Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TEASER JOTO LA ASUBUHI SEPTEMBER 22 ALHAMISI


DON'T MISS - PAMOJA CARNIVAL @ LEADERS GROUNDS IN KINONDONI, DAR ES SALAAM

$
0
0
*         CELEBRITY COOKOUT AND BBQ OUTDOORS
 
*         GAMES & ACTIVITIES (KIDS CORNER)
 
*         UPCOMING AND FUN TALENT COMPETITIONS
 
*         LIVE BAND AND KARAOKE CHALLENGE

ENTRY -
5,000 Kids/Students Ticket With download of Pamoja/Fasta Fasta Apps
10,000 Regular Ticket
15,000 Couples Ticket for 2 with pamoja/fasta fasta download
25,000 VIP Entry with Free After Party Access @ High Spirits from 9pm.

GRAB YOUR COLLEAGUES, FRIENDS AND FAMILY MEMBERS, YOU ARE ALL WELCOME!
WE HAVE FUN PAMOJA (TOGETHER) & HELP THE COMMUNITY!

DAR ES SALAAM AFYA CHECK

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI MHE. MASAUNI AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA - NAMANGA.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Hamad Masauni akisalimiana naAskari wa Uhamiaji katika kituo cha Uhamiaji cha Namanga, Mkoani Arusha wakati alipokwenda kukagua usalama wa mpaka huo ambapo aliwataka Askari hao kuendelea kufanya Oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu ambao watapita katika mpaka huo.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Hamad Masauni akitoka kukagua mojawapo ya ofisi ya Uhamiaji katika mpaka wa Namanga, Mkoani Arusha wakati alipokwenda kukagua usalama wa mpaka huo ambapo aliwataka Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Namanga kuendelea kufanya Oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu ambao watapita katika mpaka huo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Hamad Masauni akikagua mpaka wa Tanzania na Kenya (Namanga), Mkoani Arusha wakati alipokwenda kukagua usalama wa mpaka huo ambapo aliwataka Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Namanga kuendelea kufanya Oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu ambao watapita katika mpaka huo.Katikati ni Mkuu wa kituo cha uhamiaji Namanga, Abdalah Katimba na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Bw. Mwakipesile.

(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani)

Article 8

WABUNGE WA SIMBA NA YANGA KUPAMBANA SEPTEMBA 25 KUCHANGIA MAAFA KAGERA

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA RUVUMA YATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA BASI LA NEW FORCE

$
0
0

Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa ruvuma ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa ruvuma Dokta Binilith Mahenge amewatembelea majeruhi wa ajali ya basi la New Force waliolazwa katika Hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma wakipatiwa matibabu.

Article 5


MADEREVA 10 WA TANZANIA WALIOTEKWA NCHINI CONGO WAREJEA NCHINI

$
0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi  Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.

 Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistic ambayo magari yake na madereva walitekwa, Azim Dewj (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva hao.
 Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
 Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao. Kwa habari kamilio na picha zaidi BOFYA HAPA

KATIBU MKUU UJENZI ALIPOPOKEA NDEGE YA KWANZA YA BOMBARDIER Q400 NEXGEN

UJUE MWANDANI MWA SALUTI YA MAJI KWA VYOMBO VYA USAFIRI

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Utamaduni huu umekuwepo kwa siku nyingi, hata hapa Tanzania, lakini ujio wa moja ya ndege mbili aina ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kutoka Canada ndio kumezua maswali mengi kiasi hata ikabidi tufanye utafiti na kuja na majibu haya, maana upotoshaji na porojo vilitamalaki.



Kwa kawaida saluti ya maji (Water Canon Salutation) iliyofanyiwa ndege hiyo Jumanne Septemba 20, 2016 katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, hutolewa wakati wa sherehe za chombo cha usafiri kinapoanza kazi kwa mara ya kwanza ama kinapomaliza kwa mara ya mwisho.

Kwenye viwanja vya ndege magari ya Zimamoto husimama kila upande wa njia ya kupitia ndege na kuinyunyizia itapopita chini yake, huku maji yakiwa katika umbo la upanga wa sherehe kama ambavyo wanajeshi hufanya wakati za harusi ya ofisa mwenzao.
Kwa mujibu wa utafiti wetu, saluti ya maji hutumika kumuaga rubani mwandamizi aliyestaafu, mungoza ndege ama safari ya kwanza ama ya mwisho ya ndege kwenye uwanja fulani ama ndege.
Saluti za maji hutumika pia hata kwa meli na vyombo vingine vya majini vinapoanza ama vinapomaliza kazi ama wakati wa kustaafu kwa nahodha mwandamizi.

 Katika utafiiti wetu tumegundua kwamba hii ni utamaduni wa kawaida kwenye bandari ama viwanja vya ndege ila sio sheria ama lazima. Inasemekana ilianzishwa miaka ya nyuma katika bandari ya New York nchini Marekani wakati wa kukaribisha meli.
Mfano mwaka 1962 melivita ya SS France (baadaye ikaitwa Norway) ilipewa ukaribisho wa saluti ya maji, kitendo ambacho kwa kuwa kilikuwa cha kuvutia kiliendelea kila mara meli ngeni ama mgeni mkubwa akifika bandarini hapo.

Mwaka 1936 meli ya Unigereza RMS Queen Mary ilipata mapokezi hayo.

Na mbali ya kuwa saluti ya maji kuwa ya kusherehekea mwanzo ama mwishop wa chombo ama nahodha, zoezi hilo pia hutumika kufanyia majaribio vifaa hivyo vya kuzimia moto.

 New York Marekani
 Addis Ababa, Ethiopia
 New York, Marekani
 Dar es salaam, Tanzania
Kisiwa cha Malta

Rais Magufuli aipongeza Kilimanjaro Queens kwa Ubingwa wa CECAFA Chalenji

ANGALIA LIVE MASAA 24 KIKAO CHA 71 CHA KAWAIDA CHA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK KUPITIA UN WEB TV HAPA

WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAASWA KUUNGANA.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuungana ili waweze kupata fursa katika miradi mikubwa ya ujenzi itakayoanza hivi karibuni hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina endelevu ya 26 ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa na itatoa kipaumbele kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi watakaoungana ili kuwa na nguvu ya kutekeleza miradi hiyo kwa viwango.

“Tunao mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa miundombinu ya kisasa mjini Dodoma, ujenzi wa makazi ya kisasa ya wananchi, vyote hivi vinahitaji wataalamu walioungana, wenye nguvu ya kufanya kazi kwa haraka na ubora unaokubalika”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Ameitaka Bodi ya Usajili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kujitangaza na kuwatangaza wataalamu wake ili huduma zao zitumiwe na wananchi wa ngazi zote kwa gharama nafuu.

“Shirikianeni na vyuo vinavyofundisha fani yenu ili viongeze udahili wa wanafunzi na kuhakikisha kazi zenu zinafanywa kisasa na kwa kuzingatia teknolojia”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kutoa elimu ya kutosha ili kuvutia wanafunzi wengi kupenda kusoma fani hiyo na wale wanaofanya vizuri wawape motisha ya kuwasomesha katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika semina hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Mbunifu Majengo Ambwene Mwakyusa, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata ramani za nyumba kwa bei nafuu ili kuwa na jamii yenye makazi ya kisasa.

Naye Msajili wa Bodi ya AQRB, Mbunifu Majengo Jehad Jehad amesema takribani Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi 1,333 pamoja na kampuni za fani hiyo 372 zimesajiliwa na zinatoa huduma kwa mujibu wa sheria za fani hiyo.

Amebainisha kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha maadili ya taaluma hiyo hapa nchini yanalindwa na atakayekiuka atafutiwa usajili na kuadhibiwa kwa mujibu wa taratibu ya bodi hiyo.

Zaidi ya miradi ya ujenzi 1,963 imekaguliwa na bodi hiyo katika maeneo mbalimbali nchini katika kipindi cha mwaka wa 2015 lengo ikiwa ni kuhakikisha ujenzi wowote unaofanyika nchini unakuwa na viwango bora.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wadau wa sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,Jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki uandishi wa insha kuhusu sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,Jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari walioshiriki uandishi wa insha kuhusu sekta ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa bodi Bodi ya Usajili ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) mara baada ya ufunguzi wa Semina ya 26 ya wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi jijini Dar es salaam.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano.

Benki ya Barclays yazindua program ya kuwawezesha wahitimu wa vyuo vikuu

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed
(kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa
proram ya ReadytoWork inayolenga kuwapa elimu wanafunzi wa elimu ya
juu kujiandaa na ajira au kujiajiri. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Elimu
ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Lazaro Malili.
 Mkuu wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Lazaro Malili (kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa
program ya ReadytoWork ya Benki ya Barclays inayolenga kuwapa elimu
wanafunzi wa elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri uliofanyika
jijini Dar es Salaam leo.

DAR, PWANI KUKOSA MAJI KWA SAA 12

$
0
0
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza kuwapo kwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam, pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa wastani wa saa 12 siku ya Jumamosi.

Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza sababu ya kuzimwa kwa mitambo hiyo ni kuruhusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufanya matengenezo kwenye laini kubwa ya umeme inayotoka Ubungo kwenda kituo cha Tanesco Mlandizi, ambacho kinapeleka umeme kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini.

“Kutokana na Matengenezo hayo yatakayofanywa na Tanesco yatapelekea ukosefu wa huduma ya Maji kwa wakazi wa maeneo ya Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, na Luguruni,”

“Mji Wa Bagamoyo, Vijiji Vya Mapinga, Kerege na Mapunga. Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe” alisema Lyaro.

Maeneo mengine yaliyotajwa ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali Ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Changombe, Keko pamoja na Tabata. 

“Tunaomba wananchi wahifadhi Maji kwa kipindi hiki ili wasipate shida wakati tutakapozima mitambo hiyo”. alisema Bi.Lyaro 

WASHIRIKI WA DANCE 100% 2016 WAPEWA NASAHA ZA MAISHA NA WAFANYAKAZI WA VODACOM KUELEKEA FAINALI

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wanne kulia) akifafanua  jambo kwa washiriki wa shindano la Dance 100% 2016 wakati walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania  zilizopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazofanywa na kampuni. Washiriki hao walipata nafasi ya  kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi iliwaweze kujituma wakati wa  fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola.

 Washiriki  wa shindano la Dance 100%  2016 wakimsikiliza Meneja wa Huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Msamo Willnevilline(kulia) alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi ili waweze kujituma wakati wa  fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola, watatu kutoka kuliani  Meneja  Msaidizi wa Chapa ya Coca-cola, Mariam Sezinga.

 Mmoja wa washiriki wa shindano la Dance 100%  2016,akionyesha umahiri wa kucheza wakati washiriki hao walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola.
Meneja  Msaidizi wa Chapa ya Coca-cola, Mariam Sezinga(katikati)akiwa na washiriki wa shindano la Dance 100%  2016,wakati  walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma  mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa nasaha na baadhi ya wafanyakazi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay  jijini Dar es Salaam, Mshindi wa shindano hilo ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Coco-Cola

Bodi ya Vyombo vya Habari vya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) yajiuzulu

$
0
0


Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Peoples’ Media Communication Limited (PMCL) inayoendesha kituo cha redio Uhuru imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj Adam O. Kimbisa.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli amepokea barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo leo tarehe 22 Septemba 2016 ambayo nakala yake imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana. Barua hiyo inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.

Bodi ya Uhuru Media Group ndiyo iliyokuwa na majukumu ya kusimamia, kuzielekeza na kuzishauri Menejimenti ya Makampuni hayo na kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa vyombo vya habari vya Chama.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tarehe 22/09/2016.

HOSPITALI YA KISASA YA MUHIMBILI-MLOGANZILA KUANZA KUTOA HUDUMA JANUARI 2017.

$
0
0
 Mwonekano wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.




Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Dkt. Said Aboud.

 Baadhi ya Madaktari na wakuu wa vitengo wa Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam leo.
Mtaalamu wa Tehama, Andrew Fundamali akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika mitambo ya tehama katika hospitali hiyo.
  Wandishi wakipewa maelekezo walipotembelea katika chumba chenye mashine za MRI na CT scan.
 Daktali wa kitengo cha Koo, pua na masikio akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

UJENZI wa Hospitali ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma -shirikishi ya Muhimbili iliyopo Mbezi eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam yakaribia kumalizika kufunga vifaa tiba na kuanza kufanya kazi ifikapo Januari 2017 itaanza kutoa huduma mbalimbali  kwaajili ya kufundishia fani za afya na kutoa huduma ya matibabu yapasayo kwa wagojwa.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya wakati waandishi wa habari  walipotembelea katika hospitali hiyo ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa  afya na kutolea huduma mbalimbali za afya hapa nchini.

Amesema kuwa eneo la hospitali hiyo linaukubwa wa ekari 3800 na inauwezo wa kuchukua vitanda 571 na ipo umbali wa Kilomita 25 kutoka jijini Dar es Salaam pia inauwezo wa kuchukua wanafunzi 4000 ikitofautishwa na waliopo sasa ni 1500 tuu.

 Profesa Kaaya amesema kuwa upungufu wa wataalamu wa afya katika mikoa na wilaya hapa nchini ndiko kulikosababisha  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili kuanza kutafuta maeneo yakupanua na kujenga hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.

Profesa Kaaya amesema kuwa wagojwa watakaopelekwa katika hospitali hiyo ni wale watakaokuwa wamepewa rufaa kutoka hospitali za mikoa mbalimbali ya hapa nchini.

Amesema kuwa jengo hilo lina sehemu mbili na linaghorofa tisa za juu na ghorofa moja chini ya ardhi linaeneo la Mapokezi, Idara ya Utawala, Idara ya Mahesabu, Phamasia, Idara ya Mionzi, Idara ya wagonjwa wa dharula pamoja na upasuaji wa Dharala, Idara ya afya ya kinywa na meno,chumba cha wagojwa  mahututi, chumba cha kusafisha figo na wadi ya kujifungulia.


Eneo jingine ni vyumba vya kufundishia wanafunzi maktaba ya hospitali, ofisi ya mkuu wa hospitali, ofisi za madaktari na waalimu, ofisi ya Muuguzi Mkuu na kituo cha kopyuta.

Article 18

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images