Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA SANAA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA LA PAMBA MOTO

$
0
0
Tamasha la sanaa za Ufundi la za Jukwaani lenye lengo la kupamba Siku ya Makumbusho Dunia limeanza rasmi katika viwanja vya Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam. Hadi sasa watu wengi wanazidi kumiminika ili kujifunza na kuburudika kwa njia mbali mbali za sanaa.

Matukio mbali mbali ya wanunuzi na wajasiriamali kama yanavyo onekana katika picha zilizo pigwa hivi punde.
Afisa Mkuu wa Raslimali watu wa Makumbusho ya Taifa Bw Fredrick Mwakalebela akimpongeza Bi Josephine Mpugusi wa TUFAFO ENTERPRISES kwa jitihada zake za ujasiriamali alizozianza mika 21 iliyo pita. Bi Mpugusi ameshiriki tamasha hili ili kuwakumbusha watanzania namana ya kupika Vyakula vya asili, kuvaa kiasili na kutumia mapambo ya kiasili.
Picha zote juu zinaonesha namna watu mbali mbali wakimiminika katika viwanja vya Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam mkabala na chuo cha IFM ili kujipatia bidhaa mbali mbali za asili. Picha habari na SIXMUND J. BEGASHE wa Makumbusho ya Taifa.

pinda akutana na bosi wa UNHCR nchini na wataalamu wa nyuki mjini Dodoma leo

$
0
0
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu Mjini Dodoma leo
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Joyce Mends-Cole, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mjini Dodoma leo
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata Maelezo kuhusu mizinga ya nyuki  iliyofinyangwa kwa udongo kutoka kea Mkurugenzi wa Shirikala African SoilHives Technology la mafinga Iringa, Donald Kalinga (kushoto) kwenye makazi yake Mjini Dodoma leo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Farida Mgalama, Tekla Pila na Beather Mkono, wote ni wananchama wa Shirika hilo
  Watalaamu wa nyuki kutoka Kampuni ya National Beekeeping Supplies Limited ya Dodoma, David Kamala  (kushoto) na Abubakar Salum wakilina asali kwenye shamba la ufugaji nyuki na kilimo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda lililopo Zuzu Mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Mzinga mmoja ulitoa wastani wa lita 10 za asali

OSHA YAKOSHA WANANCHI KATIKA Maonesho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii Dodoma

$
0
0
 .Mwananchi akipata maelezo toka kwa ndugu Claver Happy Mwinuka mshiriki wa maonesho kwenye Banda la Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA) kwenye wiki ya Hifadhi ya Jamii Dodoma.
 Mtendaji Mkuu wa OSHA Dr. Akwilina Kayumba, akimkabidhi Machapisho mbalimbali ya OSHA,Bi Irene Isaka alipotembelea Banda la OSHA kwenye maadhimisho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii Dodoma.
  Mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza Magodoro cha Modern Mattress cha mjini Dodoma akipima afya yake, kwenye Viwanja vya Nyerere Square, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii
 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Magodoro cha Mdoern Matresscha mjini Dodoma wakipata maelekezo kutoka kwa Dr. Wambura juu ya upimaji wa mapafu kabla ya kuanza kwa zoezi la upimaji kwenye banda la OSHA. 

.Mfanyakazi akipima uwezo wa mapafu kuafanya kazi kwenye Banda la OSHA kwenye maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii Dodoma. Picha na Afisa Habari-OSHA

UJENZI WA KITUO CHA SIKOSELI NCHINI WAPIGWA JEKI

$
0
0
 Mwenyekiti wa  Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (kulia) akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.   Wengine ni baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.
  Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Mhe. Abdallah Mwinyi (kuli) akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.   Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Grace Rubambey.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya ugonjwa wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey  (kulia) akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia walikuwa wakimkaribisha mwendesha baiskeli Alan Knight (wa tatu kushoto), ambaye hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam 
 Mwambata wa Kisiasa kutoka Ubalozi wa Canada nchini, Dk. Carol McQueen  (kulia) akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia walikuwa wakimkaribisha mwendesha baiskeli Alan Knight (hayupo pichani), ambaye hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Ubalozi huo ulitoa shs milioni 30 kwa ajili kusaidia suala la utoaji elimu kwa jamii kuhusu sikoseli.
 Baadhi ya watu waliohudhuria hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ua ujenzi wa kituo cha kuhudumia wagonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika hafla hiyo ambayo jumla ya shs milioni 54 zilichangishwa. Ujenzi wa kituo utagharimu shs milioni 75.

BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAPITA BUNGENI

$
0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akisoma hotuba ya Wizara yake Bungeni
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu wakisikiliza kwa makini michango ya Wabunge kwa Wizara yao.

 Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia mawasilisho ya bajeti yao Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwaongoza Mawaziri na Naibu Mawaziri kuwapongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory  Teu baada ya  Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Naibu wake Mh Gregory Teu wakipongezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Joyce Mapunjo nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa na Bunge.
Watumishi na Viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ukumbi wa Bunge baada ya Bajeti yao kupita.

ankal akipigwa sop-sop kwa Bitebo junior mwanamyamala

$
0
0
Ankal akiritachi kialaza kwenye saluni ya Bitebo jnr Hair Designer chini ya mikono  stadi ya kula vichwa ya Masudi Bitebo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es salaam. Yeye anaipenda saluni hii kwa sababu mataulo, mikasi na hata sabuni huwekewa mteja mahususi tena kwa jina. Hakuna kuchanganya madawa hapo....

MHE. MEMBE AMKARIBISHA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CANADA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,  Mhe. John Baird  alipowasili kwenye Hoteli ya HyattyRegency Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki Chakula cha Mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Membe. Mhe. Baird alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine pia walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Canada pamoja na kusaini Mkataba "Foreign Investment, Promotion and Protection Agreement" (FIPA).


Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Baird wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.



Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Baird akimsikiliza. Kushoto ni Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Alexandre Leveque.





Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Baird zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. Picha na Rosemary Malale


JESHI LA POLISI ARUSHA LAKANUSHA KUMWACHIA MTUHUMIWA WA UJANGILI.

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,  Liberatus Sabas 

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekanusha taarifa ya kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa ujangili  Bw. Frank William Silangei maarufu kwa jina la “Ojung’s Mwarusha” mkazi wa Ngaramtoni Kibaoni iliyotolewa na gazeti moja la kila wiki.  

Akizungumza katika mahojiano kwa njia ya simu na Idara ya habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema kuwa mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 32  hivi sasa yuko mahabusu na taratibu za kumfikisha  mahakamani zinaendelea kufanyika.

Kamanda Sabas ameeleza kuwa  mtuhumiwa  Silangei hajaachiwa huru kama ilivyoripotiwa na gazeti  hilo linalotoka kila Alhamis katika ukurasa wake wa kwanza na wa pili na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo liko makini katika kutekeleza majukumu yake.

“Si kweli hajaachiwa, natamani ungekuwa hapa Arusha nikakupeleka mahabusu ukamuona mtuhumiwa kwa macho yako”, amesema Kamanda Sabas.

Kamanda Liberatus Sabas amesema Serikali kupitia Jeshi la Polisi  itaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa vitendo vyote vya ujangili vinatokomezwa na yeyote atakayehusika na vitendo hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA WAENDELEA NA VIKAO VYA MAJADILIANO

$
0
0
 MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko y a Katiba, Bi. MwatumuMalale (kushoto) akichangia hoja katika Kikao cha ndani cha Tume hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam leo.Wengine ni Wajumbe wa Tume, Bw. Awadh Said (katikati) na Bw. Richard Lyimo.


MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Joseph Butiku (katikati) akichangia hoja katika Kikao cha ndani cha Tume hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Wajumbe wa Tume, Alhaji Said El Maamry (kushoto) na Bw. Yahya Msulwa.
(PICHA NA TUME YA KATIBA)

CONSULTANCY ASSIGNMENT - TRAINING MATERIAL REVIEW AND TRANSLATION TO KISWAHILI

$
0
0

Hello Friend,

I am looking for a Consultant who is capable of Reviewing The Training Material and make them Resource Book particular for Financial Education (Wealth Creation) targeting SME.

The work will also involve Translating the said Training Material from English to Kiswahili.

Please send me your CV if you meet the following:

1.     Knowledge on Financial Operations
2.     Experience in SME
3.     Experience in Stock Market; Investments; Trading
4.     Post-Graduate in Finance or Economics or Business Administration
5.     Able to review and write manuals and translate them into Kiswahili Sanifu.

Kind regards

Sanctus Mtsimbe
ConsNet Group Limited (EA Regional Consultancy Network)

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya kidum ft juliana ya 'Haturudi nyuma' si ya kawaida

DCI MANUMBA ATOA MBINU KUUKABILI UHALIFIU

$
0
0
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba akizungumza na Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika mafunzo ya kufanya Operesheni za Pamoja kati ya SARPCCO na EAPCCO.Mafunzo hayo yanafanyika jijini DAR Es Salaam.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi mbalimbali za Afrika ambao wanashiriki mafunzo ya kufanya Operesheni za Pamoja kati ya SARPCCO na EAPCCO.Mafunzo hayo yanafanyika jijini DAR Es Salaam.

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi. 

Wakurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai kutoka nchi 25 barani Afrika wametakiwa kutumia vizuri mafunzo ya Operesheni za pamoja ili kuweza kukabiliana na uhalifu ikiwemo vitendo vya ugaidi na uhamiaji haramu vinavyojitokeza katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa kasi hivi sasa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Pamoja na Umoja wa Wakuu wa Polisi Afrika Mashariki (EAPCCO) kuhusu kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.

DCI Manumba amesema uhalifu unaofanyika hapa nchini na ukanda huu wa Afrika Mashariki ndio huo huo unaotokea katika nchi nyingine hivyo ushirikiano na kubadilishana taarifa kutasaidia kutambua na kuweka mikakati thabiti ya kuweza kudumisha amani na usalama katika bara la Afrika.

“Kwa mfano suala la Wahamiaji haramu hatuwezi kupambana nalo sisi wenyewe kwa kuwa wanatoka katika nchi nyingine na hapa wanapita tu kwenda katika nchini nyingine hivyo lazima tubadilishane taarifa na kuwa na mkakati wa pamoja wa kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo” Alisema Manumba.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa Kimataifa INTEPOL kanda ya Afrika Mashariki kutoka Nchini Kenya Bw.Rego Francis amesema Majeshi ya Polisi yana wajibu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waweze kutoa taarifa za uhalifu mapema kwa vyombo vya usalama ili ziweze kufanyiwa kazi mapema kabla ya matukio kutokea.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (INTEPOL) Tanzania Kamishna Msaidizi wa Polisi Gustavus Babile amesema Mafunzo hayo ya siku mbili lengo lake ni kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na kuweka mikakati ya kufanya operesheni zitakazoweza kuutokemeza uhalifu.

Babile alisema kupitia mafunzo hayo wataweza kuandaa Operesheni zenye mafanikio zitakazoweza kushirikisha nchi nyingi katika kukabiliana na Ugaidi, Madawa ya kulevya, wahamiaji haramu, wizi wa magari na uhalifu wa aina nyingine unaotokea hapa Afrika. Mafunzo hayo yanafanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kumi na nane wa Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO ambapo katika maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na kufanya operesheni za pamoja baina ya SARPCCO na EAPCCO.

TANGAZO LA AJIRA KATIKA NCHI ZA AFRIKA KWA WATANZANIA WALIOPO UINGEREZA NA MAJIRANI

$
0
0

CAREERS IN AFRICA INAWATANGAZIA WALE WOTE WENYE SHAUKU YA KUTAFUTA KAZI BARA LA AFRIKA KUHUDHURIA KONGAMANO KUBWA LA KAZI LITAKALOFANYIKA JIJI LA LONDON KUANZIA TAREHE 17 MPAKA 19 MEI , 2013.

CCM UK -TUNAOMBA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE, BILA YA KUJALI ITIKADI ZAO ZA KISIASA, KUJIANDIKISHA NA KUHUDHURIA KWA WINGI KONGAMANO HILI KWA KUJITAFUTIA AJIRA, AMA HATA KUJIFUNZA MENGI MAZURI YATAKAYOJIRI.

KWA MAELEZO ZAIDI NA JINSI YA KUJIANDIKISHA TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI YA: www.careersinafrica.com

MKURUGENZI MKUU WA PPF ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA ZEP-RE

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bwana William Erio (pichani) amechaguliwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa mwaka wa kampuni ya Zep-Re kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi na wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kampuni hiyo. Uchaguzi huo umefanyika wakati wa Mkutano Mkuu huo uliofanyika jijini Mombasa, Kenya tarehe 10 Mei mwaka huu.

Bwana Erio, ambaye atashika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 3, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Gavana wa Benki Kuu ya Zambia, Dr. Michael Gondwe aliyemaliza muda wake. Wajumbe wengine wa Bodi hiyo wanatoka katika nchi za Kenya, Rwanda, Djibouti, Eritrea, Zambia, Sudan na PTA Bank.

Zep-Re ni kampuni ya bima mtawanyo kwa nchi za PTA yenye makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya na ina ofisi ndogo katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Sudan na Cameroun

Article 1


Nani kuficha mabango ya utani wa jadi siku ya Jumamosi?

$
0
0

Mashabiki wa Yanga, Kuendelea kurekodi matukio ya furaha Jumamosi??
Mashabiki wa Simba.....wataendeleza Kidedea hiyo siku ya Jumamosi???

Tiketi kwa ajili ya pambano la kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba na Yanga,zitakazokutana kesho (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar zinaanza kuuzwa leo (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali vya jijini Dar.

Vituo vitaanza kuuza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni na vitakuwa kama ifuatavyo,ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.

Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A.

Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (tapsea) kufungwa rasmi leo jijini arusha.

$
0
0
Mtoa mada iliyohusu Maadili kazini,Bwa.Alex Senzota kutoka Idara ya Usalama Kazini (GSO),akifafanua zaidi kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi husika,mapema leo kwenye Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) uliofanyika ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama chama cha Makatibu Muhtasi  Nchini Uganda (NASAP),Bi Edith Kutesa Giita akifafanua jambo kuhusiana na mada mojawapo ya iliyohusu Ni namna gani unaweza kuwa Katibu Muhtasi unaekwenda na wakati/wa kisasa,mapema leo kwenye Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) lililofanyika ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.

 Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Muhtasi  (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA),Bi Pili Mpenda akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi  likiendelea ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha,kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama chama cha Makatibu Muhtasi  Nchini Uganda (NASAP),Bi Edith Kutesa Giita.
 
Baadhi washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazojadiliwa  kwenye kongamano hilo lililofanyika dani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha. 
  Mmoja wa wachangia mada kutoka chuo  cha Sokoine,Bi Teddy Salum akizungumza kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi,wakati Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) likiendelea ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
 Mmoja wa wachangia mada kutoka chuo Kikuu cha Dar- Es Salaam (UDSM),akifafanua jambo kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi,wakati Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) likiendelea ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazojadiliwa  kwenye kongamano hilo lililofanyika dani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Article 23

$
0
0

JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA

   

    WIZARA YA MAJI 







              TAARIFA KWA UMMA

Katika gazeti la Nipashe la Jumapili tarehe 12 Mei 2013 mwandishi Mashaka Mgeta aliandika makala yenye kichwa cha habari “Aibu kwa Profesa Maghembe na dharau kwa wataalamu wa Wizara” na kuwa, Wizara ya Maji imejiwekea rekodi chafu kwa bajeti yake kurejeshwa kabla ya kupitishwa na Bunge na wataalamuwa wa Wizara ya Maji wamekuwa miongoni mwa wasiosikilizwa na kupuuzwa suala hilo si la kweli.

Mnamo tarehe 24 na 25 Aprili, 2013, Waziri wa Maji Mhe. Prof. Jumanne  Abdallah Maghembe (MB) aliwasilisha Bungeni Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2013/2014. Bajeti hiyo iliwasilishwa na mjadala uliendelea kwa muda wa Siku mbili. 
jadala mkubwa ulikuwa Bungeni baada ya kuwasilisha maoni ya Kamati ya kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa Bajeti ya Wizara ya Maji haitoshi.
Mjadala ulihairishwa na Mhe. Spika chini ya Kanuni ya Bunge 67(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kama Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 2 Toleo la 2002.

mji wa mtwara waghubikwa na ukimya leo, shughuli zimesimama kwa hofu ya vurugu, polisi waimarisha ulinzi

$
0
0
Na Abdulaziz Video,
Hali ya usalama ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni tete. Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi. Usafiri wa Pikipiki unapatikana katika baadhi ya maeneo machache ya mji, huku maneo makuu ya biashara yakiwa wazi bila ya pilikapilika za watu kama ilivyo kawaida. 
 Polisi wakiwa kwenye magari wameonekana katika maeneo mbalimbali ya mji, na wengine kuweka makambi madogo katika maeneo yanayoaminika kuwa na msongamano wa watu katika siku za kawaida.
Mwandishi huyu ameshuhudia magari ya polisi yakiwa na askari katika maeneo ya Bima, Soko kuu ambako pia kulikuwa na gari la kumwaga maji ya kuwasha, Magomeni, Skoya na Majengo.
 Hata hivyo hadi kufikia saa 7 mchana hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa amani, makundi ya vijana walionekana wakijadiliana mambo katika maeneo mengi ya mji. Hali hiyo imejitokeza kufuatia kusambazwa kwa vipeperushi na ujumbe wa simu za mkononi na watu wasiojulikana ukiwataka wafanyabishara kusimamisha shughuli za biashara kwa siku ya (leo) jana ili kutoa fursa kwa wananchi hao kusikiliza bajeti ya Nishati na Madini iliyotarajiwa kuwasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma. Hata hivyo bajeti hiyo itawaslishwa Bungeni Mei, 22, mwaka huu. 
 Sehemu ya kipeperushi hicho kilichopambwa na picha ya mtoto aliyeshikia kombora kinasomeka “Wote kwa pamoja siku ya tarehe17.05.2013 (Ijumaa saa 3 asubuhi) tusikilize bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (Bungeni) ili kujua mustakabali mzima wa gesi yetu na ili kuonyesha kilio, msimamo wetu kwa serikali wa kutaka maendeleo kwa mikoa ya kusini, siku hiyo huduma zote za jamii zisimamishwe” 
 Licha ya polisi mkoani hapa kuwasihi wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa jeshi hilo litaimarisha ulinzi bado wananchi wameonesha kutokubaliana na wito huo. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa ameliambia amesema kuwa hali ni shwari na kwamba jeshi lake limeimarisha ulinzi.
 “Hali ni shwari, wapo madereva Bodaboda wanaendelea na kazi zao, wananchi wanatembea kama kawaida, ispokuwa baada ya maduka yamefungwa” alisema Sinzumwa
Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi.
Ulinzi umeimarishwa kila kona
Mji wa Mtwara ni sehemu ya pilika pilika ya watu lakini leo hali si hivyo na katika kituo kikuu cha mabasi cha Mtwara hakuna basi lililoingia au kutoka kutwa nzima leo.

imeelezwa baadhi viongozi ndio wanaongoza kuvujisha siri za ofisi na si masekretari.!

Viewing all 110020 articles
Browse latest View live




Latest Images