Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WENGI WAJITOKEZA WIKI YA HIFADHI YA JAMII DODOMA

$
0
0
 Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Bima ya Afya, Grace Michael akimpa maelekezo juu ya shughuli za mfuko Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA, Jayne Nyimbo
 Mmoja kati ya watu walihudhuria maonesho hayo akipatiwa huduma ya afya na afisa wa NHIF.
 AfisaMasokowa SSRA, Naima Bakari akitoa maelezo ya kazi Kuu za Mamlaka kwa wananchi wa Dodoma.
 Mmoja kati ya wananchiwa Dodoma akijiandikisha katika banda la SSRA
 Afisa Masoko wa SSRA, Naima Bakaria kitoa maelezo ya kazi kuu za Mamlaka kwa wananchi wa Dodoma
Mh Arden Rage akijiandikisha katika banda la GEPF baada ya kupata maelezo ya Mfuko kutoka  kwa, Aloyce Ntukamazina na Josephat Mshana
 Bw Lewis NgirwaakielezeafaidayakujiunganaMfukowa GEPF
 Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Anna Shayo akimkabidhi kitambulisho cha uanachama Mh. Margaret Agnes Mkanga, Mbunge wa Viti Maalum mara baada ya kujiunga na PPF alipotembelea banda la Mfuko.

Mbunge wa Viti Maalum Mbeya Mh. Dr. Mary Mwanjelwa  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF Kutoka kulia ni  Afisa Majanga wa Mfuko Bw. Noel Assenga, Meneja  Uhusiano Bi. Lulu Mengele na Mhasibu wa PPF  Bi. Grace Fihavango alipotembelea banda PPF.

JK aongoza kilele cha maadhimisho Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Dodoma leo

$
0
0
Meneja Uhusiano Mfuko wa PPF Bi Lulu Mengele akimweleza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mfuko huo unavyosaidi kuendeleza kielimu watoto wa wanachama waliofariki wakati Rais alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali ya mifuko ya Hifadhi za jamii hapa nchini wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii yanayofanyika mjini Dodoma.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio. Picha na Freddy Maro

MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII PAMOJA NA SSRA YATOA MISAADA KATIKA WODI YA WAZAZI YA CHIKANDE PAMOJA NA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI CHA MIYUJI

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha uhusiano bi Sara Msika akikabidhi msaada wa shuka 100 na magodoro 30 katika wodi ya wazazi ya chikande

Mkuu wa kitengo cha uhusiano cha SSRA Bi Sara Msika akiwa amembeba mmoja kati ya watoto waliozaliwa katika Hospital ya Genera,  wodi ya wazazi ya Chikande mkoani Dodoma..

Wawakilishi wa Mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na SSRA wakikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu wa akili cha Miyuji Cheshire mkoani Dodoma.

Taarifa toka shirikisho la soka nchini (TFF) leo

Diwani awanusuru wanafunzi kuanguka shuleni

$
0
0
Mganga wa jadi Aweso Kipaku ambaye ni diwani wa kata ya Mswaha iliyopo wilayani Korogwe, akiwa ameshikilia kitu kinachodaiwa ni jini alilolitoa katika moja ya darasa la shule ya msingi Kwemsala iliyopo kata ya Mtindiro wilayani Muheza juzi, wengine aliyevaa fulana ya punda milia ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Shabani Hamisi.
Na Mashaka Mhando,Muheza

DIWANI wa kata ya Mswaha iliyopo wilayani Korogwe, Aweso Kipaku amefanya kazi ya kuwanusuru wanafunzi wa shule ya msingi Kwemsala iliyopo kata ya Mtindiro wilayani Muheza, waliokuwa wakianguka kutokana na kuwepo madai ya imani za kishirikina.

Akifanya kazi hiyo, juzi katika shule hiyo Diwani huyo aliyealikwa na kamati ya shule ya kijiji hicho, alianza kupita kila darasa la shule hiyo huku akionekana amepandisha mapepo yaliyokuwa yakimuongoza huku wananchi wa kijiji hicho wakijazana kuona kazi anayofanya diwani huyo.

Diwani huyo mara baada ya kukimbizana na vitu vilivyokuwa havionekani kwa macho, alipoingia kwenye ofisi inayokaliwa na walimu, alipiga kelele kutaka aletewe unga wa sembe, maji na kuku alipopata vitu hivyo, aliibuka na pembe kubwa iliyokuwa imefungwa vitambaa vyeupe na vyekundu.

"Wananchi hivi vitu vilivyotoa mnavyoviona ndivyo vilivyokuwa vikiwasumbua wanafunzi, lakini jini jingine kubwa limekimbia huko katika makazi...Kazi ya kupambana nalo nitaifanya kesho (Ijumaa iliyopita)," alisema diwani huyo huku akiwa amekishika mkononi.

Akizungumza na wananchi mara baada ya diwani huyo kutoa vitu hivyo, Mwenyekiti wa kamati ya shule Shaban Hamis alisema tatizo la wanafunzi kuanguka katika shule hiyo lilianza tangu mwaka juzi na walipoitisha mkutano wa kijiji, viongozi wa dini walisema wangefanya maombi kuwanusuru watoto hao, lakini hawakuweza kufanya maombi hayo.

"Tuliona watoto wetu wanaendelea kuanguka wakipelekwa hospitali wanelezwa wana matatizo ya kisaikolojia, lakini tukiwapeleka kwa waganga wa kienyeji wanatibiwa na kupona, tukaona ni vema tumlete mganga huyu Kipaku (Diwani) ili awanusuru watoto wetu," alisema mwenyekiti huyo.

Mwalimu mmoja shuleni hayo Sophia Msangeni, alisema tatizo la wanafunzi kuanguka limekuwa likisababisha kushuka kwa taaluma shuleni hapo hatua ambayo ilikuwa ikileta kero na usumbufu mkubwa mara inapotokea suala la watoto kuanguka ambapo kwa siku wanaanguka watoto 20.

Golden Bush kushiriki Bonanza Staki Shari.

$
0
0
 Wapenzi wetu wa Staki Shari, Tunapenda kuwafahamisha kwamba timu yenu ya Golden Bush imethibitisha kushiriki katika Bonanza ya tarehe 19/05/2013 litakalo fanyika katika viwanja vya Staki Shari. Golden Bush itakuja na kikosi kamili kama kinavyoonekana katika picha hapo chini.  

Golden Bush itaingia uwanjani mnamo saa mbili kamili asubuhi tayari kutoa kipigo stahiki kwa timu yoyote itakayopambana na sisi. Waandaaji wa mashindano wanatambua ubora wa Golden bush itakoyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Wisdom Ndlovu, hivyo tunategemea kupangiwa timu itakayoonyesha upinzani na kuleta burudani kwa mashabiki watakaokuja kushuhudia Bonanza hilo.
Tungependa kuwataarifu kwamba mchezaji wa zamani wa yanga na timu ya taifa ya Tanzania Salum Athuman Mbududu amesajiliwa rasmi baada ya kufuzu majaribio ya wiki moja, hivyo tunapenda kumtangaza kuwa kuanzia leo Salum Athuman atakuwa mchezaj halali wa Golden bush Veterans.

Imetolewa na msemaji wa timu
Onesmo Waziri "Ticotico"

PSPF MKOANI RUKWA YATOA SOMO KWA WADAU JUU YA UMUHIMU WA MFUKO HUO KATIKA KUHITIMISHA WIKI YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

$
0
0
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akitoa somo kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa (Rukwa Teacher's College) juu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Umma. Semina hiyo imeenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini iliyofanyika kitaifa Mkoani Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza kilele cha maadhimisho hayo leo tarehe 17.05.213.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakimsikiliza mtoa mada kwa umakini mkubwa. Wahitimu hao ni sehemu ya wadau wakubwa wa baadae wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiendelea na kutoa mada alizoandaa kwa wahitimu hao juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wenye mafao mbalimbali.
Malipo ya uzeeni, Malipo ya ulemavu, Malipo ya mirathi, Malipo ya wategemezi, na Malipo ya mazishi ni sehemu ya mafao muhimu yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa umma. 

Wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakionekana kukolea na mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiagana na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu chuoni hapo baada semina ya shughuli na mafao muhimu yanayotolewa na mfuko wa PSPF nchini.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)

Tembo wa Selou wazidi kuteketea, Juhudi za wadau zipo wapi?

$
0
0
Mmoja wa wananchi wanaoshiriki katika ulinzi wa Pori la Akiba la Selou akingoa jino la Tembo aliyeuawa na majangili na kisha kukurupushwa na askari wanyama pori kabla hajafanikisha mpango wake wa kuchukua meno ya tembo huyu. Wadau wa wanyamapori wanabashiri kuwa hivi sasa idadi ya tembo wanauawa kwa ujangili ni kubwa mno kiasi cha kuhatarisha uwepo wa wanyama hao katika kipindi kifupi kijacho endapo hatua za kukabiliana na ujangili hazitachukuliwa haraka na kwa nguvu kubwa.
Meno ya Tembo yaliyokutwa yakiungua kwa moto baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majangili kukurupushwa na askari wanyama pori wakati wakijiandaa kukamilisha zoezi la kukausha meno hayo ili yasafishwe kwenda sokoni

Sehemu ya Pori la Akiba la Selou ambalo kwa sasa linakabliwa na chngamoto kubwa ya kukithiri kwa vitendo vya ujangili unaotishia kutoweka kwa wanyama hasa tembo.
Wakati Tembo wakiwa hatarini kutoweka kutokana na ujangili wanyama wengine wanaendelea kupeta akiwemo ngiri huyu ambaye ni mzee. hatari anayokabiliana nayo ni ya kuliwa na simba, chui, duma na wakati mwingine mbwa mwitu. hata hivyo wataalamu wa wanyamapori wanasema wanyama kama ngiri ni halali kuliwa kwa sababu wapo porini pamoja na umuhimu wao pia ni chakula kwa wanyama walao nyama.
Pundamilia nao mambo yao poa huko porini.

Rais Kikwete aongoza Sherehe za maadhimisho ya mifuko ya jamii

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau na viongozi wa mifuko ya hifadhi ya jamii wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mifuko hifadhi ya ya jamii iliyofanyika mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii nchini ni salama, iko katika hali nzuri kifedha, hakuna hatari ya mfuko wowote kufilisika, tofauti na uvumi ambao umekuwa unaenezwa na watu wachache katika siku za karibuni.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa mifuko yote ya jamii nchini inawekeza katika maeneo salama na kuwa uwekezaji huo ni endelevu na ni kwa manufaa ya wanachama wa mifuko husika.

Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Ijumaa, Mei 17, 2013 wakati alipofunga Wiki ya Mifuko ya Hifadhi Tanzania baada ya kukagua maonyesho ya mifuko hiyo kwenye Uwanja wa Nyerere Square mjini Dodoma.

Katika hotuba yake iliyozungumzia masuala mbali mbali yanayohusu maendeleo ya mifuko ya hifadhi nchini na mafanikio ambayo yamepatikana katika eneo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mifuko yahifadhi, Rais amesema tathamini ya kifedha ya mifuko yote ya hifadhi nchini imekamilika na kubaini kuwa mifuko yote iko katika hali nzuri na ni endelevu.

Amesema Rais Kikwete: “Raslimali ya mifuko ya hifadhi ya jamii imeongezeka kutoka sh trilioni 3.7 mwaka 2010 na kufikia trilioni 5.3 mwezi Desemba, 2012. Tathmini hii imefuta dhana ya watu wachache waliokuwa wanaeneza uvumi kuwa baadhi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ipo katika hali mbaya kifedha.”

Uvumi huo ulitokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyotolewa mwaka huu ambako umeonyeshwa kuwa Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF) unaidai Serikali mabilioni ya fedha, jambo ambalo Rais Kikwete amesema ni kweli na kufafanua historia ya deni hilo akisema kuwa lilizaliwa Julai, mwaka 1999 wakati watumishi wote wa Serikali walipoingizwa katika mfuko wa hifadhi ambako watumishi hao walitakiwa kulipiwa mchango kiasi fulani na Serikali.

“Awali deni hili halikujulikana. Lakini maadamu limejulikana litalipwa na kwa kuanzia mwakani Serikali italipa kiasi cha sh bilioni 50 ikiwa ni sehemu ya kulipa deni hilo. Na wala hakuna mtumishi yoyote wa umma ambaye atakosa kulipwa malipo yake halali kwa sababu ya hali hiyo. Lengo letu ni kuona kuwa hakuna mfanyakazi atakayekosa mafao yake kwa sababu ya Serikali, yaani mwajiri wake. Hatuwezi kufanya kamari na mafao ya wafanyakazi.”

Kuhusu usalama wa uwekezaji wa mifuko hiyo, Rais Kikwete amesema: “Jambo jingine linalonipa faraja ni ule uhakika kuwa sasa uwekezaji unaofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii ni salama na wenye manufaa kwa wanachama wake. Kwa maneno mengine hakuna mwanya wa kuichezea kamari michango ya wanachama inawekezwa kwenye miradi inayomnufaisha mwanachama moja kwa moja na taifa kwa jumla.”

Rais amefafanua kuwa hali hiyo imetokana na kukamilika kwa Kanuni za Uwekezaji zilizoandaliwa na Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi (SSRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu. “Tangu kuanza kutumika kwa kanuni hizo Mei, 2012, uwekezaji wa mifuko ya jamii umeongezeka kutoka sh trilioni 3.38 hadi kufikia sh trilioni 4.24.”

Annual charity Mayors ball launched

$
0
0
The Annual Mayors Charity ball, Charity fundraising cum advocacy event aimed at being the Mayor of Ilala signature event where by it shall bring all leaders from various sectors in Tanzania under one roof for one purpose, serving the society
Honoring the intentions of its founders, the Ilala Mayor’s Charity Ball., a non-profit organisation, is committed to raising money to directly benefit residents of Ilala Municipality. Proceeds from the annual Mayor’s Charity Ball will be awarded to charities chosen annually from a random selection process from an eligible pool of applicants.
“Behind Every successful nation, is an educated populace. In order to create a conducive learning environment for our children and future of the country, various tools are a necessity, one of them being a desk, Thus towards this years annual mayors ball, we shall focus primarily on making sure students in Ilala Municipality can sit on a desk with support from various organizations and public at large” stated Hon Jerry Silaa, Mayor of Ilala Municipal Council as he launched the campaign at Hyatt Kilimanjaro on 17 My 2013
This years mayors ball project is aptly named "Dawati ni Elimu" with a slogan
“Kalisha mmoja, boresha Elimu”
The First of its kind mayoral ball aims to raise TZS 4, 98 Billion towards providing desk to 30,487 primary and secondary schools in Ilala Municipality by end of financial year 2013/14. 100% of all funds shall proceeds towards realization of this project.
 “Towards the building up of the Mayors Charity ball, there will be various events such as Football match, music concerts, fashion show and charity walks that shall be part of the fundraising initiative that shall include people from various strata of the society” stated Mustafa Hassanali, managing Director of 361 Degrees, the company that have created and conceptualized the project For the Mayors office as part of the Public private partnership programme.
So far there 86,242 desks are required out of which there are currently only 55, 755 desks which are being used. Thus there is a deficit of 35.35% of desk, whose void can be filled by creating a mass campaign that will be the ownership of the public where each and every citizen will participate towards Donating minimum for facilitating desk to all schools in Ilala.


REQUIREMENTS
AVAILABLE
LACK
PRIMARY SCHOOL
44151
28018
16133
SECONDARY SCHOOL
42091
27737
14354
These are some efforts made by Ilala municipal council in past three years for supplying desks in primary and secondary schools.

2010/11
2011/12
2012/13
2013/14
175,000,000,000
210,000,000
490,000,000
380,000,000

“I request individual, companies, Parastatals, organization and public at large to donate and sponsor this campaign whole heartedly, even if its just only 500 shilling” concluded mayor Silaa

The donations can be sent to Mayors Office at arnautoglu Hall, or can be sent by Mobile money via the following numbers : 0762 1010010782 1011130659 101112, 0778 111004
Towards the Mayors Charity Ball 2013, the Dawati Ni Elimu is supported by Hyatt Kilimanjaro hotel and organized by 361 Degrees

WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI SSRA WALIPOTEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONESHO YA WIKI YA HIFADHI YA JAMII MJINI DODOMA

$
0
0
Mjumbe wa bodi ya Wadhamini SSRA, Kabeho Solo akisaini kitabu cha wageni wakati wajumbe wa bodi hiyo walipotembelea banda la NSSF. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Miradi na Uwekezaji, Gerlad Sondo na Ofisa Mwandamizi Uhusiano na Huduma kwa  Wateja, Theopista Muheta.
Ofisa Mwandamizi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Theopista Muheta (kulia) akimkabidhi jarida lenye maelekezo ya kujiandaa kustaafu kwa mfanyakazi (staafu bila hofu), Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka  wakati wakati wa wajumbe wa bodi ya udhamini ya SSRA walipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii inayoendelea mjini Dodoma. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Miradi na Uwekezaji, Gerlad Sondo. (Na Mpiga Picha Wetu)

 Ofisa Uwekezaji na Miradi Mwandamizi wa NSSF, Gerald Sondo (kushoto) akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF katika maonesho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii.
 Wajumbe wa bodi ya Wadhamini SSRA wakitembelea banda la NSSF.
 Wajumbe wa Bodi ya Udhamini SSRA wakiwa katika banda la NSSF.
 Ofisa Uwekezaji na Miradi Mwandamizi wa NSSF, Gerald Sondo (kushoto) akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF katika maonesho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii.

PRADO TX For sale

$
0
0
PRADO TX IN GOOD CONDITION 
Model: 1997
 Millage: 115,000km 
Cc 3000 Engine 1KZ Diesel, 
Color: Green 2 tone Transmission: AT 5doors, 
8passengers, AC, PS, PW, AL, ABS.
 Price: Tsh 19m/- Negotiable 

TEL: 0712155221/0784587088 
E-MAIL:badijohn30@yahoo.co.uk





MAMLAKA YA WANYAMAPORI KUANZISHWA NOVEMBA

$
0
0
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AKIWA NA WALIOWAHI KUWA MAWAZIRI WA WIZARA HIYO NA MSITARI WA NYUMA NI WALIOWAHI KUWA MAKATIBU WAKUU WAKIFUATIWA NA WALIOWAHI KUWA WAKURUGENZI WA IDARA YA WANYAMAPORI NA MAOFISA WAANDAMIZI WA SASA WA IDARA YA WANYAMAPORI.

Na Tulizo Kilaga

Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza mikutano ya mchakato wa kupokea maoni kutoka kwa watu na makundi mbalimbali kuhusu uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA).

Mkutano wa kwanza umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Bustani kwa kuanza kupokea maoni kutoka kwa viongozi waliowahi kuwa mawaziri,makatibu wakuu na wakurugenzi wa wizara kuhusu uanzishwaji wa Mamlaka hiyo.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo alisema Sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2009 inaitaka Wizara kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori kazi ambayo itakamilika Novemba mwaka huu.

Mhe. Waziri alisema kuwa Wizara kwa kutambua umuhimu wa ushirikishwaji imeamua kuanza na viongozi waliowahi kuitumikia Wizara ili waweze kutoa maoni juu ya Sheria na Muundo wa Mamlaka ya Wanyamapori pamoja na Sheria ya Idara ya wanyamapori itakayobaki katika Wizara.

“Nyalaka hizi zimetengenezwa na watu wa ndani ya Wizara wenye uzoefu wa muda mrefu na hivyo tumeona ni vizuri tuwashirikishe ninyi viongozi mliowahi kuitumikia Wizara ili muweze kutoa michango yenu itakayotuwezesha kupata kitu bora kitakachopelekwa katika Baraza la Mawaziri na kisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ili Bunge la Novemba tuweze kuiwakilisha ikiwa ina baraka na maoni kutoka kwa kamati ya Bunge ili ipitishwe kama Sheria ya Mamlaka ya Wanyamapori,” alisema Mhe. Waziri.

Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori kutasaidia katika kurahisisha usimamizi wa rasilimali watu, kujitegemea kimaamuzi, na kuwa na uwezo wakujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha kutoka hadhina.

Miongoni mwa mawaziri waliohudhuria mchakato huo ni Mhe. George Kahama, Mhe. Getruda Mongella, Mhe. Ezekiel Maige, Mhe. Dkt. Juma Ngasongwa, Mhe. Zabehi Mhita na Mhe. Arcado Ntegazwa.

Makatibu wakuu waliofika ni Mhe. Philimon Luhanjo, Mhe. Marten Rumbanga, Mhe. Rose Lugembe, Mhe. Balozi Dkt. Ladislaus Komba, Mhe. Alhaj Muhidin Ndolanga, Mhe. Salehe Pamba na waliowahi kuwa wakurugenzi wa Idara ya Wanyamapori.

JAMANI, JAMANI, JAMANI... MINAKI HIGH SCHOOL JAMANI.....

$
0
0
Kaka, 
Minaki Pamechoka. Nasikitika. The original structure hawaitunzi... 
It needs restoration!  - MDAU




tanesco yamliza mdau wa lindi kwa kutotoa huduma stahili

$
0
0

Mdau nimeletewa lalamiko toka kwa Kaka yangu Hashimu Tambala (pichani) wa Manispaa ya Lindi  kama ifuatavyo-Namnukuu akilalamika kwangu Nimelipia gharama zote zinazotakiwa Januari 14,2013 ili kuunganishiwa
Umeme lakini hadi leo 17 May 2013 soli yangu ya viatu inaishia kwa safari lukuki za kwenda TANESCO bila mafanikio. 

Sijui nimwombe nani ili nipate huduma ya Umeme wakati Taratibu zote nimefuata? Naomba nisaidiwe kupitia blog hii Tafadhali!

Na Mdau Abdulaziz Video

Taswa FC, Taswa Queens zapata vifaa vipya vya michezo

$
0
0
Kinywaji maarufu cha kuongeza nguvu, Chilly Willy Energy Drink kimetoa msaada wa jezi na mipira kwa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya Netiboli, Taswa Queens kwa ajili ya kutumika michezo yake mbali mbali.

Meneja Masoko wa Kampuni ya TSN Group kinachosambaza kinywaji cha Chilly Willy Yohana Manoli alikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyopfanyika kwenye mgahawa wa Hadees uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Manoli alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Taswa SC ni kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuendeleza michezo nchini na hasa ukizingatia kuwa kinywaji cha Chilly Willy hakina kilevi na ni maalum kwa wanamichezo.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TSN Group, Meshack Nzowah alisema kuwa kinywaji chao cha Chilly Willy kina ubora wa kimataifa na wanaamini kuwa wanamichezo na wanajamii wataanza kutumia kinywaji hicho katika shughuli mbalimbali.

“Chilly Willy ni kinywaji ambacho hakina kilevi, kina ubora wa kimataifa na kutokana na hilo, kampuni ya TSN Group ikaamua kukisambaza nchini kwa lengo la kutoa bidhaa iliyobora zaidi, tunaamini wanamichezo wataanza kutumia hiki na vile vile ni maalum kwa waandishi wa habari na wadau wengine nchini,” alisema Nzowah.

Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza kampuni inayosambaza kinywaji cha Chilly Willy na kuwaomba waandishi wa habari kuanza kutumia kinywaji hicho. Majuto alisema kuwa Chilly Willy imetambua mchango wa Taswa SC katika kuendeleza michezo na kutoa msaada huo.



“Ni faraja kubwa kuwa na kinywaji hiki hapa nchini na hasa kwa kutujali wana habari, kwa vifaa hivi, Taswa FC na Taswa Queens zitakuwa na nguvu na ubora kama wa Chilly Willy,” alisema Majuto.

Majuto alisema kuwa jezi hizo watazizindua rasmi Jumapili katika mechi dhidi ya timu ya kombaini ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini itakayochezwa kwenye uwanja wa Leaders Club kuanzania saa 5.00 asubuhi.

Alisema kuwa timu ya mabondia itaongozwa na bondia mkongwe nchini, Rashid “Snake Man” Matumla na mabondia wakali wengine kama Francis “SMG” Cheka, Cosmass Cheka, Mbwana Matumla, Karama Nyilawila, Maliki Kinyogoli, Hassan Matumla, Daudi Mhunzi, Saidi Yazidu, Francis Miyeyusho , Thomas Mashali, Charles Mashali na wengine wengi.

Majaliwa awataka wanasiasa kuacha uchochezi katika jamii

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi 
 Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa [TAMISEMI] Mhe Kassim Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa amewataka wanasiasa mkoani Lindi kuacha tabia ya kuwa chanzo cha kuchochea vurugu katika jamii badala yake washirikiane na watendaji na wananchi ili kuinua mkoa huo ambao huko nyuma kimaendeleo. 
Naibu waziri huyo ametoa wito huo wakati alipokuwa anazungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa [RCC] katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Lindi.
Alisema kazi kubwa ya wanasiasa ni kutembelea wananchi kwa lengo la kuwasikiliza kero zao ,kuwahimiza na kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na sio kuchochea kufanya vurugu na kusababisha kuvunjika kwa amani. 
"Wanasiasa wamekuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo badala ya kushiriki vurugu.
“Sio vyema wanasiasa waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kusimamia na kuwawakilisha wakatumia nafasi hiyo majukwaani kutamka maneno ya uchochezi na kusababisha kupotea mwelekeo wa kuwaletea wananchi wake maendeleo hii inaonesha usivyotosha kwa wapiga kura", alimalizia Mhe Majaliwa 




Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara
Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara

Naibu Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa ambae Pia ni ,Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Mhe Kassim Majaliwa, akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dkt.  Nassor Ally Hamid wakati wa mapumziko mafupi ya Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mhe Ludovick Mwananzila akifunga kikao cha bodi ya Barabara Mkoa

Tanzania na Canada zasaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Uwekezaji

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.Membe (Mb.), kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. John Baird wakisaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Uwekezaji (FIPA) kati ya Tanzania na Canada. Hafla hiyo fupi ilifanyika Wizarani tarehe 16 Mei, 2013.
Mhe. Membe na Mhe. Baird wakiendelea kusaini mkataba huo huku Maafisa wa Sheria kutoka Tanzania na Canada wakishuhudia. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Bw. Abdallah Mtibora, Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu (katikati), na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Bibi Grace Shangali wakishuhudia uwekaji saini wa Mkataba wa FIPA.
Wajumbe wengine waliokuwepo kushuhudia tukio hilo la uwekaji saini wa Mkataba wa FIPA.
Mhe. Membe  na Mhe. Baird wakibadilishana Mkataba huo mara baada ya kusaini.
Mhe. Membe na Mhe. Baird wakionesha kwa Wajumbe Mkataba waliosaini.

Article 2

WWF yafanya uzinduzi wa mradi shirikishi wa uvuvi katika wilaya 5 hapa nchini

$
0
0
Mbunge wa Mafia, Mhe. Abdulkarim Shah, akichangia hoja katika uzinduzi wa mradi shirikishi wa uvuvi katika wilaya za Rufiji, Mafia, Kilwa, Temeke na Mtwara vijijini, leo, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa WWF-Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato, akifungua warsha ya mradi shirikishi wa uvuvi endelevu unaofadhiliowa na Umoja wa Ulaya na kuendeshwa na WWF na wadau, katika wilaya hizo.
Washiriki katika warsha ya mradi shirikishi wa uvuvi unaofadhiliwa na EU /WWF katika wilaya za Rufiji, Mafia, Kilwa, Temeke na Mtwara vijijini, kama ulivyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images