Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1343 | 1344 | (Page 1345) | 1346 | 1347 | .... | 3278 | newer

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Septemba, 2016 ameendelea na ziara yake Visiwani Zanzibar ambapo majira ya Asubuhi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume lililopo kando ya Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) eneo la Kisiwandui Zanzibar.

  Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi hilo na baadaye wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume na kuombea amani.

  Viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa akiwemo Rais Mstaafu wa Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume ikiongozwa na Mjane wa Marehemu Mama Fatma Karume wamehudhuria.

  Baada ya kuzuru kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume, Rais Magufuli amezuru kaburi la Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi lililopo nyumbani kwake Migombani Zanzibar.

  Dkt. Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika kaburi la Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi na pia wametoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu.

  Wakizungumza katika Dua ya kuwaombea Marehemu wote wawili Viongozi wa Dini kutoka madhehebu ya Kiislamu na Kikristo wameomba kuwepo kwa amani na upendo kwa watanzania wote kama ambavyo waasisi wa Taifa walipigania.

  Baadaye leo Rais Magufuli atazungumza na Wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Demokrasia wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Unguja
  03 Septemba, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoa heshima zake baada ya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  na viongozi wengine wakiomba dua bada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.


  0 0

   Afisa  Masoko na Elimu kwa Umma wa  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hawa Duguza akitoa maelekezo kwa mwanacha  njisi ya kujaza  fom leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
   Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Yusuph Kitainda akisisitiza jambo kwa wangeni alietembelea kambi ya (NHIF) leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Wanachama wa (NHIF) wakiwa katika kambi ya hoyo leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya wa NHIF umeaandaa mkakati wa kutatua kero za wanachama wake kwa kuwafata katika maeneo yao ya kazi.

  Zoezi hilo limeanzia katika Wilaya ya Ilala ambapo Mfuko umeweka kambi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa muda wa siku tatu ili kuweza kutatua kero na kufanya marekebisho madogo madogo ya kadi za NHIF kama kwa watu waliopotelewa na kadi, kubadilisha au kuongeza mwenza, kutoa barua za utambulisho wa Polisi kama kadi imepotea.

  Pamoja na kutatua kero hizo Mfuko pia unatoa elimu kuhusu bima ya afya hiyo na kuwahimiza wananchi kutembelea banda lao.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb.), jana tarehe 2 Septemba, amezindua Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli kwa niaba ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC Organ. 
  Misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi itakayojumuisha waangalizi kutoka nchi za SADC, itashiriki kwenye uangalizi katika vituo vyote 25 vya upigaji kura nchini Shelisheli. 
  Pamoja na kuongoza misheni hiyo, Tanzania kama Mwenyekiti wa SADC Organ itaongoza timu za uandishi wa taarifa ya SADC pamoja na ufuatiliaji wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8-10 Septemba, 2016. 
  Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza asasi hii muhimu ya Jumuiya, wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 
  Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kumwakilisha Mhe. Dkt. Magufuli, katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC. 
  Wajibu wa Tanzania kuongoza Misheni hya Waangalizi wa Uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa Jumuiya ya SADC ya kuwa na chaguzi za kidemokrasia katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. Waziri Mahiga anatarajiwa kutoa taarifa ya awali ya Misheni hiyo ya waangalizi wa SADC Septemba 12, 2016.   Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino Mahiga akifungua Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016, Mahe Seychelles. Mhe Waziri anamuawakilisha Mhe. Rais John pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na  Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016 huko Mahe, Seychelles.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Zanzibar jioni hii ya Septemba 3, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Zanzibar. PICHA NA IKULU


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akionesha aina tofauti za maboksi yatakayotumika kufungashia chaki nyeupe na za rangi ambazo zinatarajiwa kuanza kuzalishwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa, Mkoani humo wakati alipohitimisha Mafunzo ya Teknolojia ya Utengenezaji wa Chaki kwa vijana hao, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa, Mhe. Peter Bunyongoli.
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe akizungumza na vijana na wadau wengine wakati wa kuhitimisha mafunzo Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwa Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa, katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
  Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi (aliyesimama) akizungumza na vijana na wadau wengine wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika hilo  kwa Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa.
  Baadhi ya Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiangalia sampuli za maboksi yaliyopendekezwa kutumika kufungashia chaki pindi uzalishaji utakapoanza wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) akihitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO kwa vijana hao, wilayani humo
  Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiweka chaki walizotengeneza wakati wa mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO katika maboksi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) kabla ya Mkuu huyo wa mkoa  kuhitimisha mafunzo hayo.   

                                     Na Stella Kalinga, Simiyu
  Serikali Mkoani Simiyu imetangaza azma yake ya  kuanza kutengeneza Chaki ambazo zitauzwa katika Wilaya za Mkoa huo na nchi nzima kabla ya Oktoba 14 mwaka huu.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony John Mtaka wakati alipohitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa Chaki kwa vikundi vya vijana Wajasiriamali wilayani Maswa, yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga.

  Mtaka amesema shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali Mkoani humo  zinatumia jumla ya katoni 1200 za chaki ambazo zinagharimu shilingi 25,000,000 kwa kila mwezi, hivyo kama Vijana wa Wilaya ya Maswa wakizalisha Chaki na kusambaza katika mkoa mzima watajipatia kipato na kuondokana na umaskini.

  Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na  Tanzania ya Viwanda, Mkoa huo umejipanga kuimarisha uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo ambavyo vitazalisha mahitaji ya kila siku ya wananchi, hivyo wamedhamiria kuwa na uzalishaji wa bidhaa moja kwa kila wilaya ( one district  one product), ambapo Wilaya ya Maswa itakuwa ikizalisha chaki.

  “ Wilaya ya Maswa imepokea shilingi 38,000,000  Meatu 31,000,000 kwa ajili ya vijana kutoka Wizara yenye dhamana na Vijana, sasa hivi  tumepeleka maombi ya wilaya zilizobaki. Tumedhamiria kuutambulisha Mkoa kwa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe, tumeanza na Chaki wilaya ya Maswa, Wilaya ya Meatu wao watazalisha maziwa,  tutaendelea kutengeza utambulisho(brand) wa wilaya nyingine kwa kuzalisha bidhaa zinazoendana na malighafi zilizopo” alisema Mtaka.

  Akizungumza katika hitimisho la Mafunzo hayo kwa Vijana, Meneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi ametoa wito kwa vikundi vya vijana kuwa na mipango itakayowasaidia kutangaza bidhaa zao na kupata soko la bidhaa hizo ndani na nje ya Mkoa ili kujiongezea kipato.

  “Mtakapoanza kuzalisha chaki, kulingana na tathmini iliyofanyika kama mtauza kwa Mkoa wa Simiyu tu mtakuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya shilingi 8,000,000 kila mwezi, hiyo si fedha ndogo mkiwa na mipango thabiti mkazalisha chaki bora mtaweza kuuza chaki zenu nchi nzima na hata nje ya nchi” alisema Moshi. 

  Naye mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya utengenezaji wa chaki, Kelvin Steven ametoa wito kwa Wananchi wa  Simiyu na Watanzania kwa ujumla,  kuunga mkono juhudi za Vijana Wajasiriamali na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuinua uchumi wa Vijana hao na Taifa kwa jumla.

  Aidha, Bi. Specioza Fundikira ambaye pia amepata mafunzo hayo amesema matarajio ya Vijana waliopata mafunzo ni kuwa uzalishaji wa chaki utakapoanza kutakuwa na soko la uhakika kwa Shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali mkoani humo na mikoa ya jirani, vijana watapata ajira na kuachana na shughuli zisizo halali kama wizi na ulevi.

  Kwa Mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe vijana kutoka vikundi 8 vya Wajasiriamali ambao wameunda kikundi kimoja cha ‘Maswa Youth Enteprises’ wamepatiwa mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa chaki na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kuanzia tarehe 29/08/2016 hadi tarehe 03/09/2016.

  0 0

  Watanzania wameshauriwa kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ili kusaidia kukuza biashara na kuunga mkono juhudi za serikali za kutaka kujenga nchi ya viwanda. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage alisema hayo wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Milkcom Dairies Limited kilichopo eneo la Kibada wilaya ya Kigamboni mwishoni mwa wiki. 
   “Tukipenda bidhaa zetu tunatengeneza soko kwa viwanda vyetu kuzalisha zaidi, kukua na kujenga uchumi wetu,” alisema. Alisifu juhudi zinazofanywa na kiwanda hicho kinachozalisha maziwa kwa jina la Dar Fresh na bidhaa nyingine za maziwa, na maji ya chupa. Pia kiwanda hicho kiko katika harakati za kuanza kuzalisha vinywaji baridi na kukamua matunda kwa ajili ya kutengeneza juisi mbalimbali. 
   “Nimefurahishwa na kazi yenu, mnafanya vizuri,” alisema. Kiwanda hicho chenye n’gombe wa maziwa 3,000 kinazalisha wastani wa lita 10,000 za maziwa kila siku. Pia kinakusanya maziwa toka kwa wafugaji hasa kutoka maeneo ya mkoa wa Morogoro na Pwani kama Dakawa, Kimamba, Lugoba na Chalinze. Mkurugenzi wa maziwa ya Dar Fresh, Bw. Yusuph Said alisema utaratibu huo umesaidia kutengeneza soko la uhakika kwa wafugaji hao.
   “Tunakusanya wastani wa lita 8,000 kila baada ya siku moja toka kwa wakulima hao,” alisema Bw. Said. Waziri aliuahidi uongozi wa kiwanda hicho kufuatilia kwa karibu ili kupata umeme wa uhakika kutoka gridi ya taifa na miundombinu mingine ya muhimu ili waweze kuwa washindani zaidi. Kampuni ya Milkcom Dairies Limited iko chini ya umoja wa makampuni ya Oilcom. Katika ziara hiyo, 
  Waziri Mwijage pia alitembelea eneo la mradi wa viwanja 240 vilivyotengwa na serikali katika eneo la Tundwi Songani, Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na viwanja 100 vya makazi kwa watakaokuwa wanaendesha viwanda hivyo. Alisema kazi kubwa ya serikali baada ya kupima viwanja hivyo ni kuhakikisha kuwa panakuwa na umeme wa uhakika, maji, barabara na miundombinu mingine ili kuvutia wawekezaji. 
   “Tuangalie jinsi ya kuvuta bomba la gesi eneo hili ili kuvutia wawekezaji haraka,” aliwaambia maafisa wa serikali aliofuatana nao. Alisema atahakikisha kuwa eneo hilo linapata miundombinu inayotakiwa ndani ya miaka miwili kuanzia sasa ili wawekezaji katika sekta ya viwanda wafanye kazi zao bila matatizo. 
   Pia alisisitiza utunzaji wa mazingira kwa wenye viwanda. Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Bw.Hashim Mgandilwa alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha maeneo hayo yanatumika kama ilivyopangwa na serikali. “Tunahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza hapa kwa faida ya pande zote mbili,” alisema. Kamishna wa Ardhi Msaidizi, Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Mathew Nhonge alisema maeneo hayo ni kwa ajili ya viwanda vidogo na viwanda vya kati.   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage (kulia) akisisitiza jambo alipokuwa akipewa maelezo wakati wa ziara yake katika eneo la viwanja 240 vilivyotengwa kwa ajili ya viwanda katika eneo la Tundwi Songani, wilaya ya Kigamboni mwishoni mwa wiki.  
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia maelezo wakati wa ziara yake katika kiwanda kinachozalisha bidhaa za maziwa kilicho chini ya Milkcom Dairies Limited eneo la Kibada wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki.  Kushoto ni Mkurugenzi wa makampuni ya Oilcom, Bw. Said Nahdi.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage (wa pili kushoto) akifuatilia maelezo wakati wa ziara yake katika kiwanda kinachozalisha bidhaa za maziwa kilicho chini ya Milkcom Dairies Limited eneo la Kibada wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki.  Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa makampuni ya Oilcom, Bw. Said Nahdi na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Bw. Hashim Mgandilwa (kushoto).
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage (kushoto) akifuatilia maelezo wakati wa ziara yake katika kiwanda kinachozalisha bidhaa za maziwa kilicho chini ya Milkcom Dairies Limited eneo la Kibada wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa makampuni ya Oilcom Group, Bw. Said Nahdi na Mkurugenzi wa maziwa ya Dar Fresh, Bw. Yusuph Said (kulia).

  0 0
 • 09/04/16--01:22: NI LEO JIONI


 • 0 0
 • 09/04/16--01:35: MAGAZETI LEO

 • 0 0

   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi na wanaCCM wa Zanzibar jioni hii wakati akiwasili kwenye Uwanja Uwanja wa Kibandamaiti katika mkutano maalum wa kuwashukuru wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja leo.


    Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanznia Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja katika mkutano maalum wa kuwashukuru wananchi wa Mikoa mitatu(3) ya Unguja

   Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanznia Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja katika mkutano maalum wa kuwashukuru wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Na Is-haka Omar, Zanzibar

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeipongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa katika ziara zake Zanzibar, iliyosisitiza dhamira ya serikali kuharakisha maendeleo kwa wananchi bila ya kujali tofauti za kisiasa.
  CCM imesema inaunga mkono na kupongeza kwa dhati hotuba hizo zilizotolewa Unguja na Pemba ziliyosisitiza dhamira ya serikali zote mbili ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar kuwaletea wananchi maendeleo bila ya kujali itikadi za kisiasa.
  Akizungumza Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya ya Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu  (pichani) alisema  viongozi na wananchi kwa ujumla wanatakiwa kushirikiana katika ujenzi wa maendeleo ya nchi ili zanzibar iweze kufikia hadhi ya kuwa nchi yenye uchumi mkubwa katika nchi za Afrika.
  Vuai alieleza kwamba ziara hiyo imetoa muongozo imara wa kuwakumbusha watendaji na viongozi nchini juu ya dhamana na mambo ya msingi wanayotakiwa kuyatekeleza kwa wananchi.
  “CCM tunaunga mkono kwa nguvu zote hotuba ya Rais wetu Dkt. John Magufuli kwani imezungumzia na kugusia mambo ya msingi yanayogusa maisha ya wananchi hasa wa kipato cha chini na kutoa muongozo wa namna gani serikali zetu zinaendelea na mikakati imara ya kuimarisha uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
  Pia tunatakiwa kuendelea kuwa wamoja na wazalendo bila ya kujali tofauti zetu za kidini, kisiasa na kikabila kwa kulinda amani na utulivu wa nchi zetu kwani ndio siri ya mafanikio ya nchi zetu.”, Alisisitiza Waride.
  Katibu huyo , alisema Dkt. Magufuli ameonyesha nia ya dhati ya kuendelea kutafuta fursa mbali mbali za miradi ya maendeleo itakayoweza kuharakisha maendeleo ya Zanzibar.
  Alisema miongozo mwa mambo ya msingi yaliyosisitizwa na Dkt. Magufuli pia yanaungwa mkono na CCM Zanzibar ni dhamira ya kuhakikisha Zanzibar inakuwa ni nchi ya Viwanda vya kusindika samaki wanaotokana na Uvuvi wa Kisasa wa Bahari kuu  vitakavyotoa fursa za ajira kwa vijana na wananchi.
  Waride,  alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Muungano wa Tanzania  kwa kufungua milango ya wawekezaji wakubwa kuwekeza Zanzibar huku wakitafuta wahisani kutoa mamilioni ya fedha za kuendesha miradi ya kijamii  ukiwemo mradi wa maji safi Unguja uliotolewa fedha za mkopo na Serikali ya India.
  Alisema kwa ushirikiano wa Rais Dkt. Magufuli na Dkt. Shein, CCM inaamini kwamba Tanzania bara na Zanzibar kwa ujumla zitakuwa nchi za kupigiwa mfano duniani katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo, kisiasa na kijamii.
   Alifafanua kwamba CCM Zanzibar, inaungana na Dkt. Magufuli kupinga siasa za misimamo mikali na utengano zinazofanywa na baadhi ya vyama vya kisiasa Zanzibar kuwa haziwezi kuleta maendeleo ya nchi badala yake zitajenga migogoro isiyokuwa ya lazima.
  Alisema CCM inasifu msimamo wa Dkt. Magufuli wa kulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 huku akiahidi kuendelea kulinda amani na Utulivu wa nchi kwa gharama yoyote.
  Pamoja na hayo  Waride  aliahidi kuwa CCM itaendelea kuwa balozi mzuri wa kuwasihi wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kufanya siasa za maendeleo zitakazoweza kwenda sambamba na malengo ya serikali.
  Aidha Waride alipongeza juhudi za Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein za kuongoza nchi kwa ufanisi mkubwa licha ya kuwepo na changamoto mbali mbali za kisiasa nchini.
  Alielezea kuridhishwa kwake na kauli ya Dkt. Shein  ya kuwataka wapinzani kusahau Serikali ya Mpito kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi huku akisisitiza hakuna sababu ya kuwa na aina ya serikali hiyo kwa sababu uchaguzi umefanyika kwa njia ya huru na haki.Katika Mkutano huo, Dk Shein alisema kazi kubwa inayofanywa kwa sasa ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa katika hatua ya mwisho ya kuanza kazi za kuchimba mafuta na ges ili kutoa hatua pana ya ajira kwa wananchi.Alisema muswada wa mafuta na gesi tayari umewasilishwa katika Baraza la Wawakilishi na kusomwa kwa mara ya kwanza ambapo katika kikao kijacho cha Baraza la Wawakilishi kitakachofanyika Septemba 26 utasomwa kwa mara ya pili na kusubiri saini yake.
  Ziara hiyo ya Dkt. Magufuli  ya kuwashukru wananchi wa Zanzibar kwa kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu uliopita, imefanyika katika maeneo mbali mbali Pemba na Unguja.

  0 0


  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  ENEO la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu  wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini eneo hilo litasaidia kwa kila mfanyabiashara kuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa hiyo ni moja ya Mkakati wa harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati.

  Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka  inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka huu wa fedha.

  Kayombo amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni  asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 923.

  Pia Kayombo ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo TRA vilivyo karibu kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo.

  Amesema kuwa vituo vya kuhakiki taarifa zao ni pamoja na vitua vya 
  Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
  Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
  Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
  Wilaya ya Kigamboni - Ofisi za TRA Kigamboni
  Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji. 

  Kayombo pia amewahimiza wamiliki wa vituo vya  mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga  mashine za EFDs kabla Septemba 30 mwaka huu  kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe Oktoba 1 na  hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

  Na walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo  wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kuhusiana na mikakati mbalimbali waliyojiwekea Mamlaka ya Mapato(TRA) ili kuhakikisha Mapato yanakusanywa ipasavyo.
  Baadhi ya waandishi wa Habri wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  Uwanja wa Amaan mjiniUnguja ni wa kihistoria, japo wengi hawafahamu. Ulijengwa kwa msaada wa serikali ya China na ulifuynguliwa mwaka 1970, ukiwa ni mradi mkubwa wa nchi hiyo wa viwanja vya michezo barani Afrika. Michezo na sherehe nyingi hufanyika uwanjani hapo. Sherehe kubwa ya kihistoria ilifanyika February 5, 1977 wakati vyama vya TANU na Afro Shirazi vilipoungana na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM.  Uwanja huo ulifungwa kwa muda na kufanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kufunguliwa tena mwaka 2010. Una uwezo wa kukaa watu 15,000. 

  0 0
 • 09/04/16--05:14: MSIKITI MABULUU, ZANZIBAR
 •  Msikiti Mabuluu mjini Unguja unavyoonekana kwa jicho la ndege
  Msikiti Mabuluu mjini Unguja unavyoonekana unavyonogesha mandhari ya Unguja. Andiko la awali BOFYA HAPA  0 0

   Bendi ya Jeshi la Magereza Zanzibar likiongoza matembezi ya wanamichezo, kushajihisha Jamii kufanya mazoezi. 
   Wanamichezo wakiwa katika matembezi ya kushajihisha Jamii kufanya mazoezi yaliyoanza Mazizini na kumalizia uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
   Naibu Spika wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma ambae ni mgeni rasmi katika matembezi yawanamichezo akizungumza na vikundi vya mazoezi vilivyoshiriki matembezi hayo.
   Kocha wa mazoezi kutoka kikundi cha Obama Fitness Club Haji Golo akiongoza mazoezi ya wanavikundi baada ya maandamano yaliyoanza Mazizini na kumalizikia uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
   Kocha wa mazoezi kutoka kikundi cha Obama Fitness Club Haji Golo akiongoza mazoezi 
   Naibu Spika wa (BLM) Mgeni Hassan Juma (alievaa flana ya bluu) na Meneja wa Jumuiya ya maradhi yasiyo ambukiza Zuhura Saleh Amour (kulia) wakifanya mazoezi.
  Mgeni rasmi Naibu Spika wa (BLM) Mgeni Hassan Juma (alievaa flana ya bluu) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya maradhi yasiyo ambukiza Zanzibar. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

  BOOK TRAILER - Lamellia, The Kingdom of Mushrooms from Gloria D. Gonsalves on Vimeo.
  The book is currently available at the following online sources:


  Like my previous books, it will also be available at:
  * Germany’s Thalia < www.thalia.de >
  * South Africa’s takealot.com <http://www.takealot.com/>

  0 0  Mama Tereza hivi sasa anajulikana kama Mtakatifu Teresa wa Calcuta, baada ya kutawazwa rasmi na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.

  Leo maelfu ya watu wamejitokeza kushuhudia tukio hilo kubwa duniani la kutangazwa kwa kwa raia huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997.

  Mama Tereza alianzisha shirika la hisani la kimishenari ili kuwasaidia walala hoi katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.

  Lakini wakosoaji wanesema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu maskini wa kabila la Hindu nchini India kuwa Wakristo.

  Sherehe za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel, zimehudhuriwa na wageni zaidi ya 1,000 wakiwemo wakuu wa nchi mbalimbali 13 na viongozi wa madhehebu hayo.

  Ulinzi umeimarishwa wakati wa sherehe hizo. Mama Teresa aliyezaliwa mwaka 1910 katika taifa ambalo hivi sasa linajulikana kama Macedonia, alianza huduma ya utawa akiwa na umri wa miaka 16.

  Ilikuwa ni kazi yake ya kuwasaidia wagonjwa na maskini huko Calcuta, India iliyompatia umaarufu mkubwa duniani kote, pamoja na kupokea tuzo ya amani ya Nobel.

  Papa Francis amesema huruma aliyokuwa nayo Mama Teresa inapaswa kuwa mfano kwa Wakatoliki wote. Kutawazwa kwa mtawa huyo kunakuja miaka 19 baada ya kifo chake.

  0 0  0 0

  Mkuu wa wilaya ya kongwa, Mh Deogratius Ndejembi amefanya kikao cha baraza la wafanya biashara wa wilaya ya kongwa, likiwa linajumuisha wafanya biashara wote wakiwamo wafanya biashara za mazao, mifugo, na biashara zingine. 

  Kikao kilifunguliwa na Mh DC akiwa kama mwenyekiti wa Baraza hilo kwa nafasi yake, Mh DC Ndejembi alipokuwa akifungua kikao alisema nakusisitiza haya, Kuwa kwa mara ya kwanza yeye kama DC anafanya kikao hicho kama Mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara hivo anaomba nakusisitiza ahitaji kuona Mtu anasimama nakuanza kulalamika hovyo, kama anamalalamiko aseme na kisha atoe utatuzi au maoni yakutatua hizo kero anazozilalamikia.

  DC Ndejembi amefanya kikao hicho nakubaini kuna Posho nyingi na gharama kubwa sana ambazo zinatumika kwa Vikao vya Baraza hilo, ikiwemo gharama za Posho, Chakula, Uchapishaji wa nyaraka mbali mbali ambazo pia amezilalamikia kwakuwa kikao hicho kuna wajumbe wa kikao wamekosa Baadhi ya nyaraka za Vikao ambazo ukitizama Gharama za kikao hicho Wameorodhesha Machapisho na hayakuwapo ndani ya kikao lakini matumizi yanaonyesha pesa imetoka kwa ajili ya machapisho ya kikao.

  DC Ndejembi amewaasa kuacha tabia zakuwa tegemezi kwani sasaivi wamekuwa wakizifuja pesa hizo kwakuwa ni Pesa zakupewa na LIC (Local  Investment Climete) kuna siku msaada huo utakwisha hivyo, waache Tabia zakulipana posho hovyo hovyo wakati vikao wanavyofanya ni vikao vyakujadili mambo yao ya msingi kwa biashara zao na kwafaida ya Taifa lao na vizazi vyao, waanze kuchangia wao wenyewe ili wawe na uchungu na pesa zao na watajadili mambo ya msingi zaidi kwakuwa na uchungu na uzalendo zaidi.
  DC Ndejembi amewaeleza wafanya biashara hao kuacha Tabia za kuweka michanga na mawe katika baadhi ya mazao ambayo yanauzwa Kongwa na hasa katika Soko kuu lakimataifa la Kibaigwa! kwani ndani ya kikao hicho kuna mjumbe alisema nakukili kulalamikiwa kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kongwa na Mkoa wa Dodoma kuwa na Tabia yakujaa mawe na michanga katika mazao ili yaongezeke kilo nakujipatia faida zaidi, kitu ambacho kinasababisha soko la mazao ya ukanda huo kushuka thamani kwa michezo hiyo michafu.
  Mkuu wa wilaya kaagiza kuanzia leo Atakaebainika kachanganya Mawe au Michanga katika Mazao basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel.
  Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.
  Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki)


  Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 

  Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8 - 10 Septemba, 2016.

  Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi za SADC .

  Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix Michel Rais wa Sheliseli .

  Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.

  Imetolewa na :
  BALOZI INNOCENT E. SHIYO.

  0 0

   Bw. Harusi Abraham Mossi na Mkewe Bi. Rachel Kissui wakiingia Kanisani tayari kwa Ibada ya Ndoa yao iliyofungwa katika Kanisa la Katoriki la Mtakatibu Isidori Bakanja, Parokia ya Boko Jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
   Maharusi wakiwaongoza ndugu na jamaa waliofika kushuhudia ndoa yao, kuongia kanisani.
   Tabasamu la nguvu baada ya kumamilisha tendo muhimu katika maisha.
   Bw. Harusi Abraham Mossi akimwaga wino, kwa muongozo wa Padri humu mamsapu wake akimshuhudia.
   Bi. Harusi Rachel Kissui akimwaga wino pia.
   "Unajua nini My Wife wangu, leo ni bonge la siku kwetu".
   Maharusi na Familia zao.


older | 1 | .... | 1343 | 1344 | (Page 1345) | 1346 | 1347 | .... | 3278 | newer