Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1319 | 1320 | (Page 1321) | 1322 | 1323 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 08/13/16--12:28: Mrema Awashauri Vijana

 • 0 0
  0 0


  TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam leo imefanya upasuaji mkubwa na  kuweka betri katika moyo wa mtu wa makamo kwa mafanikio. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa Mohamed Janabi ameiambia Globu ya Jamii jioni hii kwamba ana furaha kwa kufanikiwa kwa upasuaji huo ambao  amesema umefanyika  mara ya kwanza  kufanyiwa  mtu wa makamo nchini Tanzania.
  “Tumeweka kifaa hicho ambacho kitaalamu kinajulikana kama Pacemaker CRTD kwa mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 68 ambaye moyo wake umechoka na hivyo kushindwa kusukuma damu kwenda kwenye mishipa ili isafiri mwilini na yeye aweze kuishi,” alisema Profesa Janabi.

  "Hii ni hatua muhimu kwa taasisi hii kwani mafanikio haya yanatupa hamasa ya kuongeza juhudi za kuokoa maisha ya Watanzania wengi hapa hapa nyumbani", alisema Profesa Janabi
  Ameongezea kuwa hivi karibuni JKCI  ilifanikiwa kufanya upasuaji mwingine wa kwanza na  kuweka betri katika moyo wa mtoto mwenye umri wa miaka sita.
  Mapema Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo hapo JKCI, Peter Kisenge, alisema taasisi hiyo kweli imefanya upasuaji mara nyingi, lakini hawajawahi kufanya upasuaji  wa kuweka betri kwenye moyo wa mtu mzima ambao misuli yake imechoka na haiwezi tena kufunguka, kusukuma damu kwenye mishipa.
   Alisema utendaji kazi wa moyo wa mgonjwa huyo ulikuwa  chini ya kiwango cha asilimia 20 ndio maana mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji huo ili betri hiyo iweze kumsaidia moyo wake kufanya kazi sawa sawa.  
   Dkt Kisenge amesema JKCI imefanya  upausaji huo kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini Kenya.  0 0

  The Chair of the Commonwealth Observer Group, HE Dr Jakaya Kikwete, former President of the United Republic of Tanzania (pictured above) says that the voting, closing and counting process following the Zambian General Elections and Referendum has been credible and transparent. However, the Group will reserve full judgement of the overall process until it publishes its final report in the coming months. 
  ‘I commend the people of the Republic of Zambia for the peaceful and orderly manner in which they exercised their right to vote’, he said to a packed press conference in Lusaka. 
  ‘On Election Day, our Observers reported that most voting stations opened on time with few exceptions. They were struck by the long queues in some polling stations but found that voting generally took place in an atmosphere of calm.’
  Seventeen Commonwealth Observers were deployed to all ten provinces of Zambia. They fed back their observations over the pre-election period and Election Day. After the elections they remained in their areas to assess the post-election atmosphere.
  Over six and half million people are eligible to vote in Zambia and turn out is expected to be high. Women are active participators in the election process and Observers were pleased to see an equal number of men and women voters taking part not just as voters, but also as polling officers and other staff involved in the election process. 
  ‘We urge all political parties and candidates to respect the will of the people of Zambia’, the Chair reiterated. ‘This is the Zambian Constitutional way. It is also the Commonwealth way.’
  The Commonwealth Observer Group, composed of seventeen persons drawn from across the Commonwealth, was appointed by Commonwealth Secretary-General Patricia Scotland QC. Their mandate is to observe the preparations for the election, the polling, counting and the results processes, and the overall electoral environment.
  The observers are tasked with assessing whether the elections were conducted according to the standards to which Zambia has committed, including domestic law and relevant regional, Commonwealth and other international standards. The observers are bound by the International Declaration of Principles for Election Observation, to which the Commonwealth is a signatory.
  The Commonwealth Observer Group arrived in Uganda on 4 August and was deployed to all ten provinces of Zambia. The final report will be submitted to the Commonwealth Secretary-General, who will in turn send it to the Government of the Republic of Zambia, Electoral Commission of Zambia, political parties, and all Commonwealth governments. It will shortly thereafter be made public.

  To read full Interim Statement CLICK HERE


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano dhidi ya rushwa,ufisadi kama hatua ya kukomesha tabia hiyo ambayo inarudisha nyumba maendeleo ya wananchi. 
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 13-Aug-16 wakati anahitimisha kilele cha sikukuuu ya Kizimkazi katika kijiji cha Kizimkazi Mkunguni wilayani ya Kusini Unguja – Zanzibar ambaye yeye ni mwasisi wa sikukuu hiyo ambayo inatumiwa na wakazi wa maeneo hayo kufanya michezo mbalimbali ya jadi pamoja na kujadili na kuweka mipango na mikakati ya kujiletea maendeleo kwa ushirikiano na viongozi wao.

  Makamu wa Rais amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watendaji wanaorudisha nyuma maendeleo ya wananchi ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma ili kukomesha tabia hiyo. Amesema kuwa ili wananchi waweze kupata maendeleo ya haraka ni muhimu wananchi wakaimarisha ushirikiano miongoni mwao katika kubaini changamoto zinazowakabili na kushirikiane na viongozi wao katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
  Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema yeye kama kiongozi wa kwanza kupata wadhifa huo kutoka kwenye kijiji cha Kizimkazi - Zanzibar ataendelea kushirikiana wananchi hao kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hao ikiwemo tatizo la upatikanaji wa maji.
  Makamu wa Rais pia amehimiza wananchi wa Kizimkazi kutafuta eneo haraka kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali ambayo bado ni tatizo kubwa katika eneo hilo ili aweza kuwasaidia katika ujenzi wake kama hatua ya kuondoa kero ya watoto kushindwa kupata elimu ya awali.

  Katika Risala maalum ya wananchi wa kijiji cha Kizimkazi na Katibu wa Sherehe hizo Said Ramadhani Mgeni kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wamewapongeza viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada wanazofanya za ukusanyaji wa mapato ya serikali na wamesema wanaimani kubwa kuwa fedha zinazopatikana zitatumika katika kuinua uchumi na kujenga ustawi wa Jamii bora wananchi.

  Wananchi hao wameahidi kuwa watadumisha na kuimarisha ushirikiano kati yao na serikali hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Baadhi ya Viongozi wa wilaya na Mkoa wa Kusini Unguja waliopata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo ya hutimisha sikukuu ya wakizimkazi wamewaomba wananchi kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao. Katika kilele cha sherehe hizo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi ambao walishiriki kwenye mashindano ya siku ya Kizimkazi zikiwemo fedha taslimu.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Ndugu Idrisa Kitwana wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Kimkazi (Kizimkaziday) kwenye kijiji cha Kizimkazi Mkunguni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Mashindano ya kuzuta kamba

  Vijana wa Kiume wakishindana kukuna nazi ikiwa sehemu ya mashindano ya Siku ya Kizimkazi (Kizimkazi Day).
  Wakina Mama wakishindana kufunga kamba kwenye kilele cha sherehe za Kizimkazi. 

  0 0  0 0


  Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Tanzania Daima, Clezencia Tryphone wakiwa na furaha baada ya kufunga ndoa na Joseph Singano katika Kanisa la Mt. Nicholaus Parokia ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.
  Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Tanzania Daima, Clezencia Tryphone akiwa na furaha baada ya kufunga ndoa na Joseph Singano katika Kanisa la Mt. Nicholaus Parokia ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela jana  alitembelea eneo la Isimila na kujionea uzuri na mandhari yake. Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa huu wa Iringa.
  Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hili ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa hapo tangu mwaka 1951. Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina ya tofauti ya viboko.

  Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila ambalo lina mikondo miwili ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
  Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.Kuna nguzo za kipekee zilizotengenezwa na mmomonyoko wa udongo. dalili zinaonyesha kivutio hiki kinaweza kupotea kutokana na mvua kali zikienyesha miaka ijayo.
   
   Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa katika miamba ya kale  eneo la Isimila
    Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa katika miamba ya kale  eneo la Isimila
   Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa katika ju,ba la makumbusho ya  kale  ya Isimila

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za  Mkoa huo (hawapo pichani), katika Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa viongozi hao Mjini Bariadi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji
  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini(kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za  Mkoa huo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka (kulia) kufungua Mafunzo elekezi kwa viongozi hao
  Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za  Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji.Mstari wa Kwanza kutoka kushoto Wakuu wa Wilaya,Tano Mwera (Busega), Seif Shekalaghe (Maswa), Joseph Chilongani (Meatu), Benson Kilangi (Itilima) na Festo Kiswaga (Bariadi).
  Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za  Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji. Kutoka (kushoto) Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Afisa Uhamiaji, Kamanda wa Zimamoto na Mkuu wa TAKUKURU.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati akifungua warsha ya kimataifa kuhusu mpango wa takwimu za malengo ya maendeleo endelevu uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alibina Chuwa (kushoto), akihutubia katika warsha hiyo.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (katikati), akipitia nyaraka kwenye warsha hiyo. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
  Warsha ikiendelea.
  Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

   Kundi la DDI Crew la jijini Dar es wakionyesha umahiri wao wakati wa shindano la  robo fainali la Dance 100% 2016  lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini,Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika  hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.
   Kikundi cha The Guest Crew la jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao  kusakata dance wakati wa shindano la  robo fainali la Dance 100% 2016  lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika  hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki
   TIMU MAKOROKORO: Kundi la timu Makorokoro  Boys la jijini Dar es salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dance wakati wa shindano la  robo fainali la Dance 100% 2016  lililofanyika katika viwanja vya Don bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika  hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki.
   Kundi la J COmbaty la Zanzibar wakikonga nyoyo za mashabiki wakati wa robo fainali ya shindano la Dance100%2016 katika viwanja vya Don bosco jijini Dar es Salaam . Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhanimiwa na Vodacom Tanzania.Jumla ya makaundi 10 kati ya 13 yalifanikiwa kuingia katika  hatua ya nusu fainali itakayofanyika katika viwanja hivyo mwishoni mwa wiki. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  Na Frank Shija, MAELEZO

  Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vitakavyo jikita katika fani za Usafirishaji vitakavyojengwa Barani Afrika kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
  Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho alipokutana na Mwakilishi Mkuu wa masuala ya Uchumi na Biashara kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Bwana Lin Zhiyong wakati wa ziara ya kufanya tathmini juu ya uwezo wa NIT katika utoaji wa elimu ya Usafirishaji na namna ya kuweza kukisaidia chuo hicho.

  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo amemuhakikishia Mwakilishi Mkuu wa masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa NIT iko imara na inayo mipango kabaambe kwa ajili ya upanuzi wa chuo hicho utakao enda sambamba na kuongezeka kwa Programs zitakazokuwa zikifundishwa.

  “Kutokana na urafiki wa muda mrefu tulionao baina yetu na China ni imani yangu kuwa Chuo hiki kitakuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji vitakavyojengwa kwa masaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China barani Afrika kama ambavyo Rais wan chi hiyo alivyo dhamiria wakti wa mkutano huko Afrika ya Kusini” Alisema Dkt. Chamuriho.

  Ni dhahiri kuwa wataalamu wa masuala ya usafirishaji wanatakiwa kwa wingi kwani ukuaji wa Sekta hiyo unaenda kwa kasi hali kadhali Jiografia ya nchi yetu inatoa fusra kwa Tanzania kujenga miundombinu ya usafirishaji kama vile Barabara na miundombinu ya Reli, Viwanja vya Ndege ili kuunganisha na Bandari.

  Mpango huo umekuja katika wakati muafaka kwani utasaidia kuongeza idadi ya waataalam katika sekta ya usafirishaji kwa kuwa wanafunzi wengi zaidi watajiunga na masomo mbalimbali yatakayofundishwa katika chuo hicho kitakapo kamilika.

  Mhandisi Profesa Zacharia Mganilwa ni Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji, anasema kuwa wao kama uongozi wa chuo wanao mpango mahususi wa kufanya maboresho makubwa ya Chuo hicho ili kiweze kukidhi mahitaji halisi ya Sekta ya usafirishaji hapa nchini kwa sasa.

  “Sisi kama Taasisi tumejipanga kuhakikisha tunafanya maboresho ya Chuo chetu ili kiendane na hali halisi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji hapa nchini, katika mpango huo tumenuia kuanzisha Shule tano zitakazo jikita katika nyanja za Shule ya Uhandisi na Teknolojia, Shule ya Teknolojia ya Anga, Shule ya Usafirishaji na Logistic,Shule ya Elimu, Hisabati na Kompyuta na Shule ya Biashara NIT”. Mhandisi Mganilwa

  Aliongeza kuwa kutokana na mpango huo NIT inalo maeneo yakutosha na kukidhi mahitaji ya utekelezaji wa mpango huo kwani ina jumla ya ekari 46 katika eneo la sasa ambapo kuna ardhi ekari 46 ambapo kati ya hizo ni asilimia 30 tu ndiyo iliyotumika hadi sasa, pia chuo kimefanya utaratibu wa kupata eneo jingine la ekari 1600 katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

  kizungumza wakati wa ziara hiyo ya kufanya tathmini ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong ameonyesha imani kwa Chuo hicho na kuahidi kusaidia katika kuhakikisha kinakuwa miongoni mwa Vyuo hivyo Vitano vilivyoahidiwa na Rais wao.

  Aliongeza kuwa kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itakuwa nchi ya uchumi wa kati.

  “Nimeshawishika na niliyojionea hapa naweza kusema Serikali yetu itakuwa tayari kusaidia program mbalimbali zilizopo hapa na kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo nawahakikishia kuwa  NIT itakuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika vitakavyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kama ambavyo Rais wetu alivyo ahidi wakati wa Mkutano Jijini Johannesburg, Afrika Kusini”.Alisema Zhiyong.

  Zhiyong aliongeza kuwa ujenzi huo wa Vyuo hivyo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

  Ziara hiyo ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya program zinazofundishwa, rasilimali watu na miundombinu kwa maana ya eneo.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt. Leonard Chiriho  akizungumza na wawakilishi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China walipotembelea Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Wawakilishi hao wametembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho kinakidhi kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika.    Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi. Profesa. Zacharia Mganilwa, Katibu wa Tatu Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Sun Chengfeng, Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin Zhiyong na Mkurugenzi wa Huduma za Uasafirishaji kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Aron Johnson Kisaka.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt. Leonard Chiriho akimzungusha Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin Zhiyong (katikati) alipotembelea Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi huyo alitembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho kinakidhi kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa.
  Picha na Frank Shija, MAELEZO

  0 0

   Waziri  wa Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba akielezea hali ya upatikanaji wa umeme katika jimbo lake, mara Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhogo alipofanya ziara katika jimbo lake. Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili  ya kukagua miradi ya  umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.


   Mbunge wa Lushoto, Shaban Shekilindi akielezea utekelezaji wa miradi ya usambazji wa umeme vijijini inayotekelezwa na REA katika jimbo lake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wakazi wa jimbo hilo (hawapo pichani)

   Sehemu ya wakazi wa eneo la Mlola wilayani Lushoto mkoani Tanga wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
   
   Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zephania Maduhu (katikati) akielezea mikakati ya ofisi yake katika kuimarisha  shughuli za uchimbaji madini katika mkoa huo. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kushoto ni Mbunge wa Lushoto, Shaban Shekilindi.

   Kiongozi wa Kikundi cha Wazee wa Utamaduni cha Mlola,  Khalfan Bakari (kushoto) akitoa maoni yake mbele  ya  Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo (kulia)

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Lukozi wilayani Lushoto mkoani Tanga.


  0 0

  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), leo saa 6:00 usiku litafunga tena dirisha la usajili baada ya kulifungua jana kwa saa 48 na imebainika kuwa timu tatu zaidi zilikuwa na dosari katika usajili hivyo kufanya ongezeko la kutoka timu nane zilionekana kwa haraka mapema wiki hii mara baada ya dirisha kufungwa Agosti 6, 2016.
  Timu hizo kwa ujumla zilikuwa na dosari ya ama kutokusajili kabisa au kutokamilisha usajili wa ushiriki wa ndani kwa msimu wa 2016/2-17. Timu tatu nyingine zilizobainika leo Agosti 14, 2016 katika mtandao ni pamoja na Toto African ya Mwanza na Stand United ya Ligi Kuu Tanzania Bara kadhalika Arusha FC ya Arusha ambayo msimu huu itashiriki Ligi Daraja la Pili (SDL).

  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini

  0 0

  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ameitaka Mifuko ya Hifadhi za jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea uchumi wa viwanda utakaolisaidia taifa kukua kiuchumi na pia kuwanufaisha wanachama wa mifuko hiyo kutokana na uwekezaji huo wenye tija.

  Jenista Amesema hayo akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko pamoja na Watendaji katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (ISSA) .

  Amewataka Wakurugenzi hao kuunga mkono Agenda ya taifa ya kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda.

  Waziri huyo amewataka Wakurugenzi wa mifuko kuhakikisha kuwa wanadhibiti mifuko hiyo ili wanachama waweze kupata mafao yao kwa wakati muafaka bila kuwepo kwa ucheleweshaji.

  Mwenyekiti wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (ISSA) Eliud Sanga amesema kuwa Shirikisho hilo litaendelea kuhimiza Mifuko hiyo kutimiza wajibu wake katika kutoa mafao bora kwa wanachama wao pamoja na kubuni mafao mapya ili kuwavutia wanachama.

  Sanga amesema kuwa kwa sasa mifuko hiyo imefungua milango yake wazi kuwapokea wanachama kutoka sekta ambazo si rasmi ili nao waweze kunufaika na mafao . Na Pamela Mollel,Arusha.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akizungumza na Wakurugenzi na Watendaji wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii katika mafunzo yaliyohusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko hiyo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA),  jana jijini Arusha.
  Mwenyekiti wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (TSSA), Eliud Sanga akifafanunua jambo katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi za jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifukohhiyo.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akikabidhi cheti kwa Mjumbe wa Bodi ya PPF kutoka TUCTA, Adelgunda Michel aliyeshiriki katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi za jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA), jana jijini Arusha.

  Katibu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), Meshach Bandawe akizungumza katika mafunzo kwa bodi za Udhamini za Mifuko ya hifadhi za Jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko hiyo,  yaliyoandaliwa na Shirikisho hilo, jana jijini Arusha. 

  Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyorara.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Msanii, Ally Salehe 'Ali Kiba' akishambulia jukwaa wakati akitumbuiza kwenye  tamasha la kutimiza miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili tokea kuanzishwa Kwake. Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jana ambapo lilidhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.
   Msanii, Snura Mushi, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
   Msanii, Juma Kassim 'Juma Nature, akitumbuiza kwenye 
  tamasha hilo.
   Msanii Stamina akipagawisha  kwenye tamasha hilo.
  Wananchi wakifuatilia Tamasha la Serebula Festival la kuazimisha miaka miwili ya chanel ya startimes Swahili iliyoandaliwa na kampuni ya Bluelines kwa kushirikiana na uwawei jijini Dare s Salaam jana.
  Na Dotto Mwaibale
  MSANII wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura Lady Jay Dee na Ali Salehe Ali Kiba wameonesha umahiri wao wa kuimba kwa kutumia 'live band' katika tamasha la Serebuka na Festival 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Mashabiki walioudhuria tamashan hilo walianza kuonesha shangwe baada ya Lady Jay Dee kupanda jukaani na kuimba tungo na alioimba wimbo wa Ndindindi mashabiki walilipuka kwa vifijo.
  Shangwe hizo zilidumu hata kwa msanii Ali Kiba ambapo walimtaka aendelee kuimba licha ya muda wa kuendelea na tamasha hilo kuwa umekwisha.
  Ali Kiba aliwachangua zaidia mashabiki walipoimba wimbo wa Aje ambpo dakika za mwisho jukwaani hapo akapanda mwanadada na kushuka na msanii huyo na kuacha mashabiki wakishangilia kwa shangwe.
  Wasanii wengine ambao walionesha uhai katika tamasha hilo, Bonivecture Kabobo 'Stamina' ambaye mashabiki walionesha kumuunga mkoano kutokana na aina ya uimbaji wake kuteka mashabiki.


  Pia katika tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya King'amuzi cha Starv Times liliudhuriwa ma Juma Kasimu 'Juma Nature', Madee,Yamoto Band, Snura  na wengineo ambao waliimba kwa kutumia 'Play Back'.
  Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival liliandaliwa  na Kampuni ya StarTimes na  Kudhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.

  0 0

   Karibuni sana katika mkutano wetu muhimu tunaofanya leo tukiwa hapa Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha juu cha Jumuiya yetu yaani Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa.
  Tarehe 10 Agost mwaka huu kilianza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kikafuatia kikao cha  Kamati ya Maadili, kufuatia kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa na baadaye Baraza Kuu la UVCCM Taifa. Jumla ya Agenda tisa (9) zilijadiliwa.
  Baraza Kuu limeridhika na taarifa kadhaa kuhusiana na agenda mbali mbali na kupokea taarifa moja nyeti na muhimu kwa Jumuiya. “Ripoti ya uchunguzi wa Shamba la UVCCM Na. 454 MBYLR lenye ekari 210” lililopo Igumbilo Wilaya ya Iringa mjini Mkoani Iringa ambalo limeuzwa kwa Ndugu Suhail Ismail Thakore kinyume na taratpia  pia viwanja hivyo kuuzwa kwa watu mbali mbali na kuwahusisha Viongozi kadhaa wenye dhamana ndani ya Jumuiya yetu.

  Baada ya kupata taarifa za uuzaji wa shamba hilo Mali ya UVCCM, kwa Mamlaka iliyonayo Kamati ya Utekelezaji Taifa Ibara 91 (d), ilimwachia Mamlaka Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuunda na kuteua wajumbe watatu wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kuenda kufanya uchunguzi wa kadhia hiyo.
  Nichukue nafasi hii kuishukuru kwa dhati 
  Kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na;

  Ndugu Mariam Chaurembo    -    Mwenyekiti

  Ndg Juma Homela  - Katibu

  Ndg AmirMkalipa    Mjumbe
  Ndugu Ally Nassor  Mjumbe

  Kwa kufanikisha kazi waliyopewa na Jumuiya na hatimaye kuwasilisha ripoti yao ambayo ilibaini mambo kadhaa machafu kinyume na miongozo ya Chama na Jumuiya yetu. 


  0 0


  0 0

  Taarifa iliyotufikia mchana huu, inaeleza kuwa  kuwa Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi (1972-1984), Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 96.
  Mzee Aboud Jumbe amefikwa na mauti hayo nyumbani kwake Kigamboni, Jijini Dar es salaam. Rais wa Jamhuri wa Muungano amemtumia Salaam za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa msiba huu mzito

older | 1 | .... | 1319 | 1320 | (Page 1321) | 1322 | 1323 | .... | 3272 | newer