Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1344 | 1345 | (Page 1346) | 1347 | 1348 | .... | 3283 | newer

  0 0


  0 0


   Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi akiongea na Watanzania wa North Carolina siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika ukumbi wa hoteli ya Comfort Suites jijini Durham, North Carolina. Katika hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwaasa wanaUTNC kupendana na kushikamana na kusaidiana kuonyeshana njia za mafanikio badala ya kukalia majungu na kuchukia maendeleo ya mwenzako. Mwenzako anapofanya vizuri mpe sifa yake na muulize amefikaje hapo na yeye akusaidie ufikie hapo alipo.

  Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwasisitizia Watanzania wa North Carolina wajenge desturi ya kuwekeza nyumbani na kuwaelekeza jinsi ya kufungua akanti za akiba kwenye benki za Tanzania ili ziweze kuwasaidia kwa siku za usoni kwa maendeleo yao nchi Tanzania kwa kuwezesha kununua kiwanja na hatimae kujijengea kibanda.

  Mhe. Wilson Masilingi aliwasisitizia wanajumuiya hao kutafuta wawekezaji watakaoingia nao ubia na wahakikishe hawaingii mikataba na watu wa kati na yeye kwa kutumia ofisi ya Ubalozi ameahidi kuwasaidia ili kuwaondolea wawekezaji usumbufu unaoweza kujitokeza pindi wanapoamua kujifanyia wenyewe kwani wanaweza kuangukia kwenye mikono isioitakia mema Tanzania.

  Mhe. Balozi aliwaachia uongozi wa Jumuiya hiyo ya Umoja wa Watanzania North Carolina wito wa kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kuchangia madawati na Mwenyekiti mstaafu awamu ya tatu, Bwn. Geofrey Lepana aliitikia wito huo kwa kuchanga dola 80 pesa taslimu papo hapo kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi na yeye kuukabidhi mchango huo kwa mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex na yeye kuahidi kwa niaba ya uongozi wake kuufanyia kazi wito huo.
  Afisa Ubalozi Bwn. Abbas Missana akifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
  Bwn. Nassoro Basalama, mwenyekiti mstaafu akidadavua historia ya jumuiya hiyo kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
   Mwenyekiti mstaafu Geofrey Lepana akipena mikono na Mhe. Balozi Wilson Masilingi mara baada ya kuchangia dola 80 kwa ajili ya madawati.
  Mhe. Balozi Wilson Masilingi akimkabidhi mchango huo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.


  0 0


  CALL FOR PAPERS
  Statistics has wide application in different fields of human activity. It has a significant role in different disciplines like banking, astronomy, business, management, insurance, health and in increasing human’s thinking. With the intention of further embellishing the knowledge of statistics, the department of Statistics, The University of Dodoma, is proud to proceed with the institution of excellence by organizing “The 1st Statistical Conference” on 17th and 18th of November, 2016.  This conference will assemble statisticians from different disciplines and statistic users especially in the public and private sectors to tackle real world problems.


  Applications are invited to papers which focus on statistical methodology in any professional. You are warmly invited to participate in the conference. You can participate in the conference as a listener or presenter. Proceedings of papers will be available. Various deadlines are as follows:


  Application and submitting abstracts

  Sept. 25, 2016

  Notification of successful abstract for presentation and listeners

  Sept. 30, 2016

  Submission of full paper

  October 20, 2016

  Participation Fee Payment

  October 20, 2016


  Participation Fee is Tsh 100,000/= for Tanzanians and $ 100 for others. Students are waived to Tsh 40,000/=. The amount paid will cover conference materials, meals, refreshments and certificate of attendance. All payments should be done through; Account Name: College of Natural and Mathematical Sciences; Account no: 0150221567000 – CRDB.


  Venue: College of Informatics and Virtual Education, Tanzania

   Contact: P. O. Box 338, Dodoma

    (+) 255 718 177 818 or (+) 255 717 999 012


  0 0
  SIMU.tv: Naibu Spika wa bunge Dkt. Tulia Akson ataka wizara na kamati za kisekta zishirikishwe katika mafunzo ya bajeti; https://youtu.be/7QdpdfnQCoQ
   SIMU.tv: Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya sekondari Longido mkoani Arusha waiomba serikali msaada wa vifaa vya kukinga ngozi zao;https://youtu.be/XBnctM5_ovk
   SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia  Jeneral mstaafu Emmanuel Maganga amesema serikali itafanya uchunguzi juu ya vifo vya watoto 7 walioteketea kwa moto ;https://youtu.be/ThRCj-3CRTI
   SIMU.tv: Serikali mkoani Lindi yapiga marufuku manunuzi ya Korosho kwa kangomba ili kuwawezesha wakulima kunufaika na kilimo cha korosho;https://youtu.be/3l3MbplGEso
   SIMU.tv: Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yatenga eneo la kibiashara la kariakoo la jijini Dar es Salaam kuwa mkoa maalum wa kodi; https://youtu.be/gfh_bgY6sU0
   SIMU.tv: Wafanyabiashara wa soko la Tarakea wilayani Rombo mkaoni Kilimanjaro wasusia kufanyabiashara katika soko hilo kutokana na kuwa chini ya kiwango;https://youtu.be/iYiIJUdtkcI
   SIMU.tv: Jeshi la kujenga taifa JKT lawataka wahitimu wa mafunzo ya JKT mkoani Kigoma kuwa mstari mbele katika kudumisha maadili; https://youtu.be/PA_dj662mlc
   SIMU.tv: Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wampongeza Rais Magufuli kwa kutoa hotuba safi inayosadifu hali ya maisha ya watanzania; https://youtu.be/R6dag5B_X2I
   SIMU.tv: Chama Cha Mapinduzi CCM kimesema hotuba za Rais Magufuli alizozitoa wakati wa ziara yake visiwani Zanzibar ni dira ya kuelekea Tanzania ya viwanda;https://youtu.be/UEWTtg8iB24
   SIMU.tv: Timu ya stand united imeibuka kidedea  katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuitandika Toto African goli moja kwa sifuri:https://youtu.be/rkz0X0HZPow
   SIMU.tv: Baadhi ya vilabu hapa nchini vitalazimika kubadilisha  mifumo yao ya uendeshaji kutoka sports klabu na kuwa football klabu: https://youtu.be/pYyqpNB86C8
   SIMU.tv: Kocha wa timu ya soka ya  wanawake Tanzania bara, amesema timu yake ipo tayari  kwa michuano ya challenge itakayofanyika nchini Uganda; https://youtu.be/JBN-2ucPugQ

  0 0

   Ally Masoud  maarufu kwa jina la Kipanya akiwa katika kijiji na Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus wakijadili jambo wakati wakiwangoja washiriki wa shindano hilo hapo jana ambapo pia ilikuwa ikirushwa live na kituo cha Luninga cha AZAM TWO chaneli 102
   Masoud Kipanya akiwapa maelekezo washiriki wa Shindano la Maisha Plus kabla hawajafugua rasmi vitambaa na kujua wapo wapi
   Hivi ni Baadhi ya Vifaa na vitu ambavyo vijana wa Maisha Plus watakuwa wakivitumia kipindi wapo kijijini kwa Muda wa Wiki8
   Masoud Kipanya akitoa msisitizo wa Jambo kwa washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tano.
  Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelezo ya kina kwa washiriki wa shindano hilo ambao wanatoka katika Nchi 5 Afrika Mashariki jinsi gani wataishi, watakavyojenga nyumba zao na watakavyo ishi katika kijiji cha Maisha Plus
  Wakiwa wanaleta mizigo yao ndani ya Kijiji cha Maisha Plus

  MAISHA PLUS EAST AFRICA 2016 itakuwa ikionyeshwa na AZAM Two Chaneli 102 
  #HapaKaziTuu
  #VijanaNdioNgazi

  KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kliniki mpya za Shirika hilo zijulikanazo kama “Trust community maternity homes”. Kliniki hizo mpya ni maalumu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam.
  Meneja Masoko wa DKT International Tanzania Sialouise Shayo akionyesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.
   Mkunga kutoka DKT International Tanzania Adella Hugo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango. 


  SHIRIKA lisilo la kiserikali la DKT International Tanzania limezindua mfano wa Kliniki mpya ziitwazo “Trust community maternity homes kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kawaida zinazoendeshwa na wakunga mbalimbali.

  “Trust Community Maternity Homes” – Ni kliniki zinazojitosheleza zilizotengenezwa kwa ubunifu kwa kutumia kontena ya kusafirishia mizigo, kliniki hizi zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu.

  Kiliniki za “Trust Community Maternity Homes”  zilizinduliwa kwa umma  wakati wa uzinduzi wa kliniki ya “Trust Health & Wellness Clinic “ ya Dar Es Salaam na ofisi  mpya za DKT International Tanzania  mnamo tarehe mbili September, 2016

  “Kila mwaka, wanawake milioni moja hapa Tanzania ambao hawakukusudia kupata ujauzito hupata ujauzito” alisema mkurugenzi mkuu wa DKT international, Raphael da Silva.

  “Hali hii si tu kuwa ina athiri wanawake hawa kifedha, afya zao binafsi na hali ya kiuchumi ya familia zao, lakini pia zinapelekea kuongeza uhitaji wa Serikali kutoa huduma za kiafya pamoja na elimu kwa watoto hawa .Kama tunaweza kufanikisha kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu za afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa jamii katika miji midogo na wanajamii ambao hawapati huduma hizi kiurahisi, tutafanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake hawa” alisema.

  “Trust Community Maternity Homes ni kliniki zinazojitosheleza ndani ya kontena la kusafirishia mizigo, zinazoendeshwa na wakunga wataalamu na wenye uzoefu wa muda mrefu kama washirika chini ya kliniki mama za “Trust health and wellness clinics” .  Alisema meneja mradi, Karoli Mango.

  “Kliniki hizi zinatoa ubora ule ule wa huduma , usiri na msaada  sawa sawa na Kliniki zetu nyingine za Trust  zinazopatikana mikoani hapa nchini .Kliniki yetu ya kwanza ya “ Trust community maternity homes” ya mjini  Kahama iko katika hatua za mwisho za  maandalizi kabla ya ufunguzi” aliongeza.

  Trust ina mpango wa kuingia mikataba yenye masharti mepesi na wakunga wazoefu ambayo itawawezesha kukodisha na baadae kuzi miliki kliniki hizi.  Wakunga wanaotoa huduma hizi watatumia kliniki hizi ambazo ziko ndani ya kontena ambazo zinatumia umeme wa sola , zenye uwezo wa kutoa huduma kamili za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pamoja na huduma nyingine za afya kwa jamii. Wakunga hawa watajipatia kipato kwa kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa katika kliniki hizi. 

  Kwa sasa , kuna “ Trust health and wellness  clinic” nne  ambazo ziko Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya and Mwanza  na pia kuna kliniki  na hospitali washirika  30  ambazo zinatoa huduma kwa kutumia chapa ya Trust. 

  Kliniki ya Msasani peninsula ya Dar Es Salaam ilifunguliwa mapema mwezi Julai.

  0 0

   Walimu wa Home Gym wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 18 kwa pamoja katika sherehe zilizofanyika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki.
   Keki maalum
  Wanachama wa Home Gym Wakiwa katika mazoezi mbalimbali

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MKURUGENZI wa Kituo cha kufanyia mazoezi ya viungo Home Gym, Andrew Mangomango amesema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho ya miaka 18 toka kuanzishwa kwake yatazunguka katika baadhi ya mikoa.

  Akizungumza wakati wa maadhimishi hayo yaliyifanyika Katika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki, Mangomango amesema kuwa ndani ya miaka 18 ameweza kupata wanachama wa kudumu takribani 200 na ameweza kuwasaidia watu mbalimbali kufahamu jinsi gani ya kufanya mazoezi.

  Mangomango amesema kuwa, maadhimisho haya ni ya tano mfululizo na kwa mwaka wameamua kutembelea baadhi ya mikoa ikiwemo Tanga, Arusha na Mwanza ambapo baadhi ya wanachama wake wa siku nyingi wapo kule na watatumia fursa hiyo kuhamasisha watu mbalimbali kufanya mazoezi kwa afya.

  "Na katika kuendeleza michezo, Kituo cha Home Gym kimeweza kutoa walimu takribani nane ambao wote wameshafungua Gym zao mikoa mbalimbali, hii ni moja ya mafanikio tuliyoyapata na zaidi bado tunashirikiana nao na hata leo kwenye maadhimisho haya wapo wote wamekuja kuunga mkono jitihada za Home Gym,"amesema Mangomango.

  Katika maadhimisho yaliyohudhuriwa na baadhi ya wadau wa michezo ikiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajura, waandishi wa habari mbalimbali na taasisi zingine wameonyesha muitikio mkubwa wa kufanya mazoezi na kuhamasisha watu wajitokeze kwani Michezo ni Afya.

  Kwa mwaka huu, Mangomango amesema kuwa mwaka huu watafanya maadhimisho yao sambamba na Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, mkoani Arusha.

  0 0

  Anitha Jonas – WHUSM.
  MUSWADA wa Huduma za Vyombo vya Habari  kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni  Septemba hii na  kujadiliwa  Desemba Mwaka huu.

  Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na  TBC 1,chenye lengo la Mawaziri kueleza umma namna wanavyotekeleza majukumu.

  “Muswada huu mzuri na utasaida kuleta suluhishi la malalamiko ya kuwepo kwa sheria kandamizi,pia itasaidia kukuza tansia ya habari pamoja na kuifanya tasnia ya habari kuheshimiwa kama tansia nyingine”,alisema Waziri Nnauye.

  Waziri Nnauye alisisitiza kuwa uandaaji wa Muswada  ulishirikisha wadau mbalimbali na kuzingatia maoni yao na serikali itaendelea kupokea maoni ya wadau  hata mara baada ya kusomwa kwake.
  Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya habari nchini  kupitishwa kwa Muswada huo kutasaidia kutoa suluhisho la kuwepo na changamoto katika sekta ya utangazaji ambayo kwa sasa inaonekana kupoteza mulekeo.

  Aidha,Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inataka kuipeleka  tansia  ya habari mbali  na kupitia Muswada huo utasaidia kufanikisha hilo kwani umeeleza kuwa mwandishi anahitajika kuwa na digrii na hii ni kwalengo la kuweka heshima ya taaluma kama ilivyokwa taaluma nyingine mfano sheria.
  Halikadhalika Waziri huyo alizungumzia kuwepo na changamoto  katika Sheria ya Utangazaji kwani imekuwa haionyeshi  Mtangazaji anaporusha kipindi hewani kilicho kinyume na maadili ni adhabu gani apewe.

  “Tungependa sheria ijayo iweze kumbana mwandishi pale anapokosa maadili na kumchukulia hatua kama ilivyo kwa tansia nyingine kama uhandisi na sheria kufikia hatua kufutiwa utoaji wa huduma hiyo”,alisisitiza Mhe.Nnauye.

  Akizungumza  kuhusu changamoto ya upatikanaji  wa taarifa kutoka kwa wasemaji wa taasisi za Serikali Waziri Nape alisema tayari ametoa agizo kwa watendaji kuwashirikisha wasemaji katika vikao vya maamuzi ili waweze kuwa na taarifa za pamoja na kuwapa nafasi ya kusema ikiwa na sehemu ya kazi yao.

  Hata hivyo Mheshimiwa Waziri ameliahidi Shirika la Utangazaji nchi kulisaidia kutatua changamoto zinazolikabili ikiwemo uhaba wa vifaa,pamoja na kuboresha maslai ya watumishi wake.Pia ameeleza  Bodi mpya ya TBC 1 iliyoundwa  imepitia  mkataba wa TBC 1 na STARTIMES  kwa lengo la kutaka kuiboreshea mazingira shirika hilo na tayari imekwisha maliza kazi na kuwasilisha mapendekezo.

  0 0

   Mama Hatia na wanae, wajukuu na vitukuu
   Watoto wa marehemu mzee Isaya Innocent Hatia tumempoteza mpendwa mama yetu mpendwa Mwalimu Agnes Ndembo Hatia kilichotokea hospitali ya Regency  jana jumamamosi mchana. Mama yetu alikuwa nguzo pekee iliobakia nasi baada ya kufariki baba yetu Mzee Isaya Innocent Hatia mwaka 2011. Tunamshukuru Mungu sana kwa upendo wake kwa mama yetu aliempa nguvu ya kuishi miaka tisini na sasa amempenda zaid mama yetu, bibi yetu na amempumzisha usingizi 

  wa milele na milele Ameni

  Mwalimu Agnes Ndembo Hatia amefundisha watu wengi sana darasa la kwanza
  tangia miaka ya hamsini hadi alipostaafu Tabora, Uhuru shule yamsingi.
  Mama, ametuacha watoto wake Christina wa USA, Geofrey wa Namibia, Mwl Mark Hatia wa Tambaza shule ya secondary, Bernadetta wa Dar, Isaya wa Finland, Costancia wa Kibaha, na Oscar mdogo wetu wa mwisho. Ameacha wajukuu, na vitukuu wengi ambao ni watoto na wajukuu zetu sisi watoto wake pamoja na dada
  zetu marehemu Joyce Hatia na Mwalimu Cecilia Hatia. 
  Picha zinaonyesha mama Hatia mwaka 1966 akiwa na Constacia ambae picha yake pembeni ni Costancia alivyo sasa, na zingine ni
  Kwa taarifa za maandalizi na ratiba piga simu zifuatazo. 0653 763 201 Kilian Kamota,
  0755 333 948 Dick Hatia, 0788 627 430 Ibra Yunus, na 0763 833 893 Solmon.
   BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. TUMSIFU YESU KRISTO: AMEN  Mama Hatia mwaka 1966 akiwa na Constacia ambae picha yake pembeni ni Costancia
  alivyo sasa,


  0 0


  Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akikagua moja ya Timu hizo katika Bonanza hilo.
  Moja ya timu ikiwa imefungwa goli la kizembe huku goli kipa asijue cha kufanya na wachezaji wengine kukimbia kwa ajili ya kujipanga zaidi.
  Mpira ukiendelea huku watu mbalimbali wakifuatilia Burudani hiyo kwa makini.
  Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua ofa maalumu kwa wateja wanaotumia mtandao wa simu za Mkononi wa Zantel ofa ya shinda mbuzi, pamoja na kutoa mbuzi kwa Vituo 50 vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini National Childrens Home, Silas Kusewa Kurasini jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Tanzania Mitindo House Klichopo Kiamboni, Khadija Mwanamboka mara baada ya Mkurugenzi huyo kuzindua Ofa maalumu kwa wateja wake ya shinda mbuzi.

  KAMPUNI ya Simu za Mkononi Zantel imezindua Kampeni ya Jibwage na Mbuzi katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Adha, ikitambulika pia kama 'Sherehe ya Kuchinja' kwa kutoa mbuzi 500 kwa wateja wake wenye matumizi ya  zaidi huku mbuzi 100 wakigawiwa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema "Hii ni sehemu ya kuwashukuru wateja wetu na kusherehekea pamoja nao Sikukuu ya Idd. Imekuwa ni utamaduni wetu kurudisha katika jamii kupitia kampeni na miradi mbalimbali, hivyo kwa leo Zantel inatoa mbuzi 500 katika kusherehekea Sikukuu hii ya Kuchinja.”

  Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

  Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

   “Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” alisema  Benoit

  Mbuzi 100 wanaobaki watatolewa msaada kwa  vituo vya watoto yatima vilivyochaguliwa katika mikoa mbalimbali. 

  “ Pia tunatumia nafasi hiyo hiyo kusaidia watoto yatima na wale wasioweza kufanikisha sadaka hii ya kuchinja ili nao wafurahi pamoja na wengine na kushiriki upendo unaotokana na Idd”,  ameongeza.

  Miongoni mwa miradi ambayo Zantel imetoa misaada ni mradi wa kina mama wanaozalisha zao la mwani Unguja, huduma za maktaba Zanzibar –Zanzibar Library Services, vile vile kompyuta na internet ya bure kwa kikundi cha wasanii cha Mkubwa na Wanawe na vituo mbali mbali vya walimu Zanzibar.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akiongea wakati wa kuchezesha droo ya fainali za taifa ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake TFF Amina Karuma na katikati Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi. Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi.
   Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa. Katikati ni Mkurungenzi wa Ufundi TFF na kulia Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jana Matinde.
  Mkurungenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma.

  TIMU za soka za wasichana za Lindi na Arusha zimepangwa kukutana katika mechi ya fungua dimba ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Statrs ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam, Jumanne, Septemba 6, 2016.

  Mashindano hayo yanayojumuisha timu za wasichana na wavulana yatafunguliwa rasmi siku hiyo ya Jumanne mchana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambaye atashuhudia mechi ngumu ya wavulana kati ya Mwanza na Ilala.

  Timu nyingine zinazoshiriki katika michuano hiyo yenye lengo la kuibua vipaji ni Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha, Mbeya, Lindi na Zanzibar. Tayari timu zimeshawasili na kupiga kambi katika shule ya Filbert Bayi iliyoko Kibaha.

  Akizungumza wakati wa hafla ya kupanga makundi iliyofanyika katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Mkurungenzi wa Ufundi Mwalimu Salum Madadi alisema kuwa maandalizi yote ya mashindano hayo ngazi ya taifa yamekamilika.

  Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na mkurengenzi wa maendeleo ya soka la wanawake nchini Bi Amina Karuma ambaye aliyaelezea mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa ni chemchem ya wanasoka chipukizi wasichana kwa wavulana.

  “Mashindano ya Airtel Rising Stars yametusaidia kupata wachezaji wenye vipaji vya ajabu ambao wanaunda timu za Serengeti Boys na timu ya taifa ya wanawake yaani Twiga Stars”, alisema na kuwashukuru Airtel Tanzania kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo.

  Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Matinde.

  Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa inatarajia kufikia tamati siku ya Jumapili, Septemba 11, 2016 ambapo bingwa kwa upande wa wasichana na wavulana watapatikana na kukanidhiwa vikombe vya ubingwa.

  Vilevile TFF itatangaza wachezaji nyota kwa wasichana na wavulana wataochaguliwa kuunda timu ya Airtel Rising Stars mwaka 2016.

  0 0
  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Kamana Stanley akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kutekelezwa kwa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 inayolenga kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo Sheiba Bullu.


  Na. Fatma Salum – Dar es salaam.

  Serikali imeanza kutekeleza Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016) ili kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Kamana Stanley wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.

  Stanley amesema kuwa  kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali wanayoshuhudia yakitendeka. Vilevile itarahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa za uhalifu kwani sasa taarifa hizo zitatolewa na kupokelewa sio tu kwenye vyombo vya dola pekee bali pia kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine vinavyobainishwa katika sheria hiyo.

  “Wananchi wasiwe na woga kujitokeza kutoa taarifa za uhalifu na matendo ya aina zote yanayofanywa kinyume cha sheria kwani taarifa hizo zitakuwa siri na zitafanyiwa kazi bila ya kuwataja watoa taarifa. Pia mashahidi wanapotakiwa kufika mahakamani wasiogope kwani sheria hii inawalinda” amesema Stanley. 

  Amefafanua kuwa wahusika watakaoshindwa kushughulikia vyema taarifa zinazotolewa kwao na kuruhusu watoa taarifa na mashahidi kupata madhara, sheria hiyo imeweka utaratibu wa namna ya kushughulika nao.

  Aidha, Stanley ameeleza kuwa katika sheria hiyo wale ambao taarifa zao zitafanikisha kuokoa mali ya umma, kupatikana kwa wahalifu na kulinda mazingira na maisha ya binadamu kutokana na uhalifu uliopangwa kufanyika, wamewekewa utaratibu wa kupatiwa motisha ikiwa ni pamoja na kuwafidia wale ambao wataathirika kutokana na taarifa walizotoa.

  Stanley ameongeza kuwa Serikali inatarajia kwamba kutungwa kwa sheria hii kutaleta matokeo chanya katika kupambana na uhalifu wa aina zote hivyo kukuza ari ya wananchi kusimamia wenyewe juhudi za kujiletea maendeleo.

  “Masuala ya usimamizi wa utawala wa sheria yataimarika kutokana na kuwepo kwa utayari wa wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kufika katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi. Pia ushiriki wao katika kufichua maovu yakiwemo yanayosababisha hasara kwa taifa utasaidia kuinua uchumi ukizingatia kwamba sasahivi Serikali inapambana sana na mafisadi” ameeleza Stanley.

  Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016)imeanza rasmi kutumika Julai Mosi mwaka huu baada ya kuidhinishwa na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

  0 0

    Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza wakati wa hafla iliyowakutanisha Baraza la Madiwani na Uongozi wa Ashanti United iliyofanyika mwishoni mwa wiki na kuisaidia timu hiyo kurejea ligi na itakuwa chini ya Manispaa ya Ilala                      
   Kulia ni Diwani wa kata ya Ilala, Saadi Khimji na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United Almas Kasongo.
   Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United United Almas Kasongo akizungumza na kueleza changamoto walizokuwa nazo katika kuendesha timu na kumshukuru Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko(kulia) kwa hatua nzuri waliyoifikia ya kuamua kuisaidia timu yao.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kayeko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu ya Ashanti jijini Dar es Salaam.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko ameitaka klabu ya Ashanti kuhakikisha wanarejea ligi kuu kwani kwa sasa wapo nao bega kwa bega.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala kuona umuhimu wa kuwa na timu na sasa Ashanti itakuwa chini ya Manispaa na wataisimamia kwa hali na mali.

  Akizungumza na Viongozi wa Ashanti pamoja na Baraza la Madiwani,  .Charles Kuyeko amesema Ashanti ni timu kubwa kwani ina muda mrefu sana na imeweza kuhimili kujiendesha kwa fedha chache za wanachama na zimekuwa hazitoshelezi kulingana na bajeti yao ya kila mwaka.

  Kuyeko amesema kuwa kuna timu nyingi sana zinazosimamiwa na Manispaa na zimekuwa zikifa ya vizuri na zaidi ukiangalia kwa timu za Ilala zinazoshiriki  ligi daraja la Kwanza ukiacha Simba na Yanga zilizowafuata kuhitaji msaada wao zaidi ya Ashanti na baraza zima la madiwani wameahidi kushirikiana nao kwa hali na mali.

  Kwa niaba ya uongozi wa Ashanti United, Makamu Mwenyekiti Almas Kasongo amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa bashasha kubwa sana hasa ukifikiria walikuwa na upungufu wa bajeti ya 2016/2017 ya takribani milioni 75, na zaidi ukiachilia hilo uwepo wa Baraza la Madiwani katika timu yao ya Ashanti utaleta hamasa kubwa sana kwa watu wengine kujitokeza kuja kuisaidia.

  Ashanti United imeweza kuwakutanisha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala takribani 30 na wote wameonyesha nia ya kuiunga mkono timu hiyo na kwa kuanzia kwenye hafla hiyo, Mstahiki Meya alitangaza kuanza na Milioni tano lakini watakapokutana tena watasema ni kiasi gani watakitoa na watakapokuwa na shida wasisite kupiga hodi kwake.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba akiongea na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt. Balozi huyo aliambatana na Kamati ya Mazingira na Kilimo ya   Bunge la Sweden.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (Kulia) akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Mazingira na Kilimo kutoka  Sweden walipomtembelea Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jjijni Dar es Salaam leo.
  Sehemu ya wabunge kutoka Sweden wakifuatilia mazungumzo baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba. Ujumbe huo wa Wabunge ulimtembelea Mh. Waziri na kujadili masuala ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

  0 0


  0 0


   Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa  kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.
  baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.

  Na Fredy Mgunda, Ileje

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje, Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.

  Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.

  Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

  Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

  “Nawatahadharishakwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo, kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na sipo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu yenu”alisisitizaMnasi.

  “hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo nawataka wasimamizi wote kufanya kazi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu, pia nawaasa ndugu zangu kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisemaMnasi.

  Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.

  Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichopo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

  Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.

  mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi,Zainab Telack akikata utepe kuashiria kupokea madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia.

  Na Dixon Busagaga, Shinyanga.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amekabidhiwa madawati 2,000 yenye thamani ya Shilingi 240,800,000/= na Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Makabidhiano yamefanyika leo mjini Kahama.

  Akimkabidhi madawati hayo Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, “hii ni awamu ya nne kwa mgodi wa Acacia Bulyanhulu kukabidhi madawati ndani ya mwaka huu katika kipindi ambacho taifa linaendelea kutekeleza kampeni ya kitaifa ya dawati kwa kila mwanafunzi iliyoagizwa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa lengo la kuboresha mazingira ya elimu nchini Tanzania.”

  Ameongeza kuwa, “licha ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kuchangia madawati pia inachangia miradi mingine kwenye jamii lakini kwenye sekta ya elimu mgodi unashirikiana na jamii kuitekeleza miradi kama vile ujenzi na ukarabati wa nyumba, ofisi za walimu madarasa, maabara za sayansi na udhamini wa masomo kwa wanafunzi.”

  Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi Zainab Telack amesema, “ Tukio hili la kukabidhiwa madawati ni tukio kubwa, nimefurahi sana na ninajua furaha ya watoto watakaotumia madawati haya itakuwa mara mbili yake, kwa hivyo kwa niaba ya Mkoa wa Shinyanga nawashukuru sana Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kwa kututengenezea madawati elfu mbili, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na upungufu wa Dawati elfu 7000 lakini sasa kupitia mchango wa leo kutoka Bulyanhulu na wadau wengine sasa mkoa wetu unamaliza kabisa upungufu wa madawati.”
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ,Bi Zainab Telack (aliye vaa ushungi) akiongozwa na Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila (kushoto kwake) wakati wakielekea uwanja wa Taifa wa mjini Kahama kwa ajili ya makabidhiano ya Madawati kutoka kampuni ya Acacia. 
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akihutubia wananchi katika uwanja wa Taifa Kahama wakati wa zoezi la Kukabidhiwa madawati kutoka kwa kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia, Bulyanhulu.
  Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,kutoka kushoto ni Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Elias Kasitila, Afisa Miradi Mzee Hamisi, Afisa Mahusiano ya Jamii William Bundala Chungu pamoja na Afisa Mahusiano ya Jamii David Magege, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kabla ya zoezi la Kukabidhi Madawati.
  Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia kwa ajili ya shule katika mkoa wa Shinyanga.

older | 1 | .... | 1344 | 1345 | (Page 1346) | 1347 | 1348 | .... | 3283 | newer