Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1366 | 1367 | (Page 1368) | 1369 | 1370 | .... | 3282 | newer

  0 0

  SALAAM AND JAMBO...
  AT 3.30 PM ON SATURDAY 10TH SEPT 2016. BUKOBA WAS HIT BY A MAJOR EARTH QUAKE READING 5.7 RITCHER SCALE.
  THE IMMEDIATE REPORT SAYS THAT 19 PEOPLE DIED, 800 HOUSES FLATTENED COMPLETELY AND 2300 HOUSES DAMAGED. NOW THE NEW FIGURES ARE COMING IN,  THAT MORE THAN 10,000 HOUSES ARE AFFECTED.
  IZAAZ HAS STARTED A PROGRAM TO HELP THOSE VICTIMS WHOSE HOUSES ARE DAMAGED. WE FIRST START WITH OUR IZAAS MADRESSA CHILDREN AND IZAAS STAFF.
  0 0


  0 0

   
  Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014  katika hotel ya St Regis ya Washington, DC. 
   Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.
  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa viongozi wa Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
   Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akielezea mafanikio na utendaji wa benki ya CRDB na jinsi gani inavyowawezesha wawekezaji wazawa kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
   Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akitunukiwa tuzo na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
   kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
   Picha ya pamoja.
   Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa benki ya CRDB, Bwn. Frederick  Nshekanabo, Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei alipokua akifanyiwa mahaojiano mara tu baada ya kupokea tuzo kutoka African Leadership katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016.

   Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akifuatilia sherehe ya Tuzo kutoka kwa African Leadership iliyofanyika katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.

  Hapa ni siku Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014

  0 0

  SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV  na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kunduchi na Makumbusho.


  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.

  Taarifa hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.


  0 0


  0 0  WANANCHI  na wakazi wa jijini la Dar es Salaam wajitokeza katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Saala kupima afya zao ambapo madaktari wa hospitali mbalimbali za jijini la Dar es Salaam watakuwepo katika viwanja hivyo kwaajili ya kupima afya za wananchi wa jijini la Dar es Salaam bila malipo yoyote.
   Baadhi ya Wananchi wakiwa katika foleni ya kuelekea sehemu ambazo zimetengwa kwaajili ya kucheki afya jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Madaktari na watoa huduma ya afya wakitoa huduma leo katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
  Umati wa wananchi waliojitokeza kupima afya zao mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makondo kuomba wananchi kwenda katika viwanja vya Mnazimmoja kucheki afya leo na kesho.

  0 0


  Wakazi wa kata ya Manzese Mpakani mtaa wa mchafu wakichota Majisafi kwenye moja ya Kizimba cha Majisafi kilichojengwa na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) katika kutatua kero ya Maji kwenye eneo hilo.

       KATIKA kuhakikisha kero ya kukosa Maji inakwisha kwenye maeneo mbalimbali yanayowazunguka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) imezindua vizimba maalum vya Majisafi katika mitaa mbalimbali ya kata ya Manzese Mpakani iliyopo wilaya ya Kinondoni ili  kuwapunguzia wakazi wa maeneo hayo adhaa ya kutafuta Majisafi na salama kutoka umbali mrefu.

  Akizungumza katika uzinduzi huo wa vizimba vya Majisafi, Meneja wa Dawasco mkoa wa Magomeni Mhandisi Pascal Fumbuka ameleeza kuwa wamejenga jumla ya vizimba saba vya Majisafi ambapo mtaa wa mchafu wamejenga vizimba vitatu na katika mtaa wa Muhltani wamejenga vizimba vinne na vizimba hivyo vya Majisafi vinatarajia kuhudumia wakazi zaidi ya elfu moja wa maeneo hayo.

  “katika kutatua kero ya Maji hapa Manzese mpakani tumejenga vizimba vya Majisafi saba ambapo tunatarajia wakazi zaidi wa elfu moja watanufaika na hivi vizimba vya Majisafi hata hivyo kutokana na ujenzi holela wa makazi ya watu imetuwia ngumu kufikisha bomba kwa kila mkazi ila kwa vizimba vya Majisafi tuamini vitaondoa kabisa kero ya Maji kwani kwa kizimba kimoja tu kina bomba nane na Maji yanapresha kubwa hivyo havitaleta msongamano pamoja usumbufu kwa wakazi pale watakapokuwa wanakinga Maji” alisema Fumbuka.

  Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ya Muhltani Bw. Sudy Makamba ameishukuru Dawasco kwa kujenga vizimba hivyo vya Majisafi kwani wakazi wa mtaa wake wamekuwa wakipata adhaa ya kutafuta Majisafi na salama kwa muda mrefu hivyo amewataka wananchi kuvituza pamoja na kulinda miundombinu ya Maji iliyopo katika mtaa wao.

  “Nawashukuru sana Dawasco magomeni na uongozi wake kwa kutukumbuka na kujenga vizimba hivi vya Majisafi ambavyo vitasaidia kuondoa kero ya Maji katika mtaa wetu ambao umekuwa haupati Majisafi kwa muda mrefu ila pia natumia fursa hii kuwasihi wakazi wote wa mtaa huu kutuza hivi vizimba pamoja na miundombinu kwani tukiharibu tutarudi katika shida tuliyokuwa nayo mwanzo”  alisema Makamba.

  Nae mkazi wa mtaa wa mchafu bi. Martha Faraji amesema kuwa  vizimba hivyo vya Majisafi ni mkombozi mkubwa kwao haswa wanawake ambao wamekuwa wakihangaika na adhaa ya  kukosa majisafi na salama kwa kipindi kirefu ila ameiomba Dawasco kuongeza vizimba hivyo kwenye mtaa wao ilikuepukana na msongamano kwenye vizimba hivyo.

  “vizimba hivi vya Majisafi kwa kweli vimetuokoa sisi wanawake wa mtaa wa mchafu maana tulikuwa tunapata shida mno maana tunahangaika kupata majisafi na kwa bei ya juu ambayo sisi watu wakawaida inatuwia ngumu kumudu ila tunaomba Dawasco wajenge vingi ilikusiwe na foleni wakati tunaenda kukinga Maji” alisema Faraji.

  0 0

  Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi, lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni. Mchezo huo utafanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Kabla ya Mchezo huo, kutakuwa na michezo ya Utangulizi ambapo Timu ya Bunge ya Mchezo wa Pete (Netball) inakutana na Timu ya TBC huku Mchezo mwingine ukiwa ni ni kati ya Wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva. 
  Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkeyenge akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi, lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni. Nkeyenge amewataka wale wote watakaojitokeza kwenda kuangalia mchezo huo, wanatakiwa kuwa na tiketi za Kielekroniki ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia hiyo kesho, Pia amezungumzia hali ya usalama katika Uwanja huo kuwa itaimarishwa vizuri kwani Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha hatuna tukio lolote la uvunjifu wa amani litakalojitokeza uwanjani hapo.
  Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akionyesha moja ya vikombe vitakavyokabidhiwa kwa timu zitakazoshinda katika michezo hiyo ya kesho.
  Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication LTD, Francis Nanai ikiwa ni sehemu ya Mchango wao katika kufanikisha zoezi hilo.

  WAKATI tiketi za elekroniki zitaanza kujaribio welo, Makampuni mbali mbali wamechangia jumla ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kudhamini mchezo wa wabunge mashabiki wa Yanga na wale wa Simba utakaofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.

  Makampuni hayo ni Mwananchi Communication iliyotoa Sh milioni 20, mfuko wa bima ya afya NHIF na Jubilee Insurance ambazo zote zimetoa Sh milioni 5 kila mmoja.

  Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge William Ngeleja ambaye pia ni mnazi wa Simba alisema matokeo ya mchezo wa kesho ni hishara ya matokeo ya mchezo wa Oktoba Mosi.

  Nae Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta amesema kadi  hizo zitatolewa bure katika mchezo wa leo ikiwa ni  majaribio na kuangalia dosari ambazo zitajitokeza kabla ya kuanza kuzitumia rasmi. 

  Akizungumzia jinsi ya kuitumia kadi hiyo, Runyeta alisema “Utajisajili kwa kupiga *150*50# halafu ni lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa. Kiwango cha chini cha kuongeza salio ni Sh 1,000….: “ “Unaweza ukanunua mechi moja kwa kuandika tarehe na mchezo husika au ukachagua baadhi ya mechi au ukanunua mechi zote za msimu za timu unayoipenda.

  “Unapokwenda kuingia uwanjani, utaweka kadi yako kwenye alama husika na mlango utafunguka wenyewe. Ukishaangalia mechi uliyoinunua, hauwezi kesho yake ukaenda kutazama mechi nyingine ambayo hujailipia. Kadi itasoma kwenye mechi zilizolipiwa tu. Ukiingia uwanjani hauwezi ukatoka halafu ukarudi kwa tiketi ileile. 

  Viingilio vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu, 10000 na 15000  kwa  viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.

  Katika mchezo huo mbali na wabunge pia kutakuwa na mechi ya bongo movie na bongo fleva ambapo kikosi cha bongo movie kitaongozwa na King Majuto, Dr Cheni, Check Budi, Muhogo Mchungu na Ray Kigosi wakati kwa upande wa Bongo Fleva kitaongozwa na Rich One, Kalla Pina, Ally Kiba, Stamina, KR Muller na H baba.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Kampuni inayotekeleza mradi wa Umeme Vijijini Mkoani Kigoma ya State Grid, Wilboad Mutabuzi kulia.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza na wananchi wa eneo la mradi.
  Wananchi wa Wilaya ya Kakonko wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini kwa Mkoa wa Kigoma

  WITO huo umetolewa jana wilayani humo wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) Mkoani Kigoma ambapo alibaini changamoto mbalimbali ikiwemo ya nguzo za umeme kusimikwa vibaya bila kuzingatia utaalamu hasa ikizingatiwa kuwa maeneo hayo hua na upepo mkali unaoweza kusababisha nguzo hizo kuanguka.

  Katika ziara hiyo, Profesa Muhongo alipatiwa taarifa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Col. Hosea Ndagala ambaye alimueleza kutoridhishwa na namna mradi huo unavyotekelezwa ikiwemo uduni katika usimikaji wa nguzo za umeme.

  Alisema baadhi ya nguzo hizo zimeanza kuinama kutokana na upepo pamoja na kutosimikwa vizuri hali inayoweza kusababisha madhara kwa Wananchi wa eneo hilo endapo nguzo hizo zitadondoka.

  Kufuatia taarifa hiyo na ukaguzi alioufanya kwenye eneo la mradi, Waziri Muhongo aliagiza hadi kufikia mwisho wa Mwezi huu Mradi huo uwe umekabidhiwa kwa Meneja wa TANESCO Kigoma na kwamba kabla ya kupokelewa Mkuu wa Wilaya naye athibitishe kuridhishwa utekelezaji wake ikiwemo kurekebisha kasoro zilizobainika ili wananchi wanufaike na mradi ulio katika ubora unaotakiwa.

  Profesa Muhongo alisema endapo Mkandarasi atashindwa kutatua changamoto hizo na kasoro zilizo jitokeza katika mradi huo hatoruhusiwa kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa REA III ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya  Awamu hii ya pili kukamilika.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya State Grid, Wilboad Mutabuzi alisema usambazaji umeme mkoani humo umekamilika kwa asilimia 98 na huku akiahidi kuhakikisha anashughulikia kasoro zilizobainika ili akamilishe mradi kwa wakati na wenye ubora unaokubalika.

  Mutabuzi alisema gharama za mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) kwa mkoa wa Kigoma ni shilingi bilioni 23 na kwamba katika Wilaya ya Kakonko vijiji saba vimefaidika na mradi huo.

  Alisema  changamoto kubwa iliyojitokeza ni muitikio mdogo wa Wananchi kuunganishiwa huduma ya nishati ya umeme kutokana na sababu mbalimbali.

  Alisema kutokana na muitikio wa wananchi kuwa mdogo imesababisha kushindwa kufikia lengo ambapo kwa Mkoa mzima wa Kigoma lengo lilikuwa ni kuwaunganishia huduma ya umeme wateja wapatao 11,000  lakini hadi sasa ni wateja 7,000 tu ndio waliopatiwa huduma husika.

  0 0

  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri (Kulia)
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.
  Na Mathias Canal, Tabora.

  MWENGE wa Uhuru umewasili Mkoani Tabora ambapo unatarajiwa kuzindua miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bilioni ishirini na tatu, Milioni nne, laki nne elfu na arobaini na saba mia tano sitini na sita 23,004,447,566/= ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 40% ukulinganisha na miradi ya mwaka 2015 iliyokuwa na thamani ya shilingi 9,207,720,213.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mgongolo, Kata ya Igunga, Wilayani Igunga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri amesema kuwa sera ya Vijana Tanzania ya Mwaka 2007 inatambua kuwa vijana ni watu wote wenye umri wa miaka 15-35 ambapo kulingana na sensa ya Mwaka 2012 inaonyesha kuwa Mkoa huo una jumla ya vijana 439,455 hivyo hekari 681 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za vijana ili kukidhi kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.

  Mwanri alisema kuwa Mwaka 2015 Mwenge wa Uhuru mkoani Tabora ulikimbizwa katika Halmashauri 7 zilizokuwepo ambapo Mwaka huu utakimbizwa katika Halmashauri 8 ambazo ni Igunga, Nzega Mji, Tabora Vijijini (Uyui), Sikonge, Urambo, Kaliua, Tabora Manispaa na Nzega Vijijini.

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Aggrey Mwanri mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo naye amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo ili aukimbize katika Miradi iliyopangwa ukiwemo wa kuzindua Mradi wa maji Vijijini, Kufungua vyumba viwili vya madarasa na choo cha matundu 10 katika Shule ya Sekondari Mwayunge, Kuweka Jiwe la msingi katika Hoteli ya Mjasiriamali Zengo T. Kija, Kuzindua mradi wa Kilimo cha bustani na Ufugaji wa samaki wa kikundi cha Vijana cha Msongela, na Kuzindua zahanati ya Kijiji cha Igogo.

  Miradi mingine ambayo Mwenge wa Uhuru utazuru ni pamoja na kugawa kadi za CHF kwa wanachama wapya, Kugawa vyandarua kwa wananchi na baadaye utazuru katika Shule ya Sekondari Nanga.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kujitokeza kwa wingi kutokana na juhudi na ushiriki wao kwenye kuibua, Kutekeleza na Kusimamia miradi mbalimbali ambapo pia amewataka wananchi hao kwa umoja wao kuitunza miradi hiyo.

  Mtigumwe alisema kuwa tangu Mwenge wa Uhuru ulipokabidhiwa Mkoani Singida ukitokea Mkoani Dodoma Septemba 17, 2016 umepita kwenye miradi 61yenye thamani ya Shilingi 14,266,628,518 iliyopo katika Halmashauri saba ambayo ni pamoja na Mradi wa elimu, Afya, Maji, Barabara, Biashara, Mazingira, Kilimo, Mifugo, Ushirika na programu mbalimbali za mapambano dhidi ya Rushwa, Dawa za Kulevya, Ukimwi na Malaria.

  Mtigumwe alisema kuwa mbali na Mwenge wa Uhuru kupita kwenye Miradi mbalimbali Mkoani Singida Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa amewaongoza wakimbiza Mwenge wenzake kitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2016 ambao ni "Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" Vile vile, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesisitiza umuhimu wa vijana na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya Rushwa, Dawa za kulevya, Kuchukua hatua dhidi ya tabia hatarishi zinazoweza kuchochea maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini kuwa tayari kwenda kufanya kazi kokote watakalopangiwa na Serikali kulingana na mahitaji ya eneo husika.

  Amesema moja ya wajibu wa watumishi wa umma ni kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania sehemu yoyote walipo ili kuwaletea maendeleo na atakayeshindwa ni vema akatafuta shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana  jioni (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mkunguni wilayani Mafia.

  Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

  Waziri Mkuu alisema kila awamu inakuwa na mkakati wake, watumishi wa umma wanatakiwa kubadilika na kufanya kazi kutokana na awamu iliyoko madarakani inavyotaka

  “Hii ni awamu ya kazi zaidi. Hata kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu! si neno la kufurahisha bali lina malengo yanayowataka Watanzania wote wafanye kazi,” alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani, Dk. Beatrice Byarugaba kuimarisha huduma katika hospitali ya wilaya ya Mafia na kupeleka madaktari bingwa ili kuwapunguzia wananchi gharama za  kufuata huduma nje ya wilaya hiyo.

  Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuimarishwa kwa kitengo cha (TEMESA) kwa kupeleka mafundi watakaomudu kufanya matengenezo ya magari wilayani huko ili kupunguza gharama za kusafirisha magari hadi makao makuu ya mkoa wa Pwani kwa matengenezo pale yanapohitaji matengenezo.

  “Namna nyingine mnayoweza kufanya ni kuomba kibali maalumu cha kuruhusiwa kufanya matengenezo ya magari hayo kwenye karakana za watu binafsi zenye mafundi wenye sifa zinazotambulika na Serikali ili badala ya kuyapeleka Kibaha kwa matengenezo,” alisema.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Ndikilo ameiomba Serikali kuipa kipaumbele hospitali ya wilaya hiyo yenye kuhudumia wananchi zaidi ya 50,000 ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu, dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

  “Kwa wilaya ya Mafia mgonjwa anapokosa dawa au vipimo maana yake aende Dar es Salaam au Rufuji au Mkuranga kufuata huduma hizo. Jambo hili linawagharimu sana wananchi hasa wa hali ya chini. Naiomba Serikali ituangalie  kwa jicho la huruma,” alisema.

  Mkuu huyo wa mkoa alitaja changamoto nyingine inayowakabili wananchi wa wilaya hiyo kuwa ni usafiri wa majini kutokuwa na uhakika kutokana na kukosekana kwa meli rasmi ya abilia yenye usalama na staha.

  Alisema kwa sasa wananchi wengi wanasafiri kwa kutumia majahazi na boti ndogo ambazo si salama na kwa sababu hiyo aliiomba Serikali kutafuta namna ya kutatua tatizo hilo linaloikabili wilaya hiyo kwa muda mrefu.

  Naye Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi 469 katika kada za afya, elimu barabara, maji na utawala.

  0 0

  Kaimu Meneja Miradi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuka akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita Simon Berege katika maonesho yanayofanyika mkoani humo katika Mkutano Mkuu wa ALAT.
  Ofisa Mawasiliano TEA, Sophia Asad akitoa maelezo katika maonesho wakati wa Mkutano Mkuu wa ALAT.
  Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Sylvia Lupembe akimweleza jambo Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene kwenye maonesho yaliyofanyika katika Mkutano Mkuu wa ALAT mjini Musoma.

  0 0


  Maandalizi ya Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika kesho Septemba 25 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku ushiriki wa wa wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu kwenye mbio hizo ukitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

  Mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza zikiwa na baraka zote kutoka Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) , zikilenga kilenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio vilivyoko kanda Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Msemaji wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.

  Alisema wanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1200 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.

  “Rock City Marathon inahusisha mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake, mbio za Kilometa tano zitakazohusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee, mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 pamoja na mbio fupi za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi,’’

  “Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB, New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.

  Kuhusu barabara zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12:00 asubuhi Bw Kasonta alisema; “Kwa washiriki wa mbio za km 21 wataanzia Uwanja CCM Kirumba, kwa wale wa Km 5 wataanzia barabara ya Nyerere eneo la Polisi Mabatini, kwa wale wa Km 3 ambazo ni mbio za wazee wataanzia Barabara ya Nyerere eneo la Makaburi ya Wahindi na kwa mbio za watoto yaani Km 2 wao wataanzia eneo la Mwaloni kuelekea CCM Kirumba,’’

  Kwa upande wa zawadi kwenye mbio hizo Bw Kasonta alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. mil 1.5/- kila mmoja, sh. 900,000/- kwa washindi wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.

  “Kwa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.,’’

  Akizungumzia usalama katika tukio hilo ambalo litahusisha maelfu ya watu, Mwenyekiti Msaidizi wa kamati yam bio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na jeshi la polisi na jeshi la hilo limeshajipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo ili kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama wakiwemo watazamaji na washiriki mbio hizo.

  0 0

  kina
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai, wakati Spika alipofika kumsalimia, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Septemba 24, 2016. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa  Octoba 2016.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa REA katika Wilaya ya Kasulu.

  Waziri Muhongo yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Martin Mkisi.

  Prof Muhongo, akiambatana na Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo, wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.

   Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo 29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa wingi kwenye  mafunzo yatakayotolewa na Tanesco kuhusu umeme wa REA.

  Pia amewaagiza wakandarasi kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza siku hata moja. 
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
  Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi. 

  0 0

   Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Pogba akishukuru Mungu kwa kuweza kuapa bao lake la kwanza na la nne kwa timu yake ilipocheza na kuibanjua Leicester City ambao ni mabingwa watetezi bao 4-1 nyumbani kwao Old Trafford.
  Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Pogba akiogelea ndani ya dimbwi la furaha la mashabiki wa Man United.

  0 0

   
   Wachezaji wa Liverpool wakifurahia ushindi wao wa bao 5-1 dhidi ya Hull uwanjani kwao Anfield leo

   Coutinho akilenga nyavu ndogo kuandika bao la nne kutoka mita 25

  Kocha Jurgen Klopp akifurahia ushindi, ila safari hii kimyakimya...

  Coutinho na Roberto Firmino wakifanya utani baada ya wote kutingisha nyavu

  0 0

  Timu ya Kijitonyama Veterans, kesho Jumapili, itapambana na timu ya Warioba Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Kijitonyama maarufu kwa jina la uwanja wa Bora au “Emirates" jijini Dar es salaam.
  Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto Omary.
  Mbali ya mechi hiyo ya asubuhi, Kijitonyama Veterans pia jioni itapambana na timu ya Sinza Veterans katika mchezo mwingine wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo huo.
  Majuto alisema kuwa mechi zote mbili  ni sehemu ya kujiweka fiti kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya ligi ya timu za veterans iliyopangwa kuanza baadaye mwezi huu kwa  Manispaa ya Kinondoni. Alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo na kuahidi ushindi.
  “Tupo vizuri kwa ajili ya mechi zote mbili na hii inatokana na kuwa na kikosi kikubwa ambacho , tumejiandaa vyema na tunaahidi kufanya vyema katika mchezo huu,” alisema Majuto.
  Kocha mchezaji wa timu ya Warioba Veterans, Barnabas Emilio alisema kuwa wamejiandaa kulipa kisasi kwa Kijitonyama Veterans ambao katika mechi ya mwisho walifungwa mabao 3-0.
  “Tumedhamilia kulipiza kisasi katika mchezo huo, tunajua utakuwa mgumu, ila tumejiandaa kwa ajili ya mechi hiyo na ushindi ni lazima,” alisema Barnabas.
   Kikosi cha Kijitonyama Veterans
  Kikosi cha Warioba Veterans

  0 0

   Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali wa Jimbo la Segerea,Salma Fumbwe,akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (kushoto) katika semina ya ujasiriamali ya wanawake iliyofanyika ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima,jijini Dar es Salaam,leo. Kauli Mbiu ni Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi”.

   Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar  es Salaam leo.
   Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar  es Salaam leo.
   Mkufunzi wa Kujitegemea,Albert  Magonga,akitoa mojawapo ya mada ya kuwawezesha wanawake wajasiriamali kukua kiuchumi kupitia biashara zao.

   Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya Equity, Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa mapato.  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga  Mpina amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa kuhakikisha fukwe zote za kigamboni zinafanyiwa usafi na kuwa katika hali ya kuridhisha.

  Naibu Waziri Mpima ameseyasema hayo leo katika maeneo ya fukwe za kigamboni aliposhiriki katika siku ya  usafi kitaifa ya mwezi wa September.

  Amesema fukwe za kigamboni ni chafu sana na usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni hauridhishi, “pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kusafisha mazingira leo fukwe ni chafu na wengine wanatuangalia tunavyosafisha huku wakiendelea na shughuli zao, Angalia wale wavuvi kwenye mitumbwi yao wanaendelea na kazi zao na wao ndo wachafuzi wakubwa huko baharini na nchi kavu. “Alisema.  Mpina amemtaka mkuu wa wilaya hiyo kuwawajibisha viongozi walioko chini yake kwa kosa la uzembe wa ufuatiliaji wa sheria ya mazingira kabla hajawajibishwa yeye. “kiongozi mzembe afukuzwe kazi kabla haujafukuzwa wewe na kuingia kwenye matatizo.” Alisisitiza naibu waziri Mpina.

  Hata hivyo Naibu Waziri Mpina alimpongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda kwa kuanzisha kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘’MTI WANGU’’ na kuwashauri wakazi wa jiji kushiriki Katika siku ya uzinduzi na kuahidi kuwa pamoja nao siku hiyo.  Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa ameelezea jitihada za usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni ikiwa ni pamoja na mashindano ya usafi wa mazingira na kuwataka wakazi wa kigamboni kuongeza jitihada za kutosha kuiweka kigamboni safi.

  Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi ni siku maalum ya usafi ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais la Usafi wa mazingira ambapo mwezi huu kitaifa imefanyika Kigamboni.

   Naibu waziri wa Nchi ofis ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina akifanya usafi na wananchi wa wilaya ya kigamboni katika kutekeleza agizo la Mh. rais la kila mwisho wa mwezi kufanya usafi.      
  Naibu Waziri wa Nchi ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa na wananchi wa kigamboni waliojitokeza kwaajiri ya kufanya usafi katika fukwe za kigamboni                      

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari,hawapo pichani mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika fukwe za wilaya ya kigamboni.                 


older | 1 | .... | 1366 | 1367 | (Page 1368) | 1369 | 1370 | .... | 3282 | newer