Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1342 | 1343 | (Page 1344) | 1345 | 1346 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Nteghenjwa Hosseah –Arusha

  MKOA wa Arusha umeanza kujipanga katika utaratibu wa kulinda mji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya CCTV – Camera ili kuimarisha usalama wa mji “Safe City”, Mfumo huu utawezeshya Mji kulindwa masaa 24 dhidi ya uhalifu kwa raia, wawekezaji na watalii.

  Kauli hiyo ilitolewa leo mjini hapa na Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo ofisini kwake mara baada ya kutembelewa na Balozi wa Sweden nchini, Bi. Katarina Rangnite aliyeambatana na Ujumbe wake wa Wabunge kutoka Nchini Sweden.

  Akizungumza na ujumbe huo RC Gambo alisema, mkoa huo tayari umekwisha kuonyesha nia ya kuwekeza katika mfumo huo ili kuwaongezea wananchi na mali zao usalama zaidi.

  “Nia yetu ni kuona hali ya usalama katika mkoa wa Arusha ikiwa ya juu sana ili kuendelea kuwavutia watalii zaidi kutoka nchi mbalimbali Duniani. Malengo yetu ni kuwa na mifumo itakayoulinda mkoa wetu kwa Saa 24 na mwaka mzima,” alisema RC Gambo na kuongeza:

  “Hatua hii itaongeza ulinzi kwa raia na mali zao, pia kwa wawekezaji waliopo mkoani kwetu na watalii wanaokuja kutembelea hifadhi na vivutio mbalimbali kwani Arusha ndio kitovu cha utalii hapa nchini,” alisema.

  Kwa upande wake Balozi Rangnite ambaye kiongozi wa msafara huo uliojumuisha pia wabunge kutoka Bunge la Sweden wanaowakilisha Kamati ya Kilimo na Mazingira, alikubaliana na nia ya kuwekeza kwenye mfumo wa usalama wa mkoa wa Arusha.

  Balozi Rangnite alimueleza Mkuu wa Mkoa Gambo kwamba, nchi ya Sweden inayo wataalamu waliobobea katika mifumo hiyo ya usalama wa miji hivyo alimuomba Gambo kuwasilisha kwake maandiko ya vitu vinavyohitajika ili kuwezesha mradi huo kutekelezwa.

  “Tukipata maandiko mbalimbali ya mradi tunaweza kuangalia ni wapi Serikali ya Sweden inaweza kuwekeza ikiwamo kusaidia kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili,” alisema Balozi Rangnite.

  Aidha Gambo alitoa ombi kwa Balozi wa Sweeden kushirikiana na Mkoa wa Arusha kwenye Kampeni ya Kulinda vyanzo vya Maji ili kuwezesha mradi mkubwa wa maji unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na maji taka (AUWSA) kutekelezwa kwa mafaniko makubwa. Itakumbukwa kwamba imepatiwa Bil 476 ili kumaliza tatizo la maji Jiji hapa.

  Katika ziara ya ujumbe huo pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo la kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika Kilimo, Mazingira na maeneo muhimu kutoka mkoani Arusha.

  Ujumbe huo kutoka Sweden ukiongozwa na Balozi Rangnite uliridhishwa na kuvutiwa na maeneo ya utalii yaliyopo katika mkoa huo yakiwamo pia mazingira rafiki yanayoruhusu uwekezaji kwa jamii yao.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akizungumza aliyeambatana na Wabunge toka Sweden walipotembelea Ofisini kwake mapema leo.
  Kiongozi wa ujumbe toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns (kushoto) akikabidhi zawadi yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
  Kutoka kushoto ni Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mashaka Gambo pamoja na Kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Bi. Matilda Irnkarns kwenye picha ya pamoja baada ya Kikao
  Katika picha ya pamoja ni kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Kwitega, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnite , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns, ujumbe toka Sweden pamoja na viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. 
  Baadhi wa wabunge toka Sweden wakifuatilia kikaa wakati walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema leo.


  0 0

  Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  wakiimba wimbo wa shule ikiwa ni ishara ya kukumbuka walipokuwa wanafunzi shuleni hapo  baada ya kufika shuleni hapo  Augosti 27, mwaka huu kukabidhi msaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule ambayo  pia ilikarabatiwa na  michango yao.
   Mhitimu wa shule  ya Sekondari Kilakala , Claudia Iringo akimkaabidhi mwanafunzi wa shule hiyo madafyari  kwa ajili ya  wenzao wenye mahitaji maalumu , wahitimu hao wa zamani wapatao 15  waliosoma kuanzia 1988 hadi 1995  waliitembele shule yao  hivi karibuni.
   Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  wakiimba na kicheza kukumbusha enzi zao katika  shule hiyo.
  Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  pamoja na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa shule hiyo, walimu na bodi ya shule wakiwa ndani ya  jengo la zahanati ya  shule  baada ya kukabidhi shuka, magodoro pamoja na madatfari kwa wanafunzi.
  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba ambako aliweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Dkt Omar Ali Juma, na kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye ndege ya ATCL katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akivishwa shada la maua ya asumini baada ya kutelemka kutoka kwenye ndege ya ATCL katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na makamanda wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Pemba katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuhutubia mkutano katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba. 


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Pemba katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.PICHA NA IKULU

  0 0
 • 09/02/16--22:00: MNADA WA HADHARA
 •  Tunapenda kukujulisha mnada wa Magari pamoja na Furniture mbalimbali za ofisi na majumbani, mali kutoka Ubalozi wa Canada, Sweden na Finland.Mnada utafanyika Jumamosi ya wiki hii tarehe 03.09.2016 kuanzia saa 4 asubuhi. 
  Mahali: Golden Resort, Lion Street, Sinza 
   ( Nyuma ya  Lion Hotel) jijini Dar es salaam


  0 0  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linatoa tahadhari kwa Wamiliki na Wakuu wote wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi nchini kuwa kumeibuka matapeli wanaowaomba fedha au rushwa wakuu wa vyuo hasa vilivyopewa notisi na Baraza ya kushushwa hadhi au kufungiwa ili kuweza kuwasaidia kutatua matatizo yao kupitia namba mbalimbali za simu wanazozitoa.

  Baraza linaendelea na kuwatahadharisha wateja wetu kuwa msikubali kupokea simu zenye kuwaomba fedha au kutoa kitu chochote wakati mnapotekeleza maelekezo ya Baraza au hata baada ya kutekeleza maelekezo hayo.

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Adolf Rutayuga anatoa tahadhari hii baada ya ofisi yake kupokea malalamiko hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya Wakuu wa Vyuo na Wamiliki ambao wamedai kupigiwa simu na watu wanaojitambulisha kuwa Maafisa wa NACTE na kuwadai kiasi cha fedha kama masharti ya kutatuliwa matatizo yao. Pia Baraza limepokea taarifa kutoka kwa Wadau wanaolalamika kuwa kuna kundi watu wanaodai kupewa fedha ili wasaidiwe kupangiwa vyuo fulani vya ufundi kwa masomo mbali mbali.

  Baraza halina utaratibu wa kuomba fedha au zawadi ya aina yeyote kwa Mkuu wa Chuo au Mtu yoyote kama sharti la kupata huduma/msaada fulani.

  Ni imani yetu kwamba wakati Baraza likiendelea na uchunguzi wa kuwabaini matapeli hao ili kuwachukulia hatua za kisheria, Wadau wetu wataongeza umakini na kuchukua tahadhari binafsi na watu wa namna hiyo.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Katibu Mtendaji – NACTE
  01 Septemba, 2016.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na matapeli wanaowaomba fedha au rushwa wakuu wa vyuo hasa vilivyopewa notisi na Baraza hilo,kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Udahili wa baraza hilo, Seremani Majindo.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

  Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

  Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

  Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

  Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.
  Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
  Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
  Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.  0 0

  Na mwandishi wetu, Durham, NC

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi siku ya Ijumaa Septemba 2, 2016 alimtembelea na kufanya mazungumuzo na Mayor wa mji wa Durham, North Carolina, Mayor William V. "Bill Bell".

  Katika mazungumuzo hayo yaliyofanyika ofisi ya Mayor iliyopo City Hall, Mhe. Balozi Wilson Masilingi alimweleza Mayor William "Bill Bell" nia yake ya kutafuta wawekezaji watakaosaidia kukuza uchumi wa Tanzania kupitia seka mbalimbali huku akimweleza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli za kufufua na kujenga viwanda,

  Mhe. Balozi Wilson Masilingi alimhakikishia Mayor William "Bill Bell" wawekezaji watakaokua tayari kuwekeza Tanzania watafanyia taratibu zote na kwa haraka zaidi na bila kuwa na usumbufu huku Mayor William "Bill Bell" akimuahidi Mhe. Balozi William Masilingi kutoa ushirikiano wa karibu na kuhakikisha anamkutanisha na wawekezaji wa Durham, North Carolina watakaokua tayari kuwekeza nchini Tanzania.
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akifanya mazungumuzo na Mayor wa mji wa Durham Mayor William"Bill Bell"
  Mazungumuzo yakiendelea wengine katika mazungumuzo hayo kutoka kushoto kwa mzunguko wa meza ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Bwn. Abbas Missana, Brady Surles ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Sister Cities ya Durham yenye mashirikiano na mji wa Arusha, Tony Nturu, Dorothy Borden ambaye ndie mwanzilishi wa Sister Cities na Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex,
  Mazungumuzo yakiendelea.


  0 0

  Mbunge,Mh.Venance Mwamoto


  Na Matukiodaima Blog

  KOCHA wa timu ya Bunge Venance Mwamoto ametoa mwaliko kwa timu ya Bodaboda kilolo kwenda bungeni kucheza mchezo wa kirafiki na wabunge 

  Mwamoto ambae ni mbunge wa Kilolo mkoani Iringa alitoa mwaliko huo wakati wa kikao chake na vijana hao wa bodaboda mjini Ilula Jana.

  Alisema kuwa kabla ya kwenda bungeni vijana hao watashindana kupata bingwa wa mashindano hayo ambaye atakwenda Dodoma kucheza na wabunge.Hivyo alisema lazima kujipanga vema kwa kujiandaa ili kuepuka aibu ya kichapo kutoka kwa wabunge. 

  "Nawaomba timu itakayoshinda iwe bungeni kutangaza wilaya getu ya Kilolo kisoka pia kuanza rasmi kwa mashindano ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na mimi mbunge wenu nitadhamini "

  Hata hivyo alisema kabla ya mashindano hayo atatoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama njia ya kuondoka kero ya vifaa vya michezo. Mwamoto alisema lango ni kuona vijana Kilolo wanakuwa na timu na kupitia michezo wanapata ajira kwa kuchezea timu mbali mbali kubwa nchini. 

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ( Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora ametoa wito kwa vyuo vyote nchini kuanzisha mitaala inayohusu usalama wa mitandao ya mawasiliano ili kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandao hiyo.

  Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu huyo alipokuwa akifunga warsha ya siku ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola iliyohusu Uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama wa Mitandao iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

  Prof. Kamuzora amesema kuwa moja ya vitu vilivyoelezewa katika Sera ya Tehama iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu ni kuhakikisha mitandao ya mawasiliano inakuwa salama hivyo kila mwananchi anawajibu wa kulinda mitandao hiyo.

  “Suala la usalama wa mitandao ya mawasiliano linapelekea kuwepo kwa fursa nyingi za ajira hivyo, napenda kutoa wito kwa vyuo mbalimbali nchini kuanzisha mitaala mipya itakayohusu masuala haya kwa sababu watu watatakiwa wajikite kwenye masomo yanayohusiana na mitandao”, alisema Prof.Kamuzora.

  Ameongeza kuwa kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni zimebainisha kuwa dunia nzima inapoteza jumla ya dola bilioni 400 kwa mwaka kwa njia ya wizi wa mitandaoni hivyo kushindwa kulinda mitandao ya mawasiliano kunapelekea hasara kubwa kwa Taifa na Dunia kwa ujumla.

  Naye Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola , Fargani Tambeayuk amesema kuwa Jumuiya hiyo inawasaidia nchi wanachama katika kudhibiti usalama wa mitandao ili kusaidia nchi hizo kupata maendeleo kwa kutumia mitandao pamoja ma kuepukana na uhalifu.

  Kwa upande wake Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Makosa ya mitandao, Joshua Mwangasa amesisitiza suala la kutolewa kwa elimu ya usalama wa mitandao liwe endelevu akiamini kuwa elimu hiyo itawasaidia wananchi kuepuka kutumia vibaya mitandao ya mawasiliano.

  Aidha, ameusifia mpango huo kwani utawasaidia Jeshi la Polisi kuweza kukabiliana kirahisi na wananchi wanaofanya makosa kwenye mitandao pia amesisitiza kuwa makosa ya kimtandao ni kama makosa mengine hivyo taratibu za kuripoti makosa hayo ni zile zile za kawaida.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akifunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (hawapo pichani) kuhusu uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao nchini. 
  Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Bw. Fargani Tambeayuk akitoa shukurani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na wadau wengine baada ya kumalizika kwa warsha ya uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Shabani Pazi akizungumza wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa kufunga Semina ya Uuandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao leo. Jijini Dar es Salaam. 
  Wadau wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa kufunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola wanaoandaa mkakati huo. 

  0 0

   aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) wakati akiizindua leo Jijini Dar es Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na kuhakikisha inairudisha katika hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda.
   Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje(kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa Maendeleo (NDC) Dkt. Samweli Nyantahe nyaraka mbalimbali zitakazomuongoza katika utendaji kazi.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) mara baada ya kuizindua leo Jijini Dar Es Salaam.
  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WAZIRI wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Shirika la  Taifa Maendeleo ya Viwanda (NDC) ndio injini ya kushikiria sekta ya viwanda na hivyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka minne inakuwa  viwanda hata vitatu katika kuweza kufikia uchumi wa kati.

  Mwijage ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa BAodi mpya ya Wakurugenzi NDC, amesema kuwa bodi lazima ifanye kazi kuhakikisha inashikiria viwanda vikubwa ambayo vitafanya taifa kuwa na maendeleo ya kiuchumi kutokana miradi iliyopo chini ya NDC.

  Amesema kuwa mradi wa kwanza ni ule wa Liganga na Mchuchuma unatakiwa kufutika midomoni  mwa watu kwa kuanza kuzalisha kutokana na muda mrefu umekuwa ukizungumzwa.

  Mwijage amesema kuwa  kutokana bodi hiyo kuwa na watu wa kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana mara kwa mara hata bila kulipwa posho ili mambo yeande na kuleta tija kwa taifa.

  Amesema kuwa miradi mikubwa ikikamilika nchi itakuwa imepiga hatua kimaendeleo na kuweza kufikia uchumi wa kati  wa viwanda vyenye kwa wananchi.

  Nae Mwenyekiti wa bodi wa NDC,  Dk, Samwel Nyantahe amesema kuwa watafanya kazi kwa karibu na wizara ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi yote na kuweza kuanza kufanya kazi kwa nguvu.
  Amesema Rais Dk. John Magufuli amemuamini hivyo watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo katika sekta ya viwanda.

  0 0

  MGODI wa Dhahabu wa Geita(GGM) ulifanikiwa kuchangia Shilingi Milioni  mia nne arobaini na nne (444,000,000.00) ambazo zilinunua madawati 6000 ambayo ni asilimia 25 ya michango iliyotolewa katika tukio la uchangiaji madawati mkoani Geita.

  Akizungumzia mchango huo wa madawati,Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita  Terry Mulpeter amesema kuwa GGM inaendelea kujihusisha katika kuchangia elimu mkoani Geita kwa kuwa ndiyo fursa endelevu ya kuwakomboa wananchi na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  “Kwa kutambua umuhimu wa elimu, GGM imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, Mgodi umechangia zaidi ya Shilingi Bilioni 10 za kitanzania kujenga shule ya wasichana ya Nyankumbu Mkoani Geita ambapo zaidi ya wasichana 800 wanapata maarifa kwenye michepuo ya Sayansi” amesema Mulpeter.

  Amesema kuwa mchango wa GGM umefanikisha pia shule hiyo kuwa na Kompyuta za pamoja na vifaa vya kisasa katika maabara  na mazingira ambayo ni rafiki kwa wanafunzi kujisomea pamoja na nyumba  bora kwa waalimu kuishi. 

  Bw Mulpeter amesisitiza kuwa kuwa elimu ni mojawapo ya haki muhimu za binadamu.
  “Elimu ni jambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu, GGM inaamini kuwa kuweka mazingira bora ya kusomea ili watoto wetu wengi wahitimu vyema elimu ya msingi na sekondari na kuendelea na masomo ya juu  itakuwa chachu ya maendeleo la taifa letu” 

  Mgodi wa GGM unaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika jitihada za kuleta wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini.

  0 0


  0 0

  Taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na binafsi kutoka ndani na nje ya nchi zimeshiriki Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki, yanayofanyika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Maonesho hayo huandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini, TCCIA.

  Taasisi mbalimbali za Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Viwanda hutumia Maonesho hayo kukutana na wateja wapya, kutangaza na hata kuuza bidhaa zake. Mbali na hilo taasisi mbalimbali hutumia fursa hiyo kukutana na wananchi na kufikisha elimu husika.

  Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kujumuisha vitengo vyake ikiwemo Kikosi cha Usalama barabarani na dawati la jinsia, limetumia maonesho hayo kufikisha elimu mbalimbali kwa wananchi na hata kupokea maoni kutoka kwa wananchi.

  Na BMG
  Banda la Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Kitengo cha dawati la jinsia
  Banda la Jeshi la polisi mkoani Mwanza, kitengo cha Usalama barabarani
  Maonesho hayo yalianza Agosti 26,2016 na ufungi rasmi kufanyika Agosti 30,2016 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela alifungua Maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kama picha inavyoonekana mgeni rasmi akiwa kwenye banda la jeshi la polisi mkoani Mwanza.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne hatua kwa hatua.

  Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma, Waziri Mhagama alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko vizuri na kama Mhe. Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya kipindi hicho sisi tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa hatua”.

  Waziri Mhagama alieleza kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia mipango iliyopo na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango yote ya maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa na ujio wa Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na tutaendelea kuyafanya hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza Mhagama

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kutekeleza usimamizi wa maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati “kwa upande wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa ujenzi wa barabara unakamilika na tutakutana na Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji Mji (CDA) na Manispaa ili kuona shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu ya mkoa.”

  Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri Mhagama kwa kutembelea maeneo ya makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu.” 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifuatilia maelezo ya ramani ya Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Wataalam wa maswala ya Ujenzi kulia kwake ni Mhandisi Joseph Muhamba na wa kwanza kushoto ni Bw. Keffa Chana wakati wa Ziara yake katika makazi hayo Septemba 2, 2016 Mlimwa Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.

  0 0

   Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo akikagua timu wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi zilizofanyika kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea. Super Girls ilishinda 4-1 dhidi ya VC Vito Malaika.
   Nahodha wa timu ya Super Girls Tatu Makota akipokea kombe la ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi kutoka kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.
  Wachezaji wa timu ya Super Girls wakishangalia ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.

  TIMU ya wasichana ya Super Girls imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Mkoa wa Lindi baada ya kuichapa FC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika michuano hiyo, Mpiruka Queens iliweza kuibuka mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kipara Queens 2-1.

  Katika mchezo wa fainali, Super Girls walianza kwa kasi na kuliandama lango la wapinzani wao tangu dakika za mwanzo lakini ilibidi kusuburi hadi dakika ya 15 ili kuandika goli la kwanza. Goli hilo lilofungwa kwa ustadi na mchezaji Ashura Mfaume baada kungongeana vizuri na Tatu Makota. 

  Baada ya bao hilo, Super Girls waliendelea kutandaza kandanda safi na kufanikiwa kufunga bao la pili dakika ya 18 lilifungwa tena na Ashura Mfaume baada ya kuwalamba chenga mabeki watatu wa FC Vito Malaika. Bao la tatu lilifungwa na Alia Fikiri mnamo dakika ya 22 baada ya mabeki wa FC Vito kushindwa kuokoa mpira wa kona.

  Timu ya FC Vito Malaika walipata bao lao pekee katika dakika ya 27 baada ya mchezaji Sarah Isaac kuachia shuti kali na mpira kujaa moja kwa moja wavuni. Hadi mapumziko, Super Girls 3 FC Vito Malaika 1.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikasaka bao lakini ilikuwa ni Super Girls waliopata goli dakika ya 63 baada ya mchezaji Tatu Makota kufunga kwa penati baada ya beki wa FC Vito Malaika kunawa mpira kwenye eneo ya hatari.

   Akiongea kwenye fainali wa michuano hiyo,mgeni rasmi Hadja Sekibo ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Nachingwea aliwapongeza kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la wanawake nchini. ‘Nachukua nafasi ya kuwapongeza wenzetu wa Airtel kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye soka vijana wetu sana sana kwa wasichana. 

  Tunatambua soka ni ajira, lakini kuwapa hawa vijana wetu wa kike nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, mnawafungulia milango ya kuonekana nchini nzima na pia kunawafanya kutoweza kujiingiza kwenye makundi yenye malengo mabaya kwani muda wao wa ziada wanatumia kucheza mpira. Kwa hivyo wanapongeza kwa kuweza kuunga mkono jitihada za serikali za kuwawezesha vijana kujiajiri’, alisema Sekibo.

  Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Lindi Ally Mkadeba alisema michuano ya Airtel Rising Stars imewawezesha kupanua wingo wa kutafuta vipaji vya soka mkoani na kufikia maeneo mengi ambayo bila Airtel Rising Stars wasingeweza kufika. Mkadeba aliongeza kuwa wakati wa michuano hiyo, makocha waliweza kuchangua wachezaji 16 ambao hana uhakika kuwa watawakilisha vyema Mkoa wa Lindi kwenye fainali za michuano hiyo ambazo zitafanyika Dar es Salaam kuanzia Septemba 6-11.

  0 0

  Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), akisimamia kazi hiyo leo Septemba 3, 2016.

  NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
  WAHANDISI, na mafundi wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na wale wa kampuni za Kijapani za Yachiyo Engineering Co Limited, Takaoka na National Construction Co. Limited, wameanza kazi ya uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, imeanza leo Septemba 3, 2016.

  Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.

  “Ikumbukwe kwamba, hapa tulikuwa na laini mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila moja, kutoka hapa Ubungo kwenda kituo cha Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye Megawati 220 kila moja,” Alifafanua Meneja Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.

  Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii itawezesha umeme utakaokuwa ukisafirishwa kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na jumla ya Megawati 440 kwa laini zote mbili, tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu,” Alisema.

  Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio bora, alifafanua Injinia Bayona.

  Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake,.

  “Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi katika mazingira salama, tutakuwa tukikata umeme kuanzia leo hii Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.” Alifafanua Leila, na kuwaomba wananc hi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.

  Mradi huu ulioanza Februari 2015 na unaotarajiwa kukamilika Juni 2017 unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).
  Fundi wa TANESCO, akifunga kikombe wakati wa kazi ya kubadilisha miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kituo kikuu cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam
  Raphael Mjata, Msimamizi Mkuu wa Njia Kuu za Umeme, akionyesha uwezo wa kituo cha Ubungo cha kupooza umeme wenye kilovolti 132.
  Mafundi wa TANESCO na kampuni ya National Construction Company Limited, wakivuta nyaya hizo mpya.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Injinia Everist Ndikilo akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidi mtambo wa kisasa unaotengeneza hewa ya oxygen kwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha Mkoani Pwani. Mtambo huo umetolewa na kampuni ya Oxymat AS- Denmark kwa kushilikiana na wasambazaji KaMpa health products Ltd, Tanzania na Pulse health care Limited, Kenya.
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Injinia Everist Ndikilo akipatiwa maelezo ya namna mashine hizo zinavyofanya kazi kwa binadamu.
   Sehemu ya mashine hizo.


  0 0

   Honarable Dk. Auustine Mahinga.
  Group Photo.


  STATEMENT BY HONOURABLE DR. AUGUSTINE P. MAHIGA (MP), THE MINISTER OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (URT) AND HEAD OF THE SADC ELECTORAL OBSERVATION MISSION (SEOM) TO THE 2016 NATIONAL ASSEMBLY ELECTIONS IN THE REPUBLIC OF THE SEYCHELLES.
  It is my honour and privilege to welcome you to the official launch of the SADC Electoral Observation Mission (SEOM) to the 2016 National Assembly Elections in the Republic of the Seychelles.  

  On behalf of His Excellency Dr John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania (URT) and the Chairperson of the SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation, and indeed on my own behalf, please accept my sincere gratitude for taking time to be part of this auspicious occasion. 

  Distinguished guests 
  Ladies and Gentlemen,

  Our Mission to the Republic of the Seychelles was at the invitation of the Electoral Commission of the Republic of the Seychelles.  This practice is now part of our democratic culture and tradition in the SADC region and is in conformity with the SADC Treaty; the SADC Protocol on Politics, Defence and Security Cooperation and the revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections (2015).

  To this end, His Excellency Dr John Pombe Joseph Magufuli, President of the Republic of the United Republic of Tanzania (URT) and Chairperson of the Organ on Politics, Defence, and Security Cooperation, constituted the SADC Electoral Observation Mission (SEOM) and mandated the Executive Secretary of SADC to prepare the logistics for its deployment. 

  It is noteworthy, that a substantial amount of effort has already been invested in the preparations for this important Mission, beginning with the ground work undertaken by the SADC Secretariat, the SADC Electoral Advisory Council Goodwill Mission, the Troika and other stakeholders, to ensure the realisation of the objectives and mandate of the SADC Electoral Observation Mission.

  In this respect, it is significant to note that these National Assembly Elections in the Republic of the Seychelles build on an enduring culture among SADC Member States of consolidating democratic practice and institutions through, inter alia, the observation of national elections. 

  Over the last two decades, SADC has developed and enhanced its normative frameworks governing democratic elections which have contributed immensely to our endeavour as a region to work toward the realisation of the vision of the SADC Treaty (1992). 

  You will recall that on 20 July, 2015, the Ministerial Committee of the Organ adopted the revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections, which aim to strengthen our skills and capabilities of assessing the major inter-related segments of the electoral cycle in order to provide stronger evidence-based recommendations and electoral assistance to Member States. 

  Our revised set of Principles and Guidelines also require us to operationalise several stages to our deployment strategy which allows us to have a much better understanding of pre-election, election and post-election phases of the electoral process. The inter-related phases of deployment include the SADC Electoral Advisory Council Goodwill and pre-election assessment Missions; and the deployment of the Long Term Observers (LTOs); and the Short Term Observers (STOs).

  The arrival of the SADC Electoral Advisory Council Goodwill Mission on 22 August 2016 ahead of the main Short Term Electoral Observation Mission of the SADC Electoral Observation Mission, therefore, signifies this enhanced approach to election observation, which will eventually build our capacity to develop and sustain Long Term Election Observation (LTO) Missions, as provided for in the revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections.

  We are, hence, informed by the SADC Electoral Advisory Council Goodwill Mission that the Electoral Commission of the Seychelles has undertaken a range of activities as part of the preparations for these National Assembly Elections. We have also taken note of the issues raised at this preliminary stage by the various stakeholders regarding these preparations and management of the electoral process. We shall therefore, through the SADC Electoral Observation Mission, consolidate this body of information in order to arrive at a considered assessment of the electoral process at the end of our Mission. 

  Distinguished guests 
  Ladies and Gentlemen,

  Let me reiterate that the work of the SADC Electoral Observation Mission is guided by the revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections adopted in 2015, which are aligned to the African Charter on Democracy, Elections and Governance (2007). In addition, the work of the SADC Electoral Observation Mission is also guided by the relevant legislation of the Republic of the Seychelles, such as her Constitution which outlines the principles of universal adult suffrage, and defines the electoral systems and processes; as well as by the country’s Electoral Laws. The emphasis of course, shall be on the provisions addressing the election of Members of Parliament. 

  Informed by these inter-related regional and national frameworks, the SADC Electoral Observation Mission will assess the conduct of the elections against a set of central principles stipulated in the revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections such as:
  1.Full participation of the citizens in the political process;
  2.Freedom of association;
  3.Political tolerance;
  4.Equal opportunity for all political parties to access the state media;
  5.Equal opportunity to exercise the right to vote and be voted for;
  6.Independence of the Judiciary and impartiality of the electoral institutions; 
  7.Civic and Voter education; 
  8.Acceptance and respect of the election results by political parties as proclaimed to have been free and fair by the competent  Electoral Commission in accordance with the law of the land; and
  9.Challenge of the election results as provided for in the law. 

  Distinguished guests, 
  Ladies and Gentlemen,

  Allow me to further explain the role of the SADC Electoral Advisory Council whose arrival preceded that of the SADC Electoral Observation Mission. You will recall that the SADC Electoral Advisory Council was established by the SADC Heads of State Summit in 2005 to advise on matters of elections, democracy and good governance.  The SADC Electoral Advisory Council is composed of eminent Justices, senior advocates and distinguished scholars with immense experience in matters of democracy building and governance. As is the culture, the objective of the SADC Electoral Advisory Council Goodwill Mission was to assess the level of readiness and preparedness of the Republic of the Seychelles to hold these elections. 

  We are, hence, reliably informed by the SADC Electoral Advisory Council Mission that the Electoral Commission and the relevant stakeholders in the Republic of the Seychelles have taken necessary measures to ensure that the Principles for Conducting Democratic Elections as outlined in the revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections, are observed. We therefore conclude that the Republic of the Seychelles is generally prepared to hold elections on 8-10 September, 2016.

  Esteemed guests,
  Members of the Media,
  Ladies and gentlemen,

  As SADC observes these elections, it encourages the Electoral Commission of the Seychelles to conduct its work to the highest professional standard; the political leadership to play an exemplary role in terms of electoral conduct; and the electorate to act conscientiously and honourably. 

  As the SADC Electoral Observation Mission, we are hopeful that the deployment of our observers will contribute to enhancing the credibility of the overall electoral process.

  As a region, we have made great strides in ensuring participation of citizens in decision making, as a part of our efforts to promote democratic values, practices and strengthening institutions of democracy.   

  It is notable that our Member States continue to develop Constitutions that enshrine principles and provisions of equal opportunities and full participation of all citizens in democratic processes. In the Republic of the Seychelles, the National Assembly Elections are regulated by the Constitution, the Elections Act, the Political Parties Act (2014) and the Electoral Code of Conduct acceded to by all Political Parties.

  Furthermore, the Constitution of the Seychelles underscores the need to ensure that the electoral procedures, among other aspects, guarantee citizens the liberty to exercise their political rights. It also recognises universal adult suffrage based on the equality of a vote. 

  The country’s laws also recognise the need for the holding of elections that are free from violence, intimidation and corruption, and the timely resolution of electoral disputes. It is in light of this that we appeal to all Seychellois, that should there be any areas of disagreement, they should follow the laid down procedures, as provided for by the laws of the land. 

  Having said all this, I am pleased to inform you that the SADC Electoral Observation Mission to the 2016 National Assembly Elections is now fully constituted and comprises 19 observers from 8 SADC Member States. 

   As the voting days of the 8-10th September, 2016 approach, allow me to mention that the outcome of this election lies in the hands of the people of the Republic of the Seychelles. The manner in which they conduct themselves will determine the outcome of this election. As alluded to earlier, we strongly call upon the political stakeholders to strictly adhere to all relevant legislation governing the elections in the Republic of the Seychelles, which are provided for in the country’s statutes.

  We also urge all political parties to adhere and accept the results of the elections and lodge their complaints and grievances through the relevant institutions.

  May I, therefore, take this opportunity to encourage all stakeholders to ensure that these National Assembly Elections are managed in a peaceful, free, fair, transparent and credible manner; and that the electoral process adheres to democratic values and principles; and commend all the stakeholders, for their efforts in putting in place an enabling environment for holding these Elections.

  Lastly, may I also take this opportunity to invite you all to attend the release of our Preliminary Statement scheduled for 12 September 2016, at 1100hrs, at this very venue. 

  Distinguished guests,
  Ladies and Gentlemen,

  It is now my singular honour, on behalf of the Chairperson of the Organ on Politics, Defence and Security Cooperation, His Excellency Dr John Pombe Joseph Magufuli, President of the Republic of the United Republic of Tanzania (URT), to declare the SADC Electoral Observation Mission to the 2016 National Assembly Elections in the Republic of the Seychelles, officially launched. 

  0 0

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akifanya mazungumuzo na mmiliki wa chuo cha Mount Eagle College &University Dr. Lucas Shallua siku ya Ijumaa Septemba 3, 2016 Balozi Wilson Masilingi alipotembelea chuo hicho kilichopo Winston Salem, North Carolina.
   Mazungumuzo yakiendelea, wengine katika kufuatilia mazungumuzo hayo kutoka kushoto ni ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Dr. Dorothy Edward Shallua (mke wa Dr. Lucas Shallua), Mke wa Balozi Marystela Masilingi, na mwenyeiki wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.
   Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akimsikiliza Dr. Lucas Shallua (kulia) alipokua amkitembeza na kumwonyesha chuo cha Mount Eagle College & University kilichopo mji wa Winston Salem, North Carolina. Wengine katika picha kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex, Mke wa Balozi Bi. Marystela Masilingi, nyuma ya Balozi asiyeonekana ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana na Mke wa Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua.

  Chuo cha Mount Eagle kinatoa unafuu kwa Mtanzania anayetaka kujiunga katika masomo ya Unesi na ugawaji dawa na chuo hicho kwa kukuwezesha wewe kufanyakazi hospitanini au kwenye maduka ya dawa pia wanamsomo ya mtandaoni kwa bei nafuu. Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na Dr. Lucas Shallua barua pepe Lshallua@mounteag.com 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1342 | 1343 | (Page 1344) | 1345 | 1346 | .... | 3285 | newer