Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

MABADILIKO YA RATIBA VPL, YANGA VS JKT RUVU OKTOBA 26.

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BODI ya Ligi kupitia Shirikisho La Mpira wa Miguu Nchini TFF, limetangaza mabadiliko ya ratiba ya ligi na kutangaza tarehe ya mchezo namba 1 wa kiporo baina ya Mabingwa wa Ligi Kuu Vodacom Yanga na JKT Ruvu.

Mchezo huo iliokuwa wa ufunguzi wa ligi ulishindikana kuchezwa Agosti 21 baada ya Yanga kuwa na mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe Nchini Kongo.

Bodi ya ligi imeupeleka mchezo huo hadi Oktoba 26 ambapo ahapo awali walisema kuwa watatangaza ni lini utachezwa, na katika hilo  mchezo namba 57 baina ya Mwadui na Azam, mchezo namba 60 TZ Prisons na Simba utachezwa Novemba 09, mchezo namba 59 Yanga na Ruvu Shooting utapigwa Novemba 10.

Mchezo namba 69, Yanga na Mtibwa utachezwa Oktoba 13, mchezo namba 97 Kagera na Azam utapigwa Oktoba 28 na katika mchezo namba 100 baina ya Yanga na Mbao , namba 102 Toto na Mtibwa Sugar  utapigwa Oktoba 30, Mtibwa na Mbeya City mchezo namba 113 na namba 115 kati ya Mwadui na Majimaji zote zitapigwa Novemba 07.

Utafiti: Misitu na mazingira vikisimamiwa ipasavyo vitaboresha maisha ya wananchi vijijini.

0
0
Dr. Nicole Cross-Camp ambaye ni Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha East Anglia cha nchini Uingereza chini ya mradi wa ESPA (Ecosystem Services for Poverty Alleviation) akitoa mada kuhusiana na matokeo ya utafiti kuhusu changamoto wanazozipata wanakijiji katika utunzaji wa misitu kwa wadau kutoka Wizara mbalimbali pamoja na Sekta binafsi.

Wadau wa Mistu na Mazingira kutoka Serikalini, Taasisi na Mashirika binafsi walikutana na watafiti hao ili kujadili matokeo hayo ya utafiti na kuweza kuchanganua mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto na faida zinazotokana na usimamizi wa misitu kwa wanajamii wanazozungukwa na hifadi ya misitu hapa Tanzania.

Akizungumza na Lasima Nzao na Dr Nicole Gross-Camp walisema kuwa utafiti huo uliofanyika katika vijiji nane vya wilaya mbili, halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini na wilaya ya Kilwa kuanzia Septemba 2014 na kumalizika september 2016 na ulikuwa "unaangalia mchango wa misitu inayosimamiwa na Jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maisha kwa wanakijiji husika". 

Utafiti unaonyesha  kuwa mistu na mazingira ikisimamiwa  ipasavyo inaweza kuboresha maisha ya wananchi walio vijijini kwa kuwa wanajamii wanapenda mfumo wa misitu ya jamii japokua bado kuna changamoto nyingi katika usimamizi wa misitu kwa wanajamii hasa misitu inayosimamiwa na Jamii.

Utafiti huo ulidhaminiwa na ESPA, UKAID, NERC na ESRC na ulifanywa na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha East Anglia UEA nchini Uingereza Dr Nicole Gross-Camp akishirikiana na mtafiti kijana wa kitanzania, Lasima Nzao ambaye pia alikua meneja wa mradi wa Utafiti huo.
Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya akichangia mada baada ya wataalamu kuwasilisha utafiti uliofanyika katika vijiji nane ndani ya wilaya mbili.

MSHINDI WA NZAGAMBA AONDOKA NA NG'OMBE WILAYANI MUSOMA

0
0
Mshindi wa shindano la kunywa Nzagamba ushinde mkoa wa Mara, Majani Manyama (alieshika kofia mkononi) akikabidhiwa zawadi ya Dume la Nzagamba toka kwa mkuu wa kiwanda cha Nzagamba kanda ya ziwa, Helbert Ilembo mara baada kuibuka mshindi katika droo iliyocheshwa kwenye kitongoji cha Bukima wilayani Musoma mkoa wa Mara. kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa kinywaji cha Nzagamba kanda ya ziwa, Peter Mwambenja mwenye kofia nyekundu na katikati ni meneja mauzo ndugu James Makala.

Mmoja wa wateja wa kinywaji cha Nzagamba mkoani Mara akiwa amefungwa kitambaa usoni ili kuvuruga kuponi za shindano la Nzagamba na baadaye kumchagua kuponi moja iliyopelekea Ndugu Majani Manyama aliibuka kuwa mshindi wa dume la Ng'ombe (Nzagamba) lililofanyika katika Eneo ya Bukima wilayani Musoma mkoa wa Mara. Kushoto ni Meneja mauzo na usambazaji wa kinywaji cha Nzagamba kanda ya ziwaPeter Mwambenja na baadhi ya wateja wa eneo hilo.
Mmoja kati ya watumiajai wa Kinywaji cha Nzagamba mkoani Mara akifurahia kinywaji hicho wakati wa kufanyika kwa Droo ya kumtafuta mshindi wa shindano la Kunywa Nzagamba ushinde Dume la Ngombe, lililofanyika katika Eneo ya Bukima wilayani Musoma mkoa wa Mara.

TSN Kudhamini Pambano la Kuchangia waathirika wa Tetemeko la Ardhi.

0
0

Na Daudi Manongi,MAELEZO


Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) imejitolea kudhamini pambano la kuchangia waathiriwa na tetemeko la Ardhi Kagera litakalofanyika siku ya Jumapili saa tisa kamili kati ya Wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva katika uwanja wa Taifa.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara wa kampuni hiyo Bw.Jahu Mohamed Kessy wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

“Sisi kama Tanzania Sisi Nyumbani(TSN) tumejitolea kudhamini pambano hili kwa kushirikiana na wasanii hawa kwa kuwa tumeguswa na janga hili na hivyo mbali na michango mbalimbali tukaona ni vyema tujitolee kuwapa Mipila na Jezi kwa wasanii hawa ili kuhamasisha uchangiaji huu ”Aliongeza Bw.Kessy.

Aidha Bwana Kessy alisema kuwa wao kama TSN wanaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti, kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji huu kwa pamoja.

Pia amewataka wananchi,mashirika na makampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa kagera waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo la Ardhi.

Kwa upande wake mwakilishi wa Bongo Movie Bw.Steve Nyerere amesema kwamba wao kama bongo movie wameguswa na jambo hili na ndio maana wamejitokeza kutumia vipaji vyao ili kile kitakachopatikana ili kiweze kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Kagera.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kushoto ni Kapteni wa Timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu.
 Mwakilishi wa Timu ya Bongo Fleva, Kalapina (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, wakati makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy na Mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Movie Jimmy Mafufu, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera. Kulia ni mwakilishi wa Bongo Movie Steve Nyerere.
 Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Bongo Fleva M2 the P, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Meneja Uhusiano na Mauzo wa Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (tsn) Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi vifaa vya michezo wawakilishi wa Bongo Movie na Bongo Fleva  kwa ajili ya mechi maalum kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Septemba kwa lengo la kusaidia Waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Picha na Frank Shija, MAELEZO.

CDF TROPHY YAANZA KWA KASI LUGALO GOLF CLUB

0
0
Selemani Semunyu JWTZ

Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa Mchezo wa Golf CDF Troph imeanza kwa Michezo ya awali ambapo  Wapiga mikwaju wa kulipwa wamechuana vikali huku Geofrey Reverian  na Klabu Lugalo na Farai Chitengwa  wa Zimbambwe wakilazimika kurudia mchezo baada ya kufungana.

Katika mashindano hayo yanayofanyika katika Uwanja wa Lugalo Golf Club Jijini Dar es salaam wamefungana  mikwaju ya jumla (gross) 72 kwa kila mmoja na kulazimika kutakiwa kurudia mchezo kwa kucheza viwanja vitatu hali itakayoamua nani kuibuka mshindi katika kundi la wapiga mikwaju wa kulipwa.

Katika nafasi ya tatu ya Wapiga Mikwaju hao wa  kulipwa imechukuliwa na Salim Mwenyenza aliepata mikwaju ya Jumla 74 ikiwa ni kati ya wachezaji wa kulipwa 20 walioshiriki katika kinyanganyiro hicho ambacho mshindi atajulikana jumamosi Septemba 23 mwaka huu.

Katika hatua Nyingine wacheza Golf wa kundi la Wachezaji Wasaidizi (Carde) 30 walipambana kupata mbabe wa kundi hilo ambapo Richard Mtweve aliibuka na ushindi kwa kupata Net 69 baada kupigaMikwaju ya Jumla 76  huku akicheza kwa kiwango cha Saba.

Nafasi ya  pili imechukuliwa na Rasuri Shaban baada ya kupata Net 70 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 79 huku kiwango cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na Mwanamke pekee kwa kundi hilo Rose Nyenza kushika Nafasi ya tatu baada ya kupata net ya 87 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 111 na kiwango cha Uchezaji kikiwa ni 24.

Michezo hiyo ya Kombe la Mkuu wa  majeshi ya Ulinzi CDF Trophy yanatarajiwa kuendelea na kufikia tamati Jumamosi Septemba 24 katika Uwanja wa Golf wa Lugalo ambapo wachezi wa makundi matatu watachuana.

Makundi hayo ni Senior,Junior, Ladies na  Daraja la A Daraja B na daraja C  ambapo mbapo pia mshindi wa Jumla atapatikana kutoka katika Makundi hayo.

Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo ya Kombe la Mkuu wa majeshi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda.
Mwenyekiti wa Klabu ya golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo (Katikati) akiangalia mazoezi ya wachezaji wa Klabu hiyo wanaotaraji kushuka Uwanjani kuwania CDF Trophy.
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akikata utepe kuzindua Daraja la Kiwanja namba Tisa cha Golf Lugalo ikiwa ni sehemu ya kuboresha uwanja huo na kuwa na sifa zaidi kwa mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kimataifa. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).

PPF YAWATAKA WASTAAFU KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UHAKIKI LINALOENDELEA NCHINI.

0
0
 

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

MFUKO wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) umewataka wanachama wastaafu wa mfuko huo PPF kujitokeza katika zoezi la uhakiki linaoendelea na kumalizika nchini kote tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandsihi wa habari leo jijini Dar es salaam Meneja Kiongozi wa Shughuli za Pensheni na Huduma kwa Wanachama, John Mwalisu alisema uhakiki huo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi za wanachama wanaolipwa pensheni kupitia mfuko huo.

Mwalisu alisema zoezi hilo la kuhakiki wa wastaafu lililoanza Septemba 12 hadi Septemba 23 mwaka huu katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar ni endelevu na linatarajia kuendelea mikoani kuanzia Septemba 26 hadi octoba 28 mwaka huu.

Alisema katika zoezi hilo kila mstaafu anatakiwa kwenda na nyaraka kamili za uanachama ikiwemo Kitambulisho cha mstaafu cha PPF, picha ndogo ya rangi, nakala ya kati ya kitambulisho cha Taifa au kadi ya mpiga kura, hati ya kusafiria au leseni ya udereva.

Aliongeza kuwa awamu ya pili ya zoezi hilo litahusisha mikoa ya kanda ya kati ambayo ni Morogoro, Dodoma na Singida kati ya tarehe 26 hadi 30 Septemba mwaka huu, wakati katika mikoa ya kanda ya Ziwa zoezi hilo litaanza Octoba 3 hadi octoba 7 ikihusisha mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera.

Katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini zoezi hilo la uhakiki wa wastaafu litaanza octoba 17 hadi octoba 21 mwaka huu na katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro zoezi hilo litaanza Octoba 24 hadi Octoba 28” alisema Mwalisu.

Aidha ,alisema kuwa zoezi la ukakiki wa wastaafu hao kwa mikoa ya ya Dar es salaam, Pwani na Zanzibar limemalizika Septemba 23 mwaka huu na kutoa wito kwa wanachama wastaafu katika mikoani inayofuata kuonyesha ushirikiano katika zoezi hilo la uhakiki.

Naye Meneja Uhusiano Mfuko huo, Lulu Mengele alisema kuwa katika kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi, PPF imeanzisha mfumo maalumu wa kuchangia (WOTE SCHEME) unaohusiha sekta rasmi na isiyo rasmi kwa lengo la kukidhi mahitaji na kutambua mchango wa wanachama katika uchumi wa nchi.

Aliongeza kuwa mfumo huo pia unatoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi kuweza kunufaika ili kuweza kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Akizungumza kuhusu mfuko wa Wote Scheme, Mengele alisema wanachama wa mfuko huo kuwa ni pamoja na wakulima, mama lishe na wajasiriamali wadogowadogo ambapo kiwango cha chini cha kuchangia kwa kila mwezi ni Tanzania shilingi 20,000.

Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni PPF, John Mwalisu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki wa wanachama wastaafu wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu Mengere.
Meneja Uhusiano wa Uhusiano wa PPF Lulu Mengere akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uhakiki wa wanachama wastaafu wa mfuko huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Janeth Ezekiel na Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo, John Mwalisu.
Waandishi wa habari wakimskiliza Meneja Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu Mengere (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija, MAELEZO.

INTRODUCING "JIRANI" BY WITNESZ KIBONGE MWEPEC & OCHU SHEGGY Ft SNURA & MZEE YUSSUF

PANAFRICAN ENERGY YATOA MSAADA KWA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

0
0
Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya PanAfrican Energy Tanzania imekabidhi msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 saruji kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Kagera. Msaada huo uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu ofisini kwake ni kutoa mkono wa pole kwa wana Kagera kwa maafa yaliyowakumba takribani siku kumi zilizopita. 

Akikabidhi msaada huo Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfriacan Energy Tanzania Limited Bwana Andrew Kashangaki alisema, “Kwa niaba ya Kampuni ya PanAfrican Energy tunatoa pole kwa watanzania wenzetu wana Kagera kutokana na janga lililowakumba ndugu zetu na kuwahakikishia tupo pamoja katika hili.Kwa uzalendo mkubwa tumeguswa na yaliyowapata wenzetu na hasa kupata uharibifu mkubwa wa mali na mbaya zaidi kupoteza uhai wa baadhi ya watanzania wenzetu pia kupata majeruhi. 

Hili ni janga letu sote kwa kuguswa na hili tumekabidhi mifuko 5000 ya saruji na mabati 1900 ambayo tunaamini yatasaidia kufanyia marekebisho baadhi za nyumba zilizoathiriwa na tetemeko. Kwa hiki kidogo tunaomba kiwe kama faraja kwenu na tunawahakikishia hatutaishia hapa tutaendelea kusaidia kadiri ya mahitaji ya wenzetu hasa katika elimu yaani kufanyia ukarabati baadhi za shule zilizoharibika vibaya. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PanAfrican Energy Patrick Rutabanzibwa aliushukuru uongozi wa mkoa wa kagera kwa namna wanavyozidi kujaribu kutatua changamoto wanazopitia waathirika wa tetemeko ardhi. Alielezea namna wanavyojitokeza kusaidia shughuli za kijamii, “Kampuni yetu inashughulika na utafutaji, uchimbaji, uendelezajii na usambazaji wa gesi asili ya Songo Songo.

Kampuni ilianza shughuli hizi mnamo Mwaka 2001 na uzalishaji ukaanza 2004. PanAfrican Energy (Tanzania) inafanya miradi ya maendeleo ya kiuchumi, kisheria na kimaadili, katika kutatua matatizo ya jamii zetu na kujitolea uwezo wetu, rasilimali na watu katika kujenga maisha bora ya baadaye kwa wote. Miradi ya PanAfrican Energy (Tanzania) itatathiminiwa na kukubaliwa katika misingi ya kudumu kwenye sekta ya elimu, afya na uwezeshwaji wa jamii. 

Tunaamini huu ni mwanzo wa kushirikiana na wewe. Tumeweza kutembelea sehemu mbali mbali na kuona shule zilizopata uharibifu mkubwa na tunaahidi kwamba tukirudi Dar es Salaam tutawasilisha ujumbe huu na kwamba bado msaada unahitajika kurudisha shule zetu kwenye hali ya kawaida.” 

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu aliishukuru Kampuni ya PanAfrican Energy kwa msaada wa vifaa vya ujenzi waliowapatia na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kusaidia. 

“Hii inadhihirisha ni jinsi gani watanzania tulivyo na umoja na upendo, kwa niaba ya wana Kagera na Serikali kwa ujumla natoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa msaada huu mkubwa militupatia wa vifaa vya ujenzi. Bado tunahitaji msaada zaidi kwani athari iliyotokea ni kubwa sana kuachilia vifo vya wenzetu 17 bado majengo mengi yameathirika vibaya kwani majengo 2072 yamebomoka kabisa, zaidi ya 40,000 yapo katika uharibifu hatarishi na 9000 yana mipasuko”. 

Msaada huo ulitolewa mara baada ya mkoa wa Kagera kupatwa na tetemeko la ardhi lililotokea takribani siku kumi zilizopita.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu akimshukuru Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfriacan Energy Tanzania Limited Bwana Andrew baada ya kukabidhiwa msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 yasaruji kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu akizungumza jambo na uongozi wa kampuni ya PanAfriacan Energy Tanzania Limited baada ya kukabidhiwa msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 yasaruji kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu akimshukuru Patrick Rutabanzibwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Pan African Energy baada ya kukabidhiwa msaada wa mabati 1900 na mifuko 5000 yasaruji kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

LOWASSA AISIFU SERIKALI URATIBU MAAFA KAGERA

0
0

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leo ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa wake
Na Mwandishi Wetu-KAGERA.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.

Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.

“Napenda nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.

Adha Mhe. Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.

Katika kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.

“Tunashukuru watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema  Meja Generali Salum Kijuu.

WAASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA JIJINI DAR

0
0
Wastaafu wa Jeshi la Magereza wakiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam wakiwa wameongozwa na Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile wakielekea Jukwaa Kuu kupokea Salaam ya Heshima. Hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza imefanyika leo Septemba 23, 2016.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa katika Jukwaa Kuu akipokea Salaam ya Heshima kutoka kwenye Gwaride Maalum la kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akikagua Gwaride Maalum la kuwaaga Wastafu wa Jeshi la Magereza lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza.

NHIF YAFANYA MABORESHO YA BEI ZA HUDUMA ZA AFYA WANAZOTOA

0
0
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya bei za huduma za afya zinazotolewa na mfuko huo ikiwemo huduma ya upasuaji na ada ya kumuona daktari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amesema kuwa kutokana na maboresho hayo baadhi ya huduma zimepanda bei, nyengine zimeshushwa bei na nyengine hazijabadilishwa bei ili kumuwezesha mtumiaji wa huduma hizo kuzimudu gharama na kupata huduma zilizo bora.

Aidha Konga amesema kuwa mabadiliko ya bei na mabadiliko ya aina za huduma hazitaathiri ubora wa huduma wala uwezo wa mwanachama kuhudhuria vituo vya matibabu pindi atakapohitaji huduma kwa kuwa huduma za afya zinazingatia taratibu za tiba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Masuala ya Kitaalamu, Dkt. Aifena Mramba amesema kuwa mabadiliko makubwa ya upandaji wa bei yamefanyika kati ya yale yaliyopita na ya sasa ikiwemo upasuaji wa moyo na vipimo vya moyo umeongezeka bei pamoja na upasuaji wa uzazi na kufunga mirija ya uzazi nao umeongezeka kutokana na tathimini zilizofanyika katika soko na watumiaji wa huduma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza na waandishi wa habari juu ya maboresho ya bei za huduma za afya zinazotolewa na mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Christopher Mapunda.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Masuala ya Kitaalamu (NHIF), Dkt. Aifena Mramba akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bernard Konga.

KC GLOBAL LINKS LTD YOUR NUMBER ONE SOLUTION FOR SHIPPING AND ALL PURCHASES FROM THE UK

0
0
WE SHIP ALL TYPES OF CARGO FROM UK TO AFRICA AT UNBEATABLE RATES
40’ CONTAINER TO DAR/MOMBASA FROM £1,450
20’ CONTAINER TO DAR MOMBASA FROM £950
ANY CAR TO MOMBASA £750 (SIZE DOESN’T MATTER)
ANY VAN TO MOMBASA £900 (SIZE DOESN’T MATTER)
AIR CARGO TO DAR £3.50 PER KG INCLUSIVE CLEARANCE
AIR CARGO TO DAR £2.00 PER KG EXCLUSIVE CLEARANCE
AIR CARGO TO NAIROBI £3.50 EXCLUSIVE CLEARANCE
MZIGO KWA MELI £1.75  INCLUSIVE CLEARANCE
(CONTAINER ZINAONDOKA MARA MBILI KWA MWEZI)
YOU CAN BUY ANY ITEMS ON EBAY, AMAZON OR AUTOTRADER AND LET THEM DELIVER TO OUR OFFICE AND WE WILL DELIVER IT TO YOU WITHIN 5 DAYS
YOU CAN PAY US IN DAR ES SALAAM AT OUR AGENT OFFICE AND COLLECT YOUR PARCELL AT OU AGENT
WE ARE STILL LOOKING FOR A RELIABLE AGENT IN KENYA
OUR AGENT IN DAR
2nd Floor,Raha Tower, Bib Titi Road, Dar es Salaam
MBEYA BRANCH, MWANZA BRANCH and ARUSHA BRANCH TBA
NAIROBI BRANCH AND MOMBASA BRANCH TBA
UNAWEZA NUNUA CHOCHOTE UINGEREZA NA TUKAKUTUMIA MOJA KWA MOJA KWENYE OFISI ZETU HAPO JUU. UZITO HAIJALISHI NA UNAWEZA KULIPIA HUKO HUKO NYUMBANI
CONTACT US
KC GLOBAL LINKS LTD
SUITE 2 CLIPPER HOUSE, TILBURY DOCKS, RM18 7SG
CARGO COLLECTION  ANYWHERE IN LONDON IS FREE
WE  WILL SOON OPEN BRANCHES IN NORTHAMPTON, LEEDS, MANCHESTER, BIRMINGHAM, READING,  GLASGOW AND DUBLIN

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MHE. MRISHO GAMBO AONGOZA MKUTANO MKUU WA WADAU WA UTALII JIJINI ARUSHA

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,ameongoza mkutano mkuu wa wadau wa utalii wa Mkoa wa Arusha ambao umefanyika katika ukumbi wa AICC Arusha.Ambapo mambo mbalimbali yamejadiliwa kuhusu sekta hii ya utalii na kuangalia jinsi yakuikuza zaidi kwa miaka ya mbeleni.
---------------------------------------- 
Akizungumza na wadau hao alisema sekta hii ina changamoto mbalimbali zikiwemo za ongezeko la kodi ya utalii pamoja na kadi nyingine ndogondogo wanazotozwa pindi wakiwa na wageni wao.

“Najua wafanyabiashara wengi hapa wametishika sana nah ii kodi ya utalii ilioanza kutozwa hivi karibuni nakuwafanya muone kuwa biashara zenu zimeanza kuyumba kwa watalii kutotaka kufika tena nchini.”

Alisistiza kuwa kuna fursa mbalimbali katika sekta hii ya utalii ambazo zinaweza kukuza zaidi biashara hii nakuwavutia zaidi wageni kutoka nje napia ushirikishwaji wa wadau wa utalii na Serikali ni kitu chamuhimu sana ndio maana nimeamua kuandaa huu mkutano ili tuweze kuanzimia mambo mbalimbali kwa pamoja.

Akituoa ufafanuzi wa kodi wa utalii iliyoanza kutumika Julai 1,2016 mpaka Agosti 2016 ,Mkuu wa Kitengo cha elimu na mapato Euginia Mkumbo ,amesem kuna ongezeko la kodi kwa  kiasi cha  bilioni 5.8 ambayo ni asilimia 120 kutoka kwenye kodi za hoteli na utalii wakati  mwaka jana ilikuwa bilioni 2.5 kutoka kwenye kodi za hoteli tu.Aidha ongezeko hilo la kodi ya utalii imeonyesha kunaongezeko kubwa la mapato yaliyoingia Serikalini na wakati huo wageni wengi hawajapatwa na usumbufu wowote tokea kodi hii ya utalii ilipoanza kutumia.
Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo,amesema kuanzishwa kwa kodi hiyo ya utalii kwa upande wao haina shida isipokuwa hawakupewa taarifa mapema na taasisi husika iliwaweze kujipanga.

“Kwetu sisi hii kodi haina shida ila tatizo ni taarifa zimetufikia kwa gafla sana nakutufanya tukose mda wakujianda,”alisema Chambulo.

Pia  alilisitiza kwa Serikali kusimamia sheria zaidi ili wafanyabiashara wote wa sekta  waweze kulipa kodi  kuliko kwa sasa ni baadhi yao tu ndio wanalipa na wengine hawalipi.

Aidha aliomba utaratibu wa malipo kwa taasisi husika uwangaliwe upya kwani kwa sasa unamlolongo mrefu sana unaopelekea kuwachukua mda mrefu sana pindi wanapoenda kufanya malipo hayo au kodi zote zingewekwa kwenye fungu moja iliziweze kulipwa kwa mala moja.

Mambo mbalimbali yameadhimiwa katika mkutano huo ikiwemo kuimalisha ulinzi na usalama kwa watalii wote watakaoingia mkoani na pia litaanzishwa dawati maalumu lakusikiliza Changamoto mbalimbali zitakazo kuwa zinawakabiri wadau hao wa utalii nakuzitafutia ufumbuzi kwa haraka.




Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators bwana Wilbad Chambulo akifafanua jambo kwa wadau wa utalii waliohudhulia mkutano huo,Jijini Arusha.
Baadhi ya wageni waliohudhulia mkutano wa wadau wa utalii, uliotishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani) katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

JK ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI WA KISIASA NA UTETEZI

0
0





 Rais  Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akipokea Tuzo ya  Uongozi wa Kisiasa na  Utetezi kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa  Speak Up Afrika  Bi Kate  Campana,  katika hafla iliyofanyika siku ya Alhamis  New York Marekani. Tuzo hiyo  ni kutambua jitihada na juhudi zake za kufikisha huduma za jamii hususani  afya kwa   kwa wanawake na watoto.
 .Rais Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya  kupokea Tuzo yake akirejea kwenye kiti chake

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  baada ya kukabidhiwa Tuzo yake  na katika shukrani zake za kukubali   Tuzo hiyo, amesema Tuzo hiyo ni kwa watoto wote wa Afrika ambao ndio  wamemwezesha yeye kupata Tuzo .
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


TAARIFA KUTOKA TFF

0
0
KILIMANJARO QUEENS NEEMA TUPU
Ubingwa Kombe la CECAFA Chalenji kwa timu za mpira wa miguu za wanawake katika nchi za Afrika Mashariki, umewavutia wadau wengi kwa kiwango kikubwa hivyo kushusha neema kwa wachezaji hao wa timu ya taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Queens ambayo imeandika historia ya kutwaa taji hilo ikiwa ni taifa la kwanza katika mashindano hayo mapya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amefurahishwa na ubingwa wa timu hiyo akisema: “Si ubingwa tu, bali umefuta dhana ya Wakenya ambao siku zote wamekuwa wakitangaza Mlima Kilimanjaro uko kwao Kenya wakati upo hapa Tanzania. Kwa kuifunga Kenya, mmefanya kazi nzuri.”

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaanza wikiendi hii ambako katika kundi A, mchezo wa kwanza unapigwa leo Ijumaa Septemba 23, 2016 kwa kuzikutanisha timu za Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam na Pamba ya Mwanza katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Karume jijini.
Kwa mujibu wa ratiba, michezo mingine itachezwa kesho Septemba 24, 2016 kwa kuzikutanisha timu za Lipuli dhidi African Sports utakaofanyika Uwanja wa Kichangani mjini Iringa. Mchezo huo utakuwa ni wa kundi A wakati katika kundi B michezo itakuwa ni kati ya Kurugenzi ya Iringa dhidi ya KMC ya Kinondoni kwenye Uwanja wa Wambi ulioko Mafinga. Mlale JKT itaikaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

KAMATI YA KATIBA, SHERIA KUJADILI KESI 13 KESHO
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kesho Jumamosi Septemba 24, 2016 itasikiliza mashauri 13.
 Malalamiko hayo ni:
Mchezaji Ametre Richard ambaye atawasilisha mbele ya kamati makubaliano waliyokubaliana kukaa pamoja na kufikia mafaka. 
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

YANGA, JKT RUVU SASA KUCHEZA OKTOBA 26
Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Young Africans dhidi ya JKT Ruvu, sasa utachezwa Oktoba 26, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar s Salaam.
Pamoja na mchezo huo, Bodi imefanya mabadiliko katika baadhi ya ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom kama ifuatavyo ambako Mwadui na Azam sasa utachezwa na Novemba 9, 2016 siku ambayo Prisons itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Novemba 10, kutakuwa na mchezo kati ya Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting jijini Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

MAJALIWA AIPA SIKU 10 TAASISI YA HIFADHI YA BAHARI KULIPA DENI LA SH. MILIONI 100

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara mjini Mafia akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Pwani  Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku 10 kwa Taasisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu kulipa deni la sh. milioni 100 inayodaiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mafia.
Deni hilo linatokana na malimbikizo ya miaka mitatu ya maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo katika maeneo ya hifadhi ya bahari wilayani humo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo katika ukumbi Caltas akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi siku mbili.
“Waandikieni barua na muitume leo hii kwa njia ya mtandao (email) kuwajulisha kuwa wanatakiwa kulipa deni hilo ndani ya siku 10. Hakikisheni wanalipa deni hili ili Halmashauri iweze kufanya kazi zake vizuri,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona Halmashauri hiyo ikinufaika kutokana na vyanzo vyake vya mapato, hivyo haitakuwa tayari kuona ikihangaika.
Mbali na agizo hilo, Waziri Mkuun amesema atafuatilia kuona wajibu wa taasisi hiyo na mipaka yao ikiwa ni pamoja na kujua mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.
Awali mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ni kutolipwa kwa wakati fedha za maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na Taasisi ya Hifadhi ya Bahari.
Mkuu huyo wa wilaya ameiomba Serikali kuangalia upya majukumu ya taasisi hiyo na nafasi ya halmashauri katika kuendesha shughuli za uwekezaji pamoja na kupata mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.

Airtel yaipongeza Kilimanjaro Queens

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati),Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda (kushoto) na nahodha wa timu ya Kilimanjaro QueensSophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  na nahodha wa timu ya Kilimanjaro QueensSophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam . Asilimia kubwa ya wachezaji wa Kili Queens ni matunda ya mashindano ya Airtel Rising Star.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam. wakishuhudia ni  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (katikati) akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda
Timu ya wanawake Tanzania ya Kilimanjaro Queens ikiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Airtel na TFF wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel leo. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA




SERIKALI IMEJIPANGA KUMALIZA MGOGORO WA UWANJA WA NDEGE WA KIA - Prof Mbarawa

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi wanaozunguka eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inatafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro kati yao na mwendeshaji wa uwanja huo kampuni ya KADCO.

Prof Mbarawa amesema ufumbuzi utakaopatikana utakuwa na manufaa kwa pande zote na kujali maslahi ya Taifa.

"Msiwe na wasiwasi Serikali yenu ni sikivu, tutayakagua maeneo yote na kuangalia maslahi ya pande zote na kutoa maamuzi yenye manufaa kwa wote", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Mgogoro kati ya wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege wa KIA na kampuni ya KADCO ambao umekuwako toka mwaka 1998 umesababisha misuguano na hisia kali kwa muda mrefu hali iliyosababisha Serikali kuamua kuupatia ufumbuzi wa kudumu.

Waziri Prof. Mbarawa ametuma timu ya wataalamu kupitia eneo lote la uwanja wa ndege huo lenye kilomita za mraba 110 katika siku mbili kuanzia sasa ili kuangalia wadau wote walioko ndani ya eneo hilo, athari zake kwa uwanja na wananchi kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Amezungumzia umuhimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuilinda mipaka ya viwanja vyake na wananchi kujiepusha kuvamia maeneo ya viwanja ili kuepuka migogoro ya aina hiyo siku zijazo.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa ameitaka KADCO kuongeza mapato katika uwanja wa ndege wa KIA ambao ni wa pili kwa ukubwa hapa nchini ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuongeza mapato katika sekta zote za kiuchumi.

Amesema nia ya Serikali ni kuboresha viwanja vyote vya ndege nchini ili kuimarisha huduma ya usafiri wa anga.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa KADCO Eng. Christopher Mukama amesema KADCO inajiendesha kwa faida na kuhakikisha inaendelea na uboreshaji wa huduma ili kuvutia ndege nyingi kutumia uwanja huo.

Waziri Prof. Mbarawa yuko mkoani Arusha kukagua ujenzi wa miundombinu unaoendelea mkoani humo.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Muonekano wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua ujenzi wa miundombinu unaoendelea mkoani Arusha. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya KADCO Balozi Hassan Gumbo Kibelo.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya KADCO Eng. Christopher Mukama akitoa taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akisisitiza jambo kwa uongozi wa Kampuni ya KADCO na watendaji wa Wilaya ya Hai. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya KADCO Balozi Hassan Gumbo Kibelo na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw. Gelasius Byakanwa.

Serikali ya Jamhuri ya Korea kufungua Ubalozi Mdogo Visiwani Zanzibar

0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akizungmza na Balozi wa Jamhuri ya Korea Nchini Tanzania Bwana Song Geum Young (katikati) Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kushoto ni Msaidizi wa Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea  Bwana Songwon Shin.
Balozi wa Jamhuri ya Korea Nchini Tanzania Bwana Song Geum Young akifafanua jambo wakati akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images