Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

TEASER JOTO LA ASUBUHI AUGUST 23 JUMANNE


'UKUTA' WAPIGWA MARUFUKU JIJINI DAR

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) yanayopangwa  kufanyika Septemba 1 mwaka huu. Maandamano hayo  yamepewa jina la UKUTA ambapo wanachama wake wanataka kuingia mitaani kupinga kile wanachokiita ukandamizaji wa demokrasia.
 Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema leo kwamba maandamano hayo hayatafanyika na jeshi la polisi limejipanga kuzuia maandamano hayo.

Kamanda Sirro amesema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayedhubutu kuingia barabarani kutokana jeshi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.

Amesema kuwa utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa hivyo kufanya mikutano bila kufuata utaratibu hautaruhusiwa.

Kamishina Sirro amesema kuwa kikundi/watu  wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja Amani kwa Dar es Salaam hakuna kitu chochote kitafanyika kutokana na jeshi la polisi lilivyojipanga.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Agasti 20 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye  maneno ‘UKUTA’ fulana 6  za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’. 
Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa Yoram Sethy Mbyelllah (42) mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani. 
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya Operesheni mbalimbali za kanda hiyo pamoja na kuzuia maandamano ya UKUTA, jijini Dar es Salaam leo.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine ya kuwekea risasi zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akioyesha bastola aina ya Browning yenye  risasi sita iliyokamatwa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha site Mirror zilizoibwa katika magari leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha flana rangi mbalimbali zilizokamatwa. 
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

Rais Magufuli apokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha kusindika gesi asilia (LNG)

0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya Mafuta ya Stat Oil ya Norway, Bw. Oystein Michelsen kabla ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Meneja Biashara wa Kampuni ya Stat Oil ya Norway Oivind Holm Karlsen (watatu) kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Bw. Oystein Michelsen. PICHA NA IKULU




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Agosti, 2016 amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.
Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Statoil ya nchini Norway ambayo ni moja ya Kampuni zitakazowekeza katika mradi huo Bw. Oystein Michelsen amemueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Bilioni 30 sawa na zaidi ya Shilingi Trilion 65 za Kitanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.
Bw. Oystein Michelsen amebainisha kuwa Serikali ya Norway ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na ameomba Serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemuhakikishia Mwakilishi huyo wa kampuni ya Statoil kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi unafanikiwa na ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kushirikiana na wadau kutoka Wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa kiwanda hicho.
"Nataka kuona mradi huu unaanza kujengwa, tunachukua muda mrefu mno, kamilisheni mambo yaliyobaki ili wawekezaji waanze kazi mara moja"Amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira kwa idadi kubwa ya watanzania na utaiwezesha serikali kupata mapato kupitia tozo mbalimbali, na hivyo kutumika kuimaisha huduma za kijamii zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu.
Pamoja na Statoil kampuni nyingine zinazoshiriki katika uwekezaji wa mradi huu ni Shell, Exxon Mobil, Pavillion na Ophir.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
22 Agosti, 2016. 

Article 11

Mdau wa Soka nchini, Tippo Athuman akabidhi vifaa vya michezo kwa Timu ya Coastal Union

0
0
Nahodha wa zamani wa Timu ya Coastal Union na Mdau mkubwa wa Michezo nchini,  Tippo Athumani akikabidhi vifaa vya Michezo kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union ya Jijini Tanga, Steven Mnguto ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la kwanza Tanzania Bara. Makabidhiano hayo yamefanyika Agosti 22, 2016 kwenye Duka la Vifaa vya Michezo la Zizzou Fashion, Sinza Jijini Dar es salaam. vifaa hivyo ni pamoja na Beebs, Cones, Mipira na Jersey set mbili watakazochezea ligi hiyo.

MAGAZETINI LEO JUMANNE AGOSTI 23

MDAU BUGA AUNDA GARI LAKE JIJINI MBEYA....

HEPI BESDEI YA KUZALIWA BLOGGER MC BARAKA LEO

0
0

Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, Aug 23. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. 


Ni neema ambayo sistahili. Napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana. Niitumie kwa mambo mema. Nizingatie wajibu wa kuvitumia kikamilifu vipaji alivyonipa Mungu kwa manufaa ya wanadamu. 
Siwezi kujivunia chochote nilichoweza kufanya, bali ni kumshukuru Mungu na kuendelea kumtegemea na kila ninaposherehekea kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa kwangu.
Fikra zinanituma kufananisha mchango wangu kimkoa na Kitaifa sawa na ule wa watu maarufu.


Ukweli ni kwamba ninajitahidi lakini mchango wangu bado ni hafifu sana. 
Mengi nimefanya kupitia Bukobawadau Blog Media ninachoweza kusema ni kwamba changamoto ni kubwa sana!I will always praise God .....

-- Best Regards 

Mc Baraka 
Manager (Founder)
BUKOBAWADAU

Mambo ya Njenje hayo, kutia nazi kunoga....Salender Bridge Club jijini Dar kila Jumamosi

Wateja wa Bayport wafurahia hati zao za viwanja

0
0
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akimkabidhi hati mteja wao Mary Simon, baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinapatikana kwa njia ya fedha taslimu na mikopo maalumu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Kulia ni Meneja Mikopo wa taasisi hiyo, Nasibu Kamanda. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana imeendeleza utaratibu wake wa kugawa hati kwa wateja wao walionunua viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa njia ya mikopo na fedha taslimu.

Mradi huo wa Vikuruti ulizinduliwa mwaka jana, ambapo baada ya kufanikiwa kwake, taasisi hiyo ikaanzisha miradi mingine mitano ambayo ni Kigamboni, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha na Kilwa, huku ikiweka utaratibu rahisi na nafuu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, alisema kwamba kugawa hati kwa wateja wao ni mwendelezo wa huduma nzuri zinazotolewa na taasisi yao kwa ajili ya kuwakomboa wananchi katika suala zima la ardhi.

Alisema kwamba makubaliano yao ni kuhakikisha taasisi inasimamia sualaa la hati ili wateja wao wasisumbuke kutokana na mchakato mzima wa utendaji kazi wao unaotoa urahisi juu ya upatikanaji wa viwanja vyao vyenye hati.

“Tunaendelea na kutoa hati kwa wetu walionunua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, ambapo Watanzania wengi walichangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo, ambavyo ukiacha vya Vikuruti, wateja wetu pia wanaweza kukopa fursa hii ya ardhi kwa miradi yetu ya Kimara Ng’ombe (Bagamoyo), Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha), Kibiki na Mpera (Chalinze) na Kitopeni (Bagamoyo).
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akizungumza jambo baada ya kumkabidhi hati mteja wao Mary Simon kushoto baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Mikopo wa Bayport Financial Services, Nasibu Kamanda.
Mteja wa Bayport Financial Services Sixtus Kilenga kushoto akisaini kama sehemu ya kukabidhiwa hati ya kiwanja. Hati hizo kwa wateja walionunua viwanja vinavyopatikana kwa njia ya mkopo na fedha taslimu zinaendelea kutolewa kwa waliokamilisha taratibu zao. 

Naye mteja wa Bayport aliyopewa hati yake, anayejulikana kwa jina la Mery Simon Anthony aliipongeza Bayport kwa kutoa huduma nzuri kiasi cha kumfanya amiliki kiwanja chenye hati, huku kikiwa hakina mlolongo wowote.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu nimepata hati yangu kwa haraka na sijapata usumbufu wowote, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi katika miradi hii ya viwanja vya Bayport kwa sababu ni rasilimali nzuri,” Alisema.

Naye Sixtus Francis Kilenga alisema kwamba amefurahishwa na utaratibu mzima wa kupata kiwanja chenye hati, huduma zinazotolewa na Bayport, ambapo mteja hana jukumu lolote la kufuatilia hati katika maeneo yanayohusika.

“Utaratibu wa kununua kiwanja kasha ukapewa hati bila kufuatilia wizarani ni mpya, hivyo binafsi nimeufurahia na unaweza kuifanya Bayport kuwa moja ya ofisi zenye kujali muda na gharama za kiutendaji wa wateja wao,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya bidhaa ikiwamo viwanja pamoja na fedha taslimu isiyokuwa na amana wala dhamana, huku taasisi hiyo ikiwa na matawi zaidi ya 82 nchi nzima kwa ajili ya kuwapatia Watanzania huduma bora.

WALIOKULA FEDHA ZA CHAMA CHA USHIRIKA KUSAKWA MKOANI KATAVI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Mkoa Katavi, Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga kupeleka wakaguzi wilayani Mlele na kubaini watu waliokula fedha za chama cha ushirika cha Ukonongo na kuwachukulia hatua.

“Watakaobainika watiwe hatiani. Licha ya bodi ya ushirika huo kuvunjwa, hatuwezi kuacha suala hili limalizike kwa kuvunja bodi kwa sababu walioingia wanaweza kuiba kwa mategemeo ya kuvunjwa bodi,“ amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumatatu, Agosti 22, 2016) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Inyonga wilayani Mlele.

Amesema kila mtumishi afanye kazi na awajibike kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kwa mujibu wa taaluma yake ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwani hilo ndilo lengo la kuajiriwa kwake.

“Haiwezekani hapa kuna Ofisa Ushirika halafu Waziri Mkuu analetewa mabango ya kumtaka atatue tatizo la chama cha Ushirika. Hali hii inaonyesha hapa hakuna kazi inayofanyika,“ amesema.

Waziri Mkuu amesema wanahitaji watumishi watakaosikiliza maelekezo yanayotolewa na Serikali na kuyafanyia kazi kwa sababu malengo ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ni kuona nchi hii inabadilika hivyo wasioweza ni vema wakaandika barua za kuacha kazi.

“Msikubali kuhamasishwa kufanya mambo yatakayowaletea madhara. Fanyeni kazi ili tupate maendeleo. Hatuwezi kufananishwa na nchi ndogo ndogo, wenzenu wanafanya kazi nasi tupunguze maneno tufanye kazi,“ amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamilia kumaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme nchini ambapo imetenga zaidi ya sh. trilioni moja kwa ajili ya kumalizia kazi ya usambazaji umeme nchi nzima ikiwemo wilaya ya Mlele.

Amesema watapeleka jenereta kubwa mbili zitakazofungwa katika kijiji cha Utende ambazo zitasambaza na kuwasha umeme katika kata ya Inyonga na maeneo mengine.

“Mwezi Novemba mwaka huu umeme utakuwa umewaka wilayani Mlele. Mkakati ni kuunganisha mkoa wa Katavi na gridi ya Taifa kutoka Tabora, kupita Sikonge hadi Inyonga,“ amesema.  

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na mbunge wa jimbo la Katavi, Mhandisi Isack Kamwelwe amemuomba Waziri Mkuu kuwasaidia kupandishwa hadhi kwa kituo cha afya cha Inyonga na kuwa Hospitali ya wilaya kwa sababu wilaya yao haina hospitali.

Pia ameomba wilaya hiyo ipatiwe umeme wa Tanesco ili kupunguza gharama kubwa za kununua umeme kutoka kwa mfanyabiashara ambaye amefunga jenereta na anawauzia unit moja sh. 1000 wakati Tanesco wanauza sh. 100 kwa unit moja.

Awali Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel Kassanda alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa nyumba za watumishi hali inayosababisha mkuu wa wilaya na Katibu tawala wa wilaya kuishi kwenye nyumba za kupanga.

BREAKING: US BLOGGER AIBUKA, AMSAKA JOHN MASHAKA KWA UDI NA UVUMBA

0
0
Ankal Wasalaam,
 Wadau wote wa Blogu ya jamii, natumai mu wa wazima wa Kheri. Mimi mzima, na naendelea na kazi yangu ya u professor, nikifundisha masomo ya “Political Economics” hapa nchini Uingereza. Hii ni baada ya kumaliza Phd yangu pale Oxford University mwaka 2014 ambako nilikuwa Mwafrika wa kwanza kuvunja rekodi kwa kuandika thesis iliyokubalika na vyuo vikuu vikubwa duniani. Nadhani wasomi wengi wa hii blogu wananifahamu vizuri sana, kwa sababu bila mimi, hata John Mashaka asingeupata umaarufu alioupata. 
Niseme kwa kifupi nilimjenga John Mashaka, kwa kumsaidia sana kwenye utafiti kipindi akiwa chuo kikuu. Ingawa kila mtu ana kipaji chake cha kuzaliwa, ambayo nakiri kwamba Ndugu John anacho na ni Genius, ila pia lazima asaidiwe. Nimemsaidia mimi. Niko tayari zaidi kwenda kumsaidia Dr. Magufuli kujenga uchumi wa Tanzania.
Pamoja na wadau wengine, naungana nanyi kumuita John Mashaka atoke mafichoni na kurudi kwenye hii blogu ili mijadala ya kisomi iendelee. Nadhani Tanzania kama taifa hipo katika kipindi kigumu. Kipindo cha mpito ambapo mawazo chanya kama yangu, John Mashaka na genge lake wanaweza kuchangia. Nikiwa Professor anayeheshimika dunia nzima, kushirikiana na wakina Ndugu John Mashaka Hildebrand Shayo na wengineo kutawasaidia hata wao kukua zaidi na kujulikana kimataifa, licha ya kuleta mawazo chanya na mbadala katika ujenzi wa taifa letu.
Niko tayari kuendeleza mijadala ikiwa John Mashaka atajitokeza

Wenu katika Ujenzi Wa Taifa
Prof. US-Blogger, Bsc, Msc, PhD (Oxford)
Oxford University, Department of Economics
Political Economics
London, United Kingdom

HIVI UNAJUA KWAMBA WANYAMA AINA YA NYUMBU NI RAIA HALALI WA TANZANIA, NA ILE SAFARI YAO KULEKEA KWA WATANI ZETU HUWA WANAENDA FUNGATE???

0
0
Nyumbu ni Wanyama wanaopenda kusafiri kwa makundi makubwa kila mwaka, ni 'raia' halali wa Tanzania kwa kuzaliwa na kwa nasaba.

HAWANA vyeti vya kuzaliwa, wala hawajulikani hata mahali gani wanapotupa makondo yao ingawa ukifuatilia unaweza kuyaona, lakini Nyumbu (Wildebeest) wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni raia halali wa Tanzania.

Kwamba wanapatikana pia katika hifadhi ya Maasai Mara katika nchi jirani ya Kenya, katu hiyo haiwezi kuhalalisha uraia wao kwamba wanatokea huko. Ni bahati mbaya tu kwamba wanyama hawana pasipoti kama ambavyo hawana vyeti vya kuzaliwa, vinginevyo ushoroba (corridor) wanaoutumia ungewekwa kizuizi (Border Point) kama kile cha Sirari, Namanga, Tarakea, Holili na kwingineko hakika hati hizo zingethibitisha kwamba wanyama hawa huwa wanakwenda Kenya kutalii tu na kurejea tena nchini mwao Tanzania.

Kuweka mambo sawa ni kwamba, wanyama hawa wanapokwenda kwenye Hifadhi ya Maasai Mara, huwa wanakwenda kwenye 'fungate' kwa muda usiozidi miezi miwili na kisha kurejea kwao Tanzania kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Maelezo haya yanathibitishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti, William Mwakilema, ambaye anasisitiza kwamba kauli zinazotolewa na wenzao wa Kenya kwamba wanyama hao wanapatikana nchini mwao na ni mali yao ni za upotoshaji mkubwa kimataifa

Hakuna mahali popote duniani ambako kuna uhamaji wa Nyumbu kama wa Serengeti kuelekea Maasai Mara ambao umekuwa miongoni mwa Maajabu Saba ya Dunia na hakika ndio umeifanya Serengeti kushika nafasi ya kwanza katika Maajabu Saba ya Asili ya Afrika mwezi Januari 2013; Kifupi tu ni kwamba moja ya sababu zinazofanya watalii wengi kuja nchini ni kushuhudia maajabu haya ingawa nabii hakubaliki kwao (si aghalabu kwa Watanzania).

Zaidi ya nyumbu milioni 2 uhama kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea Hifadhi ya Maasai Mara nchini Kenya kutafuta malisho kati ya kipindi cha Julai na Oktoba.
Wanapohama ni lazima wakatize kwenye Mto Mara ambako hukumbana na mamba ingawa wengi hunusurika NA HAPA WAZEE HUTANGULIZWA KAMA CHAMBO......
Mwakilema anasema, wanyama hao wanapatikana katika Mfumo-asili wa Serengeti (The Serengeti Ecosystem), unaochukua eneo la kilometa za mraba 40,000 huku wengi wa nyumbu hao wakiwa wale wenye manyoya meupe (Connochaetes tuarinus mearnsi) ambao wanapatikana pia katika sehemu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa upande wa kusini; Hifadhi ya Serengeti na Maswa Game Reserve pamoja na Hifadhi za Jamii zinazopakana.

Kwanini wanazalia Tanzania? Mbali ya kuwa Serengeti ndiyo makazi yao ya asili, lakini wanyama hao, na wengine wengi, hupenda kuzalia huko kwa kuwa ardhi ina madini ya kutosha ya fosforasi ambayo ni virutubisho muhimu kwa majani, hivyo kuwafanya ndama wanaozaliwa kupata nguvu muda mfupi baada ya kula majani hayo. Katika kipindi cha uzazi, Nyumbu wanaweza kuzaa ndama 8,000 kila siku, hivyo kuonyesha ni kwa nini hifadhi hiyo inao wanyama hao wengi zaidi.

Kutokana na tabia yao ya uhamaji, nyumbu huwa hawana uhusiano wa kudumu. Majira ya nyumbu kupandana ni wakati nyumbu madume wanapotengeneza himaya na kuwavutia majike. Himaya hizi ndogo huwa zinaanzia meta za mraba 3,000, ambapo ndani ya kilometa moja ya mraba kunaweza kuwepo himaya 300. Madume yanalinda himaya zao zisiingiliwe na wengine na kuwaita/tongoza majike.

DSE yakuza mauzo ya hisa kwa asilimia 57

0
0
Idadi ya mauzo katika soko la hisa Dar es salaam (DSE) imekua kwa asilimia 57 na kufikia shilingi bilioni 3.3 kutoka shilingi bilioni 2.1 wiki iliyopita kutokana na ukubwa wa idadi ya mauzo.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Mwandamizi wa Masoko DSE Bi. Mary Kinabo imesema kuwa idadi ya mauzo hayo yamekua kutokana na kupanda kwa idadi za hisa zilizouzwa kutoka shilingi milioni 1.6 hadi kufikia shilingi milioni 2.2.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa Benki ya CRDB imeendelea kuongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa asilimia 49 ikifuatiwa na Soko la hisa DSE ikiwa na asilimia 43 na ya tatu ni kampuni ya Bia nchini TBL yenye asilimia 4.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa asilimia 0.67 na kufikia shilingi trilioni 23.4 kutoka trilioni 23.2 wiki iliyopita na ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwa shilingi trilioni 8.4.

Mbali na hayo taarifa hiyo imeeleza kwamba licha ya mauzo kupanda lakini viashiria vya soko katika sekta ya viwanda vimeshuka kwa alama 19.47 baada ya bei za hisa kutoka TBL kushuka kwa asilimia 0.66 huku sekta ya huduma za kibenki kupanda kwa alama 29.89 kutokana na kupanda kwa kaunta ya DSE na NMB. 

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa viashiria vya soko katika sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imebaki kwenye hali yake ya wiki iliyopita baada ya bei za hisa za Swissport kubaki kwa shilingi elfu 3.543. Na Ally Daud-Maelezo

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATEMBELEA VITUO VYA AFYA WILAYA YA KASKAZINI ''B'' UNGUJA

0
0
Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Harusi Saidi Suleiman (wapili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkunga wa Kituo cha Afya cha Kiwengwa, Khadija Ali Juma Wakati alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya Afya Kaskazini B Unguja.
Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar,  Harusi Saidi Suleiman (katikati) akiangalia shimo la Uchomwaji Taka linalotumiwa na Kituo cha Afya cha Kiwengwa baada ya kufanya ziara katika vituo vya Afya Kaskazini B Unguja .kushoto ni Mkunga wa Kituo cha Afya Kiwengwa Khadija Ali Juma.
Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Harusi Saidi Suleiman wakwanza (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Bumbwini Misufini Dk, KHamisi akitoa maelezo ya Kumkaribisha mara baada ya kufika katika Kituo hicho Mkoa wa Kaskazini B Unguja.
Mhudumu wa Afya wa Kijiji cha Bubwini Misufini Riziki Kiongwe Debe akitoa maelezo kuhusu changamoto zinazo wakabili kwa Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Harusi Saidi Suleiman (Hayupo pichani) mara baada ya kufika katika Kituo kilichopo kijijini hapo Mkoa wa Kaskazini B Unguja .
Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Harusi Saidi Suleiman akifafanua jambo alipokutana na Wauguzi wa kituo cha Afya cha Bumbwini Misufini Mkoa wa Kaskazini B Unguja.kulia ni Afisa wa Afya Wilaya Mosi Kali Makame. PICHA NA MIZA OTHMAN-MAELEZO ZANZIBAR.

DC STAKI ATENGA SIKU YA JUMATATU KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

0
0


Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki shughuli za maendeleo kwa kufyeka baadhi ya vichaka
 Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya


Dc Senyamule akishiriki zoezi la kupanga matofali yaliyofyatuliwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani humo.


Na Mathias Canal, 
Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga Siku moja katika Juma ili kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.

Huu ni utaratibu ambao Mkuu huyo wa Wilaya ameuanzisha kwa muktadha wa kuchochea ari katika utendaji Kazi na uwajibikani kwa kila mwananchi ili kuimarisha na kusukuma kwa vitendo juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa vitendo na utekelezaji wa utendaji kazi ili kuakisi dhana nzima ya serikali hii ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu.
"Nimeamua kutenga siku hii ya jumatatu kwani naamini italeta hamasa kwa wananchi kupenda kazi za maendeleo, itawatia moyo na kuona kuwa serikali ipo karibu nao ". Alisema Staki
Akizungumzia kuhusu kuanza kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Dc Staki amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaoishi kwa mazoea ya kuyumbishwa na siasa zisizo na manufaa kwao lakini huu si wakati tena wa kurudi nyuma badala yake watanzania wote wanapaswa kushirikiana katika kufanya Kazi na kulifanya Taifa Letu kufika mbali zaidi kimaendeleo.
Hii imekuwa ziara ya mwanzo ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki kwa kushiriki kufanya kazi za Jamii akiwa na dhamira ya kuwatia Moyo wananchi ili kupunguza lawama zisizo na lazima kwa serikali na badala yake kujituma katika kufanya kazi.
Ziara hiyo katika kushiriki Kazi za jamii imefanyika katika kijiji cha Mheza na Maore vilivyopo kata ya Gonja Maore huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kuishauri na kushirikiana na serikali.
Kwa upande wawananchi wa maeneo hayo walionyesha kufurahishwa na utaratibu huo ambao haujawahi kufanyika na kiongozi yeyote katika Wilaya ya Same tangu kuumbwa kwa msingi ya ulimwengu.
Wananchi hao wamemuakikishia Mkuu hiyo wa Wilaya hiyo kuwa watashirikiana nae katika shughuli za maendeleo kwani kwa kiasi kikubwa udini na uzembe wa watendaji wengi umesababisha kuendelea kuzorota kwa maendeleo ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na hayo pia Dc Staki Ametoa onyo kwa wananchi hususani Vijana ambao ni wavivu katika kushiriki shughuli za Jamii kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu kW kila mwananchi atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake.

MPINGA CUP 2016 YAPAMBA MOTO, WAENDESHA BODABODA WANUFAIKA KWA MAFUNZO NA VIFAA VYA MICHEZO

0
0
 Mratibu wa Mashindano ya Mpinga Cup 2016 , A.S.P Mbunja Matibu, akikagua timu za kundi B zinazoshiriki kwenye Michuano hiyo, kwa Madereva wa Bodaboda, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Magereza Ukonga mwishoni mwa Wiki iliyopita, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).
Picha zote na Traffic MakaoMakuu

 Mkaguzi wa Polisi Hamisi Membe akifundisha waendesha pikipiki (Bodaboda), kuhusu Alama za Usalama Barabarani, wakati wamashindano ya Mpinga Cup 2016 yanayoshirikisha Madereva wa Bodaboda, yaliyofanyika kwenye uwanja waMagerezaUkongamwishoni mwajuma, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).(
 Mrakibu wa Polisi Methew Msuyale (kushoto) akikabidhi Fulana  kwa kiongozi wa timu mojawapo zilizoshiriki kwenye hatua ya Mtoano kutoka kundi B kwenye ya Mpinga Cup 2016, iliyochezwa kwenye uwanja wa Magereza Ukonga Mwishoni mwa wiki iliyopita. Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) DCP Mohammed Mpinga akikagua timu katika  mashindano ya Mpinga Cup 2016 inayohusisha waendesha Pikipiki Mkoani Ilala, Dar es Salaam, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) DCP Mohammed Mpinga akiwataka na kuwaelimisha waendesha pikipiki (Boda Boda) kuzingatia, kuzifuata na kuziheshimu Sheria za Usalama Barabarani ili kuweza kupunguza wimbi la ajali za waendesha Pikipiki hapa nchini. Kupitia mashindano ya Mpinga Cup 2016 inayohusisha waendesha Pikipiki Mkoani Ilala, Dar es Salaam, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).


Mkuu mpya wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro ala kiapo kuanza kazi

0
0
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akila kiapo kwenye sherehe fupi za kumwapisha zilizofanyika leo jijini Arusha na kusimamiwa na mkuu wa mkoa huo Mhe. Mrisho Gambo
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa wilaya mpya ya Arusha,Gabriel Daqarro(kulia)wanaoshuhudia ni Katibu Tawala mkoa,Richard Kwitega na Afisa wa Itifaki,Mukhsin Khasim.
 Viongozi mbalimbali katika Jiji la Arusha wakifatilia tukio hilo.
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi a mkoa wa Arusha baada yasherehe za kula kiapo.

Amref TZ, HABARI Newsletter & 2015 Annual Report

WAZIRI PROF.MBARAWA AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro

0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (wa tatu kushoto), alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kanda ya Afrika Mashariki walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images