Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 07/09/2016.


WADAU WALONGA WAIKUBALI HAPA KASI TU YA VODACOM.

$
0
0
 .Mteja wa Vodacom Tanzania, Suka Keba (kushoto) akitoa maoni yake kuhusiana na kasi ya intanenti ya mtandao wa kampuni hiyo unavyofanya kazi kwa kasi ya hali ya juu ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
 Mkazi wa Dar es Salaam, Innocent Mafuru (kushoto)  akihojiwa jana jijini na waandishi wa habari kutoka Clouds FM, Herry Mijinga kuhusiana na kasi ya intanenti ya mtandao wa kampuni hiyo unavyofanya kazi kwa kasi ya hali ya juu ukilinganisha na kipindi cha nyuma hususani tangu mtandao huo uzindue huduma ya 4G.

· Yawezesha kupakua nyimbo na picha mitandaoni fasta fasta
Kutokana na kuimarishwa zaidi kwa miundo mbinu inayotumiwa na Vodacom Tanzania kwenye huduma za intanenti kumewezesha wateja wake kufurahia huduma hii zaidi kwa matumizi mbalimbali nchini kote.

Moja ya  kundi ambalo linaendelea kufurahia matumizi  ya internet yenye kasi kubwa ni wapenzi wa muziki ambao hivi sasa wanaweza kupakua nyimbo  mitandaoni kwa kasi kubwa ikiwemo kuangalia picha za sinema kwa viwango vyenye ubora mkubwa.

Wakiongea wakati wa thathmini ya kasi na ubora wa mtandao wa Vodacom,Baadhi ya wateja walieleza kuwa hivi sasa wanaweza kupata huduma za internet kwa urahisi mahali popote na kwa wakati wowote. 

Mmoja wa wateja  Innocent Mafuru alisema kuwa akiwa mtumiaji wa mteja wa Vodacom anaweza kutumia interneti bila kupata usumbufu wowote kwa matumzi yake binafsi na matumizi yake ya  ofisini.

“Intanenti yenye kasi ya Vodacom inaniwezesha kuperuzi mitandao mbalimbali na kupakua nyaraka mbalimbali mitandaoni ikiwemo kupata  burudani za muziki na picha za sinema kutoka kwenye mitandao”.Alisema Mafuru.
Mteja mwingine Sunday John alisema kuwa interneti ya Vodacom ina kasi ya kuridhisha kwa matumizi mbalimbali ya  ofisini,kupata nyaraka kutoka mitandaoni , kutuma na kupokea nyaraka kwa kasi bila kusahau kupakua muziki na picha za sinema .

“Nimekuwa mtumiaji mzuri wa mtandao wa Vodacom na mar azote nimekuwa nikifurahia huduma zake za interneti”.Alisema.

Mtandao wa  interneti umeendea kwa asilimia 90% hivyo unawezesha idadi kubwa ya Tanzania kuufurahia kwa kupata burudani za muziki na picha kutoka mitandaoni kwa ubora na viwango vya kimataifa.

MTUHUMIWA HERMAN WAHEKE KERARYO ANATAFUTWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI.

$
0
0
ANATAFUTWA KWA TUHUMA ZA WIZI
Herman Waheke Keraryo anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kugushi nyaraka na Hundi ya fedha ya Kampuni ya La Kairo Investiment Ltd ya Jijini Mwanza na kuiba amefunguliwa Jalada (RB) MW/IR/5446/2016 MWANZA.

Mkurugenzi wa Kampuni ya La Kairo Investiment Ltd anawaomba wananchi wanaomfahamu na watakao muona mtu huyo hapo juu kwenye picha watoe taarifa haraka kwake au katika Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili kuwezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Zawadi nono ya fedha itatolewa kwa mtu ambaye atatoa taarifa itakayowezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Wasiliana kwa simu no. 0786 959 400/, 0783 778 778, 0684 005 000 au toa taarifa Kituo cha Polisi kilicho karibu nawe.

WAKIMBIZI 200,000 KUNUFAIKA NA MSAADA WA SERIKALI YA JAPAN.

$
0
0
Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida, akionyesha sehemu ya msaada uliotolewa na Serikali ya Japan  leo jijini Dar es Salaam, ukishuhudiwa na  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira.
Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira  akizungumza na waandishi wa habari wa kupokea msaada wa dola  za kimarekani milioni 1.8 kwa ajili ya kununulia chakula cha wakimbizi zaidi ya 200,000  ambapo msaada huo unakwenda shirika la lisilo la serikali leo jijini Dar es Salaam.

Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.
WAKIMBIZI zaidi 200,000 walio katika Mikoa ya Kasikazini na Magharibi nchini wapwa msaada wa chakula kilichogharimu Dola za Marekani Milioni  1.8 kutoka serikali ya Japan.

Msaada huo umeshudiwa na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira wakati wa mkabidhiano ya msaada kutoka kwa Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Tanzania.

Balozi wa Japan amesema kuwa msaada huo kwa serikali ya Tanzania  ni wa kiubinadamu wa kukubali kuwa na wakimbizi.
"Serikali ya Japan imefurahishwa na utoaji wa fedha hizo kwa ajili ya msaada wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Tanzania kutokana na wakimbizi kukosa chakula na hali ya duni ya lishe." 

Kwa juhudi ambazo zinafanywa ni kutaka kuboresha upatikanaji wa chakula kwa maisha ya wakimbizi waendelee kukaa kwa amani katika mikoa ya kaskazini na magharibi mwa Tanzania.

Amesema fedha hizo  ni sawa na bidhaa tani 1,800 ambazo zimetolewa na serikali ya Japan ikiwa ni virutubishi vya mafuta, pamoja na tani za mahindi 1,100 pia manunuzi ya vyakula vya virutubishi vya uji kwa ajili ya wakina mama na watoto walio katika hatari ya kupata utapiamlo.

MFUMUKO WA BEI UMEPUNGUA HADI ASILIAMIA 4.9.

$
0
0
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mwenendo wa Bei za Bidhaa mbalimbali hapa nchini.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo  kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Ruth Minja. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa Mwezi Agasti 2016  umepungua hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 ya ilivyokuwa mwezi Julai.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma na huduma kwa mwaka ulioshia mwezi Agasti 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi julai 2016.

Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.28  mwezi Agasti 2015 na mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Agasti 2015 umepungua hadi asilimia 7.0 kutoka asilimia 7.6  ilivyokuwa mwezi Julai mwezi 2016.

Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Agasti 2016 umechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Agasti 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Agasti mwezi 2015.

Mwenendo wa wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula ivinaonesha kupungua ni pamoja na bei ya samaki kwa asilimia 7.01 mafuta ya kupikia 7.02. na mbogamboga asilimia 6.9 

Amesema kuwa uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania kununua bidhaa na huduma umefikia sh. 96 na senti 92  ilivyokuwa mwezi julai 2016.

Mfumuko wa bei kwa nchi zingine za Afrika Mashariki, Kenya umepungua hadi asilimia 6.26  kutoka asilimia 6.39 mwezi Julai 2016, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 4.3 kutoka asilimia 5.1 mwezi Julai,2016 

INTRODUCING MICHEZO FORUMS

$
0
0

 

NI MSIMU MPYA WA SOKA. JISAJILI SASA KWENYE MICHEZOFORUMS.COM
KUTANA NA WATAALAM WA MICHEZO, CHANGIA MIJADALA KUHUSU MICHEZO NA WANAMICHEZO. UNGANA NA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA POPOTE WALIPO DUNIANI MJADILIANE, PATA HABARI NA KUTOA MAONI YENU. 
JE WEWE NI SHABIKI WA TIMU ZA ULAYA?  JIUNGE SASA NA MASHABIKI WENZAKO POPOTE WALIPO MUWEZE KUJADILI MICHEZO KWA KINA. 
JISAJILI SASA KWENYE MICHEZOFORUMS.COM. TUONGEE MICHEZO 



BASATA KUSHIRIKIANA NA MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw Godfrey L. Mngereza akizungumza katika kikao cha Mahusiano mema kati ya BASATA na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugeni wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure na Mratibu wa Program ya Museum Art Explosion Bw Edgar Chatanda wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa BASATA Bw Godfrey L. Mngereza (hayupo pichani)

Na SIXMUND J. BEGASHE - Makumbusho ya Taifa.

Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni imekutana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kufanya mazungumzo ya namna vyombo hivi viwili vya Serikali vitakavyo weza kudumisha mashirikiano katika shughuli za kila siku ili kuhifadhi na kuendeleza Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Mtendaji wa BASATA Bw Godfrey L. Mngereza ameipongeza Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kuanzisha Program ya kila mwisho wa mwezi “Museum Art Explosion” ili kutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kuosesha kazi zao za sanaa za Ufundi na za jukwaani kitu ambacho kinasaidia kukuza pato la msanii na pia kuutangaza Utamaduni wetu.

“Mashirikiano yetu BASATA na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam yatasaidia vyombo hivi hasa Makumbusho kufanya kazi za Sanaa na Utabaduni kwa usalama mkubwa kwa kuwa BASATA itasaidia kuwamulika wasanii wasio tambuliwa na Baraza ambao watataka kufanya maonesho kwenye Makumbusho yetu na hasa kwenye hii program ya Museum Art Explosion” Aliongeza Bw Mngereza.

Nae Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure, ameeleza kuwa mahusiano ya BASATA na Makumbusho hiyo ni ya kihistoria kwani BASATA ilihusika kwa kiasi kikubwa kwenye kutoa ushauri juu ujenzi wa mradi wa Nyumba ya Utamaduni na namna itakavyo tekeleza kazi zake za Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni Nchini.

“Japokuwa tunatekeleza kazi zetu za msingi kama Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kupitia program mbali mbali za sanaa na Utamaduni lakini tumeona ni vyema tukakutana na wenzetu wa BASATA ili watuongezee maarifa zaidi ya namna ya kuziboresha hizi program zetu hususani hii ya MUSEUM ART EXPLOSION maana wao ni wabobezi wa Sanaa na Utamaduni”. Alisema Bw Bufure

Kikao hicho kilicho udhuriwa na wajumbe wa tano kutoka Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na wanne kutoka BASATA kiliangazia mashirikiano katika nyaja ya Utoaji elimu kwa Wasanii, Mawasiliano, Utafiti na Maonesho ya kazi za Sanaa hivyo kamati ndogo ziliundwa ili zitoke na mapendekezo zaidi yatakayo wezesha vikao vya juu kupitia na kupitisha maamudhi sahii. Na SIXMUND J. BEGASHE Wa Makumbusho ya Taifa.

LEO NI LEO MISS ILALA 2016 JIJINI DAR

$
0
0
 Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.
**************

SHINDANO la Kumsaka Miss Ilala 2016 linafanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Mbali na kufanyika kwa shindano hilo pia litatumika kuadhimisha miaka 20 ya shindano la Miss Ilala tangu kuanza kufanyika kwake na warembo mbalimbali waliowahi kushiriki na kushinda taji hilo watahudhuria.

Mratibu wa shindano hilo, Erick Othman kutoka Kampuni ya Gogetime Enterprises ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa warembo 14 watapanda jukwaani kuwania taji hilo pamoja na tiketi ya kushiriki shindano la Kitaifa la Miss Tanzania 2016 linalotaraji kufanyika baadae mwaka huu.

Othman alisema mgeni rasmi katika shindano hilo leo hii ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, huku burudani ikitolewa na wasanii mbalimbali akiwepo Rubby.

Amewataja warembo wanaoshindana kuwania taji hilo kuwa ni Osmunda Mbeyela, Mercy Zephania, Melody Tryphone, Dalena David, Nuru Kondo, Julitha Kabete, Sporah Luhende, Queen Nazil, Lilian Omolo, Mariam Maabad, Brenda Allan, Sabrina Halifa, Agriphina Nathaniel na Grace Malikita.

Kwa upande wa zawadi za washindi, Kitundu alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh milioni moja pamoja na portable TV kutoka Startimes, huku mshindi wa pili akipata sh 700,000 na kingamuzi, na mshindi wa tatu akipata sh 300,000 na kingamuzi pia.

Alisema kuwa mshindi wan ne atapata sh 200,000 na watano atapata sh 150,000 pamoja na kingamuzi huku warembo wengine watapata kifuta jasho cha sh 50,000.

Kiingilio katika shindano hilo ni Sh 50,000 kawaida na Sh 100,000 kwa viti maalum (VIP).

Wadhamini ni Coca cola, Atsko, Darling, Channel 10, Kitwe General Traders, Uefa Goo, Mustafa Hassanali, Majira, High Spirit, StarTimes, Father Kidevu Blog na wengineo.
Washiriki wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha baada ya mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. warembo hao wanataraji kupanda jukwaani Septemba 9, 2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJIKITA KATIKA UFUGAJI KUKU

$
0
0
Image result for kuku wa mayai na nyama
Na Woinde Shizza, Arusha.

Wajasiriamali nchini wametakiwa kujikita katika Ufugaji wa kuku wa Kienyeji na kisasa ili waweze kunufaika kiuchumi kufuatia ongezeko la uhitaji mkubwa wa mayai na nyama katika maeneo ya mengi hususan kwa wafanyabiashara wa vyakula.

Hayo yameelezwa na Mjasiriamali Boniventura Shiyo anayejihusisha na ufugaji huo kuwa kwa sasa biashara hiyo imemuongezea kipato ambacho anakitumia kujiletea maendeleo pamoja na kuendesha familia pasipo kuyumba.

Mjasiriamali huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya uthubutu kwani soko la biashara ya kuku ni kubwa na linazidi kukua kila kukicha.

Hata hivyo Boniventura amesema kuwa kwa sasa anatumuia mashine maalumu ya inayototoa mayai na kuwa vifaranga maarufu kama incubator ambayo imemuongezea fursa ya kuwa muuzaji wa vifaranga pia.

Biashara ya ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zinazoshamiri kwa kasi katika maeneo mingi nchini hususan maeneo ya mijini ambapo ndipo masoko makubwa yanapatikana kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa bidhaa za mayai na nyama ya kuku.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 09.09.2016

Kumbukumbu ya Flora Flowin Mkanula

$
0
0
Tunapoadhimisha miaka mitatu ya kumbukumbu ya kifo cha Mtoto wetu mpendwa FLORA FLOWIN MKANULA, ni vyema kumshukuru Mungu hasa kwa mapendo aliyotushirikisha na kutuachia kupitia maisha yake FLORA. Tunaazimisha Misa Takatifu siku ya tarehe 10/09/2016 saa 12.00 asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam. Baada ya Misa tunazuru tulipomlaza mpendwa wetu Flora Mkanula Kinondoni kuyaenzi matendo yake mema. Baada ya hapo tutaendelea kwa tafakari ya pamoja nyumbani kwa Wazazi wake Bw/Bibi F. Mkanula Yombo Vituka muda muafaka saa 7.00 mchana. Raha ya milele umpe ee Bwana.

 "Ameen"

MBUNGE COSATO CHUMI AANZA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI.

$
0
0
Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akikagua pump kwenye moja ya kisima kwenye shule ya Msingi Makalala, anayetizama ni Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi
 Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akimsikiliza kwa makini Mhandisi wa Maji wa Mji wa Mafinga Eng Eradius.
 Pichani baadhi ya wanafunzi na waalimu wa shule ya Msingi Makalala wakiwa katika picha ya pamoja na Mrs Lee na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi


 Na Fredy Mgunda,iringa

MBUNGE wa jimbo Mafinga mjini Cosato Chumi ameendeleza juhudi zake za kuwatafutia maendeleo wananchi wa jimbo lake kwa kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali za nje ya nchi ya Tanzania pamoja na taasisi za ndani.

Hivi karibu balozi wa korea nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya Kutoka Korea ya World share  alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea changamoto za jimbo hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya changamoto hizo na walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.

Baada ya balozi huyo kurudi jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo ambazo alikuwa amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.

Aidha mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends InternationalBw Donsun Lee alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua kwa kuwa ameshazifanyia utafiti.

“Leo nimetembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga na nimejionea shida ya upatikanaji wa maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun Lee.

Bw Donsun Lee alimpongezambunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za kuwashawishi kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto  ambazo wanaweza kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.


Katika ziara hiyo Bw Lee na timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga.

Aidha baada ya tafiti hizo, Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya Serving Friends International huko Seoul, Korea.

Nia ya kufanya tafiti hizo ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa sababu ndo utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani Singida

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa kufanikisha kufanya tafiti ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na taasisi hiyo.

Chumi ameongeza kuwa haya ni matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea jimbo la Mafinga Mwezi mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.

Lakini mbunge Chumi amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma na kuunganisha na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi inayotakiwa.

“Unakuta mbunge nahangaika kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini ukienda vijiweni unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga soga zisizo na malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la mafinga mjini litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi

DED KISHAPU AWAFUNDA WATENDAJI WA KATA, VIJIJI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga amekutana na watendaji wa kata na vijiji wilayani humo.

Magoiga amewataka hao kuhakikisha wanawajibika katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali badala ya kuacha watu wanakwepa kutimiza wajibu wao.

Alisema watendaji wanapaswa kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa ikiwemo kulipa kodi na ushuru mbalimbali ili Serikali ipate mapato na kuweza kuwahudumia wananchi.

“Ukusanyaji mapato uwe ajenda muhimu na mtendaji ana uwezo wa kulisimamisha gari lenye mzigo wa mazazo mahali popote kwenye himaya yake na kuhakikisha limelipa kodi.

“Hakikisheni mageti yanafanya kazi ninyi ni walinzi wa amani katika kata zenu kwa hiyo sitaki kuona sheria zinakiukwa, tuache kufanya kazi kwa mazoea,” alisema.

Aidha, mkurugenzi huyo alionya tabia ya baadhi ya watendaji na watalaamu mbalimbali kushinda maofisini badala ya kuwatembelea na kuwahudumia wananchi.

Alisisitiza maofisini ni mahali pa vikao vya ndani tu na kuwa hatapenda kuona wananchi wakikosa huduma kutokana na kutofikiwa na watalaamu au watendaji.

Magoiga alitaka ushirikiano katika utendaji huku akikemea utoro katika vituo vya kazi na kwamba mtendaji anapaswa kuhakikisha watumishi wote ngazi ya kata wanakuwepo vituoni kwao.

“Utakuta mtumishi hayupo huku mtendaji kata hana taarifa yoyote hiyo ni kazi ya mazoea, kila siku nasema sitaki kazi za mazoea, tuwajibike kwa wananchi wetu,” alisisitiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (wa pili kushoto) akizungumza na watendaji wa kata na vijiji katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa halmashauri. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Utumishi na Utawala, Jumanne Chaula, Mwanasheria wa Wilaya, Wilson Nyamunda na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya, George Kessy.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na watendaji katika kikao hicho.
Watendaji wa kata na vijiji wa Kishapu wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji, Stephen Magoiga wakati wa kikao.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 17 WA DHARURA WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Immaculate Makilika
 na Abushehe Nondo - MAELEZO
WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kutumia kipindi cha miezi 3 hadi Januari mwakani ili kuupitia upya mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA) kabla ya kukubaliana na baadhi ya vipengele vya mkataba huo. 
 Akizungumza katika mkutano wa dharula wa 17 wa Jumuiya hiyo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema hatua hiyo imetokana na mjadala na majadiliano ya kina kutoka kwa Wakuu wa Jumuiya hiyo. 
 Rais Magufuli alisema kwa mujibu wa mkataba huo, Umoja wa Ulaya ulitaka mkataba huo usainiwe mwaka huu, ambapo hata hivyo kwa kuzingatia maslahi na ustawi wa jumuiya hiyo, viongozi wa nchi wanachama wamehitaji muda zaidi wa kufanya maamuzi juu ya mkataba huo. 
 Dkt. Magufuli alisema kufuatia uamuzi huo, Viongozi hao wameitaka Sekretarieti ya Jumuiya hiyo kuandaa utaratibu wa kusimamia masuala ya mahusiano kuhusu mkataba huo kwa kufanya mawasiliano na Umoja wa Ulaya.
 “Tumewaomba wenzetu wa Umoja wa Ulaya wasiiadhibu nchi ya Kenya kwa kuwashinikiza kusaini mkataba wa EPA ifikapo oktoba mosi mwaka huu, ni vyema nchi zote wanachama tujiridhishe na vipengele vya mkataba huo kabla ya kuweka saini ya makubaliano” alisema Rais Magufuli. 
 Akitolea mfano baadhi ya sababu zinazoifanya nchi za Jumuiya hiyo kuhitaji muda zaidi wa majadiliano kuhusu mkataba huo ni pamoja na uhakika wa kulinda viwanda vya ndani vya nchi wanachama, njia bora za kulinda maslahi ya wakulima, namna bora ya makusanyo ya kodi za bidhaa kutoka nchi za Ulaya. 
 Kwa upande wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema katika ulimwengu wa sasa suala la utengamano wa jumuiya unahitaji zaidi wingi wa watu na uwezo wa kujitosheleza kwa uzalishaji na masoko yatakayoyosaidia ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama. 
 “Mwaka 1960 idadi ya watu katika nchi za Afrika Mashariki ilikuwa na takribani watu Milioni 40 ukilinganisha na watu Milioni 165 waliopo sasa ambapo uwezo wa uzalishaji na masoko umeongezeka, hivyo hatuna budi kuwa na jumuiya yenye uwezo wa kuzalisha bidhaa kwa wingi na kutoa huduma” alisema Museveni. 
 Aidha Rais Museveni aliutaka Umoja wa Ulaya kukubaliana na uamuzi wa wakuu wa jumuiya hiyo kuwapa muda zaidi wa kufanya maamuzi kuhusu mkataba huo ambao umebeba maslahi mapana zaidi kwa wananchi wa jumuiya. 
 Naye Naibu Rais wa Kenya, William Ruto alisema maamuzi kuhusu mkataba huo yanalenga usawa na kuimarisha umoja baina ya nchi wanachama hivyo ili dhana hiyo iweze kwa wananchi ni wajibu wa Viongozi kuweka maslahi ya wananchi wao. 
 Katika mkutano huo, Wakuu wa Jumuiya hiyo walipokea ripoti mbalimbali ikiwemo ripoti ya mgogoro wa Burundi, ripoti ya mabaraza la mawaziri wa jumuiya hiyo kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini Sudan Kusini pamoja na uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli na viongozi wenzie wakisimama wakati wimbo wa Jumuiya ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Dharula wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Mkutano wa 17 wa Dharula wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa 17 wa Dharula wa Nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa 17 wa Dharula wa Nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wenzie baada ya Mkutano wa 17 wa Dharula wa Nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016.

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA KITUO CHA KUCHAKATA GESI

$
0
0
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba mkoani Mtwara wawe wazalendo na wafanye kazi kwa bidii katika kulinda na kuutunza uwekezaji huo mkubwa ambao serikali inautegemea katika uzalishaji wa nishati ya umeme wakati taifa linaelekea kwenye nchi ya viwanda.


Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na watendaji wa kiwanda hicho baada ya kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.


Amesema kiwanda cha kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa  kwa Taifa hivyo ni kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.


Makamu wa Rais pia amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwajali na kuwathamini katika utendaji wao wa kazi na kwamba serikali itahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho wanapewa motisha ya kutosha ili waongeze maradufu utendaji wao wa kazi ili malengo ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda inatimia kwa sababu taifa litakuwa na nishati ya umeme ya uhakika.


Makamu wa Rais amewataka watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC) ambalo linasimamia mradi huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kila mwaka ili wananchi waweze kuwa walinzi wa mitambo hiyo.
Akitoa maelezo mafupi ya mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata gesi ya futi za ujazo milioni 210 kwa siku.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akitembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba Mhandisi.Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na kusafirishwa kwa watumiaji
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.


Sereikali imeshalipa madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara - Prof. Ndalichako

$
0
0
Na: Frank Shija, MAELEZO

SERIKALI imewataka walimu wa shule za msingi na sekondari nchini kuwasilisha madai yao yasiyo kuwa ya Mishahara ikiwemo stahili za likizo ili waweze kulipwa madai hayo kwa wakati.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1).

Profesa Ndalichako alisema kuwa Madeni ya Walimu yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni madai yatokanayo na mishahara na yasiyokuwa ya mishahara ambayo yamekuwa yakilipwa na Serikali kupitia Wizara yake ambapo hadi hivi sasa hakuna mtumishi ambaye hajalipwa.

“Hakuna jalada la madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara na kama yapo madai walete ili walipwe kwani fedha zipo”. Alisema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya mishahara yamekuwa yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo nayo yamekuwa yakifanyika.

Kwa mujibu wa Profesa ndalichako alisema Serikali imekuwa ikipata ufadhili kutoka Serikali ya Sweden kwa ajili ya kusaidia katika kulipa stahili mbalimbali za walimu ili kuboresha weledi wa taaluma yao.

Kwa upande wa ubora wa Elimu, Ndalichako alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika sekta elimu, ubora wa Elimu ya Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia program mbalimbali zikiwemo za mpango wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Akitolea mfano Waziri Ndalichako alisema kuwa kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi za mpango wa UPE miaka ya 1970 ambao lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kujiunga na elimu ya msingi.

Waziri Ndalichako mwaka 2013 Serikali iliendelea kufanya maboresho kwa kuongeza sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu ili kupata walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo ufaulu wa daraja la tatu kwa wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa masomo mawili katika kidato cha sita.

“Serikali ilianzisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu ya msingi na mafunzo mwanafunzi atatakiwa atasoma darasa la kwanza hadi la 6 kwa msingi na mafunzo ni kuanzia darasa la 7 hadi la 12”.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBER 9, 2016.

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

$
0
0
 Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya  Idara ya Nishati katika kikao hicho.
Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka  Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi kutoka katika kampuni ya Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakiwa katika picha ya pamoja.

WAZIRI WA AFYA ALIAGIZA BARAZA LA FAMASIA KUHAKIKI VYETI VYA WAUZA DAWA.

$
0
0
* Aliagiza Baraza lifanye Operesheni ya kuhakiki Vyeti vya Wataalam wa Dawa (Wafamasia) nchi mzima ili kuthibiti Wauza Dawa Feki.

* Alitaka kuwafutia usajili wafamasia wanaouza Dawa za Serikali"

Na.Mwandishi Wetu - Dodoma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Famasia nchini kuanza kazi ya uhakiki wa vyeti vya wauza dawa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kudhibiti na kuwaondoa wauza Dawa wote wasio na sifa ya kufanya kazi  hiyo. 

Pia ameligiza Baraza hilo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kuwafutia usajili wafamasia wanaokiuka kanuni na taratibu za Baraza hilo ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya upotevu wa dawa, vifaa na Vifaa Tiba vya Serikali.

Mhe.Ummy aliyasema hayo jana mjini Dodoma katika Kikao Chake cha kwanza na Bodi ya Baraza la Wafamasia nchini ambapo pamoja na mambo mengine alikemea utaratibu ulojitokeza  hivi karibuni wa kutaka kuifanya biashara ya dawa kuwa sawa na biashara nyingine za kawaida za maduka ya kuuza nguo jambo ambalo halikubaliki.

"Biashara ya maduka ya dawa lazima iheshimiwe, lazima ianzishwe kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na watu wanaoajiliwa kuhudumia maduka ya dawa kuwa na sifa zinazotakiwa, kazi ya kuuza dawa za binadamu sio sawa na biashara ya kuuza nguo au viatu", alisema Mhe Ummy.

Ameliagiza  Baraza hilo kufanya operesheni nchi nzima  kukagua maduka yote ya dawa kubaini mapungufu yaliyopo kisha kuchukua hatua kali dhidi ya wale wataogundulika kufanya biashara hiyo bila kufuata taratibu na kuongeza kuwa baraza hilo ni lazima liendelee kupambana na watoa dawa wasio na sifa  na wale wasio waaminifu wanaotengeneza vyeti bandia vya Wataalam wa Famasi.

Pia ametoa maelekezo kwa baraza hilo  kuangalia suala la mgongano wa maslahi hasa pale ambapo Mfamasia wa Wilaya anatuhumiwa kumiliki maduka ya Dawa mawili hadi matatu ndani ya Halmashauri anayofanyia kazi.

"Ni lazima suala hili tulitafutue suluhish nimefanya ziara mikoani jambo hili nimelikuta, mimi sielewi na Wananchi wengi hawaelewi pale Mfamasia wa Wilaya anapokua na maduka ya dawa hadi matatu  na muda wote yana dawa wakati dawa hizo hizo hazipatikani katika vituo na Hospitali za Serikal, Kwa nini wananchi wasiwe na hisia kuwa dawa zile ni za Serikali? Baraza nileteeni mapendekezo ya kutatua hili. Alisisitiza Mhe Ummy.

Aidha,  ameliagiza Baraza hilo kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili nchi iwe na wanataaluma wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu.

Akitoa Taarifa ya Utendaji Msajili wa Baraza la Famasia Bi.Elizabeth Shekalaghe alieleza kuwa zipo changamoto wànazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo maduka mengi ya kuuza dawa kuendesha biashara hiyo bila ya kuwa na vibali vya biashaa pia kuwepo kwa wauza dawa wasio na sifa ya kufanya shuguli hiyo. 

Pia alieleza mikakati iliyowekwa na barza hilo ili kuhakisha changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi ili kuhakikisha huduma za uuzaji dawa zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu ili kuhakikisha unora wa huduma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Bàraza là Famasia, Legu Ramadhani Mhangwa, amesema kuwa Baraza hilo limekuwa likifanya kazi zake  kwa kuzingatia sheria ili kufikia malengo liliyojiwekea na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa na Mhe Waziri pia kutatua changamoto ya  uwepo wa vyuo binafsi vinavyofundisha taaluma ya famasi kutokidhi viwango pamoja na nia ya serikali ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kada za dawa nchini. 

Pia Baraza hilo limeahidi kushughulikia uhaba wa wakufunzi mahususi katika vyuo vinavyofundisha kada za famasi katika ngazi ya cheti na diploma.

Kuhusu Mgongano wa maslahi kwa watumishi wakiwemo watendaji wa Halmashauri na wale wanaosimamia na kutekeleza kazi za baraza katika ngazi za mikoa na halmashauri, Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Baraza litahakikisha linasimamia kikamilifu Kanuni za Maadili na Miiko ya Kitaalamu za 2015 ili kutatua changamoto hizo iliwemo upotevu wa dawa za Serikali.

BREAKING NEWZZZZZ:MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN WAPATA AJALI MKOANI MTWARA,WANNE WAJERUHIWA

$
0
0
Moja ya Gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Sukuhu Hassan,namna lilivyo haribika mara baada ya Kuacha njia na kupinduka.

 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu Rais.
Majeruhi wa ajali wakipata msaada wa  huduma ya kwanza mara baada ya gari walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images