Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

SERIKALI ITUME WATAALUMU KUFANYA UTAFITI DODOMA.

$
0
0
 
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia 
Nchini(GST) Profesa Abdulkarim Mruma,
Na Sheila Simba,Maelezo.
WAKALA wa Jiolojia Nchini (GST) imezitaka Taasisi za Umma, Wizara na Idara za Serikali kuwatumia Wataalamu wa jiolojia katika shughuli za ujenzi wa ofisi za Serikali Mkoani Dodoma ili kuweza kukabiliana na athari za matetemeko la ardhi yanayotokea mara kwa mara Mkoani humo. 
Wito huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Nchini(GST) Profesa Abdulkarim Mruma, wakati wa mahojiano yake na MAELEZO kuhusiana na athari zitokanakazo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo matetemo ya ardhi hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali imepanga kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma. 

“Nashauri Serikali kutuma wataalamu kufanya utafiti ili kuangalia ni maeneo gani yanafaa kujenga ofisi za Serikali na zinatakiwa zijengwe kwa mfumo upi ili ziweze kuhimili matetemeko ya ardhi pindi yanapotokea” alisema Profesa Mruma .Aliongeza kuwa hapo awali ujenzi wa magorofa mkoani humo ilikuwa mwisho ghorofa nne kutokana na mkoa huo kupitia na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambalo kusababisha matetemeko ya mara kwa mara. 
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa maghorofa Mkoani humo, Prof. alisema magorofa yanayotakiwa kujengwa yawe mapana na yenye kuzingatia ugumu wa nondo, aina saruji inayotumika katika ujenzi na uimara wa jengo husika. “Jengo likiwa nyembamba na refu ni rahisi kupata madhara pindi tetemeko linapotekea hivyo ni vyema watu wafuate ushauri wa wataalamu kabla kufanya ujenzi na pia kuangalia maeneo yanayofaa kwa ujenzi” alisema Prof Mruma.
Aidha ameongeza kuwa majengo yote yatakayojengwa yanatakiwa kuzingatia ubora wa majengo kwa kutumia wataalamu badala ya kujenga bila kushirikisha wataalamu.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUSABABISHWA NA TETEMEKO LA ARDHI.

VODACOM YAENDELEA KUFANIKISHA WIKI YA USALAMA BARABARANI.

$
0
0
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (kulia) akikabidhiwa stika  na Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia jijini Da res Salaam leo,zitakazotumika katika zoezi la wiki   ya Usalama barabarani inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na wiki   ya Usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni,wakati wa kukabidhiwa stika zitakazotumika katika zoezi hilo zilizokabidhiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(wapili kulia)
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (wapili kulia)wakipongezana na wadhamini wa wiki ya Usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni wakati wa kukabidhiana stika maalum kwa ajili ya zoezi hilo jijini Dar eS Salaam leo,kutoka kushoto Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia,Mkurugenzi mkuu wa Puma energy,Philippe Corsaletti na Mkurugenzi wa Selcom,Benjamin Mpamo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamanda Mohammed Mpinga (kulia)akionesha stika zitakazotumika katika wiki ya Usalama barabarani itakayofanyika kitaifa mkoani Geita hivi karibuni wakati wa kukabidhiana stika hizo maalum kwa ajili ya zoezi hilo leo jijini Dar eS Salaam,wanaoshuhudia kutoka kushoto Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia,Mkurugenzi mkuu wa Puma energy,Philippe Corsaletti.

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Azzan Musa Zungu akiendesha kikao cha bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016.  
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Mwigulu Nchemba akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.

BREAKING NYUZZZZ......: HOTELI YA KCC KIBAHA MAILI MOJA YASHIKA MOTO MCHANA HUU

$
0
0
Moto Mkali ukiendelea kuteketeza eneo la jiko la hoteli ya KCC iliyopo Kibaha Maili Moja, Mkoani Pwani mchana huu. Askari wa zimamoto bado wanaendelea na uzimaji wa moto huo. haijafahakima bado kama kuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na tukio hilo la moto. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASO BLOG.
Moto ukiendelea kuteketeza Jengo hilo.
Baadhi ya Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na kazi ya uzimaji wa Moto huo, uliozuka ghafla kutokea katika Jiko la Hoteli hiyo, Mchana huu.


MAKALA MAALUM: ZIARA YA WAZIRI MKUU KATIKA MAENEO YA ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Taarifa ya Hali ya Uchumi nchini

Tamasha la uhondo wa Zantel lakongo nyoyo za wakazi wa Tameke

$
0
0
 Msanii wa muziki wa bongo flava, Seif Mwinjuma ‘sholo mwamba’ akiimba
katika tamasha la Uhondo wa Zantel lililofanyika katika viwanja vya
Temeke Mwisho, Dar es Salaam hivi karibuni ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu ya mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma mpya zilizopo sokoni.
 Meneja Habari na Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Zantel, Winnes Lyaro
(kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wakazi wa Temeke, Dar es Salaam
 kuhusu huduma na bidhaa  mpya zitolewazo na kampuni hiyo wakati
wa tamasha lililopewa jina la ‘uhondo wa Zantel’ lililodhaminiwa na
kampuni hiyo.

SERENGETI BOYS WAANZA KUJIFUA, CONGO KUINGIA KESHO MCHANA.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii.

TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imeanza mazoezi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Congo Brazaville unaotarajiwa kupigwa Jumapili ya Septemba 18 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo wa mwisho kwa Serengeti Boys utakuwa wa umuhimu mkubwa sana kwani watahitaji ushindi wa hali yoyote ile ili kuweza kufuzu kuingia kwenye kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana 2017 yatakayofanyika Nchini  Madagascar.
Kikosi  hicho kiliweka kambi ya takribani wiki moja katika visiwa vya Shelisheli iliweza kucheza mchezo mmoja wa Kirafiki na timu ya Dynamo na kufanikiwa kutoka na ushindi.
Akizungumza na Michuzi Blog, Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF, Alfred Lucas amesema kuwa kikosi cha Serengeti Boys kimejizatiti kuweza kuhakikisha wanapata ushindi ili kuweka mazingira ya kwenda fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.
Lucas amesema, wana imani na kikosi hicgo na zaidi wameshacheza michezo kadhaa na hawajapoteza hata mechi moja kwahiyo Kocha Mkuu wa yimu hiyo Bakari Shime ameendelea kuwapa mbinu mbalimbali ili kuweza kutoka na ushindi kwenye mchezo huo.
Kwa upande wa msafara wa timu ya Congo Brazavlle , Lucas amesema utakuja na watu 40 ambapo unatarajiwa kuingia kesho saa 7:45 mchana huku waamuzi wakitarajiwa kuingia Ijumaa, na kikosi cha Congo Brazaville kitafanya mazoezi kesho ijumaa kwenye Uwanja wa Karume na siku ya Jumamosi Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10 jioni na watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kuja kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri na kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Vijana.

MAJALIWA AZINDUA MIONGOZO YA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI MJINI DODOMA.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bango lenye anwani na Postikodi ya makazi yake ya Dodoma baada ya kuzindua  Miongozo ya Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi  kwenye ukumbi wa Msekwa , bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza wakati alipozindua  Miongozo ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi  Miongozo ya Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi  kwenye ukumbi wa Msekwa , bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016.

 Msanii, Mrisho Mpoto akitumbuiza katika uzinduzi wa  Miongozo ya Mfumo wa Anwani  za Makazi na Postikodi uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Msekwa , bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakakala ya kitabu cha Miongozo ya  ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi bada ya kuuzindua kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni mjini Dodoma Septemba 14, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

EWURA: VITUO VYA MAFUTA VIENDELEE KUTOA TOZO ZA HALMASHAURI.

$
0
0


Katika kuendeleza utendaji kazi kwa ufanisi kwa vituo vya Mafuta nchini ambao changamoto zake zimeonekana na gharama ambazo wanazotoa katika kutimiza huduma zinazotolewa na Halmashauri za jiji ambazo zimekuwa hazifidiwi kwenye bei inayoelekezwa na Ewura.

Kwa kuliona hilo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi ameitisha mkutano na wadau wa Mafuta ambapo lengo lilikuwa ni kujadili changamoto hizo.

Akizungumza mara baadaya kikao hicho Ngamlagosi amesema kuwa huduma zinazochangiwa ni muhimu kwani zinasaidia sana kuimarisha usalama mahali pakazi.

Aidha amesisitza kuwa tozo hizo zina umuhimu kwani husaidia pindi yanapotokea maafa kazini hasa moto na uhalali wa vipimo vya kupimia mafuta ili kuepusha wizi wa vipimo.

Kwa upande wake Malegesi Manyama ambaye ni muuzaji wa mafuta kwa rejareja yeye ameeleza kuwa Changamoto kubwa ni mtaji pamoja na upatikanaji wa mkopo katika kuendesha biashara hiyo hivyo michango hiyo huathiri gharama za mwendesha kituo.

 Mkurugenzi mtendaji wa Ewura, Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipokutana na wadau wa mafuta na kuzungumza nao.
Mdau wa kuuza Mafuta TAPSOA, Mahafudhi Maulid akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya wadau wa mafuta kuzungumza na Mkurugenzi mtendaji wa Ewura, Felix Ngamlagosi.
Wadau wa mafuta wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Ewura, Felix Ngamlagosi jijini Dar es Salaam leo.

PROF. MBARAWA ATOA MIEZI SITA KUMALIZA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA.

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi KM 2.8 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, jijini Mwanza.
Mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Mwanza.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza kazi ya upanuzi wa uwanja huo ifikapo mwezi Februari Mwakani.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua kazi ya ujenzi na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na daraja la watembea kwa miguu lililopo maeneo ya furahisha, jijini Mwanza.

Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja huo kutaimarisha hali ya usafiri wa anga kwa wakazi wa Mwanza na mikoa mingine na hivyo kukuza shughuli za kibiashara nchini.

“Hakikisheni upanuzi wa uwanja wa ndege huu unakamilika haraka ili kurahisisha na kuboresha huduma za usafirishaji kiwanjani hapa”, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Construction kumaliza kwa wakati upanuzi wa barabara ya ‘Mwanza-Airport’ eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza KM 9.15 pamoja na daraja la watembea kwa miguu la furahisha ili kukuza uchumi na kupunguza kero ya msongamano wa magari katika jiji la Mwanza.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi wa Mwanza kutoharibu miundombinu ya barabara na madaraja ambayo Serikali inatumia gharama kubwa katika utengenezaji wake.

“Naomba muitunze na kuithamini miundombinu hii kwani Serikali inatumia gharama kubwa katika kutengeneza na kukarabati”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ni mkakati wa Serikali kuhakikisha ujenzi wa uwanja huo unaboreshwa kuwa wa kisasa na wa kimataifa ili kuwezesha ndege kubwa kutua kwa wingi na kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda ya Ziwa na Kati.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

BUKOBA EARTHQUAKE

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KIJIJI RUGAZI MINZIRO KUKAGUA MADHARA YA TETEMEKO LA ARDHI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (aliyevaa miwani) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigazi - akimweleza zaidi ya nyumba 200 zilizoanguka baada ya kutokea tetemeko la ardhi. Pichani ni nyumba ya Mzee John Paulo iliyoanguka baada ya kutokea tetemeko la ardhi. Zaidi ya kaya 300 hazina makazi.






Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji Kigazi akibainisha changamoto wanazopambana nazo Wanakijiji cha Kigazi baada tetemeko la ardhi kutokea katika kijiji cha Kigazi. Mojawapo ya changamoto ni ukosefu makazi baada ya nyumba zao kubomoka.

WAZIRI WA AFYA AWAAGIZA MAKATIBU TAWALA KUTOA RUHUSA KWA MANESI KUFANYA UTAFITI WA AFYA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza Makatibu Tawala wa mikoa yote nchini kutoa ruhusa kwa manesi ambao ni wadadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 ili kufanya utafiti huo.
Akizungumza leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya wadadisi hao iliyofanyika mkoani Dodoma, Waziri Ummy amesema utafiti huu ni wa muhimu sana hivyo Makatibu Tawala hawana budi kuwaruhusu manesi hao waliopata mafunzo kufanya utafiti huo.
“Ninawaagiza Makatibu Tawala wote nchini kuhakikisha wanatoa ruhusa kwa manesi mliopo hapa leo ili muweze kulisaidia taifa letu kwa kutuletea takwimu sahihi zitakazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo hususani katika suala zima la afya”, ameagiza Mhe. Ummy Mwalimu.
Amefafanua kuwa, takwimu hizi zitasaidia kuboresha juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali za kusogeza huduma zinazohusiana na VVU kama vile huduma za upimaji wa VVU bure katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali, kutoa huduma ya kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) pamoja na utoaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU zijulikanazo kama ARV.
“Utafiti huu ni wa kipekee ukilinganisha na tafiti zingine zilizofanywa zinazohusu UKIMWI kutokana na kujumuisha upimaji wa homa ya ini ambao umekuwa tishio katika baadhi ya nchi barani Afrika”, amesisitiza Mhe. Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wote nchini kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaopita katika kaya mbalimbali zilizochanguliwa kwa ajili ya kufanya utafiti huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu utahusisha watu wote kwenye kaya zipatazo elfu kumi na sita (16,000) zilizochaguliwa kitaalam na kuwafikia watu wazima wapatao elfu arobaini (40,000) na watoto zaidi ya elfu nane (8,000).
Dkt. Chuwa ameeleza kuwa, takwimu hizi zitaisaidia Serikali katika kupanga na kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali zinazohusu sekta ya afya nchini hususani upatikanaji wa huduma za afya.
Wadadisi wapatao 187 ambao ni manesi kutoka hospitali mbalimbali nchini, wamemaliza mafunzo ya Utafiti wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI ambao unatarajia kuanza wiki ijayo.
Utafiti wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI utahusisha upimaji wa UKIMWI, maambukizi mapya na wingi wa VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU, wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count), kiwango cha usugu wa dawa za ARV, kiwango cha maambukizi ya kaswende pamoja na homa ya ini (Hepatitis B na C).
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia leo mkoani Dodoma katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya wadadisi wapatao 187 watakaofanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 unaotarajia kuanza nchi nzima kuanzia wiki ijayo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya kina kuhusu Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya utafiti huo unaotarajia kufanyika nchi nzima kuanzia wiki ijayo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumza leo mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 unaotarajia kufanyika nchi nzima kuanzia wiki ijayo.
 Mratibu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 Bi. Mariam Kitembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kiasi cha Shilingi milioni moja na laki sita (1,600,000) zilizochangwa na wadadisi wa Utafiti huo kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera hivi karibuni. Mhe. Ummy Mwalimu amekabidhiwa fedha hizo wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo mkoani Dodoma.
 Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo mkoani Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar pamoja na wakufunzi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 mara baada ya kufunga mafunzo ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 leo mkoani Dodoma(Picha zote na Veronica Kazimoto).

Mchungaji King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) atembelea waathirika wa tetemeko Bukoba

$
0
0

Na Faustine Ruta, Bukoba
Mchungaji King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) kutoka Maeneo ya Kahororo Kyamaizi Bukoba, King James ambaye pia ni  mmoja wa wadau wa maendeleo Manispaa ya Bukoba Leo jumatano septemba 14, 2016 jioni amewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Wananchi. Ni baada ya maafa kutokea katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea jummosi iliyopita mkoani hapa Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo kuongezeka na kufikia watu 17, huku wengine 253 wakijeruhiwa na kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo, pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka. King James ametembele sehemu tofauti tofauti kama Kata ya Hamugembe, Kashai, Rwamishenye na kutoa Misaada ya dharura kama Mahema, mchele, Sukari na Pesa taslimu na kuwaombea pia. Mchungaji James pia kesho ataendelea kutoa Misaada kwa Wahanga wa Tetemeko la Ardhi la nguvu ya 5.7 katika vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa Tanzania ambalo limeathiri sehemu kubwa ya Wanakagera kuanzia kwenye Makazi yao na wengine kukosa makazi na mpaka sasa kulala nje kutokana na nyumba zao kubomolewa.Takribani shilingi bilioni 1.4 zimepatikana mpaka sasa katika harambee iliyoongozwa na serikali ili kusaidia athari za tetemeko la ardhi hapa mkoani Kagera. 

Hamugembe Omukishenye ni sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la Ardhi na Nyumba Nyingi kuanguka na nyingi kubomoka huku ikiwa imepoteza zaidi ya Wakazi 6. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

ZIARA YA WAZIRI MKUU KATIKA MAENEO YA ATHARI ZA TETEMEKO MKOANI KAGERA

WAKURUGENZI WA MANISPAA, MIJI NA HALMASHURI WAAPISHWA TAMISEMI MJINI DODOMA LEO.

$
0
0

Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila kiapo wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13.
Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila kiapo wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13. 
Baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakila kiapo wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa majukumu yao katoka ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (katikati), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo (wa pili kushoto), Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma Ofisi ya Kanda ya kati Dodoma, Cathlex Makawia (kushoto) pamoja Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bernard Makali (kulia) wakiwa katika pichAa ya pamoja na wakurugenzi hao.


RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI MMOJA PAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA MITATU, IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ramadhani Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Tixon Nzunda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Adoh Mapunda kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.

WANANCHI WANAKUBALI HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI MPYA.

$
0
0
Hususani kuhusu uondoaji wa wafanyakazi hewa, sera ya elimu bure na usimamishwaji wa watumishi wa serikali kutokana na makosa mbalimbali. 
uondoaji wa wafanyakazi hewa ulitajwa na asilimia 69 ya wananchi wa Tanzania, kama juhudi mojawapo ya Rais John Pombe Magufuli, wanayoifurahia sana.

 Elimu bure (asilimia 67) na usimamishwaji wa watumishi wa serikali (asilimia 61) navyo pia vilishika nafasi za juu. Walipoambiwa wataje vitendo ambavyo hawakubaliani navyo, asilimia 32 walitaja kuzuiliwa kwa uagizwaji wa sukari na bei elekezi ya sukari. 

Hatahivyo, asilimia 58 hawapingi kitendo chochote cha Rais. Kwa ujumla kiwango cha kukubalika kwa Rais Magufuli anakubalika na asilimia 96 ya wananchi. Kiwango hiki kinaendana na viwango vya kukubalika kwa marais wa Tanzania waliopita.

Pamoja na hayo, asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo, mpaka mwisho wa awamu yake ya uongozi.

Viwango vya kukubalika vya viongozi wengine wa serikali pia vipo juu  Wananchi wanaonekana kumkubali mwenyekiti wao wa kijiji/mtaa (asilimia 78), diwani wao (asilimia 74) na mbunge wao (asilimia 68).

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye utafiti uitwao Rais wa Watu? Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano. Muhtasari huu unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, ambao ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,813 kutoka maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni 2016. 

Wananchi wengi wanasema serikali ya awamu ya tano imeleta maboresho kwenye huduma nyingi za umma. Inayoongoza ni Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo asilimia 85 ya wananchi wanasema huduma zimeboreshwa chini ya serikali mpya. Wananchi pia wanasema huduma ni nzuri mashuleni (asilimia 75), vituo vya polisi (asilimia 74), mahakamani (asilimia 73), vituo vya afya (asilimia 72) na mamlaka za maji (asilimia 67). Ni vema ikafahamika kuwa takwimu hizi zinaonyesha mitazamo na maoni ya wananchi kuhusu huduma za umma na siyo lazima ikawa ndiyo hali halisi ya mabadiliko kwenye huduma hizo. Vilevile, karibu wananchi wote (asilimia 95) wanasema watumishi wa umma wanaotoa huduma, kama madaktari, walimu, pamoja na maofisa tawala wa umma wamekuwa wakiwajibika zaidi.

Hata hivyo, wananchi wenyewe wanakubali kuwa hawapati taarifa za kutosha kuhusu masuala muhimu ya kitaifa. Ni asilimia 4 tu wanaosema wanapata taarifa za kutosha kuhusu masuala ya siasa nchini na asilimia 9 tu wanasema wanapata taarifa kuhusu masuala yanayohusu afya na elimu. Hii inamaanisha kuwa maboresho yanayosemwa kuhusu huduma za umma yanatokana na uzoefu binafsi au kutoka vyanzo visivyo rasmi. Hatahivyo, wananchi wanatamani kupata taarifa kutoka katika sekta ambazo zinagusa maisha yao. Walipoulizwa masuala gani wangependa kumuuliza mwenyekiti wao wa kijiji, diwani au mbunge, masuala yanayohusu afya, elimu, maji na barabara yalijitokeza kama mambo muhimu. Kwa upande wa Rais Magufuli, wananchi wawili kati ya kumi (asilimia 18) wangependa kumuuliza kuhusu suala la mfumuko wa bei kwa bidhaa mbali mbali.

Mwenendo unaofanana umejitokeza pale wananchi walipoulizwa iwapo wanamfahamu au wameshazungumza na viongozi wao wa vijiji, wilaya na kitaifa. Karibu wananchi wote (asilimia 96) waliripoti kumfahamu Afisa Mtendaji wa Kijiji chao na karibu nusu yao (asilimia 47) walikuwa wameshawahi kuzungumza naye. Hatahivyo, asilimia 21 ya wananchi wanamfahamu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya yao na asilimia 4 pekee wamezungumza naye.

Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa serikali ya awamu ya tano na Rais John Pombe Magufuli, wananchi wapo makini na kanuni za demokrasia na haki na wanataka zifuatwe. Wananchi nane kati ya kumi (au 80%) wanasema watendaji wa umma waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu. Asilimia 75 wanasema kuwa watendaji waondolewe pale wanaposhindwa kufanya kazi zao na siyo wanaposhindwa kufuata maagizo ya Rais. Pamoja na shauku yao juu ya uondoaji wa watumishi wa umma, wananchi wana maoni tofauti kuhusu matokeo ya kuwaondoa watumishi wa umma. Japokuwa asilimia 90 wanasema uondoaji wa watumishi hawa utawafanya watumishi wengine kuepuka vitendo viovu, asilimia 37 wanasema itawapunguzia morali watumishi wengine. Asilimia 48 wanasema uondoaji wa watumishi utawasababishia watumishi kutafuta njia mpya za kuficha maovu.

“Wananchi wana mitazamo chanya kuhusu utendaji wa serikali ya awamu ya tano pamoja na Rais Magufuli mwenyewe. Wanasema kuwa watumishi wa umma kwenye maeneo mbalimbali wanawajibika zaidi na kwamba wamegundua kuwa kuna maboresho kwenye huduma za umma. Hata hivyo wananchi wana mashaka kuhusu utaratibu unaotakiwa kufuatwa. Kwa mfano, wanataka udhibitisho wa vitendo viovu upatikane kwanza kabla ya watendaji kuwajibishwa, kulaumiwa ama kutiwa aibu. Vilevile wana mashaka kuhusu maamuzi ambayo yanaweza kugharimu fedha zao, kama kuzuia uingizwaji wa sukari. Hii inaonyesha kuwa wananchi hawatakuwa wakikubaliana na vitendo vyote vinavyofanywa na Rais bila kuhoji. Wananchi wanaendelea kuthamini  misingi ya utawala bora unaozingatia sharia zilizopo,’ anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze.

“Jambo muhimu kuhusu matokeo haya” anaendelea Bwana Eyakuze, “ni kuwa matarajio ya wananchi yamebadilika. Kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutokujali miongoni mwa wananchi, uzoefu uliotokana na utendaji duni uliodidimiza matarajio yao, na matokeo yake yakichangia utendaji usioridhisha kuendelea. Lakini mabadiliko tunayoyaona hivi sasa yanaonyesha kuwa utendaji wa sekta ya umma unaweza kuimarika. Wananchi wanaweza kutarajia viwango vya juu zaidi kama utaratibu huu mpya ni wa kudumu.”
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live


Latest Images