Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1320 | 1321 | (Page 1322) | 1323 | 1324 | .... | 3284 | newer

  0 0

  DSC_5540
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani
  DSC_5565
  Zoezi la kuwafariji Wamama Wajane likiendelea
  DSC_5568
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane
  DSC_5580
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane
  DSC_5598
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa nyuma ni baadhi ya Akina mama Wajane waliofarijiwa wakati wa kongamano hilo.

  0 0

  Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Pili wa Zanzibar Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi na Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM kilichotokea leo jijini Dar es Salaam. 
  Rais Mstaafu amemuelezea Mzee Aboud Jumbe kama kiongozi mwenye mchango mkubwa katika maendeleo na ustawi wa Zanzibar na mwenye mchango mkubwa katika uhai wa Muungano wetu. Amesema, “Historia ya Chama cha Mapinduzi na ile ya Muungano wetu haziwezi kukamilika bila kumtaja Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi”. 
  Rais Mstaafu amewatumia salamu za rambirambi Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa msiba huu mkubwa katika taifa letu.  Amesema: 
   “Naungana nanyi na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuomboleza msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Mwenyezi Mungu na awape familia ya Marehemu moyo wa subra na uvumilivu. Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajuun.”

  Imetolewa na:


  Ofisi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne


  Dar es Salaam, 14 Agosti, 2016


  0 0

  Makundi mawili makubwa ya kihalifu mtandao yanayo andika program hasidi “Malware” zenye mlengo ya kudhuru mabenki yametangaza kuungana ambapo imezungumzwa kuwa huwenda ndio sababu kuu ya kumepelekea takwimu mpya za mashambulizi dhidi ya taasisi za kifedha kwa Mwezi (4, 2016 – 6, 2016) kuongezeka kwa Asilimia 16 (16%)  kulinganisha na takwimu za Mwezi (1, 2016 – 4, 2016) .

  Makundi haya mawili ambayo ni waandishi wa “Nymaim Trojan” pamoja na “Gozi Trojan” katika hatua yao ya kuunganisha nguvu yanatabiriwa kuongeza tishio kubwa la matukio ya wizi wa fedha katika taasisi za fedha duniani kote – Na inatabiriwa makundi mengine yakielekea kufata njia hii ya kuunganisha nguvu ili kuongeza kasi ya kudhuru na kuiba fedha katika Taasisi za fedha. Kusoma zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  SIKU kadhaa baada ya Serikali kukishinda Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Chadema), katika shauri na. 52/2016 kuhusu uhalali wa tamko la Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara, undani wa kesi hiyo umebainika.
  Kwa mujibu wa hukumu iliyopatikana mwishoni mwa wiki, kufuatia kesi ya kuomba mapitio iliyowasilishwa Mahakama Kuu ya Tanzania na Wadhamini wa Chadema, mawakili wa chama hicho cha upinzani wakiongozwa na Peter Kibatala wameshindwa kesi hiyo kwa hoja kubwa mbili za kisheria, uchambuzi wa kina wa hukumu unaonesha.
  Katika kesi hiyo upande wa mawakili wa Serikali ukiongozwa na Mawakili wa Serikali, Bw. Haruni Matagane,, Daniel Nyakeha na Bi Lilian Machange ndio uliokuwa mwiba kwa Kibatala.
  Akiongoza jopo la mawakili wenzake wa Serikali, Wakili Matagane waliwasilisha hoja kuu mbili Mahakamani kupinga ombi la Chadema kutaka Mahakama ipitie upya na kufuta amri ya Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano yasiyo na kibali.
  Akitoa hoja ya kwanza kupinga ombi hilo, Wakili Matagane, alijenga hoja kuwa ombi la Chadema limewasilishwa kwa namna ambayo imeshindwa kutumia  njia sahihi za  kupinga amri hiyo  kama zilivyoainishwa kwa mujibu wa kifungu cha 43(6)  cha Sheria ya Jeshi la Polisi (The Police Force and Auxilliary Services Act).
  Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Sheria ya Jeshi la Polisi inaanisha wazi kuwa kabla ya kupinga amri ya polisi ya kuzuia mikutano au maandamano ni lazima kwanza mhusika awasilishe rufaa yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani suala ambalo mawakili wa Chadema hawakuwa wamelifanya
  Katika hoja ya pili mawakili wa Serikali pia walitumia kanuni ziitwazo “The Law Reform (Fatal Accidents and Miscellaneous Provisions (Judicial Review Procedures and Fees) Rules, 2014” zinazoainisha kuwa ombi la mapitio lazima liwasilishwe likiwa na kiapo kinachojulikana kisheria kama “statement.”
  Mawakili wa Chadema waliwasilisha kiapo hicho lakini kikiwa batili kufuatia kusainiwa au kikionekana kuwa ni kiapo kilichowasilishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) badala ya Wadhamini wa Chadema waliofungua kesi hiyo.
  Juhudi za Wakili Kibatala kujibu hoja hizo hazikufua dafu baada ya Jaji Kiongozi, Fernandi Wambali aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, kukubaliana na mawakili wa Serikali kuwa katika kufikisha ombi hilo Mahakamani, Chadema hawakutumia njia ya kwanza iliyoelekezwa na sheria ya kukata rufaa kwa Waziri na pili waliwasilisha kiapo batili.
  Kutokana na Mahakama kukubaliana na hoja za Serikali, Chadema pia kimepata pigo jingine ambapo watalazimika kulipa gharama zote za kesi hiyo ikiwa ni fidia kwa Serikali.
  Jeshi la Polisi lilipiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa Julai 7 mwaka huu kupitia taarifa yake iliyotolewa na Kamishna wa Polisi, Operesheni na Mafunzo, Nsato Massanzya ambapo alieleza kuwa Jeshi hilo limechukua hatua hiyo ili kuimarisha usalama wa nchi.

  Kwa uamuzi huo wa Mahakama, amri hiyo ya Polisi inabaki pale pale ikimaanisha kuwa maandamano ambayo Chadema imekuwa ikiyatangaza kuyafanya yanabaki kuwa batili na kwamba vyama vya siasa sasa vitaendelea tu kufanya mikutano yao baada ya kutumia taratibu za kawaida za kuomba kwanza kibali polisi.

  0 0

  Azam Media Ltd wakishirikiana na TDE (The family of Toussaint Duches Entartainment) kutoka nchini Marekani wakiungana na vipaji vya wasanii maarufu wa sanaa ya Uigizaji Tanzania Jumapili usiku wamekonga nyoyo za mashabiki wa sanaa za maonesho jukwaani kwa onesho kali la “Souper Soul Sunday” na Igizo maalum la “Mrs Lucy Goes to Africa” kwa mtindo wa Broadway, ikishirikisha wasanii maarufu kutoka Tanzania wakiwemo “Natasha” na “Monalisa” katika ukumbi wa Jumba la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam. 
   Souper Soul Sunday ni maonyesho makubwa ya mchezo wa kuigiza ambayo imechukua sehemu kubwa ya kumbi za maonyesho na kujizolea umaarufu mkubwa Marekani. Nyota wa igizo hilo walikuwa Muigizaji/Mtunzi na Mkurugenzi mtendaji wa TDE Lady Toussaint Duchess Campbell (Lady T) akishirikiana na wasanii maarufu wa Tanzania wakiwemo “Natasha” na “Monalisa. 
   Lady T alianza kwa “kutua” Uwanja wa ndege wa Dar es salaam kamavile kwa bahati mbaya kabla ya kuchukuliwa na mwenyeji wake Natasha na kutambulishwa maisha ya Afrika, hususan Tanzania, yalivyo. 
   Igizo hilo maalum la “Mrs Lucy Goes to Africa” kwa mtindo wa Broadway, lilisindikizwa na burudani ya muziki wa Jazz na chakula maalum kilichojizolea umaarufu nchini Marekani aina ya “Gumbo”. 
   Hakika “Mrs Lucy Goes to Africa” ni igizo la kipekee na lenye kusheheni vunja mbavu na kutoa burudani kwa umati mkubwa wa wadau uliohudhuria. ''Mrs. Lucy Goes to Afrika'' ilivunjwa watu mbavu na kuwaachia ujumbe mwanana wa matumaini na faraja katika muda wote wa masaa mawili uliochezwa.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, Mheshimiwa Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi. 
  Katika taarifa hiyo aliyoitoa kupitia vyombo vya habari, Alhaj Dk. Shein kwa masikitiko makubwa aliwaarifu wananchi kuwa leo tarehe 14 Agosti 2016, Mzee Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia, msiba ambao umetokea nyumbani kwake Mji Mwema, Kigamboni, Dar es Salaam.


  Alhaj Dk. Shei alieleza kuwa Marehemu Mzee Aboud Jumbe ni Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, ambaye vile vile alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Marehemu Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na umri wake. 
  Kwa taarifa ya Alhaj Dk. Shein, maziko ya marehemu yatafanyika kesho tarehe 15 Agosti 2016 saa 7.00 mchana ambapo maiti yake itasaliwa katika Masjid Mshawar, Mwembeshauri na kuzikwa nyumbani kwake Migombani. 
  Aidha, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa kufuatia mchango na juhudi kubwa ambazo Marehemu Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi alizichukua katika uhai wake kwa kuitumikia, kuiongoza na kuijenga Zanzibar pamoja na nafasi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  “Nchi yetu imekabiliwa na msiba mkubwa kwa kigfo cha kiongozi huyu mahiri”alieleza Alhaj Dk. Shein katika taarifa hiyo. 
  Kutokana na msiba huo mkubwa Alhaj Dk. Shein alitangaza rasmi siku saba za maombolezo, kuanzia kesho tarehe 15 Agosti 2016 ambapo katika kipindi hicho chote bendera zote  zitapepea nusu mlingoti. 
  Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa utaratibu wa maziko utafuata wasia ambao mwenyewe marehemu aliutoa wakati wa uhai wake. 

  “Tunaungana na Wanafamilia wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Naomba kutumia nafasi hii kutoa mkono wa pole kwa wafiwa wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabit marehemu mzee wetu na amlaze pahala pema peponi, Amin. Inalillahi wainnailaihi rajiun” Alieleza Alhaj Dk. Shein katika Taarifa hiyo.


  0 0  0 0

  Na Ankal
  Nilipopata tarifa kuwa  Blogger mkongwe Bi. Arianna Huffington (pichani) anastaafu kutoka Mtandao wa Jamii   ama blog ya Huffington Post
   (BOFYA HAPA)   ili kuanzisha mtandao wa Thrive Global unaohusiana na staili za maisha na afya (BOFYA HAPA), nilistuka sio kidogo maana daima amekuwa kichocheo changu kikubwa katika tasnia hii ya habari za mtandaoni.
  Bi. Huffington alianzisha mtandao wake huo wa  Huffington Post mwaka 2004 (Globu ya Jamii ilianza mwaka 2005) baada ya Rais George W. Bush kuchaguliwa kuongoza Marekani kwa mara ya pili, na wakati huo huo vita ya Iraq ilikuwa ikiendelea. 
  Blog hiyo ilianza kiutani-utani kwa taarifa za kawaida na michango hii na ile kutoka kwa marafiki zake, kabla ya sio tu kuwa moja ya blog kubwa duniani bali pia kampuni  kubwa ya habari mtandao duniani yenye matawi  katika nchi 15 kwa jina la Huffington Post Media Group.
  Kampuni hiyo hivi sasa inaajiri watu 850 kila pembe ya dunia na imeendelea kuwekeza katika kusaka na kutoa habari mtandao kwa picha, maandishi na video na kujizolea tuzo kibao ikiwemo ya Pulitzer Prize ambayo ni kubwa kuliko zote.
  Japokuwa  Bi. Huffington  amekuwa akijihusisha na maswala ya siasa muda wote, ikiwemo kumpinga  waziwazi  mgombe urais Donald Trump tokea atangaze azma yake hiyo ,  pia amekuwa akitumia muda wake mwingi katika maswala ya afya na maisha kwa kuandika kitabu  kuhusiana na mambo hayo mwaka 2014 kiitwacho Thrive na mwaka huu kuandika kingine kiitwacho The Sleep Revolution.  Mnamo mwezi wa June mwaka huu akatangaza kuanzisha mtandao wa Thrive Global.
  Katika mahojiano, Bi. Huffington  anaripotiwa kusema kuwa hawezi kujenga kampuni mpya kama kazi ya pembeni, hasa katika wakati huu ambapo wawekezaji wameshaanza kuwekeza mamilioni ya dola kwenye  kampuni ya Thrive Global.
  Majukumu yake yamewahi kubadilika mara moja huko nyuma, hususan pale kampuni ya AOL  kuinunua blog ya Huffington Post mwaka 2011 kwa dola milioni 315.  Katika makubaliano hayo  Bi. Huffington alibakia kuwa Mhariri Mkuu na wakati huo huo Rais wa Huffington Post Media Group.
  Kuondoka kwake katika kampuni hiyo kumekuja wakati kampuni ya Verizion ilipoinunua kampuni ya AOL  kwa dola bilioni 4.4, na kutangaza pia kutaka kuinunua Yahoo kwa dola bilioni 4.8. Ila yeye alikana kuwa kuondoka kwake kunahusiana na manunuzi hayo, bali alisema muda ni muafaka wa kuanza mambo mengine.
  Nilipata bahati ya kukutana ana kwa ana na Bi. Arianna Huffington huko  Davos, Uswisi, mnamo  Januari 26 mwaka 2012 (BOFYA HAPA) na kubadilishana naye mawazo pembezoni mwa  mkutano wa dunia wa uchumi. Nilifarijika sana pale mama huyo nguli wa habari za mitandaoni aliposema anaifahamu Michuzi Blog nami  nikamfurahisha kwa kumwambia nafuatilia kila hatua anayopitia.
  Nikikumbuka kukutana kwetu huko Davos na kuifikiria kauli hiyo, mie pia  sasa nimeanza kujiuliza endapo  kama sasa ni muda  muafaka wa kuachana na  Globu ya Jamii na kuendeleza Libeneke kwa njia zingine? 
  Jibu nitalitoa ifikapo Septemba 8, mwaka  huu wakati wa maadhimisho ya miaka 11 ya Globu ya Jamii.
  Kitabu hiki nilipewa kama zawadi na dada Emelda Mwamanga wa jariba maarufu la BANG! ambaye alitembelea ofisi za Huffington Post huko Marekani mwaka 2009. Naye akaniambia baada ya kupewa kitabu hicho akanikumbuka mara moja na kuamua kuja kunizawadia.  Asante sana Emelda. Still touched by the gesture...Nami nimeanza kuandika changu.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kabla ya hafla fupi ya kusherekea miaka 19 ya benki hiyo na kuzindua wa huduma tatu za benki hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha hatari wa Benki ya Exim David Lusala. kulia ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
   Mkuu wa kitengo cha hatari wa Benki ya Exim David Lusala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kadi za malipo za Exim (TANAPA cards, Master cards and VISA cards) ambazo zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA. Kadi hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki na pia kuzuia upotevu wa mapato katika tasnia ya Utalii. jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
   Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga akikata utepe kuzindua huduma ya  Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam leo.

  0 0
 • 08/15/16--05:47: SHUKRANI.
 • KUMBUKUMBU, mama Vailet Baraka anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa jamii hasa kuendeleza kinamama na vijana sehemu mbalimbali alipofanya kazi.

  Alikuwa ni Mbunge wa kwanza kuchaguliwa na wananchi katika jimbo la Njombe Kusini 1965 mpaka 1970.(jimbo liligawanywa sasa hivi ni Ludewa) aliweza kupigania mambo mengi jimboni kuleta meli tatu jimboni, mbili zinafanya kazi mpaka kipindi hiki baada ya moja kuzama.

  alitengeneza barabara  na kuanza ujenzi wa uwanja wa ndege uliopo Kijiji cha Masasi,alikuwa mchapa kazi hodari kuchelewa kazini ilikuwa mwiko.

  Aalipostaafu kazi serikalini alijiajiri kwa kilimo na kufundisha hisabati na kingereza, Mama Vailet alifariki 8/6/2016. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
  Amina. 

  si rahisi kushukuru mtu mmoja mmoja ila tunawashukuru sana sana wote mlioshiriki kwa njia moja au nyingine katika msiba huu Mungu awabariki, Tunashukuru Dr. wa hospitali ya Masiku aliemhudumia 7/6/2016, Tunashukuru Madakitari, wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili kitengo cha mapokezi na dharula waliomhudumia 8/6/2016. 

  Tunawashukuru wachungaji, uongozi na wanakwaya wa Anglican Viwege, Wa Injilisti Lutheran UDSM, Mchungaji G. Mwakyoma, familia ya marehem mzee Edward Salama, familia ya Dr. Wilson Marandu toka Arusha, familia ya Mwambona, familia ya Zacharia Namalimbogwa, familia ya  Msilu na Chale, familia ya mzee Sanga wa Namanga, familia ya Dr Mwaipopo na Sarah Botswana na Dar es Salaam, mama Mbwiga (Dar) familia ya Urassa Botswana na Dar, familia ya marehemu Dr. G.Komba wa Makongo, Pia , Asafu Haule, Mzee Timbuka, J. Chale, Shukurani sana sana David Marama(Australia), Jean Marama(U.S.A), Peter na Andrew Marama(Malawi),.

   Aidha familia inamshukuru sana Mhe. mama Anne Makinda,(Spika mstaafu) Mhe.William Lukuvi,(Waziri wa Ardhi) Mhe. Kate Kamba(Mbunge mstaafu) tunawashukuru pia kwa kusafiri toka Ludewa kuungana nasi Mhe. Deo Ngalawa Mbunge wa Ludewa, na Mhe. Stanley Kolimba.

  Tunawashukuru tena sana sana wote mlioacha shughuli zenu muhimu na kuja kuungana nasi, marafiki na majirani Mungu awabariki. Asante.

  0 0

  BENKI ya DCB COMMERCIAL imetoa madawati 100 kwa shule ya msingi Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi yake ya kuchangia madawati 300 kwa shule za manispaa tatu za mkoa wa Dar es Salaam.


  Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba akizungumza na waanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa benki ya DCB imeguswa na tatizo la ukosefu wa madawati kwa shule ya msingi hapa nchini.

  Amesema kuwa bodi na uongozi wa benki ya DCB inaunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na tatizo la madawati hapa nchini inetoa madawati 100 katika shule ya Msingi Lubakaya jijini Dar es Salaam leo.

  Nae Mkuu wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa, Said Chitumba amewashukueu benki ya DCB kwa mchango wao kwa kutoa madawati 100 katika shule hiyo ikiwa shule hiyo inavyumba 16 vya madarasa na sasa wanaukosefu wa madawati 300.


  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba jijini Dar es Salaam leo, madawati ambayo yatapelekwa katika shule Mpya ya Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam.

    Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakimkabidhi madawati Mkuu wa Shule ya Msingi, Lubakaya (Katikati) jijini Dar es Salaam leo. Katika Hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
     Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa shule na wa serikali katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi madawati 100 kutoka benki ya DCB jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami akizungumza na waandishi wa habari jijini  Dar es Salaam leo.

  Na. Lilian Lundo - MAELEZO.
  MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka huu jumla ya watanzania milioni 23 watakuwa na namba za utambulisho wa vitambulisho vya Uraia.

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Mamlaka hiyo kuweka saini ya mwombaji na mtoaji wa vitambulisho hivyo.

  “Tumeanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais tangu mwezi Juni mwaka huu, hii inamaanisha kwamba vitambulisho vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi Juni mpaka leo vina saini ya muombaji, saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa muombaji” amefafanua Mdami.

  Ameeleza kuwa kazi ya ugawaji wa vitambulisho hivyo inasubiri kuzinduliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli atakayekabidhiwa  kitambulisho cha uraia namba moja na baadaye vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wananchi  wengine. 

  Mdami amesema ifikapo Desemba 31 mwaka huu NIDA itakuwa imetoa namba za utambulisho wa vitambulisho hivyo  kwa watanzania milioni 23 kwa kutumia taarifa za Tume ya Uchaguzi (NEC) zilizo katika vitambulisho vya kupigia kura na kuzihamishia katika kanzi data ya NIDA.

  Amefafanua  kuwa ili mwananchi aweze kupata kitambulisho cha uraia atalazimika kufika katika ofisi za NIDA akiwa na vielelezo vinavyoonyesha mwaka wake wa kuzaliwa pamoja udhibitisho wa uraia wake hii ni kutokana na NEC kutokuwa na viambatanisho hivyo.

  Amebainisha kuwa mwananchi mwenye namba ya utambulisho anaweza kupata huduma zote zinazohitaji namba ya kitambulisho cha Uraia kutokana na namba hiyo kutobadirika na kuendelea kutumika hata baada ya kitambulisho kuchapishwa.

  Amesema mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wamekwisha patiwa vitambulisho  hivyo na milioni 6.5 wamesajiriwa kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyo. 

  Aidha, Vitambulisho hivyo vya zamani vitaendelea kutumika mpaka utakapotangazwa utaratibu wa kuvibadirisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vipya.

  Pia ametoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya watu wanaodai kwamba wa kumekuwa na mlolongo mrefu wa kupata vitambulisho hivyo kwa kueleza kuwa NIDA haina namna ya kufupisha mlolongo huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kuuza uraia wa Tanzania.

   Amesisitiza kuwa ni lazima NIDA ijiridhishe juu ya uhalali na sifa za muombaji ni kuwa ni Mtanzania kwa kuambatanisha vielelezo vinavyohitajika.

  0 0

  Afisa habari wa TFF Alfred Lucas.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini TFF, limethibisha kukamilika kwa usajili wa timu 11 zilizokuwa hazijakamilisha usajili wake kwa mfumo wa TMS baada ya kuongezewa muda wa masaa 48 baada ya kufungwa kwa dirisha la awali.

  Akizungumza na Michuzi Globu, Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa timu zote  11 zimeshakamilisha usajili wake kwa njia ya TMS baada ya kuongezewa muda wa masaa 48 na shirikisho la mpira wa Miguu Duniani FIFA.

  Awali dirisha la usajili nchini lilifungwa Agosti 06 huku timu kadhaa ikiwemo Yanga na  African Lyon za ligi kuu zikiwa hazijafanya usajili wake n kutakiwa kuandika barua za utetezi ili kuweza kupata fursa ya kufunguliwa tena kwa dirisha la usajili.

  Lucas amesem kuwa, baada ya kutum utetezi wao uliwasilishwa FIFA na wakapewa masaa 48 kukamilisha usajili huo huku TFF wakizipiga faini timu za ligi kuu kwa kulipa kiasi cha milioni tatu na timu za ligi daraja la kwanza wakitakiwa kulipa milioni moja.

  Kumalizika kwa usajili huo timu kwa sasa zinaweza kuendelea na taratibu za kujiandaa na ligi huku wakisubiri mapingamizi kwa wachezaji waliowasajili.

  0 0


   Mwananchi wa Zanzibar mwenye asili ya India Bhagwanji Meisuria maarufu kwa jina la (MSHAMBA) akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna ya Amani iliyopo Nchini kwa ujumla.
   Balozi Mdogo wa India Tek Chand Barupal akisalimiana na Wananchi wenye asili ya India wanaoishi Zanzibar katika maadhimisho ya kutimia miaaka 70 ya Taifa hilo iliofanyika katika Ofisi ya Balozi Mdogo wa India iliopo Migombani Zanzibar. 
  Balozi Mdogo wa India Tek Chand Barupal akiwahutubia wananchi wa Zanzibar wenye asili ya India waliohudhuria maadhimisho ya miaka 70 yaliofanyika Ofisi ndogo iliopo Migombani Zanzibar.
  PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR –HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KIKOSI  cha Yanga  cha Yanga leo hii kimeendelea na mazoezi ya kujianda na mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya azam unaotarajiwa kuchezwa siku ya jumatano Augosti 17.

  Mazoezi ya Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Vodacom yanafanyika katika viwanja vya Gymkhana klabu huku kikosi hicho ki knocktarajiwa kuwakosa wachezaji wake kadhaa baada ya kuwa majeruhi.

  Mshambualiaji wa kimataifa Donald Ngoma amerejea kikosini baada ya kuwa mapumziko kwa kipindi kirefu na akitumikia adhabu ya kadi mbili za njano za michuano ya kombe la Shirikisho Barana Afrika Na kuukosa mchezo dhidi ya Mo Bejaia.

  Kocha Mkuu, Hans Van De Pluijm ameonekana kuwa  makini sana katika kuhakikisha anaendelea kuibuka na ushindi kwa mara nyingine  tena Mpaka sasa Yanga wameweza kuifunga Azam mara tatu mfululizo na kuichukua Ngao mara 5.

  Wachezaji ambao ni Majeruhi ni 
  Ally Mustapha anayeuguza kifundo cha kidole, Kelvin Yondani(jicho), Juma Abdul(misuli), Obrey Chila Chirwa(goti) na Vicent Andrew Dante(nyonga).

  0 0

  ⁠⁠⁠Na Bakari Issa Madjeshi, Globu ya Jamii 

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo. 

  Pamoja na kukabidhi ramani hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema jengo hilo litagharimu kiasi cha fedha 5, 080, 155, 600 ili kukamilika. Pia amesema jengo hilo mpaka kukamilika litakuwa la kipee na kupewa hadhi kama Taasisi kubwa ya Kiislamu na kusisitiza ujenzi wa jengo hilo hautazidi miezi 14.

  Amesema amekabidhi mchoro huo kutokana na kutambua na kuthamini umuhimu wa BAKWATA katika Taifa pamoja na kuwataka Waislamu na wasiokuwa waislamu kujitokeza katika kutoa misaada hiyo. Pia ametoa shukrani kwa waislamu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushereheka nao pamoja katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo amesema mwezi huo ndio uliokuwa chimbumbo la ujenzi wa jengo hilo la BAKWATA. 

  Akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abuubakari Zuberi amewataka Waislamu kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa huyo ikiwa kuwataka kuamini ya kuwa na haki ya kupokea misaada kama Waislamu.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimuelekeza jambo Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir namna ujenzi wa ghorofa hilo utakavyokuwa,mara baada ya kukabidhiwa mchoro wa jengo hilo litakalogharimu zaidi bilioni tano,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum.PICHA NA MICHUZI JR. 
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pampja na Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir wakitazama mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu,ambapo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tano,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
  ,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum .
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja naSheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti wakionesha mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika jijini Dar mapema leo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizaungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
  Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti Abubakary Zubeir akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa,kabla ya kukabidhiwa mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
   Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum akimkaribisha Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti Abubakary Zubeir  mbele ya wageni waalikwa,kabla ya kukabidhiwa mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar ES Salaam,Mh Paul Makonda. 
   Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yalikuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi. 
   Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yalikuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi.

  0 0

  TAMASHA la wasanii wa kizazi kipya la kuchangia madawati limefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo jumla ya madawati 150 yamepatika.

  Tamasha hilo liliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe ‘Double G’ ambapo  aliwashukuru wasanii hao kwa kujitokeza kusapoti upatikanaji wa madawati kwa watoto wa Handeni ambao ni moja ya changamoto zinazokabili Wilaya yake ukiachilia ile ya Maji.

  Wasanii waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa Wilaya ya Handeni walisema wameamua kumsapoti Gondwe kwa kuwa wanamfahamu muda mrefu toka akiwa mtangazaji wa radio na alikuwa akiwasapoti kazi zao kwa kiasi kikubwa.
  Ben Paul alisema “Wasanii kama wasanii tunatakiwa tusaidie jamii yetu kama hivi, naishi kwenye jamii hivyo naona matatizo mengi yanayokabili jamii yetu ni wajibu wangu kutumia nafasi hii kusaiii, karne hii wadogo zetu bado wanakaa chini, tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kumaliza tatizo hilo.”alisema Ben Paul anayetamba na Wimbo wake wa sasa  wa ‘Moyo Mashine’ na kuongeza.

  “Vijana wa sasa wanapenda kushinda kwenye mitandao ya kijamii na kulalamikia serikali, wanataka serikali ndio iwafanyie kila kitu wakati sisi hatufanyii jambo serikali.”alisema.

  Msanii nguli, Ambwene Yesaya ‘Ay’ akizungumzia tamasha hilo alisema “Double G kwanza kabisa ni mtu wa watu, ndio maana wasanii wote unaotuona hapa tumeamua kumsapoti bure kabisa, alivyotueleza wazo lake tukamwambia ni zuri na tutamsapoti, alichokifanya ni kitu kizuri ambacho kinatakiwa kiigwe na kila mtu.
  “Itakuwa vizuri kila mtu akaweka nia ya kusaidia sio lazima tutengeneze madawati tunaweza tukafanya siku ya kuotesha miti ambayo naamini kila msanii akiotesha mti mmoja leo, utakuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.”alisema Ay.

  Aidha mwandaaji wa tamasha hilo Godwin Gondwe alisema kuwa Wilaya yake inakabiliwa na uhaba wa madawati 530 na anashukuru kwa kupata madawati 150 katika fedha zilizopatikana kwenye tamasha hilo la Wasanii hna kwamba bado ana upungufu wa madawati 380.

  “Nawashukru sana wasanii waliojitoa kunisapoti, na wakazi wa Wilaya ya Temeke kujitokeza kumuunga mkono Rais wetu ili kutengeneza historia  za wadogo zao wasikae chini tena, na katika tamasha hili tumeweza kukusanya fedha ambazo zitatuwezesha kupata madawati 150.”alisema Gondwe.
  Katika tamasha hilo, muitikio wa watu ulikuwa mkubwa na lilipendezeshwa na wasanii mbalimbali. Walioanza kufanya makamuzi mwanzoni mwa tamasha hilo ni pamoja na Bendi ya La Musica Vijana Classic, Mc wa Dar Live Brighton ‘Dalada’ na wengine wengi.

  Baada ya shoo kunoga mashabiki wa Dar Live walifurahia muziki mzuri kutoka kwa Bendi ya Injili ya GWT (Glorious Worship Team), Mfalme wa Muziki wa Uswazi maarufu kama Singeli Msaga Sumu, Sterio, Ben Pol, Linex huku Fid Q, AY, Msami na Barnaba wakikamilisha listi kwa makamuzi ya nguvu.

  Baada ya wasanii wote kutoa burudani ya nguvu, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ‘Double G’ aliwashukuru wote waliomuunga mkono na akaomba waendelee kujitolea zaidi kwenye masuala ya kujenga taifa.

  0 0
 • 08/15/16--08:43: IGP MANGU AITEMBELEA AICC.
 • Mkuu w Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu akisani kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Elishilia Kaaya. IGP Mangu alifanya ziara katika kituo hicho ili kukagua maadalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya nchi za Kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufanyika AICC katikati ya Septemba mwaka huu. (Picha kwa hisani ya AICC).

  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Elishilia Kaaya (kulia) akiongea na Mkuu w Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu alifanya ziara katika kituo hicho ili kukagua maadalizi ya mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya nchi za Kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufanyika AICC katikati ya Septemba mwaka huu (katikati) ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo. (Picha kwa hisani ya AICC).

  0 0
 • 08/15/16--09:17: Pangani Wapata Kivuko Kipya
 • Na Theresia Mwami  TEMESA
   Wananchi wa Pangani na Bweni mkoani Tanga wamepata kivuko kipya cha MV. Tanga, ambacho sasa kitasaidiana na MV. Pangani II kutoa huduma katika eneo la Pangani na Bweni.
  Akiongea na wananchi wa Pangani Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase amesema  kukamilika kwa ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Tanga ni muendelezo wa sera ya Serikali ya kuboresha huduma ya vivuko katika maeneo mbalimbali yaliyo na mahitaji ya vivuko nchini.
  “TEMESA imejipanga kuhakikisha kuwa vivuko vyake vyote vinafanyiwa matengenezo ya kinga kwa wakati, ili kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi wanaotumia vivuko hivyo inapatikana kwa wakati muafaka” Alisema Mhandisi Manase.
  Mhandisi Manase ameongeza kuwa  hivi sasa MV. Pangani II itakwenda kwenye ukarabati mdogo na baada ya ukarabati huo vivuko vyote viwili vitabakia katika eneo la Pangani na Bweni ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
  Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Lazaro Vazuri  alisema kuwa kivuko cha
  MV. Tanga ni mwanzo wa uboreshajji wa huduma ya vivuko nchini na kwa sasa wapo katika mikakati ya kukarabati vivuko vilivyopo na kujenga vivuko vibya ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa vivuko katika maeneo yenye huhitaji.
  Mmoja ya wananchi wa Wananchi wa Pangani/Bweni Bw. Othman Juma Ali ameipongeza Serikali kwa juhudi za kupambana na changamoto ya vivuko inayozikumba sehemu nyingi zilizozungukwa na maji.
  “Tumekipokea kivuko cha MV. Tanga kwa furaha kubwa na tunaiomba Serikali kutoa huduma ya kivuko hiki kwa saa 24  kila siku ili kitusaidie wananchi hasa wa eneo la Bweni kupata huduma hiyo nyakati za usiku tunapohitaji kupata huduma za kijamii upande wa Pangani” alisema Bw. Othman.
  MV. Tanga imesanifiwa na kutengenezwa na Kampuni ya kitanzania ya Songoro Marine Company Ltd na kivuko hiki kina uwezo wa kubeba tani 50 ambazo ni sawa na kubeba abiria 100 na magari 6 kwa pamoja.
   Kivuko cha Pangani II pamoja na kivuko kipya MV. Tanga vikiwasili katika eneo la Pangani Jijini Tanga. 
   Kivuko Kipya cha Pangani MV. Tanga baada ya kuwasili katika eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga.
    Abiria na Magari yakiingia kwenye  kivuko kipya cha pangani MV. Tanga kinachotoa huduma eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga. 
  Baadhi ya wasafiri wakishuka katika kivuko kipya cha pangani MV. Tanga kinachotoa huduma eneo la Pangani na Bweni Jijini Tanga. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA

  0 0


older | 1 | .... | 1320 | 1321 | (Page 1322) | 1323 | 1324 | .... | 3284 | newer