mkono wote watakaokuwa tayari kuja kuwekeza Tanzania.

Jumuiya ya Madhehebu ya Dawoodi Bohra Duniani imeadhimisha mwaka mpya wa Kiislam na kumbukumbu ya kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (S.A.W) aitwaye Imamu Hussein ambapo maadhimisho yake ya kidunia yaliyoambatana na tamasha la zaidi ya wiki mbili yamefanyika hapa nchini kuanzia tarehe 01 Oktoba, 2016 hadi tarehe 11 Oktoba, 2016.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam



13 Oktoba, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakipokea mfano wa hundi ya dola za kimarekani 50,000 ukiwa msaada wa Jumuiya ya Bohora Dar es salaam kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera toka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika dua na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakimshukuru Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016 .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiagana na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016.


Mfalme Mohammed VI wa Morocco kuzuru Tanzania

0
0

Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco (pichani) anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini kuanzia tarehe 19 hadi 23 Oktoba, 2016.

Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco hususan katika masuala ya  kiuchumi na kibiashara kwa faida ya nchi hizi mbili na watu wake.

Vilevile, Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco atatumia fursa ya ziara hiyo kutembelea Zanzibar na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Hata hivyo, ziara hiyo ambayo imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara haitaathiri msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morocco na Sahara Magharibi.

Msimamo wa Tanzania ambao umekuwa ukisimamiwa na Awamu zote za uongozi zilizopita na Awamu hii, upo sambasamba na ule wa Umoja wa Afrika (AU) unaoutaka Umoja wa Mataifa (UN) ambao ndio wamepewa jukumu la kusimamia mgogoro huo, kuongeza kasi katika kuutatua na kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.

Tarehe 20 Oktoba, 2016 Mhe. Mfalme Mohammed wa VI atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mhe. Rais Magufuli  Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na wajumbe waliofuatana nao.

Mhe. Mfalme Mohammed VI pamoja na kutembelea Tanzania, pia atatembelea Rwanda, Ethiopia na Kenya.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


Dar es Salaam, 13 Oktoba, 2016.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA MWALIMU NYERERE

0
0
Leo Tanzania inaadhimisha miaka 17 toka Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia.Kitaifa maadhimisho haya huambatana na sherehe za kuzima Mwenge na kwa mwaka huu itafanyika katika mkoa wa Simiyu.
 Akiwa mgombea wa Urais mwaka jana Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huko kijijini Mwitongo, Butiama, mkoani Mara akiwa ameongozana na ujumbe wake.
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiongea na viongozi mbalimbali waliomtembelea Butiama
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na Waziri Mkuu wa India Indira Ghandi pamoja na Rais Kenneth Kaunda wa Zambia, Rais Josef Tito wa Bulgaria, Milton Obote wa Uganda na Sir Seretse Khama wa Botswana
 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akikumbatiana na aliyekuwa mgombea Urais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya matokeo kutoka na Mhe. Benjamin Mkapa kutangazwa mshindi kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 1995.

Kwa makala maalumu ya 
Baba wa Taifa BOFYA HAPA

KUONA TAARIFA MBALIMBALI ZA MWALIMU  BOFYA LINK HIZI:







WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2016 WATUA JIJINI ARUSHA, SHINDANO HILO KUFANYIKA JIJINI MWANZA OKTOBA 29

0
0
Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchi wanaowania taji la mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania 2016/17), wameanza rasmi ziara yao ya siku tatu mkoani Arusha ambapo watatembelea maeneo mbalimbali yaliyopo mkoani humo.


Akizumza na wanahabari, Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye alisema kuwa wameingia jijini hapo leo na wanakaa kwa muda wa siku tatu, na katika siku hizo wanampango wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

Aidha alisema kuwa, pia ndani ya siku hizo tatu Warembo hao watachuana kwenye kinyang'anyiro cha 'Top model' kitakachofanyika Jumamosi Oktoba 15 katika ukumbi wa Triple A ulipo ndani ya jiji la Arusha 

"tunafanya shindano hilo katika ukumbi wa triple A na tunatarajia wananchi wengi wa Arusha watajitokeza kuwaona warembo hawa na kiingilio cha shindano hilo ni shilingi 10000 tu, hivyo napenda kutumia fursa hii kuwaalika wananchi wa Arusha kuja kumuangalia nani atakuwa 'Top Model' wa Miss Tanzania"alisema Makoye 

Mbali na kutembelea Mkoa huo wa Arusha, warembo hao wameshatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Singinda na Dar es Salaam na wanatarajiwa kuelekea Mkoani Mwanza ambako ndipo shindano la Miss Tanzania mwaka huu linafayanyika kwa mwaka huu .

Shindano la 'Miss Tanzania 2016' linatarajiwa kufanyika Oktoba 29 katika ukumbi wa Rock City Mall na warembo wote 30 wapo vizuri na wanasubiria siku yenyewe ifike na maandalizi yashindano yamekamila.

 

Baadhi ya Warembo wanaoshiriki kinyanganyiro cha kumsala 'Miss Tanzania' wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa ofisi za gazeti la Guardian zilizopo ndani ya mkoa wa Arusha mara baada ya kutembelea.NA WOINDE SHIZZA, ARUSHA.

WATANZANIA TUFANYE SHUGHULI ZENYE MANUFAA KWA JAMII INAYOTUZUNGUKA KWA AFYA YA NCHI-DC HAPI

0
0
Na Humphrey Shayo -Globu ya Jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi, ametoa wito kwa wakazi wa Kinondoni na Tanzania kwa ujumla kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya shughuli zenye manufaa kwa jamii inayotuzunguka.

Hapi ameyasema hayo leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika fukwe za Coco beach Dar es Salaam wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe hizo,ikiwa ni sehemu ya ishara ya kumuenzi Mwalimu kwa urithi aliotuachia.

"Hii ni moja ya sehemu ambazo tunapasa kujivunia, kwani mwalimu aliamua kutenga maeneo haya kwa watu wa hali ya chini kuja kujiburudisha tena pasipo kulipia chochote,  hivyo kamwe matajiri hawatopata fursa ya kuja kujipenyeza katika kunyakua eneo hili ambalo kila Mtanzania anakuja kujidai nalo" amesema Hapi.

Alimaliza kwa kusema kuwa usafi ni jambo la msingi na linapaswa kufanywa kila siku,tusingojee mahadhimisho au sikukuu,pia alichukua fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Kinondoni kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi, akisukuma mkokoteni wenye taka.
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa na walimu wao katika zoezi la usafi lililofanyika CocoBeach Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Ally Hapi, akimwaga takataka  kwa kutumia  toroli wakati wa zoezi la usafi kitika fukwe za Coco Beach.
Mkuuwa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akiweka taka kwenye mfuko ulioshikwa na Mkandarasi wa fukwe za Kinondoni Elizabeth Mhlanga kutoka  kampuni ya Flamingo,wakati wa  zoezi la usafi katika fukwe za Coco Beach.

TAASISI YA LECRI CONSULT YAENDESHA WARSHA KWA VIJANA YAWATAKA WASITEGEMEE KUAJIRIWA

0
0
Na Dotto Mwaibale

VIJANA wasomi wametakiwa kuacha kutegemea kazi za kuajiriwa badala yake wawe wabunifu katika masuala mbalimbali kulingana na elimu yao ili kujikomboa kiuchumi.

Mwito huo umetoewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Edna Kamaleki Dar es Salaam leo katika warsha ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo vijana iliyoandaliwa na taasisi hiyo. 

"Kijana umesoma kwanini upoteze muda wako kwa kuzunguka kutafuta kazi wakati fursa nyingi zipo" alisema Kamaleki.Kamaleki aliwataka vijana waoshiriki warsha hiyo kubadili na kuthubutu kuanza kufanya kitu chochote kulingana na elimu walizosomea vijana hao.

Akizungumzia taasisi yake hiyo alisema imejikita kutoa huduma za kisheria kwa jamii na ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu haki za watoto."Tuna amani kwamba haki za watoto ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa watoto, pia watoto wanapaswa kuishi katika jamii ambayo haki za binadamu na sheria zinaeleweka vizuri na kuheshimiwa na kila raia" alisema Kamaleki.

Alisema taasisi hiyo inatoa ushauri na huduma ya kisheria kwa jamii wakiwemo watoto, watu binafsi na taasisi mbalimbali na kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria na mikataba ya kisheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Legal and Child Right Consult, Edna Kamaleki (kushoto), akizungumza na vijana wasomi katika warsha ya siku moja ya kuwaongezea uwezo iliyofanyika Dar es Salaam leo. Warsha hiyo iliandaliwa na taasisi hiyo.
Mdau Julius Kionambali (kushoto), akizungumza katika warsha hiyo.

Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images