Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

MGIMWA CUP YAZINDULIWA RASMI WILAYANI MUFINDI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jumhuri William akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jumhuri William aliyeshika mpira kulia sambamba na Mwenyekiti wa CCM Mufindi, Yohanis Kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jumhuri William akikagua timu kabla mtanange kuanza.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jumhuri William akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.

Na Fredy Mgunda, Iringa. 

MASHINDANO ya kombe Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi katika kijiji cha Ikwea kata ya Ikwea wilayani Mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la Mufindi Kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji kwa wachezaji wa jimbo hilo.

Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jumhuri William kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo Taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa.

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa, hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema William

Aidha Wiliamu aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama Mbwana Samatta na wachezaji wengine wakulipwa hapa nchini hata nje ya nchi.

“ Soka limewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema William.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Felix Nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.

Kwa upande wake mlezi wa Mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Mufindi, Yohanes Kaguo alisema ataendelea kuwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza michezo wilaya ya Mufindi.

Mashindano ya Mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

MAKALA: MATUMIZI YA NISHATI MBADALA YA GESI NA MAKAA YA MAWE SULUHISHO LA UHARIBIFU WA MISITU NCHINI

$
0
0
Jengo ambalo ndani yake kuna tanuri la kuchakata makaa ya mawe ambalo limejengwa kwa msaada wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ikiwa moja ya mkakati wake wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika  kuanzisha na kutumia nishati mbadala kunusuru Misitu nchini. Jengo hilo linatumiwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Mbalawala Women Organization (MWO).

NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Misitu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai kwakua huifadhi vyanzo vya maji, kuboresha hali ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, upatikanaji wa kuni, mbao, madawa, malisho ya mifugo, kuboresha shughuli za kilimo na kuboresha mandhari ya nchi yetu mijini na vijijini. 


Aidha, misitu pia ni chanzo muhimu cha mapato kwa wananchi wengi wa vijijini na mijini.

Ni kutokana na umuhimu huo wa Misitu ndio maana Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) akapewa jukumu la kusimamia misitu na rasilimali zake kwa niaba ya Serikali Kuu ili iweze kuwanufaisha watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo kupitia matumizi endelevu.


Iko wazi kuwa kuna utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo rahisi na kikuu cha nishati nchini, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya nishati inayotumika Nchini inatokana na miti. Uvunaji mkubwa wa mkaa umeathiri sana ubora wa misitu. Kuni zinatumika zaidi vijijini na mkaa unatumika zaidi mijini.


Moja ya mashine inayotumiwa na Shirika Lisilo
 la Kiserikali la 
Mbalawala Women Organization

 (MWO) kuchakata makaa ya mawe kwa ajiliya
 matumizi ya majumbani.
Matumizi ya nishati mbadala yanatajwa kama moja ya suluhisho la tatizo hilo, Katika kukabiliana na tatizo la uharibifu wa Misitu Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) inafanya ushirikiano na wadau wa sekta mbalimbali hasa  Wizara ya Nishati na madini na jamii kwa ujumla ili kupunguza utegemezi wa misitu kama chanzo kikuu cha nishati.


Miongoni mwa asasi za kiraia ambazo Wizara inashirikiana nazo katika kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ni Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO) la Mbalawala Women Organization (MWO) ambalo lipo katika wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Makao yake makuu yakiwa katika kijiji cha Ruanda eneo maarufu kwa jina la Center D.


Shirika hilo limejikita katika uwezeshwaji wa vikundi vya wanawake kiujisiliamali ili waweze kujikwamua kiuchumi hasa wanawake ambao wanazunguka mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka uliopo Kata ya Ruanda wilayani Mbinga, wengi wao wameshindwa kuajiriwa na mgodi huo kutokana na ugumu wa shughuli husika ambazo hufanywa na wanaume.


Likiwa limejikita na shughuli za miradi ya utengenezaji wa vitofali vya kupikia vya makaa ya mawe pia lina lengo la kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti kwa kutengeneza na kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya nishati hiyo mbadala.


Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii, Meneja wa Uzalishaji wa shirika hilo, Harid Kapinga aliitaja miradi mingine ambayo inafanywa na shirika hilo kuwa ni huduma ya chakula na usafi katika kambi ya mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka, programu ya shule, bustani ya mboga na matunda, shamba la mpunga na ufinyanzi wa vyungu.



Akizungumzia uongezaji wa thamani wa makaa ya mawe ili yaweze kutumika kwa matumizi ya majumbani, Meneja huyo wa Uzalishaji alisema, awali wananchi walikuwa wanaokota makaa ya mawe pembezoni na mgodi na kwenda kupikia bila kujua madhara yake kwa maisha ya binadamu na uharibifu wa vyombo ambavyo walikuwa wanavitumia katika kupikia vyakula vyao.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MABONDIA MANYI ISSA NA MUSTAFA DOTTO KUONESHANA UMWAMBA OTCOBER 2 JIJINI DAR.

$
0
0
Mabondia Manyi Issa kushoto akitunishiana misuli na Mustafa Dotto baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya kuzipiga Mustafa Dotto October 2 katika ukumbi wa white house kimara koroge Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Manyi Issa kushoto akitunishiana misuli na Mustafa Dotto baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya kuzipiga Mustafa Dotto October 2 katika ukumbi wa white house kimara koroge Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mustafa Dotto.

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA MBALIMBALI KUZIPIGA October 2 katika ukumbi wa White House Kimara Korogwe mabondia hawo ni Manyi Issa atakaezipiga na bondia mkongwe na mzoefu Mustafa Dotto katika uzito wa kg 61 na mpambano mwingine utawakutanisha maasimu Shedrack Ignas atakae zipiga na Abdalla Ruwanje katika uzito wa kg 63 mpambano wa raundi sita

Mapambano hayo yameratibiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya masumbwi yatakayo kuwepo siku hiyo

Mapambano mengine yatawakutanisha mabondia Emanuel Kisawani atakaezipiga na Ellsame Mbwambo katika uzito wa kg 61 wakati bondia Mohamed Muhunzi atapambana na Kassim Ahmad mpambano wa raundi nne KG 56 bondia machachali anaekuja juu zaidi katika mchezo wa masumbwi nchini Saidi Chino atazipiga na Haidali Mchanjo mpambano unao subiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo uhu wa masumbwi na ndio pambano litakalo beba michezo yote ya siku hiyo
Mabondia wengine watakao zichapa siku hiyo ni Athumani Yanga atakae oneshana ubabe na Hashimu Chisora katika uzito wa KG 61 wakati Karim Migea atavaana na Bright Nazad katika uzito wa kilo gram 61 na mpambano mwingine utawakutanisha Julias Jackson atakae vaana na Emilio Norfat mpambano wa raundi sita

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. 

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

YALIYOJIRI BUNGENI LEO September 15, 2016

$
0
0

SIMU TV: Ni lini serikali itaipa halmshauri ya Itilima fedha za miradi ya maendeleo? Naibu waziri Selemani Jafo anafafanua hapa; https://youtu.be/dEiKWbr1q6k

SIMU TV: Serikali yatolea ufafanuzi kuhusu suala la mgogoro  wa ardhi baina ya kambi ya jeshi ya Monduli na vijiji vya jirani; https://youtu.be/A1RrD5itaHI

SIMU TV: Ni lini serikali itakamilisha mradi wa maji katika kijiji cha Mkwayungu? Naibu waziri  Isack Kamwele anajibu swali la Mhe. Lusinde; https://youtu.be/Y4RNRM1aTLs

SIMU TV: Je, ni lini serikali itaijenga barabara ya Nanyumbu kwa kiwango cha Lami? Naibu waziri Mhandisi Edwin Ngonyani anafafanua hapa;https://youtu.be/LhBXzuuHCeA

SIMU TV: Serikali yatolea ufafanuzi kuhusu gharama za usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi ili kwa lengo la kurahisha usafirihttps://youtu.be/bpCMRMPo5Lk

SIMU TV: Mbunge wa jimbo la Mikumi Mhe. joseph Haule aibana serikali kuhusu kutatua mgogoro wa ardhi katika kata za Tindiga na kilangali ;https://youtu.be/Jxl1l6Pe3kM

SIMU TV: Ni lini serikali itakamilisha ahadi yake ya kutoa fedha kwa ajili ya kujenga majosho katika jimbo la Mvomero? Haya hapa ni majibu ya serikali;https://youtu.be/2-4wnNMkRJw

SIMU TV: Naibu waziri wizara ya Ardhi Mhe. Angelina Mabula aelezea namna wizara yake ilivyojipanga katika kutatua migogoro ya ardhi nchini;https://youtu.be/8F60e4ZHHkU

JWTZ KIKOSI CHA NCHI KAVU MSANGANI LACHANGIA MADAWATI 200 MKOA WA PWANI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,amepokea madawati 200 kutoka kwa jeshi la nchi kavu kikosi cha Msangani,ambayo yatasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa madawati mkoani hapo .

Aidha sekretarieti ya mkoa imefanya jitihada za makusudi kuomba wadau mbalimbali kuchangia upatikanaji wa madawati ambapo imepata madawati 1,000.

Akikabidhiwa madawati hayo na brigadia general JM.Mwaseba pamoja na brigadia general AS.Bahati kwa niaba ya mkuu wa jeshi la nchi kavu Msangani,meja general James Mwakiborwa,mhandisi Ndikilo ,alilishukuru jeshi hilo kwa kuunga mkono sekta ya elimu.

Alieleza kuwa kabla ya agizo la Rais John Magufuli la kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari,katika mkoa huo kulikuwa na upungufu wa madawati 5,451 katika shule za sekondari.

Alisema upande wa shule za msingi upungufu wa madawati ulikuwa ni 43,507 lakini kwasasa wanashukuru tatizo hilo linaelekea kumalizika na kuwa historia.

Mhandisi Ndikilo alisema wilaya ya Mkuranga ,Rufiji na Mji wa Kibaha ndio zilizokuwa na mapungufu makubwa ya madawati lakini wakurugenzi wa halmshauri za wilaya hizo walijipanga kukabiliana na hali hiyo.

Hata hivyo alisema mchango huo utawezesha wanafunzi kuondokana na kero ya awali waliyokuwa wakiipata hali iliyokuwa ikisababisha kushindwa kusoma katika mazingira bora.

“Kwa niaba ya mkoa nawashukuru jeshi la nchi kavu ,mmeonyesha ni sehemu ya jamii ya mkoa,mfikishieni salamu zangu za dhani kwa meja general Mwakiborwa,tutaendelea kuwaenzi na tunawaombea muendelee kulinda amani ya nchi”alisema.

Alitaja mikakati iliyowekwa kufanikisha suala hilo,kuwa ni pamoja na wakurugenzi kuunda kamati mbalimbali za kufuatilia utengenezaji wa madawati,mbao na magogo yaliyokamatwa na askari wa maliasili vilielekezwa kutengeneza madawati.

Mhandisi Ndikilo alisema halmashauri zilitumia vyanzo vyao vya mapato,kutafuta wadau wa ndani na nje ya wilaya na mkoa,kuitisha harambee,kuhamasisha jamii na kukarabati madawati yaliyochakaa kidogo.

Awali katibu tawala wa mkoa huo,Zuberi Samataba alieleza miongoni mwa wadau waliojitokeza kuchangia zoezi hilo mkoani humo ni jeshi la nchi kavu na ubalozi wa China. Wengine ni kampuni ya goodwill Tanzania ltd ya Mkuranga,mamlaka ya bandari Tanzania ,taasisi mbalimbali binafsi na za umma,kampuni ya tigo.

Samataba alisema madawati zaidi ya 1,000 kutoka kwa wadau hao yatagawiwa katika shule mbalimbali kulingana na mahitaji. Alisema sekretriet ya mkoa inaendelea kuwasiliana na wadau wengine kuendelea kuunga mkono juhudi za kufanikisha upatikanaji wa madawati.

Brigadia general JM.Mwaseba ,alisema wakati mkoa ukiendelea na juhudi zake kufanikisha adhma hiyo jeshi hilo limejitolea kutoa madawati hayo ili kumuunga mkono rais Magufuli .

Alisema madawati hayo yametengenezwa katika kiwanda cha nyumbu chini ya brigadia jeneral AS.Bahati. Afisa elimu mkoani Pwani,Yusuph Kipengele alisema mkoa umeshakamilisha madawati ya shule za msingi na sekondari kwa asilimia 99.

Alisema mojawapo kati ya matokeo ya elimu bila malipo ni ongezeko la wanafunzi na hivyo kusababisha ongezeko la mahitaji ya miundombinu na samani ikiwemo madawati . Kipengele alieleza kuwa upande wa sekondari awali mkoa ulikuwa na mahitaji ya madawati 47,276 yaliyokuwepo 42,795 upungufu ulikuwa 4,481 sawa na asilimia 10.47.

Kipengele alisema shule za msingi mkoa ulikuwa na mahitaji ya madawati 92,586 yaliyokuwepo ni 61,318 upungufu ulikuwa ni madawati 31,268 sawa na asilimia 33.77.
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, wa katikati ,ambapo kulia ni kamanda wa jeshi la nchi kavu kikosi cha Msangani Brigedia Jenerari Jairos Mwaseba na kushoto ni Brigedia Jenerari A .S.Bahati wakiwa  wameketi kwenye moja ya madawati ambayo jeshi hilo limechangia Mkoani Pwani.  
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akipokea moja ya madawati kutoka kwa Kamanda wa jeshi la nchi kavu kikosi cha Msangani ,Brigadia Jeneral Jairos Mwaseba baada ya jeshi hilo kuchangia madawati 200 katika mkoa wa Pwani, Kulia ni Brigedia Jenerari A .S.Bahati (Picha na Mwamvua Mwinyi) 


Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimshukuru Kamanda wa jeshi la nchi kavu kikosi cha Msangani ,Brigadia Jeneral Jairos Mwaseba baada ya jeshi hilo kuchangia madawati 200 katika mkoa wa Pwani.
 

SERIKALI ITAHAKIKISHA WALIOTEKWA NYARA KONGO WANAPATIKANA WAKIWA SALAMA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO.

Serikali imesema kuwa inashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhakikisha kuwa madereva wanaoendesha magari aina ya malori ambao wametekwa nyara jana na waasi wa kikundi cha Maimai katika eneo la Namoyo jimbo la Kivu kusini katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanapatikana wakiwa salama.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuwakoa watanzania waliotekwa nyara.

“Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Kongo inaendelea kufanya kila jitihada kuhakikisha madereva hao wanaachiwa huru haraka iwezekanavyo na kurudishwa nchini wakiwa salama”

“ Waasi hao wa Maimai wametoa masaa 24 hadi kufikia leo wawe wamelipwa kiasi cha Dola 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia huru na kutishia kuwadhuru endapo hawatapata fedha hizo, hivyo basi Serikali imeendelea kuwa na mazungumzo na Serikali ya Kongo ili kupata ufumbuzi wa suala hili” alisema Kasiga.

Aliongeza kuwa malori yaliyotekwa nyara ni 12 kati ya hayo nane ni mali ya mfanyabiashara wa kitanzania Bw. Azim Dewji na mengine ni mali za wafanyabiashara kutoka nchini Kenya.Aidha, Serikali imewataka watanzania kufahamu hali ya usalama wa nchi wanazokwenda ili kujikinga na matatizo mbalimbali yanayoweza kuwapata wakiwa katika nchi hizo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 14/09/2016.

VISIMA 7 KUPUNGUZA TATIZO LA MAJI KISHAPU

$
0
0

Youth Climate Activist Network (YouthCAN) Tanzania Ni mtandao wa vijana wanaotoka kwenye taasisi za dini mbalimbali wanaofanya shuguli mbalimbali za mazingira na afya kwa ujumla kwa kujitolea chini ya Shirika la Norwegian Church Aid (NCA)

Kuanzia Tarehe 11/9 /2016 vijana hawa walianza masafara wa Kutembelea baadhi ya maeneo yaliyo athirika sana na mabadiliko ya tabia nchi. Ili kutoa elimu ya Utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji na usafi .baada ya kutoa elimu hiyo Halmashauri ya wiliya Kishapu Mkoani Shinyanga wanatarajia kwenda Kutoa elimu hiyo Mkoani Manyara kwenye baadhi ya vijiji vilivyopo Hanang.Hydom na Mbulu.

Licha ya kutoa elimu juu mazingira,Maji ana afya vijana hawa watapata nafasi ya kuzindua baadhi ya Visima vya maji vilivyo jengwa na Shirika la Norwegian Church Aid (NCA) kwa kushirikiana na Washirika wake.

Ambapo kwa kuanza wamepata fursa ya kushiriki uzinduzi wa visima 7 vilivyojengwa kwa msaada wa watu wa Norway visima hivyo vitasaidia kutatua tatizo la maji safi na salama katika vijiji vi 3 wiliyani Kishapu .ambavyo ni IKONDA A,UBATA na MWAWEJI.

Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Kishapu Bwana.Stephen M Magoiga akizindua moja kati ya Visima saba.

Afisa Mradi Mwandamizi Mama Tina Mosha Akimtwisha maji Moja ya wanakiji wa IKONDA.
Nizar Selemani Mratibu wa shuguli za vijana katika shirika la NCA na Baraka Chedego ambae ni Mratibu wa Youth CAN wakizungumza jambo wakati wa mkutano na wanakijiji cha Ikonda.
Moja visima vilivyokuwa vikitumiwa na wanachi kabla ya ujenzi wa visima vya kisasa.
Picha zote na IMANI SELEMANI NSAMILA.


MFAHAMU MCHEZAJI MWINYI HAJI NGWALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii


MWINYI Haji Ngwali ni beki wa kushoto wa timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam aliyesaini kuitumikia timu hiyo.

Yanga ilimsajili beki huyo ili kuongeza nguvu katika kikosi chao kwa kusaidiana na beki wa muda mrefu wa timu hiyo Oscar Joshua.

Mwinyi alisajiliwa na Yanga akitokea katika timu ya KMKM iliyopo visiwani Zanzibar baada ya kocha Hans Van de Pluijm kuvutiwa na kiwango chake .

Beki huyo ameonekana kuwa tegemeo katika timu yake ya Yanga pamoja na Taifa baada ya kuonekana kuwa na uwezo mkubwa uwanjani huku akiisaidia vema safu ya ulinzi.

Nyota ya mchezaji huyo ilianza kung'ara pale alipoitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ilipokuwa chini ya Mart Nooij.

ELIMU
Mwinyi alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Amani na baadaye kujiunga na shule ya sekondari ya Kwereke ambapo hakufanikiwa kumaliza kidato cha nne baada ya kutofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili na kuamua kujiingiza rasmi kwenye soka.

SAFARI YAKE KATIKA SOKA
Mwinyi alianza kujihusisha na soka wakatiyupo  shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 10.
Mwinyi amepitia katika vituo mbalimbali na kushiriki ligi visiwani Zanzibar.

TIMU ALIZOWAHI KUCHEZEA
Mwinyi alifanikiwa kujiunga na kituo cha Jiva Nile ambacho kilimsaidia katika kuendeleza kipaji chake.
Baadaye Mwinyi alijiunga katika kituo cha Junior Naturally alipokaa kwa misimu miwili na kufanikiwa kujiunga na timu ya Mapunda inayoshiriki ligi daraja la pili visiwani Zanzibar.

Akiwa na timu hiyo mwaka 2011 aliitwa katika kikosi cha Kombaini ya U-20 ya Mjini Magharibi ambapo walishiriki mashindano ya Copa Coca Cola. 2012 akiwa na timu ya Chuoni ilishiriki mashindano ya Mapinduzi Cup na kufanikiwa kuwa mchezaji bora na 2014 alisajiliwa na timu ya KMKM ya Zanzibar iliyoshirikushiriki mashindano ya Kagame 2015 na Yanga kuvutiwa nae na kumjumuisha katika kikosi chao.

NJE YA SOKA
Nje ya soka Mwinyi ana ndoto za kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa wa ndani na nje. Anasema kwa sasa ameweka mikakati thabiti na atahakikisha mikakati hiyo inafanikiwa ili aweze kutimiza ndoto alizonazo katika maisha yake ya baadaye.

NAPENDA
Mwinyi anapenda kuona familia yake inafuraha kwani hiyo ndo imekuwa msingi mzuri wa mafanikio. Anasema mara nyingi anapokuwa nyumbani hupenda kuangalia filamu mbalimbali hasa zile anazokuwa wameshiriki Mboto na Gabo pamoja na kusikiliza muziki Bongo fleva wa hasa pale anapokuwa amechoka.

SIPENDI
Mwinyi anasema kuwa hapendi kukaa maeneo yanayokuwa na vurugu au kelele kwani mara nyingi anapenda kupumzika. Anasema yeye kama mchezaji muda mwingi hupumzika hasa baada ya mazoezi hivyo hujitahidi kuepuka kukaa sehemu zinazokuwa na kelele.

MALENGO
Malengo ya Mwinyi Haji ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwani ana amini kuwa yeye ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa katika soka na anauweza wa kuchezea timu yoyote itakayomuhitaji. Anasemakuwa atakapofanikiwa kucheza soka nje ya nchi anaamini kuwa ndoto zake alizoweka katika maisha zitafanikiwa kwa urahisi.

AJIRA KWA VIJANA
Mwinyi anasema kuwa suala la ajira limeendelea kuwan tatizo kubwa kwani vijana wanaomaliza vyuo kila mwaka ni wengi ukilinganisha na ajira zinazotangazwa. Anasema vijana wanatakiwa kubadili mtazamo wao na kutafuta njia mbadala za kuweza kujikwamua kimaisha ikiwemo kujiajiri au kuunda vikundi vya vitakavyoweza kupatiwa mikopo na kujiingiza kwenye miradi itakayowasaidia kutengeneza ajira zao binafsi na kuajiri wengine.

USHAURI KWA WIZARA YA MICHEZO
Mwinyi anasema kuwa angeomba kuboreshwa kwa viwanja vya michezo ili viweze kuwa na hadhi kutokana na vingi kuwa katika hali mbaya kwani endapo Tanzania tungekuwa na viwanja vizuri basi vipaji vingi zaidi vingeendelea kujitokeza na kuacha dhana kuwa watu wanacheza mpira kutokana na kukosha shughuli maalum za kufanya.

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha saba cha bunge la kumi na moja ambapo pia alisema kiasi cha shilingi milioni themanini na tano na laki tano zimechangwa kutokana na makato ya posho ya siku moja yawabunge kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) picha juu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akijibu swali bungeni ambapo alitoa wito kwa wabunge kuisaidia kutoa elimu kwa wananchi waliovamia maeneo ya jeshi kuondoka ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina ya jeshi na wananchi, wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Jumanne Maghembe (MB) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (MB), wakati wa kikao cha saba cha Bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe. Joseph Haule akiuliza swali bungeni kutaka kujua mikakati ya serikali katika kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji inayopelekea mauaji ya raia ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaohusika na mauaji ya raia nchini hasa ikiwemo wanaohusika kwenye migogoro hii.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

BALOZI WA TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA KUKUTANA NA WANA DAR ES SALAAM KESHO

$
0
0
Balozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka, Nathan Mpangala (katikati), akielezea jambo kuhusu tukio la kesho ambalo atalitumia kukutana na baadhi ya wakaazi wa Dar es Salaam, kuanzia saa 11 jioni katika viwanja vya “Nafasi Art Space, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo atatumia nafasi hiyo kusimulia yaliyojitokeza katika tamasha hilo lililofanyika Songea miezi michache iliyopita. Wengine katika picha ni wadau wa tamasha hilo, Grace Matovolwa na Mussa Sango.
Mdau wa Tamasha la Majimaji Selebuka, Mussa Sango akisisitiza umuhimu wa wakaazi wa Dar es Salaam kushiriki mazungumzo hayo yatakayofanyika kesho kuanzia saa 11 jioni katika viwanja nya Nafasi Art Space, Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Ni tukio la wazi, halina kiingilio.

Jokate awaomba Watanzania kuchangia wahanga wa tetemeko Kagera

$
0
0
Na Mwandishi wetu

Mrembo, msanii wa filamu na mwanamuziki, Jokate  Mwegelo ametoa wito kwa jamii, mashirika na watu binfasi kujitolea kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi lililoikumba  mkoa wa Kagera na kusababisha vifo na baadhi ya watu kukosa makazi ya kuishi.

Jokate  alitoa wito huo jana wakati wa kutangaza mikakati yake ya kusaidia wahanga wa tetemeko hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM Foundation. Alisema kuwa tikio hilo ni kubwa na lemeleta majonzi kwa baadhi ya familia na kuwaomba wadau kuungana kusaidia kuondoa changamoto zinazowakumba wahanga.

Alisema kuwa wakati anajipanga chini ya msaada wa GSM Foundation, ameamua kutoa rai kwa watanzania ikiwa pamoja na wanamichezo, wasanii, wanamuziki na wadau wengine mbalimbali kuchangia ili kuondoa changamoto  hizo.

“Kwa kweli hali si nzuri kabisa, mimi kama msanii na ni Mtanzania, nimeguswa na kuamua kuingia mtaani kuhamasisha watu binafsi, makampuni  na asasi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kusaidia wahanga wa tetemeko hilo,” alisema Jokate.

Alisema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuungana katika tatizo hilo ambalo pia limeharibu baadhi ya shule na kusababisha wanafunzi kukosa sehemu ya kupata elimu. “Kwa wasanii, warembo na wanamuziki, ni wakati muafaka sasa kusaidia  na kufanya mrejesho wa mapato yetu kwa jamii kwa kusaidia wahanga,” alisema.

Alifafanua kuwa suala hili si kwa watu wenye uwezo,tu, bali hata watu wenye kipato kidogo  linawahusu kwani chochote walichonacho kama nguo, vyombo vya nyumbani, vitanda, magodoro, chakula, sabuni, mafuta na vitu vingine vinahitajika kwa wahanga wa tetemeko hilo.

Mayanja atamba kuisambarataisha Azam FC Jumamosi

$
0
0
Benchi la Ufundi la klabu ya Simba limesema hakuna kitakachowazuia kuibuka na ushindi dhidi ya Azam FC katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru.

Timu hizo mbili zitakuwa zinakutana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu na mpaka sasa hakuna timu iliyopoteza mchezo. Simba na Azam FC mpaka sasa zimekusanya jumla ya pointi 10 kutokana na mechi nne na zimefungana kwa kila kitu kwenye msimamo huo.

Mbali ya kuwa sawa katika idadi ya mechi za kucheza, kila timu imeshinda mechi tatu, kutoka sare mechi moja, kufunga mabao saba, kufungwa mabao mawili na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kutokana na hali hiyo, mchezo huo ndiyo utaamua nani atakuwa katika mstari mnyoofu wa kuongoza ligi na timu ipi itapoteza mwelekeo. Hii inatokana na ukweli kuwa mechi ya Simba dhidi ya Azam, Yanga dhid ya Simba na Yanga dhidi ya Azam ndizo zinazotoa hali halisi ya nani anaweza kutwaa ubingwa msimu huu.

Mayanja alisema kuwa wanajua mchezo huo utakuwa mgumu na wamejiandaa vilivyo ili kufanya vyema. Alisema kuwa Azam FC ni timu ngumu, lakini wamejidhatiti ili kuitwaa kushinda na kufuta aibu ya miaka mine ya kutotwaa ubingwa wa Tanzania Bara wala kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kwa kushika nafasi ya pili.

“Tunajua tutakacho kifanya katika mchezo huo, tumejiandaa na jambo zuri kwetu ni kuwa tuna kikosi kipana na hakuna majeruhi hata mmoja, nawaomba mashabiki wa Simba waje kwa wingi kuipa sapoti timu yao,” alisema Mayanja.

Aliongeza kuwa wamedhamiria kukata kiu ya mashabiki wao katika mechi hiyo ambayo anaamini itakuwa njia pekee ya timu yake kufanya vyema msimu huu. 

Zaidi ya wafanyabiashara 100 wa Tanzania na Kongo kushiriki kongamano la Biashara

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO 

Zaidi ya wafanyabiashara 100 kutoka Tanzania na Kongo wanatarajia kushiriki kongamano la biashara litakalofanyika Lubumbashi Kongo Septemba 22 mwaka huu.

Lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuongeza kiasi cha mauzo ya nje na kuboreshwa mazingira mazuri ya biashara kati ya nchi hizo mbili.

“Wafanyabiashara wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kupata soko nchini Kongo, kutokana na nchi hiyo kutegemea bidhaa nyingi kutoka Tanzania kama vile samaki wabichi na wakavu kutokana na nchi hiyo kutokuwa na bahari,” alifafanua Afisa biashara wa TANTRADE Bi. Getrude Ngwesheni.

Aliendelea kwa kusema kuwa Kongo wanaongea lugha ya kiswahili kuwasiliana, lugha ambayo inatumika na watanzania wengi, hivyo itarahisisha mawasiliano katika shughuli za biashara.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kongamano hilo kutoka Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bi. Anna Msonsa amesema kuwa kongamano hilo linatoa fursa kwa wafanyabiashara wote kuanzia wa chini mpaka wale wakubwa na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo.

Akitoa maelezo ya namna ya kushiriki Kongamano hilo Afisa Miradi kutoka Kampuni ya 361 Bi. Naomi Godwin amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kujaza fomu ambazo zinapatika katika ofisi za 361 digrii zilizoko Msasani pamoja na ofisi za TCCIA na TANTRADE au kwa kutembelea tovuti ya www.tanzaniadrc.com.

Aidha, kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Kongo, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirikisho la wafanyabiashara wa Kongo (FEC), Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Taasisi ya Sekta Binafsi Nchi Tanzania (TPSF), Kampuni ya 361 Degrees na mdhamini mkuu ambaye ni Taasisi ya GSM Foundation.  
 Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna  Msonsa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22 Jijini Lubumbashi, Congo. Kushoto ni Afisa Miradi wa Kampuni ya Uhusiano ya 361 Tanzania, Bi. Naomi Godwin.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Louis P. Accaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22 Jijini Lubumbashi, Congo. Kushoto ni Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna Msonsa.

Meneja wa Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bi. Farida Rubanza (kushoto) akielezea jambo wakati wa mkutanio wao na  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Louis P. Accaro, Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna Msonsa na Afisa Miradi wa Kampuni ya Uhusiano ya 361 Tanzania, Bi. Naomi Godwin.Picha na Frank Shija, MAELEZO.

CHINA YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 100 KWA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

$
0
0

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

UBALOZI wa china nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya china na wananchi wa china wametoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni mia moja kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea septemba 10 Mkoani Kagera.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa niaba ya Balozi wa China ambaye yupo likizo nchini China Dk. Lu Youqing, Naibu balozi wa china Zhang Biao alisema kuwa wamewatembelea wahanga wa tetemeko hilo na kujionea jinsi wananchi walivyohathirika.

"Ndugu zetu bado wanahitaji misaada kwani tetemeko limewaathiri sana kwani wapo waliopoteza makazi,waliojeruhiwa tumeona huzuni sana tulipoona hali hiyo,tunawapa poleni nyingi sana na tupo pamoja katika kipinfi hiki Kigumu"alisema Naibu Balozi huyo

Alivitaja vitu walivyotoa kwaajili ya wahanga wa tetemeko kuwa ni mahema,madawa,chakula na mablanketi.

Alisema Nchi ya china na Tanzania ni marafiki wanaoshirikiana katika sekta mbalimbali katika kujenga Taifa la Tanzania watazidi kusonga mbele.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu  baada ya kupokea msaada huo aliushukuru Ubalozi wa China kwa ushirikiano wao na kuguswa na maafa hayo ya tetemeko la ardhi kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.

Kijuu alisema kuwa msaada huo utawafikia walengwa kwa wakati na kamati ya maafa iliyoundwa itasimamia kwa karibu.amesema mpaka sasa kuna shilingi milioni 460 kwenye akaunti ya maafa ya kagera zilizotumwa  na wananchi wote Tanzania

"Ninawahakikishia kuwa msaada huu utawafikia walengwa na hakuna ujanja ujanja wowote utakaotokea,na misaada hii tutaanza kuwagawia walengwa walioathirika zaidi kama waliopoteza makazi,wazee na wajane"alisema Kijuu.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meje Jenerali mstaafu Salimu Kijuu akimshukuru Naibu Balozi wa China Zhang Biao baada ya kupokea msaada kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi
 Baadhi ya Madaktari wa kichina waliokuja bukoba kutoa huduma za matibabu kwa wahanga wa tetemeko la ardhi wakiwa kwenye picha ya pamoja. 
 Sehemu ya misaada iliyotolewa na serekali ya china kwa wahanga wa tetemeko Mkoani Kagera
 Lori lililoleta msaada wa serekali ya china Mkoani Kagera kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi


UVCCM YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU VURUGU ZA JIJINI ARUSHA,YAMSIMAMISHA KAZI KATIBU WA UVCCM ARUSHA

$
0
0

Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel kwa kutotiii agizo la Makao Makuu linalomtaka kuhama na kusibabisha mvutamo na malumbano yasio na tija kwa chama cha Mapinduzi mkoani Arusha.

Pia Jumuiya imewataka vijana wa uvccm kutambua kuwa shughuli za uendeshaji wa umoja huo zinafanyika kwa kufuata taratibu za kikanuni chini ya misingi ya nidhamu na utii.

Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka Hamdu Shaka amewaeleza wandishi wa habari katika ofisi za UVCCM mkoa wa Arusha mara baada ya kumaliza mzozo ulioibuka na kusababisha baadhi ya vijana kufunga ofisi wakimkataa Ezekiel asiendelee kubakia mkoani hapo.

Shaka alisema tokea tarehe 25 August makao makuu ilimuandikia barua Mollel kumuhamishia Makao Makuu Dar Es Salam lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.

Alisema kikao cha sekreterieti ya Taifa kilichoketi jijijini Dar es salaam 14 September kimeamua kumsimamisha kazi katibu huyo na kumtaka ampishe katibu wa mkoa mpya Said Goha aliyehamia Arusha akitokea lindi

"Mollel amekuwa akidai kuwa Arusha kuna harufu ya ubadhirifu wa mali na miradi ya Jumuiya, Makao makuu haijapinga dai hilo , kuhama kwake si kikwazo cha kuzuia kubaini nani amehusika na tuhuma hizo, amehamishwa kwa sababu za kawaida pia kutokana na sintofahamu iliopo "alisema shaka.

Alipoulizwa iwapo ni mpango wa kukuondoa ili kuficha ukweli wa ufujaji wa miradi alisema kuhama kwake hakuwezi kuzuia ukweli usijukikane, kwani Jumuiya inafanya uchunguzi wa miradi na rasilimali zake pia vyombo vya serikali vimeombwa viingiliie sakata hilo ili kupata ukweli wa mambo.

"Mtumishi unapohamishwa toka kituo kimoja kwenda kingine na kukataa huo ni uvunjaji wa taratibu, ukiukaji wa kanuni na kutoonyesha nidhamu ya kazi, amesimamishwa kazi hadi jambo lake litakapifikishwa katika vikao vya kitaifa vyenye mamlaka ya uteuzi wake wa mwisho kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM"alieleza shaka

Akijibu swali la mwandishi kwamba katibu huyo amekuwa akikaidi kuondoka kwa sababu analindwa na baadhi ya wakubwa wa makao Makuu pia makao makuu ikitaka kumlinda kiongozi mmoja wa juu asihusishwe na ubadhirifu huo, shaka alikana na kusema wanaoeneza maneno hayo ni mashabiki wa kisiasa..

"Nasema vijana wenzetu wa Arusha wafahamu uendeshaji wa kazi zetu ni uzingatiaji wa taratibu na kikaanuni, makao makuu haiwezi kumkingia kifua mwizi na kumtetea , kumlinda na kumtetea mvunja taratibu husika "alisema.

Aidha Kaimu huyo Katibu mkuu alisema kazi ya ufuatiliaji miradi, mikataba , mapato na matumizi yake yatafuatiliwa hatua kwa hatua na ukweli wa jambo hilo utaanikwaa bila mtu kulindwa na kuogopwa.

MKUU WA WILAYA, FELIX LYAVIVA :WANAFUNZI HEWA 2548 WABAINIKA MANISPAA YA TEMEKE.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
WANAFUNZI 2548  katika shule za Sekondari na Msingi 12 wamebainika  kuwa hewa katika Manispaa ya Temeke.

Akizungumza na Wakuu wa Shule wa Sekondari, Msingi, Waratibu wa tarafa na Kata, Mkuu Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva amesema wanafunzi hao wamechukua fedha nyingi pamoja na kuhangikia madawati.

Lyaviva amesema kuwa walimu wakuu katika shule zilizobaki wanatakiwa kuhakiki wanafunzi katika kuweza kuondokana na wanafunzi hewa katika kuweza kupanga bajeti vizuri.

Amesema kuwa wanafunzi hewa wa kwa shule za msingi 1986 na Shule za Sekondari 859 ambao wanafunzi hao walikuwemo katika madawati na kufanya nguvu zaidi kutumika kwa wanafunzi hewa hao.
Mkuu wa Wilaya Lyaviva amesema walimu waliohusika katika kufanya hivyo watachukuliwa hatua ikiwa ni kutaka wafanyakazi kufanya kazi kwa utaratibu.
Aidha amewataka wakuu wa shule kuwa na utaratibu wa kuhakiki wanafunzi ili kuweza serikali kupanga bajeti ambayo inaenda kufanya kazi iliyokusudiwa na sio bajeti kwenda kwa wanafunzi hewa 

BANK OF AFRICA (BOA) YAZIDUA KADI MBILI AMBAZO NI TOUCAN VISA NA PROXMA VISA JIJINI DAR.

$
0
0
Meneja Masoko, Utafiti na Maendeleo wa Bank of Africa (BOA), Bw. Muganyizi Bisheko akionesha card aina ya PROXIMA iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Benki ya Afrika (BOA) imezindua kadi mbili TOUCAN VISA CARD na PROXMA VISA CARD ambazo zinasaidia kulinda usalama wa mteja tofauti na zilizokuwa zimetolewa mwanzo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenki Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo. Picha na Emmanuel Massaka wa Blogu ya Jamii.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Wananchi wahamashwa kushiriki matembezi ya hisani kuchangia wahanga wa tetemeko la Kagera

$
0
0


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na  Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa matembezi ya hisani ili kusaidia wahanga waliokumbwa na maafa ya  tetemeko  la ardhi  lilitotokea  Septemba 10 mwaka huu, huko mkoani  Kagera.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga amesema kuwa, matembezi hayo ya hisani ya kilomita tano yataongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

   Aliongeza kuwa Matembezi hayo yatafanyika siku ya Jumamosi Septemba17 mwaka huu, ambapo yataanzia Bwalo la Polisi Osterbay (Polisi Officer’s Mess) kuanzia saa 12 asubuhi.

Aidha amesema kuwa, matembezi hayo yana lengo la kuhamasisha wafanyabiashara, taasisi za fedha, kampuni mbalimbali pamoja na  jamii ya watanzania, wanadiplomasia waliopo nchini kuchangia kwa kutoa misaada mbalimbali ili kusaidia wahanga maafa ya tetemeko la ardhi la mkoani  Kagera.

“Tunafanya kampeni hii ya tembea kwa ajili ya Kagera, kwa lengo la kuwahamasisha watanzania, wafanyabashara na jumuiya ya wanadiplomasia waliopo nchini ili kila mtu aweze kushiriki kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha kitakachosaidia wenzetu waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Kagera” alisema Kasiga

Hivyo basi, Wizara hiyo imeeandaa daftari maalumu la michango kwa jumuiya ya mabalozi  katika nchi zote zenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, ili kuunga mkono zoezi la kuwasaidia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lilitokea mjini Bukoba.


Pia Serikali imefungua akaunti rasmi kwa jina la Kamati Maafa Kagera katika benki ya CRDB ya  mkoani Kagera yenye namba 0152225617300 ambayo itakayotumika kupokea  michango kutoka kwa watu mbalimbali.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA SARPCCO EXTRA ORDINARY MEETING KESHO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Mrisho Gambo  mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa  Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) utakaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Lekule Laiza (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) utakaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbali mbali waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) utakaofanyika mkoani Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC. 
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images