Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

HAPPENINGS @ NAFASI ART SPACE IN DAR ES SALAAM THIS WEEK

0
0
Hello Art Lovers!!
How was your weekend! It’s a start of a new week and I bet you haven’t forgot about our Wachata Graffiti event which was a great success, to say the least.
Weekend yako ilikuwaje? Ni mwanzo wa wiki ila naamini bado haujasahau kuhusu tukio la wikiendi hii la Wachata Graffiti ambalo lilikuwa kabambe.

This week we have a lot of updates as always, our upcoming events, and recap from last week events. We hope you will enjoy and save some minutes for these events.
Wiki hii tuna taarifa mpya kama kawaida, matukio yetu yajayo na taarifa juu ya matukio yaliyopita. Tunatumaini utafurahia taarifa hizi na pia kupanga muda kwa ajili ya kuhudhuria matukio haya.

MUSEUM ART EXPLOSION SEPTEMBER 22th - 25th 2016

0
0
Maonesho ya Mwezi huu yatafanyika Septemba 22, 2016  saa 11 jioni kwa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya kazi za ufundi na Tarehe 23 saa 1:00 jioni hadi 3:30 usiku Maonesho ya Jukwaani.

WAKADARIAJI MAJENZI NA WABUNIFU MAJENGO KUNOLEWA

0
0
Na Dotto Mwaibale
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi kesho kutwa inatarajia kuendesha semina ya siku moja kwa ajili ya kuwanoa wadau wa sekta ya ujenzi nchini.
Hayo yamebainishwa na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Jehad wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina hiyo muhimu itakayofanyika kesho kutwa ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
"Semina hii ambayo ni ya 26  ni muhimu sana kwetu sisi watu wa sekta ya ujenzi hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linatutegema" alisema Jehad.

Alisema semina ya namna hiyo zilianzishwa tangu mwaka 2003 na hufanyika mara mbili kwa mwaka  ambapo jumla ya wabunifu majengo, wakadariaji majenzi na wadau wengine wa sekta ya ujenzi wapatao 5,328 wamekuwa wakinufaika na semina hizo.

Alisema malengo ya semina hiyo ni kuwanoa wabunifu majengo na wakadariaji majenzi na wadau wengine katika sekta ya ujenzi kutambua fursa ambazo ziko katika soko la Afrika Mashariki (EAC) na lile la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

Alitaja lengo jingine kuwa ni kuwafahanisha wadau faida na umuhimu wa sheria ya mtandao katika kuboresha huduma zao kwa wananchi na kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kitaaluma kwa lengo la kuongeza weredi pamoja na kuwapa fursa waataamu katika sekta ya ujenzi kupata nasaha kutoka kwa viongozi wa Serikali.

Jihad aliswema katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa na kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.



Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi, Jehad A. Jehad (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu semina ya 26 siku moja itakayo washirikisha wadau wa Sekta ya  ujenzi itakayofanyika kesho kutwa Septemba 22, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.
Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Utawala, Angelo Ngalla, Mwanasheria, Ibrahim Mohamed na Ofisa Uhusiano, Hamisi Sungura.

semina elekezi kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Geita

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyuga (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw.Frank Kanyusi (kulia) na washiriki wengine wakisikiliza mada ya  Naibu Msajili – Sheria za Biashara(BRELA) Bw. Andrew Mkapa  katika semina elekezi kwa wafanyabiashara mkoani humo juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara na  majukumu ya BRELA. Pia kuna usajili majina ya biashara na makampuni wa papo kwa papo kwa muda wa wiki nzima.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Bw.Frank Kanyusi katika hali ya furahana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyuga mara baada ya kufungua semina elekezi kwa wafanyabiashara wa mkoa huo juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara zao. Pia kuna usajili majina ya biashara na makampuni wa papo kwa papo kwa muda wa wiki nzima.

KITAMBI NOMA

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SERIKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO

0
0
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha 
 MKUU wa mkoa Arusha Mhe Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi. 
Mhe. Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi. 
Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufudisha na kufuatilia kila siku madeni hayo. 
 “Mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa ajili ya walimu hakikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe. 
Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo. 
 ‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi zinaelekezwa kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni madeni wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha watoto wetu vizuri”alisema Kihamia . 
Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu bora.
 Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.
 MKUU wa mkoa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha, waratibu elimu, wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiongea na walimu walioudhuria mkutano huo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KILIMANJARO QUEENS MABINGWA KOMBE LA CECAFA CHALENJI KWA WANAWAKE 2016

0
0
Haikuwa ubashiri, badala yake ilikuwa ni mipango thabiti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha kwamba inavuna ushindi na kuwa mabingwa wa Kombe la Chalenji la CECAFA kwa wanawake baada ya kuilaza Kenya mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Nambole jijini Jinja nchini Uganda.
Mabao ya timu ya taifa Tanzania ya wanawake maarufu kama Kilimanjaro Queens katika mchezo wa leo Septemba 20, 2016 yamefungwa na Mwanahamisi Omari katika kipindi cha kwanza kabla ya Kenya kujitutumua na kupata bao la kufutia machozi kipindi cha pili katika mchezo uliokuwa na ushindani wa aina yake. 
Matokeo hayo yatakuwa kupozwa kwa ndugu zao wa Zanzibar Queens ambao walitolewa mapema katika mashindano hayo yaliyoanza Septemba 11, 2016 kabla ya kufikia tamati leo katika fainali hizo zilizovutia mashabiki wa mpira wa miguu nchini Uganda ambako kila upande ulikuwa na watu wanaowasapoti.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini Uganda kesho Jumatano na kwenda moja kwa moja Kagera ambako ilipiga kambi kabla ya kwenda Jinja. Itarudi hapo kusema ahsante kwa wenyeji, lakini pia kuwapa pole ya janga la Tetemeko la Ardhi wakazi lililotokea katika mikoa huo na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani. Mikoa ambayo iliathirika zaidi ni Kagera na Mwanza kadhalika nchi jirani za Uganda na Rwanda.
Mara baada ya kuwapa pole, timu hiyo itasafiri kutoka Kagera kwa usafiri wa anga ambako taratibu za safari hiyo zitatangazwa na TFF hapo kesho ambako wananachi watapata fursa ya kuipokea na kuishangilia timu hiyo inayonolewa na Kocha Sebastina Nkoma akisaidiuwa na Hilda Masanche wakiwa chini ya Mwenyekiti wa soka la wanawake.

NDEGE YA KWANZA YA ATCL YATUA JIJINI DAR MCHANA WA LEO

0
0


Mnamo 20 Septemba, 2016, Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Canon Water Salutation).
Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
 Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na maofisa wengine wakiwa kwenye  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo Septemba 20, 2016.
 Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.



KINONDONI YAJIKITA KUTATUA AJIRA KWA VIJANA.

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jijini Dar es Salaam leo.

Na Yassiri Adam, Globu ya Jamii.
WILAYA ya Kinondoni imezindua kampeni ya wajasiriamali kwa vijana ili kuweza kutatua changamoto ajira kwa vijana na wananchi wa Wilaya hiyo.

Akizungumza na watendaji wa Wilaya hiyo wakati wa uzinduzi kampeni ya ujasiriamali, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa wananchi wakipata mafunzo ya ujasirimali itasaidia fursa kuongeza ajira kwa vijana.

Amesema mapato mengi yanayokusanywa kwa wilaya ya Kinondoni yanatokana na watu walioweza kujiajiri wenyewe wakaweza kuajiri watu wengine.

Hapi amesema kuwa vijana wakipata mafunzo ya ujasirimali kutasaidia kuondokana na kujiingiza katika vitu visivyo ikiwemo maandamano yasiyokuwa na tija , kujiingiza katika makundi ya uhalifu pamoja uzurulaji.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yataanza kwa walimu 30 ambao wakimaliza mafunzo hao watafundisha vijana wengine katika maeneo mbalimbali ujasiriamali wa kilimo cha mbogamboga, mama lishe ,ufugaji.

Waziri Nape aipongeza Kilimanjaro Queens mabingwa kombe la CECAFA

0
0

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewapongeza Wachezaji wa Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na kwa niaba ya watanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira wa miguu kwa wanawake Afrika Mashariki na Kati.Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Nnauye alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

“Kama serikali ni vyema kuipongeza timu yetu ya Kilimanjaro Queens kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania katika michuano CECAFA na kuibuka mabingwa kwa kuweza kuruka vizingiti vyote vilivyokuwepo katika muchuano hiyo” alisema Mhe. Nnauye

Serikali itaendelea kuweka nguvu ya kutosha na kuungana na timu zetu kuwasaidia kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika michezo mbalimbali, amesema Mhe. Nnauye.Mhe. Nnauye amesema kuwa Tanzania inaanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda mrefu kwani haikuwa kazi raisi kwa Kilimanjaro Queens kufikia fainali na kuwa mabingwa kwa kupambana na timu ngumu na kuweza kushinda.

Aidha Mhe. Nnauye amewahaidi wachezaji wa Kirimanjaro Queens kuwaalika bungeni katika Bunge lijalo kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaandalia mechi ya kirafiki kutambua mchango wao wa kuipeperusha bendera ya Tanzania kati yao na wabunge wanawake. Timu zilizoshiriki katika michuano ya kombe la chalenji la CECAFA ni pamoja na Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati

MSANII WA KIZAZI KIPYA NCHINI KALLAH JEREMIAH APOKEA CHETI KUTOKA SOCIETY WATCH,

0
0

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya wakati wa kukabidhi cheti utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kushirikisha watoto katika wimbo wana ndoto, amesema kuwa watoto yatima wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo kunahitaji jitihada za kuweza kusaidia watoto yatima.

Mkondya amesema kuwa mpango wa utaoji wa elimu kwa serikali kwa kundi hilo inawezekana kutokana na uchache. Amesema kuwa watoto yatima wamepata hamasa kwa wimbo wa Mwanamziki wakikizazi kipya Kala jeremiah ''wanandoto'' ambapo taasisi hiyo imeliona kundi hilo linalo umuhimu wakipekee yakutoachwa nyuma katika suala la kupata elimu .

''Hamasa ya taasisi yetu Society Watch nikuwasaidia watoto yatima walipo vijijini katika kupata elimu hasa kwa watoto wanaishi katikamazingira magumu katikamaeneo yavijijini ,hamasa hii imetokana na wimbo wa wanandoto wakala jeremamiah kwani watoto hawa wanao mchango mkubwa katika kulitumikia taifa ''Alisema Mkurugenzi Simon Mkondya.

Amesema kuwa kutokana na msanii huyo wakizazi kipya Kala jeremiah kuona umuhimu watoto yatima kupewa fusra yakupata elimu kama watoto wengine kupitia wimbo wanandoto unalenga kuihamasisha jamii kulisaidia kundi hilo maalum katika kupata elimu .

Mkondya amesema serikali inaowajibu wakipekee katika kuwasaidia watoto yatima kuwawezesha kundi hilo kuweza kupata elimu kwani kutokana naumuhimu wawatoto hao katika kujenga taifa nakuliletea taifa maendeleo katika hazina yaviongozi wakesho ,hivyo serikali najamii inawajibu wakulisaidia kundi hilo katika kuwapatiaelimu.

Nae Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah amesema kuwa yeye pamoja nawanamziki wa kizazikipya wameimba wimbo huo''wanandoto'' kuikumbusha serikali kuwaasaidia watoto yatima walipo katika mazingira magumu kuwa wanao umuhimu wakipekee katika kupata elimu . Amesema kuwa ni mara kwanza kwa watu kumpa cheti kwa kukubali kazi anayoifanya katika jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya akimkabidhi Kallah Jeremiah cheti cha utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kwa kushirikisha watoto katika wimbo wana ndoto, leojijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Society Watch,Issabela Liso .


Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kukabidhi cheti cha utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kushirikisha watoto katika wimbo wana ndoto, leojijini Dar es Salaam.kushoto ni Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah .

Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuushukuru uongozi wa Society Watch kwa kumpa cheti kwa kukubali kazi anayoifanya katika jamii.kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya
KATIKA kuhakikisha watoto yatima hawaachwi nyuma katika suala zima la elimu nchini ,Taasisi ya Society Watch imeanzisha kampeni maalum kundi hilo kutokana na watotot yatima kuwa changamoto mbalimbali zinazofanya ndoto zao zishindwe kutimia.

WAZIRI SIMBACHAWENE AZUNGUMZIA HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KWA WANAFUNZI WA IHUNGO NA NYAKATO

TAMKO KUHUSU UTUPAJI TAKA OVYO USIO WA KITAALAMU MAHOSPITALI.

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akiongea na Vyombo vya Habari juu ya hatua za Serikali za kuzuia utupaji ovyo wa taka hatarishi za Hospitalini na  kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Januari mosi 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyungi.
­­­­


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
tz
TANGAZO KWA UMMA

UZUIAJI WA UTUPAJI OVYO   USIO WA KITAALAMU WA TAKA ZA MAHOSPITALI. 

Sheria ya usimamizi  wa Mazingira ya mwaka 2004  inapiga marufuku uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na unaotokana na taka za mahospitali.  Aidha Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, zinasisitiza utenganishi wa taka mbali mbali  zitokazo kwenye mahispotitali kwa kuzitibu katika namna ambayo haitaleta athari katika mazingira na afya ya binadamu. Pia Kanuni zinahimiza matumizi ya teknologia sahihi kama vile matumizi ya incinerators ambazo huchoma taka za mahospitali na  kuziteketeza kabisa.

Ofisi yangu imefuatilia na kugundua kuwa taka nyingi za mahopitali, taka kutoka katika maduka ya  madawa zilizoisha muda wake zinatupwa ovyo  au kuharibiwa kwa utaratibu usio kubalika kitalaamu. Tumefuatalia na kukuta malundo ya madawa chakavu na vifaa vya hospitali vilivyotumika   katika maeneo ya visiwa vya Bongoyo na Mbudya. Aidha madawa chakavu yanatumpwa holela katika dampo la Pungu Kinyamwezi.  Hii ni hatari sana kwa mazingira na kwa afya ya binadamu.

Kuanzia sasa ni marufuku  kutupa taka hizi katika utaratibu usio wa kawaida. Kila hospitali na zahanati  au kituo cha afya kihahakikishe kinatumia incinerators  au utaratibu mwingine ulio sahihi kwa mujibu wa sheria ya mazingira na kanuni zake. Aidha ninaiagiza NEMC kuanzia sasa wafanye msako mkali kubaini mahospitali na watu wanaokiuka agizo hili. Nimewapa mwezi mmoja na   kwa  wale wanaofanya hivyo waache mara moja.   Kwa msako huu atakayebainika kukiuka hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.Nichukue fursa hii kutoa tena pole kwa wezentu wa Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani kwa athari za tetemeko la ardhi.

Baada ya tatetemeko kuna athari kubwa za kimazingira  ambazo zimejitokeza. Hivyo mimi binafsi ninafuatilia suala hili kwa ukaribu na kuhakikisha  athari ambazo zimejotokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashughulikiwa kwa haraka.  Nimeagiza Ofisi yangu pamoja na NEMC washirikiane kwa ukaribu sana na watendaji wa Mkoa na Kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia maafa haya na kufanya  tathmini  ya athari za mazingira zilizojitokeza na kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ilikupunguza madhara kwa mazingira na binadamu.

Pia, napenda kutumia fursa hii  kuukumbusha umma  juu ya dhamira ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya ya plastiki ifikapo Januari Mosi 2017.Adhma ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko  na vifungashio vya plastiki ni kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo. Hivyo basi wazalishaji, waagizaji, wasambazaji, wauzaji  na watumiaji  wa mifuko hiyo wanakumbushwa kuendelea na zoezi la kuondosha pamoja na kusitisha uzalishaji wa mifuko hii.

IMETOLEWA NA
JANUARY  Y. MAKAMBA (MB.)
WAZIRI WA NCHI OFISI YAMAKAMU WA RAIS
MUUNGANO NA MAZINGIRA

21/9/2016

TFF KUKARABATI UWANJA WA UHURU, SIMBA KUHAMIA UWANJA WA TAIFA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.KUFUATIA timu  mbalimbali kulalamikia Uwanja wa Uhuru kutokana na nyasi zake na kuonekana kuisha na kusababaisha majeraha kwa wachezaji hasa wakati wakiteleza na kupata michubuko kwa wingi. Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF, limeamua kuhamishai mchezo wa Simba na Majimaji kupigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Mbali na mchezo huo pia mechi ya African Lyon na Kagera Sugar utapigwa pia Uwanja wa Taifa mpaka pale marekebisho yatakapomalizika.Mabadiliko hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki ambacho limeanza kufanyia marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya nyasi bandia (artificial turf).

Hivyo, mechi ya Simba na Majimaji itafanyika Jumamosi, Septemba 24 wakati ile ya African Lyon na Kagera Sugar itachezwa Jumatatu, Septemba 26. Jumapili, Septemba 25 Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za Wabunge za Simba na Yanga ili kuchangia waathirika wa janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.

Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa Jumamosi, Septemba 24 ni kati ya JKT Ruvu na Mbeya City (Mabatini), Ndanda na Azam (Nangwanda Sijaona), Tanzania Prisons na Mwadui (Sokoine), Mtibwa Sugar na Mbao (Manungu).

Jumapili kutakuwa na mechi kati ya Stand United na Yanga (Kambarage), na Ruvu Shooting na Toto Africans kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

Kutokana na marekebisho yanayofanyika Uwanja wa Uhuru, mechi ya kundi ya A ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Ashanti United na Pamba iliyokuwa ichezwe Ijumaa, Septemba 23 kwenye uwanja huo sasa itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

HOSPITALI YA KAIRUKI YATOA MSAADA WA MADAWA KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

0
0
Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba, 10 mkoani Kagera,Hubert Kairuki Memorial University Hospital Imetoa mchango mdogo wa madawa kwaajili ya Wahanga wa tetemeko la ardhi.
 Dr Muganyizi Kairuki Naibu Mkurugenzi wa hospitali ya Hubert Kairuki Memorial University kabla ya kukabidhi msaada wa mdawa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu.
Pichani kushoto anaonekana Dr Muganyizi Kairuki Naibu Mkurugenzi wa hospitalI hiyo wakati akikabidhi Masada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu
#Bukobawadau#TetemekoBukoba

Naibu Waziri Wambura akutana na wajasiliamali wa Hand Production of Tanzania

0
0

Na Lorietha Laurence.

Wajasirimali na wabunifu wa kazi za mikono nchini wahimizwa kuwa na hatimiliki ili kudhibiti wizi wa kudurufu bidhaa zao unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura alipokutana na kikundi cha wajasiriamali cha Handproduct of Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Anastazia ameeleza kuwa endapo kazi za wajasriamali zitalindwa kwa kuwa na hatimiliki itasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi na kuongeza pato la Taifa. “Ni muhimu kulinda kazi za wajasirimali kama ambavyo kazi za sanaa ya muziki zinavyolindwa kwa kuwa na hatimiliki ili kuwasaidia katika kulinda haki zao za ubunifu” alisema Mhe. Anastazia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo ameeleza kuwa kukosekana kwa hatimiliki katika kazi zao kumeleta changanmoto kubwa na bidhaa feki kutoka kwa wafanyabiashara wa nje ambao wamekuwa wakidurufu kazi zao na kuuza bidhaa kwa bei nafuu.

Aidha Bibi. Elizabeth aliongeza kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa eneo la kufanyia maonyesho ya bidhaa zao kitendo ambacho kinasababisha kukosekana na soko lililoimara kwa bidhaa hizo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Wizara Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lilian Beleko amesema kuwa kweli changamoto hizo zipo na wanazifanyia kazi kuwawezesha wajasiriamali hao wa kazi za sanaa na utamaduni ili waweze kufanya kazi zao kiufanisi.

Kikundi cha Handproduct of Tanzania kilisajiliwa mwaka 2006 na kinajumisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na kazi za mikono kutengeneza bidhaa mbalimbali za utamaduni na sanaa katika kuenzi utamaduni wa Mtanzania.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa bidhaa ya vikapu vya asili vilivyotengenezwa kwa kitenge kutoka kwa mjasiriamali Bibi. Flora Mosha wa Nancy Tailoring Mart (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akionyeshwa vazi lililodariziwa na mjasiriamali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Handproduct of Tanzania Bibi. Elizabeth Matarimo leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Lorietha Laurence – WHUSM

TANZIA: mtangazaji wa Channel Ten kipindi cha "Utalii Tanzania" Bw. Cassius Mdami afariki dunia

0
0
Aliyekuwa mtangazaji wa Channel Ten, kipindi cha Utalii Tanzania, Bw. Cassius Mdami (pichani) amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro , ndugu na mwajiri wake  wamethibitisha. Tutawajulisha mipango ya mazishi mara tukipata taarifa.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU 
MAHALA PEMA PEPONI
-AMINA

Wafanyakazi wa Kujitolea wa Kimarekani 51 waapishwa kufanya kazi kwa miaka miwili katika wilaya 33 nchini Tanzania

0
0
Dar es Salaam, TANZANIA – Leo katika Ofisi za Wamarekani wa Kujitolea, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser amewaapisha wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani (Peace Corps Volunteers) wapatao 51 ili kuanza huduma yao ya miaka miwili. 
Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watafanya kazi katika sekta ya elimu. Mwaka uliopita katika Programu ya Elimu, wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps 110 walifundisha katika shule za sekondari 108 katika mikoa 22 kwenye zaidi ya wilaya 30 nchini Tanzania na kuwafikia takriban wanafunzi 36,000.  Hawa wafanyakazi wa kujitolea 51 wanaungana na wengine 195 ambao tayari wako nchini wakifanya kazi katika elimu ya sekondari (hisabati, sayansi na kiingereza), kukuza sekta ya afya, na elimu ya mazingira.  
Mheshimiwa Salum S. Salum, Afisa Elimu Mkuu, aliiwakilisha wizara ya elimu katika hafla ya uapisho. Hafla hii ilihudhuriwa pia na wafanyakazi wengine wa kujitolea wanaoendelea kuhudumu na wale waliomaliza muda wao pamoja na maafisa kutoka taasisi wabia.

Mbali na kufundisha madarasani nchini kote, wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps hushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii. Shughuli hizi ni kama kusaidia kuboresha maktaba za shule, kuandaa programu za kukuza uelewa wa VVU/UKIMWI, na kukuza stadi za maisha za wanafunzi. Wafanyakazi wa kujitolea walioapishwa leo, watapangiwa kufanya kazi katika wilaya zifuatazo nchini kote: Karatu, Kongwa, Chamwino, Mufindi, Iringa Rural, Hai, Rungwe, Lushoto, Wete, Nzega, Sumbawanga, Same, Ruangwa, Nachingwea, Hanang, Babati, Kiteto, Busokelo, Kyela, Chunya, Mbarali, Masasi, Newala, Mtwara rural, Mbinga, Morogoro Manispaa, Shinyanga, Kishapu, Maswa, Wanging’ombe, Singida, Njombe, Nzega na Lushoto. 
"Wiki hii inaadhimisha miaka 55 ya kupitishwa kwa sheria ya Peace Corps, ambayo ilianzisha rasmi taasisi ya Peace Corps mwaka 1961. Kuwaapisha hawa wafanyakazi wa kujitolea katika maadhimisho haya maalum ni ishara ya kielelezo muhimu ya ushirikiano kati ya watu-kwa-watu ambao Peace Corps inahamasisha nchini Tanzania,” alisema Kaimu Balozi wa Marekani Virginia Blaser.  
Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira. 
Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. 

Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:

·         Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao; 
·         Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea; 
·         Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.

 Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika Nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira.
Sehemu ya wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani (Peace Corps Volunteers) wapatao 51 wakila kiapo ili kuanza huduma yao ya miaka miwili leo  katika Ofisi za Wamarekani wa Kujitolea jijini Dar es salaam. Picha kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani

UBORESHAJI HUDUMA ZA UTOAJI HAKI KWA MWANANCHI

MHE. JENISTA MHAGAMA AFANYA ZIARA WILAYANI MISENYI MKOANI KAGERA NA KUWAPA POLE WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDH

0
0
SERIKALI imetibu wananchi bure ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Kauli hiyo imetolewa leo Mkoani Kagera na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama wakati alipofanya ziara Wilayani Misenyi kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.
Mhe. Mhagama ameeleza kuwa, Serikali hadi hivi sasa imewatibu watu zaidi ya 400 kupitia hospitali zake za Wilaya na Mkoa kwa kuagiza madaktari kutoka nchini China ambapo zoezi la kusambaza damu pamoja na dawa za kutosha kwa waathirika lilifanyika na hakuna mwananchi aliyetozwa fedha kama malipo ya huduma hiyo.
“Tuishukuru Serikali yetu kwa kutusadia kupata dawa na damu ya kutosha na tulihakikisha kuwa kila mtu aliyepatwa na tetemeko na kujeruhiwa anatibiwa kwa gharama za Serikali ndiyo maana tuliagiza madaktari kutoka China pamoja na Mwanza ili kusaidia kuwatibu wananchi waliopatwa na majeraha makubwa”, alisema Mhe. Mhagama.
Aliongeza kuwa jumla ya wagonjwa ambao kwa sasa wanaendelea kutubiwa hospitalini ni 23 na ndiyo ambao wamefanyiwa upasuaji mkubwa na hali zao zinaendelea vizuri tofauti ilivyokuwa hapo awali.
Alifafanua kuwa, Serikali haiwezi kumsaidia kila mtu kwani haina uwezo huo lakini inajitahidi kurejesha miundombinu yake na taasisi zake zikiwemo zahanati, shule barabara kwa kushirikiana na wadau wanaojitokeza kuunga mkono juhudi za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo, hivyo ametaka wananchi kujitokeza na kushirikiana kwa pamoja katika kuwasaidia waliopatwa na tukio hilo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katiika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.
Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ni ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika pia.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa ambapo amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.

Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila wakati alipowasili Wilayani kwake kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila (wa pili kulia) wakati alipowasili Wilayani kwake kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili mbele) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila wakielekea kuangalia eneo la Shule Msingi Bieju ya Kata ya Mtukula wakati alipowasili Wilayani kwake kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia athari ya tetemeko katika eneo la Shule ya Msingi Bieju Kata ya Mtukula wakati alipowasili Wilayani Misenyi kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea maelezo juu ya idadi na thamani ya uharibifu katika shule ya Sekondari Mtukula toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila wakati alipowasili Wilayani hapo kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images