Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

POPOTE PALE ULIPO UNAKARIBISHWA KWA MAHITAJI YA HUDUMA HIZI

$
0
0
Nakukaribisha Mac Travel Agency Tanzania  Kwa mahitaji ya huduma za Usafiri wa Ndege  local and International flights,Tunafanya kazi masaa 24/7 ,Pia tunasaidia kuprocess visa za Dubai kwa uharaka ndani ya masaa 24 & Visa za China & Turkey utapatiwa msaada wa kupata kwa uharaka.Kwa mawasiliano nasi piga namba hizi:- 0715 120 222 / 0715 000 890 /0752 120 128

Book your flight by email us :reservations@mactravel.co.tz
      Info.mactravel@gmail.com

 Tunapatikana Sinza - Mori near GBP petrol station.Karibuni sana✈✈✈

Tufollow leo Instagram upate offer @mactravelagency @mactravelagency @mactravelagency @mactravelagency

#Mac Travel Agency Tanzania
#Hotline-0715 000 890
#Tunafanyakazisiku7kwaWiki
#Flywithconfidencewithus.


WATUMISHI WA UMMA WASHEREHEKEA KILELE C HA MAADHIMISHO YA MBIO ZA MWENGE KWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUSAJILIWA VTAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Watumishi wa Umma mkoani Simiyu wamekuwa miongoni mwa watumishi waliojitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa katika zoezi linaloendelea kote nchini, pamoja na kusherehekea kilele cha mbio za Mwenye wa Uhuru zinazoadhimishwa kitaifa mkoani Simuyu. 
Kilele cha sherehe hizo ni Octoba 14,2016 sherehe zitakazoambatana na kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Miongoni mwa watumishi wanaoendelea na Usajili katika mabanda maalumu ya maonyesho mkoai humo; ni Walimu na watumishi wengine kutoka sekta ya Afya, WIzara, Wakala na Taasisi za Serikali Wakizungumza wakati zoezi hilo likiendelea; mbali na kupongeza elimu kwa umma inayoendelea kuhusu namna zoezi la Usajili ili na Utambuzi litakavyoendeshwa nchi nzima, watumishi hao wamepongeza jitihada kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kutofumbia macho matatizo ya watumishi na hasa jitihada zake katika kupambana na watumishi hewa. 
 “ Iwapo kweli mfumo huu utatumika vile tunavyoelezwa kwa hakika shughuli za utendaji Serikalini zitaboreshwa sana hususani masuala yanayohusu maslahi ya watumishi na kuondokana kabisa na watumishi wachache ambao kwa udanganyifu wao wamepelekea sisi watumishi wa Umma kutothaminiwa na jamii” walisisitiza baadhi ya watumishi waliozungumza na NIDA wakati zoezi hilo likiendelea 
Kwa upande wa wananchi wengi wameonyesha kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu faida za kuwa na Vitambulisho vya Taifa, na mfumo wa kielektroniki utakaounganishwa na mifumo mingine ya Serikali ingawa baadhi wamesisitiza bado elimu kwa umma kuhusu Vitambulisho inahitajika hususani kwa wananchi walioko vijijini 
Sherehe za mwaka huu za kilele cha mbio za Mwenge Kitaifa, zimekwenda sambamba na maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi, Masharika na Wakala za Serikali; katika kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo
 Baadhi ya Watumishi wa Umma wakiendelea kupata huduma ya usajili na Utambuzi katika viwanja vya Sabasaba ambako maonesho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru yanafanyika. Wakati wa zoezi hilo mbali na kjaza fomu za maombi ya Vitambulisho, watumishi hao wamepata fursa ya kupigwa Picha, kuchukuliwa alama kumi (10) za vidole pamoja na saini ya Kielektroniki na hivyo kuwa wamekamilisha taratibu zote muhimu za usajili
 Mmoja wa Watumishi akiendelea na taratibu za usajili na kuchukuliwa alama za kibaiolojia wakati wa usajili watumishi wa Umma, zoezi linaloendelea mkoani Simiyu
 Mmoja wa Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ofisi ya Wilaya ya Bariadi (mwemye kofia nyeupe), akiendelea kuingiza taarifa za mmoja wa Watumishi wa Umma aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la Usajili watumishi wa Umma likiendelea mkoani Simiyu. Wengine waliomzunguka ni Watumishi kutoka Idara, Taasisi na Wizara za Serikali wakiendelea kusubiria huduma hiyo
 Mmoja wa Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ofisi ya Wilaya ya Bariadi (mwemye kofia nyeupe), akiendelea kuingiza taarifa za mmoja wa Watumishi wa Umma aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la Usajili watumishi wa Umma likiendelea mkoani Simiyu. Wengine waliomzunguka ni Watumishi kutoka Idara, Taasisi na Wizara za Serikali wakiendelea kusubiria huduma hiyo
Akiweka saini ya kielektroniki kwenye kifaa maalumu cha kukusanya taarifa wakati wa zoezi la Usajili ni mmoja wa maafisa afya katika Mkoa wa Simuyu ambaye alikuwa miongoni mwa watumishi waliojitikeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa sambamba na maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mwenge

singeli michano ndani ya Dar Live Mbagala Ijumaa Oktoba 14, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WILSON MASILINGI NA PHILIP MARMO PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI GEORGE WAITARA IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa  Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kitabu  kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
akiagana na  Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali, George Waitara baada ya kukutana   naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe: Philip Marmo alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016

MJI WA DODOMA LAZIMA UPANGWE – WAZIRI MKUU.

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Molad Bwana Abeid Abdallah akimuonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baadhi ya picha na michoro ya nyumba za kisasa na zabei nafuu zinazo weza kujengwa Dodoma Picha na ofisi ya Waziri Mkuu.

 Waziri Mkuu Kassim Majiliwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molad Tanzania Bwana Abeid Abdallah ambaye kampuni yake inajishughulisha na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa gharama nafuu Waziri mkuu ameikaribibisha kampuni hiyo kujenga nyumba za watumishi Mkoani Dodoma mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mji wa Dodoma ni lazima upangwe ili uwe tofauti na miji mingine hapa nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Oktoba 12, 2016) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah ambaye alifika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam na kuelezea nia yake ya kutaka kuwekeza mjini Dodoma.

Amesema Serikali haitaki kurudia makosa yaliyofanyika kwenye miji mingine. “Katika kuupanga ule mji, ni lazima mji upangwe kama ambavyo miji mingine mikuu inapangwa. Kila eneo kutakuwa na nyumba za aina fulani. Hatuwezi kuachia watu wajenge popote na wanavyotaka, mji unakuwa haupangiki. Na hilo ndilo kosa lililofanyika kwenye miji mingine mikubwa ambayo tunayo kwa sasa.”

Amesema Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya kuhamia Dodoma imepewa jukumu la kupitia upya Master Plan ya mji wa Dodoma na kuainisha maeneo ambako nyumba za aina mbalimbali zitajengwa.

“Kimsingi tunataka tuanze kujenga miji iliyopangiliwa na Dodoma tunataka uwe wa mji kwanza kuujenga vizuri kwa standard ya sasa. Kutakuwa na nyumba za ghorofa katika maeneo fulani, na nyumba za kawaida katika maeneo fulani. Mkurugenzi wa CDA amekwishaandaa ramani rasmi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu ujenzi kwenye maeneo ambayo tayari wananchi wanaishi, Waziri Mkuu amesema Serikali itaweka utaratibu ili kuwe na mikataba baina ya mwekezaji na mwananchi anayemiliki eneo husika ili asinyimwe haki ya kumiliki eneo lake.

“Kama tutahitaji eneo ambalo tayari lina makazi, taratibu zetu ni zilezile kwamba tutaweka mikataba kati ya mwekezaji na mwananchi. Kama anataka kujenga kwenye eneo lile, basi lazima amhusishe mwenye eneo na kama anataka kujenga ghorofa ni lazima ahakikishe mwenye eneo anapata umiliki kama tulivyofanya kule Magomeni,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla amemweleza Waziri Mkuu kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali katika zoezi la Serikali kuhamia Dodoma kwa lengo wa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata makazi bora na ya kudumu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM.
JUMATANO, OKTOBA 12, 2016.  

Bongo Flava on the BBC

$
0
0
On Sat 15 October, the BBC World Service programme: Global Beats takes a journey into Tanzanian hip hop. Tracing the music’s transformation into Bongo Flava, which incorporates hip hop, Indian filmi, taraab, muzik wa dansi, dancehall beats and its latest development into Singeli. 
Presenter Salim Kikeke talks to pioneers of the genre Dully Sykes and producer P Funk from Bongo Records, as well as prominent and upcoming artists including Fid Q and Vanessa Mdee. 
The term Bongo Flava is derived from the Swahili word "ubongo", meaning brains. The genre has fans way beyond Tanzania, with the most popular artists performing in South Africa, Nigeria and Sierra Leone, as well as Europe and America. The self-proclaimed "best internet station for Bongo Flava", Bongo Radio, happens to be based in Chicago, Illinois.

The programme can be heard on the BBC World Service at 1300-1400GMT on Sat 15 Oct or online here: http://www.bbc.co.uk/programmes/p01yvy2g.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Asasi za kiraia na wadau wa ardhi nchini wameunga mkono mabadiliko ya sera ya ardhi yanayofanywa na serikali ili kuwezesha jamii kunufaika kwa usawa.https://youtu.be/sFGXYY8TfEI

SIMU.TV: Serikali imeombwa kufanyia marekebisho ya sheria ya ndoa na ya ardhi ili kuhakikisha inaondoa vikwazo vinavyomnyima wanawake haki ya kumiliki ardhi.https://youtu.be/SwraQC9WP2Y

SIMU.TV: Waumini wa dini ya kiislamu madhehebu ya Shia wamefanya matembezi ya hisani jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa mtume.https://youtu.be/M_Bu5j73RDw

SIMU.TV: Jamii imekumbushwa kuvisaidia vituo vya kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi ili kuwatatulia changamoto zinazowakabili. https://youtu.be/DU29CZaA4mE

SIMU.TV: Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSPF umewataka wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na mfuko huo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. https://youtu.be/INxsk6FhZ5k

SIMU.TV: Serikali imesema inaendelea kuhakikisha watanzania wanapata uzoefu wa kufanya kazi za kuendesha mitambo ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia.https://youtu.be/6Xa1yqFzPEU

SIMU.TV: Kampuni ya simu ya Vodacom imemkabidhi zawadi ya shilingi milioni 20 mshindi wa wiki wa shindano la jiongeze na M Pawa. https://youtu.be/NkdE7NSTLpw

SIMU.TV: Shirika la taifa la hifadhi ya jamii limesema mipango yake ya sasa ni kuwekeza katika miradi itakayotoa ajira moja kwa moja kwa watanzania. https://youtu.be/Os2k05y57n8

SIMU.TV: Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeonesha ubabe mbele ya wapinzani wao klabu ya Mtibwa kwa kuwafunga mabao matatu kwa moja.https://youtu.be/mJtLfLd4GLw

SIMU.TV: Jumla ya vikundi sita vya utamaduni kutoka nchini India vinatarajiwa kushiriki katika tamasha la utamaduni litakalofanyika nchini . https://youtu.be/ThzBK_8ngRU

SIMU.TV: Uongozi wa klabu ya Gofu ya Lugalo umewaaga wachezaji wa klabu hiyo wanaoenda kushiriki mashindano ya Arusha Open yatakayofanyika mkoani Arusha.https://youtu.be/pflhve2Jltk

MANAGER Wa Diamond SALLAM Ajibu Tuhuma Za Kuhujumu Show Ya ALI KIBA -Mambo Mseto Na Mzazi Willy Tuva


MTANDAO WA WANAWAKE, KATIBA NA UONGOZI WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS NA KUFANYA MAZUNGUMZO NAE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza nae Ikulu jijini Dar es Salaam na kujadiliana nae masuala mbali mbali yanayohusu changamoto za mtoto wa kike na mwanamke.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi Profesa Ruth Meena ambaye pamoja na ujumbe wake uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza nae Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza nae Ikulu jijini Dar es Salaam na kujadiliana nae masuala mbali mbali yanayohusu changamoto zinazomkabili mtoto wa kike na mwanamke.

MATEMBEZI YA AMANI YA SIKU YA ASHURA JIJINI DAR ES SALAAM

MPIGANAJI WA KICK BOXING EMMANUEL SHIJA KAJALA "NINJA SHIJA" APAA KWENDA KENYA, KUZIPIGA OCTOBER 15.

$
0
0
Mpiganaji wa mchezo wa  Kick Boxing Emmanuel Shija Kajala maarufu kama "NINJA SHIJA" (kushoto)  akiwa na mmoja wa wadau wa mchezo huo  Joe Anena katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo tayari kwa safari yake ya kwenda nchini Kenya ambako anatarajiwa kuzipiga na Moses Golola wa Uganda kugombea ubingwa wa Bara la Afrika  wa 75 Kg. katika ukumbi wa uwanja wa Kasarani jijini Nairobi October 15, 2016.
Taarifa zaidi BOFYA HAPA

Emmanuel Shija Kajala maarufu kama "NINJA SHIJA" na mpinzani wake Golola Moses wa Uganda.




Rais Magufuli afuta safari za Viongozi wa Serikali wa Mikoa na Wilaya kwenda Bariadi Kuzima Mwenge wa Uhuru.

$
0
0

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akitangaza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana na sherehe za kuzima mwenge mkoani Simiyu.
PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.
Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.
Kwa kuwa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Taifa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka Viongozi wote wa Mikoa na Wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza Wilaya zote ambazo zimefanya vizuri katika shughuli za maendeleo wakati Mwenge ulipokuwa katika maeneo yao, zitambuliwe kwa kutangazwa rasmi katika siku ya kilele cha Mbio za Mwenge na kwamba zawadi zilizoandaliwa zitapelekwa kwa wahusika kwa utaratibu utakaoelekezwa na Mamlaka inayohusika kutoa zawadi hizo.


Hata hivyo Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa kutokana na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kwa Taifa, Viongozi wote wa Serikali ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya zake pamoja na wananchi wote wa mkoa huo wajitokeze kwa wingi na kushiriki katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru siku hiyo ya tarehe 14 Oktoba, 2016.
Mgeni Rasmi katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam          

12 Oktoba, 2016

GAPCO KUDHAMINI MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON KILOMITA 10 KWA WALEMAVU

$
0
0
Kampuni GAPCO Tanzania, imetangaza kuendelea kudhamini mbio za Kilimanjaro Marathon 2017 za kilomita 10 kwa walemavu. Akizungumza wakati wa kutangaza udhamini huo jana katika uzinduzi wa mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi alisema Kampuni yake inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa walemavu.

“Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tumeanza kudhamini mwaka wa 2011 na pia kufurahia faida wanayopata wakimbiaji na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mbio hizi, Tanzania Paralympic Committee na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo,” alisema Kakwezi.

Alisema kama njia ya kutoa mchango katika sekta ya michezo na kuendelea kusaidia jamii ambayo GAPCO inafanya biashara, imekuwa mstari wa mbele katika kudhamini mbio za walemavu na mwakani itagharamia usafiri, chakula na malazi kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na usafiri kwa washiriki kutoka Arusha. Washindi watapata zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ujumla.

“Kakwezi alisema mbio za Kilimanjaro Marathon zimekuwa maarufu na zinawavutia wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo zimesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile mlima Kilimanjaro na kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa mji wa Moshi”.

Tunawathamini wateja wetu ambao mchango wao kwa miaka sita umetuwezesha kuendelea kudhamini mbio hizi za kilomita 10 hususani kwa watu wenye ulemavu.

Alisema GAPCO ina matarajio kuwa mbio hizo zitakuwa za kufana na kuwaomba wateja wao kuendelea kutumia bidhaa na huduma za GAPCO ili kampuni iendelee kudhamini shughuli kama hizi.
 Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon, iliyofanyika jijini Dar es salaam jana.

Dkt. Mwakyembe mgeni rasmi mahadhimisho ya miaka 50 ya Tume ya haki za Bianadamu na utawala bora

$
0
0
Na Humphrey Shao, 
Globu ya Jamii

Waziri wa katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe ametajwa kuwa mgeni rasmi katika mahadhimisho ya miaka 50 ya tume hiyo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Iddi Ramadhani Mapuri, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari maelezo, jijini Dar es salaam.
"Maadhimisho haya yanalenga kuangalia uzoefu tulioupata na kujifunza kutokana na mafanikio au mapungufu na changamoto zilizojitokeza katika kipindi hicho kwa lengola kuangalia hali ilivyo hivi sasa ,ikiwa ni tathmini ya kuona iwapo TKU ilifika matarajio ya wananchiau lamna kuona jinsi ambavyo THBUB imeendelea na majukumu ya TKU tangu mwaka 2001 hadi sasa"amesema Mapuri.
Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yatatumika kutambua michango ya watu mbalimbali katika kuinua masuala ya utawala bora wa nchi.
Alitaja kuwa miongoni mwa watu wengine watakaoshiriki ni Jaji Mstaafu Gad Mjemmas, Profesa Paragamba Kabudi na Jaji Mstaafu Damiani Lubuva.

MISRI YADHAMIRIA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

$
0
0
Na Veronica Simba

Balozi wa Misri nchini Tanzania, Yasser El Shawaf amesema nchi yake ingependa kuwekeza katika sekta ya nishati hapa nchini ili pamoja na mambo mengine, isaidie katika kuzalisha umeme wa kutosha na hivyo kuunga mkono kwa vitendo azma ya Rais John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Aliyasema hayo hivi karibuni, alipomtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kujadili kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati.

Kwa upande wake, Waziri Muhongo alimhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta husika na hivyo kumkaribisha Balozi huyo kwa niaba ya nchi yake kuja kuwekeza nchini.

Katika mazungumzo yao, walijadili kwa kina kuhusu fursa mbalimbali zilizopo nchini, zikiwemo za uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama vile makaa ya mawe, jotoardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari na gesi asilia. Pamoja na kujadili fursa hizo, Profesa Muhongo alibainisha kuwa, utaratibu ambao Serikali imedhamiria kuutumia katika kuwapata wawekezaji mbalimbali ni kupitia ushindani wa wazi utakaozingatia vigezo muhimu ikiwemo uwezo/mtaji, utaalam na uzoefu wa mwekezaji husika.

Wataalam mbalimbali wa sekta husika kutoka wizarani na taasisi zilizo chini yake, pamoja na Ujumbe ulioongozana na Balozi Shawaf, walishiriki pia katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akiwa na Balozi wa Misri nchini, Yasser El Shawaf, baada ya kikao baina yao kilichofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Misri nchini, Yasser El Shawaf (wa pili kutoka kushoto) na Ujumbe wake, wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AWASILI MKOANI KILIMANJARO, KUKAGUA ENEO LITAKALOJENGWA KIWANDA KIPYA CHA VIATU

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) akipokea salaamu ya heshima kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro alipowasili Mkoani humo katika ziara ya kikazi ambapo atafanya ukaguzi wa eneo la mradi wa Uwekezaji wa Kiwanda kipya cha Viatu Gereza Karanga, Moshi ambapo mradi huo ni wa ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa Jamii wa PPF, leo Oktoba 13, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo mara baada ya kuwasili Mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Gereza Kwamugumi, SP. Christopher Mwenda(kushoto) pamoja na Mkuu wa Gereza Korogwe, ACP. Lenard Mushi wakimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) aliposimama kwa muda kukagua Gereza la Wilaya Korogwe wakati akielekea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro, leo Oktoba 13, 2016 (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

TASAF NA WADAU WA MAENDELEO WAHITIMISHA MKUTANO WA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI-PSSN.

$
0
0
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – umehitimisha mkutano wa wadau wa Maendeleo ambao wamepitia utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru kaya maskini unaotekelezwa nchini kwa  lengo la kuona utekelezaji wake katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Licha ya kuwa na mkutano , wadau hao wa maendeleo, maafisa kutoka baadhi ya wizara, taasisi za serikali na mashirika yasiyokuwa ya  kiserikali na watumishi wa TASAF walipata fursa ya kutembelea wilaya za Mbarali, Muheza,Chato,Mkulama na Pemba na kukutana na walengwa wa Mpango huo na kuona namna wanavyonufaika na ruzuku ya fedha inayotolewa kwa kaya maskini.

Majumuisho ya mkutano huo yameonyesha kuwa kuna  mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Mpango ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa walengwa kwa wakati, kuhamasisha walengwa kubuni miradi ya kujiongezea kipato na kushirikisha jamii katika utekelezaji wa shughuli za Mpango.

Aidha imeelezwa kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini na kuongezeka kwa mahudhurio ya watoto katika kupata huduma za kliniki mambo ambayo ni miongoni mwa masharti kwa walengwa kupara moja ya ruzuku zinazotolewa na Mpango wa Kunusuru kaya maskini.

Akizungumza mwishoni mwa mapitio hayo ambayo hufanyika kila baada ya miezi sita, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga ametaka jitihada zaidi ziendelee kuchukuliwa na wafanyakazi wa TASAF na wadau wengine wanaotoa huduma kwa kaya maskini ili walengwa waweze kunufaika na huduma za mpango.

Kwa upande wake Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Abdulahi Muderis amesema mafanikio yaliyoanza kuonekana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini ni kielelezo thabiti kinachoonyesha kuwa serikali ya Tanzania  imo katika jitihada kubwa za kupambana na umaskini  .

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyeshika kipaza sauti) akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za  Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za  Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. 

Baadhi ya watumishi wa TASAF wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa Mpango huo kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wake.


Tanzania na China zasaini Mkataba kusaidia sekta za maendeleo nchini,Kutoa msaada wa fedha wa kiasi cha shilingi 97 BILIONI

$
0
0
Serikali ya Watu wa China imeahidi kuipatia Tanzania msaada wa fedha wa kiasi cha Shilingi bilioni 97 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) baada ya kukutana na ujumbe kutoka China unaongozwa na Naibu Waziri wa Biashara wa nchi hiyo, Mhe. Dkt. Kian Keming.

Dkt. Kian na ujumbe wake upo nchini ambapo pamoja na mambo mengine walishiriki kikao cha tano cha Kamati ya pamoja ya Uchumi, Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kiteknolojia kilichofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mhe. Mwijage alieleza kuwa katika kikao hicho walijadili masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika viwanda, miundombinu na nishati. Alisema Serikali ya awamu ya tano imeweka mkazo katika maeneo hayo ili kufikia lengo la nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alieleza kuwa katika harakati za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020, viwanda viwili vya chuma na marumaru vilivyojengwa na wawekezaji kutoka China vinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao. Kiwanda cha tatu kitaanza kujengwa na wawekezaji wa China muda wowote watakapopewa eneo kwa ajili ya ujenzi huo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Kushirikiana katika masuala ya uchumi na teknolojia .
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Charles Mwijage akizungumza katika mkutano kati yake na Naibu wa Viwanda wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Dkt. Qian Keming.Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na China katika kuboresha miundombinu.
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Dkt. Keming wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mwijage hayupo pichani. 

Dkt Shein awasili Mwanza leo kuelekea Simiyu kuzima Mwenge kesho.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,John Mongela mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akielekea katika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe za uzimaji mbio za Mwnge wa Uhuru Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,John Mongela (wa pili kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenister Muhagama (wa pili kushoto) na Waziri wa kazi,uwezeshaji Vijana,Wazee Wanawake na Moudeline Cyrus Castico (kushoto)baada ya mapokezi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akielekea katika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe za uzimaji mbio za Mwnge wa Uhuru Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika kesho,[Picha na Ikulu.]

SERIKALI YA TANZANIA IMEPOKEA Tsh BILIONI 97 TOKA CHINA

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini makubaliano ya kikao cha tano cha kamati ya pamoja ya ushirikiano wa masuala ya uchumi, ufundi na biashara kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China.

Katika makubaliano hayo Serikali ya Tanzania imepokea kiasi cha shilingi Billioni 97 za kitanzania ambao utafadhiliwa na Serikali ya China kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu, Afya na Usalama kwenye viwanja vya ndege na Bandari nchini.Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, pamoja na Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Keming.

Waziri Mwijage alisema kuwa makubaliano hayo yanalenga kusaidia Serikali ya Tanzania kuboresha sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya Elimu, Afya, na Usalama wa Bandari na Viwanja vya Ndege ili kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na China uliodumu kwa muda mrefu.Aidha, Waziri Mwijage alisema kuwa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya China imekubaliana kushirikiana katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ambapo Serikali ya China imeahidi kutekeleza Mradi wa Mlandizi wa utengenezaji wa chuma unaotarajia kuanza wakati wowote.

Pia alisema kuwa, Serikali ya China imeahidi kujenga kiwanda cha Vigae katika eneo la Mkuranga ambacho kitakuwa na uwezo wa kutengeneza kilomita za mraba 80,000 kwa siku ambapo uzalishaji huo utaanza mara baada ya kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara na kinatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu.Vilevile alisema kuwa ifikapo mwaka 2019 Tanzania itaachana na uvaaji wa nguo za mitumba, hivyo Serikali ya China imeahidi ujenzi wa kiwanda cha nguo nchini chenye uwezo wa kuajiri wafanyakazi 14,000 na kuzalisha nguo baada ya kukamilisha upatikanaji wa ekari 700 za eneo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage (wa pili kushoto) na Naibu Waziri wa Biashara wa Serikali ya China Dkt. Qian Keming (wa pili kulia), wakisaini Makubaliano ya Kikao cha Tano cha Kamati ya pamoja ya Ushirikiano wa masuala ya Uchumi, Ufundi na Biashara Baina Serikali ya Tanzania na China, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage (kushoto) na Naibu Waziri wa Biashara wa Serikali ya China Dkt. Qian Keming (kulia), wakibadilishana hati ya makubaliano ya Kikao cha Tano cha Kamati ya pamoja ya Ushirikiano wa masuala ya Uchumi, Ufundi na Biashara Baina Serikali ya Tanzania na China, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika (wa pili kushoto) na Naibu Waziri Biashara wa Serikali ya China Dkt. Qian Keming (wa pili kulia), wakisaini Mkataba wa Ushirikiano wa masuala ya Uchumi na Ufundi baina ya Serikali ya Tanzania na China, katika ukumbi wa Wizara jijini Dar es salaam.

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images