Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1349 | 1350 | (Page 1351) | 1352 | 1353 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Teghenjwa Hoseah, Arusha .

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe Mrisho Gambo amewaagiza Wakuu wa Wilaya tatu za Mkoa wa Arusha zinazotekeleza mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi kuwa Wenyeviti wa kamati za mradi huo ili kuharakisha utekelezaji wake katika maeneo hayo. 

  Akizungumza katika kikao cha kutambulisha mradi huo wa awamu ya Pili utakaofanya kazi katika wilaya za Ngorongoro, Monduli na Longido za Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 alisema kuna haja ya kuimarisha usimamizi wa mradi huu ili kuwajengea uwezo wanajamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi ili mradi huu uweze kuleta Tija iliyokusudiwa. 

  Alisema awali kamati hizo zilikuwa zikisimamiwa na Maafisa Mipango katika halmashauri hizo ila kutokana na majukumu yao ameonyesha wasiwasi iwapo wanaweza kuusimamia ipasavyo hivyo aliwataka Wakuu wa wilaya kuwa vinara wa kuusimamia na kuratibu kwa karibu ili kuleta mapinduzi katika maeneo ya wafugaji na kuhakikisha wanatengeneza mfumo imara na utekelezaji wa mradi huo unafanikiwa kuanzia ngazi ya kijiji. 

  “Nahitaji kuona halmashauri ambazo zinatekeleza mradi huu ifikapo mwezi Novemba ziwe zimeshaanza kutekeleza majukumu yake bila vikwazo vyovyote na nipate taarifa zake mara kwa mara ili fedha zilizotolewa na wafadhili zilete matokeo chanya,”alisema Gambo 

  Akizungumza wakati wa Kikao hicho Mwakilishi Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa imekua ni tishio kubwa kwa wananchi haswa wa maeneo haya ya wafugaji na ndio maana tulianza na Halmashauri hizi kutokana na athari zilizojitokeza katika jamii za wafugaji ambapo mifugo mingi katika maeneo yao ilipoteza uhai. 

  Aliongeza kuwa mradi huu unatofauti na miradi mingine tuliyoizoea kwa sababu Jamii inakuwa na nafasi ya kuamua jinsi Fedha za Mradi zitakavyotumika huku malengo ya mradi yakiwa ni kuijengea uwezo Ofisi ya Raisi –TAMISEMI katika maeneo makubwa mawili ambayo ni uimarishaji wa taasisi katika uratibu wa mradi na uwezo wa kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kuziwezesha mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini ziweze kutoa elimu kwa jamii kutambua na kutekeleza Miradi ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi 

  Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Mazingira na Maendeleo (IIED), Haki Kazi Catalyst (HKC), Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza (UK-aid) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) itatekeleza mradi huu katika Halmashauri 15 huku zaidi ya Bilioni 6 zinatarajia kutumika katika mradi huu.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo(Kushoto) akibadilishana business card Mwakilishi Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat.

  Mwakilishi Mshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat (aliyesimama)akiwasilisha mada ya kutambulisha mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya Nchi kwa Sekretariet ya Mkoa wa Arusha
  Viongozi wa Mkoa wakifuatilia mawasilisho ya mradi wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya Nchi ambao unatekelezwa kwa awamu ya pili katika Wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro
  Mratibu wa Mradi kutoka Tamisemi Sanford Kway akielezea wajibu wa Wizara katika kusimamia Mradi huu wa Mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi katika halmashauri 15 Tanzania.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitoa maelekezo katika kikao cha kutambulisha Mradi wa Mabadiliko ya hali ya hewa na Tabia ya Nchi.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava pamoja na Mkuu wa program ya Maji toka Ubalozi wa Ujerumani Bw. Ernst Doring wakisaini hati za makubaliano ya Serikali ya Ujerumani kuisaidia Ofisi ya Makamu wa Rais kiasi cha fedha yuro laki nne  kwa jaili ya kuendesha program  za mabadiliko ya tabia Nchi.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava na Mkuu wa program ya Maji toka Ubalozi wa Ujerumani Bw. Ernst Doring  wakibadilishana hati za makubaliano mara baada ya kusaini  mkataba huo.

  0 0


  0 0


  0 0


  Na Salum Vuai, MAELEZO

  MKUU wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa Said, ametoa muda wa wiki moja kwa daktari wa kituo cha afya Unguja Ukuu kuhamia katika nyumba anayopaswa kuishi kijijini humo kuanzia jana Septemba 9, 2016.

  Amesema kama kuna matatizo yoyote yanayosababisha daktari huyo ashindwe kuhamia kwenye nyumba hiyo, afike ofisini kwa kiongozi huyo kabla ya Septemba 15, mwaka huu kumueleza ili hatua za kurekebisha zichukuliwe.

  Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya alisema nyumba hiyo imekamilika ikiwa na huduma zote muhimu, maji, umeme na pia iko safi, lakini anashangazwa kwa nini haijahamiwa hadi alipotoa agizo.

  Amri hiyo ni ya pili kutolewa na Bi. Mashavu, ambapo wiki chache zilizopita alifika katika kituo hicho, akakikagua na kujiridhisha kwamba hakina tatizo na kuagiza kwa watendaji wa afya wilayani kuhakikisha daktari husika anahamia mara moja.

  Alieleza kushangazwa kwake kuona hadi sasa hakuna daktari aliyehamia katika nyumba hiyo.

  Alilazimika kurejea kutoa agizo hilo, baada ya suala hilo kutajwa na baadhi ya wakaazi wa Unguja Ukuu juzi kuwa ni kero, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mabaraza ya vijana wa shehia za Kaepwani, Tindini na Kaebona iliyofanyika kijijini hapo.

  Alisema si vyema kwa daktari kuishi mjini na kuiacha nyumba hiyo bila kukaliwa, hali aliyoeleza kuwa ni usumbufu kwa wananchi wa huko hasa pale kunapotokezea dharura ya kuugua wakati wa usiku.

  “Nyumba hii imejengwa ili daktari awepo karibu na wananchi na aweze kuwahudumia pale kunapokuwa na mgonjwa mwenye hali mbaya nyakati za usiku. Nataka ndani ya wiki moja daktari awe amehamia, na kama kuna tatizo waje wanione tutafute ufumbuzi,” alisisitiza.

  Alieleza kuwa iko haja kwa daktari kuhamia haraka katika nyumba hiyo, kwani mbali na Unguja Ukuu, kituo hicho kinategemewa na shehia nne ikiwemo jirani ya Kikungwi.

  Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, walikaririwa wakisema kwamba hakuna sababu ya kukosekana daktari wa kuishi kijijini hapo, kwani nyumba hiyo iko katika hali nzuri.

  “Hali hii inatusumbua sana kwani mara nyingi akitokezea mgonjwa usiku na hulazimika kutafuta gari kwa ajili ya kwenda ama Makunduchi au mjii. Ni Tunaomba muhusika atekeleze agizo la DC kwa ajili ya kuwahudumia wananchi,” alifahamisha Salama Abdalla, mkaazi wa shehia ya Tindini.

  Hata hivyo, akizungumzia suala hilo, sheha wa shehia ya Tindini Haroun Rashid Haroun, amesema ingawa nyumba hiyo imekamilika kiujenzi, lakini haina samani yoyote kama vile vitanda na vifaa vyengine vya matumizi.

  Alisema, kwa mujibu wa daktari huyo, anachosubiri ni kupatiwa kwa vifaa hivo ili aweze kuhamia.

  Aidha, alisema daktari huyo alikuwa likizoni na kwamba sasa ni wiki ya pili tu tangu aliporipoti kazini, lakini ukosefu wa samani ndio uliomzuia kuhamia katika nyumba hiyo.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Mh.Januari Makamba.


  Na Salum Vuai, MAELEZO

  WAZIRI wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mambo ya muungano Januari Makamba, ameyachangia mabaraza ya vijana Unguja Ukuu shilingi milioni tatu na kuyataka yaelewe kuwa mustakbali wa taifa la Tanzania umo mikononi mwao.

  Makamba, alikuwa akizungumza na vijana wa shehia tatu za kijiji cha Unguja Ukuu wakati wa uzinduzi wa mabaraza ya vijana wa shehia hizo uliofanyika juzi katika uwanja wa mpira wa Tindini katika jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati.

  Mabaraza yaliyozinduliwa ni yale ya shehia za Kaepwani, Tindini na Kaebona.

  Hata hivyo, Waziri huyo aliyepangwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, aliwahutubia vijana hao kwa kuunganishwa na teknolojia ya mtandao akiwa mjini Dodoma ambako ametingwa na vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Makamba aliwataka vijana hao kutojiingiza katika siasa chafu zinazoweza kuwafarakanisha na kurudisha nyuma jitihada zao na za serikali katika kuleta maendeleo nchini.

  Badala yake, aliwaeleza kuwa siasa nzuri ni zile zilizojikita katika kuwaunganisha watu, kuimarisha upendo, na kujenga taifa kwa lengo la kuwakomboa na umasikini.

  Waziri huyo pia aliwashauri vijana kutoendekeza mihemko kwa kujiingiza kwenye vitendo viovu ikiwemo biashara au matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji bangi, uasherati na uporaji, ambavyo alisema havina hatima njema kwao na kwa taifa.

  Alieleza kuvutiwa kwake na ubunifu wa vijana hao katika kujishughulisha na miradi mbalimbali ya kuwaendeleza kimaisha na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

  Mapema, Mwakilishi wa jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said, na kwa niaba ya mbunge Khalifa Salum Suleiman, aliwapongeza vijana hao kwa kuitikia wito wa serikali kuunda mabaraza yao ambayo ndiyo njia inayoweza kuwainua.

  Aliwahakikishia kuwa viongozi wa jimbo wako pamoja nao kwa kuwasafishia njia ya kutimiza mipango yote ya maendeleo wanayoipanga, huku akiwataka wasiyumbishwe na watu wasiokuwa na nia njema, ambao wamelenga kuwarejesha nyuma.

  Aidha aliyachangia mabaraza hayo kwa pamoja shilingi laki tano.

  Katika risala yao, vijana wa mabaraza hayo walisema wamejidhatiti kuupiga vita umasikini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji nyuki, kuku, mbuzi na ng’ombe, pamoja na kilimo ingawa wanakabiliwa na changamoto kadhaa za uhaba wa vitendea kazi walizoomba wasaidiwe kuzipatia ufumbuzi.

  Hafla ya uzinduzi huo iliyopambwa kwa burudani za sarakasi, muziki, tenzi, ngongoti na maigizo, ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa Said, madiwani wa wadi za jimbo la Tunguu, masheha na wananchi mbalimbali.

  0 0

   Beki wa Kinondoni Haji Mohammed Haji  (nyekundu) akipinga mpira kichwa kuondoa hatari golini kwake huku akisongwa na washambuliaji wa Mbeya wakati wa fainali za taifa za Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.
  Mshambuliaji wa timu ya Mbeya (nyeupe) akichuana vikali na beki wa timu Kinondoni wakati wa fainali za taifa za Airtel Rising Stars yanaoendelea kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kinondoni ilishinda 2-1.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa atakuwa mngeni rasmi wakati wa kufunga fainali za taifa za michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Jumapili 11 Septemba mwaka huu kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Salum Madadi amesema hiyo ni heshima kubwa kwa vijana, viongozi na wadhamini wa mashindano hayo. “Ujio wa Waziri Mkuu utaamusha ari ya wachezaji”, alisema Madadi. 

  Fainali za mashindano hayo zilifunguliwa Jumanne 6 Septemba na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Jumla ya timu 12 zinashiriki mashindano hayo huku sita zikiwa za wavulana na sita wasichana. Mikoa inayoshiriki niTemeke, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Morogoro na Mwanza kwa wavulana na Temeke, Ilala, Kinondoni, Arusha, Lindi na Zanzibar kwa wasichana.

  Katika hatua nyingine, timu za mkoa wakisoka wa Kinondoni za wavulana na wasichana zimekuwa za kwanza kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya Airtel Rising Stars baada ya mechi zilizochezwa asubuhi, Alhamsi Septemba 8 kwenye uwanja wa Karume. Timu ya wasichana Kinondoni waliwafunga Lindi 10-0 huku wavulana wakishinda 2-1 dhidi ya Mbeya.

  Wasichana Kinondoni walianza vyema mashindano hayo baada ya kuwafunga Arusha 4-0, kwa hivyo waliingia uwanjani wakiwa wakitaka sare ya aina yeyote kutinga hatua ya nusu fainali. Iliwachukua dakika tano kupata goli la kwanza likifungwa na Aisha Juma. Mchezaji nyota wa mechi hiyo Prisca Bahela aliifungia timu yake mabao matano peke yake kati ya dakika ya 16, 20, 25 kipindi cha kwanza na 30 na 31 kwenye kipindi cha pili. 

  Magoli mengine yalifungwa na Isabela John dakika ya 7 na 19 kipindi cha kwanza huku Mwantum Ramadhani na Veronica Mapunda wakifunga dakika ya 23 na 29 kipindi cha pili.

  Kwenye mechi kati ya wavulana Kinondoni na Mbeya, timu hizo ziliingia uwanjani kila moja ikiitaji ushindi ili kusonga mbele. Hali hiyo ilisababisha mechi kuwa kali na ya kuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu. 

  Timu ya Kinondoni ndio iliyokuwa ya kwanza kupata goli kwenye dakika ya 14, goli likifungwa na Shaban Maguli  aliyewashinda nguvu mabeki wa Mbeya na kuruka juu kufunga akiunganisha krosi nzuri kutoka kwa mshambualiaji mwenzake Marco Muhiru. Baada ya kupata bao, kasi ya mchezo iliongezeka huku Mbeya wakitafuta goli la kuzawazisha na Kinondoni wakitaka kuongeza bao kujihakikishia ushindi. Mpaka kipindi kwa kwanza kinamalizika Kinondoni 1 Mbeya 0.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ileile lakini walikuwa ni Kinondoni waliowafurahisha mashabiki wake kwenye dakika ya 57 baada ya kiungo Salum Yohana kupokea pasi nzuri kutoka kwa Hassan Kipera na kufanya kazi nzuri ya kuwachambua  mabeki watatu pamoja na mlinda mlango na kuiandikia timu yake bao ya pili. 

  Baada ya bao hilo, Mbeya waliongeza kasi iliyosababisha kupata bao dakika ya 77 likifungwa na Pius Crinton akiunganisha mpira wa kona uliopingwa na Ernest Kamange. Matokeo yalibakia hivyo mpaka mwisho wa mechi na kufanya Kinondoni wavulana na wasichana kusonga mbele. 
  Robo fainali za michuano hiyo zitachezwa Jumamosi Septemba 10 huku zikihitimishwa na kilele cha fainali Jumapili 11 Septemba.

  0 0

   Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akielezea siku ya kisomo duniani na dhumuni la UNESCO kuanzisha siku hiyo.

  Na Mwandishi wetu
  Katika kutambua umuhimu wa kusoma na kuandika Tanzania na mataifa mengine duniani zimeungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya Kisomo Duniani ambayo huadhimishwa kila Septemba, 8 ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho hayo pia iliambatana na Uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani (GEM).

  Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez alisema kuwa dhumuni la UNESCO kuweka siku hii ya Septemba 8 kila mwaka kuwa siku ya kisomo kimataifa ili kuziunganisha jamii zote za kimataifa duniani kuweka na kuendeleza nguvu na juhudi kwa watu kujua kusoma na kuandika ili kuleta maendeleo katika jamii mbalimbali.

  “Kauli mbiu hii inatufungulia milango ya uelewa juu ya malengo na mafanikio ya miongo mitano iliyopita ambayo yaliwekwa ya kutaka kila mtu anajua kusoma,” alisema Bi. Rodrieguez na kuongeza.  “Tunataka kujua ni changamoto gani zinazoikabili sekta ya elimu katika kusoma na kuandika na tunataka kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufikia malengo ambayo UNESCO iliyakusudia kufikiwa ya kila mmoja awe anajua kusoma.”
   Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akizungumzia juhudi za serikali za kuhakikisha kila mtanzania anajua kusoma.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
  TAMKO LA MHESHIMIWA UMMY MWALIMU (MB) WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU WATOTO WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI LILILOTOLEWA TAREHE 09/09/2016

  Ndugu Wanahabari, Nitumie fursa hii kupitia kwenu kuongea na watoto wa Tanzania, wazazi / walezi na jamii kwa ujumla katika kipindi hiki muhimu ambacho watoto wetu wamemaliza Elimu ya Msingi.  Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza watoto wote waliomaliza mtihani wa Taifa wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu, Hongereni sana!. Ni jambo la ufahari kwetu sisi wote kama wazazi/ walezi na Taifa kwa ujumla kwani hii ni fursa adhimu kwa ustawi na maendeleo ya mtoto na ni moja ya njia ya kutimizwa kwa haki ya msingi ya mtoto ya kuendelezwa ambayo inamjengea mtoto msingi imara wa maisha yake ya baadae. Pongezi zangu nyingi kwa watoto wote wa kike na wa kiume walioweza kufikia hatua hii muhimu kwa maendeleo na ustawi wao.

  Ndugu Wanahabari, Takwimu zinaonyesha kuwa, wanafunzi 795,761 (wavulana 372,883 sawa na asilimia 46.86 na wasichana 422,878 sawa na asilimia 53.14) wamesajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu. Hivyo ningependa kutumia fursa hii kuwaasa watoto waliomaliza darasa la saba kutojihusisha na tabia au vitendo vyovyote vinavyo hatarisha afya, usalama na maendeleo yao, kama vile kujihusisha kwenye masuala ya ngono, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo ya mitihani yao.

   Watoto wetu wa Kike na Kiume wajitambue, na wajue kuwa wao ni hazina ya pekee katika maendeleo ya nchi yetu. Kipindi hiki wakitumie vizuri kwa kuwa waadilifu, waaminifu, wenye bidii na kuzingatia kanuni za nidhamu na tabia njema huku wakijiandaa kwa ajili ya kuendelea na elimu ya Sekondari. Tukumbuke kuwa Serikali imekusudia kumpa kila mtoto nafasi ya kupata elimu ya Sekondari. Msingi tayari umeshawekwa na Rais wa Awamu ya tano, Mheshimiwa John Pombe Magufuli wa kutoa Elimu ya Sekondari bure. Hivyo tusingefurahi mmojawapo kati ya watoto hawa waliomaliza elimu ya msingi jana akaikosa nafasi hii kwa sababu zinazoweza kuzuilika. Nawaasa watoto wote kutumia kipindi hiki kwa kukataa kurubuniwa, kushawishiwa na kujiingiza katika mambo yenye kuhatarisha afya, usalama na maendeleo yao.

  Ninawataka Wazazi wenzangu, Walezi na jamii kwa ujumla:-
  Kutowaozesha watoto wote wa kike waliohitimu darasa la saba mwaka huu wakati wa kipindi hiki cha kusubiria matokeo yao, iwe ni kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya mahari. Kila Mzazi/Mlezi anapaswa kutambua umuhimu wa mtoto wake kuendelea kielimu, na kukua kimwili na kiakili kabla ya kuingia katika ndoa. Ieleweke kuwa Elimu ya watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayostawi. Kila mwaka wa elimu kwa mwanamke utaongeza mapato yake ya baadae kwa asilimia 15, ikilinganishwa na asilimia 11 kwa wanaume. Aidha, Kila mwaka wa mtoto wa kike kuwa shule humuepusha na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) mara 7. 

  Pia, uzoefu unaonyesha kuwa, kila mwaka wa kuelimika humsaidia msichana kufanya maamuzi bora yake na ya familia yake. Benki ya Dunia ilibainisha ya kwamba kila mwaka wa elimu huzuia vifo 2 vya uzazi katika wanawake 1000 kila mwaka!. Kwa hiyo kumpa mtoto wa kike fursa ya elimu inamsaidia sio yeye tu kukua kiakili na kimwili lakini pia inamnusuru na ndoa na mimba za utotoni na kuchangia maendeleo yake, ya familia yake na jamii kwa ujumla. Ni vyema jamii hasa wazazi na walezi wafahamu kuwa ndoa kwa wasichana sio njia muafaka ya kutatua changamoto za kifedha za wazazi/walezi. Bali elimu ndio njia bora ya kutatua changamoto hizo.

  Kuwalinda watoto wote wa kike na wa kiume waliohitimu darasa la saba mwaka huu dhidi ya vitendo vyote vya Ukatili, hasa kwa watoto wa kike kupewa mimba au kuwahusisha katika mahusiano ya kimapenzi. Kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 ambayo imefanyiwa marekebisho na kuhuishwa kwenye Makosa ya Jinai (Penal Code Cap 16)  inaelekeza kuwa ni kosa la jinai  kwa mtu yoyote kumlaghai mtoto wa chini ya miaka  18 kwa kumpa mimba au kufanya nae mapenzi. 

   Kifungu cha 130 (e) cha Sheria hii kinaeleza wazi kuwa “Ni kosa kwa mtu wa jinsia ya kiume kumbaka msichana au mwanamke; kwa ridhaa au bila ya ridhaa akiwa chini ya umri wa miaka kumi na nane. Mtu yeyote atakayetenda kosa la kubaka atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo kisichopungua miaka thelathini. Aidha, Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 Kifungu cha 83 kinaelekeza kuwa ni kosa kumuhusisha mtoto katika kazi, biashara au mahusiano yoyote yenye mlengo wa kingono iwe ni kwa malipo au bila malipo. 

  Mkono wa Serikali ni mrefu. Tutahakikisha tunawakamata na kuwafikisha Mahakamani wale wote watakao kwenda kinyume na sheria hizi.

  Aidha, natoa Rai kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa kwa mamlaka husika za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata, Wilaya na hata katika Madawati ya Jinsia na Watoto yaliyopo Polisi, pale watakapobaini mzazi au mlezi au taasisi anaenda kinyume na jitihada za serikali za kumuendeleza mtoto kielimu hasa katika kudhibiti ndoa za watoto waliomaliza Elimu ya Msingi hususan katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao.

  Vunja ukimya toa taarifa kwa maendeleo ya watoto wetu.
  Nawatakia kila la kheri watoto wote wa Tanzania katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao ya mtihani wa Elimu ya msingi.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watoto wa Tanzania.

  Imetolewa na:-
  UMMY A. MWALIMU (MB)
  WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, 
  WAZEE NA WATOTO
  DODOMA
  09/09/2016

  0 0

  Asasi isiyo ya Kiserikali ya wakazi wa tarafa za Ilongero, Mtinko na Mgori ya WAENDELEE yenye mkusanyiko wa watu wenye jamii ya Wairwana wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe mchango wa madawati 1055 yenye thamani ya shilingi milioni 97,125,000.

  Akiongea kabla ya kukabidhi mchango huo wa madawati Mwenyekiti wa WAENDELEE Joseph Jingu Kijeruda amesema asasi hiyo imeona umuhimu wa kutoa mchango huo ili kuunga mkono nitihata bza serikali katika kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini.

  Kijeruda amesema asasi hiyo yenye lengo la Kuhamasisha na kushiriki katika maendeleo ya Wilaya ya Singida, imeguswa na changamoto za sekta ya Elimu zinazosababisha ufaulu duni kwakuwa wanafunzi wengi wa tarafa hizo tatu wamekuwa wakikaa chini wakati wa masomo.

  Ameongeza kuwa makubaliano na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida ni kuyagawa madawati katika shule zenye upunguzu zaidi kuliko nyingine huku akiomba madawati hayo yawekwe kwenye kumbukumbu ya mali za serikali na kutunzwa vizuri.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew J. Mtigumwe ameishukuru na kuipongeza Asasi ya WAENDELEE kwa kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania la kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa kwenye dawati ifikapo June 2016.

  Mtigumwe amesema hadi kufikia Juni mwaka 2016 halmashauri za Iramba, Mkalama, Itigi, Ikungi na Halmashauri ya Manispaa zilikuwa zimekamilisha utengenezaji wa madawati huku Manyoni ikiwa bado haijakamilisha madawati 1,229 na halmashauri ya Wilaya ya Singida ikiwa haijakamilisha madawati 667.

  Amewasisitiza na kuwaagiza wakuu wa Wilaya na wakurugenzi kufanya uhakiki wa madawati, viti na meza kwa shule za msingi na sekondari, kufanya tathmini ya mahitaji ya matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari, kufanya uhakiki wa mali zote za shule na kuhakikisha kuwa maeneo yote ya shule yanapimwa na kupatiwa hati.

  Mwanzoni mwa mwaka 2016 mahitaji ya madawati kwa halmashauri ya wilaya ya Singida yalikuwa 16,556 huku upungufu ukiwa 6,122.

  Hadi sasa kupitia jitihada mbalimbali kama vile harambee mbalimbali, mchango ya mfuko wa jimbo, mchango wa chama cha mapinduzi wilaya ya Singida, nguvu za wanakijiji na asasi ya WAENDELEE, halmashauri imefanikiwa kuvuka lengo na kupata madawati17,384 ikiwa na ziada ya madawati 828.

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilongero Wilayani Singida wakiwa wameketi katika madawati yaliyotolewa na asasi ya WAENDELEE.
  Baadhi ya ndogo kati ya madawati 1055 yaliyotolewa na asasi ya WAENDELEE.

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew J. Mtigumwe (aliyevaa miwani) mara baada ya kuyapokea madawati hayo yaliyotolewa na asasi ya WAENDELEE, katikati yao ni Mwenyekiti wa asasi hiyo Bw. Joseph J. Kijeruda.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

  Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

  Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

  Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.

  Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  09 Septemba, 2016

  0 0  NAPE KUZURU TFF JUMAMOSI, KUTETA NA MALINZI

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) kesho Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

   KOZI YA MAKOCHA WANAWAKE YAFUNGWA

  Kozi ya makocha wa Mpira wa Miguu imefungwa leo Septemba 9, 2016 saa 5.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine ndiye aliyefunga kozi hiyo ambako pamoja na mambo mengine, alitoa shukrani za pekee kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) akisema: “Tunajivunia kwa upendeleo huu, bila shaka ni kwa sababu hata wanafunzi wanaofanya kozi hii, wanafanya vema.”

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

  LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA SIKU TATU MFULULIZO

  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.

  Miongoni mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini


  KOCHA MOHAMMED MSOMALI AZIKWA

  Kocha na mchezaji mahiri wa zamani wa Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mohammed Msomali amezikwa leo Septemba 9, 2016 kwenye makaburi ya Kola yaliopo barabara ya zamani ya Dar es Salaam-Morogoro.

  Mbali ya wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) waliohudhuria mazishi hayo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi katika maziko hayo ya Msomali aliyefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 74.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

  KILIMANJARO QUEENS YAENDA UGANDA

  Baada ya jana Septemba 8, 2016 kuilaza Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’, inatarajiwa kuondoka leo kwenda Jinja, Uganda kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) maarufu kama Kombe la CECAFA itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016.

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

  0 0  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
  Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
  Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kulia) akiwa na Viongozi wengine wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.

  0 0

  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba 

  Na Beatrice Lyimo-
  MAELEZO, Dodoma.

  Serikali imetoa kauli kuhusu hali ya chakula nchini na kusema kuna chakula cha kutosha pamoja na ziada ya asilimia 123. Ziada hiyo ya chakula inatokana na uzalishaji wa msimu wa mazao mwaka 2015/2016 ambao unapelekea upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017.
  Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba leo mjini Dodoma alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu hali ya chakula nchini.“Takwimu zinaonesha upatikanaji na mahitaji ya chakula nchini ni wa kuridhisha kwa kiwango cha utoshelevu wa ziada kwa asilimia 123” Dkt. Tizeba.
  Katika kufafanua hali hiyo, Dkt. Tizeba amesema kuwa kulingana na takwimu zilizopo hali ya upatikanaji na mahitaji ya chakula nchini inautoshelevu wa ziada kwa asilimia 123 ambapo nafaka ni asilimia 113 na mazao yasio ya nafaka ni asilimia 140 ambapo viwango vya ziada kwa mazao yote ya chakula ni tani 3,013,515.
  Dkt. Tizeba ameongeza kuwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) inauwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 246,000 ambapo kufikia Septemba 6, ilikuwa na akiba ya tani 67,506.920 za chakula kinachojumuisha mahindi, mpunga na mtama.
  Pia amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango wake wa kuiongezea NFRA uwezo wa kuhifadhi chakula katika kanda sita baada ya kupata mkopo wa dola za Kimarekani million 55 kutoka Serikali ya Poland ambazo zitatumika kujenga vihenge vyenye uwezo wa kihifadhi tani 190,00 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000.
  Kuhusu muda wa Serikali wa kutoa vibali vya kuuza chakula nje ya nchi, Dkt Tizeba amesema kuwa lengo ni kutoa nafasi kwa Serikali kukamilisha taarifa ya tathimini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/2016 na hali ya upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017. 

  Mbali na hayo, Dkt Tizeba amesema kuwa katika kuboresha hali ya usalama wa chakula nchini, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inapitia upya mfumo wa utoaji wa vibali vya kusafirisha chakula nje ya nchi ili kuwezesha ufuatiliaji wa karibu kuliko ilivyo sasa.
  Aidha, Dkt. Tizeba amesema kuwa utoaji wa vibali vya kusafirisha mazao nje umejitokeza baada ya kuona chakula kinasafirishwa nje bila kufuata utaratibu maalumu ambapo wafanyabiashara wa nchi jirani walijihusisha kununua vyakula vikiwa bado mashambani kabla ya kuvunwa.
  Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhifadhi chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya ambapo ameitaka sekta binafsi kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye uhaba.
  Kuhusu hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inayoikabili dunia ikiwamo upungufu wa mvua , Dkt Tizeba amesema kuwa Serikali itaendelea na juhudi za kuhimiza na kupanua kilimo cha umwagiliaji mashambani kwa kuimarisha miundombinu iliyopo na uvunaji wa maji ya mvua ili kuongeza uzalishaji wa mazao wenye tija. 
  Hata hivyo, Serikali inaendelea kuhamasisha na kuelimisha wafanya biashara kuuza unga nje ya nchi badala ya mahindi au mchele badala ya mpunga ili kuendana na Sera ya kuendeleza Viwanda nchini na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

  0 0  SIMU.tv: Serikali inampango gani wa kutatua changamoto katika vyama vya ushirika wilaya ya Karagwe? Naibu waziri  Antony Mavunde anatoa ufafanuzi.https://youtu.be/sDFyQYjoiaM.

   SIMU.tv: Serikali yatolea  ufafanuzi juu ya kuzisaidia hospitali zinazomilikwa na taasisi za dini ili kuziwesha kutoa huduma bora za afya kwa jamii;https://youtu.be/ootCiuZuO2s
   SIMU.tv: Serikali inampango gani wa kutatua shida ya maji wilayani Bagamoyo? Naibu waziri wa maji Mhe.Isack Kamwelwe anajibu swali la Mhe.Kawambwa;https://youtu.be/0Jzm1N6FQ60
   SIMU.tv: Serikali inamkakati wa kuiwezesha TRA kupata rekodi za moja kwa moja kutoka kwa wafanyabiashara? Naibu waziri Ashatu Kijaji anafafanua.https://youtu.be/WIObrtoO74c
   SIMU.tv: Hii hapa kauli ya serikali kuhusu vigezo inavyotumia kutoa mikopo kwa vyama vya  ushirika pamoja na Vicoba; https://youtu.be/_Irp-ehjY6E
   SIMU.tv: Je,Serikali inampango wa kuwamilikisha ardhi wakazi wa Nachingwea? Naibu waziri wa ardhi Mhe.Mabula akijibu swali la Mhe.Masala;https://youtu.be/abDHp4qkgs4
   SIMU.tv: Je, serikali inampango gani wa kuweka sheria kali kwa watu wanaohusika kuwanyanyasa watoto? Haya hapa ni maelezo ya serikali. https://youtu.be/HDCpoL-reJI
   SIMU.tv: Fahamu kauli ya serikali kuhusu kuboresha miundombinu ya mawasiliano katika vijiji vya Kichelu, kiasi na Mbwela. https://youtu.be/J6U8KgVgyY8

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma

  Serikali imewasilisha Miswada miwili inayohusu Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016 na ule wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016 ambayo imesomwa kwa mara ya pili Bungeni ili ijadiliwe na wabunge.

  Awali akisoma Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016, Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim amesema kuwa madhumuni ya Muswada huo ni kuanzisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuweka kisheria majukumu yake.

  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Muswada huo umezingatia masuala mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na kuainisha majukumu yake na kuanzisha Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

  Mambo mengine yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni kubainisha utaratibu wa uteuzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali, majukumu yake na mamlaka yake, kuifanya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa maabara ya rufaa na msemaji wa mwisho wa Serikali katika shughuli za uchunguzi wa kimaabara wa kikemia, sayansi jinai na vinasaba na Muswada huo utawwzesha kuwekwa utaratibu wa kusajili, kuratibu na kusimamia maabara na shughuli zote za maabara za kikemia, sayansi jinai na vinasaba.

  Zaidi ya hayo, Waziri Ummy amesema kuwa kupitia Muswada huo kitawekwa kifungu maalum chini ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kitakachogharimiwa na Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vielelezo vya makosa ya jinai, majanga na masuala mengine yenye maslahi ya taifa ili kuwezesha utekelezaji wa jukumu hilo kwa ufanisi hali itakayosaidia utoaji wa haki katika vyombo vya maamuzi na kuleta utengamano katika jamii.

  Aidha, Muswada wa pili uliowasilishwa unahusu Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016 ambapo maoni na ushauri yaliyotolewa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii yaliyosawilishwa na Jasmin Tisekwa (Mb) kwa niaba ya Mwenyekiti wakamati hiyo Peter Serukamba amesema kuwa Muswada huo utasaidia kutungwa kwa sheria ambayo italeta tija kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

  Zaidi ya hayo, Jasmini amesema kuwa Muswada huo utasaidia wanataaluma ya Kemia kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja kwa kuzingatia taaluma hiyo kwani ina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta za elimu, kilimo, viwanda, sheria, afya, mazingira na jamii kwa ujumla wake. 

  Akisoma maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Waziri Kivuli wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ester Mtiko amepongeza jitihada zinazofanywa na wataalamu wa kemia katika sekta mbalimbali kwa kuwa wana wajibu mkubwa kwa maslahi ya taifa kwa ajili ya usalama na kuendeleza maarifa ya kisayansi.

  0 0

  Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Projestus Rubanzibwa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, kwenye kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.

  Amesisitiza kwamba Wakuu wa Vyuo vya vya Ukunga nchini wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba wanatoa mafunzo bora kwa wahitimu wa vyuo hivyo ili watakapohitimu masomo yao waweze kusaidia kutoa huduma bora afya.

  Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini, unatekelezwa na Shirika la Jhpiego kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakunga nchini Canada, Shirika la Amref, Serikari ya Canada, Taasisi ya Wakunga Tanzania na Wizara ya Afya nchini, lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa akina mama na mtoto ili kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi maeneo ya Vijijini nchini.

  Na BMG
  Kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dr.Silas Wambura, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, ambapo amesema mkoa wa Mwanza unakabiriwa na upungufu mkubwa wa idadi wa wakunga pamoja na vifaa tiba hali ambayo inasababisha kuwepo kwa vifo vya akina mama na watoto.
  Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha unaongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga maeneo ya Vijijini hapa nchini ambapo wahitimu wa masomo ya Sayansi katika maeneo hayo watakuwa wakipewa ufadhiri wa masomo kwa makubaliano ya kurudi kwenye maeneo yao ili kutoa huduma za afya. Mradi huo unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2021.
  Kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza ujuzi na idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella (wa kwanza kulia)  kwenye boti wakati alipoitembelea Bandari ya Tanga kuona utendaji wao  Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari wa Tanga Henry Arika

   Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika wa pili kutoka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia wakati alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi kwa ufanisi
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga bandari ya Tanga wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo

   Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akipanda ngazi kuelekea kwenye meli hiyo akifuatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kushoto akionyeshwa kitu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,(Ras) Mhandisi Zena Saidi wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo. 

  0 0
 • 09/09/16--09:44: CASTING YOUR VISION

 • 0 0

  Tunapoadhimisha miaka mitatu ya kumbukumbu ya kifo cha Mtoto wetu mpendwa FLORA FLOWIN MKANULA (pichani), ni vyema kumshukuru Mungu hasa kwa mapendo aliyotushirikisha na kutuachia kupitia maisha yake FLORA.  
  Tunaadhimisha Misa Takatifu kesho  tarehe 10/09/2016 saa 12.00 asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam.  
  Baada ya Misa tunazuru tulipomlaza mpendwa wetu Flora Mkanula Kinondoni kuyaenzi matendo yake mema.  
  Baada ya hapo tutaendelea kwa tafakari ya pamoja nyumbani kwa Wazazi wake Bw/Bibi F. Mkanula Yombo Vituka jijini Dar es salaam muda muafaka saa 7.00 mchana.
  Raha ya milele umpe ee Bwana.

older | 1 | .... | 1349 | 1350 | (Page 1351) | 1352 | 1353 | .... | 3272 | newer