Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

PPF yakabidhi mfano wa hundi katika matembezi ya hisani ya kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera

0
0
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto), ambayo waliiahidi kwa Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuchangia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele.
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassani Mwinyi (wa tatu kushoto)  akiongoza matembezi ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na maeneo ya jirani. Wengine alioambatana nao ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maige, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi, Mbunge wa Jimbo la Muleba, Prof. Anna Tibaijuka pamoja na wengine wengi.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza katika hafla hiyo.


KUZIONA SERENGETI BOYS NA CONGO BRAZZAVILLE NI BUREEE..... LEO UWANJA WA TAIFA

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Serengeti Boys  katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 unapigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa dhidi ya Timu ya vijana ya Congo-Brazzaville.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mhe. Nape amesema milango ipo wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri katika  mechi hii ambayo ni muhimu sana kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.

“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki, tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa timu ya Congo-Brazzaville” alisema Mhe. Nape.

Waziri Nape amekutana na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na kuwataka watanzania  kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa kuwashangilia  na kuwatia moyo.

Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ila zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo Fleva.

Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17 ambapo katika mchezo huo watahitaji ushindi na baadaye kufanya mechi ya marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini Congo-Brazzaville.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye akipena mkono na mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys" alipokutana nao mapema leo asubuhi. Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

KUONA SERENGETI BOYS NA CONGO BRAZZAVILLE LEO BURE, VIJANA WAJAZWA NOTI

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa ofa kwa wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016 katika mchezo wa mpira wa miguu utakaozikutanisha timu za vijana taifa za Tanzania na Congo-Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka. Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo. 

Nape alitoa ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi Septemba alipata kifungua kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako alitoa Sh 200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti Serengeti Boys ambao walichangia Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka kwa wadau wengine.

Nape ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”

Kuingia bure kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal Malinzi amemshukuru Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo imelenga kutoa hamasa kwa Watanzania kwenda kushangilia timu yao.

Katika mchezo huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema kwamba amemaliza kila kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani leo kuishangilia timu yao, utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako mpiga kipenga atakuwa Nelson Fred akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie wakati mwamuzi wa akiba akiwa Allister Barra. Kamishna wa mchezo atakuwa Gladmore Muzambi kutoka  Zimbawe.



MCHEZAJI BORA WA MWEZI AUGUST WA SIMBA SPORT CLUB AKABIDHIWA TUZO YAKE

0
0
Mchezaji bora wa Klabu ya Simba kwa mwezi Agosti, 2016 Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' akikabidhiwa  tuzo yake na Imani Kajula mbele ya mashabiki waliokuja kushuhudia mchezo wa kati ya Azam Fc na Simba Sc. Pamoja na tuzo hiyo Zimbwe Jr pia amekabidhiwa Tsh 500,000/= kama sehemu ya zawadi kwa mchezaji bora. 
Hii ni tuzo ya kwanza kutolewa kwa msimu huu 2016/2017 ambapo ilikabidhiwa kwa Zimbwe Jr na Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula pamoja na Makamu wa Rais wa Simba Geophrey Nyange kabla ya mchezo wa kuanza, mchezo ambao ulikwisha kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuifunga Azam FC kwa goli moja bila, goli lililofungwa na Shiza Kichuya Dakika ya 68 Kipindi cha Pili.

UVCCM WAISHAURI SERIKALI KUTUMIA JESHI LA JWTZ KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI NA KUTATHMINI PAMOJA NA KUGAWA MISAAADA KWA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

0
0
  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

UMOJA wa vijana wa chama cha CCM Taifa(UVCCM)wameishauri na kuiomba selikari kutumia jeshi la wananchi JWTZ  katika zoezi la kuhakiki na kutathimini pamoja na kugawa misaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Shaka Hamidu Shaka alitoa ombi hilo kwa kamati ya maafa ya Mkoa ambayo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu alisema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa waathirika wa tetemeko kuwa hawatendewi haki na wale wanaopita kufanya tathimini kwenye nyumba zao zilizoathirika.

"Jeshi la wananchi hawana chama wala Dini hivyo hawezi kubagua mtu nina amini watatenda haki kwa kila mwananchi aliyeathirika na itasaidia kuondokana na migogoro ambayo inaweza kujitokeza kwa wale watakaokosa haki zao pia watafanya zoezi kwa wepesi na uharaka zaidi kuliko hali ilivyo sasa"alisema Shaka

Wakati huo huo umoja huo umekikabidhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu.

"Umoja wa UVCCM Taifa tunawapa pole sana wahanga wote wa tetemeko la ardhi,ila tunawaomba wanasiasa wasitumie tetemeko hili kama sehemu ya kutangaza siasa zao,hili ni janga za watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za vyama wala dini zao"alisema

Baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu alisema kuwa mambo ya ubaguzi kwa waathirika wa tetemeko ameshayakemea sana na anaendelea kuyakemea ndiyo maana ameelekeza misaada yote ipitie ofisini kwake ili iwafikie walengwa kwa utaratibu mahususi uliopangwa.

"Endapo mtu yeyote atabainika anafanya ubaguzi nitamchukulua hatua kali sababu bado misaada inahitajika sana"alisema Mkuu wa Mkoa.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa vija Shaka Hamidu Shaka akichangia damu kwenye viwanja vya mashujaa Mkoani Kagera kwaajili ya majeruhi wa wahanga wa tetemeko la ardhi.
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamidu  Shaka akibadhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu kwaajili ya wa waathirika wa tetemeko la ardhi

Waziri Nape atoa million tano kwa Serengeti Boys.

0
0

Na Shamimu Nyaki- WHUSM.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa kiasi cha shilingi million tano kwa timu ya Serengeti Boys kama motisha katika mchezo wao dhidi ya Congo Brazivile utakayochezwa leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es Salaam.

Akikabidhi pesa hizo leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Waziri Nape amewataka wachezaji hao kujituma zaidi katika mechi hiyo ili wapate ushindi utakaowawezesha kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 .

“Watanzania wote tupo pamoja na nyie endeleeni kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya pili, Sisi kama Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia heri ili mlete heshima kwa Taifa.”Alisema Mhe. Nape.

Kwa upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw.Bakari Shime amemuhakikishia Waziri na Watanzania kwa ujumla kuwa mechi ya leo watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo tayari kuivaa Congo Brazavile.

Aidha Nahodha wa Timu hiyo Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata ushindi.

“Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi ili tusonge mbele zaidi ” Aliongeza Nahodha Makame.

Timu hiyo ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wachezaji wa Serengeti Boys katika hafla fupi ya kuwakabidhi Shilingi Milioni Tano kama motisha kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa maelezo juu ya maaandalizi ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari Shime akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kwa kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.

Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame akiahidi kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kuibuka na ushindi dhidi ya Congo-Brazaville katika mechi itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimkabidhi Millioni tano Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi Makame kama motisha kabla ya kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM) .

MDAU KELVIN AHITIMU KIDATO CHA NNE SHULE YA TUSIIME, DAR ES SALAAM

0
0
 Kelvin akipongezwa wakati akipita mezakuu kupokea cheti chake cha kuhitimu kidato cha nne wakati wa mahafali hayo.
 Kijana Kelvin Jackson Kalasha akitafakari kwa furaha, wakati wa Mahafali ya kumaliza kidato cha Nne katika shule ya Tusiime, Kampasi ya Tabata, Dar es Salaam, jana, Septemba 17, 2016
 Kijana Kelvin Jackson Kalasha (Kushoto) akiwa na wahitimu wenzake wa kidato cha nne, wakati wa Mahafali ya kumaliza kidato hicho katika shule ya Tusiime, Kampasi ya Tabata, Dar es Salaam, jana, Septemba 17, 2016
 "Mama Mdogo", Kijana Kelvin akimwambia Caroline Kisamo, mwanzoni mwa sherehe hiyo ya mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Tusiime, jana. Katikati ni Mama Kelvin, Ever Kalasha
Wanafamilia wakiwa kwenye mahafali hayo. Kushoto ni Caroline Kisamo.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MCHEZAJI BORA WA MWEZI AUGUST WA SIMBA SPORT CLUB AKABIDHIWA TUZO YAKE

0
0



Mchezaji bora wa Klabu ya Simba kwa mwezi Agosti, 2016 Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amekabidhiwa tuzo yake mbele ya mashahiki waliokujakushuhudia mchezo wa kati ya Azam Fc na Simba Sc. Pamoja na tuzo hiyo Zimbwe Jr pia amekabidhiwa Tsh 500,000/= kama sehemu ya zawadi kwa mchezaji bora. Hii ni tuzo ya kwanza kutolewa kwa msimu huu 2016/2017 ambapo ilikabidhiwa kwa Zimbwe Jr na Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula pamoja na Makamu wa Rais wa Simba Geophrey Nyange kabla ya mchezo wa kuanza, mchezo ambao ulikwisha kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuifunga Azam FC kwa goli moja bila, goli lililofungwa na Shiza Kichuya Dakika ya 68 Kipindi cha Pili.

Plan International waishauri VETA kuongeza walimu wa mahitaji maalum

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Kisarawe .

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International wameishauri Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) kuongeza walimu waliobobea katika ufundishaji wa wanafunzi walemavu ili kuhakikisha wanapata elimu sawa na wengine. 

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) – Tanzania, Simon Ndembeka baada ya kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaohitaji kupatiwa elimu ya ufundi katika vyuo hivyo. 

Meneja Mradi amesema kuwa nyakati za kuwaficha walemavu majumbani zimekwisha na kwa sasa wazazi wanafahamu kuwa ulemavu sio mwisho wa maisha hivyo muamko wa walemavu wanaohitaji kusoma umekuwa mkubwa tofauti na zamani. 

“Mradi huu umetenga asilimia 10 kwa ajili ya jamii ya vijana wenye ulemavu kupatiwa mafunzo ya ufundi katika chuo cha VETA ili baadae waweze kuendesha maisha yao lakini lengo hilo lina changamoto kubwa ya upungufu wa walimu wa taaluma hiyo hivyo, tunaishauri VETA kuongeza walimu wa aina hiyo ili kukidhi uhitaji wa idadi ya wanafunzi walemavu”, alisema Ndembeka. 

Ndembeka ameongeza kuwa kitendo cha kuwawezesha vijana wenye ulemavu ni moja ya lengo la mradi huo kwani kundi hilo ndilo kundi lenye changamoto nyingi za kimaisha kuliko kundi lingine lolote hivyo kuwapatia elimu kutawasaidia kuweza kupata ajira au kujiajiri na hatimaye kuweza kuyakomboa maisha yao. 

Aidha, Ndembeka ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wao wa kutoa misaada ya mikopo, elimu, maeneo ya vijana kufanyia mazoezi pamoja na ushiriki wao kama wageni rasmi katika mahafali mbalimbali za vijana wanaohitimu elimu ya ufundi chini ya mradi huo. 

Kuhusu suala la kuwasaidia vijana kupata ajira amefafanua kuwa mara nyingi wamekuwa wakifanya vikao na waajiri wa sekta mbalimbali nchini ili kuwajengea ufahamu waajiri juu ya uwepo wa vijana hao pamoja na kujadili jinsi ya kuwasaidia kwa kuwapatia ajira. 


Mradi huo wa miaka mitatu unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

Baadhi ya Vijana waliohitimu katika fani ya ufundi wa magari chini ya Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) wakifanya mazoezi ya kurekebisha magari katika gereji ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, (mwenye tisheti jekundu) ni fundi msaidizi wa gereji hiyo, Haji Faki.
Meneja wa Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) – Tanzania, Simon Ndembeka akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uhitaji wa walimu wa mahitaji maaalum watakaoweza kukidhi idadi ya wanafunzi walemavu wanaohitaji kupatiwa elimu ya ufundi katika Chuo cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA) chini ya mradi huo.

KUTOKA VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 94: Miley Cyrus, Natalie Portman, Kylie Jenner, Zendaya and Taylor Swift

0
0
Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki ambacho hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo Wiki hii, sikiliza alichosema Miley Cyrus, mabadiliko katika maisha ya mcheza sinema Natalie Portman,alichofanya Dada mdogo wa Kim Kardashian,kauli ya Zendaya juu ya ubaguzi wa rangi na pia Tay;or Swift na nyota wengine waliowabwaga wapenzi wao KARIBU

Mhe. Jenista Mhagama akutana na Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifungua kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera Septemba 18, 2016, kulia kwake niKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.Salum Kijuu akiwasilisha taarifa ya tathimini ya hali ya waathiri wa Maafa ya Tetemeko la Ardhi mkoani hapo wakati wa kikao cha Kamati ya Mkoa ya Uratibu wa Maafa.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe.Deodatus Kinawiro akichangia hoja wakati wa Kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa Kagera.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakiendelea na kikao cha kujadili na kufanya tathimini ya hali ya athari ya Maafa ya Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAPENZI WA SOKA KUNUFAIKA NA ‘SOKA BANDO’ YA VODACOM

0
0
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella (kulia) akishuhudia mojawapo ya mechi za Vodacom Premier League katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara , “Vodacom Premier League” imesikia kilio cha mashabiki na wapenzi wa soka nchini na kuamua kuwaletea kifurushi maalumu kinachojulikana kama ‘Soka bando’ ambacho ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote.

Vodacom Tanzania imebuni kifurushi hiki kwa ajili ya kuwapatia taarifa za soka za hapa nchini na ligi za kimataifa kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-Kifurushi cha ‘Soka bando’ kitakuwa kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa saa 24. 

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella amesema “Kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-mashabiki wa soka wanaotumia mtandao wa Vodacom watapata taarifa  mbalimbali za soka za hapa nyumbani na kimataifa kwa kipindi cha siku 7,dakika 14 za muda wa maongezi Vodacom kwenda Vodacom, dakika 2 za muda wa maongezi kwa mitandao  yote na jumbe fupi za maneno (SMS) 20 kwa kipindi cha masaa 24”

Alisema Vodacom Tanzania imeleta kifurushi hiki cha ‘Soka bando’ kipindi hiki ambacho msimu wa ligi ya VPL unaendelea ni furaha kwa Mtandao wa Vodacom kuwawezesha mashabiki kupata taarifa za ligi kwa urahisi kupitia mtandao wake ikiwemo kuwapatia burudani wateja wake na watanzania wote kwa ujumla.

“Kampuni inathamini na kutambua mchango wa mashabiki katika kukuza ligi hii tangu ilipoanza kuidhamini hivyo ndio maana tumewaletea kifurushi hiki ili wapate  burudani na taarifa za soka kwa wakati na kwa gharama nafuu”.Alisema Mwiyombella.

Ili kununua kifurushi hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga  namba *149 * 01#, na kuchagua ‘Soka Bando’. Baada ya  hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga”  “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya  Mspoti.vodacom.co.tz.

Wateja watakaojiunga na huduma hii pia watapata  nafasi ya kufurahia ofa na zawadi mbalimbali kutoka  Vodacom kama vile muda wa bure wa maongezi, sms au  MB za akuperuzi inteneti hususani timu wanazoshabikia zitakapokuwa zimeibuka na ushindi wa mchezo.

Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania  bara unaendelea  katika viwanja mbalimbali nchini.



DC wa Iringa Mhe Kasesela afungua mafunzo ya Mgambo kijiji cha Mboliboli kwenye tarafa ya Pawaga

0
0
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akifungua kwa ukakamavu mafunzo ya Mgambo kijiji cha Mboliboli kwenye tarafa ya Pawaga. Kikosi hiki kitashirki kikamilifu katika kupambana na ujangili. zaidi ya washiriki 357 wamejiunga na mafunzo ya mgambo wilaya ya Iringa. Baada ya Mkuu wa wilaya kuhamasisha vijana wajiunge na mafunzohayo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akipiga jalamba wakati  akifungua kwa ukakamavu mafunzo ya Mgambo kijiji cha Mboliboli kwenye tarafa ya Pawaga

Serikali Kuwasaidia Watanzania Kushiriki Katika Ujenzi wa Tanzania ya Viwanda

0
0
 Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda akiandamana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutagerukawakitembelea maonyesho ya siku moja ya bidhaa za ngozi yaliofanyika leo kwenye Viwanja wa Maonyesho ya Saba Saba, vya Mwl. J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam yalioandaliwa kwa pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) (TanTrade) ikishirikiana na na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi (TALEPPA)

  Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda akiandamana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka wakitembelea maonyesho ya siku moja ya bidhaa za ngozi yaliofanyika leo kwenye Viwanja wa Maonyesho ya Saba Saba, vya Mwl. J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam 
 Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka wakipata maelezo toka kwa mmoja ya vibanda vya maonesho

Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda akiandamana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka wakiangalia bidhaa katika moja ya mabanda.

TAARIFA KWA WANA-DIASPORA/WATANZANIA KUHUSU JUHUDI ZA KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA- TANZANIA

0
0

Ndugu Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na wana-Diaspora wote popote pale mlipo. Salaam.
Kamati ya Mpito ya Jumuiya ya Watanzania/Wana-Diaspora Uingereza,inaitikia wito wa serikali na inapenda kuwajulisha kuwa inaendelea na juhudi za kuwashirikisha Watanzania na marafiki wa Watanzania duniani kote katika kuchangia maafa yaliyowapata ndugu zetu wa mkoa wa Kagera na maeneo jirani yaliyokumbwa na maafa . 
Taarifa kutoka vyombo vya habari zinaonesha kuwa mpaka sasa ndugu zetu 20 wamepoteza maisha, na wengine wengi  wanahitaji huduma mbali mbali za kiafya na kijamii, hususa ni matibabu na makazi ya kudumu. 
Tumependekeza utaratibu wa kuchangia kwa njia ya mtandao ili kurahisisha uchangiaji na kuweka uwazi katika kufuatilia maendeleo ya michango. Tunawaomba Watanzania wote na marafiki wa Watanzania walioguswa na maafa haya, tuchangie kwa hali na mali kupitia kwenye tovuti hii hapa chini na michango hii itawakilishwa moja kwa moja kwa kamati ya maafa ofisi ya waziri mkuu mara zoezi litakapokamilika.
 Njia hii itarahisisha kupunguza gharama za “international transaction money transfer fee” hasa kwa wanadiaspora na marafiki zao wanaotaka kuchangia kwa kiasi kidogo kidogo kama £10, $10, or 10 euro nk. Idadi ya watu wa namna hii ni kubwa sana, ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha zoezi hili. 
Kamati ya mpito inawajulisha Watanzania wote waishio Uingereza kuwa hivi karibuni ilialikwa Ubalozini na kukutana na Balozi wetu Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro. Maongezi yalikuwa mazuri na bado yanaendelea. 
Kwa sasa tunawaomba tuungane kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu, wale wote waliopoteza maisha yao na pia, kuwaombea majeruhi ili wapone haraka. Tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kuwachangia ndugu zetu katika kipindi hiki kigumu.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu atuzidishie moyo 
wa upendo ili “Tuwapende Majirani zetu kama Tunavyojipenda”.


Ili kuchangia bonyeza link hapa chini


Mungu Ibariki Tanzania.


Eng. Dr Julius Hingira                                                                        Abraham Sangiwa                                                                

Mwenyekiti – Kamati ya Mpito.                                                         Katibu Mkuu – Kamati ya Mpito


TZUK DIASPORA / TANZUK                                                              TZUK DIASPORA / TANZUK


Waziri Nape aahidi kutoa Millioni kwa kila goli litakalofungwa na Serengeti Boys katika mechi ya marudiano nchini Congo Brazaville.

0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwapongeza  wachezaji wa Serengeti Boys Jijini Dar es Salaam mara  baada ya  kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016 Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3-2.
Na Raymond Mushumbusi - WHUSM. 
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Millioni moja kwa kila goli litakalofungwa na Serengeti Boys katika mechi ya marudiano nchini Congo Brazaville. 
 Ametoa ahadi hiyo wakati akiongea na kuwapongeza wachezaji hao mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Congo Brazaville uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 
 “Kwa niaba ya Watanzania wote nawapongeza kwa mchezo mzuri mliouonesha na kuibuka na ushindi lakini bado mnatakiwa kujituma kama mlivyofanya katika mechi hii na naahidi kutekeleza ile ahadi yangu ya laki tano kwa kila goli na nitatoa tena kwenu Millioni moja kwa kila goli mtakalofunga Congo Brazaville.”Alisema Mhe. Waziri Nape.
 Kwa upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw. Bakari Shime ameshukuru Waziri na Watanzania kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo na watahakikisha wanapata ushindi katika mechi ya marudiano kwani wameshayaona mapungufu yaliyojitokeza na watayafanyia kazi wachezaji watakuwa tayari kuivaa tena Congo Brazavile. 
 Aidha Nahodha wa Timu hiyo Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa marudiano. 
 “Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi tukiwa ugenini ili tuweze kufuzu” Aliongeza Nahodha Makame. 
 Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inayowania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017 inatakiwa kupata ushindi ili kujihakikishia kufuzu kwa fainali hizo.

SERENGETI BOYS YAIBURUZA CONGO BRAZZAVILLE 3-2 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

0
0
TIMU ya Serengeti Boys leo imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazaville katika mchezo wa kufuzu kuingia fainali za mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Madagascar  uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi na kila upande kushambuliana kwa zamu zilianza kuzaa matunda kwa timu ya Serengeti Boys kuandika goli la kwanza dakika ya 38 liliolofungwa na Yohana Mkomola na dakika ya 42 akafanikiwa kuongeza goli la pili kwa Serengeti Boys.

Mpaka inafikia mapumziko Serengeti Boys walikuwa mbele kwa goli 2-0 lakini dakika ya 73, Langa-Lesse Percy anaiandikia Congo Brazzaville goli la kwanza kwa mkwaju wa penati baada mchezaji kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Issa Makamba anaipatia Serengeti Boys goli la tatu akitumia nafasi nzuri aliyoipata lakini halikudumu sana katika dakika ya 90 Poboumela Chardon akaipatia Congo Brazzaville goli la pili kwa kutumia uzembe wa goli kipa Kelvin Kayego aliyeingia kuchukia nafasi ya Ramadhan Kabwili aliyeumia wakati akiokoa penati.
Mpaka mpira unamalizika Serengeti Boys wametoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-2.
Kila timu iliweza kufanga mabadiliko na kwa upande wa Serengeti Boys walimtoaYohana Mkomola na kuingia Issa Makamba, Ibrahim Ali na kuingia Muhsin Makame na kwa Congo Brazaville alitoka Mboungou Prestige na kuingia Mountou Edoward, Mantourari Aldo na kuingia Makoina Beni na Kiba Konde Rodrique na kuingia Bopoumela Chardon.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys", Yohana Oscar Mkomola akikimbilia upande walipo mashabiki mara baada ya kuipatia timu yake Goli, katika Mchezo wao dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Serengeti Boys imeibuka na ushishi mwembamba wa bao 3-2, hivyo watajipanga kwa mchezo wa marudiano utakaochezwa juma lijalo. Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Yohana Oscar dakika ya 38 na 42 na Issa Abdi Makamba dakika ya 70, huku magoli ya Congo Brazaville yakifungwa na Langa-Lesse Percy kwa mkwaju wa penani na dakika ya 90 Poboumela Chardon. 

Shambulizi la hatari langoni mwa Timu ya Serengeti Boys.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.
Mabeki wa Timu ya Congo Brazaville wakiusindikiza kwa macho mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mchezaji wa Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba na kuipatia timu yake bao la tatu, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani.
Beki wa Timu ya Taifa ya vijana ya Congo Brazaville, Moundza Prince akiwa ameruka juu kuondosha hatari iliyokuwa imeelekeswa langoni kwake, katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

IBADA YA HIJJA YAMALIZIKA MAKKAH NA MADINA, MAHUJI 2000 WA TANZANIA WASHIRIKI

0
0
Na Kamati ya Hijja ya Tanzania.
Ibada ya hijja imemalizika rasmi katika mji wa Makkah na Madina na mahujaji wa dini ya kiislamu zaidi ya milioni 2 kutoka nchi zipatazo 164 wameanza kurejea makwao walikotoka.
Ibada ya mwaka huu imekuwa ya mafanikio kwa kumalizika salama. Hii ni kutokana na Serikali ya Saudi Arabia kuwa na mipango madhubuti kwa kuimarisha miundombinu, usafiri, ulinzi na usalama na kurekebisha dosari zilizojitokeza mwaka jana.
Maeneo ya misikiti yote miwili ya Makkah na Madina yaliimarishwa na yanaendelea kujengwa ikiwa ni pamoja na kupanuliwa ili kuongeza nafasi za kutosha kufanyia ibada.
Mahujaji kutoka Tanzania wapatao 2,000 wako salama na wao ni miongoni mwa walioshiriki katika ibada na sasa wako njiani kurejea Tanzania. Hatua zilizochukuliwa na mamlaka za ulinzi za Saudi Arabia ni pamoja na kuhakikisha kuwa makundi ya misafara ya mahujaji hayagongani kati ya wanaokwenda na wanaorudi, njia mbalimbali zilikuwa zikifungwa na kufunguliwa ili kuruhusu misafara kwenda uelekeo mmoja bila kukutana. Hatua hii ilisaidia kuepusha ajali kama iliyotokea wakati wa ibada ya hijja ya mwaka 2015.
Mahujaji wa Tanzania walipokuwa katika misafara ya majaribio (rehearsal) ya kujua njia kuelekea Jamarat eneo la Mina.      

Tume ya Mipango yaendesha mafunzo kwa Maafisa Mipango na wachumi jijini Mbeya

0
0
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo ya Mwongozo wa Uwekezaji na Usimamizi wa Miradi ya Umma yanayoendelea katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya. Kushoto kwake ni Mhandisi Happiness Mgalula Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma na Dkt. Joihn Mduma, Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi ni Dkt. Lorah Madete, Kaimu Nibu Katibu Mtendaji, anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgani rasmi (hayumo pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe, Iringa na Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

KAMPUNI YA MOKONO KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mikono, Deogratius Kilawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, juu ya kampuni yake kutoa kiasi cha asilia 10 ya mapato ya Kongamano la Huduma za Kifedha (Financial Services Expo 2016) kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililowata wananchi wa Mkoa wa Kagera hivi karibuni pamoja na NGO za Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mikono, Niss Richard na kushoto ni Meneja Mauzo na Masoko, Rory Dossa.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images