Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1356 | 1357 | (Page 1358) | 1359 | 1360 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road,  Dk. Julius Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kuhusiana na kupimepitisha muongozo wa tiba shufaa kwa wagonjwa waliokata tamaa katika hospitali za hapa nchini.
  Baadhi ya waandishi wa jamii wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road,  Dk. Julius Mwaiselage jijini Dar es Salaam leo.

  Na Yassir Adamu, Globu ya Jamii.
  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya Maendeleo Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imepitisha muongozo wa tiba shufaa (Tiba kwa wagonjwa walio kata tamaa) ili kuweza kutumika kwa wagonjwa mbalimbali.

  Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road,  Dk. Julius Mwaiselage  amesema kuwa kuna umuhimu kwa kila hospitali za serikali na Binafsi kuwa na utoaji wa tiba shufaa.(Tiba kwa wagonjwa walio kata tamaa)

  Amesema kuwa shufaa  inatumika kwa wagonjwa wa muda mrefu ambao wamekata tamaa katika kuondoa maumivu makali kuliko huduma nyingine kwa wagonjwa.

  Dk. Mwaiselage amesema huduma hiyo lazima itolewe kwa mujibu wa daktari na sio kutumia vinginevyo na nchi nyingi zimeweza kutumia dawa hizo wamekuwa na mfanikio.

  Dk. Mwaiselage amesema kuwa wagonjwa wa saratani wanapitia katika hatua nne ambazo ya kwanza mtu anaweza kutibiwa na kupona na hatua ya pili anaweza kupona kwa asilimia 50 hatua ya tatu na ya nne wagonjwa hao wanakuwa na kiwango cha juu hivyo huduma tiba yao kupata shufaa.

  Amesema kuwa wadau wameutengeneza muongozo ili kuweza kutumika kutokana na wagojwa asilimia 80 wanahitaji huduma ya tiba ya shufaa.

  0 0


  Na Daudi Manongi,MAELEZO.

  Dar es Salaam

  TAKWIMU zilizotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza imeonyesha kuwa asilimia 96 ya wananchi wanakubali hatua za kiutendaji kazi za Rais John Pombe Magufuli ikiwemo uondoaji wa wafanyakazi hewa na sera ya elimu bure.

  Taarifa iliyotolewa leo katika vyombo vya habari na Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano wa Twaweza, Risha Chande alisema asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo mpaka mwisho wa awamu yake ya kwanza ya uongozi.

  “Utafiti huu unaonyesha kuwa asilimia 69 ya wananchi walifuraishwa na juhudi za Rais za uondoaji wa wafanyakazi hewa, wakati asilimia 61 walipongeza sera ya elimu bure wakati asilimia 61 walifurahishwa na usimamishwaji wa watumishi wa serikali” alisema Chande.

  Chande alisema kuwa katika utafiti huo unaonyesha wananchi wengi kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ya kufanya maboresho katika huduma za umma ikiwemo mamlaka ya mapat (asilimia 85), mashuleni (asilimia 75),vituo vya polisi (asilimia 74),mahakama (asilimia 73), vituo vya afya (asilimia 72).

  Aliongeza kuwa kwa upande wa huduma zinazotolewa katika utumishi wa umma, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 95 ya wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na madaktari, walimu, na maofisa tawala katika ofisi za umma.

  “Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa Serikali ya wamu ya Tano wananchi wamesema suala la umakini na kanuni za demokrasia na haki ni vyema zifuatwe ambapo wananchi nane kati ya kumi wanasema watendaji waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu” alisema Chande.

  Akifafanua zaidi Chande alisema utafiti huo pia umeonyesha kubadilika kwa matarajio ya wananchi ambapo katika kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutojali miongoni mwa wananchi kulikotokana na utendaji duni kutoka kwa watendaji.

  0 0

  The office situated on Samora Towers in Dar es salaam is 170 Square meters, readily partitioned with higher floor overlooking the Indian Ocean & Dar es salaam port.

  Price $17 per square meter plus service 
  charge $3 per square meter.
  For further details and information 

  Call or Sms +255 784 786 455


  Office readily partitioned

   Room with a view
   Office overlooking the Indian Ocean & Dar es salaam port
  Modern office

  0 0
 • 09/15/16--10:00: KUMBUKUMBU YA KIFO.


 • 0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akiongea na waandishi wa Habari juu ya Siku ya Kimataifa ya tabaka la Ozoni. Siku hii huadhimishwa Septemba 16 kila mwaka. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyungi. (Picha kwa hisani ya Idara ya Habari Maelezo)
  …………………………………………………………..
  Tarehe 16 Septemba mwaka huu tutaungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Azimio lake nambari 49/114 la tarehe 19 Desemba 1998 kama kumbukumbu ya tarehe ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol – 1987) kuhusu kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni angani.

  Ozoni ni hewa iliyoko kwenye angahewa ya juu, takribani kilometa 10 hadi 50 juu ya ardhi. Kazi yake kubwa ni kuchuja sehemu kubwa ya mnururisho wa mionzi kama “Ultraviolet B” isifike kwenye uso wa dunia. Ujumbe wa mwaka huu ni “Kuhuisha Tabaka la Ozoni na Tabia-Nchi kwa pamoja Duniani”. Ujumbe huu umeambatana na Kauli mbiu isemayo “Kukabiliana na ongezeko la gesi Joto Duniani HFCs chini ya Itifaki ya Montreal”. 

  Tabaka la Ozoni linapoharibiwa huchangia kuruhusu mionzi zaidi ya “Ultraviolet B” kufika kwenye uso wa dunia na hivyo kusababisha kuongezeka kwa magonjwa kama vile saratani ya ngozi, uharibifu wa macho yaani “mtoto wa jicho” unaosababisha upofu, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi na kujikunja kwa ngozi. Aidha, madhara mengine ni kuharibika kwa mimea hasa mazao ya kilimo kutokana na kuathirika kwa maumbile na mifumo ya ukuaji. 
   
  Vile vile, baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.
  Ili kulinda tabaka la Ozoni, Serikali za mataifa mbalimbali zilikubaliana kuunda Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa Hifadhi ya Tabaka la Ozoni mwaka 1985. Mkataba huu unasisitiza ushirikiano katika utafiti, usimamizi na ubadilishanaji wa taarifa za hali ya Tabaka la Ozoni kutokana na kupungua kwa matumizi yake. 
   
  Vile vile ulianzishwa Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol) unaohusu udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni na Mkataba huu ulipitishwa tarehe 16 Septemba, 1987. Lengo kuu la Mkataba huu ni kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hili. 

  0 0

  Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF) limewasilisha mapendekezo kwa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria likitaka kufutwa kwa sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini . 

  Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga amesema mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwakanadamiza wanawake na kuwanyima haki ya kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume zao. 

  Amesema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba Serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanaume ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki. 

  “Tulipoonana na Mhe Waziri Dkt Mwakyembe alituagiza kama tunataka kuwasaidia wanawake nchini basi tuwasilishe wizarani mapendekezo yetu juu ya nini kifanyike, sasa leo tumekuja hapa kutekeleza agizo la Mhe Waziri, tunampatia Katibu Mkuu mapendekezo husika, ambayo kwa asilimia kubwa yanapendekeza kufutwa kwa sheria zote za kimila ambazo zinamkandamiza mwanamke na mtoto wa kike na kutungwa kwa Sheria moja itakayoshughulikia masuala yote ya mirathi nchini na tuna imani kuwa yatafanyiwa kazi na kufanikisha azma ya WILDAF ya kuwasaidia wanawake nchini, alisema Mwenyekiti wa WILDAF Bi. Judith Odunga 

  Akipokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam amewapongeza na kuwashukuru WILDAF kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ili kuwasaidia wanawake na Serikali kwa ujumla wake kwani kitendo hicho kitasaidia sheria husika kufanyiwa marekebisho yatakayostahili ili ziendane na wakati, zikidhi mahitaji na kutafsiriwa katika lugha ambayo wananchi wengi ambao ndio walengwa wazielewe sheria hizo 

  Amesema sasa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa sheria zote nchini zinatafsiriwa na zile zinazotungwa zitakuwa kwa Kiswahili na Kingereza, uamuazi ambao utawawezesha watanzania wengi kuzielewa sheria hizo. 

  Prof Mchome alaiwashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaadi kuwa wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yaoi ili kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia wananchi wengi na kuwataka wadau wengine kuja wizarani kuzungumza pale watakapoona kuna haja ya kufanya hivyo kwani wizara ipo tayari kuwasilikiza na kuyafanyia kazi mapendekezo yao.   Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo hayo yanayotaka kufutwa kwa sheria za kimila nchini ambazo zinadaiwa kuwakandamiza wanawake kwa kuwanyima haki sawa ya kumiliki mali pindi wanapofiwa na waume au wazazi wao anaeshuhudia kushoto ni Bibi Thabita Siwale Mwenyekiti wa Kikosi cha kupambana na haki za mirathi Tanzania- KIKUHAMI.

  Wajumbe mbalimbali wa WILDAF walioambatana na Mwenyekiti kushuhudia uwasilishaji wa mapendekezo yao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome Ofisini kwa jijini Dar es Salaam

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ameshirikiana na Gsm Foundation na MOI kusaidia kutibu watoto nane wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

  Katika matibabu hayo watoto wapatao 23 walifanyiwa vipimo na 8 kati yao walikutwa na matiatizo hayo na kufanyiwa upasuaji,na kuongeza kuwa watoto wengine walikutwa na matatizo tofauti na hayo,na kupelekwa katika hosptali ya taifa Muhimbili na wengine walipelekwa kwa madaktari bingwa wa magonjwa kwa matibabu.

  “Watoto wote waliofanyiwa operesheni tuliwakuta wanaendelea vizuri wakiwa na wazazi wao wakiendelea kuwapatia huduma za mwisho kabla ya kuruhusiwa”,alisema Kikwete

  Aidha,Mbunge huyo amewaomba wazazi kutowaficha watoto wenye matatizo kama hayo kwani yanatibika na kuacha kuendekeza Imani potofu za kuwafungia ndani na badala yake kuwapeleka katika vituoa vya afya ili kupata matibabu.

  “Nawashauri wazazi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo kwa kufanya hivyo ni kuwanyima watoto nafasi ya kupona na kuishi maisha kama watoto wengine”,alisema Kikwete.

  Kikwete amewaomba wadau katika sekata ya afya kujitokeza kuungana na Gsm Foundation katika kusaidia katika sekta hiyo ili kumkomboa mtanzania kuondoka na matatizo ya kiafya yanayowakabili.

  “Nawashukuru sana Gsm kwa kujitoa kusadia watoto hawa kupata matibabu kwa ni jambo la kupigiwa mfano na wadau wengine katika kusaidia jamii”,alisema Kikwete

  Mbunge huyo ameshukuru madaktari kwa kujitolea muda wao na kuwatibu watoto hao na kutoa wito kwa Gsm Foundation kuondelea kusaidia katika Mkoa wa Pwani ili kuwafikia watoto wengine katika maeneo ya Mkuranga,Kibiti,Mafia na Rufiji.

  Katika hatua nyingine Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa polisi Mkoa wa Pwani,polisi Wilaya ya Chalinze na kituo cha udereva wa vyombo vya moto cha Winners Driving School wameendesha mafunzo ya udereva kwa vijana 160.

  Mafunzo hayo ya udereva yamewezesha vijana hao kupatiwa leseni mara baada yakumaliza mafunzo yatakayo wasaidia katika shughuli zao za kila siku za kujitafutia kipato,mafunzo hayo yamegharimu shilingi milioni 20.

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete atembelea Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha Mkoani Pwani, kufunga mpango wa kusaidi watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa zoezi hilo linalofadhiliwa na Gsm foundation wakishirikiana na Moi. 
  Mbunge wa Chalinze akiwa katika wodi ya watu waliopata ajali na matatizo mengine ya viungo wakisubiri kupatiwa huduma na wale waliopatiwa huduma ya mifupa kuwajulia hali na kuwapa pole.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete akipata maelezo toka kwa madaktari wa Moi waliokuwa wanawapokea na kuwaaangalia watoto walikua na matatizo.

  Baadhi ya vijana waliofuzu mafunzo na kupatiwa leseni ya udereva wa bodaboda msaada wa Ofisi ya Mbunge wa Chalinze wakifuatilia kwa makini yanayotokea katika kikao hicho .


  0 0

   Ikiwa ni takribani mwaka na usheee sasa tangu kuanza kwa utaratibu mpya wa matumizi ya Barabara za Jijini Dar es salaam, lakini bado kumekuwa na changamoto katika eneo hili la Faya kwani kuna madereva bado wanatumia utaratibu ule ule wa awali. Kamera yetu leo iliangazia eneo hilo la Faya na kukutana na hali hii ya upishanaji wa magari ambao si salama kabisa kwa watumiaji wa barabara hiyo. Jambo hili limekuwa limekuwa likiendelea kufanyika kimazoea maana si gari moja au mbili zinazotumia utaratibu ule wa awali (Ukiangalia picha hizi utabaini kinachoelezwa hapa) Maana unakuta taa zimeruhusu kwa gari zinazokenda moja kwa moja, halafu ghafla tu unakutana na gari lingine likikatisha mbele yako kuelekea upande mwingine. hiki ni kijipu upele ambacho kikija kutumbuka balaa lake litakuwa si dogo, hivyo inapaswa litafutiwe ufumbuzi sasa, na kuna umuhimu wa kutoa mafunzo ya kutosha kwa matumizi ya barabara hizi.
   Hivi ndivyo mambo yanavyokuwa pale taa za kuongozea magari zinaporuhusu magari yananyokwenda moja kwa moja lakini wengine hukatisha ghafla namna hii.
  Inafika wakati gari zinazokwenda moja kwa moja zinalazimika kusimama katikati ya barabara ili kupisha zinazokatisha ambazo ziko nje ya utaratibu.


  0 0

  Premier League outfit, Sunderland AFC, have been sharing its expertise this past week with a local football club in Tanzania as club’s partnership with Acacia Mining continues to benefit local community.

  The football partnership with Acacia Mining has seen Sunderland AFC support the organisation’s CSR programme, delivering the club’s globally recognised community sports initiatives to community sites across the north-west region of Tanzania. 

  Most recently the club’s Head of International Football Development, Graham Robinson, worked with Ambassador FC on a variety of classroom activities that focussed on the business side of football, identifying new potential revenue streams for the club.

  Graham said: “The classroom session went very well and it was great to see how keen they were in identifying new sponsors and developing the club off the field.”

  Graham also delivered a number of coaching sessions with the team, working on passing, attacking play, defending from the front as well as conditioned games to improve the fitness of the players.

  Graham added: “I was also blown away at the ability and quality of the young players, so much so that after speaking with the coach we are looking to make contact with clubs in the higher divisions of Tanzanian football to help progress the youngsters’ development.

  “Since working in the mining regions there has been a lot of young talent on show and hopefully through the work the club are doing with the local coaches and football teams we will be able to nurture and develop that talent.”

  For more information about Sunderland AFC’s global activities please visit www.safc.com. Join the conversation by following @SunderlandAFC on twitter or Like www.facebook.com/SunderlandAFC.

  0 0

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea kiasi cha Shilingi Milioni 1.6 kutoka kwa Mratibu Taifa wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Bi. Mariam Kilembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa ajili ya Kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, leo Bungeni Mjini Dodoma.

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 121.679 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.Msaada huo umetolewa leo (Ijumaa, Septemba 16, 2016) na wadau mbalimbali wakiwemo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Caspian, Bw. Omid Karambech aliyetoa sh. milioni 100.

  Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bordar Limited, Bw. Wu Yahui aliyetoa sh. milioni 20 pamoja na Bi. Mariam Kitembe aliyetoa sh. milioni 1.679 kwa niaba ya Wauguzi walioshiriki mafunzo ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).Akipokea msaada huo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya fedha na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.

  Jumapili, Septemba 11, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kagera ili kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo pamoja na kujionea madhara yaliyojitokeza.

  Pia aliongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba kuaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko hilo. Aliwaomba wananchi wawe watulivu na kuwaahidi kuwa Serikali itakuwa pamoja nao.

  Jumanne, Septemba 13 mwaka huu Waziri Mkuu aliongoza hharambee ya kuchangia waathirika wa teteme hilo na kupokea zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.

  Mbali na kusababisha vifo, watu wengine 253 walijeruhiwa na maelfu ya wananchi walikosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
  DODOMA.

  IJUMAA, SEPTEMBA 16, 2016

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu(kushoto)Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(katikati)wakimshuhudia mshindi wa kitita cha shilingi milioni 20/- wa promosheni ya Kamata Mpunga, Frank Lyimo Mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam akionesha kitita chake kwa waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hay oleo jijini Dar es Salaam. Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
  Frank Lyimo Mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam(kulia)akipokea kitita cha shilingi Milioni 20/-kutoka kwa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu(kushoto)alizojishindia katika droo ya wiki ya promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100. Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,katikati ni Meneja wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewataka wadau wa habari na wananchi kwa ujumla kutoa maoni juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari wa mwaka 2016 uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni leo mjini Dodoma.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhairishwa Bunge, Waziri Nape amesema kuwa muswada huo unalengo la kuboresha tasnia ya habari ili kuweza kurahisha utendaji kazi wa wanahabari na kuifanya tasnia hiyo kuheshimika nchini.
   
  “Ombi langu kwa wadau wa tasnia hii wausome vizuri muswada huo na  kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni yao ili tuwe na sheria itakayoleta magezuzi na kukuza tasnia ya habari” amesema Waziri Nape.
   
  Waziri Nape amewataka wadau wa habari kuendelea kusoma muswada huo ili kuweza kupata mapendekezo ya namna ya kuifanya sheria hiyo kuwa bora kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.Aidha, Waziri Nape amewaahidi wadau wa habari kukutana nao mara kwa mara wakati wa kutoa maoni na mapendekezo yao yatakayosaidia kuboresha mazingira ya wanahabari nchini ili waweze kufanya kazi yao ipasavyo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma.
   

  Vile vile, Waziri Nape amewapongeza waandishi wa habari kwa kushiriki vema katika kuhabarish umma kuhusu mkutano wa Bunge uliohitimishwa leo na kuahidi kuendelea kushirikiana nao wakati wote.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto, Dodoma

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma kwa kuanza kujenga jengo lake mkoani humo.

  Jengo hilo litakalokuwa nyuma ya Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya ujenzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema jengo la NBS lilipangwa kujengwa jijini Dar es Salaam lakini kutokana na agizo la Rais imebidi jengo hilo lijengwe mkoani Dodoma.

  “Kabla ya agizo la Mhe. Rais, jengo la NBS lilipangwa kujengwa Dar es Salaam na tayari maandalizi yalikuwa yameshafanyika lakini kutokana na agizo hilo imetupasa kujenga jengo letu hapa mkoani Dodoma,” amesema Dkt. Chuwa.

  Kwa upande wake Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo hilo amesema atahakikisha anafanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

  “Nimepewa siku 12 za kumaliza suala zima la upimaji wa udongo katika eneo hili na mpaka sasa hali ni nzuri na nina uhakika kuwa kampuni yangu itamaliza kazi hii ndani ya muda uliopangwa,” amesema Mhandisi huyo.

  Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu utaanza rasmi mwezi Novemba 30 mwaka huu na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akipewa maelezo na Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo la ofisi hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea eneo litakapojengwa jengo la ofisi hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
  Wahandisi wa Kampuni ya Norplan Tanzania wakiendelea na kazi ya upimaji wa udongo kwa ajili ya upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika eneo itakapojengwa ofisi hiyo inayopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo la ofisi hiyo itakuwa na ghorofa 6 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. Picha zote na Emmanuel Ghula.

  0 0


  Washiriki wa Miss Temeke 2016 wakifanya mazoezi ya kujiandaa na shindano lao jijini Dar es Salaam. Shindano hilo, litakalofanyika Viwanja vya Sigara TCC Chang'ombe Septemba 24 mwaka huu.


  Na Dotto Mwaibale

  WAREMBO 16 wanatarajia kupanda jukwaani katika shindano la kumpata Miss Temeke 2016 litakalofanyika Septemba 24 mwaka huu.

  Akizungumza Dar es Salaam katika mazoezi yao, Mwalimu wa warembo hao Neema Honest alisema warembo wote wapo fiti na wanaendelea vizuri na mazoezi Chang'ombe Sigara TCC.

  "Washiriki wote wapo katika hali nzuri na sasa wanaendelea na mazoezi tayari kwa shindano hilo litakalofanyika Chang'ombe Sigara TCC" alisema Honest.Aliwataja warembo kuwa ni Jesca Nassary, Diana Nyaki, Juliet Pallangyo, Irene Tomitho, Macrina Kudema, Anitha Mugisha, Khadija Masoud na Sia Kiweru.

  Aliwataja wengine kuwa ni Sara Bigambo, Nancy Mushi, Mwantum, Esther Mnaki, Anitha Kisimba na Clara Premsinga

  0 0

  Na John Stephen, MNH

  Dar es Salaam, Tanzania. Mashine ya MRI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepona baada ya kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine hiyo iliharibiika baada ya kutokea hitilafu ya umeme. Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52 wamepatiwa kipimo cha MRI. 

  Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare amesema baada ya mashine hiyo kuharibiika, mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wa Muhimbili walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hiyo.
  “Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi,” amesema Dk Lwakatare. 

  Mmoja wa ndugu wa wagonjwa, Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba tangu kuharibiika kwa mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi baada ya kurejea kwa huduma hiyo. “Tunashukuru huduma za MRI zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni nafuu kuliko kuliko kupata matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza madaktari na wauguzi kwa utendaji bora. 


  Naye Hawa Hussein mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa. Hawa ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za kuiwezesha mashine hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa. Amesema kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana imani wataendelea kupata huduma bora na kwa wakati.

  Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo. 
  Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya mashine ya MRI kuanza kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Joshua Job na Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa hospitali hiyo. 
  Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hospitali hiyo. 
  Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa leo.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akiwaasa wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote
  saba Mkoani Singida  katika kikao cha Jumuiya za Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
  Wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida  wakiendela na katika kikao cha Jumuiya za
  Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
  ……………………………………………………………………………
  Na Mwandishi Wetu Singida
   
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewaasa
  wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida kutumia vikao vya mafuzo ya Jumuiya za Serikali za mitaa (ALAT) kutatua kero za halmashauri.
   
  Mhandisi Mtigumwe ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ALAT
  mkoa wa Singida na kuwasisitizia kuwa mafunzo hayo yawe na tija na sio kukaa vikao visivyo na matokeo chanya.
   
  Ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi sita tangu ateuliwe na
  Mhe Rais amebaini halmashauri zina changamoto za ukusanyaji hafifu na
  usioridhisha wa mapato ya ndani pamoja na mikataba mibovu inayosainiwa na halmashauri na hivyo kuiletea hasara serikali.
   
  Mhandisi Mtigumwe amesema kumekuwa na migogoro ya ardhi
  inayosababishwa na maafisa ardhi wasio kuwa waadilifu, watumishi na madiwani,kujimilikisha ardhi na vibanda kinyume na utaratibu pamoja na kutotengwa kwa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana.
   
  “Halmashauri hazijatenga maeneo ya viwanda vidogo na vya kati,
  uchafu umekithiri katika maeneo mengi, watumishi wanaokiuka taratibu
  hawachukuliwi hatua za kinidhamu na mawasiliano hafifu kati ya viongozi na watumishi, viongozi na viongozi na hata watumishi wenyewe, hizi ni baadhi ya changamoto ambazo kikao cha ALAT kitumike kuzitafutia majibu, alisisitiza.
   
  Mhandisi Mtigumwe amewasisitiza wakurugenzi kuunda mabaraza ya
  wafanyakazi na halmashauri zenye mabaraza hayo basi vikao vifanyike ili kero na changamoto za watumishi zisikilizwe na kutafutiwa ufumbuzi.
  Kwa upande wao meya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri
  wamemshukuru mkuu wa Mkoa kwa nasaha alizowapa na kuahidi kuyatumia mafunzo ya ALAT katika kuleta mabadiliko katika halmashauri zao.
   

  Wajumbe walipata fursa ya kujifunza juu ya Mfumo ya serikali za
  mitaa Tanzania bara, ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye halmashauri,
  utaratibu wa manunuzi katika serikali za mitaa , uwazi na uwajibikaji na
  mawasiliano kwa viongozi.

  0 0  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uingereza Mhe. Sarah Cooke na kufanya mazungumzo naye. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 16 Septemba, 2016.
  Dkt. Mahiga akizungumza na Balozi Mteule wa Uingereza nchini, Mhe. Cooke mara baada ya kupokea Nakala zake.

  Balozi Mteule Mhe. Sarah Cooke akizungumza huku Dkt. Mahiga akimsikiliza.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki Bw. James Bwana (wa kwanza kulia) akielezea jambo kwa Dkt. Mahiga na Balozi Cooke .
  Mazungumzo yakiendelea.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

  0 0

  Na Sheila Simba,Maelezo

  Serikali meshauriwa kusimamia uwekezaji  katika sekta za kilimo,madini na viwanda ili kufikia malengo waliojiwekea ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

  Wito huo umetolewa na Profesa Haji Semboja katika mahojiano na MAELEZO kuhusu hali ya uchumi nchini katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

  “Muhimu sasa Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya Madini,kilimo na viwanda na hili litasaidia kufanya nchi kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nchini kwa wingi bila kutengemea bidhaa kutoka nje ya nchi”,alisema Prof.Semboja.

  Ameeleza kuwa taarifa ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki Kuu nchini imeweka wazi hali ilivyo kwa sasa,na kuongeza kuwa ni kweli uchumi upo imara kutokana na taarifa zilizokusanywa na Benki  hiyo kutoka vyanzo mbali mbali.

  “Ni kweli kwamba uchumi wetu upo imara na kwamba uchumi wetu unapimwa kwa kuangalia vigezo vinne ambavyo  ni pato la taifa,mfumuko wa bei,urari wa biashara na upungufu wa fedha serikalini”,alisema Prof. Semboja.

  Aidha,Prof Semboja amesema kuwa serikali kwa sasa imepunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima na imeongeza makusanyo ya kodi kutoka vyanzo mbalimbali.  

  “Serikali haina matumizi makubwa ya fedha kwani matumizi yanendana na mapato yanayokusanywa ”,alisema Semboja
  Amesema kuwa wanaolalamikia kutoonekana kwa fedha mtaani ni wale waliokuwa wanapata pesa kwa njia ambazo sio halali na hivyo kupelekea kushindwa kupata kwa sasa kutokana na udhibiti uliwekwa na Serikali katika kukusanya na kusimamia kodi kwa utaratibu halali.

  Ameongeza kuwa Serikali fedha inazokusanya zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na sio kwa wachache waliokuwa wakijinufaisha wenyewe.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akilihutubia Bunge kabla ya kutoa kauli ya kuliahirisha bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016 ambapo mbali na mambo mengine amesema serikali itaendelea kutekeleza yale iliyoyaahidi na kuwashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kujitolea kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiimba wimbo wa taifa baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma. 

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali itahkikisha inaipa kipaumbele miradi ya maji ambayo haikutekelezwa kwa awamu ya kwanza, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdalah Ulega (katikati)akiwaeleza jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. James Mbatia akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


older | 1 | .... | 1356 | 1357 | (Page 1358) | 1359 | 1360 | .... | 3272 | newer