Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1338 | 1339 | (Page 1340) | 1341 | 1342 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Meneja wa Bendi ya Dar Music, Khamis Maero (Katikati)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha wasanii wapya wa bendi hiyo pia amesema kuwa wafanya uzinduzi wa Albamu yao Septemba 16 mwaka huu katika ukumbi wa Mango Gaeden Jijini Dar es salaam.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  BENDI ya Dar Music inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 16 huku uzinduzi huo ukisindikizwa na Malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na bendi ya Msondo.

  Uzinduzi huo utaenda sambamba na utambulisho wa albamu ya bendi hiyo iliyobeba nyimbo 6 pamoja na video ya wimbo wao wa Chozi la Maskini.

  Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja wa bendi hiyo Khamis Maero amesema kuwa uzinduzi huo mkubwa unafanyika kwa mara ya kwanza toka Rais mpya Jado Fideforce aingie madarakani na kutambulisha wanamuziki wapya waliojinga na bendi hiyo.

  Kwa upande wake Fide Force amesema kuwa nyimbo zitakazotambulishwa katika uzinduzi huo ni pamoja na wimbo uliobeba albamu yao ya Chozi la Maskini pamoja naSalmaga.

  Nyimbo nyingine ni Bongo mchango, Maisha Upendo, Mtu Box, Jibebishe  na Ama zao Ama zangu.

  "Ndani ya bendi yangu nimeamu kuchukua wanamuziki wazuri ili kuhimili ushindani uliopo katika tasnia ya muziki kutokana na ushindani uliopo" amesema Fideforce.

  Fideforce kuwa ana uzoefu mkubwa na kile kinachopelekea bendi nyingi kuvunjika hivyo hawawezi kuruhusu kitu hicho kitokee ndani ya bendi yao.

  "Uzuri ni kwamba ninaelewa muziki wa bongo ulivyo na nini huwa kinafanyika na kipi cha kuepuka ili bendi kutovunjika" , amesema Fideforce.

  0 0

  Na Abushehe Nondo na Sheila Simba - MAELEZO.


  Serikali imesema kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini. 
  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT) 

  Mbarawa alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

  “Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa Mbarawa.

  Mbarawa aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.

  Aliongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.

  Prof. Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa safari moja.

  Waziri Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na  Kampuni hiyo.

  Mpaka sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19 septemba mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15 septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.

  Akizindua mafunzo hayo ya wakufunzi wa  marubani, Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo  kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.

  “Hatutaki kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu,hakikisheni mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro lakini bado anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof.Mbarawa.


  Aidha amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za urubani ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini.   0 0

   Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  anayesimamia sekta Mawasiliano mhandisi Dkt. Maria Sasabo kushoto akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano, kulia ni Katibu wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano  Bi. Mary Shao Msuya.

   Mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bw. Stanley Mwabulambo akimkaribisha mgeni rasmi  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo kuzungumza na wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano 

   Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za Msingi  Jane Michael Andrew  kutoka shule ya msingi ya Mbuyuni akipokea zawadi ya cheti ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
   Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu Bw. Omari Abbas kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Ualimu (DUCE) akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt.   Maria Sasabo.

  Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za sekondari Bw, Ramadhani Mohamed kutoka Shule ya sekondari ya Kibasila  akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo. 


  0 0

  On Friday 26 August 2016 at  Kilwa Masoko in Lindi Region the the European Union (EU) Representative and Head of Finance and Contracts, Mr. Hans-Juergen Scheck, the French Representative of the Head of Cooperation and Cultural Affairs, Ms. Franca Berthomier, together with the District Planning Officer, Mr. Francis Kaunda on behalf of the District Commissioner of Kilwa, participated in a closing ceremony of the Kilwa cultural heritage project.  

  The three year project implemented in Kilwa with the support of the European Union and the Government of France has been completed. Titled “Promoting Heritage Resources in Kilwa to strengthen social and economic development”, the project aims to identify, protect and promote heritage resources in Kilwa, Southern Tanzania.
   The EU Representative, Mr. Hans-Juergen Scheck, the Vice-Chairman of the French urban community of Rochefort-Océan, Bruno Bessaguet, the French Representative, Ms. Franca Berthomier, the Chairman of the NGO CRAterre, Thierry Joffroy and Kilwa Local Project Coordinator, Ms. Tatu Magina listening to one of the tour guide, Ms. Jamila Mpoka after the event.
   Holding the project catalogue titled 'Karibu Kilwa' is the Chairman of Kilwa Islands Tour and Information, Mr. Abdalah Ahmadi.

  0 0

  Jumatatu jioni  umoja wa familia za Watanzania waishio UK almaarufu kama THE BIG FAMILY walitembelea nyumbani kwa mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Chris Lukosi (aliyekaa chini)  na mkewe Adela Lukosi huko Reading, Uingereza, kuhani msiba wa  Mama mkwe wake Bibi Mkami, aliyefaririki tarehe Agosti 2, 2016 jijini   Dar es salam  na kuzikwa tarehe Agoisti 4, 2016 kijijini Image mkoani Iringa. 
   Adela Lukosi (aliyekaa chini akiwa na THE BIG FAMILY waliofika kuhani msiba wa  Mama yake mzazi  Bibi Mkami, aliyefaririki tarehe Agosti 2, 2016 jijini   Dar es salam  na kuzikwa tarehe Agoisti 4, 2016 kijijini Image mkoani Iringa
   THE BIG FAMILY wakibadilishana mawazo kwa wafiwa
    THE BIG FAMILY wakiwa  kwa wafiwa
  THE BIG FAMILY wakiendeleza utamaduni wa kuwa pamoja wakati wa shida na raha.

  0 0

  Viongozi Wakuu pamoja na Sekretieti ya Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wake. Katikati  mwenye suti ni Waziri Mkuu wa Mauritius Sir Anerood Jugnauth. 
  Ujumbe wa Tanzania walioshiki Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid katikati kulia Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mussa Zungu  na kushoto Dk Raphael Chegeni.Kutoka kushoto Maryam Rajab, Mbarikiwa Masinga, Mhe,Maria (MB) Mhe. Raphael Chegeni (MB)Mhe Juma Hamad Omar (MB) Mhe Simai Mohammed Said (BLW)  Aziza Makwai.  
  Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said, akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo juu ya  Suala la Nishati kwa Bara la Afrika, uliofanyika nchini Mauritius, Balaclava. 
  Spika wa Baraza la Wawkilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe kutoka Tanzania wakishirika katika Mkutano huo wakifuatilia Mada zinazowasilishwa na Wajumbe wakati wa Mkutano huo nchini Mauritius.  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016. 
   2016.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza  balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016.


   Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Adelhem Meru akisalimiana na balozi wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo kabla ya kufanya naye  mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (aliye nyuma).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya  mazungumzo na balozi wa Cuba Mhe Jorge Lopez Tormo nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC- ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dkt. Seretse Khama Ian Khama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.
  Rais huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI anawakilishwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.
  Amesema ana Imani kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.

  Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.
  Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika).
  Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini ubao wa kumbukumbu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wenye majina ya viongozi waliohudhuria mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika Lozitha, Mbabane Swaziland.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Mandvulo uliopo Lozitha, Swaziland.
  Mfalme Mswati wa III (kushoto) akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwenye ukumbi wa Mandvulo, Lozitha Swaziland.
  Binti akionyesha bendera ya Tanzania wakati wa kuimba shairi maalum ya ufunguzi wa mkutano wa 36 wa SADC
  Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa  Afrika (SADC) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 36, Lozitha Swaziland.
    ....................................... 
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) juu Maadhimisho ya kilele cha miaka 52 ya jeshi hilo.
   Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ),Kanali Ngemela Lubinga(aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kazi mbalimbali watakazozifanya katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi hilo. 
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisalimiana namakamanda wa Jeshi la Ulinzila Wananchi wa Tanzania JWTZ, alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016. JWTZ itaadhimisha miaka 52 kwa kufanya usafi kote nchini.


  Na Bakari Issa Madjeshi, Globu ya Jamii

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linatarajia kuadhimisha siku ya kilele cha miaka 52 tangu kuzaliwa kwake kwa kufanya usafi wa mazingira sambamba na uchangiaji wa damu.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokutana na Maafisa wa Jeshi hilo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema JWTZ inapotimiza miaka 52 ni fahari kubwa hivyo tunapaswa kuwapongeza kwa kudumisha amani na mshikamano,kusaidia mataifa mbalimbali pamoja na kulinda mipaka ya nchi.

  Makonda amesema kuwa Wananchi wanapaswa kuungana nao katika kazi mbalimbali wanazofanya katika mkoa wa Dar es Salaam.

  "Wakuu wa Wilaya wamejipanga kuainisha maeneo ambayo yatafanyiwa usafi hivyo kama kuna mwananchi anataka kushiriki nao usafi na Wanajeshi siku ya kilele, Septemba mosi basi asubuhi na mapema waripoti kwa Wakuu hao wa Wilaya na watapangiwa jinsi gani wataweza kushirikiana nao"amesema Makonda.

  " Pia wamekubali kuchangia Damu hii itasaidia kutokana na mahitaji ya Damu ni makubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia hospitali za Mwananyamala, Temeke na Amana"ameeleza Mkuu wa Mkoa huyo wa Dar

  Pia ametoa wito kwa wananchi wapenda amani kujitokeza kwa wingi kuchangia damu katika maeneo ya Lugalo, JKT Kawe na maeneo mengine ya kambi yenye vituo vya uchangiaji damu.

  Akithibitisha kuwepo kwa Maadhimisho ya kilele cha miaka 52 ya JWTZ, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema Mkuu wa Majeshi amefarijika kushiriki kikamilifu katika shughuli zao za kuadhimisha miaka 52 ya Jeshi hilo.

  Kanali Lubinga amesema wamefarijika kuona Mkoa wa Dar es Salaam umeshiriki nao katika shughuli mbalimbali za Jeshi hilo ikiwemo shughuli za usafi.

  "Siku hiyo ya kilele shughuli zetu zitakuwa ni utoaji damu, kufanya usafi kutokana na usafi ni afya na ni amani" amesema Kanali Lubinga

  Amesema kutakuwa na Madaktari wa Jeshi watakao toa huduma za ushauri kwa magonjwa mbalimbali kama Kisukari pamoja na Shinikizo la Damu sambamba na kushiriki Michezo.

  Pia amesema Ndege za kivita zitakuwa zitapita kuashiria siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi hilo.

  0 0


  0 0  Sehemu ya Agizo la Mahakama.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) akimjulia hali mwanafunzi wa Darasa la 4 wa Shule ya Msingi ya Mount Kibo ya Mbezi Beach ya Jijini Dar es Salaam, David Kamoga, anayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba, Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI),  baada ya kujeruhiwa kwa kugongwa  na gari aina ya Hiace eneo la Tegeta, Namanga, Jijini Dar es salaam. Kulia ni baba wa mtoto huyo, Bw. Hudson Kamoga ambaye ni mtangazaji wa Clouds TV. (PICHA  NA KHAMISI MUSSA)


  0 0
 • 08/30/16--14:14: Events in france


 • 0 0
 • 08/30/16--14:15: Article 13

 • 0 0
 • 08/30/16--21:00: TANZIA MWANZA
 • Familia ya bwana na bibi Rutegama Robert wa Nkuhungu Dodoma inasikitika kutangaza kifo cha shemeji yao mpendwa Ruben Kabuti (pichani) kilichotokea ghafla leo asubuhi katika hospital ya Kamanga, Nyegezi,  Mwanza. 
  Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ngudu, Kwimba, Mkoani Mwanza, siku ya Alhamis  ya Septemba 1, 2016.
  Habari ziwafikie ndugu, jamaa marafiki na jirani wa marehemu  popote pale walipo.

  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA. JINA LAKE NA LIHIMIDIWE 
  AMINA

  0 0
 • 08/30/16--23:00: Article 11


 • 0 0


  0 0


  0 0

  KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge/mlongo/ mronge, mrongo/mkimbo au mzunze (kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera ) unaweza kuwa unaongoza. 

  Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu ingawa kwa bahati mbaya sana huenda wengi hatuujui ima tunaujua na kuupuzia. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu.
  Profesa Mmoja wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) amenukuliwa akisema   “imethibitishwa na kufanyiwa utafiti  kupitia Idara ya Sayansi na Chakula iliyopo SUA na kugundua kuwa mti wa mlonge ni mti muhimu sana katika jamii na una faida nyingi.”....

  Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume.

  Mbegu za Mlonge hutibu maradhi pia kama Malaria, Saratani ya tumbo, hupunguza sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji, jambo amabalo ni adimu kwa watu wengi

  Faida nyingine  itokanayo na unga wa majani ya mti wa mlonge ni kusafishia maji ambayo ni machafu na kuweza kuwa safi na salama na kuwa tayari kwa matumizi yoyote ya nyumbani kama vile kupikia na kunywa,  hii inaweza kuwa ni mbadala ya madawa mengine yanayoweza kutibu maji kama vile watergard na mengineyo.

  Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwasababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu. Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi.

  Majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.

  Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.
  Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
  -Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
  Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.

  -Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.

  -Waweza kutumia majani kama unavyotumia mchaichai na hapo unatibu MALARIA bila kujua.......Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi (zingatia usikaushe kwenye JUA)
  ​Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.

  Licha ya kuwa dawa nzuri sana ya kusafisha tumbo (Jaribu kutafuna mbegu zake tatu baada ya kumenya huku ukinywa maji mengi sana na kuhakikisha upo jirani na choo) Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.

  Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.

  Magome

  Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung'atwa na wadudu kama nyoka na nge. mmea huu pia ni MBOLEA 

  ...........HIZI NI BAADHI TU LAKINI WAWEZA JISOMEA ZAIDI KUPITIA VYANZO MBALIMBALI ..............

  Ndugu tuna tabibu mbalimbali, za asili na zisizo na madhara kama ya vidonge vya makemikali na bado tunapuuza.
  Nimekuwa nikiusikia huu mmea leo umepata undani matumizi yake.

  ni zao zao rahisi kupanda unapanda umbali wa mita 3 unapanda punje mbili kila shimo ikiota vizuri unang'oa moja baada ya miezi 9 inaanzakuzaa unavuna x2 kwa mwaka mlonge unazaa sana ila kung'oa mlonge sio kazi rahisi una kiazi ambacho hakifi

  imeandikwa na Geofrey Chambua kutoka vyanzo mbalimbali​

  0 0

  SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha 


  Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa

  Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .

  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo amewataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

  Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya.

   Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia. 

   Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune 
   Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi. 
   Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi . 
   Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi . 
  Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog, Mbarali, Mbeya . 

older | 1 | .... | 1338 | 1339 | (Page 1340) | 1341 | 1342 | .... | 3283 | newer