Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi waliokuwa nje ya nchi wala kiapo cha maadili ya Viongozi wa Umma

$
0
0

 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Kiongozi,Charles Mwankupili akizingumza jambo wakati wa hafla ya kula kiapo cha Maadili kwa  Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Modestus Gasper Lyimo na Juma Yussuf Ali (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Mwakilishi wa IGP, Kamishina wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani Mssazya.
 Manaibu Kamishina Modestus Gasper Lyimo (kushoto) na Juma Yussuf wa Jeshi la Polisi wakila kiapo cha maadili ya viongozi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao hawakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.
 Manaibu Kamishina Modestus Gasper Lyimo (kushoto) na Juma Yussuf wa Jeshi la Polisi wakitia saini katika fomu za kiapo cha maadili ya viongozi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.


 Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda(waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi DCP Modestus Gasper Lyimo na DCP Juma Yussuf Ali walioapishwa leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda(waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi DCP Modestus Gasper Lyimo na DCP Juma Yussuf Ali walioapishwa leo Jijini Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Sekretaieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Picha zote na Frank Shija, MAELEZO

Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva amtembelea Spika Wa Bunge Job Ndungai Kumjulia hali

$
0
0
By Christina Njovu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai nyumbani kwake  Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.
Akiwa nyumbani  kwa  spika Jaji Lubuva pia amemkabishi  Mh. Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani  ya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao. 
Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai ameipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane katika kutoa elimu kwa wananchi.
Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi  cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu  na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika. 

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva  (kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhi  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.

JWTZ BINGWA WA MPIRA WA PETE MICHUANO YA MAJESHI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na Selemani Semunyu JWTZ
Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwa Mpira wa Pete wametangaza ubingwa wa michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki kwa mchezo huo yanayoendelea katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.,
Tanzani]a ilifikia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Kenya  39-33 katika Mchezo uliokuwa vuta nikuvute ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Timu hiyo kushinda na hivyo kupata alama ambazo haziwezi kufikia na Timu yeyote.
Katika Mchezo huo Tanzania ilianza vyema tangu Robo ya Kwanza ambapo ilitoka 17-13 wakati robo ya pili 20-16 huku robo ya Tatu wakitoka 31 kwa 24 na mwisho Tanzania kuibuka Washindi.
Nahodha wa Tanzania Dorita Mbunda alisema wanafuraha kwa kurejesha ubingwa walioupoteza mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda.
Nahodha wa Uganda Carlo Alepo alisema walikuwa na wachezaji wachanga amabao ni wageni katika mashindano hivyo wanajiandaa kwa michuano ijayo kwani wachezaji wao watakuwa na uzoefu Tayari wa Mashindano.
Kikosi cha Tanzania kilichoibuka na Ushindi huo  ambacho kilicheza Mwanzo had Mwisho wa mchezo huo ni  Dorita Mbunda,Faraja Malaki,Joyce Kaira,Veronica Patric,Mwanaidi Hassan,Nasra Suleiman Na Lulu Joseph.
Kwa upande wake  MaKocha wa Timu hiyo Grace Mgyabuso na Argentina Kienzevya kwa Nyakati tofauti walisema  ahadi waliyoitoa kwa Watanzania na Mkuu wa majeshi wameitimiza kilichobaki ni kusubiri kukabidhiwa kombe.
Naye Kanali  Mary Hiki wa Tanzania  aliwapongeza wachezaji na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao yaliyowawezesha kuibuka na ushindi huo ambao aliuita ni muhimu kwa Taifa.
Awali Timu ya Tanzania iliifunga Timu ya Rwanda ambayo ni mabingwa wattezi kabla ya Kuwafunga Wenyeji Rwanda kwa matokeo ambayo hayajafikiwa na Timu yeyote katika Michuano hii.
 Mchezaji wa kati wa Timu ya Pete ya Tanzania (C) Faraja Malaki akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilishinda 39-33(Picha Na Dora Mushi) .
 Mchezaji  Mpira wa Mikono wa  Tanzania Bonnerge Kasanga (mwenye Mpira) akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilifungwa 26-15
 Mchezaji wa wa Timu ya Pete ya Tanzania (GA) Nasra Suleiman  akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilishinda 39-33
 Kiongozi wa msafara wa Timu za Tanzania Brigedia Jenerali Jairosi Mwaseba akisalimiana na majeshi kwa Nchi za Aachezaji wa Timu ya mpira wa Kikapu ya Tanzania katika uwanjani  wa Ndani wa Amahoro Kigali Rwanda wakati wa mashindano ya Ahariki kwa majeshi 
 Timu ya Pete ya Tanzania  katika Picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa Mchezo wake  Dhidi ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilishinda 39-33
Picha zote na  Dora Mushi.

Miss Dodoma 2016 Anna Nitwa akumbuka yatima

$
0
0
 Mrembo wa Dodoma 2016 Anna Nitwa akikabidhi sehemu ya msaada aliotoa kwa Bibi Bashura Mussa ambaye anaishi Mtaa wa Muungano Manispaa ya Dodoma. Bashura na wajukuu wake wanaishi kwa kuokota katika jalala la Mbwanga Manispaa ya Dodoma.
Mrembo wa Dodoma 2016 Anna Nitwa akisalimiana na baadhi ya wajane na yatima alipowatembelea katika Mtaa wa Bochela Manispaa ya Dodoma jana. Mrembo huyo alikwenda kukabidhi vyakula kwa wahitaji hao pamoja na vitu mbalimbali.

TANAPA,NGORONGORO NA IDARA YA WANYAMAPORI SASA KWENDA KIJESHI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi 
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa askari na maafisa wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. 






WAKUU WA WILAYA WASTAAFU WAJIUNGA PSPF, RAIS MAGUFULI AWAPONGEZA KWA KUJIPANGA KIMAISHA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya Wastaafu, Ramadhan Maneno, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Jackline Liana, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (katikati), akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Katibu wa Wakuu wa  Wilaya Mstaafu, Betty Mkwasa,  mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Gerald Guninita, mara baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wakuu hao, iliyoandaliwa na PSPF jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2016. Waziri Simbachawene alimwakilisha Rais John Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, George Yambesi.
 Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, viongozi wa PSPF, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na kamati tendaji ya wakuu wa wilaya wastaafu.


DScED admitted candidates for 2016/2017 academic year

MANJI ABWAGA MANYANGA YANGA??

$
0
0

HABARI zilizotufikia zinasema kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji, amejiuzulu wadhifa wake wa kuiongoza Yanga na kuamua kukaa pembeni.

Mbali na kujiuzulu huko pia imeelezwa na chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Klabu hiyo, kuwa Mwenyekiti huyo pia ameamua kusitisha lengo lake la kuimiliki Yanga na Nembo yake ili kuiendesha kibiashara.

''Endapo maamuzi ya Mwenyekiti huyo yatakuwa ni kama zilivyoenea habari katika baadhi ya mitandao basi litakuwa ni pigo kubwa sana kwa wanayanga, waliokwisha jenga imani kubwa kwa Mwenyekiti huyo''. alisema shabiki mmoja wa Yanga. 

Aidha imeelezwa kuwa chanzo cha Manji kujitoa Yanga ni pamoja na figisu figisu za baadhi ya viongozi wa Serikali zinazomshutumu na baadhi ya Wananchama wa Yanga wasio kubari mageuzi anayotaka kuyafanya ndani ya Klabu hiyo, ambao wengi wao wanadaiwa kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara. 
Miongoni mwa watu wanaoweza kuwa kichwani mwa Mwenyekiti huyo hadi sasa pia anaweza kuwepo Katibu wa Baraza la wazee Mzee Akili Mali, aliyesikika katika mahojiano na moja ya kituo  cha Radio akimshutumu Mwenyekiti wake 'eti kuwa amekurupuka' kutaka kuichukua timu yao.

Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake.
Hata hivyo viongozi wa Secretarieti ya Yanga leo wameonekana kuchanganyikiwa huku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka Ofisi za Manji zilizopo Quality plaza.
Huko Klabuni nako hali si hali, Baadhi ya WanaYanga wamefurika nje ya Jengo la Yanga, lililopo kwenye makutano ya Mtaa wa Twiga na Jangwani kutaka kujua hatma ya Kiongozi wao huyo waliemchagua kwa kura nyingi hivi karibuni. Globu ya jamii inaeendelea kufatilia segere hili kwa ukaribu na tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.

WATU WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUGUSHI VYARAKA MBALIMBALI ZA IDARA YA AFYA.

$
0
0

Na  Abel Daud wa Globu 
ya Jamii, KIGOMA
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma kwa kushirikiana na wataalamu kutoka baraza la Famasia linawashikiria watu watano kwa tuhuma za kugushi vyeti mbalimbali vya idara ya afya,ambavyo vinasadikika kutumiwa kufanya kazi katika sekta ya afya.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo hii Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi wa Polisi FERDINAND MTUI,amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambapo amebainisha kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na MGENI NYABUZOKI mzanaki mwenye umri wa miaka 52 ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania mkazi wa mlole ambaye ndiye mmiliki wa stationary inayotumika kutengeneza vyeti hivyo vya kugushi.
Kamanda Mtui ameongeza kuwa wengine walio kamatwa katika tukio hilo ni pamoja na Dikson Mshahilizi (47),ambaye ni muuguzi katika Hospital ya rufaa Maweni,mkazi wa Air pot,Zawadi James  (42) muuguzi katika kituo cha afya Ujiji, mkazi wa Kazegunga Stephano Erasto (18) mkazi wa mlole na mwanafunzi wa shule ya sekondary mlole pamoja na Jonson Nyabuzoki ,ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Mlole na mtaalamu wa kutumia Kompyuta mpakato katika kutengeneza vyeti hivyo.
Kwa upande wake Mratibu wa maduka ya dawa muhimu baraza la Famasi Taifa Domick Mfoi ,amesema kuwa kutokana na huduma inayotolewa na watu ambao hawakupitia mafunzo katika sekta ya afya inapelekea madhara makubwa ya vifo kwa umma,kwani huduma watakayoipata haitaendana na huduma sitahiki kwa mgonjwa.
Ameongeza kuwa katika kudhibiti hali hiyo msako na uchunguzi wa kina utaendelea kufanyika ili kubaini kama kuna watu wengine wanaofanya kazi katika vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.
 RPC Mtui  akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa ofisini kwa RPC Mtui wakipata maelezo kuhusiana na tukio hilo. 
 Baadhi ya vyeti vya kugushi vilivyokamatwa
Mihuri iliyokamatwa katika tukio hilo. 
 Kompyuta mpakato,Laptop,Printer na Scarner pamoja na mihuli  ni vifaa vilivyokamatwa katika Steshanari hiyo

WAZIRI WA ULINZI WA CANADA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JWTZ JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Picha namba 2469 JPG, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia), akimkabidhi zawadi ya Nembo ya JWTZ Waziri wa Ulinzi wa Canada, Mhe. Harjit Singh Sajjan (kushoto) ofisini kwake Makao Makuu Upanga jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi wa Canada Mhe. Harjit Singh Sajjan (kushoto) akifurahia zawadi ya Kinyago alichokabidhiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) alipomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam.

HE Dr Jakaya Kikwete, Chair of the Commonwealth Observer Group to Zambia’s General Elections and Referendum, urges calm and tolerance following the declaration of the results of the Presidential Elections.

$
0
0
Dr Jakaya Kikwete, the Chair of the Commonwealth Observer Group, has congratulated the President-Elect, and commended the Electoral Commission of Zambia for the successful conduct of the recently concluded General Elections and Referendum. 
Zambia's President Edgar Lungu has been re-elected, according to official results.The electoral commission said Mr Lungu had secured 50.35% in Thursday's vote, just over the 50% threshold needed to avoid a second round under a new electoral system.His main rival, Hakainde Hichilema, won 47.67%.
Dr Kikwete has once again praised the people of Zambia for the peaceful manner in which they voted on 11 August.
Immediately after the Chairperson of the Electoral Commission of Zambia, Justice Esau Chulu, announced the final results of the Presidential Election, Dr Kikwete said:
“On 11 August, Zambians voted in dignity to elect their leaders. They continued their country’s cherished and admirable legacy of peaceful elections. The winner must be magnanimous, and those who were unsuccessful must show statesmanship and a commitment to upholding this country’s noble reputation in Africa and beyond.”
He has urged all leaders and citizens of Zambia to respect the will of the people and to channel any grievances and concerns through the prescribed legal channels.
Dr Kikwete continued: 
“As I said in the Group’s interim statement, this is the Zambian Constitutional way.”
The Commonwealth Observer Group have been in Zambia since 4 August and will depart on 18 August. An Advance Team was deployed to Zambia on 22 July.

Mazishi ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi Zanzibar leo

$
0
0


Viongozi wa kitaifa wakishiriki katika sala ya kumwombea Ras wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, marehemu Alhaj Abood Jumbe iliyofanyika kwenye msikiti, Mwembeshauri Zanzibar Agosti 15, 2016. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais, Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein.
Wananchi waliobeba jeneza la mwili wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika Nyumbani kwake Migombani Unguja leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya mapinduzi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika mazishi ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika Nyumbani kwake Migombani Unguja leo mchana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ,nyumbani kwa marehemu Migombani Zanzibar.

BASATA YAMFUNGULIA NAY WA MITEGO, YAMWEKA CHINI YA UANGALIZI

Marufuku kutumia mafuta ya transfoma kukaagia chipsi- Profesa Muhongo.

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa ajili ya kukaangia chips na kutengeneza mikorogo.

Profesa Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa kijiji cha Kirongo wilayani Muheza mkoani Tanga alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa huo.

BLACK WOOD NA BENKI YA ACB WAZINDUA HUDUMA YA MIKOPO YA KUBORESHA MAKAZI JIJINI DAR LEO.

$
0
0





Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla akizungumza na wadau wa benki ya ACB jijini Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa  huduma ya mikopo na kuboresha makazi kati ya Black wood na Benki ya ACB.
Mkurugenzi wa Mipango kampuni ya Black Wood, Zouhra akizungumza na wa wadau wa benki ya ACB na kampuni ya Black Wood jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa kampuni ya Black Wood inakukopesha Viwanja vilivyopimwa na vya bei nafuu kwa watu wote wenye kipato cha chini anaweza kupata kiwanja kilichopimwa na chenye miundombinu yote.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya ACB, Israel Chasosa akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo jijini Dar es Salaam leo kati ya Benki ya ACB na Kampuni ya Black wood katika kununua viwanja vya kuanzia shilingi milioni tatu tu.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya ACB, Israel Chasosa na Mkurugenzi wa Mipango kampuni ya Black Wood, Zouhra wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya ACB na wafanyakazi wa kampuni ya Black Wood jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi wa huduma ya mikopo ya kuboresha Makazi.

WANACHAMA YANGA WAMLILIA MANJI, WATAKA AKILIMALI AFUTWE UANACHAMA.

$
0
0
 Baadhi ya wanachama wa Yanga wakiwa inje ya Jengo la Makao Makuu ya Yanga.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUFUATIA tetesi za Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kutaka kujiengua pamoja na  kubadili msimamo wake wa kuikodi timu hiyo, wanachama wa klabu ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam wamempigia magoti na kumsihi asibadili maamuzi yake.

Wanachama hao wamemuomba Manji kutobadili msimamo wake leo katika kikao cha dharula kilichofanyika leo kwenye Makao Makuu ya timu hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Aidha wanachama hao wameikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuzungumza na vyombo vya habari pasipo kupata ridhaa ya chama.

Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam, Robert Lyungu Kasera ameutaka uongozi wa timu hiyo kuweka mkutano mkuu wa dharula ili kupitisha pendekezo lao la kumvua uanachama katibu wa Baraza la wazee Ibrahim Akilimali kwa madai kuwa kiongozi huyo anashirikiana na timu pinzani kukwamisha mpango wa Manji kuikodi timu.

“Huyu mzee ana mikakati ya  kuiharibu Yanga na hatufahi, haiwezekani aongee masuala ya Yanga pasipo ridhaa ya uongozi wa klabu na viongozi mfikishe taarifa hii kwa usahihi bila kumun'gunya na kikao hiki kinalaani kitendo alichofanya,” amesema Lyunga.

Katika hatua ya kujitetea Mzee Akilimali ameomba radhi na kuwataka wanachama wa Yanga wasifikirie  vibaya kwa kauli aliyoiongea kwani wao kama Baraza la Wazee wanamuhitaji sana Mwenyekiti wao Manji na ameweza kuisaidia timu yao kwa takribani miaka 10. "Labda niseme hivi Kama kukurupuka ni tusi kama nilivyomwambia Yusuf, basi naomba radhi kwake Manji na wanayanga wote”.

Kufuatia hilo Kaimu Katibu Mkuu Yanga amethibitisha kupokea pendekezo hilo ila amesema wao hawana uwezo wa kumfukuza mwanachama hadi mkutano mkuu ufanyike.

VIVUTIO VYA UTALII LUKUKI VYAIBULIWA KATIKA HIFADHI YA MKINGU

$
0
0

Hifadhi asili ya Mkingu ipo wilaya ya Muvemero Mkoani Morogoro. Hifadhi hii ni eneo muhimu sana kiutalii kutokana na upekee wake wa maisha ya viumbe, mimea pamoja na maisha ya binadamu kiujumla.

Hifadhi hii ina ukubwa wa hekta 26, 334 na imezungukwa na vijiji vitano ambavyo vipo ndani ya kata sita na tarafa mbili. Tangu kuanzishwa kwake Hifadhi hii mwaka 2016, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) imekuwa ikihudumia hifadhi hii kutokana na kuwa na mimea na viumbe ambavyo ni vivutio pekee vya Utalii nchini ambavyo havipatikani mahali popote duniani.

Mhifadhi Mkuu wa Mazingira asili ya Mkingu, Bw. Abeid Kindo anasema kutokana na sifa hizo za kipekee zinazopatikana katika Hifadhi hiyo imekuwa na umuhimu wa aina mbili ambao ni umuhimu wa kidunia na umuhimu wa kitaifa, Katika umuhimu wa kidunia upo katika viumbe, mimea na wanyama.

Anasema hifadhi hii ina wanyama wenye uti wa mgongo 392 kati ya hao 32 hawapatikana mahali popote duniani isipokuwa ni Mkingu tu yaani ni endemic species. Aidha , alisema kuna vyura na ndege wanaopatikana katika hifadhi hiyo tu. Bw. Kindo anasema kuwa hifadhi hiyo imejaliwa kuwa na wanyama wanaotambaa 42 kati ya hao 14 hawapatikanimahali popote duniani isipokuwa Mkingu tu pamoja na aina ya ndege 214 kati ya hao ni aina nne ndio wanaopatikana katika hifadhi hiyo. Mbali na hiyo, Anasema kuwa ndani ya hifadhi kuna msitu unaotumika kwa masuala ya mila za Waluguru kuwa eneo hilo ni zuri sana amabalo nalo ni kivutio cha utalii ndani ya msitu huo

Mbali ya kupatikana kwa wanyama na mimea katika Hifadhi hiyo Bw, Kindo anaeleza kuwa kuna pango la Malolo ambalo wenyeji wa Mkindo wana historia kubwa ya pango hilo ambalo wenyeji hawataweza kusahau kwani kuna mwanaume mmoja aliiba mke wa Mtu akaishi naye ndani ya pango hilo kwa muda wa miaka 3 bila kujulikana kijini. Pango hilo lina vyumba mithili ya nyumba iliyojengwa.

Pia anasema kuwa nadni ya hifadhi hiyo kuna pango ambalo ukikaa nje kuna upepo unaotoka ndani unapuliza hiyo ni ishara tosha kuwa humo ndani ndani kuna uhai. Anabainisha kuwa hifadhi hiyo ina jiwe lenye alama za nyayo za binadamu, kwato za mifugo ikiwa hiyo ni ishara tosha kuwa maisha ya kale ya binadamu yalianzia ndani ya hifadhi hiyo. .

Aliongeza kuwa mbali ya mapango ndani ya hifadhi hiyo , kuna maporomoko Lusingizo yenye mita zaidi ya 50 , hadi hivi sasa kuna wawekezaji wamejitokeza ili waweze kuzalisha umeme katika kivuto hicho cha utalii. Pia kuna magofu ya kale ya Wajerumani ambayo waliishi ndani ya hifadhi kabla vita vya pili vya dunia na baada ya kuondoka kwa Wajerumani ilikuwa shule ya msingi ya kijiji cha Mafuta, na baada ya eneo hilo likatangazwa kuwa hifadhi , Shule ile ilitolewa na kujengwa kijijini.

Bw. Kindo anasema licha ya hifadhi hiyo kuwa na vivutio lukuki bado imekuwa ikitembelewa na idadi ya watalii isiyoridhisha licha kwa mwaka jana wameweza kupata watalii 75 kutoka Ujerumani, ‘’Tokea mwaka jana hadi hivi sasa tumeweza kuibua vivutio saba vya utalii na tunaendelea kufanya jitihada za makusudi ili kuhakikisha tunakuwa na vivutio vingi vya utalii ili tuweze kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi ‘’.alisema Bw. Kindo

Aidha,Alisema Hifadhi hiyo ndio chanzo cha mto Wami, mto Ruvu na Mto Mkingu ambapo maji hayo yamekuwa yakitumika katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo,uvuvi,mazalia na makazi ya mimea na wanyama bila kusahau maji hayo ndiyo hutumika kuwanyesha wakazi wa Dare s Salaam na mikoa ya jirani

Amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali wasisubili watafiti kutoka nje ya nchi kwenda kufanya tafiti katika Hifadhi hiyo badala yake wao wawe mstari wa mbele katika kuvumbua vitu vingi ambavyo vinapatikana katika hifadhi hiyo.

Huyu ni aina mojawapo ya chura ambaye hapatikani mahali popote duniani isipokuwa katika Hifadhi ya Mazingira asili ya Mkingu ambaye ni mojawapo ya kivutio cha utalii katika hifadhi hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii)
Baadhi ya sehemu za kuvutia katika Hifadhi ya Mazingira Asili ya Mkingu ambayo ni njia mojawapo inayotumiwa na watalii kwenda kijiji cha Maskati kuangalia vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika Hifadhi hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii).
 Maporomoko Lusingizo yenye mita zaidi ya 50 yaliyoko katika Hifadhi ya Mazingira Asili ya Mkingu ambayo ni mojawapo ya kivutio cha Utalii katika Hifadhi hiyo, Hadi hivi sasa kuna wawekezaji wamejitokeza ili waweze kuzalisha umeme katika kivutio hicho cha utalii. ( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii).

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AAGIZA UTOAJI WA MATIBABU BURE KWA WAGONJWA WA FISTULA NCHINI.

$
0
0
Waziri UmmyMwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Waziri Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali zote za Rufaa nchini  ngazi ya Mikoa, Kanda na Hospitali ya Taifa Muhimbili kutoa Matibabu Bure kwa Wagonjwa wa Fistula.

Waziri Ummy aliyasema hayo mjini Tanga kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Bombo katika uzinduzi wa kambi ya matibabu ya Wagonjwa wa Fistula itakayodumu kwa kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 15 hadi 19 agosti,2016

Alisema  tatizo la Fistula limekuwa likiongezeka kila siku na waathirika wengi ni akina mama wa vijijini na wale wa  kipato cha chini ambao wanashindwa kupata huduma sahihi za afya ikiwemo kuchelewa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa kujifungua.

Takribani kina mama 2500 hadi 3000 hupata tatizo la ugonjwa  wa Fistula kila mwaka japo idadi hii ni ndogo sana kuliko hali halisi ilivyo kwa kuwa wagonjwa wengi hunyanyapaliwa na familia zao na jamii kwa ujumla.

"Serikali ya Awamu ya Tano imejikita zaidi katika kuwahudumia Wanyonge, kwa mamlaka niliyopewa natoa msamaha wa kulipia matibabu ya Fistula ili kuwapunguzia mateso wanawake hawa"."Kwa kuwa wenye tatizo la Fistula ni wanawake wa kipato cha chini na wa vijijini naziagiza Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na Kanda kutoa Matibabu ya Fistula Bure kwa Wagonjwa watakaofika kutaka Huduma hizo."

Waziri Ummy alisema ili kuhakikisha huduma hizo zinatolewa ameziaagiza hospitali hizo kuandaa Kambi za Matibabu ya Fistula angalau mara moja kila mwaka na apatiwe Taarifa.

Aidha ,ameeleza kuwa kina mama wengi wenye tatizo la Fistula wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli za uchumi kama biashara ndogo ndogo kwa kuwa ugonjwa huu ni wa aibu ambao hupelekea watu kunyanyapaliwa na jamii.

Akieleza hatua mbalimbali  zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana tatizo la ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma za ujauzito na uzazi, mafunzo ya huduma za dharura za uzazi kwa watoa huduma za afya pamoja na usimamizi shirikishi, uimarishaji wa ubora wa huduma za ujauzito na uzazi,kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya ujauzito na uzazi,kuimarisha mifumo ya rufaa na kuhakikisha huduma za dharura za uzazi zinapatikana hasa maeneo ya vijijini na wataalam waliobobea katika maeneo hayo.

"Utaratibu huu wa kushirikiana na wadau na marafiki zetu ni Mzuri, kwani unasaidia kuongeza ujuzi kwa wataalam wakiwa katika maeneo yao ya kazi. Pia,amewaomba wadau hao kuongeza wigo wa ushirikiano katika eneo la Afya ya Uzazi  ikiwemo matibabu ya Saratani ya Shingo ya Kizazi"alisema Waziri Ummy.

Kuhusu uhaba wa watumishi katika hospitali hiyo ya Rufaa,Waziri Ummy  ameahidi kupanga watumishi  wanaohitajika katika Hospitali za Rufaa za Mikoa pindi kibali cha ajira kitakapotoka,Vile vile  kutoa kipaumbele cha ufadhili wa masomo ya juu kwa madaktari watakaoomba kuchukuwa masomo yatakayowawezesha kubobea kwenye magonjwa ya akina mama na watoto.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Asha Mahita,alieleza kuwa hospitali ya Bombo ina changamoto ya kuwa na miundombinu chakavu, uhaba wa vifaa tiba na  watumishi kiasi ambacho wanashindwa kutoa huduma ya kutibu akina mama wenye tatizo la Fistula kwa kuwa hawana wataalam waliobobea katika maeneo hayo.

Naye Mwenyekiti wa The Sunshine Muslim Volunteers (SMV) Tanzania Dkt Juma Mwimbe alisema wameguswa na tatizo la fistula kwa kuwa linawakumba wanawake maskini na wa hali ya chini. Hivyo wataendelea kujitolea kwa kufanya kambi kama hizi kadri watakavyoweza ili waweze kuwafikia kina mama wengi zaidi hasa wa vijijini.

Kambi hii ya wiki moja inatarajia kuhudumia kina mama wapatao 100 kutoka Mikoa wa Tanga na Manyara ambapo wameweza kupatikana madaktari bingwa 7 kutoka nchi za Afrika Kusini, Pakistani, Australia na Uingereza.

KHADIJA KOPA ALIVYONOGESHA HAFLA YA UZINDUZI WA BIDHAA MPYA YA NYWELE ZA KINA DADA JIJINI DAR

$
0
0


Malkia wa Mipansho na Mwanamuziki Mkongwe wa Taarab, Bi. Khadija Kopa akizikonga nyoyo za mashabiki wake waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya Mafuta ya nywele aina ya Aliyana ya Kampuni ya Darling Group, iliyofanyika jana kwenye Kiota cha Akemi, Jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi akizungumza kwa niaba ya Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya Mafuta ya nywele aina ya Aliyana ya Kampuni ya Darling Group, iliyofanyika jana kwenye Kiota cha Akemi, Jijini Dar es salaam.

Wawakilishi Kampuni ya Darling wakingumza kuhusiana na bidhaa yao hiyo mpya.
Muigizaji wa filamu nchini, Jackieline Wolper akiwa sambamba na Mwanamitindo, Martin Kadinda pamoja na Mdau wakiyasakata magoma katika hafla hiyo, iliyofanyika jana kwenye Kiota cha Akemi, Jijini Dar es salaam.

MBUNGE ULEGA ASHIRIKI KUHAMASISHA WANANCHI KUFYATUA MATOFALI KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ameshiriki na kuhamasisha wananchi wa Kijjji cha kikundi ,kata ya mkamba kufyatua matofali Kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho. 

Akiwa katika eneo la tukio alishirikiana kikamilifu na vijana ,wazee ,na akina mama waliojitokeza Kwa wingi Kwa ajili ya kujitolea,akizungumza katika eneo hilo akiwa sambamba na Diwani wa Kata hiyo Hassan Dunda, mbunge Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa ameshiriki shughuli hiyo ikiwa sehemu ya majukumu yake na ahadi alizotoa Kwa watu wake na kwamba maendeleo ya kijiji cha kikundi na Mkuranga Kwa ujumla yataletwa na wao wenyewe.

Alisema kuwa katika kipindi chake chote cha ubunge atahakikisha anafanya mambo makubwa Kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo huku akidai kuwa Mkuranga imechelewa sana lazima wakimbie mbio. Kwa upande wa Wazee wa kijjji hicho wamesema kuwa Ulega ameonesha nia ya dhati mno katika uongozi wake na wanaimani naye sana kwamba atafanya mambo mengi makubwa.

Akizungumza kwa niaba ya Wazee wezake Idrisa Pelete amesema kuwa kuna wabunge wengi wamepita na hawakuweza kufanya lolote lakini Kwa sasa wanaamini wamepata kiongozi wa kweli na hicho ndicho walikuwa wanakihitaji.Pia Kijana aliyejitambulisha kuwa ni shaweji Mohammed akitoa neno la shukrani Kwa mbunge alisema kuwa pamoja na kwamba yeye ni mpinzani lakini kwa kazi kubwa alionesha Mbunge kwakweli wanampenda mno.
 Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akishiriki kufyatua tofari za  ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kikundi kilichopo kata ya Mkamba wilayani Mkuranga,mbali na kushiriki huko pia alichangia viloba vya unga wa sembe,maharagwe,maji ya kunywa kutokana na vijana wa kijiji hicho kuweka kambi ya kufyatua matofali hay oleo mkoani Mpwni.
 Wazee wa kijiji cha Kikundi ,kilichopo kata ya Mkamba wilayani mkuranga  wakiteta jambo na mbunge wa jimbo hilo Abdallah ulega, ambapo pamoja na mambo mengine walimpongeza mbunge huyo kwa kuonesha moyo wa kuitumikia wilaya hiyo nakudai katika wabunge saba waliotangulia haijawahi kutokea katika kile anachofanya Ulega ikiwamo kufanya ziara za vijiji kwa lengo lakuwashukuru.
Vijana wa kijiji cha kikundi ,kata ya mkamba wakiwajibika katika kufyatua matofali ya ujenzi wa Zahanati kijijini hapo ambapo kwa muda mrefu imekuwa kero kubwa hali inayowafanya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika kijiji cha kizapala wilayani humo.
(Pichs na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images