Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

JE YANGA KUENDELEZA UBABE KWA AZAM?

$
0
0
 Na Zaina  Nyamka, Globu ha Jamii.
IKIWA Yanga wanahitaji kuendelea kunyakua Ngao ya Hisani kwa mara ya nne mfululizo na wakiwa tayari wameshanyakua mara sita, timu ya Azam nayo imejizatiti kuhakikisha mara hii wanachukua kwa mara ya kwanza.

Katika historia ya timu hizo mbili zimekutana mara 25, Yang ikifanikiwa kushinda mara 10 Azam wakishinda mara nane wakienda sare mara saba.

Yanga wamefanikiwa kuifunga Azam mara tatu mfululizo katika mchezo wa ufunguziwa ligi yaani Ngao ya Hisani na kufanikiwa kulinyakua mara tatu mfululizo kombe hilo.
Benchi la ufundi la Yanga, likiwa chini ya Mholanzi Hans Van De Pluijm anakutana na Azam kwa mara ya pili mfululizo  huku Azam wakiw chini ya benchi jipya la makocha kutoka nchini Hispania.

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas ametangaza viingilio vya mchezo huo ni 5000 kwa viti vya bului, Kijani na machungwa, VIP B /C ni 15000 huku VIP A itakuwa ni 20000 na katika mapato ya mchezo huo kiasi cha fedha kitakachopatikana kitanunua madawati 200 na kuyapeleka kwenge Ofisi za Bunge na kumkabidhi Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Thomas Kashilila.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 10 alasiri katika dimba la uwanja wa Taifa unatarajiwa kuonyeshwa na kituo cha Televisheni cha ATN baada ya kupata haki za kurusha matangazo ya mechi hiyo.

MABALOZI NA WAWAKILISHI WA MABALOZI HAPA NCHINI WASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO.

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefungua kitabu cha maombolezo kwa ajili ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa walioko nchini kutoa salaam zao za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee ABOUD JUMBE MWINYI. 

Kitabu hicho kitakuwa wazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Albert Luthuli, Dar es salaam kuanzia leo siku ya Jumanne Agosti 16 hadi Ijumaa Agosti 19, 2016 toka saa 4 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

Mzee ABOUD JUMBE ambaye pia alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifariki dunia juzi nyumbani kwake Mji Mwema, Kigamboni, Dar es salaam na kuzikwa jana katika makaburi ya Migombani Unguja, Zanzibar.

Wana-diplomasia wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kutoka Finland, Msumbiji, Burundi, Uganda na Angola tayari wameweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.

Mzee JUMBE alishika madaraka ya kuongoza Zanzibar mwaka 1972 baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume baada ya Baraza la Mapinduzi kumchagua kwa kauli moja. Kutokana na kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar mwaka 1984, Mzee JUMBE alilazimika kujiuzulu na viongozi wengine.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam

Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Finland Bw. Simo Pekla Parvianen akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. 


Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Bi. Monica Patricio Mussa akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. 
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Elitrea Bw. Saleh Azaril 
Kaimu Balozi wa Burundi nchini Tanzania Bw. Pierre Ndayishimiye 
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Angola Bw. Joel Cumbo .Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Selikarini, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Je Unaujua Undani wa Mapacha?? wajue hapa Kiundani

$
0
0
Imekusanywa na Geofrey Chambua

Yasemekana mapacha ni watu ambao hupendwa sana na jamii kwa muonekano wao pia.

Ufuatao ni ukweli wa kushangaza kuhusu watoto mapacha.

1. Yumkini Mapacha wanaweza kuzaliwa na Baba wawili tofauti iwapo mama atajamiiana na wanaume wawili tofauti akiwa kwenye kipindi cha kushika ujauzito (ovulation period) ......ingawa wanasayansi wanasema uwezekano ni mtoto 1 kati ya watoto 400

2. Uwezekano wa kuzaa watoto mapacha umeongezeka sana hadi kufikia 76% tangu 1980 hadi sasa na hasa kutokana na ukweli kwamba wanawake wengi kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakishika ujauzito haliyakuwa umri umesogea na wengi wana uwezekano wa kupata mapacha iwapo watazaa katika umri wa miaka 30 na kuendelea (wanawake katika umri wa 30yrs wana uwezekano mkubwa kuzaa mapacha kuliko wanaume katika umri wa 20yrs).....sababu za wanawake zinaelezwa ni kutokana na kuzalisha homoni nyingi za 'kiraghbishi' katika umri huu na hasa wanaposhika ujauzito katika umri wa miaka 35 (Follicle Stimulating Hormones). 
3. Utafiti uliofanywa na Taasisi moja ya Lafudhi ( Institute of General Linguistics) umeonesha kwamba watoto mapacha hujifunza matamshi baina yao wenyewe kwa njia ya kubwabwaja (babbling) na zaidi ya 40% huunda lugha tashtiti kwa mawasiliano baina yao (privacy) wakingali wadogo (cryptophasia)

4. Mapacha wengi huakisi taswira kinzani baina yao wenyewe wiki 14 tu baada ya ujauzito, mathalani pacha mmoja anaweza kuwa na alama fulani ya kuzaiwa upande wa kushoto ilihali mwingine ikawa upande wa kulia ama mmoja akawa mashoto na mwingine akawa malia japo mashoto wana weledi mkubwa sana wa kufaragua kuliko malia. Utafiti unaonesha kwamba baada ya wiki 28 mapacha huanza hata kushikanashikana (sio ngumi) wangali tumboni.

5. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah kati ya mwaka ya 1800 hadi 1970 umeonesha kwamba watoto mapacha hurefusha maisha ya mama zao, yaani mama mwenye watoto mapacha ana uwezekano wa kuishi miaka mingi sana kuliko asiye na mapacha

6. Mapacha huanza kufumbatana na kufungama wiki 14 tu baada ya mimba kutungwa. Mwaka 2008 wanandoa maharimu huko Uingereza, walijigundua kwamba walizaliwa mapacha kwani mara tu baada ya kuzaliwa walitenganishwa na kwenda kulelewa na wazazi tofauti (adopted) kabla ya kuona wenyewe kwa wenyewe, dhahiri shari ilibidi ndoa ya ibatilishwe (annulled) na mahakama.
7. Unadhani mapacha wawili wa kiume (identical male twins) wakioa mapacha wawili wa kike (identical female twins), watoto wao watakuaje kisheria?.....Hao ni ndugu wa damu

8. Mama ambaye amewahi kuwa na jumla ya watoto 69 kwa uzao wa tumbo lake, akiwa na umi wa miaka 40 tu tayari alikua na mapacha 16!!!. Mama huyu amefariki mwaka 2010 akiwa na miaka 93!!!

9. Kila mtu duniani ana kinasaba chake (DNA) ingawa ni tofauti kwa mapacha wa kulandana (Identical twins) kwani DNA ziko sawa bin sawia . Hata hivyo hutofautiana alama za vidole (finger print) ambazo ingawa hulandana wakati wakiwa kwenye kijusi (embryos) , alama hizo huachana baada tu ya kijusi kutengana

10. Jimbo la Massachusetts nchini Marekani ndilo linaloongoza kwa kuwa na mapacha wengi duniani, idadi ya mapacha huko ni 20% ilihali Nigeria ikiongoza kwa mapacha wa kulandana (ingawa Nigeria inaongoza kwa mengi pia ikiwamo 'usanii')

11. Uwezekano wa wanaume mapacha kuzaa watoto mapacha utategemea na uwezo wa mwanamke ikiwa anaweza kuzalisha mayai mawili kwa mkupuo

12. 22% ya Mapacha ni mashoto ukilinganisha na 10% ya wasio mapacha duniani, ipo nadharia 'mizania' kwamba mazoea haya huanzia tumboni kutegemea na ......
13 Hii nimeipenda ya Viongozi wakuu wa nchi waliokua mapacha nchini Poland, Marehemu Lech Kaczynski (1949-2010) alikua pacha wa kulandana na Jaroslaw Kaczynski na wote wakichapa siasa. Wakati Lech alikua Rais wa Poland tangu 2005 hadi 2010, Jaroslaw yeye alikua Wazii Mkuu wa Poland kutoka mwaka 2006 hadi 2007. 

Yasemekana George W. Bush ndiye amewahi kuwa Raisi pekee duniani kuwa na mapacha.

KIPINDI CHA "SAFARI YA DODOMA" KESHO TAREHE 17 AUGUST 2016 SAA 3:00 USIKU TBC1

$
0
0

Katika kufanikisha agizo la mhe. Rais John Magufuli, na kutekeleza maamuzi ya kuhamishia makao makuu ya serikali dodoma, tbc imeamua kuandaa kipindi maalum ili kuwafahamisha wananchi juu ya uamuzi huo, faida zake na pia nini kifanyike au nini kimefanyika mpaka sasa. Kipindi hiki kinaitwa “SAFARI YA DODOMA” ambacho kinarushwa kila siku ya jumatano saa 3:00 usiku, TBC1.
Kipindi hiki cha muda wa saa moja, kinawakaribisha wadau mbalimbali toka serikalini, mashirika na jamii kupata fursa kuja kuelezea umuhimu na jinsi ambavyo wamejiandaa kuhamia Dodoma, pia ni fursa gani zilizopo Dodoma, zikiwemo jitihada za wafanyabiashara na wawekezaji kutumia nafasi hii kuelezea namna ambavyo wanaweza kustawisha makao makuu ya nchi, Dodoma.
Kipindi cha kwanza kilichorushwa jumatano iliyopita ya tarehe 10 agosti 2016, tulikuwa na mhe. Cleopa Msuya, waziri mkuu mstaafu. Ambaye alitueleza hali ilivyokuwa wakati huo ameteuliwa kuwa waziri mkuu, na jinsi ambavyo maamuzi ya kuhamia Dodoma yalitekelezwa.
Katika kipindi cha jumatano tarehe 17 Agosti 2016, saa 3:00 usiku, kwenye studio za TBC1 tutakuwa na mgeni, mhe. Jenister Mhagama, waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu.

Pia tutakuwa na nafasi ya kuwasikiliza wadau mbalimbali wakitoa maoni yao kuhusiana na maamuzi haya, pia tutakaribisha simu ili kujibu maswali mbalimbali yatakayotolewa kwenye kipindi, ambapo mshindi atajipatia zawadi toka chuo kikuu cha Dodoma (udom).

Nakukaribisha kutazama kipindi hiki, Jumatano saa 3 usiku, TBC1
Kwa maoni tutumie barua pepe: maonidodoma@tbc.go.tz

Pia jiunge nasi katika mitandao ya kijamii:
SMS: Andika dodoma, acha nafasi, Ujumbe wako, tuma kwenda 15559
WhatsApp: 0678 279 107
Facebook: tbconetanzania
Twitter: tbconetanzania
Instagram: tbconetanzania
Youtube: TBC1

Obituary - Nargis Bhimji

CBE, TFDA NA AFRICAN RELIEF ORGANISATION WAMKABIDHI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA SHILINGI MILIONI 31.7 ZA MADAWATI

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dk. Emmanuel Munishi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kushoto) Mfano wa hundi ya shilingi milioni 8,000,000/= zilizotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kama mchango wa chuo hicho kwa jamii kwa ajili ya kununulia madawati yatakayotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi katika mkoa huo.Katikati ni Afisa Uhusiano wa Jamii wa Chuo hicho Leonidas Tibanga.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dk. Emmanuel Munishi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi mchango wa wa madawati wa shilingi milioni 8 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) leo jijini Dar es salaam. Mchango huo umetolewa na chuo hicho kununulia madawati yatakayotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo, Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Jamii wa Chuo hicho Leonidas Tibanga.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 17,700,000/= Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kushoto) kama mchango wa madawati kwa wanafunzi wa shule za Msingi jijini Dar es salaam leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kushoto) akiangalia mfano wa hundi ya shilingi milioni 6 zilizotolewa na Taasisi ya Kijamii inayojihusisha na masuala ya Kijamii ya African Relief Organisation ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kununulia madawati. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Shekh Abdallah Ndauga na Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo Moadh Shannawi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupokea msaada wa Fedha kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Taasisi ya Kidini ya Masuala ya Kijamii ya African Relief Organisation kwa ajili ya kununulia madawati kwa shule za Msingi za Dar es salaam. Picha/Aron 


Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mbalimbali jijini Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uchangiaji wa hiari wa madawati kwa shule za msingi linaoendelea jijini humo ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia yatakayozalisha  wanafunzi bora wa shule za msingi.
Akizungumza mara baada ya kupokea mchango wa fedha za kununulia madawati kiasi cha shilingi milioni 31.7 kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Taasisi ya kidini ya masuala ya jaamii ya African Relief Organisation leo jijini Dar es salaam Mhe. Makonda amesema kuwa bado jamii inao wajibu  na jukumu la kuhakikisha kuwa mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule za msingi yanakuwa bora ili kuzalisha wahitimu walio na msingi imara.
“Napenda kutumia fursa hii kuzishukuru taasisi hizi ambazo zimeitikia wito wa kutoa michango yao ili kuwezesha upatikananji wa madawati, nawashukuru sana viongozi wa taasisi hizi kwa kuitikia wito wa mkoa wetu na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha shule zetu zina madawati na hakuna mwanafunzi anayekaa chini” Amesisitiza Makonda.
Ametoa wito kwa wananchi ambao wanaguswa kwa namna moja au nyingine  kuendelea kutoa michango yao ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za Msingi katika jiji la Dar es salaam ambao walikuwa wanapata shida ya kusomea katika mazingira magumu.
Ameongeza kuwa ili taifa liweze kuwa na wataalam wazuri katika Nyanja zote lazima msingi wa elimu katika shule za msingi uwe mzuri na kufafanua kuwa ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkoa wa Dar es salaam ni kukamilisha upatikanaji wa madawati na majengo ya madarasa.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Emmanuel Munishi akizungumza mara baada ya kukabidhi mfsno wa hundi ya shilingi milioni 8 kama mchano wa chuo hicho kwa jamii amesema kuwa wao kama Chuo cha Elimu ya Biashara chenye kampasi mikoa minne ya Tanzania ukiwemo Mwanza, Dar es salaam, Dodoma na Mbeya kimeguswa kuchangia kiasi hicho cha fedha kwa kuwa kinawategemea wanafunzi waliofundishwa vizuri kutoka shule za Msingi.
Amesema wameamua kuunga mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kuhakikisha kuwa shule Zote za Dar es salaam zinaondokana na shida ya madawati.
“Sisi tumeguswa na uchangiaji wa madawati kwa kuwa ni taasisi ya ya elimu ya juu, kama taasisi ya elimu ya juu hatuwezi kupata wanafunzi wetu kama hakuna shule za msingi, tumeamua tusiwe watu wa kuvuna tu tukaamua kwenda moja kwa moja kwenye msingi ili kujenga msingi imara wa shule zetu” Amesisitiza.
Ameziomba taasisi zote za Elimu ya juu nchini kuiga mfano wa CBE katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini ya Masuala ya Kijamii ya African Relief Organization ya jijini Dar es salaam Shekh Abdallah Ndauga iliyochangia shilingi milioni 6 amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa moyo wake wa kuendelea kuwahamasisha wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuchangia madawati.
Amsesema Taasisi ya African Relief Organisation itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na mkoa wa Dar es salaam katika kuleta maendeleo ya wananchi wake kupitia miradi mbalimbali wanayotekeleza ikiwemo uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na Mamlaka hiyo wa shilingi milioni 17.7 amesema TFDA inaunga mkono jitihada za Rais, Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha kuwa kila mtoto anakaa katika dawati ambapo katika bajeti yake ya mwaka 2015/16 inatoa mchango wa madawati 236.

Sillo ameongeza kuwa TFDA pamoja na majukumu iliyonayo inatambua kuwa elimu ndiyo nguzo muhimu katika kupambana na maadui wakubwa wa maendeleo, hivyo itaendelea kutoa mchango wake katika kusaidia sekta ya elimu hapa nchini.






SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Baadhi ya wajane na yatima wanaonufaika na msaada wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF, wameiomba serikali kuongeza walengwa wanaoweza kunufaika na mpango huo; https://youtu.be/84qCbA5-R6s
Wakazi wa kijiji cha Kilongo wilayani Muheza mkoani Tanga, wamewataka wananchi wenzao kufanya kazi kwa juhudi kama inavyofanya serikali ya awamu ya tano;https://youtu.be/mlNx929UWos

Mwenyekiti wa chama cha wakulima Said Sudi, amesema wakati umefika wa kuacha kuruhusu wagombea wenye umri wa miaka 70 kugombea urais visiwani Zanzibar;https://youtu.be/OWFTQlcJs5c

Kutana na mlemavu wa miguu anayetumia baiskeli ya matairi mawili kujitafutia riziki yake ya kila siku ili aweze kuhudumia familia yake; https://youtu.be/OOuiz3Lff5g

Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanzisha mfumo wa kuhakiki namba za walipa kodi wake ili kuepusha uwezekano wa mtu kukwepa kodi; https://youtu.be/VOFf9fz8Fmk  

Taasisi ya sekta binasfi imeiomba serikali kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kurahisisha zoezi serikali kuhamia mkoani Dodoma; https://youtu.be/UKYzI7HDbpU

Benki ya mkombozi imezindua mpango wa kutoa mikopo ya bima za afya kwa wajasiliamali ili kuwawezesha kuwa na uhakika wa afya zao;https://youtu.be/jG26byXZh9M

Zaidi ya wanawake 3000 wilayani Kasulu, wameungana na kuunda kikundi ili kujiandaa na milioni 50 alizoahidi mheshimiwa Rais Magufuli kipindi cha kampeni;https://youtu.be/XC93vNiREU8

Mchezo wa ngao ya jamii unaoashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu Tanzania bara, utapigwa hapo kesho ukiwakutanisha Yanga na Azam huku baadhi ya pesa zikitumiwa kununulia madawati; https://youtu.be/T890RGt8CkU

Rais wa zamani wa shirikisho la mpira duniani FIFA Joao Havalange mwenyeji wa Brazil, amefariki dunia hii leo nyumbani kwao Brazil akiwa na umri wa miaka 100;https://youtu.be/gDHc7zYo0p4

Kocha wa Chelsea Antonio Conte ametetea kitendo cha mwamuzi aliyechezesha mchezo wao wa jana dhidi West Ham kutomuonesha kadi nyekundu Diego Costa huku akisema Costa hakumkanyaga mlinzi wa West ham; https://youtu.be/kkphSCmVtUM

KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

"YES" PROGRAM WELCOMES TANZANIAN STUDENTS TO THE U.S.

$
0
0
Dar es Salaam, TANZANIA.  Eighteen Tanzanian Secondary School students from Zanzibar and the mainland have been selected to live and study in the United States for one academic year from August 2016 to June 2017.  The students left Tanzania on August 8, 2016 to begin their experience in the U.S. 
Through the U.S. Department of State's Kennedy-Lugar YES program, foreign secondary school students live with American host families, attend high school and engage in activities to learn about American society.  Students also acquire leadership skills and help Americans to learn more about their country and culture.  
While in the U.S., the students perform two hours of community service each month to get exposed to the benefits of volunteerism and civic engagement, and enhance their ability to contribute to their communities when they return home. 
A total of 800 Tanzanian students with the highest academic achievement in the Form II National Examinations were selected to compete for the YES program, out of which 18 were selected as participants during academic year 2016-2017.  
Of the 18 Tanzanian students, eight are from Zanzibar and 10 are from the mainland.   In Arusha region, students come from Canalland, Ilboru, Akeri, and Ailanga Lutheran Seminary.  From Morogoro region, they come from Kilakala, Mgulani, Kola Hill and Mzumbe secondary schools. Students from Zanzibar were selected from Lumumba, Laureate, High View, Glorious, Filter, Trifonia, Konde and Vikokotoni Secondary Schools. 
The U.S. Department of State’s Bureau of Educational and Cultural Affairs created the Kennedy-Lugar YES program in 2003 to enhance mutual understanding and build bridges between citizens of the U.S. and countries around the world.  The program for Tanzanian students is conducted in partnership with the U.S. Embassy in Dar es Salaam through an American non-profit organization called the Iowa Resource for International Service (IRIS). A total of 183 Tanzanian secondary school students have participated in the YES program since its introduction in Tanzania in 2006.

 
 United States Embassy Dar es Salaam Cultural Affairs Officer Jeffrey Ladenson (1st right - in front) talking with Tanzanian Secondary School students.  Eighteen Tanzanian Secondary School students from Zanzibar and the mainland left Tanzania on August 8, 2016 to live and study in the United States for one academic year from August 2016 to June 2017.
United States Embassy Dar es Salaam Cultural Affairs Officer Jeffrey Ladenson, (standing front row - center) in a group photo with 18 Tanzanian Secondary School students from Zanzibar and the mainland, who left Tanzania on August 8, 2016 to live and study in the United States for one academic year from August 2016 to June 2017. (Photos Courtesy of U.S. Embassy)
For additional information, please see: http://www.yesprograms.org/.

KAMISHNA WA TRA AZINDUA KAMPENI YA KUHAKIKI WA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)

$
0
0
tr1 Kamishna wa TRA Bw. Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TRA jengo la Milenium Makumbusho leo wakati akielezea kampeni ya kuhakiki namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN itakayoendelea mpaka mwezi wa kumi mwaka huu nchini kote. Kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani Bw.Elaijah Mwandumbya. tr2 Kamishna wa TRA Bw. Alphayo Kidata akipata maelezo kutoka kwa Rehema Shayo Meneja wa Usajili TRA wakati akikagua utekelezaji wa uhakiki huo. ................................................................................................. 
  TRA kupitia kwa Kamishina Mkuu wa Ofisi hiyo imezindua zoezi maalumu la  kuhakiki na kuboresha taarifa za usajili wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) . 
  Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo Bw, Alphayo Kidata kwa kushirikiana na wafanyakazi wa ofisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es salaam. Hivyo kuanzia sasa zoezi hilo litakuwa endelevu katika mikoa yote nchini ya bara na visiwani . 
  Kidata alisema kuwa lengo kubwa la uzinduzi wa zoezi hilo ni kubadili mfumo wa sasa wa kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi kwa kuweka mfumo mpya unaoendana na ukuaji wa teknolojia ambao utakuwa na walipa kodi wake wanaostahili kuwepo kwenye wigo. 
  Aidha aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuwaondoa walipa kodi hewa ,kuongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi wa ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu na kuwezesha ulipaji kodi kuwa nafuu kwa mlipaji.
Hata hivyo katika hatua nyingine Kidata ametoa wito kwa yeyote mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi kufika katika ofisi za mamlaka hiyo ili kuweza kupata utaratibu wa zoezi zima jinsi linavyokwenda

Mahojiano na Olympian Hilal Hemed Hilal (Live) kutoka Brazil

$
0
0
Photo Credits: MissiePopular.com
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU (Jumatatu Agosti 15 2016) Mubelwa Bandio alifanya mahojiano ya moja kwa moja na Hilal Hemed Hilal. Nahodha wa Tanzania katika mchezo wa kuogelea kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro nchini Brazil.
Alikuwa mkarimu kujiunga nasi kwa njia ya Skype sambamba na kocha wake Alexander Mwaipasi
Karibu uungane nasi

Rais Magufuli awatembelea na kuwajulia hali Mzee Malecela na Mhe. Ndugai

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Agosti, 2016 amewatembelea na kuwajulia hali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwajulia hali, Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amewaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone na kupata nguvu haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kawaida katika ujenzi wa Taifa.Akizungumza na Rais Magufuli nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemshukuru Rais Magufuli kwa kumtembelea, kumjulia hali na kufuatilia kwa ukaribu wakati wote alipokuwa akipata matibabu nchini India hadi aliporejea hapa nchini.

"Kwa kweli nimefarijika sana, kwanza naomba nimshukuru sana Mhe. Rais kwa sababu nilipopata matatizo haya ya maradhi alikuwa karibu sana na mimi nikiwa hapa nchini na hata nilipopelekwa nchini India alinipigia simu mara kwa mara na kunifariji sana, na hapa amekuja kuniona kwa niaba ya watanzania kwa kweli namshukuru sana na namuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpa moyo huu wa kuwajulia hali wale wenye matatizo mbalimbali"Lakini niwahakikishie Watanzania, kwamba kwa sasa nina nafuu kubwa sana, naweza kufanya kazi nyingi tu sasa lakini tuendelee kuombeana"Ameeleza Mhe. Ndugai alipokuwa akizungumzia hali yake kwa sasa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela pamoja na kumshukuru Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli kwa kumtembelea amesema afya yake inazidi kuimarika na pia amewashukuru Madaktari wanaompatia matibabu.

"Mheshimiwa Rais nakushukuru sana, namshukuru pia Mama Janeth Magufuli kwa kunitembelea na kunifariji, naendelea vizuri na matibabu na afya yangu imeimarika kwa kiasi kikubwa" Ameeleza Mhe. Malecela.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

16 Agosti, 2016.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Spika Sala sala jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

TEASER JOTO LA ASUBUHI AUGUST 17 JUMATANO

BREAKING NEWZZZZ....KUNDI LA ORIGNAL COMEDY MATATANI KWA KUVAA SARE ZA POLISI KWENYE HARUSI YA MASANJA MKANDAMIZAJI

$
0
0
Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi. 
Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.


 Imetolewa na:

Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)

Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.         

MWANAMUZIKI CHRISTIAN BELLA NDANI YA KIPINDI CHA THE AVENUE

MAGAZETINI LEO JUMATANO AGOSTI 17


Article 2

DC MTATURU AKEMEA SIASA TAKA ZINAZOCHANGIA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI

$
0
0

Na Mathias Canal, Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu ametoa onyo kwa wanasiasa wanaotumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa uchangiaji huduma za afya na badala yake kuwafanya kudumaa kifikra na hatimaye kushindwa kufika hospitalini kupatiwa matibabu hivyo kupelekea vifo vya baadhi ya wananchi ambao wameamini maneno ya kisiasa kuliko kauli za watendaji za kufika Hospitalini kwa ajili ya matibabu.


Ametoa onyo hilo hii leo wakati alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Hospitali teuli ya Makiungu Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida pamoja na Hospitali ya Misheni Cathoric Malkia wa Ulimwengu inayomilikiwa na Shirika la Mothers of the Holy Cross an Missionaries of the Holy Cross.

Mtaturu amesema kuwa serikali inatambua umuhimu na huduma bora zinazotolewa na taasisi za dini katika Wilaya ya Ikungi kwani sekta ya afya ni sehemu muhimu kusukuma maendeleo ya nchi endapo wananchi watakuwa na afya bora itakuwa nguzo yao ya kufanya kazi na kuendana na falsafa ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

Kauli ya watumishi wa umma ambao wanatumia vyeo vyao vibaya ikiwemo kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa Vituo vya afya na Dispensari jambo ambalo linajikita zaidi katika kudhoofisha afya za watanzania waishio katika maeneo ambayo hayana huduma za afya karibu.

Mtaturu amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na hospitali hizo ili kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinatatuliwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba, uwepo wa madaktari bingwa lakini ni muhimu wananchi kuchangia huduma za kijamii hususani sekta ya afya ili kuimarisha afya zao na kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima.

Hospitali ya Makiungu ilianzishwa na Masista Wamisionari wa huduma ya tiba mnamo mwaka 1954 kwa mwaliko wa Baba Askofu Winters aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida wakati ule na ndio ilikuwa Taasisi ya kwanza kutoa huduma za afya katika Mkoa wa Singida.

Pamoja na huduma za tiba katika Hospitali ya Makiungu pia inatoa huduma za kinga kwa vijiji vilivyo karibu na hospitali katika vituo vitano kwa njia ya kiliniki tembezi walengwa wakuu wakiwa ni wajawazito na watoto wenye umri chini ya Miaka mitano.

Dc Mtaturu amesema kuwa katika Wilaya ya Ikungi kuna jumla ya Zahanati 34 katika Vijiji 34 pekee kati ya Vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo kinyume kabisa na sera ya Taifa inavyoelekeza ya kuwa na Zahanati kwa kila Kijiji ili kupunguza kadhia wanazokumbana nazo madaktari bingwa kwa kuwahudumia wagonjwa wenye mafua badala ya magonjwa sugu na makubwa.

Amesema kuwa uchache na kusuasua kwa ujenzi na upatikanaji wa huduma za afya umechagizwa na kauli za kisiasa za kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo jambo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya Vijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu inahudumia wagonjwa wa ndani ya Wilaya ya Ikungi na Wilaya nyingine za Mkoa wa Singida na hata nje ya Mkoa wa Singida kama Shinyanga, Manyara, Tanga, Dodoma, Mwanza, Arusha na hata nchi jirani kama vile Kenya na Malawi.

"Changamoto zote mlizo nazo tumezichukua na serikali itazifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuinua huduma za afya na kuokoa vifo vya wananchi kisa matamko ya kisiasa, Lakini pia nataka niwakumbushe kuwa siasa zilishamalizika Tarehe 25 mwezi Octoba mwaka jana baada ya wananchi kufanya maamuzi yao kwenye uchaguzi Mkuu hivyo huu ni muda wa kufanya kazi kama ambavyo tumekuwa tukimsikia Rais akisema, Kwahiyo kuanzia leo sitaki siasa taka zenye kurudisha nyuma shughuli za maendeleo" Alisema Mtaturu

Aidha Dc Mtaturu amewapongeza watumishi wote katika Hospitali hizo mbili kwa jinsi ambavyo wanawahudumia wananchi kwa moyo mkunjufu pamoja na uchache wa vifaa tiba pamoja na uchache wa madaktari na Wauguzi lakini ameziomba Hospitali hizo kupunguza gharama za Dawa kwani kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya gharama kubwa zinazotakiwa baada ya matibabu sawia na kuwataka watumishi wote kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa ili wagonjwa hao kupata tiba kwa amani na upendo.
Baadhi ya wagonjwa wakiwa katika hali ya ahueni mara baada ya kulazwa katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyopo katika Kijiji cha Puma
Dc Mtaturu Mtaturu akiwasisitiza watumishi wa Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili wawe mabalozi katika kuwashawishi wananchi nao kujiunga katika mfuko huo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na watumishi ngazi ya juu katika Hospitali ya teule ya Makiungu pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
Dc Mtaturu akisisitiza jambo kuhusu utoaji bora wa huduma za afya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasalimu baadhi ya wagonjwa ambao wamefikakupatiwa tiba hospitalini.


KUTOKA MAKTABA: ANKAL ALIPOHOJIWA NA SPORAH NJAU WA SPORAH SHOW JIJINI LONDON MWAKA 2010

$
0
0

Usikose kesho kutoka maktaba Ankal akimhoji Sporah Njau alikoanzia kabla ya show yake kuwa moja ya show baabkubwa kutoka Afrika

Blue Star mabingwa Kinondoni Airtel Rising Stars

$
0
0
Timu ya wavulana ya Blue Star jana wametangazwa mabingwa wa vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuwafunga timu ya Makongo Sekondari 2-0 kwenye mchezo uliokuwa wakuvutia uliochezwa jana kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
Kwenye mchezo huo ambao ulivuta umati mkubwa wa mashabiki, ulitanguliwa na mchezo wa fainali wa wasichana kati ya Mburahati Queens na Upendo Queens ambapo Mburahati Queens waliibuka na ushindi wa 1-0, huku Fatuma Idd akiifungia timu yake bao pekee kwenye dakika ya 46 ya mchezo.
Kwenye mechi ya wavulana ambayo Makongo walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda lakini walijikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya Blue Stars ambayo washambuliaji wake walikuwa wakilishambulia lango la wapinzani wao mfululizo.
Timu ya Blue Star walijipatia bao lakuongoza dakika ya 20 kupitia kwa Shabani Mangula kwa mpira wa kichwa, akimalizia kazi nzuri iliyoanzia upande wa kulia. Baada ya bao hilo, Makongo waliongeza mashambulizi kutafuta goli la kuzawazisha, lakini juhudi zao zilikuwa zikiishia kwa mabeki wa Blue Stars ambao walicheza kwa umakini mkubwa muda wote wa mchezo.
Hadi kipindi kwa kwanza kinamalizika, Blue Star walikuwa mbele kwa bao moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana huku Makongo wakitafuta goli la kusawazisha lakini walijikuta kwenye hali ngumu zaidi baada ya mshambuliaji wa Blue Star Ally Hamisi Ally kuifungia timu yake goli la pili dakika ya 47
Goli hilo liliamsha nderemo kutoka kwa mashabiki wa Blue Star ambao walikuwa wamejitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.
Wakati Mkoa wa kisoka wa Kinondoni wakifikia tamati ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016, mechi zingine za michuano hiyo zilikuwa zikiendelea katika mikoa ya Mbeya, Temeke, Mwanza na Zanzibar jana. Timu ya Mbagala ya Temeke walizindisha ndoto za kushinda taji kwa mkoa huo baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Twalipo kwenye uwanja wa Tandika Mabatini.
Mkoani Mwanza, Timu ya Hamasa FC waliwafunga Nyamangana United 2-1 kwenye nusu fainali ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa DIT.
Mechi za mkoa zitafuatiwa na fainali za taifa za michuano ya Airtel Rising Stars ambazo zitafanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam Septemba 6 mpaka 11.
 Mchezaji Israel Luvamba wa timu ya Blue Star na Salum Mkana wa Makongo Sekondari wakigombania mpira wakati wa fainali za Airtel Rising Stars mkoa wa Kinondoni. Blue Star walishinda 2-0.

 Nahodha wa timu ya wasichana ya Mburahati Queens Shehati Juma akipokea kombe kutoka kwa Diwani wa Kata ya Vikumbulu Siri Gongo baada kuwafunga Upendo Queens 1-0 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Kinondoni. Mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Tanganyika Packers.

Timu ya Mburahati Queens wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe kuwa washindi wa michuano ya Airtel Rising Stars (wanawake). Mburahati waliwafunga Upendo Queens 1-0 kwenye uwanja wa Tanganyika Packers, Dar es Salaam.

Nahodha wa timu ya Blue Star Ally Hamisi Ally akipokea kombe kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam Stephania Kabumba kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam jana. Blue Star walishinda 2-0 dhidi ya Makongo Sekondari.

Article 23

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images