Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1364 | 1365 | (Page 1366) | 1367 | 1368 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza  wakati  akifunga mkutano wa wadau  wa sekta ya mawasiliano wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa  Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016. 

   Baadhi ya wadau wa sekta ya mawasiliano wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani)  akizungumza wakati akifunga  mkutano wa wadau  wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa  Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  upande wa sekta ya Mawasiliano Mhandisi Clarence Ichwekeleza akitoa mada wakati wa Mkutano  wa   wadau  wa sekta ya mawasiliano wa kujadili  mkakati wa utekelezaji wa  Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 


  0 0

  TAASISI sita zikiwemo za dini na kijamii zimechanga jumla ya sh. milioni 172.5 zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu. Mchango huo umepokelea leo jioni (Alhamisi, Septemba 22, 2016) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. 
  Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Ian Ferrao alisema kiasi cha sh. Milioni 100 kimekusanywa kutoka kwenye mfuko wa Vodacom Foundation pamoja na wadau wao. Bw. Ferrao amesema kampuni ya Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidiana na Serikali katika uboreshaji wa miradi mbalimbali za kijamii..... 
  Taasisi nyingine iliyochangia ni Mfuko wa Pensheni wa LAPF ambapo Meneja wa Kaya ya Dar es Salaam, Amina Kassim amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 20. Pia Jumuiya ya Kiislam Ahmadiyya imekabidhi msaada wa sh. milioni 10 kati ya hizo sh. milioni nne ni fedha taslimu na zilizobaki ni mabati na mifuko ya saruji. 
  Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Advent, Dhruv Jog amemkabidhi Waziri Mkuu msaada wa tani 40 za saruji yenye thamani ya sh. milioni 16.5 na kusema kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari saruji hiyo imeanza kupelekwa Kagera. 
  Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya kimataifa ya Art of Living, Neetu Kulshreshtha wametoa msaada wa vyakula mbalimbali pamoja dawa vikiwa na thamani ya sh. milioni 10. Dk. Ave Maria Semakafu amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh milioni 16 kwa niaba ya makundi mawili ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp. 
  Makundi hayo yanaitwa Leaders na Uongozi. Akitoa shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa. “Tunashukuru sana kwa michango yote. Tunashukuru na makundi ya WhatsApp ya Leaders Forum na Jukwaa la Uongozi ambayo nayo yameamua kuja kutuchangia. 
  Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa,” amesema. Waziri Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. 
  Amewaomba wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao. Akaunti ya maafa imefunguliwa katika 
  Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz 
  na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni
   0768-196-669 (M-Pesa), 
  au 0682-950-009 (Airtel Money) 
  au 0718-069-616 (Tigo Pesa). 
   Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri. Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Meneja wa Kanda wa LAPF, Amina Kassim (kulia) na  Kafiti Kafiti wa LAPF  ukiwa ni mchango wa Mfuko huo  kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo  yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea sehemu ya  msaada ya vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Art of Living ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016.  Kutoka kushoto ni Nishitha Kulshreshtha,  Nishit  Patel,  Neha Movaliya,Sharik Choughule ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Shina la Pamba Road, Upanga  na Neha Movaliaya. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani  40 za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka  kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor (kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi ya  Advent ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba  22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.  0 0

  Na Benedict Liwenga-WHUSM, Bukoba.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba amewatoa wasiwasi waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea Wilayani Bukoba Mkoani wa Kagera.
   
  Mhe. Makamba ameyasema hayo leo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na tetemeko hilo kwa lengo la kuwapa pole waathirika na kuwap ujumbe wa Serikali kuhusu namna inavyojitahidi kuwasaidia waathirika hao.
   
  Amesema kwamba, wananchi wasiwe na wasi wasi kuhusu suala la kupatiwa misaada ya dharura kwani Serikali imejipanga na bado inaendelea na zoezi la kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea ingawa zoezi la kuwapatia baadhi ya huduma za msingi linaendele.
   
  “Tumekuja kutoa msaada kwa mji kwa ujumla wakati tunapanga namna ya kusaidia katika masuala ya mazingira na tambueni kuwa Serikali inawajali ndiyo maana kuna viongozi wakubwa wako hapa na wengine wanazidi kuja”, alisema Mhe. Makamba.
   
  Aliongeza kuwa, suala la kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo limepewa uzito mkubwa na Serikali na suala la kuchelewa kwa kutolewa kwa misaada kunatokana na umakini unaoendelea kufanywa sasa hivi na Serikali ili kuwatendea haki waathirika pekee.
   
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.
   
  Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika hao.
   
  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa na amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.
   
  Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akimpa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba leo 22/9/2016.
  maka2
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akiwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba leo 22/9/2016.
  maka4
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kulia) akimpa pole Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Ihunga Bw.Thomas Bonevanture mara alipowasili shuleni hapo kuwapa pole waathirika leo 22/9/2016.
  maka5
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo kwenda kuangalia maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi leo 22/9/2016 Wilayani Misenyi.
  maka6
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakiwapa pole baadhi ya waathirika wa tetemeko la ardhi Wilayani Misenyi leo 22/9/2016.

  0 0
  0 0

   Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akimpa pole mwalimu Anna Mollel wa shule ya msingi Ileega ambaye nyumba yake imebomoka kutokana na tetemeko la ardhi.
  kye8
  Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akikagua nyumba ya mwalimu Anna Mollel wa shule ya msingi Ileega ambaye nyumba yake imebomoka kutokana na tetemeko la ardhi.
  kye9
  Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na baadhi ya watoto wilayani Kyerwa wakati akiwa kwenye ziara kujionea madhara ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
  kye10
  Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na watoto wakati wa ziara ya kujionea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
  kye12
  Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akiongea na mkulima wa viazi wilayani Kyerwa Shakiru Issa wakati wa ziara ya kujionea maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera.


  0 0

   The Minister for Constitutional and Legal Affairs Dr. Harrison George Mwakyembe launches the decentralized births and deaths registration system for the under-five cohort in Iringa and Njombe Regions, today. 
  The Minister for Constitutional and Legal Affairs Dr. Harrison George Mwakyembe thanks Emmy Hudson Acting Chief Executive Officer of the Registration, Insolvency and Trusteeship Agency (RITA), responsible for the programme.
  The Minister for Constitutional and Legal Affairs Dr. Harrison George Mwakyembe (MP) launched the decentralized births and deaths registration system for the under-five cohort in Iringa and Njombe Regions, today. The exercise will benefit more than 200,000 under -five children in these two regions, reducing the backlog of unregistered children and establishing a system for registering all new births in the regions.

  The programme brings registration closer to the community by establishing registration points at health facilities, providing reproductive and child health services, and at the community ward executive offices in line with the government policy of decentralization through devolution.  This will enable parents in these two regions to have access to more than 700 registration points. Moreover, there will be more than 1,500 Registration Assistants to support the registration process.

  0 0

  Picha na habari na Lusungu Helela
  Afisa Habari Maliasili na Utalii
  Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inamshikilia Dereva Bw.  Emanuel Bisama  (37) ambaye ni  mkazi wa Kimara Suka Dar es Salaam,kwa kosa la kusafirisha magunia mawili ya mkaa ambayo baada ya kupekuliwa ndani yake  kulikutwa na viroba viwili vyenye uzito kilo 50 kila kimoja vikiwa vimejaa bangi.

   Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani , ACP. Bonaventura Mushongi  alisema  Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa  gari lenye namba za usajili T876 DDL  aina ya DAF Leyland  Bw. Emanuel Bisama (37) alikamatwa Septemba 21  saa 4.00 asubuhi  katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro akitokea Tunduma na kwa sasa yupo mbaroni  kwa mahojiano licha ya kukana kuwa hakujua kilichomo ndani ya magunia hayo.

  Kamanda Mushongi alisema walifanikiwa kumkamata wakiwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa mazao ya Misitu katika Barabara kuu ya Morogoro hadi Dare Salaam, aliongeza kuwa Dereva huyo wa gari amefunguliwa kesi CHA/RB/3039/2016 kwa kosa la kupatikana na bangi

   Kwa upande Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania (TFS) Kaimu wa Kanda ya Pwani Bw. Jonathan Mpangala alisema kuwa Mtuhumiwa huyo amefunguliwa kesi ya pili yenye CHA/RB/5113/2016 kwa kosa la kumiliki na kusafirisha mazao ya misitu bila kibali kwa sheria ya misitu namba 14 ya 2012 kifungu 88 na 89.

  Alisisitiza kuwa Operesheni ya kukamata usafirishaji wa mazao ya misitu bila vibali itakuwa ya kudumu baada ya kuona magari mengi hasa makubwa yakiwa yamepakiwa magunia ya mkaa kuanzia mawili hadi matano ambayo yamekuwa yakioneka waziwazi hata ukiwa  barabarani namengi yakiwa hayalipiwa ushuru wa Serikali kuu na hata magari mengine yakiwa hayajalipiwa ushuru wa Halmashauri

   Askari polisi wa kituo cha polisi cha Chalinze  akionesha viroba  viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja vilivyokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa  mazao ya Misitu yasiyo na kibali  katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Barabara kuu ya Morogoro wakitokea Tunduma wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL  aina ya DAF Leyland
   Gari lenye namba za usajili T876 DDL  aina ya DAF Leyland viroba  lililokutwa na viroba viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja  jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa  mazao ya Misitu yasiyo na kibali  katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Barabara kuu ya Morogoro wakitokea Tunduma


  0 0

   Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo (wa nne kutoka kulia) akiongoza kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
   atibu Msaidizi Tume ya Maadili (Kanda ya Kusini) Be. Muhuwa R. Kapangawazi akitoa mada kuhusu Maadili ya 
  Utumishi wa Umma na Tamko la Ahadi ya Uadilifu wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
   Kaimu Mshauri wa Kitaalamu Ofisi ya ushauri wa Mafuta na Gesi ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Emma Msaky, akitoa mada kuhusu utendaji wa ofisi yake wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016
  Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo (katikati mbele) na viongozi wengine pamoja na wajumbe wakipata picha ya pamoja baada ya kikao cha kawaida cha Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Ikulu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2016. PICHA NA IKULU

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Bw. Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
  Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipeana mkono na Msajili  wa Bodi hiyo Bw. Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba yake. Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhani akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika  mjini Musoma leo.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi alipotembe banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi na wadau mbalimbali nchini.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiangalia vipeperushi na machapisho mbalimbali kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 09/22/16--12:39: TANZIA


 • 0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Mkisi, akifungua Kikao kazi cha Kudhibiti Utumikishwaji wa watoto.

  Col Mkisi, akishiriki ktk kikao kazi na wadau wengine.

  Mkuu wa Wilaya Col Mkisi ktk picha ya pamoja na washiriki ktk kikao kazi cha Kudhibiti Utumikishwaji wa Watoto.
  *****************
  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col Martin Mkisi amefungua na kushiriki katika kikao kazi cha kubuni mikakati na usimamizi wa utekelezaji wa sheria za kudhibiti tatizo sugu wilayani hapa la utumikishwaji wa watoto.


  Mpango huo umeshirikisha watekelezaji wa sheria Wilayani( Law enforcers) kama vile: watendaji ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara, Mahakimu, polisi,Usalama na Maafisa Magereza.


  Mpango huo unaofadhiriwa na WEKEZA chini ufadhiri wa USAID,pamoja na mambo mengine, unalenga katika kupinga utumikishwaji wa watoto, ajira za watoto, utoroshaji wa watoto kwenda kufanya kazi hatarishi na mimba za utotoni, katika mikoa ya Tanga na Kigoma.


  Aidha,Washiriki ktk mpango huo, wameondoka na azimio la kwenda kukomesha tatizo hili sugu hasa ktk kata za Kagerankanda, Heru -Ushingo, Kitagata na Nyamidaho Wilayani Kasulu.

  0 0

  Waziri Mkuu Mhe.  Majaliwa Kassim Majaliwa akipokea Mfano wa hundi ya shilingi Milioni 16 kutoka kwa mratibu wa magrupu ya Whatsapp ya LEADERS NA UONGOZI, Dk. Ave Marie Semakafu katika hafla fupi ya makabidhiano hayo ambayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mratibu wa magrupu ya Wasap, Dk.Ave Marie Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachanachama wa magrupu ya Whatsapp ya LEADERS  FORUM NA JUKWAA LA UONGOZI   katika hafla fupi ya makabidhiano hayo ambayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam leo.
  ----------------------------------------------------
  Imedhihirika kuwa magrupu ya Whatsapp  yanaweza kuwa chachu ya Maendeleo  baada  ya wanachama wa magrupu mawili ya whatsapp ya LEADERS FORUM na  JUKWAA LA UONGOZI  leo Septemba 22, 2016 kumkabidhi Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa jumla ya shilingi  16m/-, kwa ajili kusaidia waathirika wa tetemeko  la ardhi mkoani Kagera.

  Akizungumza katika hafla hiyo, mmoja wa waratibu wa magrupu hayo Dk.Ave Marie Semakafu amesema fedha hizo ni michango ya wanachama wa magrupu hayo yenye jumla ya wanachama 491. Amesema wanachama hao wameguswa na yaliyowakuta Watanzania wenzao mkoani Kagera hivyo waliona njia pekee ya kuungana nao katika majonzi ya janga hilo ni kutoa kidogo walichonacho. 
  Dk Semakafu amewaasa watanzania wengine, hasa walioko kwenye vikundi mbalimbali hususani vya mitandaoni, kushiriki katika zoezi hilo la kuwachangia waathirika hao kwa vyovyote wawezavyo, maana hali bado ni mbaya mkoani Kagera. Hatua hiyo ni ya kwanza kwa magrupu ya mitandaoni nchini Tanzania kufanya harambee na kukusanya pesa kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
  Dkt Semakafu alisema madhumuni ya magrupu hayo ni kujadili maendeleo ya Taifa pamoja na kutoa ushauri mbinu mbadala kuifikia ndoto ya Tanzania tunayoiyaka.
  Tetemeko hilo lilitokea Septemba 10, mwaka huu ambapo watu 17 wamepoteza maisha,wengine zaidi ya 200 wameruhiwa,huku nyumba zaidi ya 800 zikiwa zimeharibika,zingine kuanguka. 
  Akiongea katika hafla hiyo Waziri Mkuu Majaliwa aliwashukuru wanachama wa majukwa hayo akisema wanapaswa kuwa mfano wa  kuigwa na makundi mengine nchini. 
   "Sisi kama serikali tunawashuru sana kwa moyo huo wa upendo kwa wenzetu wa Kagera,na hatutaishia hapa bali tutafanya hivyo kwa maandishi", alisema Waziri Mkuu na kuyaahakikishia wachangiaji waliokabidhi misaada yao leo yakiwemo  makampuni mbalimbali na vikundi vingine vitano kuwa atahakikisha misaada yote itawafikia walengwa.

  Wanachama wa majukwaa hayo ni watu wa kada mbalimbali hususani viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu,akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Mizengo Pinda.Wengine ni Mawaziri,Wabunge, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi, wanataaluma wa vyuo vikuu, wanahabari, Wafanyabiashara na Viongozi wa vyama vya Siasa.

  Waratibu wengine wa magrupu hayo ni Dereck Murusuli,Benjamin Thompson Kasenyenda,Leila Sheikh, Dr.Michael Francis, Maggid Mjengwa, Mustafa Ismail Kambona, Zamaradi Kawawa na June Warioba. 

  0 0

   Prime Minister Rt Hon. Kassim Majaliwa (left ) receives a dummy cheque  for 100M/= from Vodacom Tanzania Managing Director,  Mr. Ian Ferrao, the money donated by the company to help  earthquake  victims  in Kagera region. The handover of the money, held in Dar es Salaam today September 22,2016  was akso attended by the company’s  Chief Officer Corporate Affairs, Ms. Rosalynn Mworie
   Prime Minister Rt. Hon Kassim Majaliwa in a   jovial mood as he receives a dummy cheque  for 100M/= from Vodacom Tanzania Managing Director, Mr. Ian Ferrao to help victims and destruction caused by earthquake in Kagera region. 


   Prime Minister Rt. Hon assim Majaliwa holds talks with  Vodacom Tanzania Managing Director Mr. Ian Ferrao during the handover of the 100M/=  donated by the company  to help victims and  destruction caused by earthquake in Kagera region. 
  Prime Minister Rt. Hon Kassim Majaliwa shakes hands with Vodacom Tanzania Chief Officer Corporate Affairs, Ms Rosalynn Mworie shortly after the  donation of 100M/= by the company in Dar es Salaam today

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa Taifa Tanzania Disc Music Associatiaon (TDMA) Bw Asanterabbi Mtaki (kulia) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na maandalizi ya Tamasha la Salsa in Dar 2016 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi Octoba 1, 2016 katika ukumbi wa Highspirit lounge katika jengo la IT Plaza jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa balozi wa Cuba nchini Mhe. Jorge Luis Lopez  Tormo. Katikati ni DJ Charles Kandulu, kushoto  Naibu Makamu Mwenyekiti wa TDMA  DJ John Peter Pantalakis
   Naibu Makamu Mwenyekiti  wa TDMA  DJ John Peter  Pantalakis (kushoto) na  wakionesha CD  zenye nyimbo za Salsa na charanga akiwa na DJ Charles Kandulu, leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Taifa Tanzania Disc Music Associatiaon (TDMA) Bw Asanterabbi Mtaki  (kulia) akicheza  charanga na uongozi wa Tamasha la Salsa in Dar 2016 Dj John Peter Pantalakisa (kushoto) na Dj Ebony Moualim leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka,Glob ya jamii.

  0 0  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini  hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa  nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

  On the second full day of her various side events at the 71st United Nations General Assembly, more world leaders welcomed Zuriel to the debate and listened to her ideas on perhaps how to simplify the climate change challenge. She was received earlier in the afternoon by the leader of one of the countries most affected by the rising sea level - the Prime Minister of Tuvalu - H.E. Enele Sapoaga, where she continued to be a careful listener to the various challenges, before proffering simplifying the approach to dealing with the already established effects. Tuvalu is just 2000 feet above sea level.

  Later in the afternoon, she spoke at a session on Climate change at the UN.

  Earlier in the morning, 14 year old Zuriel was invited to the Equal Futures session organized by the State Department hosted by Secretary John Kerry and chaired by the President of Croatia. The initiative was started by President Obama 4 years ago, as a challenge to governments around the world to creating an enabling environment for women to participate in government, business, and civil society.
  She started her full day yesterday with one-on-one meetings with more world leaders, including the Prime Minister of Samoa and the Prime Minister of Jamaica.

  0 0  NA  TAKDIR ALI. MAELEZO ZANZIBAR.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuifanyia ukaguzi mitaala ya Skuli za binafsi ili kwenda sambamba na mitaala ya  Skuli za Serikali.

  Hayo ameyasema leo huko Uwanja wa Amani mjini Zanzibar wakati akihutubia wananchi  katika maadhimisho ya miaka 52 ya elimu bila malipo.

  Amesma mitala ya skuli za binafsi haiendi sambamba na ile ya serikali kitu ambacho hakipaswi ,hivyo amesema  ikohaja ya Wizara ya elimu namafunzo ya amali Zanzibar kushirikiana katika kuangalia mitaala miataala hiyo ya ufundishaji  ili iende sambamba  na skuli za serikali.

  Aidha amesema  mashirikiano ya pamoja yapande hizo mbili yatapelekea wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya majaribio na ile ya mwisho wa mwaka.

  Dkt. Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vyema katika kuhakikisha kwamba  inakabiliana na changamoto mbalmbali  zinazoikabili sekta ya elimu hapa Zanzibar ili kuhakikisha inafikia dhana ya Raisi wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alioitangaza Elimu bila malipo  mwaka 1964.

  Akiwazungumzia Wazazi juu ya suala zima laelimu kumpatia mtotoDkt. Ali Mohamed Shein amesema suala la elimu kwa mtoto hali mlazimu mwalimu pekeyake bali ni jambo la wote  ambalo linahitaji ushirikiano kati ya mwalimu wazazi na wanafunzi.

  Amesema wasiachiwe walimu pekeyao kufundisha na kuwaongoza bali wae na ushirikiano wa pamoja.

  Pamoja na hayo  Dkt.Ali Mohamed Shein alisema kabla ya Mapinduzi ya Mwaka1964  ilimu Zanzibar ilikuwa ikitolewa kwa misingi ya ubaguzi kituambacho kiliwafanya wonyonge kuikosa hakihiyo ya elimu  kitu ambacho  kwa sasa Zanzibar imepiga hatua kubwa mbele kwani upatikanaji wa elimu ni wakila mmoja ambae kafikia umri wa kwenda skuli.

  Ameseama haki hiyo sasa imefikiwa kukua nakwasaa kua na vyuo vikuu vitatu kwa ujumla wake mbapo kwa kiasi ya miaka 20 iliopita Zanzibar haikuwa na hata chuo kikuu kimoja na kupelekea wanaotaka kusoma kuenda nje ya Tanzania.
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi mara alipowasili katika   Maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu Bila malipo, sherehe zilizofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
   Wanafunzi wanawake wa Skuli ya Ben Bella Secondary wakiwa katika maandano kusherehekea miaka 52 ya Elimu bila Malipo sherehe zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
    Wanafunzi wa Skuli za Mkoa wa Mjini Magharibi wakibeba bango lilalotoa ujumbe kumpa “heko Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuimarisha Elimu na Michezo”wakati wa maandamano ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya Elimu bila Malipo,sherehe zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
   [Picha na Ikulu.] 23/09/2016.

older | 1 | .... | 1364 | 1365 | (Page 1366) | 1367 | 1368 | .... | 3272 | newer