Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 131 | 132 | (Page 133) | 134 | 135 | .... | 3283 | newer

  0 0
 • 05/11/13--23:48: Article 15


 • 0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akiwa ameshikilia Tuzo ya Bia ya Safari Lager mara baada ya kuipokea mkoani kwake mwishoni mwa wiki ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  ilikuwa Mkoani Iringa.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akizungumza na wananchi wa Mji wa Iringa katika Uwanja wa Mwembe Togwa  wakati upokeaji Tuzo za Bia ya Safari Lager mkoani kwake mwishoni mwa wiki ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  ilikuwa Mkoani Iringa. Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kulia) na Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma wakinyanyua Tuzo za Bia ya Safari Lager ilizoshinda katika mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembe Togwa mjini Iringa wakati wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia yake ya Safari Lager.

  0 0


  Jumuia ya watanzania Wasabato walioko Marekani inawaalika katika mkutano mkubwa wa mwaka wa kiroho (TAUS Retreat 2013) utakaofanyika Houston TX. Wote mnawakaribishwa kujumuika nasi.

  TAREHE ZA MKUTANO: July 11-14, 2013

  MAHALI- Oak SDA School, 11735 Grant Road, HUSTON, TEXAS 77429 USA

  MGENI RASMI: Mchungaji Lucas Nzungu wa Arusha University, Tanzania

  Gharama za mkutano, chakula na hoteli (Holiday Inn) ni $292.50 kwa mtu aliye tayari ku’share’ chumba (double bed). Kwa wanaotaka chumba cha pekee (single bed), jumla yao ni $465. Kuna wafadhili kadhaa wanaoweza kusaidia malazi na chakula. Tafadhali ulizia kama unahitaji msaada huo.

  Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na mmoja wetu- Msafiri Lugoe (TX) 281-760-6805; Jeoffrey Ngullu (PA) 267-582-6276; Shukrani Magoma (DC) 2020-607-1976. Asanteni sana na karibuni tubarikiwe pamoja.

  0 0


  Na Mwandishi Wetu

  KAMATI ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya International Agency ikiongozwa na Mkurugenzi wake pia Mratibu Hashim Lundenga imewafunda ipasavyo warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Kibaha 2013 litakalofanyika Mei 17 katika ukumbi wa Container mailimoja Kibaha.

  Akizungumza wakati alipowatembelea katika kambi yao warembo hao Lundenga aliwataka washiriki hao wajijengee hali ya kujiamini na kila mshiriki asimwogepe mshiriki mwenzake huku akiwataka kila mmoja awe amejiwekea lengo la kufika katika shindano la Kanda na hatimaye taifa.

  Aidha Lundenga amewaasa warembo hao kumpa sapoti mrembo atakayetwaa taji hilo ,” endapo mrembo mwenzenu yeyote ataiobuka na kutwaa taji lazima mumpe sapoti kubwa kwani ‘crown’ huvaliwa na mrembo mmoja tu hivyo nawatakia kila la kheri katika shindano lenu na niwaahidi tutakuwa pamoja hadi siku ya shindano”alisema Lundenga.

  Mwisho Lundenda alimazia kwa kusema kuwa mrembo atakayeonesha utovu wa nidhamu atatolewa katika shindano hata kama itakuwa ni siku ya fainali hivyo amewataka wawe makini wakati wote.

  Wakati huohuo Miss Tanzania 2012 Brigite Alfred aliyeambatana na kamati hiyo alitumia fursa hiyo kutowa mashaka ya mrembo kupangwa kuanzia katika ngazi ya awali hadi taifa.

  “Warembo wenzangu kwanza nawapongeza kwa hatua hii ya kujitosa kushiriki kwani ni hatua kubwa kwa sababu hata mimi nilianzia katika ngazi ya awali kama hii lakini tangu nilipoingia katika shindano hilo nilijiona ni mshindi hali iliyonijengea kujiamini hata nilipokwenda katika shindano la Kanda na hatimaye taifa hivyo nawatakia kila la kheri.

  Shindano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution litapambwa na bendi ya Mashujaa huku kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa VIP na siti za kawaida sh. 6,000.
  Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Redds Premium Cold, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Multichoice DSTV, Times FM, Michuzi Media Group (MMG), Santorine Holiday Resort ,PR.Promotion, Aco Catering Servises , Amazon Night Club na Panandipanandi Pub . 

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi katikati akizunguza katika mkutano wa Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue) uliofanyika Mkoani Iringa na Kushirikisha makundi ya wananchi kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capt. Aseri Msangi na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Bw. Raymond Mbilinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, ambapo jadiliano hayo yalikuwa yanalenga kupata maoni ya wananchi juu ya matumizi ya sayansi na teknolojia katika uzalishaji.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi katikati akibadiliashana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kushoto) na kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa la Biashara TNBC, Bw. Raymondi Mbilinyi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) katika majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue) uliofanyika mkoani Iringa na kuyashirikisha makundi ya wananchi kutoka mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe, majadiliano hayo yalikuwa yanalenga kupata maoni ya wananchi juu ya matumizi ya sayansi na teknolojia katika uzalishaji.

  0 0

  Wachezaji wa timu za Taswa FC (wenye jezi za bluu) pamoja na wapinzani wao wa Bongo Movie,wakisikiliza kwa makini maelekezo toka kwa refarii wa mchezo huo ambaye alikuwa ni Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Ally Kiba (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mtanange wao ulipigwa kwenye Viwanja vya Sigara (TCC),Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana jioni.Mtanange ulikuwa ni mkali sana kwa pande zote mbili na hadi mwisho wa mchezo timu ya Bongo Movie iliibuka kidedea kwa bao 2 - 0.hii ikiwa ni kwa upande wa mpira wa miguu lakini katika mpira wa pete,timu ya Taswa Queens iliibanjua timu ya Bongo Movie kwa Mabao 38 - 10.
  Straika wa timu ya Taswa FC,Juma Pinto akichuana vikali na Beki wa timu ya Bongo Movie (ambaye hajawahi kuonekana kwenye movie) wakati wa mtanange wao uliopigwa jana jioni kwenye Viwanja vya Sigara (TCC),Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
  Watazamaji upande wa Taswa FC.
  Watazamaji upange wa Bongo Movie.
  hapa ni bambi kwa bambi,huku Refa akiangalia kwa makini kuona kwamba hachezewi mtu faulo.
  Taswa FC kwa chenga tu hawajambo.
  Mtanange mkali kati ya Taswa Queens dhidi ya timu ya Bongo Movie ukiendea kwa kwa kasi.hadi mwisho wa mchezo huu Taswa Queens iliibuka kidedea kwa Mabao 38 - 10.


  0 0

  TANZANIA ni mwenyeji wa Kongamano kubwa la siku tatu la kikanda wa kilimo wa muungano wa umoja wa vyama vya kilimo kusini mwa Afrika (SACAU)ambao unaanza leo jijini Dar es Salaam na kumalizika kesho kutwa.

  Kongamano hilo litakaloangalia kwa undani swala la jinsi ya kuhudumia kifedha kilimo cha Afrika limeandaliwa na Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) kwa kushirikiana na SACAU ambapo maandalizi yake yamekamilika.

  Mkurugenzi Mtendaji wa ACT, Bi. Janet Bitegeko, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa takribani washiriki 200 kutoka nchi 14 za kusini mwa Afrika pamoja na wawakilishi wa vyama vya wakulima kutoka maeneo mengine ya Afrika wamethibitisha ushiriki wao.

  “Mkutano utaangalia ushirikiano kati ya SADC/COMESA/EAC katika maswala ya kilimo na mambo mengine ambayo yanalenga kuleta mapinduzi ya kilimo katika nchini husika,” Bi. Bitegeko alisema.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, mkutano huo ambao unafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza hapa nchini moja ya mambo mengine utaangalia makisio ya mahitaji ya bidhaa za kilimo duniani na kuona fursa na tishio lake kwa wakulima.

  Bi. Bitegeko aliongeza kuwa kongamano ambalo litakalokusanya wakulima toka sehemu mbalimbali Afrika litashuhudia kuzinduliwa kwa mradi wa majaribio wa kilimo wa SACAU hapa Tanzania.

  “Mkutano utaangalia ushirika huo kwa undani, muundo wake na umuhimu wake kwa wakulima na biashara katika sekta hii ya kilimo,” alisema na kuongeza kuwa kongamano hilo linakuja na majibu thabiti ya jinsi ya kuinua kilimo hapa nchini, katika kanda na Afrika kwa ujumla.

  Baada ya kongamano hilo, SACAU itafanya mkutano mkuu wake wa mwaka na kufanya uchaguzi wake. Kwa sasa, Tanzania inawakilishwa na Bw. Salum Shamte katika bodi ya SACAU.

  “ washiriki wa mkutano/kongamano huo watafanya ziara kutembelea wakulima wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani,” Bi. Bitegeko alisema. ACT ni chama kinachounganisha wadau mbalimbali wa kilimo hapa nchini.

  0 0

  Na Abdulaziz Video

  Baadhi ya Abiria na Wasafishaji wa Abiria wilayani Nachingwea,mkoa wa Lindi wametishia kuandamana na kususia kutumia kituo kipya cha Mabasi wilayani huo kutokana na kutokamilishwa kwa miundo mbinu ikiwemo kutowepo kwa sehemu ya kupumzikia Abiria.Umeme,maji na Umbali wa kituo cha Mwisho hadi kituo kikuu kipya ambacho kipo pembezoni mwa mji.

  Wakizungumza na mtandao huu,jana Ahmeid Mmow na Abdallah Ng’itu kwa niaba ya abiria waliitaka Halmashauri hiyo kuharakisha inakamilisha huduma walizobainishiwa na uongozi wa wasafirishaji ikiwemo uwepo wa kituo kidogo cha kushushia abiria katikati ya mji ili kupunguza gharama huku wengine wakiwa walemavu na wagonjwa ambao hawana uwezo wa kugharamia bodaboda hadi kwenye kituo hicho kipya.

  Mmow alisema kuwa abiria hawana tatizo la kituo hicho kuamishwa bali wanachohitaji ni kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana na kuwa bila kufanya hivyo wasafiri wa wasafirishaji watafanya maandamano makubwa kupinaga hatua ya halmashauri hiyo kuwamisha kituo bila kukamilisha mabmbo muhimu.

  “ Hatuna tatizo la kuhamia kwenye kituo hicho kipya bali tunachohitaji ni kuhakikishiwa halmashauri inakamilisha mahitaji hasa jengo la kupumzikia abiria na warejeshe vituo vingine”alisema Mmow.

  Uamuzi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya kufunga kituo cha Mabasi cha awali kimezua malalamiko makubwa kufuatia uwepo wa kituo kipya kuwa nje ya mji na kupelekea ongezeko Kubwa la gharama za usafiri na uhakika mdogo wa usalama wao pindi basi litapoingia usiku au Alfajiri kwa kuanza safari.

  Mwenyekiti wa wasafirishaji wilayani Salum Jabu alisema kuwa kufuatia tatizo hilo ambalo kwa kiasi kikubwa kinawaathiri wasafiri wengi ambao wanatoka nje ya mji kwani wanakosa mahali pa kulala kwani awali abiria wengi ambao hawana uwezo wa kulala kwenye nyumba za wageni walikuwa wanapata mahali pa kulala kwenye ofisi za wakala wa kusafiriashia kitu ambacho kwa sasa haiwezekeni kutokana na eneo la kituo kipya kutokuwa na majengo.

  Hali ni tofauti kwani wakati wasafiri na wasafirishaji wakilalamika madereva wa boda boda wao wanaona kuwa hiyo ni fursa kwao kwani wanapata kpato kikubwa kwa kuwasafirisha abiria hadi kituo hicho kipya au kwenye kituo cha pili ambacho kipo Stesheni zakizungumnzia hilo mwakilishi wa waendesha bodaboda Abdalah Ngitu alisema kuwa kwa sasa kwao ni biashara mzuri kwani kutokana na umbali ba hali ya usalama wananlazimika kusafirisha abiria mmoja kwa kati ya shilingi 3000 hadi 5000 kwa muda wa usiku.

  Akizungumzia malalamiko hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nachingwea,Arbogast Kiwale alikiri na kudai kuwa kwa sasa halmashauri imeamua kufungua kituo hicho na kuwa tayari ujenzi wa mahali pa kupumzikia abiria lipo kwenye hatua za mwisho na kutarajiwa kuwa limekamilika muda mfupi ujao.
  Sehemu ya Mabasi yakiwa yamepaki kwenye kituo hicho.
  Abiria
  Vibao vinavyoonyesha namna ya mabasi yatakavyoegeshwa,japo hakuna hata moja lililopo.
  Basi zikipishana


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwasalimia viongozi wa Chama alipowasili uwanja wa Ofisi ya CCM KIsiwandui Mjini Unguja kukiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika leo.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halamashauri Kuu ya CCM Taifa,katika ukumbi wa CCM KIsiwandui leo,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, na Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto).
  Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri kuu ya Taifa,wakipitia agenda mbali mbali za kikao hicho kinachoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa mikutano wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri kuu ya Taifa,wakipitia agenda mbali mbali za kikao hicho kinachoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa mikutano wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

  Minister/Head of Chancery, Nigeria High Commission in Tanzania, Mr Joseph Atodo; Nigeria High Commissioner to Tanzania and Comoros, Dr Ishaya Samaila Majanbu; former Nigeria’s President, Chief Olusegun Obasanjo; Director General, International Institute of Tropical Agriculture (IITA), Dr Nteranya Sanginga; Director for IITA Eastern Africa Hub, Dr Victor Manyong; and Tanzanian Director for Africa, Ambassador Vincent Kibwana, during the arrival of the former president for the inauguration of the IITA Science Building in Dar… on Sunday.
  Director General, International Institute of Tropical Agriculture (IITA), Dr Nteranya Sanginga; Director for IITA Eastern Africa Hub, Dr Victor Manyong; Nigeria High Commissioner to Tanzania and Comoros, Dr Ishaya Samaila Majanbu; and former Nigeria’s President, Chief Olusegun Obasanjo; during the arrival of the former president for the inauguration of the IITA Science Building in Dar… on Sunday.


  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walioshiriki katika warsha ya wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati,iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa,Warsha hiyo inayofanyika mara moja kwa mwaka ilifanyika jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha wanawake zaidi ya 150.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika warsha ya wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati,iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa,Warsha hiyo inayofanyika mara moja kwa mwaka ilifanyika jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha wanawake zaidi ya 150.
  Washiriki wa warsha ya wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati,wakifungua warsha hiyo kwa kusali.Warsha hiyo iliandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa.Warsha hiyo iliyoshirikisha wanawake zaidi ya 150 hufanyika mara moja kwa mwaka jijini Dar es Salaam.
  Mkufunzi na Mtaalamu wa maswala ya ujasiriamali Bi.Rehmah Kasule,akitoa elimu kwa wanawake zaidi ya 150 juu ya kuwawezesha kujua mbinu za kujiendeleza katika kukuza biashara zao,Warsha hiyo iliandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa,na kufanyika mara moja kwa mwaka jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa nyimbo za injili ambaye pia ni mjasiriamali Bi. Elizabeth Benard akiimba wimbo wa "anafanya jambo" katika warsha ya wanawake wajasiriamali zaidi ya 150.Warsha hiyo iliandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa.Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream,Bi.Emelda Mwamanga,akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari juu ya warsha ya wanawake wajasiriamali iliyoandaliwa na tasisi yake na kudhamaniwa na Vodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa.Warsha hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Uholanzi na Comoro. Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.

  Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-

  Bw. Wilson M. K. Masilingi (kulia) Ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw. Masilingi ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010. Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005 alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora. 
  Bw. Chabaka Faraji Ali Kilumanga (kushoto) , ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya Ubalozi nchini Uingereza.

  Bw. Modest Jonathan Mero (kulia), ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva. Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New York.

  Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang’ka Marmo  (kushoto) kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.
  John M. Haule
  KATIBU MKUU,
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, 
  DAR ES SALAAM.
  12 MEI, 2013
  0 0

  KATIKA kuelekea mchezo wa jana dhidi ya Flamingo FC ya Arusha, Machava FC ambo ndio mabingwa wa ligi daraja la Tatu, mkoa wa Kilimanjaro, wamekabidhiwa vifaa vya michezo na uongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi.

  Machava FC walikabidhiwa vifaa hivyo ambavyo ni mipira mitano na Jezi, kama sehemu ya mchango wa Chama hicho kwa timu hiyo ambayo kwa sasa ndio inayobeba Roho ya mkoa wa Kilimanjaro katika medani ya soka.

  Akizungumza baada ya kukabidhi vifa hivyo vilivyotolewa kwa timu hiyo na Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM, Jerry Silaa, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini Aluu Segamba aliwahakikishia wapenzi wa soka mkoani hapa kuwa wako tayari kushirikiana nao hadi mwisho wa Safari.

  “Leo tunatimiza ahadi yetu kwa wawakilishi wetu, mabingwa wa Mkoa timu ya Machava, tunaamini kuwa timu hii kama roho ya kilimanjaro katika mchezo wa soka itafanya makubwa na kinachotakiwa ni kuwapa sapoti inayostahili,” alisema Segamba.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Abuu Masoud, baada ya kupokea msaada huo kutoka CCM, alisema kutokana ushirikiano unaoneshwa na wadau wa soka kwa timu yao wanaahidi kufanya vizuri katika michezo yao yote na kuwapa raha wapenzi na mashabiki wa Machava mkoani Kilimanjaro.

  Kwa upande kocha msaidizi wa machava aliwaondoa hofu mashabiki wa timu yake kuhusu hali ya Afya ya mshambuliaji wa kutumainiwa wa klabu hiyo, Isa Kipese na kuelekea mchezo wa jana na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni ripoti za madaktari wanaomshughulikia mchezaji huyo.


  Machava FC ambayo inauwakilisha mkoa katika michezo ya Mabingwa wa mikoa imekuwa ikipokea sapoti kutoka kwa wadau wa michezo mkoani hapa ambapo hivi karibuni tu Mbunge wa Moshi Mjini, Filemon Ndesamburo na Mstahiki Meya wa Moshi, Jafary Michael walitembelea kambi ya timu hiyo na kuchangia fedha taslimu shilingi laki saba.


  Katika hatu nyingine chama cha Mapinduzi CCM pia imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya Gillete Fc ya kata ya Kaloleni kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho za kutoa fursa nyingi za ajira kwa njia ya michezo.

  Akikabidhi vifaa hivyo, mipira miwili na Jezi kwa diwani wa kata ya Kaloleni, Michael Mwita, Segamba alisema kuwa wanalenga kuunganisha umma wa mkoa wa Kilimanjaro, kupitia michezo na kuongeza kuwa katika swala la michezo watu wote ni ndugu bila kujali itikadi zao.

  0 0

  Familia ya Bwana Thomas Martin Kiama wa mtaa wa Bongoyo, Oysterbay wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Victoria Thomas Kiama (pichani) kilichotokea tarehe 11.05.2013 saa mbili na nusu usiku katika Hospitali ya Aga Khan mjini Dar es Salaam. 

  Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu -Bongoyo, Oysterbay. Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo.
  Bwana Mungu ametoa, Naye ametwaa, 

  Jina lake libarikiwe milele na milele. 
  Amina.

  0 0

  Wakiwa na nyuso za furaha ni  Watanzania Pastor Emmanue Masanja Mbaaga (Kulia), Milcah Thomas (kati) na Mghana  Pastor Charles Koomson  (Kushoto) ambao  wahitimu wa shahada ya uzamili wakipiga picha ya pamoja kabla ya kupokea shahada zao jana, Jumamosi May 11, 2013, katika chuo kikuu cha Liberty , Lynchburg, Virginia,  nchini Marekani `
  Wakiwa na nyuso za furaha ni  Watanzania Pastor Emmanue Masanja Mbaaga (Kulia), Milcah Thomas (kati) na Mghana  Pastor Charles Koomson  (Kushoto) ambao  wahitimu wa shahada ya uzamili wakipiga picha ya pamoja kabla ya kupokea shahada zao jana, Jumamosi, May 11, 2013, katika chuo kikuu cha Liberty, Lynchburg, Virgia nchini Marekani 
  0 0


  Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU  kwa minajili ya kuielimisha jamii  kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na  kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.

  Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii (wote waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA . 

  Waziri Mkuu Pinda akizungumza mbele ya  baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine wa sanaa waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.

  Mh.Pinda aliishukuru kampuni ya Clouds Media Group kwa kazi nzuri walioianzisha ya kuwasaidia vijana kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwaamsha na kuwafungua macho na kuwaelimisha namna ya kuziona fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,aliongeza  kuwa kupitia ujumbe huo wa MADE IN TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga ratiba nzuri ya kuliendeleza zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha taasisi nyingine zikiwemo za serikali katika kuhakikisha jambo hilo linaendelea.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda.
  Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema leo kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
  Sehemu ya umati wa watu ukiwa kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika nafasi ya kujikwamua kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
   Baadhi ya Wasanii wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake Kajala walikuwa ni miongoni mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo ya mshikamano yaliyokuwa yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba jumbe mbalimbali za kupinga wizi wa kazi sanaa.
   Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini .
   Baadhi ya Watangazaji wa clouds FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya/tasnia ya filamu na wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa pamoja kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh Waziri Mkuu Pinda.
  PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0

  It is 15 years time since you became called by almighty God on May 1998 There Is A Wonderful Legacy Of Which We Wish To Tell About A Wonderful Man That We Loved So Well His Strength Lives Within Us And Grows Stronger Each Day His Honor Still Lingers Though His Life Has Slipped Away We Miss The Sound Of His Laughter And His Stern Lectures Too!

  We Miss Hearing Him Say, “Keep The Faith! Do Not Forget To Pray!” He Fought A Good Battle He Finished The Race But Gave Up The Worldly

  To Rest In The Arms Of Jesus What A Beautiful Sight… He Is Now Looking at Jesus Face to Face

  What A Delight……….

  Three years Later, You are Still Fondly remembered by Your wife Edeth Mwamlima,Your son’s Lupe Mwamlima,Borady Mwamlima,Alinuwila Mwamlima,your daughters, your Friends and thousands of people whose lives you touched! I have fought a good fight, I have finished my course, I have kept the faith.

  0 0


  0 0


   Baadhi ya Viongozi, Wajumbe na  Wanachama Wapya katika picha ya pamoja
    Mwenyekiti wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Maina Ang’iela Owino akimkabidhi vitendea kazi  ikiwemo katiba ya chama kwa Ndugu Chande Kigwalilo mwenye kofia Mwenyekiti Shina jipya la Cardiff.
  Katibu wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Bi. Mariam Mungula akimkadhi kadi za wanachama wapya Katibu wa shina Jipya la CCM Cardiff Bi. Rosemary Kiputa.


  0 0
 • 05/13/13--00:17: GADO LEO


older | 1 | .... | 131 | 132 | (Page 133) | 134 | 135 | .... | 3283 | newer