Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1372 | 1373 | (Page 1374) | 1375 | 1376 | .... | 3270 | newer

  0 0


  Tanzania imekubali kuyatekeleza mapendekezo 131, kuyakataa 94, kuyakubali kiasi mawili kati ya mapendekezo 227 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Taarifa ya Serikali iliwasilishwa mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Profesa  Sifuni Mchome (pichani) lililokaa September 21 hadi 23, 2016.
  Aidha, Baraza hilo limepitisha Taarifa hiyo ya pili ya Tanzania ya Haki za Binadamu chini ya Mfumo wa Mapitio wa Umoja wa Mataifa kwa Kipindi Maalum (Universal Periodic Review (UPR) Mechanism) katika kikao kilichofanyika mjini Geneva nchini Uswisi.
  Mapendekezo ambayo Tanzania imeyakubali yanahusu; ukamilishaji wa Mchakato wa Katiba, kuijengea uwezo wa kifedha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kutekeleza Malengo endelevu ya Dunia, Uandaaji wa Taarifa za Nchi za Utekelezaji wa Masuala ya Haki za Binadamu, Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Haki za Binadamu, haki za wanawake na watoto, watu wenye ulemavu, wazee, haki ya elimu, afya, maji, mazingira na mengineyo.
  Aidha, Mapendekezo mawili  ambayo yalikubaliwa nusu yalikuwa na baadhi ya mambo ambayo yanaendana na Katiba, Sera na Sheria za nchi na mambo mengine ambayo yanakinzana na hayo. Masuala hayo yanahusu Serikali kuziwezesha Asasi za Kiraia kimuundo na kifedha na kutoa fidia kwa wahanga wanaotokana na mashambulizi yanayofanywa kwa watu wenye ualbino.
  Mapendekezo ambayo Tanzania imeyakataa yanahusu suala la hali ya kisiasa Zanzibar, Sheria ya Makosa ya Mtandaoni, uhuru wa kupata taarifa , adhabu ya kifo, utoaji mimba, mapenzi na ndoa za jinsia moja, ubakaji ndani ya ndoa na umiliki wa ardhi kwa kuwa yanakwenda kinyume na Katiba, Sheria, Sera, Dini na Tamaduni za nchi kwa ujumla.
  Akiwasilisha taarifa hiyo ya Serikali, Prof Mchome amesema Serikali imejidhatiti kutekeleza mapendekezo yote yaliyokubaliwa na kuongeza kuwa Tanzania inaunga mkono Azimio la Vienna na kwamba itaendelea kutekeleza mpango wa Taifa wa Haki za Binadamu.
  “Tumejidhatiti kutekeleza mapendekezo tuliyoyakubali na tutaendelea kuimarisha taasisi ya Taifa ya Haki za Binadamu kwa kuipatia rasilimali fedha, watu na vifaa ili ifanye kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa mtindo wa haki za binadamu,” alisema.
  Pia alisema kuwa kuna baadhi ya mapendekezo ambayo Serikali imeyachukua kwa ajili ya kuyafanyia kazi. Mapendekezo hayo ni pamoja na haki za watu wenye ualbino, adhabu ya viboko na haki ya mtoto kuandikishwa bure baada ya kuzaliwa ili apatiwe cheti cha kuzaliwa.
  Profesa Mchome alisema Serikali imepokea mapendekezo matatu kuhusu haki za watu wenye ualbino ambayo yanataka Serikali kuifanyia mabadiliko Sheria ya Dawa na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 ili kuwazuia waganga kutowadhuru watu wenye ualbino na kuahidi kuwa wataipitia upya.

  Alisema kuwa Serikali imepokea na kukubali sehemu ya pendekezo la kuzisaidia kifedha na kimuundo asasi zinazojishughulisha na masuala ya watu wenye ualbino. “Tumepokea na kukubali sehemu ya pendekezo hilo ambalo linaitaka Serikali kuzisaidia kifedha na kimuundo asasi zinazojishughulisha na masuala ya watu wenye ualbino,” alisema.

  0 0

  SIMU.TV: Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ametoa wito kwa viongozi nchini kuwatumikia wananchi wao na kuacha kutumia madaraka kujinufaisha wenyewe;https://youtu.be/OSvATdFGIQA

  SIMU.TV: Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako, ameitaka tume ya vyuo vikuu nchini TCU kuvifuatilia na kufahamu sifa za vyuo nchini na sio kugeuka kuwa madalali wa vyuo;https://youtu.be/c0nGuZfHo58

  SIMU.TV: Wakazi wa baadhi ya vijiji wilayani Newala mkoani Mtwara, wameelezea furaha yao ya kumalizika kwa kero ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji safi na salama;https://youtu.be/Tvm2n58KyuQ

  SIMU.TV: Waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage, amewataka wanawake wajasiriamali kuwa na uthubutu mkubwa wa kufanya biashara kubwa kubwa;https://youtu.be/oKmk1YFTog4

  SIMU.TV: Kaimu kamishina wa uchambuzi wa masuala ya fedha wa wizara ya fedha Augustini Ollao, amesema mashindano ya fedha na mikopo nchini yanasaidia kuimarisha sekta ya uchumi; https://youtu.be/UXO-DrUEoAw

  SIMU.TV: Maonyesho ya 98 ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidigo yanatarajia kuanza kesho mkoani Mbeya ili kutoa fursa kwa wenye wajasiriamali wadogo kujifunza;https://youtu.be/WVH3vZiYLIk

  SIMU.TV: Tiketi za kielekitroniki kwa ajili ya mchezo wa Yanga na Simba tayari zimeanza kuuzwa ili kuondoa usumbufu kwa wateja ambao wengi ni wageni wa mfumo huu;https://youtu.be/_FuLusb4tko
  SIMU.TV: Timu zinazoshiriki ligi daraja la nne mkoa wa kisoka wa Kinondoni zimetakiwa kuonyesha kandanda maridadi ili kuweza kuwavutia mashabiki wao;https://youtu.be/gcoYh5aVcj4

  SIMU.TV: Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umeanzisha mashindano ya michezo kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo ili kuweza kuwa na mahusiano mazuri na kupunguza migogoro na wananchi; https://youtu.be/TlzPUnKflRY

  SIMU.TV: Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Mauritius anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa tuhuma za kukutwa na kete kadhaa za madawa ya kulevya;https://youtu.be/YPWuEealrMY

  0 0

  Na PMO
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi. 
   Amesema mtumishi yeyote aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo. 
   "Tayari nimemuagiza ndugu Zuberi Samatabu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo waishi Kibiti na si Ikwiriri," amesema. 
   Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ilifuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri Mkuu kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya 74 waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo wameripoti katika kituo cha kazi 
   Ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi. 
   Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Septemba 28, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo,utendaji wa serikali na kutoa msimamo wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku 
   Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka madiwani wa halmashauri hiyo wawe wakali katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kuomba omba kwa wakuu wa idara ili kuepuka kujishushia hadhi zao na kupelekea kuhujumiwa kwa miradi mbalimbali ya jamii Aidha aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kutengeneza mazingira ya kukaribisha wawekezaji na wahakikishe kwamba uwekezaji utakaofanyika hausababishi migogoro ya ardhi kwa wananchi. 
   Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa maana Serikali imebeba mzigo wote wa gharama za ada na uendeshaji wa shule hizo. 
  Alisisitiza kuwa njia pekee na ya haraka kuondoa umaskini ni kusomesha watoto Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameagiza halmashauri zote nchini kutumia mfumo wa kieletroniki katika ukasanyaji wa mapoto ili kuziba mianya ya uvujaji mapato haswa ya maliasili
   Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia Septemba 28, 2016 licha ya mvua kubwa iliyonyesha
   Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia leo Septemba 28, 2016 licha ya mvua kubwa iliyonyesha
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika  Mji wa  Kibiti akiwa katika ziara yake wilayani humo.

  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kampuni ya China Electronics Corporation ya kutoka nchini China, Ikulu jijini Dar es Salaam
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka kampuni ya China Electronics Corporation ya kutoka nchini China, Ikulu jijini Dar es Salaam 
   BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kwenye ndege mojawapo na kuelekea ingine baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  0 0


  0 0

   Moja ya kadi za kieletroniki.
  Mashabiki wa Mpira wakiwa wamepanga foleni ya kwenda kukata tiketi za kieletroniki jijini Dar es Salaam leo.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  MFUMO mpya wa kadi za kieletroniki umeonekana kupokelewa kwa mwitikio mkubwa sana na wananchi wengi kujitokeza kupata kadi zitakazowawezesha kukata tiketi kwa njia ya kuingia uwanjani kuangalia mpira.

  Katika maeneo mbalimbali kadi hizo zimekuwa zikitolewa kwa shilingi 1000 hadi 3000 zimekuwa chachu ya serikali kupata mapato halisi tofauti na ulivyokuwa mfumo wa tiketi za kawaida na utatakiwa kuisajili kwa jina lako la kwenye kitambulisho cha kupigia kura sambamba na namba ya simu unayoitumia na utatakiwa kujaza fedha na kulipia kulingana na sehemu unayotaka kwenda kukaa.

  Mfumo huo rasmi unaanza kutumika Oktoba 01 kwenye mchezo baina ya Yanga na Simba na utamlazimu mwananchi au shabiki anayetaka kushuhudia mchezo huo kuwa na kadi maalumu atakayotumia kuingilia mlangoni na kumuonyesha ni mahala gani anatakiwa kwenda kukaa

  Kuja kwa mfumo huo timu mbalimbali zitaacha kulalamika kuhusiana na tiketi feki zilizokuwa zinauzwa na watu wasiojulikana na kuhujumu mapato ya timu zao.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Iringa, Rose Tweve amekutana na wakinamama wa wilaya ya Mafinga na kuwataka kuhakikisha wanajiingiza katika vikundi vya ujasiriamali, katika mkutano huo amewataka wakinamama hao kuacha kujibweteka na kusubiri kuletewa na wanaume zao bali wanatakiwa kujishughulisha ili kujiongezea kipato.

  Mbali na hilo amewaasa wanawake na kuhakikisha wanakuwa macho na masikio kwenye jamii zao juu ya ubakaji Wa watoto na wawe wanatoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

  Baada ya kumalizika kwa mkutano huo Mbunge huyo wa viti maalumu aliweza kuzungumza na wakinamama mbalimbali na kuweza kujua changamoto wanazokutana nazo na kuwataka wajitume kuweza kuepukana na utegemezi.
   Mbunge wa Viti Maalumu Iringa akibadilishana mawazo na moja ya akina mama wa Wilaya ya Mafinga wakati wa mkutano wake akiwataka kujiunga na vikundi vya ujasirimali.
                                        
  Mbunge wa Viti Maalumu Rose Tweve akiwa anazungumza na wakinamama wa Wilaya ya Mafinga na kuwaasa kujiunga na vikundi vya Ujasiriamali pamoja na kuwapatia mbinu za kujiondoa kwenye utegemezi         


   Mbunge wa Viti Maalumu Iringa, Rose Tweve akiwa katika picha ya pamoja na wakina mama wa Wilaya Mafinga Mkoani  Iringa.      0 0

  Mashabiki wa Timu ya Yanga na Simba wakizungumza na Michuzi Tv leo katika Soko la Buguruni jijini Dar es Salaam kuhusu mchezo wa Jumamosi utakaofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Shabiki wa timu ya Yanga,Ayubu Nampea akizungumza na Michuzi Tv kuhusu mchezo wa yanga na simba utakaofanyika jumamosi hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Shabiki wa timu ya Simba, Ramadhan Machenje akizungumza na Michuzi Tv kuhusu mchezo wa Yanga na Simba utakaochezwa jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kitua Sheria na Haki Binadamu, Dk.Hellen Kijo Bisimba akizummza na waandishi wa habari leo katika mdahalo wa kupinga ndoa za utotoni iliyoandaliwa na Shirika la Serikali C-SEMA iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Picha ya pamoja ya wadau wa kutetea haki za watoto.

  Na Chalila Kibuda, Globu Jamii.
  WADAU wa kutetea haki za watoto wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya ndoa mwaka 1971 ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa miaka 14 kwa idhini ya wazazi kutokana na sheria hiyo kupitwa na wakati na kufanya mtoto wa kike kukosa haki msingi ya kupata elimu ambayo ndio inaweza kubadlisha maisha mtoto na taifa likapata maendeleo.

  Wadau hao wameyasema leo katika mdahalo wa kutetea kwa kuondokana na ndoa za utotoni  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Serikali la C-SEMA iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, wamesema kuwa ndoa za utotoni zimefanya watoto wa kike kukosa elimu pamoja na kupoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana viungo vyao kukosa utayari kubeba uzauzito.

  Akizungumza katika mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa ndoa za utotoni sasa ifike mwisho ili kuwapa watoto wakike kufurahi maisha yao ya kupata na waweze kuleta mchango katika taifa.

  Amesema kuwa watoto wa kike wamekuwa wakiolewa  wanaume ambao hawawafahamu ambapo inamfanya mtoto wa kike kuwa na kidonda maisha yake ya duniani kuolewa na mtu asiyemjua hivyo wakati umefika wa kuondokana na ndoa  za utotoni ili kuweza kuwapa furaha ya maisha ya watoto wa kike.

  Katika mdahalo huo mtoto  X  mkoani... ameeleza kuwa wazazi wake walichukua mahali kwa mwanaume ambaye hamujui lakini aliweza kutoroka ili asiolewe siku moja kabla harusi na kuweza kuhifadhiwa na taasisi na kuweza kuendelea na masomo ya elimu ya watu kuanza kidato cha kwanza.

  Mtoto X ametaka wadau wasaidie katika kuwasaidia watoto wa kike katika ndoa za utotoni kwani mateso makubwa wanayapata na wakati mwingine wanakuwa wanaolewa watu wasio wajua na wenye umri mkubwa kuanzia mika 50.

  Aidha mtoto X  ametaka sheria ya mwaka 1971imekuwa ndio kimbilio ya wazazi kuozesha watoto katika umri mdogo na kufanya watoto wa kike kushindwa kufurahia maisha pamoja kukosa elimu ikiwa ni silaha ya mtoto wa kike.

  Naw Mratibu wa C-sema, Michael Kehongoh amesema kuwa kampeni ya kumtetea mtoto wa  kike ni endelevu hivyo kunahitaji sauti moja ya katika kuokoa watoto hao.

  0 0

  Kanisa la EAGT Posta “B” Mabatini Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Lameck Nkumba, linawakaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika katika viwanja vya kanisa hilo vinavyotizamana na geti la polisi Mabatini nyuma ya iliyokuwa Orange Tree Hotel.

  Mhubiri wa kitaifa na kimataifa ambaye amehubiri mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, Canada, Uingereza, Ireland, Wales , Scotland, Ujerumani, Dernmark, Swirtzland, Afrika Kusini, DRC Congo na mengine mengi, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), atahudumu kwenye mkutano huo akishirikiana na wahubiri wengine.

  Ni wiki moja yenye miujiza na uponyaji wa nguvu ya Mungu, kuanzia jumapili tarehe 9.10.2016 hadi jumapili tarehe 16.10. 2016 muda ni kuanzia saa 9.00 mchana hadi saa 12 jioni, kila siku.

  Waimbaji mbalimbali akiwemo Mwanyamaki kutoka Morogoro, Emannuel Mgogo kutoka Dar es salaam pamoja na kwaya zinatotamba Jijii Mwanza kama vile Havillah Gospel Singers kutoka EAGT Lumala Mpya, na kwaya ya EAGT Posta “B” zitahudumu kwenye mkutano huo.

  Ewe baba, mama, kaka, dada, ndugu, jamaa na marafiki, fika kwenye mkutano huo ili ukutane na nguvu ya Mungu ambapo wagonjwa mbalimbali, wenye mapepo, mikosi na waliofungwa na vifungo vya ibirisi watafunguliwa kwa jina la Yesu, bila malipo.
  Kwa msaada wa Kiroho, piga simu nambari 0784 43 77 82 
  Bonyeza HAPA Kusikiliza, Au Bonyeza Play hapo chini.

  0 0

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

  TAREHE: Jumamosi 01 Oktoba, 2016
  MUDA: 02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni
  SABABU: Kujenga laini mpya ya Mburahati na ukarabati wa laini za Tandale Textile ili kuboresha hali ya umeme.

  MAENEO YATAKAYOATHIRIKA: 
  Maeneo yote ya Tandale, Manzese, Sinza Uwanja wa TP, Sinza Vatican, Namnani Hotel, Iteba, Sinza Kijiweni, Sinza Kumekucha, Sinza Mwika, TTCL Manzese , Urafiki Quarters, Urafiki Textile,TSP Ltd Millenium business, Sinza Lion Hotel, Rombo Sunflower, Strabag compound, Engen petrol station, Masamaki Plastic Bags Ltd pamoja na maeneo ya jirani.


  TAREHE: Jumapili 2 Octoba, 2016
  MUDA: 02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni 
  SABABU: Matengenezo kwenye Kituo cha Kupozea Umeme Ubungo 33kv ili kuboresha hali ya umeme.

  MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
  Parts of Mandela road, I ndustrial area near Mandela road, Ubungo NBC, Tbs Ubungo, Ubungo Bus Terminal, Parts of Sinza, Part of Kimara, Baruti,Kimara Kimara Korogwe,Kimara Mwisho, Kimara Matangini, Kimara Mavurunza, Ubungo Maziwa, TTCL Ubungo Kisiwani, Mabibo,TGNP Mabibo, Mabibo Hostel, Mabibo Jeshini, Mabibo, Makabe, Mpigi Magohe, Goba,Kimara King’ong’o, Tegeta A,Mavurunza, Suka, Stopover, Changanyikeni, Makongo Mwisho pamoja na maeneo ya jirani.

  Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo Magomeni 0222171759/66, 0784/0715271461, Kimara Ofisi ya Wilaya 0717/0788379696, Au Kituo cha miito ya simu 2194400 Au 0768 985100.

  Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
  Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano, TANESCO Makao Makuu..

  0 0
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wakala uuzaji wa mafuta kwa pamoja, Bw. Michael Mnjinja akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na uuzaji  wa mafuta hapa nchini

  Na Yassir Adam, Globu ya Jamii.
  WAKALA wa uuzaji wa mafuta  kwa pamoja  na Petroleum Bulk Procurement Agency imedhamiria kuhakikisha bei ya mafuta nchini inashuka kwa kiwango kikubwa hasa baada ya kuanzisha utaratibu mpya wa kuwa na zabuni kwa kila meli inayoleta mafuta nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha utaratibu mpya wa zabuni,  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wakala uuzaji wa mafuta kwa pamoja, Bw. Michael Mnjinja amesema kuwa kwa sasa kila meli itakuwa na zabuni yake na mpaka sasa wameshapata meli sita tofauti kwa mafuta ya dizeli mbili, petrol tatuna mafuta ya ndege pamoja na ya taa meli moja.
  Mnjinja amesema kuwa mpaka sasa wameweza kupata premium ya bei ya chini kwa dola 18 na dola 14 ambapo kutokana kwa kushuka kwa bei hiyo kunaleta unafuu katika kupanga bei za mafuta nchini na yatashuka bei tofauti na mwanzo waliweza kupata premium kwa dola 19.

  Ameyataka makampuni ya ndani na nje ya nchi kujitokeza kuja kujisajili kwani kwa mwaka huu wameweza kupata kampuni moja tu kutoka nchini ila hawataweza kuruhusu tena makampuni kutoka nje kuwania zabuni za uuzaji wa mafuta, na mabli na hilo zabuni hizo zitakuwa znafanyika kila mwezi.
  Baadhi ya wadau wa mafuta wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  0 0


  Akiongea na mtandao huu kwa niaba ya Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamni wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bi. Nandi Mwiyombella (pichani), amesema wakiwa kama wadhamini wakuu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara,Wanazitakia kila la kheri timu ya Yanga na Simba katika mzunguko wa kwanza kwa timu hizi kubwa hapa nyumbani zitakazomenyana siku ya jumamosi ya tarehe 1 mwezi Oktoba katika uwanja wa Taifa jijini Da res Salaam. 

  "Naamini kwamba mchezo huo utakuwa mzuri na wakuburudisha washabiki wote wa timu hizi watakaofika uwanjani kuushuhudia kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangia msimu huu kuanza.
  "Pia napenda kuwatoa wasiwasi wapenzi wa mchezo huu ambao hawatapata na nafasi ya kufika uwanjani kwani Vodacom Tanzania haitawaacha mbali na matokeo yatakayokuwa yakiendelea uwanjani hapo”LIVE” ili kupata matokeo ya mchezo huo ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi cha ‘Soka bando’ na utakuwa unapata frusa ya kupata matokeo kiurahisi kabisa popote pale ulipo ya timu yako uipendayo kati ya Simba na Yanga.
  Kifurushi hiki ni chenye gharama nafuu ya shilingi 500/- tu na ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote kwani kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa masaa 24. 
  Ili kununua kifurushi hiki unachotakiwa kufanya mteja ni kupiga namba *149 * 01#,  chagua "Ofa mpya" halafu chagua ‘Soka Bando’. Baada ya hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga” “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya Mspoti.vodacom.co.tz.

  0 0

  Meneja wa Taasisi inayopiga vita maambukizi dhidi ya maradhi ya ukimwi  Tanzania (TPHS) Frida Godfrey akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Malik Juma Akili msaada wa vifaa vya kutendea kazi kwa ajili ya matumizi  ya wadau wa afya kwa lengo la kuongeza ufanisi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya akitoa shukrani kwa Taasisi ya TPHS baada ya kupokea msaada wa komputa, Printer na UPS katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
  Na Miza Kona/Mwanaisha Mohamed
                                                           Maelezo Zanzibar                                                                                 
  Taasisi inayopiga vita maambukizi dhidi ya maradhi ya ukimwi Tanzania (TPHS) imeikabidhi Wizara ya Afya  msaada wa vifaa vya kutendea kazi kwa ajili ya matumizi  ya wadau wa afya kwa lengo la kuongeza ufanisi.
  Vifaa vilivyokabidhiwa vikiwa na  thamani ya sh. milioni 27,820,000 ni pamoja na komputa 10, Printer saba  na UPS.
  Akikabidhi msaada huo Meneja wa Taasisi hiyo Frida Godfrey Radegunda katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, amesema lengo  ni kuimarisha vitendea kazi  katika kutoa huduma bora za Afya kwa jamii.
  Amesema Taasisi hiyo kwa kushirikana  na Wizara ya Afya itaendelea kutoa  huduma na kuwawezesha wananchi kuelewa njia za  kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na maambukizi ya ukimwi
  “Taasisi yetu inashirikiana na wizara ya Afya kupambana na madawa ya kulevya katika vituo vya afya na kutoa elimu ya ukimwi na madhara ya kujidunga sindano, ” amefahamisha Meneja huyo.
  Aidha amewataka wadau wa Afya kuvitumia vyema vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu ili kufikia lengo lililokusudiwa la kutoa huduma  bora kwa wananchi.
  Katibu Mkuu Wizara ya  Afya Dkt Malik Juma Akili ameishukuru Taassisi ya TPHS kwa msaada huo pamoja na  kuisaidia kutoa elimu kwa jamii dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
  Amesema vijana wengi wanaathirika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya na kupelekea kuwepo kwa wimbi kubwa la maambukizi ya ukimwi kwa kujidunga sindano ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
  “Vijana wasikilize yale wanayoelekezwa kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na maambukizi kiwango cha maambukizi ni kikubwa Unguja ni asilimia 1.2 na Pemba ni 0.3 tusjiachie tujitahidi katika kupunguza,” alisisitiza Dkt. Malik.
  Katibu Mkuu  ameishukuru Taasisis hiyo kwa kufanikiwa kuifanyia matengezo Maabara kuu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa lengo la kuboresha  huduma kwa jamii pamoja na kukisaidia kituo cha huduma ya kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya  kupata nafuu (Methodone Clinic).
  Mapema Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad amesema kitengo cha Mfamasia Mkuu kilikuwa na upungufu  wa vitendea kazi lakini  msaada huo utasaidia  kutoa huduma  kwa ufanisi zaidi.
  Vifaa hivyo vimekabidhiwa Tume ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Bohari Kuu ya dawa pamoja na Hospitali ya Mnazi Mmoja.

  0 0


  0 0


  0 0


  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Lindi aagiza kutatuliwa kwa changamoto kadhaa zinazoikabili hospitali ya rufaa ya Sokoine mkoani Lindi. https://youtu.be/1n6iKnNlHFU

  SIMU.TV: Wakazi wa kata ya Kibirizi katika manispaa ya Kigoma Ujiji waiomba serikali kumuondoa mwekezaji katika bwawa la Katosho ili kuondoa migogoro iliopo.https://youtu.be/1I6LQZvdG7k

  SIMU.TV: Wananchi wa kata ya Kasamwa katika halmashauri ya Geita walalamikia usafishaji wa bwawa la Kasamwa kuwa wa kutoridhisha. https://youtu.be/PBIrkmlifbw

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa apokea michango mbalimbali kutoka kwa taasisi na makampuni binafsi kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa ya tetemeko la ardhi.https://youtu.be/X3VX7IPEbgE

  SIMU.TV: Vijana nchini watakiwa kujiunga na vyuo vya ufundi ili kuweza kunufaika na fursa za ajira zitakazotolewa na wawekezaji hapa nchini. https://youtu.be/wcJamqmiPiU

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam atoa wito kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza katika zoezi la kupanda miti siku ya Oktoba mosi.https://youtu.be/-MkLpg4kBms

  SIMU.TV: Walaji wa bidhaa watakiwa kukataa kutumia bidhaa zenye viwango hafifu ili kuweza kufanikisha vita dhidi ya bidhaa duni nchini. https://youtu.be/ZCTSRyCnIiY
  SIMU.TV: Taasisi ya REPOA yatoa utafiti wake kuhusu uratibu usiokamilika na madhara yake katika uzalishaji wa miwa nchini. https://youtu.be/CpiN9oHlHnU

  SIMU.TV: Pato la taifa katika robo ya pili ya mwaka 2016 limeendelea kuongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa na asilimia 5.8 kwa mwaka 2015. https://youtu.be/Jx-9vj3SBno

  SIMU.TV: Wakala wa uingizwaji wa mafuta kwa pamoja nchini  waanza utaratibu mpya wa uingizaji wa mafuta hapa nchini ili kupunguza gharama za mafuta nchini.https://youtu.be/vsirW4PLasE

  SIMU.TV: Zaidi ya wasanii tisa wa vichekesho kutoka Tanzania na Kenya kesho wanatarajia kuvunja mbavu za wakazi wa jiji la Mwanza katika ukumbi wa Rock city Mall.https://youtu.be/O5ra14wu8Moolder | 1 | .... | 1372 | 1373 | (Page 1374) | 1375 | 1376 | .... | 3270 | newer