Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1370 | 1371 | (Page 1372) | 1373 | 1374 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) anayemaliza muda wake, Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kushoto), leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Mtangulizi wake, Dkt. Kazaura.[/caption] KAIMU Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dk. Kamugisha Kazaura. Utambulisho wa awali wa kiongozi huyo mpya umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, anaesimamia sekta ya Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora. Makabidhiano rasmi ya ofisi yatafanyika baadae. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dkt. Kamugisha Kazaura. Wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa TTCL.

  0 0

   Meneja Mahusiano Mkuu wa Kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini Tiper, Bw Emanuel Kondi akimkabidhi zawadi na cheti cha ushiriki wa Rock City Marathon mmoja wa washindi kwa upande wa mbio fupi katika michuano hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kampuni ya Tiper ni miongoni wa wadhamini wakubwa wa mbio hizo. Wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi (wa pili kulia)
   Meneja Mahusiano Mkuu wa Kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini Tiper, Bw Emanuel Kondi akimkabidhi zawadi na cheti cha ushiriki wa Rock City Marathon mmoja wa washindi katika michuano hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kampuni ya Tiper ni miongoni wa wadhamini wakubwa wa mbio hizo. Wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi (wa pili kulia) na Mwanariadha mkongwe hapa nchini Bw Juma Ikangaa.
   Meneja Mahusiano Mkuu wa Kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini Tiper, Bw Emanuel Kondi akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Rock City Marathon mmoja wa washindi kwa upande wa mbio fupi katika michuano hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kampuni ya Tiper ni miongoni wa wadhamini wakubwa wa mbio hizo. Wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi (wa pili kulia)  0 0


  Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo ameanzisha mashindano ya kusuka mitindo mbalimbali lijulikanalo kwa jina la “Msusi Wao’ ambalo ni maalum kwa wasusi ambao hawamiliki vibanda vya saluni.

  Shindano hilo linaanza leo Manispaa ya Temeke ambapo washindi watatu watapata zawadi mbalimbali zitakazotolewa na kampuni ya Kidoti kwa kushirikiana na wadau wengine kama Umoja Switch, Abee Naturals na wengine.

  Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atazawadiwa sh 300,000, nywele za Kidoti zenye thamani ya Sh milioni 1.5 na mashine ya kukaushia nywele ‘Dryer’.

  Mshindi wa pili atazawadiwa Sh250,000, nywele za kidoti zenye thamani ya Sh milioni Moja na mashine ya kukaushia nywele ‘Dryer’ na mshindi wa tatu atazawadiwa Sh200,000, nywele za Kidoti zenye thamani ya Sh 500,000 na mashine ya kukaushia nywele ‘Dryer’.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo la kwanza, Jokate alisema kuwa washiriki wanatakiwa kujaza fomu maalum ambazo zinapatikana katika duka la Kidoti lililopo mtaa wa Bonde na Pemba Kariako.

  “Msusi anayefanyakazi saluni haruhusiwi kushiriki katika mashindano haya, tutatumia njia mbalimbali kuweza kubaini wasusi ambao wanafanyakazi katika saluni na kuwaondoa, hii ni fursa pekee kwa wasusi ambao wanasukia kwenye vibaraza au vibanda ambavyo siyo rasmi,” alisema Jokate.

  Alisema kuwa kutakuwa na majaji watatu katika kila shindano ambao watakuwa chini ya Jaji Mkuu, Conchester Ishengi ambaye ni mtaalam wa masuala ya ususi. Ishengi alisema kuwa watazingatia vigezo vilivyowekwa ili kumpata mshindi.

  “Lengo ni kuwawezesha wasusi ambao hawana uwezo wa kupanga vyumba vya saluni, kupitia shindano hili, tutaweza kuwapta wasusi wengi kwani kipaji chako ndiyo utajiri wako,” alisema.

  Afisa Masoko wa Umoja Switch, Jasmin Shamshama alisema kuwa wameamua kusaidia shinadno hilo kama sehemu ya kuisaidia jamii kupitia mashindano hayo.

  “Tumeandaa ATM kadi za Umoja Switch ambazo si lazima uwe na akaunti, hii unaweza kutumia hata kwa namba yako ya simu, hivyo mashindano ya ‘Msusi Wao’ ni sehemu halisi ya kuwawezesha wajasiriamali,” alisema Jasmin.

   Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wasusi wa mitindo ya nywele (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la “Msusi Wetu” jana yaliyoanzishwa na kampuni ya Kidoti.
   Mwakilishi wa masuko kutoka Umoja Switch Jasmin Shamshama katikati akizungumzia jinsi watakavyoshiriki katika mashindano ya ususi wa staili mbalimbali za nywele yajulikanayo kwa jina la “Msusi Wetu” jana yaliyoanzishwa na kampuni ya Kidoti.
   Baadhi ya washindani wa mashindano ya  kumtafuta msusi bora wa aina mbalimbali ya nywele yajulikanayo kwa jina la Msusi Wetu wakifuatilia uzinduzi huo.
   Mtangazaji wa kipindi cha  Leo Tena ya Clouds Fm Husna Abdul 'Dahuu' wa kwanza kushoto akizungumza katika uzinduzi huo.

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha (kushoto) kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipokea msaada wa seti ya televisheni yenye thamani ya Sh 2.4 milioni kwa ajili ya jengo la wazazi (Maternity II). Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Kibosho (UVIKI), Severine Mushi akikabidhi msaada huo LEO na anayefuatia ni Mwenyekiti wa UVIKI, Marcel Mushi (wa tatu kushoto).
   Mlezi wa umoja huo, Dk Methew Kalanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kinamama Muhimbili akiwapongeza vijana hao kwa kutoa msaada wa seti ya televisheni na kuchagia damu leo. Kulia ni Kaimu Meneja wa Jengo la Wazazi namba mbili, Sister Stella Gerald.
   Vijana hao wakichangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo.
  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  Mercy Kaanaeli, MNH.
  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea jumla uniti  19 za damu kutoka kikundi cha Umoja wa Vijana wa Kibosho (UVIKI). Kikundi hicho chenye wanachama 40 kimeka katika hospitali hiyo leo na kutoa msaada wa seti ya televisheni na kuchangia damu.

  Msaada huo umetolewa leo katika hospitali hiyo una thamani ya Sh 2.4 milioni na seti hiyo itafungwa katika Jengo la wazazi namba mbili. Seti hiyo inahusisha Runinga moja ya nchi 50, Dishi na King’amuzi cha AZAM pamoja na deki.

  Akishukuru baada ya kupokea seti hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha amesema seti hiyo ya televisheni itatumika kutoa elimu ya afya kwa kinamama wajawazito.

  Kaimu Meneja wa Jengo la Wazazi namba mbili, Stella Gerald amesema seti hiyo ni msaada mkubwa na kwamba  itasaidia kuelimisha kina mama wakati wakisubiri kupata huduma.

  “Huwa tunatoa elimu ya maandalizi kwa kinamama ikiwamo vidokezo vya hatari, uandaaji wa chakula lishe pamoja na mambo yanayopaswa kufanywa, hivyo badala ya muuguzi kuongea tutatumia runinga kutoa elimu hiyo,”amesema Stella.

  Naye Mkuu wa Idara ya Kinamama, Dk Matthew Kallanga amesema mchango wa damu uliotolewa na kikundi hicho utasaidia kina mama kuwa na uzazi salama.

  “Damu iliyochangiwa na kikundi hiki, itasaidia kina mama kuwa na uzazi salama kwani mama mjamzito mmoja huweza kutumia chupa 5 hadi 6,” amesema.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha ametoa wito kwa jamii kuiga mfano wa kikundi cha UVIKI na kutoa damu kwa wingi ili kuokoa maisha ya wagonjwa.

  Mwenyekiti wa Kikundi cha UVIKI, Marcel Mushi amesema kuwa watatoa elimu katika jamii wanayoishi ili wanajamii wengi zaidi wajitokeze kuchangia damu.

  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itapitia upya sababu za kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) kufuatia mamlaka hiyo kuendeshwa kwa ubabaishaji.

  Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka hiyo kushindwa kusimamia uendelezaji wa bonde hilo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikwiriri mkoani Pwani.

  Alisema baada ya mapitio hayo shughuli za mamlaka hiyo zitahamishiwa kwenye mamlaka nyingine za serikali kwani RUBADA  imeshindwa kufanyakazi hiyo kwa muda mrefu.

  “RUBADA wamepewa ardhi lakini wameshindwa kuiendeleza, tutafanya upya mapitio ya kuanzishwa kwake,” alisema.
  Akizungumzia kuhusu Kampuni ya Agro Forestry Plantation inayotaka kujenga kiwanda cha sukari wiyani Rufiji aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 60 ya watumishi watakaowaajiri wawe ni vijana wa wilaya hiyo.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, kwenda wilayani Rufiji kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mkuranga na Ikwiriri.

  Waziri Mkuu amelitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Ikwiriri kuhusu kutotatuliwa kwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.

  Naye Mkurugenzi wa halshauri ya wilaya hiyo, Rashidi Salum alimweleza Waziri Mkuu kuwa, mgogoro huo umeshatatuliwa kwa ngazi ya wilaya  hivyo hatua iliyosalia ni kwa uWaziri wa Ardhi kufika na ramani ili kutoa uamuzi.

  0 0

   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof.Abdulkarim Mruma akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Bi. Maimuna Tarishi maeneo sahihi ya ujenzi wa majengo katika shule ya sekondari Ihungo.
   Mkufunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Jiolojia akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Bi. Maimuna Tarishi maeneo sahihi ya ujenzi wa majengo katika shule ya sekondari Ihungo.
   Mkufunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Jiolojia akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Bi. Maimuna Tarishi ramani ya maeneo katika maeneo sahihi ya ujenzi wa majengo katika shule ya sekondari Ihungo.

  0 0

  Na Woinde Shizza, Arusha

  Kambi tiba ya GSM Foundation inayotembea nchi nzima kutafuta watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi imemaliza mkoa wa 13 tangu kuanza kwake, na Jumatano hii itaanza kazi mkoa wa Mara ambao utakuwawa 14.

  Mkuu wa kambi tiba hiyo, Dk Othman Kiloloma Amebainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

  Akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha, Dk Kiloloma ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya Muhimbili, MOI alisema kuwa wao kama taasisi walikaa chini na kuona kuna watoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya gharama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho hakina ukweli.

  "Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 hatujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma

  Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kichwa, Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17 aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.

  Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada.

  "Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto usisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua, tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.

  Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususa ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa.

  Alisema anapenda kuwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

  Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini hapa Tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa.


  0 0

  STARTIMES  imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.

  Akizungumza wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na mahusiano mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

  “Mahusiano mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii. Kupitia kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande. 

  Nawapongeza StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura

  “Pia ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za  michezo ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao yenu makuu yaliyopo Beijing. 

  Hii ni hatua nzuri na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura

  Akielezea umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,. Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti itakayoenzi mahusiano hayo.

  ‘’Utofauti ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China, 

   Xi Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema  ZiQi

  ‘’Kwa kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na filamu. 

  Mpaka hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi
   Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo  baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.
   Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China  wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili,  Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi wa China nchini,  Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,  Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia ndani ya bwawa la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara wa Kampuni ya Simu za Mkononi YA Airtel (kulia), akimpa zawadi Beatrice Nalingigwa baada ya kuibukas kidedea katika shidano la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
    Baadhi ya wafanyakazi na familia zao wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
   Mwanafamilia wa Airtel akiwapa chakula watoto ikiwa ni ishara ya upendo ulio ndani ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .

  Ni muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na  kujumuika kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya matunda waliyoyapata kwa mwa huu.

   Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao. "Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.

  Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia  600 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea.  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.

  0 0


  0 0

  Kila mwaka shirika la Four Corner Culture Program (4CCP) huandaa tamasha la kiutamaduni ili kukuza na kuenzi tamaduni halisi za kitanzania . Tamasha la mwaka huu limekuwa la kipekee kutokana na matukio mablimbali ya kimaendeleo na kiutamaduni yaliyofanyika .Ambapo Shirika la Norwegian Church Aid kwa kushirikiana na 4CCP Hydom walizindua miradi mbali mbali ya maendelea katika sekta ya maji (Visima)ili kupunguza tatizo kubwa la maji linalo wakumba wananchi wa wilayani Mbulu mkoani Manyara na mkoa jirani wa Singida.
  Naibu Balozi Norway bwana TRYGVE BENDIKSBY .akizindua kisima cha maji kijiji cha ENDAGAW wilayani Mbulu. kutoka kulia ni TALE HUNGNES Mwakilishi Mkazi wa Shirika la NCA Tanzania,Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh.Flatey Massay, Balozi Msaidizi TRYGVE BENDIKSBY, Bwana Abeli Mfanyakizi wa NCA na Afisa Mradi wa WASH NCA Tanzania Bwana.Zakayo Makobelo.PICHA ZOTE NA IMANI NSAMILA.


  Bwana Zakayo Makobelo akitoa ufafanuzi Juu ya kisima hiki kitumiacho Nishati ya Jua.

  Mbunge wa Jimbo la Mkalama Mhe Allan Kiula  akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa kijiji cha Munguli wilayani Mkalama Mkoani Singida.

  Mkuu Wa wilaya ya Mkalama Mkoani Singida na Mbunge wa Mkalama Mhe Allan Kiula wakionyweshwa Vifaa vifaa hivi vya kuzilisha nishati ya jua kwa ajili ya kusaidia Usamabazaji wa maji kijjijni.


  Vijana wa YouthCAN wakitoa elimu YA MAZINGIRA,AFYA NA MAJI SALAMA kupitia muziki wakati wa Tamasha la kiutamaduni. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu wawili ambao ni Mme na Mke kwa tuhuma za matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha za moto katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es salaam.

  Watuhumiwa hao ambao wametambulika kwa majina ya Bakari Abdallah (40) na Sihaba Omary (28) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni walitiwa mbaroni mnamo tarehe 23 Septemba mwaka huu na Kikosi Maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha.
  Akizungumza mbele ya wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema kuwa mnamo tarehe 26 Septemba mwaka huu Askari walifika nyumbani kwa watuhumiwa hao na kukuta bastola aina ya "Browning" yenye usajili namba CAR A081900 ikiwa na magazine mbili na risasi tano pamoja na simu aina ya Nokia Lumia ambayo inadaiwa kuwa iliporwa katika matukio ya unyang'anyi.
  Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya oparesheni ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam. ambapo Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu mmoja kwa tuhuhuma za ujambazi wa kutumia silaha za moto.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionesha kwa wanahabari silaha zilizokamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Verosa likiwa limesheheni magunia saba za bangi leo iliyokamatwa hivi karibuni jiji Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Noah ikiwa wan a magunia ya bangi.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha namba za gari za bandia ambazo zimekuwa zikitumiwa na waharifu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kushoto) akimkabidhi tofali Afisa Miradi wa Kikundi cha vijana cha Tuinuane cha Bukoba Mjini Christopher Vincent wakati wa makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali iliyotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yenye ubora unaofaa kujengea katika mazingira ya Bukoba kulingana na asili ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera.
  nhc2
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bi.Susan Omari (kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kushoto) wakati wa kukabidhi mashine za kuengenezea matofali ya kisasa kwa vijana wa kikundi cha Tuinuane cha Bukoba Mjini yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera leo mjini Bukoba.     
  nhc4
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bi.Susan Omari (kulia) akitoa maelezo kwa vijana wa kikundi cha Tuinuane cha Bukoba Mjini yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera leo mjini Bukoba.     
  nhc5

  Baadhi ya mashine zilizotolewa kwa vijana hao

  0 0

  Jonas Kamaleki, MAELEZO

  Wakazi wa Kinyerezi Sokoni, Dar es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha sheria.

  Pongezi hizo zimetolewa leo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati hizo mara moja na kulirejesha eneo la makaburi kwa wananchi.

  Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kinyerezi, Mwanasheria, Mwinjuma Mzee amesema kuwa Wanakinyerezi wanamshukuru sana Mhe. Waziri kwa kurejesha eneo la makaburi kwa wakazi hao.
  “Mhe. Waziri na msafara wake wote tunawashukuru kwa kumaliza mgogogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na tumemwomba Waziri ashughulikie na maeneo mengine yanayohusu huduma za jamii kama zahanati na shule,” alisema Mzee.

  Naye mkazi wa Kinyerezi, Bi. Maimuna Forogo ameelezea furaha yake kwa kumshukuru sana Mhe waziri kwa hatua aliyoichukua ya kubatilisha hati za umiliki wa makaburi.

  “Mimi namnshukuru sana Mhe. Waziri na Serikali ya awamu ya Tano kwa ujumla kwa kutujali sisi wananchi, mimi kwenye makaburi haya nilimzika babu yangu sasa wanataka nimpeleke wapi kwanza ni mifupa mitupu,”alisema Maimuna.

  Kwa upande wake, Mhe. Lukuvi amesema ameamua kubatilisha hati tatu za viwanja zilizotolewa na watumishi wasiowaaminifu wa Serikali ili eneo hilo liendelee kutumika kwa ajili ya maziko.

  “Nimemuagiza kamishna anitafutie wahusika ambao walishiriki katika kumilikisha eneo la makaburi kwa watu ili wachukuliwe hatua za kinidhamu, watu hawa inabidi wafukuzwe kazi kwani kitendo cha kumilikisha eneo la kuzika hakivumiliki,”alisema Waziri Lukuvi.

  Ameongeza kuwa watu ambao wanadiriki kuuza makaburi ambayo yametumiwa tangu mwaka 1962 na kwa sasa yapo zaidi ya 500, ni watu ambao hawana hata hofu ya Mungu hivyo kufukuzwa ni halali yao.

  Mhe. Lukuvi ametoa wito kwa viongozi wenzake wanapofanya shughuli za mipangomiji nchini kutenga sehemu za huduma za jamii ikiwemo mahali pa kuzikia kwani kila mtu atakufa na anahitaji kuzikwa.  

  “Serikali ya awamu ya Tano tumeamua kurekebisha pote palipokuwa pamepinda ili wananchi wapate haki zao,”alisema Lukuvi.

  Aidha amewataka waliokuwa wamemilikishwa wafike wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili wampe Waziri uzoefu wanaoutumia kununua maeneo ya huduma za jamii ikiwemo maeneo ya makaburi ili imsaidie kujua jinsi mtandao ulivyo.
  Hati tatu zilizofutwa ni 213, 215 na 217 Kitalu B, Kinyereze, Kata ya Segera jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Anthony John, Globu ya jamii.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanahabari,Theophil Makunga ameipongeza Serikali kwa niaba ya wanahabari kwa kuanza mchakato kuondoa Sheria ya Magazeti ya mwaka1976 kwani Sheria hiyo amedai ilikuwa inawabana wanahabari. Pia akifafanua kuwa,serikali imeanza mchakato wa kubadilisha Sheria  hiyo ya Magazeti iliyo kuwepo kwa Miaka 40 tangu ianze kutumika,hivyo alisema Sheria itakayo anzishwa itafanya kazi kwa muda mrefu kwa Miaka 40 hadi 50.
  Serikali imesikiliza kilio cha wanahabari na imeanza mchakato wa kubadilisha hiyo Sheria,sasa kwa sababu hiyo kama alivyosema katibu ni kwamba Sheria hiyo imekaa kwa muda wa Miaka 40 kwa hivyo hata mpya itakayotugwa sasa itakaa Miaka 40 hadi 50 inayokuja.
  Hivyo Hivyo,Katibu Mkuu wa Jukwaa la wanahabari Neville Meena amesema watapata maoni ya wadau mbali mbali wa Habari kupitia klabu za waandishi wa habari watakao kwenda kuwaeleza maudhui yaliyomo ndani ya Sheria yenyewe ilikupata maoni yao wenyewe vila kuwashawishi.

  "Maana yake tukienda kufanya uchambuzi watachukua maoni yetu kama maoni yao, hata hivyo tumekuwa tukipokea lawama nyingi kutoka kwa waandishi kutokushiriki na wakati wao ndio wako kwenye vyombo vya Habari" hayo,"amesema  Meena. 
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanahabari Bw. Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuipongeza Serikali kwa niaba ya wanahabari kwa kuanza mchakato wa kuondoa Sheria ya Magazeti ya mwaka1976 kwani Sheria hiyo ilikuwa inawabana wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wanahabari, Bw. Neville Meena.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura amewataka vijna kutumia fursa ya Tamasha la Kimataifa la 35 la Sanaa na Utmaduni Bagamoyo kuonesha vipaji kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
  Akifungua Tamasha hilo juzi ambalo mwaka huu limeshirikisha vikundi 65 vya sanaa na utamaduni kutoka nchini na nje ya nchi, Naibu Waziri huyo alisema sanaa ni ajira yenye uhakika kama wasanii watafanya kazi zao kwa uadilifu.
  Mhe. Wambura amesema anafahamu changamoto zinazoikabili Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa za ukosefu wa fedha  na wafadhili hivyo aliwataka kushirikisha wadau wa ndani na nje ili matamasha kama hayo yaboreshwe na kushirikisha nchi mbalimbali duniani.
  Alisema kutoka TaSUBa kianzishwe mwaka 1982 kimekuwa kivutio na kubadilishana tamaduni na nchi mbalimbali kama Ujerumani, Norway, Kenya, Japan na China ambazo zimeshiriki kwaka huu katika tamasha hilo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa wizara hiyo, Francis Songoro aliwaomba wadau waendelee kujitokeza kuwatia moyo wasanii katika kazi zao.
  Katika tamasha hilo Naibu Waziri aliongoza kucheza ngoma ya Kigogo huku kikundi cha wanachuo kikitia fora kwa ngoma ya asili ya Kizaramo kutoka mkoa wa Pwani ya Mkwaju Ngoma.
  Awali Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majjid Mwanga aliwataka wananchi wa Bagamoyo kukienzi chuo hicho ambacho ni cha kwanza Tanzania kinachozalisha wasanii nchini na kukuza uchumi wa wilaya kwa kuwapokea wageni wengi wanaokuja kujifunza sanaa ya Tanzania.
  Tamasha la TaSUBA litafanyika kwa wiki mmoja mfululizo ambako vikundi mbalimbali vitaonesha umahiri wao wa kucheza, kuimba na bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kutumia vifaa vya asili.
  Pia katika tamasha hilo ambalo Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) iliwakilishwa na wajumbe sita wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa mtadano huo Suleiman Kissoky ambako kikundi chao cha ngoma na sarakasi cha Splendid kitawakilisha.
   Wapiga ngoma wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) wakipiga ngoma katika ufunguzi wa tamasha hilo. 
   Wacheza ngoma za utamaduni wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) wakitumbuiza katika ufunguzi wa tamasha hilo. 
   Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo, Anna Wambura (katikati)akifuatilia ngoma ya kikundi cha wanachuo wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBA) wakicheza ngoma ya Kizaramo ya Mkwaju Ngoma kutoka mkoa wa Pwani. Kushoto ni Dkt. Herbert F. Makoye Mkurugenzi Mtendaji wa TaSUBa na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Mwanga.
   Wadau mbalimbali wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia maoneshoa ya ngoma wakati wa ufunguzi
   Wadau wa sanaa  wakifuatilia maoneshoa ya ngoma wakati wa ufunguzi.


  0 0


older | 1 | .... | 1370 | 1371 | (Page 1372) | 1373 | 1374 | .... | 3284 | newer