Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1361 | 1362 | (Page 1363) | 1364 | 1365 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California, jana kwa pamoja walikusanyika katika kanisa la Lutheran Oakland ili kukusanya michango ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea kanda ya ziwa nchini Tanzania, hususan mkoani Kagera ambako madhara makubwa yamerekodiwa.

   Jumla ya dola za Kimarekani  4,000 za ahadi na fedha taslim zilipatikana hiyo jana.
  “Tuna mpango wa kukusanya pesa zote   ifikapo Jumamosi  Septemba 24, 2016 na kuzituma  Jumatatu Septemba  26, 2016 katika  ofisi ya Mkuu wa mkoa  wa Kagera ambapo shughuli zote uratibu na makusanyo yote yanaelekezwa pale kama serikali ilivyoagiza” amesema Bw.

  Erick Byorwango, Katibu mwenezi wa Jumuiya ya Watanzania - Northern California. 
   Bw. Byorwango ameongeza kusema kuwa jitihada za kukusanya michango zinaendelea na mwitikio wa mkutano huu ulikuwa na matumaini. 
  "Tunaomba mungu aendelee kutupa nguvu na upendo ili tukamilishe zoezi hili na hatimaye tuwakilishe msaada wetu serikalini" amemalizia. 
   Mchungaji  Chussi akiongoza sala kabla ya kuanza mkutano wa Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California nchini Marekani waliokutanika jana kukusanya michango ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea kanda ya ziwa nchini Tanzania

   Wajumbe wakiendelea na kikao
   Sehemu ya watoto wa  Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California
  Mwenyekiti wa jumuiya ya  Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California  Dr Mathias Kaaya akiongoza kikao.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0  0 0


  MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
  Arusha, Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya
  milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali
  kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao
  kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

  Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
  shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

  Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
  ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo
  linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila
  siku madeni hayo.

  “mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa
  ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa
  ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani
  haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
  wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo
  hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni
  madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha
  kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za
  halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.

  Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa
  ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo
  kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani
  mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai
  yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

  ‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha
  za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo
  jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi
  zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
  wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni
  tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha
  watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

  Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
  wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu
  kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo
  zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili
  zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu
  bora.

  Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
  tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku
  wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja
  bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.


  MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata .
  Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliohuthuria mkutano huo.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
  .

  wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao.
  picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha.
  Habari picha na Woinde Shiza-Arusha.

  0 0

  KAMATI ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, limependekeza kwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) kumvua uongozi Mwenyekiti wa umoja huo mkoani Arusha, Lengai Ole Sabaya, kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kufikishwa mahakamani akituhumiwa kwa utapeli. 

  “Wakati tukisubiria uamuzi wa Chama, Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa imemsimamisha uongozi wa nafasi yake ndani ya UVCCM kutokana na kesi iliyoko Mahakamani na kumtaka kuanzia leo (jana) asijihusishe na shughuli zozote za uongozi wa UVCCM hadi hatima ya tuhuma zake itakapoamuliwa na Mahakama na vikao husika vya UVCCM na CCM. 

  Mbali na Sabaya, UVCCM pia imemtimua kazi aliyekuwa katibu wake mkoani humo kwa kukiuka utaratibu na maagizo ya UVCCM na CCM ikiwemo vitendo vya utovu wa nidhamu. 

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Dar es Salaam na kutiwa saini na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, ilisema Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa ilikutana Septemba 19, nwaka huu Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Sadifa Juma Khamis ambapo pamoja na mambo mengine walifikia uamuzi huo. 

  Ilisema kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili na Nidhamu ya UVCCM Taifa, ambapo pamoja na mambo mengine kilipokea na kujadili uhai wa CCM na umoja huo mkoani Arusha. Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo walijadili kuyatolea ufafanuzi mambo mbalimbali kuhusu makada wake hao wawili. 

  Taarifa ya Shaka ilisema miongoni mwa mambo yaliyomhusu Sabaya ikiwemo kuyaongoza makundi ya vijana wa CCM na wasiokuwa wa CCM ili kumkataa Katibu wa UVCCM aliyehamishiwa mkoani Arusha, Said Goha kuchukua nafasi ya Ezekiel Mollel. Ilisema kuwa Sabaya licha ya kupewa heshima na kuelimishwa na vikao vya juu na viongozi mara kwa mara kupitia Mwenyekiti wa UVCCM taifa, kuhusu mamlaka za kikanuni ikiwemo ya utumishi na maadili ya UVCCM lakini ameshindwa kujirekebisha. 

  “Sabaya amesababisha taharuki iliyosababisha ofisi za UVCCM Arusha kufungwa kwa minyororo hadi Jeshi la Polisi kuingilia kati. Vile vile taharuki hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa Vijana wa mkoa wa Arusha kugawanyika katika makundi na kusababisha hali ya usalama na maadili kwa umoja huo na Chama kuwa ya wasiwasi. 

  “Sabaya kufikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kujifanya mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Huku kosa la pili katika muda usiojulikana akidaiwa kughushi vitambulisho vya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) chenye namba MT 86117 wakati akijua ni kinyume cha Sheria za nchi. 

  “Kamati ya Utekelezaji ilipitia tuhuma mbalimbali na vielelezo vya utapeli na ulaghai unaodaiwa kutendwa na Sabaya katika maeneo tofauti huku akijua ni kinyume na miiko na maadili ya uongozi wa UVCCM na CCM.
  “Kwa makosa yote hayo Sabaya amekukiuka kanuni ya uongozi na maadili ya CCM Fungu la (3) ukurasa wa 16 na 17, na fungu la (4) ukurasa wa 29, 30 na 31. Pia makosa hayo ameyatenda kinyume na utaratibu wa uongozi na maadili ya UVCCM, Ibara ya 6.3.2 Ibara ya 7.5.1, 7.5.4 na 8.2.5,”alisema.


  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe akizungumza na wanachama wa mfuko huo jijini Mwanza jana kabla ya kuwakabidhi kadi za matibabu ya mfumo wa uchangiaji wa hiari(Wote Scheme).

  Na Baltazar Mashaka,Mwanza

  WANACHAMA 106 kati ya 7, 185 wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa kupitia mfumo maalum wa uchangiaji wa hiari wa WOTE Scheme wamekabidhiwa kadi zitakazo wawezesha kupata huduma za matibabu.

  Akikabidhi kadi hizo kwa wanachama hao, Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshach Bandawe alisema mfumo huo umewalenga wanachama waliojiajiri wenyewe katika Sekta isiyo rasmi ambao kwa mujibu wa takwimu za kitaifa ni zaidi ya asilimia  90 ya nguvu kazi ya taifa.

  Alisema kuwa bahati mbaya kundi hilo lilisahaulika na halijakingwa kikamilifu na sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini ingawa ni ukweli usiopingika kuwa wanapatwa na majanga hatarishi sawa na wafanyakazi wa sekta rasmi.

  “ Watu waliojiajiri kwenye Sekta isiyo rasmi wanafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na uzalishaji mali  na kuwaingizia kipato cha uhakika na kumudu kuendesha maisha yao.Bahati mbaya hawana akiba yoyote wanayoweza kunufaika nayo kwa maisha ya baadaye iwapo wangejiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii,” alisema.
  Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe akimkabidhi Anastanzia Magere kadi ya matibabu ya mfumo wa uchangiaji wa hiari(Wote Scheme) jijini Mwanza jana. Mpaka sasa Kanda hiyo wamekwishajiunga wanachama 7185 kwa kipindi cha Agosti 2015 mpaka Agosti 2016. Picha na Lordrick Ngowi

  Meneja huyo wa PPF alieleza kuwa mfuko kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) utatoa huduma ya matibabu kwa wanachama baada ya kuchangia sh.60,000  na watatibiwa magonjwa yaliyoanishwa kwenye sera ya kitaifa.

  Bandawe alisema wanachama hao watapata huduma hiyo ya matibabu katika hospitali zaidi ya 6,000 nchini ambazo zimeingia mkataba na NHIF na wanastahili kuwa na kadi watakazotumia kupata huduma hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja na akatoa wito kwa makundi mbalimbali yaliyoko katika sekta isiyo rasmi yajiunge na mfumo huu kwa faida ya maisha yao na wanufaike na huduma mbalimbali zinazotolewa na PPF .


  0 0

   Muonekano wa mtambo wa kusaga kokoto katika kiwanda cha Kongolo cha TAZARA mkoani Mbeya unaotumika kutengeneza kokoto za kujaza tuta la reli.
  Muonekano wa kokoto zinazosagwa na kiwanda cha Kongolo cha TAZARA mkoani Mbeya zinazotumika katika uimarishaji wa tuta la reli.
  Baadhi ya nondo zinazotumika kutengeneza mataruma katika kiwanda cha Kongolo cha TAZARA Mkoani Mbeya.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  WAKATI Serikali ikiwa katika hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa reli ya kisasa nchini (Standard Gauge), Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imesema imewasilisha andiko kwa Kampuni miliki ya rasilimali za Reli (RAHCO) ili kuanza utengenezaji wa mataruma na uzalishaji wa kokoto zitakazotumika kwenye ujenzi wa reli hiyo.

  Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi Mzalishaji wa kiwanda cha kuzalisha mataruma cha TAZARA mkoani Mbeya, Eng. Boniface Phiri ikiwa ni siku chache baada ya RAHCO kutangaza zabuni hiyo ambapo amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo mkubwa wa kuzalisha mataruma kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

  Eng. Phiri amesema pamoja na agizo la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano alilolitoa kwa mamlaka hiyo Mwezi mmoja uliopita alipotembelea kiwanda hicho na kuelekeza kuwa Mamlaka ijipange kuzalisha mataruma na kokoto.

  “Mamlaka imejitathmini na kuona kwamba kutokana na uwezo tulionao tumeshawasilisha andiko letu kwa RAHCO na tunasubiri majibu yao ili kuanza kazi ya uzalishaji”, amesema Eng. Phiri.

  Amebainisha kuwa kwa sasa Mamlaka inaboresha mitambo na kuangalia namna ya kuanza kutumia teknolojia ya mvuke kwenye uzalishaji ili kuongeza idadi ya mataruma na  ubora unaokidhi viwango ambapo kwa siku kiwanda huzalisha mataruma zaidi ya 200.

  Aidha Eng.Phiri ameishukuru Serikali Ya Tanzania na Zambia kwa kuisadia Mamlaka hiyo tani 300 za nondo ambazo zimesaidia kuongeza uzalishaji wa mataruma katika kiwanda.

  Kwa upande wake Mhandisi Mzalishaji wa mgodi wa kokoto Eng. Juma Mizambwa amesema uzalishaji wa mataruma unaenda sambamba na uzalishaji wa kokoto ambapo kwa sasa mgodi huo unazalisha tani 180 kwa siku.

  Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa unatarajiwa kuanza Mwezi Desemba mwaka huu ambapo kwa mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imetenga shillingi Trilioni moja kwa ajili ya utekelezaji wake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi 1,000,030,100/= kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi (katikati) na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru  (kushoto) kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera .  Fedha hizo ni michango ya watumishi wa serikali na  Taasisi zake. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 20, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea hundi ya shilingi 1,000,030,100/= kutoka kwa  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi (katikati) na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru   (wapili kulia) na Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru  (kushoto) .Fedha hizo ni michango ya watumishi wa serikali na taasisis zake na makabidhiano yalifanyika Ofisni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 20, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. bilioni 1.040 kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

  Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo mchana (Jumanne, Septemba 20, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

  Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi alisema kiasi cha sh. 1,000,030,100 kimekusanywa kutoka kwa watumishi wa idara na Wizara zote  za Serikali na kwamba michango zaidi bado inaendelea kukusanywa.

  “Tunaamini michango hii itasaidia kuwafuta machozi wenzetu waliopatwa na maafa japokuwa tunajua haitatosha kurudisha kile walichopoteza. Tuna imani itasaidia kupunguza makali ya machungu waliyoyapata,” amesema.

  Hata hicyo, Balozi Kijazi amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba bado wanaendelea kukusanya michango kutoka kwenye nyingine ambazo zilichelewa kupata taarifa na kwamba wakikamilisha wataiwasilisha mapema iwezekanavyo.
                 
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea michango ya sh. milioni 40 na kati ya hizo, sh. milioni 20 zimetolewa na kampuni ya ujenzi ya CHICO ya China na sh. milioni 20 nyingine zimetoka kwa Umoja wa Wafanyabiashara na Wenye Viwanda wa India waliopo nchini (India Business Forum).

  Akiwasilisha mchango wake, Mwakilishi Mkuu wa kampuni ya CHICO hapa nchini, Bw. Guo Zhijian alisema wamesikitishwa na maafa yaliyotokea mkoani Kagera. “Tumefanya miradi mingi mkoani Kagera ikiwemo ujenzi wa barabara za urefu kilometa 300, kwa hiyo mkoa huu tunaujua zaidi. Tunatoa pole kwa wote waliopatwa na maafa  hayo,” amesema.

  Naye Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara na wenye viwanda kutoka India (IBF), Bw. Gagan Gupta alimweleza Waziri Mkuu kwamba wameshtushwa na tukio hilo na kwamba wametanguliza kiasi hicho ili kisaidie juhudi za Serikali katika kukabiliana na maafa hayo.

  “Bado tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wengine na tukipata michango zaidi tutaiwasilisha mapema iwezekanavyo,” amesema.

  Akitoa shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

  “Tunashukuru sana kwa michango yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa. Napenda niwahakikishie kuwa Kamati za Maafa za Mkoa, Ofisi ya Waziri Mkuu na kamati za wilaya, ziko pale kuhakikisha walengwa wanafikiwa,” ameongeza.

  Waziri Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. Amewaomba wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao.

  “Ninawaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao na wale walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya kuchangia maafa hayo,” amesisitiza.
  Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye namba 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa) au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

  Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu, lilisababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa. Kati yao, watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.

  Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 - DAR ES SALAAM.

  JUMANNE, SEPTEMBA 20, 2016.

  0 0

   Meneja masoko Huduma  za kifedha wa Vodacom Tanzania, Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa  mshindi wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa   wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka  kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-pawa wa beki ya CBA  Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.
  Meneja masoko Huduma  za kifedha wa Vodacom Tanzania, Noel Mazoya (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari namba ya  mshindi  wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa   wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka  kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-pawa wa beki ya CBA  Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.  Hadi sasa  washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2 wamejishindia milioni 20 mshindi wa jumla washilingi milioni 100 atapatika mwezi wa kumi.

  0 0

    Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wao kati ya wabunge wa Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Septemba 25 katika Uwanja wa Taifa ikiwa na lengo lenye kuchangia wa wahanga wa tetemeko la Ardhi wa wamkoani Kagera, Kulia ni nahodha wa timu ya Bunge, Sixtus Mapunda na kushoto ni Mkurugenzi wa benchi la ufundi Professa Maji marefu.
  Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuelekea Mchezo  utakaochezwa Septemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie jijini Dar es Salaam leo.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatarajiwa kucheza mechi ikiwa na lengo la kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera.

  Mwenyekiti wa klabu ya Michezo ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, William Ngeleja amesema kuwa mchezo huo utakaochezwa Septemba 25 katika Uwanja wa Taifa utajumuisha wabunge wanaochezea Simba na Yanga.

  Ngeleja amesema kuwa, wabunge hao watacheza mchezo huo kwa pamoja ila mwaka huu kumekuwa na sura mpya nyingi sana ambazo mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa lakini lengo kuu ikiwa ni kuchangia wahanga wa Kagera.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' amesema kuwa taifa limepata janga la taifa Kwahiyo anawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwachangia watanzania wenzetu ambao kwa kipindi hiki wanaishi katika mazingira mabaya.

  Viingilio vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu, 10000 na 15000  kwa  viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.

  Katika siku hiyo pia Kutakuwa na mechi ya mpira wa pete kati ya TBC na wabunnge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawake huku Wasanii wa  bongo fleva na Bongo Movie.

  0 0


  WANAFUNZI wataokosa nafasi za vyuo vikuu bado na wana nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu vya nje kupitia Global Education Link (GEL).

  Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakati kuondosha wanafunzi 200 kwenda katika vyuo vikuu vya nchini China, amesema GEL ni kampuni inayoongoza kupeleka wanafunzi kwenda vyuo vikuu vya nje vya Afrika Mashariki hivyo wazazi watumie nafasi kupeleka wanafunzi katika vyuo vya nje.

  Amesema kuwa Global Education Link(GEL) ina uhakika wanafunzi watakayehitimu watakuwa na mchango mkubwa kwa taifa katika Teknolojia ya uhandisi wa petrol , Biashara pamoja na utabibu.

  Mollel amesema kuwa wanafunzi wanaweza kukopeshwa kwa asilimia 50 na kulipa ndani miezi sita ikiwa kuhakikisha wanafunzi wanatimiza ndoto zao n kuwa na mchango a taifa. Aidha amesema kuwa wanafunzi wanaokwenda mazingira ya usalama ni uhakika kwa kuanza kwa safari hadi wanafika katika vyuo husika .

  Mollel amesema kuwa vijana wasikate tamaa Global Education Link (GEL) iko kwa ajili ya yao katika kuhakikisha ndoto zao hazipotei kutokana na kukosa nafasi katika vyuo vya ndani

  Amesema kuwa wazazi waache kuogopa gharama za kusoma vyuo vya nje kwani gharama za kusoma nje ni sawa na vyuo vya ndani hivyo vijana watumie furssa hizo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizunguza waandishi wa habari leo wakati akisafirisha wanafunzi 200 kwenda vyuo vikuu vya nchini China katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Wafatnyakazi wa Global Education Link (GEL) wakifanya uhakiki wa hati za kusafiria pamoja na Viza kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya China leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda Vyuo Vikuu nchini China wakiagana na familia zao kwa kupiga picha ya pamoja katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda katika Vyuo Vikuu nchini China wakiingia kwenye jengo la maalumu la ukaguzi kabla ya kuanza safari katika uwanja huo Jijini Dar es Salaam. 

  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo iliyofanyika katika ukumbi namba moja wa Mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Shaban Ali Lila,  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.
   Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipongezwa na mototo wake wa kike, Bi. Noera Kileo wakati wa hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.
  JK5: Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mahakama Kuu, leo Jijini Dar es Salaam.  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama Tanzania.
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (watatu kutoka kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Engera Kileo (kulia) wakati wa hafla ya kumuga Jaji huyo leo Jijini Dar es Salaam.  Mhe. Kileo ameagwa leo baada ya kutumikia takribani miaka 40 katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Idara ya Mahakama.
  Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.

  0 0

  Mkuu wa uwendeshaji wa Azam Media, Yahya Mahamedi, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akitangaza huduma mpya ya Full Dowzy kutwa mara tatu (kulia) ni Ofisa habari na Mawasiliano ya nje Azam media, Irada Mtonga. 

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KITUO cha Azam Tv yazindua Promosheni mpya ya 'Full Dowzy kutwa mara tatu' ambapo mteja mpya atapewa king'amuzi bure, dishi,remote na vifaa vyote bure pamoja na kufungiwa king'amuzi hicho bure endapo mteja huyo atalipia kifurushi kikubwa cha Azam Play mwaka mzima.

  Mteja wa Azam atatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 336,000 kwa mwaka ambapo ni sawa na kifurushi cha 28,000 cha Azam play kinachohusishwa na promosheni hii.

  Mkuu wa Uwendeshaji wa Azam Media, Yahaya Mohamed amesema kuwa promosheni hii itamsaidia mteja kupata king'amuzi kipya na kuokoa kiasi cha shillingi 165,000 na kupata chaneli zaidi ya 100.

  Mohamed amesema kuwa, kifurushi cha Azam Pure kina zaidi ya chaneli 45, Azam Plus Chaneli zaidi ya 65 na Azam Play  unapata chaneli zote zaidi ya 100 na kama mteja atatalipia hicho basi atapewa king'amuzi na kufungiwa bure.

  Uamuzi huo unakuja ili kuleta maudhui ambayo yanakidhi haja na viwango kwa watanzania na kwakuwa Azam ipo Afrika Mashariki na Kati lakini wameamua kuanza na hapa nchini.

  Mohamed amesema kuwa huduma hii itadumu kwa mwezi mmoja lakini itakuwa ni promosheni endelevu

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.


  Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.

  Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.


  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.


  Balozi Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.


  Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Bw. Fidelis Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam

  20 Septemba, 2016


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi  Mhe.George Simba Chawene akizungumza jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya ya kutembelea shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imeathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi.
   Waziriwa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na wahandishi wa habari kuhusu hatua ambayo serikali imechukua kusaidia ukarabati wa shule ya Ihungo ambayo imeathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi.KUlia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi  Mhe.George Simba Chawene
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi  Mhe.George Simba Chawene akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imeathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi.Kushoto kwake ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama.  Wafanyakazi wa VETA wakiendelea na ubomoaji wa Shule ya Ihungo ambayo  inavunjwa na kujengwa upya kwa msaada wadau na Serikali baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi la hivi karibuni Mkoani Kagera.

  0 0

  Na Ally Daud-Maelezo 

  SERIKALI imesambaza chakula salama na kutoa tiba bure kwa waathirika wa ugonjwa wa mlipuko wa sumukuvu katika mikoa ya Dodoma na Manyara uliotokea hivi karibuni.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu.

  Dkt. Kigwangala alisema Serikali imeandaa utaratibu wa kuwapelekea vyakula salama waathirika wa ugonjwa huo na kuteketeza vyakula vyenye sumukuvu.

  “Tumepanga utaratibu wa kupeleka vyakula salama kwa waathirika wa ugonjwa a sumukuvu katika mikoa husika bila malipo ili kusaidia kuondoa ugonjwa huo na kuteketeza mabaki ya vyakula vyenye vizaria vya sumukuvu” alisema Dkt. Kigangwala

  Aidha Dkt. Kigwangala alisema kuwa Serikali ipo bega kwa bega na waathirika wa sumukuvu ili kuhakikisha wanaondoa ugonjwa huo kwani tayari umethibitishwa na wataalamu na unapatikana kwenye mazao ya vyakula kama vile mahindi, uwele, mtama na karanga.

  Kwa mujibu wa Dkt. Kigangwala alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo Serikali imeamua kushirikiana na wataalamu wa kimataifa ili kuweza kuondoa ugonjwa huo kwenye vyakula vinavyolimwa nchini ili kuyawezesha mazao mazao hayo kuuzwa kwa urahisi hapa nchini.

  Dkt Kigwangala aliwashukuru watafiti hao kwa kugundua chanzo cha ugonjwa huo ambao unasababishwa na Jamii ya fangasi wanaoitwa Aspergillus wanaojikita zaidi kwenye vyakula na kuwataka wapate matokeo chanya ya kutokomeza sumukuvu.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Silo alisema katika mkutano huo watafiti hao wanatarajia kujadili na kupata ufumbuzi wa tafiti za vyakula mbalimbali ili visiendelee kuleta madhara kwa Watanzania.
  Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari na watafiti mbalimbali hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala wa kwanza kulia akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu Bw. Hiiti Silo kushoto na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na ubora Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed katikati wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam. 
  Watalaamu wa utafiti na wadau mbalimbali wa afya kutoka nchi mbalimbali  wakifuatilia kwa makini maelezo ya Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigangwala hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Picha zote Na Ally Daud-Maelezo 

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji  Mhe,Ali Abeid Karume pamoja na Viongozi mbali mbali mara alipowasili Kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Jendele-Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja leo ,inayojengwa na Idara ya Ujenzi ya Mfuko wa Barabara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Fundi Mkuu wa Mitambo ya ZBC Redio Nd,Ali Aboud (wa pili kushoto)alipotembelea mitambo ya  kurushia matangazo ya masafa ya Kati kiliopo Bungi Miembemingi leo
  Picha na Ikulu. 20/09/2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika Mstaafu, Samwel Sitta na mkewe Margaret wakati alipomjulia hali jijini Dar  es salaam Septemba 20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 1361 | 1362 | (Page 1363) | 1364 | 1365 | .... | 3282 | newer