Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1360 | 1361 | (Page 1362) | 1363 | 1364 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha fedha wa benki ya DTB, Joseph Mabusi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji wa saini wa mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom wenye thamani ya Milioni 250 kwa msimu wa mwaka 2016/17,na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Rais Jamali Malinzi.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamal Malinzi akitia saini mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom wenye thamani ya Milioni 250 akiwa sambamba na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya DTB Joseph Mabusi ikishuhudiwa na waandishi wa wa habari na viongozi wengine wa Bodi ya ligi pamoja na wawakilishi kutoka katika timu za ligi kuu.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamal Malinzi wakikabidhiana mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa DTB Joseph Musiba wenye thamani ya Milioni 250.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 250 na Benki ya Diamond Trust kwa ajili ya udhamini wa ligii kuu ya Vodacom.

  Mkataba huo wa msimu wa mwaka 2016/17, DTB wanaungana na wadhamini wengine ikiwa ni lengo la kuziwezesha timu hususani kwenye maendeleo ya soka nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Rais wa TFF Jamali Malinzi amesema kuwa amezitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

  Malinzi amesema kuwa, kuanzia sasa huduma zote za tiketi za kieletroniki zitakuwa chini ya benki ya Diamond Trust kwa msimu wa 2016/2017.

  Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya DTB  Joseph Mabusi amesema kuwa udhamini huu utasaidia zaidi kukuza soka na pia wanajivunia kuwa sehemu ya ligi kuu na wanaamini udhamini huu utazidisha ari ya kuwahudumia watanzania wote.

  Mabusi amesema, mbali na kuidhamini ligi kuu Vodacom pia wanadhamini timu ya ligi daraja la tatu Agathon iliyopo Mbagala na nia wadhamini wa michuano ha Afrika Mashariki na Kati CECAFA Kagame Cup mwaka 2015.

  Mkataba huo utakuwa chachu ya maendeleo ya soka kwa nchi pamoja na kuzifanya timu kujituma zaidi uwanjani pia unatarajiwa kuwa endelevu na kila mwaka kutakuwa na mabadiliko mbalimbali kwenye mkataba huo.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga- MAELEZO.
  SEKTA  ya kilimo inayojumuisha ukulima, ufugaji na uvuvi, imeendelea kuwa sekta kiongozi katika kutoa ajira na kuwa tegemeo la maisha kwa asilimia 75 ya Watanzania wanaoishi Vijijini.
  Kujitosheleza kwa chakula ni muhimu kwa usalama na utulivu wa nchi. Taarifa ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonyesha kuwa kiwango cha kujitegemea kwa chakula kimeongezeka kutoka asilimia 95 mwaka 2005 hadi asilimia 125 mwaka 2014.  
  Pamoja na uzalishaji kuwa mkubwa, inaelezwa kuwa kiasi kikubwa cha mazao ya nafaka yanayozalishwa nchini  huharibika na kupotea baada ya kuvunwa. Upotevu huo hutokana na matumizi ya mbinu duni za kuhudumia mazao wakati wa uvunaji, usafirishaji na uhifadhi kwenye maghala.

  Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka na asilimia 80 ya nafaka huzalishwa na kuhifadhiwa vijijini, ambapo hata hivyo uwezo mdogo na maghala duni yanayotumiwa na wakulima vijijini wakati wa kuhifadhi huruhusu upotevu wa nafaka hadi asilimia 10.
  Takwimu za Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonyesha kuwa, asilimia 30 hadi 40 za nafaka zinazovunwa hupotea kila mwaka nchini.
  Mahindi ni miongoni mwa  mazao makuu ya nafaka hapa nchini yanayolimwa nchini Huzalishwa kwa wastani wa tani 2,393,000 kwa mwaka ambao ni sawa na asilimia 63 ya mazao yote ya nafaka.
  Takwimu za Wizara ya Kilimio, Mifugo na Uvuvi zinaonyesha uzalishaji wa mahindi unaongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 2011 uzalishaji wa mahindi katika nchi nzima ulifikia tani 4,341, mwaka 2012 tani 5,104 na mwaka 2013 tani 5,174.
  Taarifa kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi zinaeleza kuna uwezekano mkubwa wa kuharibika kwa tani 40,000 za mahindi yanayoendelea kununuliwa katika msimu huu na Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kutokana na uhaba wa maghala ya kuhifadhi.
  Wakala katika mikoa hiyo anakabiliwa na changamoto ya uwezo mdogo wa kuhifadhi chakula hicho katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mahindi na kusababisha akiba kubwa ya chakula kuhifadhiwa nje ya maghala.
  Utafiti uliofanywa na mradi wa USAID Tuboreshe Chakula umebaini kuwa kutokana na uhifadhi duni na mbinu bora za kilimo cha mazao ya nafaka kama mahindi, alizeti na maharage unasababisha ukungu kwenye mazao hayo  hali inayosababisha sumu kuvu yenye madhara makubwa kwa mlaji.

  Mhadhiri Mwandamizi wa chuo kikuu cha sayansi cha Nelson Mandela, Dk. Martin Kimanya anasema sumu hiyo haiwezi kuondolewa kwa kupika chakula na badala yake watumiaji wanapaswa kuchagua nafaka kwa kuondoa zile ambazo zimebadilika rangi na kuwa na ukungu.

  “Wakati Tanzania ikiwa katika nafasi ya nne kwa ulizalishaji wa zao la mahindi barani Afrika, imeelezwa kuwa watumiaji wa mahindi wanakula 30% ya sumu kuvu inayotokana na uhifadhi duni wa mahindi” anasema Prof Kimanya.
  Kutokana na tatizo hilo mradi wa USAID tuboreshe chakula umeanza mikakati ya kuinusuru jamii ikiwemo kwa kutoa elimu kwa wasindikaji wa vyakula pamoja na wakulima ili kufahamu sumu kuvu na madhara yake.

  Katika  kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula nchini, Serikali kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula Nchini (NFRA) imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.
  “Serikali  kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya ” anasema Majaliwa
  Aidha Majaliwa anasema Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
  Anasema maghala yanakayojengwa si kwa ajili ya kuhifadhi chakula tu bali hata kuweka dawa kwa urahisi, kukausha, kuondoa unyevunyevu na kusafisha kwa kiwango kinachohitajika.
  Waziri Mkuu anasema kuwa anasema ujenzi wa magahala hayo utaliongezea taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.
  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba  anasema Serikali imeiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA)  kununua mahindi moja kwa moja kutoka  kwa wakulima na kuachana na mfumo wa zamani ambapo wakulima walikuwa wakipeleka mahindi kwenye wakala huo au kupitia kwa wanunuzi binafsi.
  Kwa mujibu wa Waziri Tizeba anasema mkulima atauza kuanzia tani moja hadi mbili na kiwango cha mwisho cha ununuzi kufanywa na NFRA  ni tani tano.
  Aidha Dkt. Tizeba anasema  serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya ununuzi wa mahindi kutoka kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini. 
  Mary Sheto kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi anasema Serikali imeweka mikakati madhubuti kwa ajili ya kuwasaidia wananchi maskini waliopo  vijijini ambao asilimia 98 hutegemea kilimo kama njia kuu ya uchumi na maisha yao ya kila siku. 
  Anasema lengo la Serikali ni kuzalisha tani milioni tano za mahindi ili nchi ijitosheleze kwa chakula kwa nia ya kupunguza mfumuko wa bei ya chakula na kuongeza kipato kwa mkulima hatimaye kukuza uchumi  na kuuza ziada ndani na nje ya nchi ambako imebainika kuwa na soko kubwa la mazao hayo.
  Kwa mujibu wa Sheto anasema Serikali imefanya mazungumzo na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa ajili ya ununuzi wa mahindi hayo na wameonesha kukubali, lakini kwa masharti ya kuzingatia ubora wa mahindi husika.
  “Kwa kuzingatia hilo, Serikali katika wilaya ambazo zitaanzishiwa utaratibu huo, wakulima wataelekezwa namna ya kuandaa zao hilo kwa ubora unaotakiwa kisha kuwahimiza kuwa katika vikundi huko huko vijijini ambako ununuzi utafanyika” anasema Sheto.
  Akifafanua zaidi Sheto anasema Serikali itahakikisha maghala mapya yanajengwa na yale ya zamani yataboreshwa kwa kukarabatiwa, ili mahindi yawe katika mazingira safi kwa lengo la kumvutia mnunuzi atakayenunua zao hilo katika soko la pamoja la wakulima.
  Anaitaja Mikoa itakayofaidika na mpango huo kuwa ni Rukwa /Katavi, Ruvuma, Njombe na Iringa, mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dodoma na lingine katika mikoa ya Tanga/Arusha na Kilimanjaro.

  0 0


   Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo ya Mwongozo wa Uwekezaji na Usimamizi wa Miradi ya Umma yanayoendelea katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya. Kushoto kwake ni Mhandisi Happiness Mgalula Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma na Dkt. Joihn Mduma, Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi ni Dkt. Lorah Madete, Kaimu Nibu Katibu Mtendaji, anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla.
   
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgani rasmi (hayumo pichani)
  Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe, Iringa na Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
  0 0

   Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) akipokea zawadi ya nembo ya jeshi la China kutoka kwa Mkuu wa tawi la ugavi wa China Luteni Jenerali Liu Shengjie alipomtembelea  ofisini kwake jana makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa tawi la Ugavi wa jeshi la china Luteni Lenerali Liu Shengjie akipokea zawadi ya nembo ya JWTZ  kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) alipomtembelea  ofisini kwake jana makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maofisa wa jeshi toka China ukiongozwa na Mkuu wa Ugavi wa jeshi hilo Luteni Jenerali liu Shengjie mara baada ya kumtembelea ofisini kwake makao makuu ya jeshi jana jijini Dar es salaam.(Picha na  Luteni Selemani Semunyu)

  0 0
 • 09/19/16--07:13: Article 18


 • 0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman , akionesha   nakala ya kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama ya Tanzania, alipokuwa katika Mkutano kati yake na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo katika Ofisi za Mahakama ya Rufani (T), lengo la Mkutano huo lilikuwa ni kutoa taarifa juu ya uzinduzi rasmi wa Mpango huo utakaofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa niaba ya Mhe. Rais, mnamo tarehe 21.09.2016, katika jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, kulia ni Mhe. Katarina Revocati, Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari walioshiriki katika Mkutano huo, miongoni mwa mambo aliongelea ni pamoja na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Maboresho wa huduma utakaotekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB).
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini. 
  (Picha na Mahakama ya Tanzania)

  0 0

  On September 19, 2016, at a ceremony at the U.S. Embassy in Dar es Salaam, United States Chargé d’Affaires, a.i. Virginia Blaser awarded community grants to 22 organizations working to improve the lives of Tanzanians.  The grants awarded today will directly benefit more than 30,000 people in 16 regions across the country and will improve services and opportunities in water and sanitation, health, education and economic development. 
  Awarded under the U. S. Embassy’s Community Grants Program, these grants provide direct assistance to small, community-based, improvement projects through the “Ambassador's Special Self-Help Fund” and the “Ambassador's Fund for HIV/AIDS Relief.”  The Special Self-Help Fund provides direct assistance grants to Tanzanian community organizations for projects designed to benefit villages and urban communities.  The Fund for HIV/AIDS Relief provides assistance specifically to communities heavily impacted or vulnerable to HIV/AIDS.   
  “Behind each grant is an invaluable contribution of time, energy and dedication, which translates into a powerful impact.  We are proud to be involved with such a wide range of partners, all of whom have taken the initiative to tackle critical issues in their communities,” commented Chargé d’Affaires, a.i. Virginia Blaser.
  The Ambassador's Special Self-Help Fund was established in 1965, during Mwalimu Julius Nyerere’s first presidential term.  For over 50 years, these grants have helped community-based organizations in every region of Tanzania to improve the lives of local Tanzanians by building schools, providing access to clean water, sanitation, utilizing solar energy and starting new commercial initiatives.


  The Ambassador's Fund for HIV/AIDS Relief started in 2009 and has provided grants to 81 community-groups in Tanzania. Both programs continue the strong tradition of U.S.-Tanzania citizen partnership.

   United States Chargé d’Affaires, a.i. Virginia Blaser with representatives from various organizations after she awarded community grants to 22 organizations working to improve the lives of Tanzanians.  The grants awarded at a ceremony held at the U.S. Embassy in Dar es Salaam will directly benefit more than 30,000 people in 16 regions across the country and will improve services and opportunities in water and sanitation, health, education and economic development
  United States Chargé d’Affaires, a.i. Virginia Blaser (center) and Community Grants Coordinator Mike Connors (second from right) in a group photo after she awarded community grants to 22 organizations working to improve the lives of Tanzanians.  The grants awarded at a ceremony held at the U.S. Embassy in Dar es Salaam will directly benefit more than 30,000 people in 16 regions across the country and will improve services and opportunities in water and sanitation, health, education and economic development. 
  (Photo Courtesy of the  U.S. Embassy)


  0 0

  WAZIRI MKUU Mhe Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japani nchini, Mheshimiwa Masaharu Yoshinda ambaye amemueleza kwamba Serikali yake ipo tayari kukarabati shule zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. 
   Pia imeomba kupatiwa orodha ya mahitaji ya dharura yakiwemo mahema, mablanketi, dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo. 
   Balozi Yoshinda ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 19, 2016) wakati alipokutana na Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya maafa yalitokea Kagera. 
   Kwa upande wake Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Japani kwa hatua hiyo na kukiagiza Kitengo cha Maafa kilicho chini ya Ofisi yake kuwasiliana na Ubalozi wa Japan nchini na kuwasilisha orodha ya shule zilizoharibika pamoja na mahitaji ya dharura. Wakati huo huo Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 2.5 za mchele, magodoro 200, mablanketi 100 na fedha taslimu sh. milioni 10 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko hilo. 
   Msaada huo umetolewa na wadau mbalimbali akiwemo Ofisa Utumishi wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini, Bi. Anna Jiang aliyetoa magodoro 200 yenye thamani ya sh. milioni sita. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, George Shumbusho aliyetooa sh. milioni 10 pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya Serikali ya Tanzania na China, Bw. Joseph Kahama aliyetoa mchele tani 2.5 pamoja na mablanketi 100 vyote vikiwa na thamani y ash. milioni 10. 
  Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. 
   Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 wametibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri. Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida kuhusu namna  ambavyo Japan inaweza kusaidia waathika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Mazungumzo yao yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dares salaam Septemba 19, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida na afisa wake  kuhusu namna  ambavyo Japan inaweza kusaidia waathika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Mazungumzo yao yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dares salaam Septemba 19, 2016. Picha na habari na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Saidick akihitimisha ukaguzi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza asakari walitekeleza vyema majukumu yao.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34  waliotekeleza vyema majukumu yao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick akitoa cheti kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline, Ibrahim Shayo akitambua mchango wa wadau kwa jeshi la Polisi. 
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0  0 0

  Na. Abushehe Nondo na Immaculate Makilika- MAELEZO

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman amesema kuwa Serikali inatarajia kuzindua mpango mkakati wa Mahakama ya Tanzania kwa miaka 5 unaolenga kuboresha huduma za kimahakama nchini.

  Aidha Jaji Mkuu alisema uzinduzi wa mpango huo utaenda sambamba na mradi wa maboresho wa huduma za utoaji haki nchini uliogharimu kiasi cha Tsh Bilioni 140.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Jaji Chande alisema kuwa mradi huo una nguzo tatu ambazo ni utawala bora na uwajibikaji , fursa ya kutoa na kupata haki na uharakishaji wa mashahuri ambapo kwa pamoja umekusudia kutoa haki kwa wote na kwa wakati.

  “Katika kujenga imani ya wananchi kwa mahakama tunataka kufikia sehemu ambapo mtu yeyote akileta shauri lake Mahakamani basi litasikilizwa kwa wakati” alisema Jaji Chande.

  Aliongeza kuwa taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia 47 ya Watanzania hawana fursa sawa ya kupata haki ya Mahakama katika maeneo waliopo hususani mikoani kwa kuwa mikoa mingi haina Mahakama Kuu, hivyo mpango huo utakaozinduliwa utalenga kuboresha utendaji na utoaji huduma za kimahakama nchini.

  Akizungumzia kuhusu mradi wa maboresho ya huduma za Mahakama ambao unaandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia Jaji Chande alisema kuwa mradi huo unalenga kuimarisha mifumo ndani ya Mahakama, kuendesha kesi na utoaji wa hukumu kwa wakati.

  Jaji Chande aliongeza kuwa mradi huo utapanua wigo wa utoaji huduma za kimahakama ambapo itatoa fursa za mafunzo endelevu kwa watumishi wa Mahakama 6400 wa ngazi mbalimbali.

  Aidha alisema mpango huo utasaidia kuimarisha Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kukijingea uwezo wa kutoa taaluma bora kwa watumishi pamoja na wadau katika masuala ya Sheria.

  Jaji Chande alisema tayari mradi huo umewezesha kujengwa kwa Mahakama tano za kisasa zilizopo katika maeneo ya Kibaha, Kawe, Kisarawe, Kigamboni na Bagamoyo ambazo zitakuwa mfano wa uanzishwaji wa Mahakama za kisasa nchini.

  Mradi huo unaogharimu bilioni 140 utazinduliwa Kibaha mkoani Pwani Septemba 21 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

  0 0

   
    Mmoja wa kamishna rais mstaafu Jakaya Kikwete.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/video capture).
   
  Mmoja wa makamishna wa tume ya kimataifa ya kusaka uchangishaji kwa elimu Duniani, amesema mapendekezo yao ya kuinua kiwango cha elimu yasipozingatiwa, watoto wengi zaidi hatawakuwepo shuleni ifikapo mwaka 2030.
  Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania ameiambia Idhaa hii jijini New York, Marekani baada ya uzinduzi wa ripoti yao kuwa,
  Mapendekezo yao ni pamoja na mbinu mpya za uchangishaji ikiwemo taasisi za kimataifa za kibenki akisema kinachohitajika..

  Ripoti hiyo inasema serikali zisipowezeka katika elimu, watoto katika nchi hususan za kipato cha chini watatwama kwenye mzungumzo wa umaskini na kusalia bila stadi zinazohitajika.

  0 0

  MKURUGENZI Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel amesema wanafunzi wanaokwenda nje waliohitimu masomo katika vyuo vya nje wanatakiwa watafutwe na waajiri na sio wawe wa kutafuta ajira.

  Mollel ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina na wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka kesho katika vyuo vikuu vya nchini China, amesema kuwa kutokana na vyuo hivyo kuwa na vifaa vya kujifunzia wanafunzi wakitumia vizuri katika soko la ajira watatafutwa.

  Mollel amesema nchi haina tatizo la ajira hivyo watu wanatakiwa kuwa na uwezo binafsi ambao utamfanya mwajiri kutafuta mtu wa kumuajiri hivyo wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo wanatakiwa kutumia maarifa ya kuja kuzalisha nchini.

  Amesema wazazi watumie muda wao katika kuwafuatilia watoto wao wanaosoma nje ili kuweza kuona thamani ya fedha wanazozitoa na elimu wanayoipata.

  Aidha amesema kuwa wale ambao wanahitaji vyuo vya nje bado nafasi zipo na wanafunzi wote watafuata taratibu zote ikiwa ni pamoja Tume ya Vyuo Vikuu nchini kujiridhisha na vyuo wanavyokwenda. Mollel amesema haitakuwa tayari kuona wanafunzi wanahitimu vyuo vya nje kupitia GEL kuwa hawatambuliki.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika semina ya wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka kesho kwenda vyuo vikuu vya nchini China, iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wanaokwenda nje wakichukua tiketi pamoja na viza kwa ajili ya safari kwenda katika vyuo vikuu vya nchini China iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wazazi na wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel hayupo pichani katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam. 

  0 0


  0 0


  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na WIzara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  imeanzisha na kuzindua namba maalumu kwa watanzania kuchangia ili kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mnamo tarehe 10 Septemba 2016 majira ya mchana huko Bukoba mkoani kagera. Watu 17 wamepoteza maisha na kuacha mamia wakiwa hawana makazi kufuatia tetemeko hilo.
  Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Huduma za jamii Hawa Bayumi alisema, “Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na wanafamilia kutokana na tetemeko hili pia limewaacha mamia wakiwa hawana makazi.  Leo tunaungana na wakazi wa Kagera katika janga hili kwa kutoa mchango kwa waathirika wa tetemeko na kuwaomba watanzania wote kuungana nasi kwa kuchangia kupitia namba maalumu 155990 itakayotumika kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa janga hili wanaohitaji msaada wa haraka.
  Jinsi ya kuchangia ni rahisi,

  1.    unapiga *150*60# kuingia kwenye airtel money

  2.       unachagua 5 yaani lipa bili kwa Airtel Money,

  3.        kisha unachagua 4 andika jina la biashara ambapo utaandika 155990,

  4.       Kisha ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuchangia

  5.       Weka kumbukumbu namba ambayo ni  jina lako

  6.       Kisha malizia kwa kuweka namba ya siri.  0 0

  Waziri Mkuu, Kaassim Majliwa akipokea msaada wa mgodoro 200 yenye thamani ya sh. 6, 000,000 kutoka kwa Bi. Anna Jiang wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwake jijjini Dar es salaam Septemba 19, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni 10 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya EXIM, Bw. George Shumbusho (watatu kulia) ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 19, 2016. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki hiyo, Fredrick Kanga, wapili kushoto ni Chief Finance Officer wa benki hiyo, Selemani Ponda na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa benki ya Exim, Abdul Nkondo. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Msaada wa tani mbili na nusu za mchele na mablanketi 100 vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Septemba 19, 2016. Kulia ni Meneja wa Uwekezaji wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation, Bw. Le Tong, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Urafiki Kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama, na wapili kushoto ni Afisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Nice Munissy. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akipata maelezo yautendaji kazi, kwa msaidizi Mkuu wa utangazaji ZBC Radio Salum Othman Said alipofanya ziara kuona utendaji kazi zao.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akizungumza na watangazaji wa ZBC Radio katika Studio za Shrika hilo Raha leo mjini Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Muhamed Shein (katikati) katika picha ya pamoja na Watangazaji wa ZBC Radio.

  0 0

   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta anayeendelea kupata matibabu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mke wa Mzee Sitta, Mama Margaret Sitta. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam
   Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta akiongoza Sala mara baada ya kujuliwa hali na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto ni Mke wa Mzee Sitta, Mama Margaret Sitta.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wafanyakazi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Magazeti hayo zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wafanyakazi hao wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakwaza (kulia) pamoja na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti hayo Ramadhani Mkoma wakwanza (kushoto) wakiomba dua mara baada ya kumaliza kuzungumza na wafanyakazi hao jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1360 | 1361 | (Page 1362) | 1363 | 1364 | .... | 3282 | newer