Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA UPANDAJI MITI KESHO JIJINI DAR

0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema upandaji wa miti unaanza kesho hivyo kila mwananchi wa Dar es Salaam anatakiwa kupanda mti mmoja ikiwa ni kwa ajili ya ustawi wa afya.

Amesema kuwa upandaji miti utafanywa katika Wilaya yaTemeke kwa kupanda miti katika barabara ya Kilwa na baada kupanda miti atakagua miundombinu ya maji kwa ajili ya kumwagilia miti katika Wilaya Ilala pamoja na Kinondoni.

Makonda amesema miti hiyo itakayopandwa ni faida ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili hewa na pamoja na vivuli vya kupumzika.Aidha amesema kila mwananchi lazima afanye jitihada za kupanda miti ikiwa ni pamoja watendaji wote wa mitaa na kata kuhamasisha wananchi kupanda miti.

Hata hivyo amewataka mashabiki wa yanga na simba kupanda miti kabla ya kuanza mpira kati timu hizo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza leo na waandishi habari juu ya upandaji miti utaozinduliwa kesho,jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

YANGA VS SIMBA NI TUMBO JOTO.

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHAMRA SHAMRA za mechi ya watani wa Jadi baina ya Yanga na Simba zinazidi kupamba moto kwa kila upande kujinadi kwa kila namna.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa saa 10, ukichezeshwa na Mshambuliaji wa beji ya FIFA, Martin Sanya akisaidiwa na Frank Chacha na Mpenzu huku mezani akiwa Hery Sasii.

Mechi hiyo itakayoanza kutumia mfumo mpya wa kadi za kieletroniki umekuwa na hamasa kubwa sana kwa mashabiki na wengi kujitokeza kuchukua kadi hizo.

Yanga wakiwa njiani kuingia Dar es salaam wakitokea Pemba walipoweka kambi ya wiki moja, Simba tayari wameingia jijini na asubuhi ya leo kufanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Gymkhana.

Timu hizi zimeweza kukutana mara 96 na tayari  Mabao  196 yakiwa yamefungwa huku katika mechi tano  tano za mwisho Yanga ameshinda mara mbili, Simba ikishinda mara moja na sare mbili. Yanga Ikiwa haijabadilisha benchi la ufundi  pamoja na kikosi kwa muda mrefu wanakutana na Simba ambayo imebadilisha asilimia kubwa ya wachezani na benchi la ufundi.

Lakini siku ya Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbeya City itaikaribisha Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro. Mbao na JKT Ruvu Jmwatakuwa  kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

WIZARA YA AFYA YAUPONGEZA MKOA WA SINGIDA KWA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI..

0
0
Grace Singida.

Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imeishauri mikoa yote ya Tanzania bara kuiga mfano wa mkoa wa Singida wa kuanzisha huduma za kibingwa za mkoba kwa ngazi za wilaya ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji.

Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara hiyo Dokta Magreth Mhando ametoa ushauri huo katika hospitali ya Mtakatifu Calorus Mtinko Singida Vijijini alipotembelea kujionea awamu ya pili ya zoezi la huduma za kibingwa za Mkoba. Dokta Mhando amesema kumekuwa na huduma za kibingwa za mkoba ila hazikufanyika vizuri kama ambavyo mkoa wa Singida umekuwa ukifanya na kutoa pongezi za Wizara kwa Mkuu wa mkoa na Mganga mkuu wa mkoa kwa ubunifu huo.

Amesema huduma za kibingwa za mkoba zimekuwa zikiratibiwa na taasisi au hospital kubwa kama Muhimbili ambapo madaktari bingwa wamekuwa wakitoa huduma kwa ugonjwa fulani na kwa ngazi ya hospitali za Mkoa tofauti na zoezi linaloendelea Mkoani Singida la kutoa huduma za kibingwa kwa magonjwa mbalimbali.

Dokta Mhando ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa madaktari bingwa nchini wizara imetenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari na kuwashauri waajiri ambao ni makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari hao kwakwuwa wizara pekee haitaweza.

Amesema utaratibu ni kuwa na madaktri bingwa angalau watano kila Mkoa lakini mikoa mingi haina idadi hiyo huku akiongeza kuwa lengo la kutembelea zoezi hilo Singida nikujionea hali halisi na sio kusubiria taarifa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe mara baada ya kutembelea wodi zote na kuzungumza na wagonjwa waliopata huduma za kibingwa amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kuongeza muda wa kutoa huduma hiyo kutoka siku tano hadi nane kutokana na wingi wa wagonjwa waliojitokeza.

Mhandisi Mtigumwe amesema huduma hiyo inasaidia kutambua magonjwa na kuyatibu kabla hayajawa sugu lakini pia gharama zikiwa nafuu kutokana na kusogezwa kwa ngazi za halmashauri. Ameongeza kuwa lengo la ofisi yake ni kuhakikisha huduma za kibingwa za mkoba zinapelekwa kwa kila halmashauri na endapo zoezi likikamilika na kukiwa na uhitaji mkubwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudia zoezi hilo.

Mhandisi Mtigumwe amesema kuelekea Tanzania ya viwanda afya bora ni muhimu na wazalishaji wakubwa ni wananchi wa ngazi za chini hivyo huduma hiyo itasaidia kuimarisha afya ili waweze kuzalisha bidhaa kwa wingi na zenye ubora.

Amesema kwa wale wagonjwa watakaopewa rufaa kwenda nje ya Mkoa utaratibu utaangalia wa kuwapatia usafiri wa Mkoa ili kuwapeleka hasa wale wasiojiweza. Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki amesema kwa muda wa siku tano wagonjwa zaidi ya 800 wameonana na madaktari bingwa huku idadi ikitarajiwa kuongezeka kutokana nakuongezwa kwa siku za klutoa huduma.

Dokta Mwombeki amesema wagonjwa wengi wanaofika wanatoka maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kijijini na wenye hali duni ya maisha hivyo zoezi hilo limesaidia wananchi hasa wwenye kipato cha chini. Amesema madaktari bingwa wanaotoa huduma za kibingwa za mkoba ni madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, watoto, macho, meno, magonjwa ya ndani na daktari bingwa wa upasuaji.

Wagonjwa waliopata huduma wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kubuni utaratibu wa kuwafuata wagonjwa karibu ili kuwapatia huduma za kibingwa kwakuwa inawasaidia kupata matibabu mapema kabla magonjwa hayajawa sugu na kushauri huduma iwe endelevu angalau kila mwaka.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe (katikati) akizungumza na wagonjwa, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na kushoto ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.
 Wagonjwa waliofanyiwa operesheni ya macho na madaktari bingwa wakizungumza na Mkuu wa Mkoa (hayupo).
 Wagonjwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa alipowatembelea na kuona huduma za mkoba za kibingwa zikiendelea kutolewa, wagonjwa hao walikuwa wakisubiri kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA.

PPRA YAKABIDHI RIPOTI YA UKAGUZI KWENYE UNUNUZI WA UMMA MWAKA 2015/2016

0
0


Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akikabidhiwa Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga. Makabidhiano yaliyofanyika Wizarani jijini Dar es Salaam, Septemba 30, 2016

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (kushoto kwa waziri wa Fedha na Mipango aliyekaa katikati), akifafanua jambo kabla ya kukabidhi Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (kushoto), akifafanua jambo kabla ya kukabidhi Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA-Dkt. Laurent Shirima.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (kushoto), akitoa taarifa aya ripoti hiyo mbele ya waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kwenye makao Makuu ya Mamlaka hayo, Jijini Dar es salaam, Septemba 30, 2016. Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dkt. Laurent Shirima na kushoto kwake ni Wajumbe wa Bodi hiyo Dkt. Leonard Chamriho ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) na Dkt. Edmund Mndolwa.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango baada ya kupokea Ripoti ya Ukaguzi wa Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Waziri Mpango aliwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango).

WAREMBO 30 MISS TANZANIA WAINGIA KAMBINI LEO, LILIAN KAMAZIMA AWAPA SOMO

0
0
Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.

Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30 wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU NCHINI WATOA MICHE YA MITI 600 KUUNGA MKONO KAMPENI YA UPANDAJI MITI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina akipanda mti katika Shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete, Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya upanadaji miti Jijini Dar es Salaam iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, Kampeni hiyo ijulikanayo kama "Mti Wangu" itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umechangia miche ya miti 600 katika shule hiyo na miche ya miti mingine 3,000 itatolewa kesho wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa ajili ya Jijiji la Dar es Slaam, katika awamu ya pili watachangia tena miche ya miti 5,000.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, Elestina Chanafi (wa pili kushoto) baadhi ya miche ya miti kati ya miche 600 iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya shule hiyo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) miche 600 ya miti iliyotolewa na ofisi yake kwa ajili ya shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam ijulikanyo kama “Mti Wangu” . Katika uzinduzi huo TFS imechangia miche ya miti 3,000 kati ya miche 8,000 ambayo imepanga kutoa kwa ajili ya kupandwa katika Jiji la Dar es Salaam. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.

PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA BARABARA YA JUU KUKAMILIKA KWA WAKATI.

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya kikandarasi ya Sumitomo Mitsui inayojenga mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara kumaliza ujenzi huo kwa wakati mradi huo ili kusaidia kupunguza tatizo la msongamano. 

Akizungumza mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutajenga historia nchini kutokana na kuwa ni wa mwanzo kujengwa.

“Nimefurahi kuona mradi huu upo katika hatua nzuri, naomba mkamilishe mradi huu unakamilika kwa ubora na kwa wakati ili tatizo la msongamano lililopo katika maeneo haya kupungua au kuisha kabisa”, amesema Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa umakini na kwa uangalifu wakati wa kipindi chote cha ujenzi ili kuitokuweza kusababisha foleni katika eneo hilo. Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili kurahisisha kazi za ujenzi huo kukamilika kwa wakati na kupata matokeo chanya.

“Nawaomba watanzania wenzangu kuwa wavumilivu na usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote, kwani ukamilifu wa mradi huu utasaidia kupunguza tatizo la msongamano katika barabara hizi”, amefafanua Waziri Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amekagua daraja la watembea kwa miguu eneo la Buguruni Sheli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitunza daraja hilo ambalo uwepo wake umesaidia kupunguza ajali katika maeneo hayo.

“Ni matumaini yangu sasa wakazi wa maeneo haya mtavuka kwa amani kupitia daraja hili, na ajali zilizokuwa zikitokea maramara hazitakuwepo tena”’, amesema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemuahidi Waziri huyo kumaliza kwa wakati ujenzi huo na kumhaakikishia Waziri kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa na viwango vilivyo bora.

Mradi wa Tazara Flyover ni msaada kutoka Serikali ya Japan ambao umegharimu shilingi bilioni 93.4 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale(Wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya ramani ya Ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa( Wa kwanza kushoto) wakati alipokagua ujenzi huo Jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (Kulia kwake) wakati alipokagua ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover, Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akifafanua jambo mara baada ya kukagua daraja la wapiti kwa miguu lilopo Buguruni Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa barabara wa Wizara Eng. Light Chobya. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Wananchi mara baada ya kumaliza kukagua daraja la wapiti kwa miguu lililopo Buguruni Jijijni Dar es salaam. 

WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YA KUHAMIA DODOMA

0
0
Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.


Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.


“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba  huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote."


“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo


Amewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.

Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.


"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.


Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa  viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.


"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma," amesema.


Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA

IJUMAA, SEPTEMBA 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi wa Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba (kushoto) kuashiria kupokewa rasmi kwenye manispaa hiyo. Makbidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba 30, 2016 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016.  

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

KATIBU TAWALA WILAYA YA CHEMBA AZINDUA MASHINDANO YA DIWANI CUP,MSHINDI KUJINYAKULIA MBUZI BEBERU.

0
0

Katibu Tawala wa Wilaya,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wilaya Ndugu Nyakia Ally,amefungua mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba,huku akiwasihi vijana kucheza mpira wa miguu wakitambua kuwa kwa sasa ni ajira inayolipwa kwa pesa nyingi kulinganisha na michezo mingine hapa nchini.  

 Ndugu.Nyakia alieleza kuwa mashindano hayo yameandaliwa na Diwani wa Kata ya Chemba, Mhe Joseph Saini ambapo yanashirikisha timu sita kutoka katika Vijiji vitatu vinavyounda Kata ya Chemba.

Mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya Mbuzi beberu,Katika mashindano hayo yatakayokuwa ya kusimumua wilayani humo,Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally ameahidi kuongeza zawadi ya mipira miwili kwa mshindi wa kwanza, mpira mmoja kwa mshindi wa pili na watatu. 

 Vile vile Katibu Tawala huyo aliwataka vijana kushirikiana katika mashindano hayo bila kujali Itikadi zao za kisiasa, dini wala rangi kwani michezo hujenga Udugu, urafiki na upendo miongoni mwa wapenzi wa michezo husika.

Pamoja na hayo Ndugu Nyakia amemtaka Afisa Utamatuduni wa Wilaya hiyo kushirikiana na Waratibu wa mashindano hayo ili kupata timu nzuri miongoni mwa wachezaji wanao shiriki ligi hiyo,ili hatimaye kupata wachezaji watakao kuwa waanzilishi wa timu ya Wilaya ya Chemba, ili siku za usoni washindane na Wilaya nyingine za hapa Dodoma na baadae Kitaifa na kimataifa kwa kushiriki Soka la kiushindani katika ligi mbalimbali. 
Baadhi ya Washiriki na Washabiki wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye ufunguzi wa mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba mapema leo,ambapo mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,ambaye ni Mweyekiti wa kamati ya michezo,Ndugu Nyakia Ally (hayupo pichani).

TAMASHA LA 35 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO LAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WA BURUDANI

0
0

 Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, limeendelea kukonga nyoyo za wakazi wa mji wa Bagamoyo na maeneo ya jirani ikiwa ni muendelezo burudani za kila siku tangu lilipofunguliwa mwanzoni mwa wiki hii, tamasha hilo limesheheni madhari halisi ya Muziki na ngoma mbalimbali za kiasili, Sanaa za Uchoraji na Uchongaji pamoja na Sanaa za Sarakasi na Maigizo mengi ya kuvutia na ya aina yake, linandelea kufanyika katika Kumbi za Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) Mkoani Pwani, huku likitazamiwa kufikia tamati siku ya Jumapili Oktoba 2, 2016. Zifuatazo ni picha za kuvutia za matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye Tamasha hiyo.


UKAWA YASITISHA TENA MAANDAMANO YA UKUTA

0
0

Mwenyekiti  wa Chama cha CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe


Na Anthony John,
Globu ya Jamii
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kimesitisha  shughuli  zote  za maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango wa siku moja.
 Hayo yamesemwa leo na  Mwenyekiti  wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati  akizungumza  na Waandishi  wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda  Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano  ya  kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu  wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe

TASWIRA MBALIMBALI UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA ILOMBA JIJINI MBEYA

0
0
 Bendi ya Jeshi la Askari Magereza Likiongoza maandamano Kutokea Stendi ya Mabasi ya mzunguko maharufu kwa jina la Daladala Kabwe na kuelekea katika uwanja wa Ccm Rwanda Nzovvwe Jijini Mbeya kuajili ya kuzinduwa Jengo Moja lililo jengwa na Shirika la "UNICEF" Eneo la Ilomba Jijini Hapo kwa kazi maalum ya kuwasaidia watoto wanaofanyiwa vitendo vya kikatili na kuchukuliwa hatua kali za kisheria na Dawati Hilo la Kijinsia ambalo lipo chini ya Jeshi la Polisi Mkoa Wa Mbeya pamoja na Wadau wa Dawati la Jinsia.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akifurahi Jambo wakati akihutubia katika uzinduzi huo wa Dawati la Jinsia Ulio fanyika katika Uwanja Wa Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla mwenye Suti ya Bluu akikata Utepe kuashiria kuwa Kituo Hicho Kimeanza kufanya kazi rasmi na Hakita munea huruma yoyote Atakae husika na kubainika ni miongoni mwa waalifu wanao fanya Vitendo vya Kikatili kwa Watoto Ikiwemo Ubakaji na Kulawiti watoto Jeshi La Polisi kupitia Dawati la Jinsia Litawashughulikia Vilivyo Waalifu na kuwafikisha kwenye Vyombo Vya Sheria.
 Baadhi ya wadau wa Dawati la Jinsia wakiburudika kwa pamoja katika Uzinduzi huo Wa Dawati la Jinsia Ulio Fanyika Uwanja wa Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 30/09/2016

SUZA admitted candidates for 2016/2017 academic year

BRITISH COUNCIL WAZINDUA UTAFITI WA SAUTI ZA VIJANA JIJINI ARUSHA

0
0
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini,kulia ni Meneja Mradi wa British Council Tanzania Bi. Elizabeth Nkanda. 
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini. 
Mtaalamu wa sera za ufugaji Bi. Carolyn Kandusi akiongoza shughuli nzima iliyofanyika jijini Arusha. 
Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana. 

KC GLOBAL LINKS LTD CARGO UPDATES..!

0
0

Cargo No 1001 to Dar has been dispatched to the airport and will arrive Dar es salaam on Tuesday 04/10/2016 and will be ready for collection on Wednesday 05/10/2016.


Customers are adviced to contact our agent in Dar es salaam , MSS LOGISTICS who are based at Raha Tower, second floor, Bibi Titi Road
QUALITY IS OUR MAIN TARGET.



HAPA NI KAZI TU...!
CONTACT US ON;


KC GLOBAL LINKS LTD
SUITE 2 CLIPPER HOUSE, TILBURY DOCKS, RM18 7SG

Rais Magufuli afunga Maadhimisho ya Miaka 52 ya JWTZ ashuhudia Zoezi la Amphibious Landing Bagamoyo

0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo. Mkoani Pwani.
Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano za JWTZ  ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na  Jeshi la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi kavu kutoka majini na kukomboa eneo lililotekwa.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa hali ya juu.
''Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika''amesema Dkt. Magufuli.  
Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi la kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza  JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi  wa Jeshi hilo.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya Mzee.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam.
30 Septemba, 2016
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati  wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
 Vifaru vinavyopita baharini na nchi kavu vikiwa katika zoezi la "Ambhibious Landing" katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016. PICHA NA IKULU.

JOZI LOUNGE YADHAMINI MISS TANZANIA 2016

0
0
Club maarufu kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jijini Dar Es Salaam, imejitokeza hivi karibuni kujiunga na moja katika kampuni na taasisi zilizokwisha kujitokeza kudhamini zoezi zima la kutafuta mrembo wa tanzania atakayepeperusha na kuitangaza Tanzania katika anga za kimataifa katika Nyanja mbalimbali yakiwemo utalii na huduma ya jamii yenye mahitaji maalum.

Akizungumza na warembo kutoka mikoa yote Tanzania ambao wanatarajia kuchuana vikali mwishoni mwa mwezi wa kumi huko jijini Mwanza na hatimaye kumpata mshindi wa Miss Tanzania 2016, Mkurugenzi wa Jozi Lounge Bw.Dismas Massawe amesema Jozi Lounge itawadhamini warembo hao kwa kuwapatia malazi, chakula na mahitaji mengine muhimu kwa kipindi cha siku tatu ambapo jana ilikuwa uzinduzi na leo ni siku ya semina mbalimbali na siku ya jumapili itakuwa siku ya kusherehekea ushindi wa mikoa tayari kuelekea katika mapambano ya ngazi ya Taifa.

Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika moja ya pozi jana mara baada ya kuwasili Jozi Lounge, ambapo watakuwa hapo kwa siku tatu mfululizo. Jozi lounge ni mojawapo wa wadhamini wa mashindano ya miss tanzania mwaka huu 2016
 Wakipata vinywaji kwa pamoja huku wakifurahia utulivu mwanana ndani ya Jozi Club
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016,ambapo jana wameingia kambini pia walipata muda wa kuserebuka ndani ya Club maarufu kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jiji Dar EsSalaam. 
 Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakiserubuka ndani ya Jozi Club kwa raha zao



MASAUNI AZITAKA TAASISI ZA KIDINI NCHINI KUPAMBANA NA MAOVU, AFUNGUA MKUTANO WA 47 WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA.

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya katika Mkutano wa 47 wa jumuiya hiyo nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokea zawadi ya vitabu vya dini kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry wakati Naibu Waziri huyo alipomaliza kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo wa 47 unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 47 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

WAFANYAKAZI WA MANISPAA YA UBUNGO WAUNGANA KUPANDA MITI KATIKA MANISPAA YAO JIJINI DAR LEO.

0
0
Kaimu Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo, Joseph Alute akipanda mti katika kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kupanda miti kwaajili ya kutunza mazingira pamoja na kupendezesha mazingira ya jiji.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dkt. Sivila Mwanisi akishirikiana na mfanyakazi wa manispaa ya Ubungo Kupanda miti ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam za kupanda miti  jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari wakipanda mti jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Yasir Adam.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images