Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1358 | 1359 | (Page 1360) | 1361 | 1362 | .... | 3282 | newer

  0 0

   Mwanafunzi Eugene Kephasi, akimvika skafu, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alikuwa  mgeni rasmi katika mahafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School  Bunju jijini Dar es Salaam leo mchana.

   Kafulila (katikati) na viongozi wa shule hiyo wakielekea meza kuu tayari kwa mahafali hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu, Mkurugenzi wa Shule, Nipael Mrutu, Lupi Kiyabo na Mchungaji Elisifa Kephasi.
   Wanafunzi wakiwa tayari kwa gwaride.
   Wanafunzi wa darasa la saba wakiwa kwenye mahafali yao.

  0 0

  Mshindi wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai akipunga mkono kwa mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Clara Nyaki (kulia). Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Sehemu ya wadau na wapenzi wa masuala ya urembo wakiwa katika mapozi ya picha kwenye Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana.
  Sehemu ya Jopo la Majaji wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakijadiliana jambo kabla ya kutoa matokeo kwenye shindano hilo jana.. Sehemu ya Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakichuana katika miondoko mbalimbali ya mavazi.
   
  Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa TTCL ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakipiga picha na Balozi wa TTCL, Glory Gidion mara baada ya kumaliziki kwa shindano hilo.

  0 0

  Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, mbunifu wa mavazi na mwanamuziki , Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na kampuni ya GSM Foundation amesaidia waathirika  wa tetemeko la ardhi wa mkoa wa Kagera kwa kukabidhi magodoro 400.
  Jokate ambaye pia ni msanii wa luninga alikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja  Jenerali mstaafu, Salum Kijuu makoa makuu ya mkoa huo.
  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Jokate alisema kuwa  kampuni ya GSM Foundation nay eye wameguswa na athari za tetemeke hilo ambalo mbali ya baadhi ya watu kupoteza maisha, kuna waathirikia mbalimbali.
  Jokate alisema kuwa kuna watu wamepoteza makazi yao ya kuishi na mali zao mbalimbali, jambo ambalo limewafanya kurudi nyuma katika kimaisha.
  Alisema kuwa magodoro ni moja ya mahitaji makubwa ya wahanga katika mkoa huo kuamua kukabidhi kontaina la futi 40 kwa Mkuu wa Mkoa.
  “Ni janga la kitaifa kwani waliokumbwa na matatizo hayo ni watanzania wenzetu na wanahitaji msaada mkubwa, kuna majeruhi, kuna waliopoteza wazazi na jamaa zao huku wanafunzi wakikosa sehemu ya kusomea,” alisema Jokate.
  Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali  Mstaafu, Salum Kijuu aliwashukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huo ambao utapunguza changamoto za wahanga wa  tetemeko hilo.
   “Namshukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huu, ni msaada mkubwa, lakini bado tunahitaji misaada zaidi, bado kuna changamoto nyingi sana kwa wahanga, hivyo tunaomba mashirika, watu binafsi  na wadau wengine waunge mkono katika janga hili,” alisema Kijuu.
  Alisema kuwa kama kila Mtanzania atachangia sh 100, wataweza kukusanya jumla ya Sh bilioni 5 ambazo zitawasaidia kuondoa changamoto mbalimbali na kuwafanya wahanga kurejea katika maisha yao ya kawaida.
   Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (kushoto) akizungumza mara mara baada ya kupokea moja ya magodoro 400 yalitolewa na Kampuni ya GSM Foundation kupitia kwa Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia).

   Jokate Mwegelo akizungumza mara baada ya kukabidhi magodoro hayo ambayo yametolewa na kampuni ya GSM Foundation kwa wahanga wa tetemeko la ardhi la mkoa wa Kagera.
   Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya watoto yatima ambao nyumba yao waliyokuwa wanaishi iliathirika na tetemeko la ardhi. Jokate kwa kupitia kampuni ya GSM Foundation walisaidia watoto hao baadhi ya magodoro.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa pili kulia) pamoja na Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia) mara baada ya kupokea magodoro 400 yalitotolewa na kampuni ya GSM Foundation.

  0 0

  Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo.
  Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge.
   Timiza wajibu wako kata Mnyoro wa Rushwa
  Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akisoma salamu za shukrani mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma katika Kijiji cha Lusilile

  Na Mathias Canal, Singida
  KATIBU tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi leo ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge ambao utakimbizwa Mkoani Singida kwa siku saba katika Halmashauri saba ambapo utaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

  Dkt Lutambi amekabidhiwa Mwenge huo pamoja na wakimbiza Mwenge Kitaifa katika eneo la Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni ukiwa umewaka na kuahidi kuukabidhi kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora pasina mashaka utakapomaliza muda wake Mkoani Singida.

  Lutambi alisema kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo utalitia jumla ya miradi 61 inayohusu sekta ya ufugaji, Mazingira, Maji, Afya, Elimu, Barabara, Utawala Bora, Kilimo, Ushirika, Biashara, Ardhi na Programu za mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Malaria Rushwa na Ukimwi.

  Alisema kuwa jumla ya Miradi 33 itazinduliwa, 13 itawekwa jiwe la msingi minne itawekwa jiwe la msingi na mingine mitano itatembelewa ambapo miradi yote hiyo itakayopitiwa itakuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 14.

  Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2016 zimebeba kauli mbiu ya "Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" ambapo hata hivyo kila Halamashauri nchini zimeelekezwa kutenga asilimia 5% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana na asilimia 5% nyingine kwa ajili ya kina mama.

  Katika kumaliza mizizi wa Rushwa, Dawa za kulevya, ukimwi na Malaria Mwenge wa Uhuru umejikita zaidi katika kauli mbiu ya "Timiza wajibu wako kata Mnyororo wa Rushwa" kwenye mapambano dhidi ya Rushwa, Kauli mbiu ya "Tujenge jamii, Maisha na Utu wetu bila dawa za kulevya" kwenye Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Kauli mbiu ya "Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana" kwenye Mapambano dhidi ya Ukimwi na Mapambano dhidi ya Malaria, chini ya kauli mbiu ya " Wekeza katika maisha ya baadae, Tokomeza Malaria".

  Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya zote saba za Mkoa huo ambapo jumla ya Miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 12.

  Bi Madenge amewapongeza wananchi wote kwa ushirikiano na juhudi kubwa walizofanya katika kuianzisha, kuiendeleza na kuikamilisha Miradi yote.

  Pia alisema kuwa katika Wilaya zote walizozuru wakimbiza Mwenge wamepata taarifa za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuelezea namna inavyoendelea kutekelezwa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe wakati akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na katibu Tawala wa Mkoa wa Singida amesema kuwa Mwenge huo unataraji Kutembelea Miradi 18 ambapo hii leo utatembelea miradi 7 na hapo kesho utatembelea Miradi 11.

  Miongoni mwa Mirafi itakayofunguliwa ni pamoja na uzinduzi wa Programu  ya Ufuatiliaji na kuteketeza mbu, Kufungua Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu nane ya vyoo na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa, Ufunguzi wa daraja la Makutupora, Kuzindua Klabu ya  wapinga Rushwa, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Maarifa ya kupambana na UKIMWI, Kuzindua Mradi wa Vijana wa kufyatua matofali, na Kuzindua Klabu ya Kupambana na Dawa za Kulevya.

  Kwa mujibu wa ratiba za mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, unakimbizwa katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Octoba 14 mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.

  Mwenge wa Uhuru unaashiria Nuru na Mwanga, Uliwashwa rasmi kwa mara ya awali juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro Disemba 9, 1961.

  0 0


  Upo mjadala unaoendelea na kufukuta kuhusu uamuzi wa Serikali kupeleka Muswada wa Sheria Bungeni kufanya marekebisho katika Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Muswada huo sijauona na haujawekwa hadharani. Hata hivyo, lililopenyezeka katika vyombo vya habari ni taarifa ya azma hiyo ya Serikali iliyotamkwa katika kikao cha Serikali na wadau kuwa Muswada huo utafuta FAO LA KUJITOA.

  Nimefuatilia mjadala huo na kuisoma barua ya wazi ya vyama vya wafanyakazi kwa umma ikilaani vikali nia hiyo ya Serikali na muswada. Nikasikia na kusoma tena kauli mbalimbali za Serikali na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuhusu azma hiyo na mambo mengine mengi yanayoambatana na muswada unaondaliwa. Kwa maelezo hayo, muswada huo una mambo mengi zaidi ya kinachoitwa fao la kujitoa. Aidha, maelezo yao ni kuwa muswada wenyewe haujakamilika isipokuwa ni hatua ya maoni tu.
   Ninachokiona kwa haraka haraka ni kuwepo kwa ombwe la taarifa katika suala hili jambo linalofanya mjadala wenyewe kwenda harijojo. Ombwe hili litafanya hata muswada wenyewe ukitolewa tushindwe kuujadili vizuri  na kwa nafasi. Kwa sababu hiyo, nimejitolea kuchokoza mjadala kwa kuyaweka bayana mambo 10 ya msingi ya kuyaelewa kuhusu hifadhi ya jamii kama ninavyoyainisha hapa chini...


  0 0  0 0

   Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Songea mkoani Ruvuma  Enock  Lugenge kushoto akikabidhi jana,  madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5  kwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Titus Ng'oma ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa ajili ya kuwanusuru wanafunzi wa shule za msingi  wilayani humo kukaa chini.

   Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Titus Ng'oma kulia akipokea moja kati ya madawati 90 yenye thamani ya shilingi  milioni 5 yaliyotolewa na Benki ya CRDB Tawi la Songea kutoka kwa meneja wa Benki hiyo Enock Lugenge kushoto,  ikiwa ni  kuitikia wito wa Rais Dkt John Magufuri ya kuwataka wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na serikali yao kupunguza uhaba wa madawati kwa shule za msingi na sekondari hapa nchini,wanaoshuhudia kwa nyuma ni wajumbe wa kamati ya fedha uchumi na mipango wa  halmashauri ya wilaya hiyo.
  Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  Titus Ng'oma aliyekaa katikati,meneja wa benki ya CRDB Tawi la Songea Enock Lugenge wa kwanza kushoto,na afisa elimu ya msingi wa wilaya ya Namtumbo Alberto Mbilinyi  kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ndogo ya fedha uchumi na mipango ya baraza la madiwani wa halmashauri hiyo mara baada ya benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shlingi Mil 5 kwa halmashauri hiyo. Picha na Muhidin Amri

  0 0


  Karibu katika kipindi cha REGGAE TIME ya Pride Fm Mtwara Tanzania.

  Na leo, ni mazungumzo yangu na Innocent Galinoma ambaye alikuwa mkarimu sana kufika Kilimanjaro Studios kwa mahojiano.

  Ni kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, mbili kamili kwa Marekani Mashariki Jiunge nasi kupitia 87.8 Fm kwa mikoa ya kusini, ama www.878pridefm.com ama kupitia TuneIn, bofya tun.in/seTTx.

  0 0

  The State University of Zanzibar and Precious Technologies organised a five-day Ethical Hacking training to a number of  IT Specialists from different parts of the country at the The State University of Zanzibar (SUZA) Vuga campus. The training ended successfully on Friday. 
  Ethical Hacking, also known as penetration testing, intrusion testing, or red teaming, is the  act of locating weaknesses and vulnerabilities of computer and information systems by duplicating the intent and actions of malicious hackers.
  An Ethical Hacker, also known as a whitehat hacker, or simply a whitehat is a security professional who applies their hacking skills for defensive purposes on behalf of the owners of information systems. Nowadays, certified ethical hackers are among the most sought after information security employees in large organizations.
   IT Specialists from different parts of the country  pose with their attendance certificates after completion of the five-day Ethical Hacking training at the The State University of Zanzibar (SUZA) Vuga campus. Left is Eng. Mussa Kimolo IT Manager of  Dar es salaam-based Michuzi Media Group (MMG) whose management is grateful for extending the invitation for its IT manager.

  0 0

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umewahimiza madereva wa boda boda kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibu wakati wote.
  Wito huo umetolewa na Afisa Mawasiliano Mkuu wa NHIF, Bwana Luhende Singu alipokuwa akizingumza na waendesha boda boda wanaoshiriki katika mashindano ya Kombe la Kamanda Mpinga yanayeondelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
  Amesema kupitia mpango wa bima ya afya kwa wajasiliamali (KIKOA), waendesha boda boda hao waliojiunga katika vikundi vya wajasiliamali vilivyosajiliwa, wanaweza kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  Ameongeza kuwa mpango huo unawapa fursa waedesha boda boda kupata huduma za bima ya afya kwa kuchangia shilingi 76,800/- kwa mwaka kwa kila mwanachama.
  Bwana Singu amesisitiza kuwa kutokana na kazi zao ambazo zinawaweka katika mazingira ya ajali mara kwa mara ni muhimu waendesha boda boda hao wakajiunga na bima ya afya ili kuepukana na gharama za matibabu wanazokabiliana nazo hivi sasa mara wanapohitaji matibabu.
  Mashindano ya Kombe la Mpinga yanashirikisha timu zinazoundwa na Waendesha boda boda katika Manispaa ya Ilala ambapo zaidi ya timu mia moja zinawania kombe hilo.
  01-2Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bwana Luhende Singu akizungumza na waendesha boda boda kuhusu kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibu wakati wote leo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bwana Luhende Singu akizungumza na waendesha boda boda kuhusu kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibu wakati wote leo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Bwana Luhende Singu akizungumza na waendesha boda boda kuhusu kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibu wakati wote leo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
  Maafisa wa NHIF wakiwa katika picha ya pamoja na waendesha boda boda wanaoshiriki katika mashindano ya Kombe la Kamanda Mpinga yanayeondelea katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii

  0 0


  0 0

  Na: Frank Shija, MAELEZO
  TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera.
  Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.
  “Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.
  Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.
  “Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.

  Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.
  Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.
  Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.
  Baadhi ya washiriki wa  hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana. 
   Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Katika matembezi hayo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kimepatikana. 
   Wawakilishi wa Jumuiya ya Wabohora nchini  wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera kwa Rasi wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Bw. William Erio na Afisa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Waziri wa Mmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga.
   Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashari katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “ Walk for Kagera” Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Busemaker akipokea cheti kwa ajili ya kutambua udhamini wa Benki hiyo katika kufanyikisha matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Kagera leo Jijini Dar es Salaam.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula akiwa chini huku Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akijiandaa kushangilia baada ya Kipa huyo kupitwa na mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya (hayupo pichani) na kuingia moja kwa moja wavuni na kuifanya timu hiyo kujipatia bao la kuongoza. Mchezo huo ambao ulikuwa ni wenye kasi na wakuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu, umemalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam huku Timu ya Simba ikiondoka uwanjani hapo ikiwa kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0. Kwa ushindi huu wa leo, Timu ya Simba sasa inashikilia ushukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na pointi 13, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 10 sawa na Azam FC.
   Mshambuliaji wa Timu ya Azam FC, John Bocco akituliza Mpira mbele ya Beki wa Simba, Novaty Lufunga, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Simba imeshida bao 1-0.
   Beki wa Azam FC, David Mwantika akindoka na mpira baada ya kumshinda maarifa, Mshambuliaji wa Simba, Fredrick Blagnon, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Simba imeshida bao 1-0.


  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha  dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban Tshs. 437,000,000/-  taslimu kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika  wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha  cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) - takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais  Uhuru Kenyatta  wa Kenya na kwa misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo magodoro na mashuka ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa fedha dola laki mbili za Kimarekani (takriban Tshs. 437,000,000/- )  taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA Tanzania, Dk Gift Shoko akizungumza na wateja mashuhuri wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ uliofanyika jinni Dar es Salaam hivi karibuni. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.Mwenyekiti wa Tanzania CEO Roundtable, Ali Mufuruki akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Dk. Gift Shoko wakati wa uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ jijini Dar Es Salaam hivi karibuni. Mufuruki alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana.

  Benki ya CBA yaja na huduma za kisasa za kibenki Katika mkakati wake wa kuendelea kuboresha huduma zake nchini,Benki ya CBA imezindua huduma mpya kwa wateja wake binafsi zitakazowawezesha kupata huduma za kibenki kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kupata huduma za kibenki kimtandao kupitia simu zao za mkononi. Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya,Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania,Dk.Gift Shoko,alisema kuwa huduma hizi zimelenga kuwarahisishia maisha wateja na kuwawezesha kupata huduma za kibenki kulingana na matakwa yao na kwenda sambamba na mtindo wa maisha wanaoishi.

   Alisema pia wateja wa CBA Tanzania kuanzia sasa wanaweza kutumia kadi za kimataifa za kufanya mihamala ya malipo za Visa Platinum Debit Card na Visa Gold Credit Card kwa fedha za kitanzania na Dola za Kimarekani ambazo zinawawezesha kupata huduma mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege wa JKIA kwenye sehemu ya kupita watu maarufu (VIP lounge).Alisema huduma hii itawawezesha wateja wa kundi hili kufanya mihamala wakiwa katika viwanja vya ndege 600 kwenye nchi 1,000 na miji mikubwa ipatayo 300 duniani kote.

   “Tunazidi kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja ili wazipate popote na kwa wakati wowote watakapokuwa bila kupoteza muda kama ilivyokuwa hapo awali”.Alisema. Kitengo cha kuhudumia wateja watakaojiunga na huduma hii kwa kuanzia itapatikana jijini Dar es Salaam katika matawi yaliyopo kwenye mitaa ya Ohio na Samora vilevile katika tawi la Arusha. Benki ya CBA Tanzania ambayo ni moja ya Benki kubwa zinazoongoza kwa ubunifu wa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wake ,moja ya huduma ambayo imeianzisha na kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya makazi ya kutoa mikopo ya nyumba inayolipwa hadi kufikia kipindi cha miaka 20. 

   Benki ya CBA Tanzania hadi kufikia sasa inayo matawi 11 nchini kote ambapo 5 yapo jijini Dar es Salaam na mengine katika miji ya Mbeya, Tunduma, Mtwara, Moshi, Mwanza, na Arusha.Pia benki ipo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki za Kenya,Uganda na Rwanda ambazo ziko chini ya mwamvuli wa CBA GROUP.

  0 0  0 0


  0 0


  0 0

  Katika kuendeleza kampeni yake kabambe ya “Sibanduki”  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeweka gulio la simu yaani Smartphone Baazar  mwishoni mwa wiki ndani ya Mlimani City jijini Dar es Saalam ili kuwawezesha wateja wake kupata simu za kisasa , origino na kwa gharama nafuu

  Airtel Smartphone Bazaar ina lengo la kuwapatia wateja wa Airtel simu za kisasa na pia kutoa nafasi kwa wateja wa Airtel kujiunga na timu Sibanduki” na kufurahia huduma lukuki ikiwemo ,kutuma na kutoa pesa bure, kujitengenezea vifurushi vya yatosha na kupata MB zaidi, SMS zaidi na intaneti zaidi,  kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana, kutoa pesa benki na kuweka kwenye akaunti zao za Airtel Money wakati wowote na kwa wateja wapya kupata vifurushi vya dakika 60, SMS 2000 na MB 200 bure bila , vifurushi hivi vitadumu kwa muda wa siku 60
  Akiongea kuhusu Smartphone Bazaar, James Kagashe, Afisa bidhaa na masoko alisema “ Tunayofuraha kuwaletea sokoni wateja wetu simu za kisasa , origino na zenye gharama nafuu hadi shilingi 24,000. Tunazo simu nyingi ikiwemo simu Aina ya fero 280 inayouzwa 24,000, simu ya smartphone aina ya Magnus Z11 inayouzwa kwa shilingi 83,000 na simu ya Huawei Y3C kwa shilingi 140,000. Pamoja na simu hizi tunazo simu aina ya Samsung, Techno pia zinapatikana hapa katika Bazaar hii.
  Natoa wito kwa wateja na watanzania kujitokeza na kutembelea hapa ndani mlimani city na kujipatia simu kwa bei poa na kujiungana timu Sibanduki kwa huduma bora za kipekee na kibunifu wakati wote
  Smartphone Bazaar itakuwepo pia wiki ijayo siku ya Jumamosi na Jumapili hapo haop Mlimani City  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, NandiMwiyombella(wapili kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo ambayo ni wadhamini wakuu wa ligi, Jacquiline Materu wakisalimiana  na wachezaji wa Azam FC walipokuwa wakikagua timu  hiyo wakati wa   mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara  kati ya Azam na Simba uliofanyika jana   uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda 1-0.
   Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella akikagua timu ya Simba SC akiwa na maafisa waTFF wakati wa   mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara  kati ya Azam na Simba uliofanyika jana   uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda 1-0.
   Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella,(wapili kulia) na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu,wakiongozwa viongozi wa TFF mara baada ya kukagua timu za Simba na Azam wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,Simba ilishinda 1-0
   Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(wapili kulia) akisalimiana na mwanachama wa Simba Juma Kapuya  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba na Azam uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya usajili wa timu hiyo Zacharia Hanspoppe,Simba ilishinda 1-0.
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella,(wapili kulia) na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu,wakiangalia mechi kati ya  timu za Simba na Azam wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,Simba ilishinda 1-0

older | 1 | .... | 1358 | 1359 | (Page 1360) | 1361 | 1362 | .... | 3282 | newer