Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

KITUO CHA REDIO CHA JEMBE FM CHATEKA MAWIMBI YOTE KANDA YA ZIWA


JAMANI FOUNDATION KWA KUSHILIKIANA NA TEA WATOA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI WILAYANI TEMEKE

$
0
0
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiwa wamekaa katika madawati waliyokabidhiwa na taasisi ya Jamani Foundation. Kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari, Meneja wa TEA, Tito Mganwa na Anne Mlimuka.Mkurugenzi wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari (kushoto) akikabidhi madawati Mameneja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa (kulia), Anne Mlimuka (wa pili kulia). Katikati ni Mwalimu Kasyupa kutoka Shule ya Msingi Yombo akiwakilisha kwa niaba ya waalimu wa shule zilizopokea msaada wa madawati 100. Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuk (kushoto), akikabidhi madawati yaliyotolewana JAMANI Foundation kupitia TEA kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Umoja, Juto Komba.

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA LEO JUMAMOSI 13 August 2016 FRANKFURT,UJERUMANI

$
0
0
Na Zainab Ally Hamis, (DSJ)

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya, Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani, wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival litakalo fanyika jumamosi hii 13 August 2016 katika viwanja vya Rebstock Park,jijini Frankfurt,Ujerumani, ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani.

Kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja a.k.a Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu (Anunnaki Aliens) kinadumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya.

usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

CHRISTIAN BELLA ALIVYONOGESHA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI JIJINI MWANZA

$
0
0

 Mwanamuziki nyota Christian Bella akikonga nyoyo za maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akitumbuiza  maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016. 
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akiimba mbele ya maelfu ya wananchi wa  jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akipongezwa kwa kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwanamuziki nyota Christian Bella baada ya kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016

MWENYEKITI MPYA WA CCM RAIS DKT MAGUFULI APOKELEWA DAR ES SALAAM KWA NDEREMO NA VIFIJO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.

Hakuna fidia kwa wakazi watakaopisha miradi ya REA - Prof Muhongo

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa hakuna fidia yoyote itakayotolewa kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vijijijni unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). 
Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi kutoka katika vijiji vya Kweditibile na Kamgwe vilivyopo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga. 
Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi. 
Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imetenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya usambazaji wa umeme vijijini ambapo iwapo fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kulipa fidia, inaweza kuathiri utekelezaji wa miradi ya REA 
“Mkumbuke kuwa iwapo fedha hizi zitatumika kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya umeme vijijini, fedha nyingi zitatumika na kukwamisha utekelezaji wa miradi ya REA,” alisema Profesa Muhongo 
Aliendelea kusema kuwa miundombinu ya umeme haihitaji eneo kubwa hivyo haiwezi kuathiri mazao kwenye mashamba kama inavyoaminika na watu wengi Alifafanua kuwa nishati ya umeme ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuongeza kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote nchini vinapata huduma ya umeme na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi 
Alisema kuwepo kwa nishati ya uhakika vijijini kutapelekea wanavijiji kuanzisha viwanda vya kusaga na kukoboa nafaka, kilimo cha kisasa na kuongezeka kwa ufaulu darasani. 
Hata hivyo Profesa Muhongo alitoa agizo kwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha kuwa wananchi waliostahili kuunganishiwa umeme kupitia REA Awamu ya pili wanaunganishiwa kabla ya mwezi Oktoba mwishoni kwa gharama ya shilingi 27,000. 
Wakati huohuo Mbunge wa Handeni Vijijini, Mboni Mhita aliishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kasi kubwa ya usambazaji wa umeme vijijini na kuwataka wananchi wa jimbo lake kuchangamkia fursa hiyo.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akipokea zawadi  ya mbuzi kutoka kwa wakazi wa eneo la Kweditilibe wilayani Handeni mkoani Tanga

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika  kata ya Kwamgwe wilayani Handeni mkoani Tanga.

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea mikakati ya usambazaji wa umeme vijijini itakavyotekelezwa na  Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya  Tatu katika eneo la Kweditilibe wilayani Handeni mkoani Tanga

 Mkandarasi kutoka kampuni ya Future Century Limited  ya  Tanzania Hellen Masanja (kushoto) akielezea utekelezaji wa usambazaji wa umeme  katika jimbo la Handeni Vijijini mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) katika eneo la Kweditilibe wilayani Handeni mkoani Tanga. Profesa Muhongo  yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisikiliza maoni yaliyokuwa yanawasilishwa na mmoja  wa wakazi wa Kata ya Kamgwe wilayani Handeni mkoani Tanga. Kulia ni Mbunge wa Jimbo  la Handeni Vijijini, Mboni Mhita.

Top designer Sheria Ngowi will be streaming live his show tonight from 20:30

$
0
0

We will be streaming live our show tonight at 20:30Pm (CENTRAL AFRICAN TIME) and 21:30 PM (EAST AFRICAN TIME)
What You Need to Do?  
Follow these 4  easy Steps;

Step 1.
1.Go to App Store & Download- >Livestream App (Iphone Users)
Step 2.
2.Go to Play Store & Download- >Livestream App (Android Users)
Step 3.
>Then Search name SHERIA NGOWI
Step 4.

>Follow Us -Now Now.
To Watch Click Link Below:

ZAIDI YA WAVUVI TISA WALIOKUWA WAKIFANYA UVUVI MTO KAGERA WAFARIKI DUNIA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog 
ya jamii,Kagera Karlo,Kagera

ZAIDI ya wavuvi tisa waliokuwa wakifanya shughuli zao za uvuvi ndani ya mto Kagera wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa nyakati tofauti.
Akisoma taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchini Lameck Mwigulu Nchema,Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kanali mstaafu Shaabani Lissu alisema kuwa wavuvi hao wanatokea katika mialo ya Rubwela,Kanyika, Katwe na Ruko katika ziwa ngoma.
Alisema matukio hayo ya vifo vya utata yameanza kutokea kuanzia mwezi wa pili mwaka huu wakati wavuvi hao wanapoenda kuvua ndani ya mto Kagera unaotenganisha nchi ya Rwanda na Tanzania.
"Mara nyingi wavuvi wakienda kuvua ndani ya Mto Kagera huwa hawarudi,huwa wanatekwa na kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani ya Rwanda"Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Alisema hivi karibuni wavuvi wawili walienda kuvua ndani ya mto Kagera na mmoja aitwaye Emanuel Kahonda alipigwa risasi na kufariki dunia huku mwenzake Yoha Misago akinusurika katika tukio hilo na kukimbia na kwenda kutoa taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

"Mhe.Waziri ni juzi tu kuna mvuvi alipigwa risasi ndani ya mto Kagera hata msiba kwake bado upo, mwenzake aliyeshuhudia na kufanikiwa kuwatoroka wauaji hao yeye kunusurika ndiyo alikuja kutoa taarifa ofisini kwangu"alisema
Naye mwenyekiti wa mwalo wa Kitwe Ustadhi Hakimu alimthibitishia Waziri kuwa wavuvi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kuuwawa kikatili na askari wa nchi jirani ya Rwanda.
"Hapa kijijini kuna wajane wengi,waume zao walikuwa wakienda kuvua samaki ndani ya mto Kagera hawarudi,wanadai tunavua samaki kwenye maji yaliyopo nchi mwao,na mto kagera wameufanya wao peke yao,Tunaomba utusaidie Mhe.Waziri hili tatizo liishe
Upande wa kule kwao kuna misitu sana na huwa wanajificha humo,yaani wakikuona tu wala hawakusemeshi wanakupiga risasi tu humo humo majini,na maiti zimekuwa zikipotelea mtoni humo humo"alisema Mwenyekiti huyo.
Naye waziri wa mambo ya ndani ya nchini Mwigulu Nchemba aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyerwa kukutana na viongozi wa mialo ili wapate taarifa rasmi ya chanzo cha matukio hayo na kuipatia wizara ili waweze kutoa tamko rasmi juu ya mauaji hayo ya wavuvi.

"Hali hii imenistua sana,hatuwezi kuruhusu watanzania wenzetu wawe wanauwawa kikatili kiasi hiki,nikipata taarifa rasmi nitafuatilia jambo hili hata kwa kuwasiliana na wenzetu ili nijue kama ni msimamo wa serekali yao au ni uhalifu"alisema Nchemba.

Mwenyekiti wa wavuvi wa mwalo wa Kitwe akimuelezea waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba jinsi wavuvi wanavyouwawa katika mto Kagera  wanapoenda kuvua samaki.
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akiwa kwenye mmoja wa mtumbwi unaotumiwa na wavuvi wa mwalo wa Kitwe Mkoani Kagera

MBUNGE VITI MAALUM KAGERA ATOA ZAWADI MBALIMBALI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA KAGERA

$
0
0
Na Editha Karlo wa
Globu  ya jamii,Kagera.

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Kagera Oliver Semuguruka ametoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospita ya Mkoa wa Kagera.
Ametoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wanawake waliojifungua,watoto na wanawake wajawazito wanaosubiria kujifungua alisema kuwa akiwa kama kiongozi wa jamii anaguswa na masuala mbalimbali hasa yanayohusu wanawake.
"Mimi ni kiongozi wa jamii hasa wanawake,ninaguswa sana na matatizo ya wanawake wenzangu siyo wa hapa Kagera tu wanawake wa Tanzania nzima leo nimekuja kuwapa pole na nimewaletea zawadi za sabuni za kufulia,kuogea,juisi na biscuti "alisema Mbunge huyo

Akizungumzia zawadi hizo Ofisa muuguzi msaidizi wa zamu wa wodi ya wazazi Evelyne Lugabandana alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada alitoa kwa wagonjwa.
"Tunamshukuru mbunge wetu kwa moyo wake wa upendo wa kuwakumbuka wanawake wenzake na watoto na kuamua kuja kuwapa pole na kuwapatia zawadi pia"alisema Muuguzi huyo
Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye wodi hizo ambazo Mbunge ametoa zawadi walimshukuru mbunge kwa zawadi na kumtaka awasaidie kutatua kero waliyonayo ya kulala wawili kitanda kimoja na kwenda na vifaa vya kujifungulia.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Oliver Semuguruka akisikiliza maelezo kutoka kwa ofisa muuguzi wa wodi ya wazazi Mkoa wa kagera kabla hajatoa zawadi kwa wodi hiyo. 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Oliver Semuguruka akiwa amembeba mmoja wa watoto aliyezaliwa kwenye hospital ta Mkoa wa Kagera alipoenda kuwasalimia na kuwapatia zawadi. 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera akiwa na wajumbe wa umoja wa UWT Mkoa wa Kagera wakiwa nje ya wodi ya wazazi kabla ya kwenda kutoa zawadi kwao

YANGA YASHTUKIA MCHEZO KARIBIA KUNAKUCHA, YAILAZA MO BEJAIA BAO 1-0 TAIFA LEO

$
0
0
TIMU ya Yanga yenye makao yake Mtaa wa Twiga na Jangwani leo imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kupata goli 1-0 lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Amisi Tambwe dakika ya tatu ya mchezo dhidi ya Timu ya Mo Bejaia ya nchini Algeria, mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.

Akizungumza baada ya kupata ushindi huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm amesema ushindi huu umempa nguvu katika kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe.

Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana na wameweza kulinda goli katika dakika zote ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya. 
 Naye Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wanatoka ushindi na wamecheza timu nzuri sana yenye uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia wachezaji wenzake kwa jitihada walizozifanya.

Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama ukitarajiw kuchezwa kesho nchini Ghana. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Obren Chirwa akiwa katikati ya Mabeki wa Timu ya Mo Bejaia.
 Washabiki wa Timu ya Yanga wakiishangilia timu yao baada ya kupata ushingi dhidi ya Timu ya Mo Bejaia ya Algeria, katika Mechi ya Kombe la Shirikisho iliyopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda Bao 1-0.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atoa Tamko la Tathmini ya Jumuiya ya Madola la Uchaguzi Mkuu wa Zambia

$
0
0
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa tamko la Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola  la Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya, Madiwani na Kura ya Maoni ya Katiba. 
Rais Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.
Kwa mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa chaguzi. Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.
Amewapongeza wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa amani na kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. Amewasihi viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa kuheshimu maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote kutoridhika na matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta ufumbuzi.

TANZANIA YANDELEA KUTESA MASHINDANO YA MAJESHI AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Na Selemani Semunyu JWTZ 

Timu ya Mpira wa Pete ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imedhihirisha Ubabe wake katika mchezo huo baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Rwanda RDF kwa Magoli 56-13 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na Timu zote tangu kuanza Mashindano hayo. 

Tangu Mwanzo wa Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Rwanda walionekana kuzidiwa na kiwango kilichoonyeshwa na Tanzania kupitia Nyota wake Mwanaidi Hassan aliyefunga 37 na Nasra Suleiman aliyefunga 19 waliokuwa mwiba kwa Timu ya Rwanda kutokana na kupachika magoli kila wapatapo mpira. 

Tanzania iliweza kumiliki vipindi vyote vine vya mchezo huku Rwanda wakionekana kutoelewana kutokana na idadi ya magoli waliokuwa wakifungwa tangu Robo ya Kwanza mbayo ilimalizika kwa Tanzania kuongoza kwa 13-2 huku Robo ya pili 32-6 na Robo ya tatu 42-10.
Kwa upande wake Mchezaji Nasra Suleiman alisema mbali na kupata ushindi huo lakini hawatobweteka kwani wanawasubiri Kenya ili kutangaza Ubingwa kwa kushinda Michezo yote. 

Kwa upande mwingine Tim u ya Mpira wa Miguu ya Tanzania wameinyamazisha Timu ya Jeshi ya Kenya baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kigali Nyamirambo.
Katika Mchezo huo Kenya Ndio walianza kupata bao Muda mchache kabla kwenda mapumziko katika Dakika ya 42 kupitia kwa mchezaji wake Private Peter Onyango kabla ya Dakika tatu Baadae Private Prosper Mkwama kusawazisha bao na kwenda mapumziko wakiwa Sare.; 

Kipindi cha Pili kilianza huku Timu zote zikifanya mabadiliko na kosa kosa ya magoli kwa Nyakati tofauti lakini Mnamo dakika ya 77 Private Abdulrahman Musa akaiandikia Tanzania bao la Pili na la ushindi.
Kufuiatia matokeo hayo sasa Tanzania wamebakiza Mchezo mmoja na Rwanda utakaopigwa siku ya ufungaji Agosti 17 katika Uwanja wa Amahoro huku Timu ya mpira wa Pete wanatarajia kukutana na Kenya Agosti 14. 
 
Mlinzi wa Timu ya Mpira wa Pete wa Tanzania Joyce Kaira (GK) akiwa katika hekaheka za kuzuia Wachezaji wa Rwanda Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13
Kocha wa Timu ya Tanzania kwa Mpira wa Pete Argentina Daudi akitoa maelekezo kwa Wachezaji wake katika muda wa mapunziko katika mchezo baina yao na Rwanda uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali ambapo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
Nyota Chipukizi wa Mpira wa Pete wa Tanzania Nasra Suleiman ( Mwenye Mpira)akiwa katika hekaheka za kuisaidia Timu yake kupata Ushindi katika  mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13 

Kikao cha baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo

$
0
0
 MKURUGENZI wa  Halmashauri ya  wilaya ya Namtumbo Bw. Christopher  Kilungu (kushoto)  akiongoza baraza la madiwani kulipitia kabrasha la  kikao hicho. 
Kikao hicho cha baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  kilimkataa kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa  walimu (TSC)  Boniphace Fungo na kutoa onyo kwa watumishi wawili - Mkuu wa  idara ya kilimo Ally Lugendo na mkuu wa idara ya Ujenzi  David Mwanapemba - na pia kilimuagiza Mkurugenzi wa  Halmashauri hiyo kuwachukulia hatua ya kinidhamu Mkuu wa  idara ya fedha Clodwick Mapunda na Mkuu wa idara ya Manunuzi  kwa  utendaji usioridhisha kwenye idara zao

 Kikao cha baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kikiendelea

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo wakiwa kwenye kikao cha baraza

RC MAKONDA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA, AELEZA VIPAUMBELE VYA MKOA WAKE NA KUAHIDI KUSIMAMIA SHERIA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhani Madabida.

Wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam wakifuatilia kikao cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema, akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hamphrey Polepole na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi.

 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita akizungumza na wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MBUNGE ULEGA AWATAKA WANANCHI WA KIJIJI CHA MWALUSEMBE KUILINDA MIUNDOMBINU YA KISIMA IKIWAMO SOLAR

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amezindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ,ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation
 
Mara baada ya uzinduzi huo,Mh. Ulega aliwashukuru wafadhili hao na kuwaomba kuendelea kusaidia wilaya hiyo ili kukabiliana na uhaba wa Maji uliopo na kuwa Wilaya ya Mkuranga ni moja ya maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya Maji.
 

Mh.Ulega Pia aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia Maji hayo vizuri ikiwa pamoja na kulinda miundombinu yake ikiwamo solar na vinginevyo ili visiibiwe,Mh Ulega tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa jimbo hilo tayari ameshachimba visima katika vijiji zaidi ya vitano huku akisaidia kutatua mbalimbali ya wananchi ambayo yamekuwa kero kwao.

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwalusembe kweye hafla ya uziduzi wa kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe, ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani. 
.Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.

Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwasil katika kijiji cha Mwalusembe kwa ajili ya kuziduzi kisima cha Maji ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo mkoani Mpwani.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

Zaidi ya Shilingi Bilioni 7.56 zimepatikana katika mnada wa madini ya Tanzanite, Serikali yakusanya mrabaha wa zaidi ya milioni 331.

$
0
0
Na Zuena Msuya Arusha
Serikali imekusanya mrabaha wa zaidi ya shilingi milioni 331  katika mnada wa madini ya Tanzanite yaliouzwa kwa  zaidi ya shilingi bilioni 7.56 kutoka kampuni  mbili za uchimbaji madini hayo katika eneo la Mirerani mkoani Manyara.
Akitangaza  washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, Mkurugenzi wa kitengo uthaminishaji Almas na madini ya vito(TANSORT), Ardhard Kalugendo alisema kuwa katika mnada huo kampuni tano zilijitokeza, mbili kati ya hizo ziliuza madini yake kwa wanunuzi mbalimbali; Kampuni tatu hazikuweza kuuza kutokana na kutokubalina bei na wanunuzi.
Kalugendo alifafanua kuwa mnada huo ulifanyika kwa njia ya uwazi na kushirikisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera alisema kuwa mnada huo umeiwezesha Serikali kupata mrabaha pamoja na kuzuia utoroswaji wa madini hayo nje ya nchi uliokuwa ukiikosesha Serikali mapato yake kwa maendeleo ya taifa.

Katika hatua nyingine Bendera aliwatoa hofu wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika migodi ya Mirerani mkoani Manyara kuwa kwa Serikali imeimarisha ulinzi kwa usalama pamoja na mali zao; Pia wafanyabiara wa Tanzanite watoe ushirikiano kwa vyombo vya usalama pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

Aidha aliwasihi wanunuzi na wachimbaji wa Tanzanite kufuata sheria na taratibu za uchimbaji na ununuzi ili kuhakikisha kuwa madini hayo adhimu yanayopatikana nchini tanzania pekee duniani yanawanufaisha watanzania wote.

Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe alisema kuwa pamoja na manufaa yaliopatikana katika mnada huo, Serikali itaendelea kuboresha mnada huo kwa kuongeza muda zaidi ili kutoa fursa kwa kila  mfanyabiasha wa Tanzanite kushiriki; Vilevile  kuwepo na majadiliano zaidi kati ya wauzaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Profesa Mdoe aliongeza kuwa lengo la Serikali katika mnada huo ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite kupata matokeo chanya  na yenye tija katika shughuli zao, pia Taifa linufaike kutokana na matokeo hayo kwa njia mbalimbali.

Mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Tanzanite, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzaniteone Faisal Shuhbhai aliipongeza Serikali kwa kuweka utaratibu huo ambao ni  wa kwanza kufanyika nchini kwakuwa utawawezesha wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Faisal alisema kuwa utaratibu wa mnada utawawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite waliokuwa wakikwepa kodi, kulipa mirabaha kwa wakati baada ya kuwepo kwa mpango huo ambao haukuwepo hapo awali; Aidha utawasaidia wafanyabiara kupata bei elekezi inayoendana na soko la dunia na hivyo kuacha kutorosha  madini ya Tanzanite nje ya Tanzania kwa madai ya kutafuta masoko.

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera( aliyesimama)akihutubia  wakati wa kumtangaza mshindi wa zabuni ya kununua madini ya Tanzanite, katika mnada wa madini hayo uliofanyika mkoani Arusha. Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini  Profesa James Mdoe(wa pili kushoto),  Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito, Archard Kalugendo( kulia) na Kamishna Msaidizi wa Madini, Salim Salim( kushoto)

 Baadhi ya wauzaji na wanunuzi na madini ya Tanzanite walioshiriki katika mnada,Mkurugenzi wa Kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shahbhai,(kulia) Hussein Gonga( wa pili kulia) mchimbaji, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VGL Group ,Sunil Agrawal( wa pili kushoto), na Mmoja wa Wakurugezi wa Kampuni ya TanzaniaOne, Rizwan Ullah  ( kushoto)

 Mkurugenzi wa kitengo cha uthaminishaji Almasi na madini ya vito,Archard Kalugendo( kulia)akitangaza washindi wa zabuni za kununua madini ya Tanzanite,mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera( wa pili kulia) Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia madini wa Wizara ya Nishati na Madini  Profesa James Mdoe(wa pili kushoto).

Mhandisi Juma Lunda( kulia)akitoa bahasha katika sanduku maalum la kuhifadhia maombi ya zabuni za kununua madini ya Tanzanite katika mnada. 

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe,( kushoto) akishuhudia uchambuaji wa barua za maombi ya zabuni ya kununua madini ya Tanzanite wakati wa mnada.

Kambi tiba ya GSM yaokoa maisha ya watoto 12 jijini Mbeya, kuanza kazi Jumanne Iringa

$
0
0
 Na Mwandishi Wetu
Jumla ya watoto 30 wamehudhuria Kambi tiba ya GSM jijini Mbeya ambayo inaelekea katika kumaliza msimu wake wa pili, huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha vifo vya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi nchini, huku lengo kuu likiwa ni kutibia angalau watoto 400 katika kambi hiyo inayozunguka nchi nzima huku ikiwa imeshapita mikoa nane mpaka sasa.
Mkuu wa kambi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya MOI, Dk Othman Kiloloma, aliyeambatana na madaktari wenzake 10 wanaoshiriki kambi tiba hiyo amesema, tofauti na awamu ya kwanza, safari hii muitikio haukuwa mkubwa kutokana na sababu mbali mbali za kiutendaji lakini kubwa likiwa ni taarifa kuchelewa kuwafikia wananchi.
Dk Othman amesema kati ya watoto hao 30 waliohudhuria kambi tiba, 12 wamefanyiwa upasuaji, ambayo ndiyo tiba pekee inayotumika kuokoa maisha ya watoto waliokumbwa na ugonjwa wa vichwa vikubwa na mgongo wazi, huku wengine watatu wakihamishiwa katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Muhimbili, na wengine 15 wakipatiwa ushauri baada ya kugundulika kuwa umri wao hauruhusu kufanyiwa upasuaji huo.
Umri sahihi wa kuokoa maisha ya mtoto anayezaliwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi ni chini ya miaka mitano, ambaye bado fuvu la kichwa chake linakuwa bado halijakomaa na hivyo kumrahisisha mtoa tiba kupunguza maji yanayojaa kichwani kwa urahisi.
PICHANI JUU: Madaktari walioendesha zoezi la kuona watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi jijini Mbeya wakifurahia jambo wakati zoezi likiendelea, kutoka Kushoto ni Daktari Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dk  Lazaro Mboma, Daktari Bingwa wa Upasuaji ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kambi Tiba hii Hamis Shaaban,  Dk Benedict Austard, MwanaAbbas Sued, John Mtei na Siah Richard kutoka Taasisi ya Upasuaji na Mifupa MOI 


COMFORT ZONE WATOA MSAADA KWA YATIMA WA KITUO CHA HUSENE MJINI DODOMA

$
0
0


Baadhi ya wanachama wa Comfort Zone waliopo Dodoma wakitoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Hasene kilichopo eneo la Chang'ombe wilaya ya Dodoma mjini.

Misaada iliyotolewa ni vitu mbalimbali ikiwemo mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wajenzi wa madarasa na bweni la kulala watoto.
Wanachama wa Comfort Zone wakiwa wamebeba baadhi ya Misaada kabla ya kuikabidhi kwa Watoto yatima wa kituo cha Hasene kilichopo eneo la Chang'ombe wilaya ya Dodoma Mjini.
Wanachama wa Comfort Zone wakiwa wameketi na Watoto yatima Baada ya Kuwakabidhi Misaada mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia.

MKUU WA MKOA RUVUMA AZINDUA KAMPENI YA UFYATUAJI TOFALI MADABA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge(aliyevaa kofia) akiwa na mbunge wa Madaba Joseph Mhagama wakiwa kwenye zoezi la ufyatuaji tofali kwenye kijiji cha Magingo kata ya Mkongotema
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akishiriki kazi ya ufyatuaji tofali ikiwa ni kampeni ya Mkoa kuwezesha kupata benki ya tofali kwenye halmashauri ya wilaya ya Madaba leo.Jumla ya tofali 430,000 zimelengwa kufyatualiwa kijiji cha Magingo sasa zipo tofali 150,000
 Wananchi wa kijiji cha Magingo wilaya ya Songea wakishiriki kazi ya ufyatuaji matofali
 Sehemu ya matofali yaliyofyatuliwa na wanakijiji wa Magingo kata ya Mkongotema wilaya ya Songea
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge akikagua mradi wa maji wa kijiji cha Mkongotema unaohudumia wananchi wapatao 9,500.

Kilele Cha Maadhimisho ya Miaka Mitano Tangu Kuanzishwa Kwa Shule ya Little Treasures

$
0
0
Wanafunzi wa darasa la watoto (Baby Class) wakitoa burudani ya wimbo 
Wanafunzi wa shule ya awali daraja la pili (Middle Classa) wakiimba wimbo
Wanafunzi wakiwa eneo la tukio

Wanafunzi wa Middle Class wakitoa burudani ya wimbo.
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live




Latest Images