Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

NENO KUTOKA KWA ERIC SHIGONGO

$
0
0

"Kosea njia utaelekezwa, lakini usikosee mtu wa kukuoa au kuolewa naye, vinginevyo majuto yatakuwa sehemu ya maisha yako. Tuliza kichwa unapochagua mwenzi wa maisha." 
ERIC SHIGONGO.

MAADHIMISHO YA SIKU YA NDEGE WAHAMAO DUNIANI TAREHE 11 – 12 MEI 2013

$
0
0

Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Ardhioevu ambayo ni makazi na mapito ya ndege wahamao kushirikiana na Serikali katika kuwalinda ndege hao na kuhifadhi mapito na makazi yao. Wananchi pia wanakumbushwa kuwa maeneo ya ardhioevu ndio vyanzo vya maji ambayo yanafaa kwa matumizi ya kila siku ya binadamu, wanyama na ndege, hivyo maeneo hayo yalindwe.
Taarifa hii imetolewa na Wizara wakati huu wa maadhimisho ya Siku ya Ndege Wahamao Duniani ambayo huadhimishwa kimataifa tarehe 11 na 12 Mei kila mwaka.

Aina za ndege hao ni kama vile Heroe mkubwa na mdogo (flamingos) ambao wanahama kila mwaka kutoka sehemu moja ya dunia kwenda nyingine kutafuta malisho, maji, kukwepa hali mbaya ya hewa na kupata sehemu salama ya kuzaliana.

Tanzania ni nchi mojawapo yenye sehemu nyingi ambazo ni salama kwa mazalia ya ndege. Kwa mfano, Ziwa Natron ni maarufu kwa mazalia ya ndeye aitwaye Heroe mdogo. Inakadiriwa kuwa asilimia 80 ya Heroe mdogo kote duniani huzalia katika Ziwa Natron liliko Kaskazi mwa Tanzania.   Ziwa hilo ni kivutio cha utalii kutokana na ndege hao.

Maadhimisho ya Siku ya Ndege Wahamao Duniani yalianza mwaka 2006 na kuendelea kusherehekewa kila mwaka mwishoni mwa wiki ya pili ya kila mwezi Mei.  Watu duniani kote huitumia fursa hii kutoa elimu na kufanya matembezi katika sehemu zenye Ndege hawa  kwa ajili ya kusherehekea siku hii.

Ujumbe wa mwaka huu wa Siku ya Ndege Wahamao ni: "Tuunganishe juhudi zetu katika kuwahifadhi ndege wahamao mapito na makazi yao (Networking for migratory birds), ". Tafsiri ya ujumbe huu ni kuwa nchi, mashirika na watu binafsi wanatakiwa kuunganisha maeneo ya ardhioevu kwa ajili ya uhifadhi endelevu wa ndege wahamao.

Utunzaji kwa ndenge wahamao ni sababu mojawapo iliyofanya Tanzania kusaini Mkataba wa Uhifadhi wa Ardhioevu (Ramsar) mwaka 2000. Ardhioevu, pamoja na maufaa mengine,  ni makazi ya ndege wahamao.

Kutokana na Mkataba huo Tanzania imetenga maeneo ya Ramsar ambayo ni muhimu katika kuhifadhi bioanuwai. Maeneo ya ardhioevu yaliyotengwa ni pamoja na Ardhioevu zenye umuhimu wa kimataifa kama vile:- Malagarasi-Muyovozi ambayo ni muhimu kwa uhifadhi wa ndege aina ya Korongo domokiatu (Shoebill stork), na eneo la Ramsar la Ziwa Natron ambalo ni muhimu katika kuhifadhi  ndege aina ya Heroe mdogo (lesser flamingo) .

Serikali imekuwa ikiwajengea wananchi uwezo wa kuhifadhi na kutumia rasilimali za ardhioevu nchini kwa kutoa elimu ya uhifadhi katika maeneo yanayozunguka maeneo ya Ramsa. Maeneo hayo ambayo ni makazi muhimu ya ndege wahamao yanasimamiwa na Sheria ya Kuhifadhi Mazingira ya mwaka 2004 na ya Kuhifadhi Wanyamapori ya Mwaka 2009. 

George Matiko

MSEMAJI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

11 Mei 2013

DKT SHEIN AKUTANA NA BALOZI MPYA WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU NCHINI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania Abdulla Ibrahim AL-Suwaidi,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza  na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania Abdulla Ibrahim AL-Suwaidi,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania Abdulla Ibrahim AL-Suwaidi,baada ya mazungumzo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Flaviana matata katika mkasi na salama jabir palepale amaya

Clouds Media Group yazindua msimu wake mpya kwa kishindo mjini Dodoma leo,yafanya semina dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na  harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa.  Aidha pia mchana huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika uwanja wa jamhuri .
 Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la   Patrick Ngowi  kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo.
 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwa kuhusiana na mambo mbalimbali ya ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo katika kujikwamua kimaisha.
 Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia.

Mtangazaji wa clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast-Gerald Hando akiikaribisha Meza kuu pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds Media Group unaokwenda sambamba na ujumbe wao thabiti kabisa  ulioitwa MADE IN TANZANIA,ikiwa na hamasa kubwa ya kuleta msingi wa fursa kwa watanzania, msukumo ikiwa ni kuwashawishi watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizi kwa umoja na maendeleo ambapo TWENZETU, inakuwa neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa  ikiwemo semina ya fursa kwa watanzania,burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania zitapatikana uwanja wa jamhuri mapema leo mchana.
Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zenno  Ngowi kutoka kampuni ya Tanzania Home Expo akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ardhi,ujenzi,na mengineyo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye semina hiyo leo mjini Dodoma.


Mmoja wa wasanii mahiri wa Mashairi,Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusiana na mambo mbalimbali katika suala zima la wasanii kujipa nafasi ya Fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao na namna ya kuzifanyia kazi na kuziboresha zaidi.
Mhe Zitto Kabwe akiwasili kwenye ukumbini mapema leo kwenye hoteli ya African Dreams mjini Dodoma,Mh Zitto pia alikuwa ni mmoja wa wasemaji wa semina hiyo.
Pichani ni washiriki wa semina hiyo kutoka sehemu mbalimbali mjini Dodoma leo. PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

WAZIRI MKUU PINDA AFANYA UZINDUZI WA MAABARA YA ELEKTRONIKI JIJINI ARUSHA JANA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua akizindua mpango wa maktaba ya dijitali kwenye shule ya msingi ya Nganana wilayani Arumeru May 10,2013. Wengine pichani kutyoka kushoto ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinoloji, Profesa Makame Mbarawa, Mbunge wa Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia cha Mandela, Bulton Mwamila na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nganana , Samweli Paanjo.
Wanafunzi wa Shule ya Misingi ya NGanana wilayani Arumeru wakionyesha kifaa cha elektrononiki kiitwa Electroni Reader che uwezo wa kuhifadhi vitabu zaidi ya 2000 kila kimoja katika uzinduzi wa Maktaba ya Elektroniki uliofnywa na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda kwenye shule ya Misngi ya Nganana., May 10, 2013.
Baadhi ya washiriki wa sherehe za uzinduziwa maktaba ya elektroniki kwa shule za msingi uliofanyika kwenye shule ya Msingi ya Nganana May 10, 2013. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo pinda.(Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu).

WANANCHI MAKETE MJINI WAOMBA VIFUSI KWENYE BARABARA ZA MITAA VISAMBAZWE

$
0
0

Moja ya barabara za mitaa kata ya Iwawa Makete mjini zikiwa zimelundikwa vifusi kwa zaidi ya miezi mitatu sasa huku kukiwa na kibao kikionesha barabara imefungwa ilihali magari yanapita hivyohivyo licha ya maelekezo ya kibao hicho(Habari/picha na Edwin Moshi)
Vifusi vikiwa vimelundikwa barabara ya kuelekea hospitali ya wilaya ya Makete 
Hapa inalazimu magari kupita kwenye mifereji
 Vifusi vingine hadi vimeyeyuka kutokana na kukaa muda mrefu
Wananchi wa kata ya Iwawa wilayani Makete ambao ni watumiaji wakubwa wa barabara za mitaa katika kata hiyo, wameiomba halmashauri ya wilaya ya Makete kusambaza vifusi vilivyopo katika barabara hizo ambavyo vimewekwa zaidi ya miezi mitatu sasa

Wananchi hao wametoa ombi hilo kufuatia adha wanayoipata hasa wanapotumia magari kwa kuwa barabara hizo zimekuwa nyembamba hivyo kuleta usumbufu kwa watumiaji hasa wakati wa magari kupishana


Mmoja wa mwananchi aliyezungumza na ripota wetu Bw. Sipati Mbwilo amesema wanashangaa vifusi hivyo kukaa muda mrefu barabarani bila kusambazwa, jambo linalosababisha usumbufu kwa watumiaji na wakati mwingine kulazimika kuzunguka kupita kwenye barabara nyingine ili kufuata huduma hata kama huduma hiyo ipo jirani

“Unajua braza unaweza kukuta umepata kazi ya kupeleka kuni ama kwenda kuchukua kuni kwa gari, lakini inakulazimu uzunguke umbali mrefu ili kukwepa hivi vifusi ambavyo hatujui vitasambazwa lini, ni bora wangeviweka pindi watakapokuwa tayari kuvisambaza leo mwezi wa tatu vifusi vipo barabarani mambo gani haya” alisema Mbwilo

Naye dereva wa lori aliyejitaja kwa jina la Kisauti amesema vifusi hivyo vinawapa tabu wanaoendesha magari makubwa kutokana na wembamba wa barabara na wakati mwingine kulazimika kukataa baadhi ya kazi wanazozipata kutokana na magari yao kushindwa kupita kwenye barabara hizo

Ripota wetu amezungumza na mhandisi wa ujenzi wilaya ya Makete Mhandisi Samwel Ndoveni ambaye amekiri kuwepo hali hiyo lakini amesema kero hiyo itaondolewa hivi karibuni kwa kuwa msimu wa mvua uliokuwa ukikwamisha utekelezaji wa zoezi hilo unamalizika na mkandarasi ataanza kazi mara moja

Amesema kwa mwaka huu mvua zilinyesha kwa wingi na ndiyo maana zoezi hilo lilishindwa kutekelezeka kwa wakati kama ofisi yake ilivyokuwa imepanga

“Ni heri lawama za kutokusambaza vifusi zitupate kuliko tungesambaza vifusi wakati mvua inanyesha, matokeo yake tungetengeneza tope jingi na barabara zisingepitika huo ungekuwa ni uharibifu wa fedha za serikali” alisema Mhandisi Ndoveni

BEST Air and Sea Freight solutions from UK

$
0
0

Swift freights UK Ltd. Offers Air and Sea Freight solutions from UK and other countries to all destinations around the world. We ship commercial and domestic goods, vehicles and  any size of freight from a pin to a ship.


For Air service WE OFFER:

·        Door-2-Door* service by air for smaller parcels to DAR or ZanzibarDoor-2-Door* service- from our office in London, to our office in Dar-Es-Salaam. We offer collection from other cities in Uk and delivery to Mwanza and Arusha or other cities in Tanzania at an extra charge.

                     Cargo leaves our office on Wednesdays and arrives within seven days.


·        Express parcels can be booked to collect from any address

·        For bigger consignments we can offer bargain rates for airport-2-airport service.


Special SEPTEMBER offers for shipping vehicles with RoRo service:

Saloon cars to Dar-Es-Salaam and Mombasa £750

4x4(SUVs) to Dar-Es-Salaam and Mombasa £850

High and Heavyto Dar-Es-Salaam and Mombasa rates based on dimensions


For Trucks rates depend on the size of the vehicle and are available on request.

For Tractor units rates from £2200


For Sea/Container service WE OFFER:

·        20 foot Containers Dar/Mombasa from £1,400

·         40 foot Containers Dar/Mombasa from £1,950

·        40 foot Containers to Boma, DRC –from £4,600

Door-2-Port* service rates given are for straight load, container on the trailer service. The price may vary depending on loading location.


For Sea freight Partial Load(LCL) service WE OFFER:

·        Partial loads by sea also available to any destination. Minimum booking volume is 1 cubic meter (cbm)£145 per cbm for Dar-Es-Salaam. This is 35 days service.


We also offer for you:

Collection from any UK mainland address

Air and See freight insurance

Full packing facilities

Vehicle pre-shipment inspection services for Kenya

For more information please call us Today: Office :(+44)208 801 9800  or Mobile:(+44)7852260024


OFL Ltd our Tanzania partners can facilitate ordering of vehicles, tractors, trailers and other items from the UK contact OFL on 0222666967 Monday to Friday 08:00 to 17:00hrs at Sida Flats,Madai Crescent in Ada Estate


Visit us: Unit 6, Tudorleaf Business Centre,2-8 Fountayne Road ,London N15 4QL , Please visit our website: www.swiftfreightsuk.com


Office hours are Monday to Friday 09:00-17:00hrs


Balozi Seif Ali Iddi afungua Kiwanda cha maji ya Kunywa cha Super Shine Mjini Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria kukifungua rasmi Kiwanda cha maji ya Kunywa cha Super Shine Kinachomilikiwa na Kampuni ya Safari yenye Makao Makuu yake Nchini India.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayesimamia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee akiwa na akiambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kukagua baadhi ya sehemu ya KiwandaKipya cha Maji ya kunywa kiliopo maeneo ya Viwanda Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia baadhi ya mashine za Kiwanda cha maji ya kunywa kiliopo maeneo huru ya Viwanda yaliopo Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia moja ya sampuli ya chupa ya maji yenye ujazo wa nusu lita ambayo tayari imeshakamilika utayarishaji wake katika kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo Maeneo huru Amani.
wasanii wa Kikundi cha sanaa Zanzibar wakitoa burdani safi katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo amani maeneo huru ya viwanda.
Balozi Seif akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wakishangiria moja ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na kikundi cha sanaa kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo maeneo huru ya Viwanda Amani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa hapo maeneo huru amani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari inayomiliki kiwanda cha maji ya kunywa cha Super Shine kiliopo amani maeneo huru na Bibi Mala Kalwan mara baada ya uzinduzi wa kiwanda hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na wale wa Kampuni ya Safari inayomiliki Kiwanda cha maji ya kunywa hapo amani eneo huru la Viwanda.

Article 8

Mkapa tells EU to ensure Economic partnership do not threaten development aspirations of Africa.

$
0
0



Retired President Benjamin William Mkapa (pictured above) has argued Inter Action Council European members to press on their governments to ensure that the Economic Partnership Agreements (EPAs) they are negotiating with African countries do not threaten the development aspirations of Africa.
 
Participating in the debate on the economic situation in the present state of the world in Manama, the Kingdom of Bahrain, President Mkapa said the European Union (EU) proposals seriously impede the development path of the African countries. In particular, they would lead to the de-industrialization, stop the value addition on their primary goods exports and deny them market success, while by insisting on removal of import tariffs and export taxes, deny government revenue for effective fair governance.
 
He pointed out that the EU – EPA proposals placed production risks for locally produced products at 51.3% in East African Community countries, 54.1% in ECOWAS countries and 80.5% in SADC countries.
 
Weighing gains against cost of signing the EPAs for Sub – Saharan African countries, he said under the most favoured nation clause (MFN), the countries would gain annually $ 946 million on average against costs of $ 3,385 million.  In every instance he affirmed, the cost of EPA is higher than the benefit.
 
He told the Council that African countries had been given the deadline of January 2014 to sign. The underlining principle of this deadline and the proposals is the principle of equal undifferentiated responsibilities, and the imperative of reciprocity. Additionally, the EU has now come up with new issues for reciprocal action including; services, investment, intellectual property, labour and environment.
 
In the Final Communiqué, the Council asks: “The international community to recognize the centrality of the African Union on issues of African development and to encourage regional economic integration. Trade with investment is the most important factor to states seeking to reduce poverty and improve living standard of their people.”
 
“The IAC calls on entities negotiating new economic partnerships, such as the EU and other development partners, to ensure market access for African exports consistent with the realization of the Millennium Development Goals and promotion of an agreed post 2015 agenda”.
 
The InterAction Council (IAC) is an independent international organization comprising more than 30 former heads of state or government. It aims to foster international cooperation and action in areas of peace and security, revitalization of the world economy and the nexus of development, population and environment and universal ethics.
 
The Council is co- chaired by former Canadian Premier Jean Chretien and Dr. Franz Vranitzky, former Chancellor of Austria.

Redd’s Miss IFM kumekucha

$
0
0
Meneja wa Kinywaji cha Redd's Victoria Kimaro katikati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaa juu ya maandalizi ya shindano la Redd's Miss IFM 2013.
Mratibu wa Redd’s Miss IFM, Daniel Sarungi katika akizungumza na waandishi wa Habari jijini dar es salaam juu ya shindano la Redd's IFM linalotarajiwa kufanyika May 25,2013, kulia ni meneja wa Kinywaji cha Redd's Victoria Kimaro.
Warembo wa Redd’s Miss IFM wakiwa katika picha ya pamoja.

wadau wa japani wajiandaa na mkutano wa tano wa kimataifa wa maendeleo ya Africa

$
0
0
 Baadhi ya Watanzania waishio nchini Japani wakionyesha mavazi yavaliwayo Tanzania, katika maonyesho ya mavazi jijini Yokohama ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mkutano wa tano wa kimataifa wa maendeleo ya Africa (TICAD V) utakaofanyika katika jiji hilo juni 1 – 3 mwaka huu.
Banda la vyakula vya kitanzania katika maonyesho ya African Festival jijini Yokohama. Sambuza, bagia, mandazi, ugali na pilau vilikuwepo na vilichangamkiwa na wajapani

RAIS KIKWETE AREJEA TOKA AFRIKA KUSINI LEO

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymon Moshi mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 11, 2013 akitokea Cape Town, Afrika ya Kusini, alikohudhuria mkutano wa nchi SADC.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali (kulia) mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 11, 2013 akitokea Cape Town, Afrika ya Kusini, alikohudhuria mkutano wa nchi SADC. PICHA NA IKULU

wakazi wa dodoma waupokea kwa kishindo msimu mpya wa clouds Fm,wamiminika uwanja wa jamuhuri kushuhudia live.

$
0
0
 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.

Aidha msimu huo umekwenda sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.
 Msanii mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
 Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua msimu wake mpya.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya watu.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.

msaada tutani

Da' Aisha Mkassi ala nondozzz ya MBA kutoka chuo kikuu cha Wales

$
0
0
Da' Aisha ambae anaishi mji wa kusoma (yaani Reading) nchini UK, amelamba nondozzz ya pili ya business administration wiki iliyopita, na kuamua kusheherekea na ndugu pamoja na marafiki zake kwa juhudi na mfano mkubwa aliouonyesha kwa watanzania wengine, na wanawake kwa ujumla. Hongera sana dada Aisha Mkassi, kwa kutudhihirishia watu tulioko ughaibuni kwamba, tusikazane na kubeba maboxi tu bali pia tukumbuke kilichotuleta huku ughaibuni. Mungu akubariki na akupe maisha bora zaidi Da'Aisha..
Da' Aisha na Shangazi yake pamoja na rafiki yake Kubra
Da' Aisha na shangazi yake baada ya kulamba nondozzz ya  MBA
Da' Aisha akila pozi baada ya kulamba nondozzzz yake ya Master ya Business Administration

Susan G Komem May 11, 2013

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Sikia ngoma na sauti ya Paul Ndunguru na Bendi ya Wahapahapa  wakikupa 'Naisaliti Nafsi'

Vodacom yaungana na UN wiki ya nenda kwa usalama

$
0
0
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu huyo katika kutoa elimu kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea,anaeshuhudia kulia ni Meneja uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
Mkuu wa kitengo cha huduma za mtandao Vodacom Tanzania Bw.Andrew Lupembe,akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga katika kutoa elimu kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Bi.Ena Mwangama,akimkabidhi kitabu cha sayansi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa vodacom Tanzania,walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya Usalama Barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza Mei 6 hadi 12.kila mwaka.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania , wakiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Mapambano ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapa msaada wa vitambu vya sayansi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) kutoa elimu kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
Meneja wa Vodacom anaye husika na masuala ya elimu Grece Lyon akimkabidhi mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Uzuri Tandale jijini Dar es Salaam, Vitabu vya Sayansi wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini).
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Rukia Mtingwa akiwaongoza wanafunzi wa shule ya msingi ya Uzuri iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwenda kujifunza jinsi ya kutumia alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,kila mwaka .Wafanyakazi wa Vodacom waliambatana na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) Pia walitoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vitabu vya Sayansi.
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images