Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Mahojiano na mjasiriamali na mwanaharakati Diana Gasper

0
0
Katika huyu na yule wiki hii, tumezungumza Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kinyago Travels and Tours na Stuka Tanzania Diana Gasper, ambaye pamoja na mambo mengine, amezungumzia historia yake, ya kampuni zake na harakati nzima za biashara na harakati za kuikomboa jamii ya Tanzania
Amezungumza mengi
Unaweza kutembelea tovuti yao http://kinyagotravel.com/ ama kupitia Instagram @diana_gasper ama @kinyagotravel ama @stukatanzania

FEDHA ZA MAENDELEO KUUNGUZA WATAKAOZICHEZEA - WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa halmashauri mkoani Katavi kuwa makini na matumizi ya fedha za maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea zitamuunguza.

“Fedha hii tafadhali ni ya moto. Msicheze na hii ya halmashauri tunayoileta hapa halmashauri kwa ajili ya wananchi itawakunguza vidole. Tunaileta kwa madhumini, tunataka wananchi wahudumiwe,“ alisema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 21, 2016) wakati akihutubia umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Azimio wilayani Mpanda.

Alisema Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri mbalimbali hivyo ni vema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Waziri Mkuu alisema ni lazima wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri wahakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao kuwa inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda wilayani Mpanda na kuangalia namna ya kuipanua hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambayo inahudumia mkoa wote wa Katavi.

Alisema hospitali hiyo ilijengwa mwaka 1957 kama zahanati ambayo kwa sasa yanatumika katika kuwahudumia wananchi wate wa mkoa huo imezidiwa hivyo alimuagiza mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga kuharakisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.

Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa wakati mkoa ukiwa kwenye harakati za ujenzi wa hospitali ya mkoa wilaya nazo zianze ujenzi wa hospitali za wilaya ili kuhakikisha sera ya Serikali ya kuwa na hospitali katika kila wilaya inatekelezwa.

Alisema kwa sasa madaktari na wauguzi wanaofanya kazi kwenye hospitali ya Manispaa ya Mpanda wamezidiwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kuliko uwezo wao. Hivyo amewataka madaktari na wauguzi wa wilaya ya Mpanda kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzao wa Manispaa.

Awali hospitali hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa halmashauri ya Mpanda. Hospitali hiyo kwa sasa ipo chini ya Manispaa ya Mpanda hivyo Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa huo kuboresha huduma kwa kupeleka dawa na vifaa tiba vitakavyoweza hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa wa mkoa.

Mkoa umetenga sh. bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake) wakiwapungia wananchi wa Mpanda wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda Agosti 21, 2016. 
Wananchi wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 21, 2016. Katika hotuba yake Waziri Mkuu alizitolea majibu kero zote zilizoandikwa kwenye mabango hayo akiwahusisha watendaji wa Halmashauri, mkoa na wilaya.
Wasanii wa kijiji cha Katumba wilayani Mpanda wakicheza ngoma ya Kasimbo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016.

DC KASESELA AWASWEKA NDANI WALINZI 2 WA KAMPUNI YA AMAZON SECURITY KWA KUNYANYASA WANANCHI.

0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alipokea wakina mama watatu wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji ya baridi walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa waliolazwa Katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa.

Akinamama hao wengi wao wametoka maeneo ya mbali na hospitali hiyo walimwagiwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa. 

Mkuu wa wilaya hiyo alifika hospitali kujionea hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi wa kampuni hiyo alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula katika hospitali hiyo na kumwaga kwa mateke. 

Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. "Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuloweshwa maji." alisema Mh Kasesela.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitembelea katika jengo ambalo lililomwagwa maji na Mlinzi wa Kampuni ya Amazon Seculity na kuwaondoa akinamama walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa waliolazwa Katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa.
Baadhi ya watu walioondoka eneo la kusubiri wagonjwa na kukaa nje katika hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa. 
Eneo la Kupumzika watu nwanaoenda kuwaona wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa likiwa limemwagwa maji.

HUU NDIO UKWELI KUHUSU NGUVA (Dungong and Mermaid)

0
0
Mnyama aina ya Nguva ambaye watu wamekuwa wakimwelezea kwa namna tofauti tofauti na endapo mazingira ya bahari yataendelea kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho kutoweka.

Hii habari ya kiumbe kinachoitwa nguva ni kweli yupo ila ni samaki tuu na sio kweli kuwa ni nusu mtu nusu samaki!. Picha zote za kiumbe hicho unazoziona ni za kutengeneza, yaani ni hoax. 
 1. Nguva ana rangi ya kijivu na umbo la mwili wake ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe. Awapo katika maji hutoa kichwa chake juu ya maji kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua yaliyopo upande wa juu wa kichwa chake.

2. Nguva ni mnyama anayezaa na kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine na wakati akinyonyesha husimama na kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya mtu aliyemuona kudhani kuwa ni mtu.

3. Mnyama huyo huzaa kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto mmoja pekee hivyo nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho ima kuweka kwenye maeneo tengefu.
4. Mtoto wa mnyama huyo anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153 hadi 200, wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400 hadi 1, 000 huku chakula chake kikuu kikiwa ni majani

5. Alikuwa akionekana Dar es Salaam, Kimbiji, Buyuni, lakini sasa haonekani tena kwani ni mnyama mwenye aibu sana na anapogundua kuwa maeneo alipo kuna binadamu huamua kuhama na kwenda mbali zaidi kwenye utulivu.

6. Kuna simulizi za ajabu ajabu kuhusu huyu samaki; kwa mfano wanasema kwamba mvuvi akimvua lazima kwanza afanye naye tendo la ndoa kama tambiko.)
Ni kufikirika tu................Na wafikirika ni wengi......................
imeandaliwa na Geofrey Chambua

Procurement of Cleaning and Gardening Services at the State University of Zanzibar, Tunguu Campus - Unguja South Region, Zanzibar

MAWAKALA WA AIRTEL MONEY KUPATIWA MAFUNZO KUKUZA BIASHARA ZAO.

0
0
Meneja wa Jumo Tanzania, Rwebu Mutahaba akiongea na mawakala wa Airtel (hawapo pichani) wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Airtel  Timiza Wakala itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya mawakala wa Airtel Money jijini Dar es Saalam wakifatilia kwa makini maelezo juu ya huduma ya Airtel Timiza yaliyotolewa kwenye semina ya mafunzo inayoshirikisha kampuni ya simu ya Airtel na washirika wake Jumo Tanzania.
 Wakala wa Airtel Money wa maeneo ya msimbazi kariakoo bwana Maneno George akiuliza swali wakati wa semina ya uzinduzi wa mpango utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu ya huduma ya Timiza itakayowasaidia kupata mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara zao . Semina ya mawakala iliyofanyika jijini Dar es saalam mwishoni mwa wiki.

Mawakala wa Airtel Money kupatiwa mafunzo kukuza Biashara zao
Airtel Tanzania inatangaza uzinduzi wa mpango wake utakaowawezesha mawakala wa Airtel Money katika mikoa mbalimbali kupata elimu zaidi kuhusu fursa zinazopatikana  katika bidhaa na huduma zake  ikiwemo  huduma ya Airtel Timiza wakala inayowawezesha mawakala kupata mikopo isiyo na masharti na kusaidia kukuza mitaji na biashara zao

Mafunzo hayo, ambayo yatawasilishwa kwa mawakala zaidi ya  1000 katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha, Mwanza Morogoro na Dodoma yameanza mwishoni mwa wiki katika mkoa wa Dar es salaam na yanategemea kumalizika agost 28 katika mkoani Morogoro .

Jackson Mmbando, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania anasema, “Kusaidia biashara zistawi ni sehemu muhimu ya biashara ya Airtel na tuna shauku ya kuanzisha bidhaa za kibunifu zenye faida kwa jamii na wateja wetu wenye lengo la kuinua uchumi wao kote nchini. Mafanikio ya huduma ya mikopo ya Airtel Timiza yanatokana moja kwa moja na mtandao wetu mpana wa mawakala.  tunaamini mafunzo haya yataongeza uelewa mkubwa zaidi wa huduma za kifedha zinazopatikana kwa mawakala wa Airtel Money.”

Timiza Wakala,ni huduma inayowawezesha mawakala wetu nchi nzima kupataa mtaji wa kufanyia kazi  kupitia simu zao za mkononi,huduma hii  iliyozinduliwa mwaka mmoja uliopita, kwa sasa mtandao wa mawakala  50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni moja.

Akizungumzia kuhusu jinsi Mawakala wanavyonufaika na Timiza Wakala, Mmbando anasema “Utafiti wetu unaonyesha kwamba mawakala wengi hutumia Timiza wakala  kuendesha biashara yao ya uwakala kwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money kwaajili ya kufanya miamala na kuhudumia wateja.  Wakala anaamua kiasi cha pesa wanachotaka kukopa pia na masharti ya marejesho, hivyo kuwapa udhibiti wa fedha zao”

Mmbando alisema Katika kipindi cha mwaka jana Timiza imekuaa  kwa kiasi kikubwa na wateja wanathamini jinsi huduma hii inavyobadili maisha yao “Uhusiano kwa misingi ya kuaminiana umejengeka ambao unaturuhusu kutoa mikopo isiyo na dhamana kwa urahisi, wakati wowote mteja anapohitaji.  Sambamba na hilo wateja wetu wanaelewa kwamba kuzingatia masharti ya mkopo ili kupata mikopo mikubwa na kutumia huduma ya Timiza kama benki”.

Tunayo mabadiliko tuliyoyafanya katika kuboresha huduma hii ya   Timiza Wakala ikiwa nia pamoja na  kuwapatia mawakala uwezo zaidi wa kuchagua jinsi ya kulipa mikopo mapema kwa mafungu na kupata mikopo mikubwa, lengo la semina za mafunzo haya ni kuwaelimisha mawakala ili kupata uelewa zaidi kulinganisha na ilivyo sasa. Huduma ya Airtel Timiza pia inawawezesha wateja wetu kupata mikopo isiyo ya dhamana ya hadi shillingi laki tano, mawakala na wateja nchi nzima  kwa ujumla wanafaidia na huduma hii aliiongeza Mmbando

“Huduma ya Airtel Timiza imeendele kuungwa mkono na serikali na Benki kuu , na kuiwezesha Tanzania kuweka rekodi nzuri  katika kuwapatia wananchi wake mazingira wezeshi yanayowanufaisha kifedha.  Sisi Kama mtandao mkubwa zaidi wa simu nchini, tunajivunia mafanikio haya na  kuendeleza dhamira yetu ya  kutoa huduma za kibunifu za  kifedha kwa wateja nchi nzima,” anahitimisha Mmbando.

WAZIRI NAPE AKABIDHIWA UWANJA WA UHURU MUDA HUU NA KAMPUNI YA BEIJING CONSTRUCTION YA NCHINI CHINA.

0
0


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekabidhiwa Uwanja wa Uhuru uliokuwa unakarabatiwa kwa takribani miaka mitatu.

Akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Elissante  Ole Gabriel amekabidhiwa uwanja huo uliogharimu zaidi ya bilioni 22 uliojengwa na  Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China.

Nape amesema kuwa, uwanja huu mbali na kutumika kwa ajili ya michezo anatoa fursa kwa vyama vya michezo kuja kufungua ofisi zao kwani kuna eneo kubwa sana ambaloliko wazi.

Uwanja huo kwa sasa una uwezo wa kuchukua mashabiki 27000 watakaokuwa wameketi tofauti na awali na ukarabati huo utaudumu kwa takribani  miaka 200.
Uwanja wa Uhuru ulivyo karabatiwa na  Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Elissante  Ole Gabriel kulia akisaini baada ya kukabidhiwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. aliyekaa kushoto ni mwakailishi wa   Kampuni ya Beijing Construction kutoka nchini China wakisaini mikataba kabla ya kukabidiana uwanja huo jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhiwa uwanja wa Uhuru uliokuwa ukikarabatia na kampuni kutoka nchini China.

SERIKALI YAZITAKA TAASISI 145 AMBAZO HAZIJAWASILISHA TAARIFA YA WATUMISHI HEWA KUWASILISHA KABLA YA TAREHE 26 AGOSTI,2016

0
0
Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora imetoa orodha ya majina ya Taasisi ambazo hazijawasilisha Taarifa ya Watumishi Hewa katika Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora. Serikali imetoa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ambayo ni 26 Agosti, 2016.

Mara baada ya tarehe hiyo, Ofisi ya Rais-Utumishi  itawasilisha taarifa rasmi ya watumishi hewa kwa Mheshimiwa Rais ikiwa na orodha na majina ya Taasisi ambazo zimewasilisha taarifa ya watumishi hewa na na zile ambazo hazijawasilisha taarifa hizo.

Ifuatyo ndio orodha ya Taasisi hizo:-

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO

MBUNGE WA RUFIJI ATOA MSAADA WA MABATI 650 KWA AJILI YA UJENZI WA UZIO WA UWANJA WA MPIRA MUHORO

0
0
 Mbunge wa  jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa kushoto akikabidhi msaada wa mabati kwa ajili ya kuweka uzio katika uwanja wa mpira ulipo katika shule ya msingi Muhoro Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani
Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akisalimiana na wazee maarufu ambao ni wadau wakubwa wa mchezo wa kandanda waliohudhuria sherehe hizo  katika kijiji cha muhoro mara baada ya hafla fupi ya kukabidhi mabati 650 kwa ajili ya kuweka uzio katika uwanja wa mpira uliopo shule ya msingi muhoro.
(Picha na Victor  Masangu).

NA VICTOR MASANGU, RUFIJI.
MBUNGE wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa katika kuunga juhudi za serikali katika kuboresha viwanja vya mpira ametoa msaada wa mabati 650 kwa ajili ya kuweza kuweka uzio ambao utaweza kusaidia kuingiza ukusanyaji wa mapato pamoja na kukuza na kuviendeleza  vipaji vya  mchezo wa soka kwa vijana.

Akikabidhi msaada huo wa mabati 650 katika hafla iliyofanyika katika uwanja huo wa mpira wa shule ya msingi Muhuro Mchengerwa aliesema kwamba uwanja huo  umekuwa ukitumika katika mashindano mbali mbali lakini changamoto kubwa ilikuwa hakuna uzio.

Mchengerwa alionngeza kuwa  lengo lake kubwa ni kuona katika jimbo lake vijana wote  wanashiriki kikamilifu katika michezo  ili kuweza kupata wachezaji wenye vipaji ambao wataweza kuchezea hata timu ya Tiafa katika siku zijazo.

“Mimi kama mbunge a jimbo la Rufiji nia yangu kubwa ni kuhakikisha kwamba ninawekamikakakti kabambe ya  kuwaendeleza vijana katika suala zima la michezo, na ndio maana nimeona kuna umhumihu mkubwa katika uwanja huu kuuzungushia uzio wa mabati, ili pindi ligi mbali mbali zinapofanyika kuweze kuwa na kiingilio ili fedha zitakazopatikaka ziweze kusukumu gurudumu ya kuendeleza michezo,”alisema Mchengerwa.

Aidha alibainisha kwamba wakati alipokuwa katika mchakato wa kampeni zake aliwaweza kuahidi kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya michezo kuanzia ngazi zote z vijiji hata ngazi ya Wilaya ikiwemo sambamba na kuboresha viwanja ambavyo vipo katika jimbo lake la Rufiji.

Pia alisema katika ktimiza azma yake ya kufufua vipaji kwa vijana na  kuviendeleza endeleza anatarajia kuanzisha mashindano makubwa ya mchezo wa soka ambayo yatazishirikisha timu mbali mbali kutoka kata zote 13 zilizopo katika jimbo lake.

Katika hatua nyingine Mchengerwa aliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuweka utaratibu wa kwenda kutembelea  timu zilizopo katika maeneo ya vijijina kwani kuna vijapi vingi ambavyo vinashindwa kuonekana kutokana na kutokupata sapoti ya kutosha hivyo kusababisha kukokosa wachezaji wazuri ambao wanatokea ngazi za chini.

“Hapa kwa hili pamoja na kuendeleza na juhudi za ngungu za kuendeleza vijaji vya wachezaji lakini TFF, ambao ndio wasimamizi wa mchezo huu wa soka kulianagalia suala hili kwa jicho la tatu, hususan kwa upande wa wachezaji wa ngazi za chini, kwani mimi nimeweza kubaini kuna wachezaji wengi wazuri sana ila changamoto wanajikuta wanakosa sapoti na kuwepo kw achangamoto ya viwanja,”alisema Mchengerwa.

Katika hatua nyingine aliongeza kwamba katika kukuza  sekta ya michezo atahakikisha kwamba kwa sasa anaweka program maalumu kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo wa soka ili kuweza kuwasaidia wachezaji wenye vipaji, sambamba na kuwapatia vifaa mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kufanya mazoezi.

COSTECH YAANDA Kongamano la tano la kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kuanzia tarehe 23 hadi 25 Agost, 2016.

0
0
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imeandaa Kongamano la tano la kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Kongamano hili ni fursa kwa wataalam wakiwemo watafiti, wabunifu, watunga sera pamoja na wajasiriamali kukutana na kujadili na kuelezea mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika kufikia taifa la viwanda. 

Kongamano la mwaka huu litafanyika kwa muda wa siku tatu, ukumbi wa Kisenga jengo la LAPF Kijitonyama, jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 23 hadi 25 Agost, 2016.  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.
Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: waziri@moh.go.tz

HITILAFU YA MKONGO WA MAWASILIANO (OPTIC FIBER), YATATIZA HUDUMA ZA TANESCO WILAYANI BAGAMOYO, SHIRIKA LAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE

0
0
Sehemu ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
NA MWANDISHI MAALUM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kuwatangazia wateja wake wote wa Wilaya ya Bagamoyo kuwa, kutokana na kukatika kwa waya wa mawasiliano, (Optic Fiber) kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, Ofisi ya Shirika hilo wilayani Bagamoyo bado inashindwa kutoa huduma za kupokea malipo na kuuza LUKU kwa muda mpaka hapo waya huo utakapoungwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Uhusiano MakaoMakuu yaTANESCO, Kwa sasa Shirika linawaomba wateja wake wanaotaka kununua umeme au kulipia huduma zingine za umeme kutumia njia mbadala ya mitandao ya Simu na makampuni mengine yenye mikataba na TANESCO.
Jitihada zinaendelea ili kuhakikisha mkongo huo wa mawasiliano unaungwa mapema iwezekanavyo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.



ASASI ZENYE MWELEKEO WA KUSHABIKIA USHOGA, KUKIUKA MAADILI KUWAJIBISHWA

0
0
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amezitaka asasi za kiraia zisiyumbishwe na misaada toka nje yenye mwelekeo wa kukinzana na mila, desturi, utamaduni, imani za Watanzania, sheria na Katiba ya nchi. 
Mhe. Dkt Mwakyembe ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam alipokutana na uongozi wa Taasisi ya Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) ofisini kwake  na kuwaambia kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za asasi mbalimbali za kiraia kama vile TGNP  za kuelimisha jamii na kutetea haki za watoto, wazee, wanawake, walemavu na makundi mengine maalum yanayostahili fursa na haki  sawa katika jamii yetu lakini haitazivumilia asasi ambazo zinaenda kinyume na maadili ya nchi na kukiuka sheria na taratibu ambazo kama nchi imejiwekea. 
“Serikali inaunga mkono kazi zinazofanywa na asasi za kiraia nchini lakini niweke wazi  kuwa hatutazivumilia asasi za kiraia zinazoyumbishwa na misaada toka nje na kujihusisha na vitendo ambavyo vinakiuka maadili, taratibu na sheria za nchi ambazo zipo kwa mujibu wa sheria,” alisema Mhe. Waziri. 
Alitolea mfano wa mashinikizo hayo kutoka kwa nchi zenye nguvu kiuchumi duniani kama ya kutaka nchi zinazoendelea au asasi zikubali ushoga na ndoa za jinsia moja kama sehemu ya haki za binadamu kama njia ya kuendelea kupata misaada kutoka kwao na kuongeza kuwa asasi zenye muelekeo huo nchini zinachunguzwa na zitakazobinika zitachukuliwa hatua kali. 
"Nchi hizo zimekuwa zikitoa mashinikizo kwa nchi zetu na hasa asasi nyingi zikizitaka zikubali ushoga na ndoa za jinsia moja, tunazichunguza asasi zote za kiraia zenye mwelekeo huo na tukibaini mapungufu hayo tutazichukulia hatua kali za kisheria, uchafu na upuuzi huo wa Wazungu, ubaki hukohuko kwao," alisisitiza.
Waziri Mwakyembe alionya kuwa nchi ikilegeza kamba katika suala hili, tutashinikizwa baadaye kufunga ndoa na wanyama wa kufugwa kwamba nayo ni sehemu ya haki za binadamu. 
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amon Mpanju, alisisitiza umuhimu wa asasi za kiraia kuisaidia Serikali kwa kupeleka kwenye jamii ujumbe sahihi wenye mafundisho badala ya kusubiri kukosoa tu na kuzitaka asasi za kiraia kuacha kuunga kuunga mkono hoja za ushoga kwa kishawishi cha fedha wanazopewa kutoka kwa wafadhili wao
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea katika kikao na watendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju (wa tatu kulia) baada ya kumaliza kikao jijini Dar es Salaam.

NEEC yatoa onyo kali kwa wanaolaghai wananchi juu ya upatikanaji wa sifa ya kupata shilingi milioni 50 kwa kila kijiji zilizoahidiwa na serikali ya awamu ya tano.

0
0
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) limetoa onyo kali kwa taasisi au watu binafsi wanaowatoza wananchi fedha kama ada ya usajili wa vikundi vyao vya kijasiriamali kwa madai ya kuwawezesha kuwa na sifa ya kupata Tshs milioni 50 kwa kila kijiji zilizoahidiwa na serikali ya awamu ya tano.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taasisi au watu binafsi ambao wanafanya udanganyifu huo.
“Serikali haijatoa fedha hizi na zitakapo toka mpango huu utatekelezwa na serikali na siyo taasisi wala watu binafsi,” alisema jana jijini Dar es Salaam na kusema wanaofanya hivyo waache mara moja tabia hiyo.
Hadi sasa pamekuwa na taarifa za udanganyifu huo katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mbeya, Tanga na Njombe.
Taasisi hizo na watu binafsi hao huvitoza vikundi hivyo vya wananchi kati ya Tshs 10,000 na Tshs 100,000.
“Taasisi au watu binafsi hawa wanadanganya wananchi kuwa wametumwa na baraza, jambo hili si kweli,” alifafanua.
Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola mara wanapobaini taasisi au mtu binafsi anayewashawishi kutoa fedha hizo kama ada ili vikundi vyao viweze kusajiliwa na kufaidika na fedha za kila kijiji.
Kwa mujibu wa Bi. Issa, fedha kwa kila kijiji zitatolewa kwa kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia vyama vya ushirika vya akiba na mikopo (SACCOS), Vikundi vya Kifedha vya Jamii (VICOBA) na vikundi vingine ili viweze kuanzisha au kuendeleza shughuli za kiuchumi.
“Ni vyema sheria na taratibu za nchi zikafuatwa,” alisema na kuongeza kuwa serikali ipo mbioni kukamilisha utaratibu wa utekelezaji wa mpango wa fedha hizo kwa kila kijiji na kwamba ukiwa tayari taarifa itatolewa rasmi kwa umma.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa za kuwepo kwa taasisi na watu binafsi wanaowatoza wananchi fedha kama ada ya kujisajili katika vikundi vya kijasiriamali ili wawe na sifa ya kupata Tshs milioni 50 kwa kila kijiji zilizoahidiwa na serikali ya awamu ya tano.

JESHI LA POLISI LAWAONDOA HOFU WANANCHI KUHUSU MAZOEZI YA KAWAIDA YA POLISI

0
0
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 
Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi. 
Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi. 

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)

Msemaji wa Jeshi la Polisi,


Makao Makuu ya Polisi.

Viongozi wa kisiasa watakiwa kuwa wavumilivu ili kulinda amani nchini

0
0

Na Sheila Simba-MAELEZO
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa viongozi wakisiasa Nchini, kuwa wavumilivu ili kulinda Amani ya Nchi.
 Sheikh Alhad ameyasema hayo leo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam ambapo amewataka viongozi hao kutii mamlaka iliyoko kwani mamlaka hiyo imewekwa na Mungu na hivyo ni vema kutafuta njia nyingine kumaliza matatizo yanapotokea.
“Ipo haja ya kuvumiliana kwa ajili ya Taifa letu, kwani yanapotokea machafuko waathirika wakubwa ni wanawake, watoto na vijana wetu ambao wanaweza kupata madhara makubwa na hata kupoteza maisha’’alisema Alhad
Akizungumzia maandamano ya ukuta yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi, amesema kuwa kauli ya kuzuia maandamano hayo imetolewa na Rais wa Nchi na kuomba kauli hiyo kuchuliwa kwa uzito wa kipekee, kwani busara ni kusikiliza mamlaka imesema nini na kutii kauli hiyo ya Rais.
“Nawashauri  Watanzania wenzangu, viongozi wangu wa kisiasa jambo hilo si vyema tukashiriki kwani kutotii mamlaka ni dhambi ndivyo vitabu vya dini vinanavyosema,’’ alifafanua Sheikh Alhad
Ameongeza kuwa suala la kulinda amani ni la watanzania wenyewe kwa kusaidiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha amani inaendelea kuwepo, kwani ni rahisi kupoteza amani tuliyonayo lakini ni vigumu kurudisha amani.
Amesema kuwa vijana wasikubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine kwani kufanya hivyo ni kushindana na dola na kutolea mfano wa machafuko yanayoendelea kwa baadhi ya Nchi Duniani na kupelekea mataifa hayo kutokalika kutokana na vurungu za kisiasa.
Aidha amewaomba vijana kutokubali kulitia doa Taifa, kwani Tanzania inafahamika ni kisiwa cha Amani Duniani na inapaswa kulinda heshima hiyo ili kuendelea kutunza amani ya Watanzania wote bila kujali tofauti za kisiasa.
Amewaomba viongozi hao wa kisiasa kuwasilisha malalamiko yao kwa njia tofauti kwani Serikali iliyopo madarakani ni sikivu na ipo kwa ajili ya wananchi wote.

IBADA YA SHUKRANI

0
0
Kama Kristo alivyokufa na kufufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye I The. 4:14


Famila ya Bw. Barnaba Leo Kidulile wa Mbezi beach, Dar es Salaam tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote kwa maombi pamoja na msaada wenu wa hali na mali mliotoa katika kufanikisha mazishi ya mama yetu mpendwa Anna Mary Kidulile (pichani) aliyeitwa na Mungu tarehe 28/02/2016 katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa tarehe 02/3/2016 makaburi ya Ununio Tegeta – Dar es salaam. 
Tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Familia ya Bw. E.P Mkwawa, Familia ya Bw. S. Ezekiel, Familia ya Bw. J. Mapunda, Familia ya Bw. B. Kimwaga na Familia ya Bw. F. Kayombo, Wana Ludewa, Mufindi, Nyanyembe na Malangali. Pia tunapenda kutoa shukrani kwa Ukoo wa kina Kilatu na Mlyuka, wafanyakazi wa TANESCO, Dar es Salaam Community BANK PLC, PPRA, TRA, Shule ya Msingi Kunduchi, waalimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili na majirani wote wa Kilongawima.
Shukrani za pekee ziwaendeee mapadre wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Mikael Kunduchi, wana jumuiya ya Mtakatifu Andrea, madaktari na wauguzi wa hospitali za Regency na Muhimbili. 
Kipekee tunapenda kuwaalika ndugu, jamaa na marafiki pamoja na waumini wote katika ibada ya shukrani itakayofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Mikael Kunduchi, Dare es Salaam, siku ya Jumamosi ya tarehe 27 Agosti 2016 saa 3.00 kamili asubuhi na baadae chakula cha mchana. 

Ibada hiyo itatanguliwa na mkesha na maombi yatakayofanyika nyumbani kwa Familia ya Barnaba Leo Kidulile Mbezi beach - Mtaa wa Jangwani siku ya Ijumaa tarehe 26 Agosti kuanzia saa 3.00 usiku. Wote Mnakaribishwa.


Heri wenye moyo safi maana 
hao watamuona Mungu – Mt. 5:8



  

KARIBU “ JIKO DISH “ : LISHE MAALUMU KWA WANAUME WENYE TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

0
0
NEEMA  LISHE  CAFÉ  ni  waandaaji  na  watayarishaji   wa  lishe  maalumu  kwa  watu wanao  sumbuliwa  na  matatizo mbalimbali ya kiafya  kama vile, kisukari, presha nakadhalika.

Tunayo  furaha  kuwatangazia  wateja  wetu   waliopo jijini  Dar  Es  Salaam,  kuwa, sasa tunaandaa  na  kutayarisha   lishe  maalumu  iiwatyo  “JIKO DISH ”  maarufu  kama  KIBOKO YA  PWEZA. 

Lishe  hii  ni  maalumu  kwa watu  wanao  sumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu na upungufu  wa nguvu  za  kiume.  Lishe  hii  maalumu,  inaandaliwa  
kwa  kutumia  vyakula –lishe  mbalimbali, pamoja  na mmea  uliomo  katika  orodha  ya mimea  inayo  tambuliwa  na  SHIRIKA  LA AFYA  ULIMWENGUNI  
yaani W.H.O na  ambao  UMEKAGULIWA  na  KUTHIBITISHWA  NA MKEMIA  
MKUU  WA SERIKALI.

Lishe  hii inatumika  mara  moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini.  
Lishe  hii INATIBU  na  KUPONYESHA  kabisa  tatizo  la  UKOSEFU  
na  UPUNGUFU  WA  NGUVU ZA  KIUME ndani  ya  siku  thelathini.

                                                            JINSI   YA  KUIPATA  LISHE  HII.

Kuipata  lishe  hii, wasiliana  nasi  kwa  simu namba  0766  53 83 84,  na   utaletewa  mahali popote  ulipo  jijini  Dar  Es  Salaam.

Kwa maelezo  zaidi kuhusu  huduma  zetu  nyingine, tutembelee  kila  siku  kwenye  blogu yetu ;


                                                                         www.neemaherbalist.com

EFM KUZINDUA TAMASHA LA MUZIKI MNENE AGOSTI 28 MWAKA HUU BOKO JIJINI DAR

0
0
 Meneja Mkuu wa Efm  Bw. Denis  Ssebo akizungumza leo na waandishi wa habari  juu ya tamasha kali  la kila mwaka lijulikanalo kama MUZIKI MNENE  ambalo litaanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko  jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Vodacom Bi.  Nandi Mwiyombella akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon  jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

REDIO ya burudani ya Efm imezindua tamasha la kila mwaka lijulikanalo kwa jina la MUZIKI MNENE,ambalo linatarajia kuanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Efm, Denis  Ssebo amesema tamasha hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki 12 sawa na miezi mitatu ambapo muziki utapigwa  katika bar 12 za vijijini vya Dar es Salaam na  Pwani ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Tunasepa na kijiji '.

Alisema mziki mnene mwaka huu itaenda sambamba na kampeni ya nje ndani ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku nne mfululizo.
Ssebo alivitaja vipindi hivyo kuwa ni Uhondo ambacho kitafanyika siku ya jumatano, Sports headquarters siku ya Alhamisi, joto la asubuhi siku ya Ijumaa na Funga mtaa siku ya jumamosi ,ambapo pia utapigwa muziki wenye ladha ya singeli kwa lengo la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki huo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano vodacom Nandi Mwiyombella alisema wanafurahi kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon."Burudani ndio sehemu ya maisha ya kila mtu na lengo ni kuhakikisha kwamba wateja wetu anapata burudani ya muziki kupitia Efm,"amesema Nandi.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live


Latest Images