Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1333 | 1334 | (Page 1335) | 1336 | 1337 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Meneja wa kampuni ya Jumo Tanzania, Rweb Mutahaba akizungumza na Mawakala wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel mbinu za kukuza biashara na kuongeza mtaji kupitia huduma ya Airtel Timiza katika semina iliyofanyika jijini Arusha.
  Mmoja wa mawakala wa kampuni ya Airtel jijini Arusha,David Lima akiuliza swali wakati wa semina iliyotolewa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na washirika wake Jumo kuhusu huduma ya Airtel Timiza inayowapatia wateja na mawakala nchi nzima mikopo isiyona dhamana kupitia simu zao za mkononi.
  Mmoja wa mawakala wa kampuni ya Airtel jijini Arusha,Chihiyo Malick akizungumza wakati wa semina iliyotolewa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na washirika wake Jumo kuhusu huduma ya Airtel Timiza inayowapatia wateja na mawakala nchi nzima mikopo isiyona dhamana kupitia simu zao za mkononi.

  0 0

  Mmoja ya Fundi gereji katika Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Bw. Mohamed Ali akielezea sababu za wao kuvamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (hayupo pichani).
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza kwa makini Afisa Ardhi toka Manispaa ya Ilala Bw. Furaha Mwakapalila akielezea historia ya eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex ambalo kwa sasa limevamiwa na mafundi magari wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
  Afisa Tarafa wa Ukonga Bw. Jeremiah Makorere akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya waziri huyo kubaini migogoro mbalimbali ya ardhi katika eneo la Pugu Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) abdulmalik mollel amesema wanafunzi wanaokwenda vyuo vya nje ya nchi ni 350 kwa masomo ya utabibu, uhandisi, pamoja na biashara.

  Akizungumza na wazazi na wanafunzi jana katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam, juu safari hiyo ,Mollel amesema kila kitu kifanyike kwa utaratibu ili kuondoa usumbufu wakati safari hiyo kwa wanafunzi hao.

  Amesema wanafunzi hao wanakwenda huku tume ya vyuo vikuu nchini (TCU), ikiwa inatambua vyuo hivyo na kuwataka wazazi kuondoa hofu juu ya vyuo wanavyokwenda kusoma.

  Aidha amesema Global Education Link (GEL), iko tayari kuhakikisha nchi inapata vijana wanapata elimu bora katika vyuo vya nje.

  Amesema kuwa kusoma nje sio anasa kutokana na mahitaji yaliyopo vijana wanatakiwa kupata utaalam tofauti tofauti ili kuweza kufikia uchumi wa kati was viwanda.
  Sehemu ya wazazi na wanafunzi na wazazi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel hayupo pichani katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.


  Sehemu ya wafanyakazi Global Education Link (GEL), wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi juu ya safari wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vya nje ya nchi katika mkutano uliyofanyika jijini Dar es salaam.
  Mbunge wa Mfindi Kusini, Meadrad Kigola akichangia katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. 

  0 0


  0 0

  Watanzania wameshauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili katika ulimwengu wa uandishi ili kuutangaza Utamaduni wa nchi.

  Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).

  Mkurugenzi amesema kuwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na kuenzi juhudi za kuenzi na kuendeleza juhudi za watetezi za masuala ya lugha wa masuala ya Lugha na Utamaduni wa mtanzania.

  Ameongeza kuwa Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa imeandaa kanuni za Sheria ya BAKITA ya mwaka 1967 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni ambayo itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili waandishi hapa nchini pamoja na haki zao katika kuendeleza fani mbalimbali za Lugha.

  “Katika azma ya kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa Rais wetu Mhe.Dkt John Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika hotuba zake mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat Shani.

  Kwa upande wake mmoja ya wajumbe wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa katika risala yao kwa mgeni rasmi amesema kuwa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania(UWARIDI) wameamua kutafuta njia ya kurudisha, kutetea, kulinda na kuipandisha heshima yetu kama waandishi na heshima ya kazi zetu zote.

  “Tumeamua kutafuta mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu zinatambuliwa rasmi kiserikali na kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja wetu ambao utakuwa na sauti katika kutetea haki za waandishi na kazi zao alisisitiza Bi. Matilda.

  Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) umeanzishwa kwa lengo la kuwatetea waandishi wa Riwaya nchini ili waweze kunufaika na kazi zao.
  Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
  Rais wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw. Hussein Tuwa akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Ibrahim Gama akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu Umoja wao wakati wa uzinduzi wa Umoja wa huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.


  0 0

  Bibi Sarah Cooke, Balozi mpya (Mteule) wa Uingereza nchini Tanzania amewasili jana 25 Agosti, 2016 Dar es Salaam.

  Bi. Cooke amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi.Dianna Melrose (ambaye amestaafu) na ni mwanamke wa tatu kushika nyadhifa ya ubalozi kuiwakilisha Uingereza nchini Tanzania.

  Bi Cooke alijiunga na Utumishi Uingereza mnamo mwaka 2002. Alifanya kazi kadha wa kadha katika idara za Serikali ya Uingereza ikiwemo Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID), Wizara ya Mambo ya Nje na Kitengo cha Mikakati cha Waziri Mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri. Pia alipata kuhudumu kama Makamu Mkuu wa Tume ya Sekretariati ya Africa. 

  Hivi karibuni, alikuwa ndiye Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (DFID) nchini Bangladesh. Kabla ya kujiunga Utumishi katika Serikali ya Uingereza, alipata kufanya kazi kama Mchumi jijini London, Guyana na visiwa vya Solomoni.

  Juu ya uteuzi wake, Bi.Cooke alisema; “Nimefurahi na ni heshima kubwa kwangu kupewa jukumu hili jipya kama Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Uingereza na Tanzania inafurahia mahusiano na ushirikiano wa muda mrefu na kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ambayo tunashabihiana katika vipaumbele ikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo na usalama. Nina dhamiria kuimarisha ushirikiano huu bora zaidi na nina taraji kuijua vyema Tanzania na watu wake”

  0 0

  Mwenyekiti wa UDP Mh. John Cheyo akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar,akiwaomba viongozi wa chama cha CHADEMA,Kusitisha maandamano yao waliyoyapa jina la UKUTA,wanayotarajia kuyafanya Septemba Mosi nchi nzima,Mh Cheyo amekiomba chama hicho kutofanya maandamano hayo kwa lazima na badala yake watumie njia ilio sahihi ambayo ni ya mazungumzo ya mezani na kuendelea kuitunza amani ya nchi iliopo,pia amewaomba Watanzania kupaza sauti zao kuyakataa maandamano hayo yanayoweza kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu.Pichani kulia ni Kaimu Katibu MKuu wa chama hicho Mh,Goodluck Ole Medeye.

  "Ukitaka kufanya maandamano,vyombo vya usalama vikikukatalia,basi usitumie nguvu,jaribu kutafauta njia nyingine ambayo itakuwa ya amani zaidi kuliko kulazimisha,jambo ukililazimisha bila kufuata taratibu na sheria za nchi,matokeo yake hayatakuwa mazuri,yataleta machafuko na kutia doa amani ya nchi yetu ambayo tumekuwa tukijivunia,hivyo nawasihii ndugu zangu wa CHADEMA bado kuna njia nzuri za kufuata na kufikia muafaka wa jambo hilo bila kusumbua amani ya nchi yetu iliopo kwa sasa" alisema Mh Cheyo.
  Mh,Cheyo akisitiza jambo wakati alipokuwa akijiabu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kukitaka chama cha CHADEMA kusitisha maandamano yake,kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO,Vicent Tinganya.PICHA NA MICHUZI JR.


  Na: Lilian Lundo-MAELEZO
  Dar Es Salaam

  Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia (CHADEMA).

  Cheyo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.

  “Watanzania wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.

  Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.

  Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.

  Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.

  Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.

  Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote. Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.

  0 0

  Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa, Mwandishi Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amepata ajali mapema asubuhi ya leo, na kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu. Ajali hiyo imehusisha gari alilokuwa akiendesha yeye aina ya Benz na gari nyingine iliyoigonga gari hiyo upande wa Ubavuni.

   Tutaendelea kuwaletea taarifa kadri zitakavyotufikia.

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) wakionesha ujumbe wa maadhimisho mara baada ya kuzindua hafla ya maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki. Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) wakionesha ujumbe wa maadhimisho mara baada ya kuzindua hafla ya maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki. Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo akizungumza na walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day', Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (mwenye gauni jeusi) ambaye ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa NMB kwenye maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki. Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando (mwenye gauni jeusi) ambaye ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa NMB kwenye maadhimisho ya siku ya walimu 'Teachers Day'. Benki ya NMB imewakutanisha walimu katika maadhimisho hayo na kuwapa semina ya masuala anuai ya kibenki.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume ya taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt Stephen Nindi ( Kulia ), akikabidhi Mpango wa miaka 20 wa Matumizi Bora ya Ardhi wa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mpango huo umelenga kutunza mazingira na Bio anuai Zilizopo nchini pamoja na kumnufaish Mwananchi wa Kipato cha kawaida. 
  Kiongozi wa Urasimishaji kupitia Programu ya LTSP, iliyo Chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi SAGWILE MSANANGA akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuwezesha Umilikishaji Ardhi kwa Wananchi pamoja na Vijiji Vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani MOROGORO. 
  Mratibu wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Wilaya za MALINYI, KILOMBERO na ULANG, Godfrey Machabe aliyevaa Tai Shingoni, akimsikiliza kwa Umakini Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Sagwile Msananga alipokuwa akielezea kuhusu Programu ya LTSP, kwa Washiriki wa Mafunzo ya Kuwezesha Umilikishaji wa Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani MOROGORO. 
  Kaimu kamishna wa Ardhi nchini Bi Mary Makondo ( katikati), akimsikiliza Katibu tawala wa Wilaya ya ULANGA mkoani Morogoro Ndugu Abraham Mwaivile aliyevaa Koti la Rangi ya Kijivu akisisitiza Jambo kwa Washiriki wa mafunzo ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Halmashauri hiyo, ambapo zoezi la Upimaji Mipaka ya Vijiji na Utoaji hatimiliki za Ardhi litafanyika.  0 0

   Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akionesha albamu yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mkutano wa kutambulisha uwepo wake katika Tamasha linalozinduliwa jijini Dar es salaam siku ya kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam.
    (Kutoka kulia) Mkurugenzi wa Stra8up Vibes, Sniper Mantana ambao ni waandaaji wa Tamasha la “Monte Carlo Classic’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) pichani wakati wa kumtambulisha Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama ‘Kiss Daniel’atakayepamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera, Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, mbia wa Tamasha hilo kutoka Malaysia DeJurist Global na Meneja wa Msanii huyo Louiza Williams.
   Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera akizunguzmza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumtambulisha Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel atakayepamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
   Mmoja wa washiriki katika uandaaji wa Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist Global kutoka Malaysia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kumtambulisha msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye yupo nchini kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja na kulia ni Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, Meneja masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera na Mkurugenzi wa Sta8up Vibes, waandaji wa Tamasha Sniper Montana. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
   Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akifurahia jambo na Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera (kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Stra8up Vibes Sniper Mantana (katikati) mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Monte Carlo Classic tukio lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.

  Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa tukio hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio.

  Akizungumza mapema hii leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya tukio hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
  Aliongeza kwamba kabla ya tukio hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.

  Alisema tukio la the Monte Carlo Classic limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burdani.

  “Kwenye miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu, huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.

  Nae Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii benki hiyo. Tunayofuraha kuwa sehemu ya uzinduzi wa tukio hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.

  "Tukio hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo maeneo mbalimbali nchini. 

  Mwezi uliopita Benki ya Bacrays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania. Kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tunapenda kuwahamasisha kadi zetu za Debit na Cretid kwenye tukio hili," alisema
  Kwa upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.

   “Nimefuarahi sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa kutambua umuhimu wangu.”

  Msanii huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye tukio hili.

  Kwa hivi sasa amejiunga na lebo ya G-Worldwide Entertainment iliyomwezesha kurekodi nyimbo zake tatu; Woju, Mama na aliouachia hivi karibuni wa Jombo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kushoto) akiwa ameongoza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kushoto), Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
   Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo aliwahimiza kusoma kwa bidii vitabu hivyo ili kupanua ufahamu wao zaidi na hata kimasomo pia vitasaidia kuinua viwango vyao vya ufaulu.
   Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi na uongozi wa shule hiyo kwa pamoja wakiimba na wanafunzi wa shule ya Msingi Kinondoni.
   Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa maktaba ya vitabu aliyoipa jina la Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika hatua za kumuenzi marehemu baba yake ambaye aliyemjengea misingi mizuri ya usomaji wa vitabu wakati wa makuzi yake.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akizindua rasmi Miradi ya upatikanaji wa picha za anga (Basemap) na mfumo unganishi wa taarifa za Ardhi (ILMIS) . Wanaoshuhudia pamoja naye; Kulia kwake ni Waziri nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Mhe. George Simbachawene, kushoto kwake ni Naibu wake; Mhe. Angeline Mabula katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akiwa amemaliza tukio la Uzinduzi wa Miradi ya upatikanaji wa picha za anga (Basemap) na mfumo unganishi wa taarifa za Ardhi (ILMIS) . Wanaoshuhudia pamoja naye; Kulia kwake ni Waziri nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Mhe. George Simbachawene, kushoto kwake ni Naibu wake; Mhe. Angeline Mabula na pembeni kabisa ni Katibu Mkuu wake; Dk. Yamungu Kayandabila katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akisisitizia jambo wakati wa Uzinduzi wa Miradi ya upatikanaji wa picha za anga (Basemap)  na mfumo unganishi wa taarifa za Ardhi (ILMIS) , katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akiwaongoza Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia(FFU)kuingia katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC baada ya kumaliza mbizo zake halmashauri ya wilaya ya Meru zote zikiwa katika wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha .

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akisalimiana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC kabla ya kuanza kuweka Mawe ya Msingi na kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh 3 bilioni.

  Mkurugenzi wa New Age Company Ltd,Godson Ngomuo akimwonyesha Samani zinazotengenezwa na kuuzwa na kampuni yake na kusaidia kutengeneza ajira kwa vijana wazawa.

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijimaakizungumza na maafisa wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilaya ya Arumeru wanaotoa elimu dhidi ya Rushwa.

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima  akijiandaa kukabidhi hundi yenye thamani ya Sh 3 milioni kwa kikundi cha Vijana waliopata mikopo yenye riba nafuu,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Alexander Mnyeti.

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akiwakabidhi  hundi yenye thamani ya Sh 3 milioni kikundi cha Wanawake  waliopata mikopo yenye riba nafuu,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Alexander Mnyeti.

  0 0

  Msanii nguli wa Bongo Movies, Gabo Zigamba, anatoa tahadhari kuhusu matapeli mbalimbali wanaotumia jina lake. Awali, msanii huyo alipoteza simu mbili za mkononi, ambazo baadaye zilikuwa zikitumiwa na matapeli hao kuomba misaada kwa watu mbalimbali wakijifanya kuwa wao ndio Gabo.
  Kadhalika, majuzi, akaunti ya Facebook ya msanii huyo ilidukuliwa na ikatumika kwa muda na matapeli hao kwa kujifanya wao ndio msanii huyo. Hatimaye alifanikiwa kuirejesha akaunti hiyo katika himaya yake.
  Gabo ameeleza kuwa anahisi kuwa yeye ndio msanii anayeongoza kwa jina lake kutumiwa na matapeli kwa sababu amekuwa akipata taarifa mbalimbali kuhusu watu wanaotumia jina lake, kwa mfano binti mmoja aliyejifanya ndiye Gabo na amekuwa akitapeli kwa kudai anauza mabegi.

  Msanii huyo ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia majina ya watu wengine, hususan watu maarufu, kwa minajili ya kutapeli. Amesema kuwa yupo katika mchakato wa uzinduzi mpya wa akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii ili, pamoja na sababu nyingine, iwe rahisi kwa watu kuwasiliana nae pindi wanapokumbana na matapeli hao wanaotumia jina lake.

  0 0

  Wateja waendelea kujiunga katika mtandao wa TTCL 4G- LTE katika maonesho ya wiki ya huduma za Kifedha na Uwekezaji, yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam. 
  Katika maonesho hayo, TTCL  inatoa huduma za laini za 4G, na vifaa vya 4G LTE, kama vile Routers, Mi-Fi, Modemu.  

  Wafanyakazi wa TTCL wakihudumia wateja katika Maonesho ya wiki ya huduma za Kifedha na Uwekezaji, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.

   Wateja wa TTCL katika Maonesho ya wiki ya huduma za Kifedha na Uwekezaji, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.
    Wateja wa TTCL katika Maonesho ya wiki ya huduma za Kifedha na Uwekezaji, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.
  Mteja akioneshwa namna ya kujiunga na mtandao wa TTCL 4G- LTE katika Maonesho ya wiki ya huduma za Kifedha na Uwekezaji, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.
  Mteja akipewa maelezo ya namna ya kujiunga na mtandao wa TTCL 4G- LTE katika Maonesho ya wiki ya huduma za Kifedha na Uwekezaji, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.

  0 0

  Kwenu ndugu jamaa na marafiki, Mzee wetu John Lugendo maarufu kwa jina la Mzee Joel  (pichani) hatunaye tena. Mzee Joel amefariki baada ya kudondoka ghafla na kuchukuliwa na ambulance hadi hospital ya Washington Adventists.
  Binafsi nafahamiana na Mzee Joel kwa zaidi ya mika 10. Mzee Joel ni moja ya watu walio nipa miongozo nilipo fika Marekan. Kwa sasa tunafanya mpango wa kumrudisha nyumbani.
  Bajeti ya gharama za kumrudisha nyumbani ni $15,000.00 ambapo tumefungua account ya bank na gofundme. Kwa moyo mkunjufu na wadhati nakuomba utusaidie chochote ili tuweze kumrejesha nyumbani Mzee wetu Joel.
  Bank of America
  Jasmine Bennett
  Checking Acc #: 4460 3716 4777
  Routing #: 052001633

  Pia tutakua na harambee Jumapili hii August 28, 2016:
  Indian SpringsTerrace Local Park
  9717 Lawndale Dr, Silver Spring MD, 20901

  Kuanzia 6:00pm to 10pm
  Correction kwenye mawasiliano:
  Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na:
  1. Iddi Sandaly 
  301-613-5165

  2. Mchungaji Mbatta
  703-863-2727

  3. Lilian Morgan 
  240- 351 3438

  4. Samuel Mushi 
  469- 290 -9529

  5. Saidi Mwamende 
  301-318-1501

  6. Mama Mushala 
  301-807-4934


  Mungu akuzidishie pale utakapo toa
  Liberatus Mwang'ombe "Libe"

  0 0

  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Japan,(JICA) Bw. Hiruchi Kato (kulia kwake) na ujumbe wake , jijini Nairobi Agosti 26, 2016 ambako anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa sita Wa Tokyo International Conference o n Africa Development (TCAD). Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili Nairobi, Kenya kuhudhuria Mkutano wa Mkuu wa Sita wa Wakuu wa Nchi wa TICAD (TICAD VI) utakaofanyika Agosti 27 -28, mwaka huu. Waziri Mkuu anahudhudia mkutano huo kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

  Leo asubuhi (Ijumaa, Agosti 26, 2016) Waziri Mkuu amekutana na viongozi wakuu mbalimbali wa makampuni ya kibiashara kutoka Japan ambao wamekuja kuhudhuria mkutano huo.
  Waziri Mkuu amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation, Bw. Tadashi Izawa ambapo katika mazungumzo yao, pamoja na kuangalia fursa nyingine katika sekta ya gesi Tanzania, kampuni hiyo imekubali kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa wataalamu kwa sekta ya gesi hususan usindikaji wa gesi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi (Liquefied Natural Gas).
  Bw. Izawa amemweleza Waziri Mkuu kwamba wamefurahiswa na taarifa za ugunduzi wa gesi ya Helium hapa nchini Tanzania na kwamba kampuni yake ina teknolojia na uzoefu wa muda mrefu katika kutekeleza miradi ya gesi (Gas value Chain Planning and Execution).
  “Tunao uzoefu wa muda mrefu, pia tunazo teknolojia za kuendeleza sekta ya gesi ikiwemo Helium kwa mfano ujuzi wa kutenganisha gesi asilia na helium (Separation of Natural Gas and Helium). Tumetekeleza miradi ya namna hii nchini Qatar ambayo kwa sasa ni ya pili kwa uzalishaji wa gesi hiyo duniani ikitanguliwa na Marekani,” amesema.
  Amesema mafunzo hayo yatafanyika kuanzia mwakani na yatalenga vijana wasiopungua 10 kutoka Tanzania ambao wamehitimu shahada za uhandisi kwani wameshafanya hivyo kwa vijana wanane kutoka Msumbiji.
  Waziri Mkuu alimshukuru Vw. Izawa kwa mpango wao wa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania lakini akamtaka pia waangalie uwezekano wa kuwasaidia vijana wanaotoka maeneo husika yenye gesi ili wapatiwe mafunzo ambayo yatawawezesha kumudu baadhi ya kazi kwenye viwanda vya kusindika gesi.
  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato na kujadiliana mambo kadhaa yakiwemo ya nishati na miundombinu.
  Katika mazungumzo hayo, Bw. Kato alimweleza Waziri Mkuu nia ya shirika hilo kuendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo hapa nchini na hasa katika sekta za afya, maji, kilimo na miundombinu ambazo imekuwa ikijihusisha nazo kwa muda mrefu sasa.
  Waziri Mkuu alimshukuru kwa ushiriki wa shirika hilo kwenye miradi ya nishati ya Kinyerezi na akamtaka aendelee kuisaidia Serikali ya Tanzania inainginia kwenye awamu ya tatu ya Kinyerezi (Kinyerezi III).
  Katika hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe alimwoba makamu wa Rais hyo waangalie uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta za nishati na miundombinu ya mkoa Dodoma hasa katika kipindi ambacho Serkali imeamua kuhamia huko.
  “Tunaomba muangalie sana suala la kuendeleza nishati ya umeme kwani nchi yetu imeamua kuwa nchi ya viwanda. Tutahitaji kuwa na umeme wa kutosha kuendesha viwanda vya usindikaji bidhaa zetu, lakini pia si mbaya mkiangalia suala la kuboresha miundombinu ya barabara na usafirishaji katika mji wa Dodoma,” amesema.

  0 0
 • 08/26/16--20:39: MAGAZETI YA LEO AGOSTI 27


 • 0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba, Israel Chasosa.

  BENKI ya Akiba imetangaza gawio la shilingi 75 kwa hisa kwa wanahisa wake kwa mwaka unaoishia Desemba 31, 2015.

  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba Israel Chasosa amesema hili no ongezeko la zaidi ya asilimia 100 ikilinganishwa na gawio la shilingi 30 kwa hisa lililotolewa mwaka 2014.

  Chasosa amesema kutolewa kwa gawio hilo ni matokeo ya benki hiyo kufanya vizuri kibiashara ikiwemo kupata faid tangia kuanzishwa kwake miaka 18 iliyopita.

   “Wakati wa kuamua ulipaji wa gawio, bodi ya benki yetu huangalia zaidi uwiano kati ya gawio hilo na kubakiza faida nyingine ili iweze kurudishwa kwenye uendeshaji wa benki kwa ajili ya kukuza biashara,” alisema.

  Chasosa alibainisha kwamba hii ni mara ya tatu mfululizo kwa benki hiyo kutoa gawio kwa wanahisa wake.

  “Hii ni ishara kwamba wanahisa wetu wana imani kubwa na benki yetu kwani tumekuwa tukipata faida endelevu kwa muda wote ambao tumekuwa kwenye biashara,” alisema.

  Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyokaguliwa, benki hiyo ilipata faida ghafi ya shilingi bilioni 5.3 mwaka jana, ambapo kiwango kama hicho kilipatikana katika kipindi cha mwaka 2014.

  Ripoti hiyo inaonyesha kwamba, katika kipindi cha mwaka 2015 benki hiyo ilitoa mikopo ya shilingi bilioni 107.3 ikilinganishwa na shilingi bilioni 77.2 zilizokopeshwa mwaka 2014.

  Rasilimali za benki ziliongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 163.7 mwaka 2015 ikilinganishwa na shilingi bilioni 135.3 kwa mwaka 2014 wakati mtaji wa benki ulikuwa na kufikia bilioni 19.3 mwaka jana kutoka bilioni 16 mwaka 2014.

  Pato kwa kila hisa lilikuwa ni shilingi 466 mwaka jana ikilinganishwa na shilingi 400 mwaka 2014.

  Chasosa alisema mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa mageuzi makubwa kwa benki hiyo kwani kulikuwepo na ubunifu mkubwa ambao ulisababisha bidhaa na huduma zake kuongezeka.

  “Akiba inaendeshwa katika mazingira ya ushindani mkubwa kwani hadi sasa kuna benki zaidi ya 50 na taasisi za fedha. Benki yetu imeendelea kuhakikisha kwamba huduma zake zinawafikia walengwa ambao ni wale wenye vipato vya chini na kati hasa wale ambao hawajafikiwa na huduma za benki,” alisema.

  Amesema mwaka huu, benki imejidhatiti kuhakikisha kwamba inapanua huduma zake kupitia wakala wa benki (agency banking) ili kuhakikisha kwamba walengwa wote wanafikiwa.

  Pia matumizi ya huduma za benki kwenye simu za mikononi (Akiba Mobile) imeboreshwa zaidi ili kuwafanya wateja wa benki hiyo kupunguza gharama na muda, kupata huduma kwani ni rahisi kutumia.

older | 1 | .... | 1333 | 1334 | (Page 1335) | 1336 | 1337 | .... | 3272 | newer