Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1371 | 1372 | (Page 1373) | 1374 | 1375 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
  “Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
  Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja  zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
  Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali  ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
  Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali  ikiegeshwa karibu na pacha wake iliyofika wiki moja uliopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho  akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi (kushoto kwake) pamoja na maafisa wengine kutoka taasisi mbalimbali za serikali wakiwa katika Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali  mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ili fedha hizo zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akipokea msaada wa majokofu sita kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Majembe Auction Mart Ltd, Sethi Moto. Majokofu hayo yatatumika kuhifadhi dawa katika wodi namba 16 Kibasila. Kulia ni Meneja wa Jengo la Kibasila, Sister Leonarda Lodovick. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).


  0 0


  0 0

  Serikali ya Uingereza inatarajia kutoa takribani TZS 6.3 bilioni (sawa na Paundi 2.23 milioni) kusaidia ukarabati wa shule baada ya athari za tetemeko la ardhi mkoani Kagera mnamo Septemba 10.
  Msaada huu wa ziada umetangazwa mapema leo wakati Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke alipokuwa akikabidhi hati ya kibalozi kwa Mheshimiwa Rais wa Magufuli.
  Hii ikifuatiwa na ziara iliyofanywa na Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiambatana na Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo ya Uingereza (DFID), Ndugu Vel Gnanendran.
  Misaada hii itatumika katika kukarabati, kuboresha na kuwezesha Shule ya Sekondari ya Ihungo kuwawezesha zaidi ya wanafunzi 740 kuendelea na masomo yao mapema iwezekanavyo. Kwa kuongezea, Serikali ya Uingereza itasaidia pia kukarabati nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa ambazo zilianguka. Shule hizi ndizo ambazo zimeathiriwa zaidi katika tetemeko la ardhi.
  Balozi Mpya, Sarah Cooke alisema; “Serikali ya Uingereza inapenda kutoa salamu zake za masikitiko kwa wale wote ambao wameathirika na tetemeko la ardhi Kagera. Tunaona ni muhimu sana kusaidia Wizara ya Elimu mapema iwezekanavyo ili kuwawezesha watoto wa Bukoba wasiendelee kuangaika zaidi na kuweza kuendelea na masomo yao ndani ya muda mfupi iwezekanavyo.
  Hivyo basi, tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uingereza itatoa msaada wa ziada kusaidia elimu iendelee kutolewa hasa katika kipindi hiki cha athari za tetemeko Bukoba” Serikali ya Uingereza itadumu imara katika kutoa ushirikiano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kuboresha elimu kwa watoto wote wa Tanzania.

  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupoka msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 kutoka Idara ya Maendeleo ya Nje ya nchini Uingereza (DFID) ikiwa ni sehemu ya kusaidia Shule zilizoathirika na tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini, Vel Gnanendran.
  Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini, Vel Gnanendran akizungumza na waandishi wa habari juu ya Serikali ya Uingereza kutoa msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 wenye lengo la kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi hususan kwa shule zilizoathiriwa na tetemeko hilo. kulia ni Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  0 0

   Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule Direct kwa wanafunzu wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo, amewaasa wa wanafunzi kusoma kwa kutumia mtandao wa www.shule.co.tz kwaajili ya kujifunza zaidi masomo yao na si kutembelea mitandao mingine ambayo haihusiana na masomo yao.
  Pia amewaasa kujiwekea akiba zao kupitia akaunti ya Chupukizi ya NMB kwa pesa kidogokidogo wanazopewa na wazazi wao ili ziwafaidisha baadae na si kutumia pesa hovyo.

   Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu akizungumza wakati wa kuzindua Shule Direct ambapo wanafunzi watatembelea mtandao wa www.shuledirect.co.tz kwaajili ya kujifunzia masomo mbalimbali ambapo wanafunzi watatembelea mtandao huo  kwaajili ya kujifunza masomo mbalimbali. 
   Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,  Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua programu ya Shule Direct katika shule hiyo.

  0 0

  Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu ya Yanga pamoja na kituo maalumu cha Kukuza vipaji vya michezo.
   Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Fatuma Karume wakati wa uzinduzi wa eneo la Uwanja lenye zaidi ya ekari 700 Geza Ulole lililopewa jina la Kijiji cha Yanga leo Jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Fatma Karume akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Kamati ya utendaji ya Yanga na wawakilishi kutoka kwa wadhamini wa timu hiyo Quality Group

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipatia klabu yake eneo la zaidi ya ekari 700  lilipo Geza Ulole, Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Kisasa.

  Akiwa amewakilishwa na wasaidizi wake  wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

  Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume akiwa ameambatana na  Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay, Sizya Lyimo na Kaimu katibu mkuu Baraka Deusdedit.

  Eneo hilo lililopewa jina la Kijiji cha Yanga, rasmi utafanyika ujenzi wa kijiji cha michezo cha yanga ambapo patakuwa na uwanja wa kisasa wa mazoezi, uwanja wa mechi, hosteli na kituo cha kukuza vipaji kwa vijana pamoja na Hospital na shule.

  0 0

  Mwibaji wa Nyimbo za Injili, John Lissu anatarajia kuzindua albamu yake ijulikanayo kwa jina la 'UKO HAPA' katika ukumbi wa CC Upanga jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mwimbaji Angel Bernard na Mercy Masika kutoka nchini Kenya. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

   Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwimbaji Lissu alisema kuwa maandalizi yameshakuwa tayari anawaomba Watanzania na wapenzi wa Muziki wa Injili kumuunga mkono ili kuhudhuria katika uzinduzi huo. Mwimbaji John Lissu aliongeza kuwa waimbaji wote wamefanya mazoezi ya kutosha hivyo mwenye shughuli ambaye ni (Yesu) anasubiri watu wakife siku hiyo ili aanze kazi yake. Waimbaji watakao msindikiza John Lisu ni Pastor Safari Paul, Cosmas Chidumule, Glorious Celebration, Bomby Johnson, The Voice na Next Level. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huwa Media, Bw. Jacob alisema kuwa kila kitu kimesha kamilika kuanzia vyombo vya Muziki, muonekano wa Ukumbi na pia alitoa rai kwa watu wote kuwahi kwani saa nane kamili shughuli nzima itaanza. Ni Tarehe 3/2/2012 katika ukumbi wa CCC Upanga kwa kiingilio cha sh 5000/=.Muda ni Saa nane (8) Mchana.
  Mwimbaji Mercy Masika kutoka nchini Kenya akiongea machache.
  Mwimbaji Angel Bernard akiongea machache.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke kufatia mchango wa Waziri Mkuu wa Uingereza alioutoa kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kiasi cha Paundi za Uingereza Milioni 2.3 sawa na Takribani Shilingi Bilioni sita za Kitanzania. PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0


  Katika hali isiyotarajiwa katika kijiji cha Maisha Plus, jana washiriki wawili, KAREKEZI Jean kutoka Rwanda na BASWARI Nibigira kutoka Burundi walipigana hadharani huku wakirekodiwa na camera zilizofungwa kijijini hapo. 
  Ilikua hivi;
  SOLANGE kawakuta KAREKEZI na PATRICK wamekaa wanapiga stori akawaambia kwamba BASWARI alikua anamsema KAREKEZI kwa watu. 
  KAREKEZI hakuonyesha kufurahishwa na ile hali, akapata hasira, PATRICK akachochea, akamwambia asikubali kudharauliwa, lazima akapigane. 
  "Muacheni, kwani nyie hamjui BASWARI anavyojifanya anajua kila kitu?" SOLANGE akahoji.
  PATRICK akaendelea kushauri kwamba KAREKEZI asikubali kuliacha liishie hapo.. Akampige BASWARI. 
  Baada ya kuona KAREKEZI anashawishika kwenda kupigana 
  SOLANGE akamzuia asiende ili isijulikane kwamba yeye ndio ameleta hizo taarifa. 
  KAREKEZI akiwa amekasirika akasema, "Mimi sipendi dharau... awe anawadharau nyie wanawake sio sisi wanaume." 
  PATRICK akazidi kuchochea.. 'Nenda kampige asituchukulie hivyo... Kwanini atuseme vibaya?'
  SOLANGE: "Usimdanganye mwenzio aende kupigana... Be gentle, men can't act like that... be gentle..''
  Baada ya kuona mambo hayataishia pale, SOLANGE akaomba wasiseme kama yeye ndio ameleta hayo maneno.
  KAREKEZI akamfuata BASWARI. Akamshika. BASWARI naye akamshika. Wakavutana. KAREKEZI akamwambia BASWARI, "Usiwe unaingilia maisha yangu, haunijui, wala sipendi unavyonisema kwa watu..." 
  KAREKEZI akamtukana BASWARI kwa kifaransa. 
  Ugomvi ukaendelea kwa muda.
  SOLANGE akakasirika akatoka eneo la tukio akaona kama amesalitiwa... "Kwanini umenifanyia hivi, watu wakijua mimi ndio nimesema hayo maneno nitakua na bad image kwenye society.."
  "Unaharibu reputation yetu kwa kugombana kijijni."
  BABU hapendagi Ujinga. Kuna kikao cha kijiji asubuhi hii. Mjadala mkali unaendelea juu ya hatima ya hawa washiriki. Tukutane Azam Two saa 3.30 usiku kujua kitakachojiri. 

  #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu

  0 0

   Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo Brazaville Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville.  Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini humo. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).

   Kutoa kushoto, Kibwana Shomari, Yohana Mkomola na Rashid Ada wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda.

   Wakiingia Hotelini.

   Serengeti Boys wakiingia Hotelini.
  Makocha wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed Sultan maarufu kama Shilton (kushoto) anayewanoa makipa, Kocha Mkuu Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi na Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini Brazzaville, Congo.


  0 0

  Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na wadau wa habari kwenye maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Haki za Kupata Taarifa Septemba 28 KATIKA ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameibuka washindi wa TUZO ya UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika hoteli yaa Sea Shells hapa Dar es Salaam.

  Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma.
  MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016.

  Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer akiwazungumza jambo na Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa baada ta tuzo ya Kufuli la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2016 lililokwenda kwenye Wizara ya Sheria na Katiba
  Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Makao, Gabriel Mwangosi baada ya kutwa tuzo ya TRA katika utoaji wa taarifa kwa umma. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.
   Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini wa SSRA, Ansgar Mushi akitoa mada katika warsha hiyo.
   Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0
  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limeendelea kufanya opresheni maalum ya kubaini wizi wa Maji kwenye maeneo ya jiji la Dar es salaam na kubaini baadhi ya majengo ya kata ya kariakoo yakiwa yamejiunganishia kinyume cha utaratibu.

  Akizungumza katika operesheni hiyo maalum, kiongozi wa operesheni kutoka ofisi ya Dawasco mkoa wa Ilala Bw. Gadimula Temba amesema kuwa wamebaini wizi wa Maji kwenye jengo linalomilikiwa na ndugu Mahsen Mohamed ambapo alikuwa amefungiwa laini ya Majisafi na amekuwa akidai hapati maji kila ifikapo kipindi cha kusoma mita licha ya mita yake kusoma nakuonyesha kuwa ana deni la shilingi laki tisa na ndipo walipokwenda mafundi kuchunguza nakubaini kuwa amejiunganishia laini tatu za majisafi pamoja nakufunga mota yakuvuta maji kwenye laini hizo zisizokuwa na mita.


  “leo tumebaini wizi wa Maji kwenye jengo la ndugu Mahsen Mohamed ambaye amekuwa akidai kuwa hapati Maji ya Dawasco kwa muda mrefu licha ya mita yake kusoma nakuonyesha anadaiwa kiasi cha shilingi laki tisa ndipo tukaamua kufanya uchunguzi nakubaini anatumia Maji yetu na pia amejiunganishia laini tatu za maji zisizokuwa na mita pamoja nakufunga mota yakuvuta maji.


  “Ila pia tumebaini kuwa amejiunganisha kwenye huduma ya mfumo wa Majitaka  kinyume cha utaratibu bila kibali kutoka Dawasco na amekuwa akikataa kuwa hatumi mfumo wetu” alisema Temba.

  Hata hivyo Dawasco imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kung’oa mota ya kuvuta majisafi, kufunga laini zote za majisafi na ya majitaka pamoja na kumtaka mmiliki wa jengo hilo kufika kwenye ofisi za Dawasco kwa taratibu zingine za kisheria.


  Nae afisa mtendaji wa kata ya Kariakoo Bw. Adeltus Kazinduki amewataka wamiliki wa majengo makubwa kariakoo kuachana na tabia ya wizi wa maji kwani ofisi yake kata inashirikiana na Dawasco mkoa wa Ilala kubaini watu wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika.


  “kwa kweli ofisi yangu ya kata ya kariakoo haitamvumilia mmliki yoyote ambaye anafanya wizi wa Maji kwasababu sisi na Dawasco tumekaa kikao cha pamoja nakukubaliana kuwa na ushirikiano hivyo mmiliki wa jengo lolote atakaye kamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheria” alisema Kazinduki.


  Hata hivyo mmiliki wa jengo hilo Bw. Mahsen Mohammed hakuweza kupatikana na hata wapangaji wa jengo hilo walidai hawajui makazi yake kwani ni mtu wa kusafiri mara kwa mara .  0 0

  WAJASIRIAMALI nchini wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho mbalimbali yanayoandaliwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),ili kuweza kuzitangaza bidhaa zao na kujifunza mbinu za kuboresha thamani bidhaa wanazozitengeneza.
  Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji, amesema maonyesho ya biashara kwa wajasiriamali yana umuhimu mkubwa kwani hutoa fursa ya kipekee kwa kujifunza na pia kutafuta masoko ya bidhaa.
  “Maonyesho  ya kikanda yanayoandaliwa na SIDO yanawaleta pamoja wajasiriamali wengi wakiwepo wale wanaotoka nchi za jirani ambao nao huja na bidhaa mbalimbali kuzionyesha na kuzinadi kwenye maonyesho,” Profesa Mpanduji alisema.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maonyesho ya Kanda ya Kusini ambayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho jijini Mbeya na kumalizika Oktoba 4, Profesa Mpanduji amewaka wajasiriamali kuchangamkia fursa za maonyesho hayo kuzitangaza bidhaa zao.
  “Zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 200 wamethibitisha kushiriki kwenye maonyesho hayo,” alisema na kuongeza kuwa SIDO kwa kushirikiana na wadau wengine imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazotengeneza na wajasiriamali wadogo zinakuwa na ubora unaostahili na kushindana kimataifa.
  Profesa Mpanduja alisema bidhaa mbalimbali za ngozi, kusindika na mikono zitakuwepo kwenye maonyesho na pia wajasiriamali kutoka nchini Kenya watashiriki.
  “Haya ni maonyesho ya 98 na SIDO inayapatia kipaumbele kikubwa kwani yanatoa fursa kwa wajasirialimali kujifunza mbinu na maarifa yakufanya biashara ikiwemo kupata masoko, mikopo na pia namna ya kuboresha bidhaa zao,” alisisitiza.
  Alizitaja baadhi ya Taasisi za fedha  kama benki za CRDB, NMB, Diamond Trust kuwa nazo zitashiriki kwenye maonyesho hayo ya kanda ya kusini ambayo inaundwa na mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe.
  “Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Dawa na Chakula (TDFA) pamoja na Mamlaka ya Biashara nchi (TAN-TRADE) watashiriki katika maonyesho hayo muhimu,” Profesa Mpanduji alisema.
  Profesa Mpanduji ametoa wito kwa wajasiriamali  kutoka katika kanda nyingine za jirani kujitokeza na kuchangamkia fursa za maonyesho hayo ya kipekee.
  “Ninapenda kupongeza mwamko mkubwa wa wajasiriamali na wanavyotengeneza bidhaa za kiwango cha juu,” alisema na kuongeza kuwa wakati umefika kwa watanzania kununua na kujivunia bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.

  Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji, akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana kuhusu maonesho ya wajasiriamali kwa kanda ya kusini yanayoanza Mkoani Mbeya kesho ambapo washiriki zaidi ya 200 wamethibitisha ushiriki wao.

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Viongozi na washirika wa maendeleo katika Sekta ya Elimu kuzijengea uwezo zaidi wa miundombinu skuli mbali mbali Nchini ili ziwe na uwezo kamili wa kuhimili ushindani wa kitaaluma uliopo katika kiwango cha Kitaifa na Kimataifa.
  Alisema wakati wa sasa ni ule wa sayansi uliobadilika kabisa Kiteknolojia tofauti na uliopita kiasi kwamba jamii inapaswa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira yanayokubalika kivifaa pamoja na walimu waliobobea.
  Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 13,078,000/- kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Kisasa la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Jimbo la Mahonda.
  Katika hafla hiyo fupi ambayo pia alikabidhi hundi ya shilingi Milioni  1.7 kukamilisha gharama za ujenzi wa Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni kwa msimamizi wake Nd. Yasir De Costa Balozi Seif aliahidi kutoa vifaa vyote vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari ya Kitope mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.
  Balozi Seif  alisema Zanzibar kama Nchi nyengine yoyote Duniani inahitaji kuwa na wataalamu wa kutosha katika kusimamia majukumu ya Serikali na hilo litawezekana na kupatikana iwapo watoto wa Taifa hili watajengewa msingi imara wa Taaluma wawapo maskulini.
  Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda alieleza kwamba Uongozi wa Jimbo hilo daima utakuwa kamini na imara katika kuhakikisha watoto wote wa Jimbo hilo wanapata elimu ya msingi hadi Sekondari kutegemea uwezo halisi wa mwanafunzi husika.
  Akitoa shukrani kwa niaba ya Walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Suleiman Juma Makame alisema msaada huo ni faraja kubwa itakayozaa mafanikio yanayotarajiwa kupatikana katika kipindi kifupi kijacho.
  Mwalimu Suleiman alisema Skuli  hiyo ilikuwa ikipata changamoto kubwa la kupoteza fedha zaidi ya shilingi Laki sita hadi Saba kufanya  maandalizi ya vifaa kwa ajili ya matayarisho ya mitihani ya wanafunzi wa Darasa la Kumi na Mbili    
  Kwa upande wake  Msimamizi wa ujenzi wa Majengo ya Maabara ya Skuli za Sekondari Fujoni na Kitope Ndugu Yasir De Costa alisema Jengo la Fujoni limeshakamilika ujenzi wake na tayari lina uwezo wa kutoa huduma ya Maabara kwa kiwango kinachokubalika.
  Nd. De Costa aliahidi kwamba ukamilishaji wa jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope unaotarajiwa wakati wowote kuanzia sasa utachukuwa takriban wiki Nne.
  Naye Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi Bibi Safia Ali Rijali  kwa niaba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  alimpongeza Balozi Seif Ali Iddi kwa jitihada anazochukua katika kusaidia sekta ya Elimu hasa Vikalio, Kompyuta pamoja na vifaa vya Maabara.
   Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini  “B”  Nd. Issa Juma kushoto yake wakikaguwa maendeleo ya ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Fujoni.
   Balozi Seif kati kati akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi kwa ajili ya kugharamia uendelezaji wa ujenzi wa jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope.
  Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wiaya ya Kaskazini B Nd. Issa Juma na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Safia Ali Rijali.
  Kulia ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Suleiman Juma Makame na Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa.
  Msimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa wa kwanza kushoto akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa majengo ya Maabara ya skuli hizo. Picha na OMPR – ZNZ.

  0 0


  MWENYEKITI wa Yanga SC  Yusuf Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.
  Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.
  Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.
  Sasa rasmi utafanyika ujenzi wa uwanja na uwekezaji mwingine katika eneo hilo lililobatizwa kijiji cha Yanga SC.

older | 1 | .... | 1371 | 1372 | (Page 1373) | 1374 | 1375 | .... | 3272 | newer