Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1317 | 1318 | (Page 1319) | 1320 | 1321 | .... | 3272 | newer

  0 0


  MFUKO wa Pensehni wa PSPF, umeendelea kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS, wakati wa Maonyesho ya taasisi na makampuni ya kutoa huduma yaliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mikononi, Airtel na kwenda na jina la Airtel Bazzar na kufanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco jijini Dar es Salaam, Agosti 12, 2016.

  Akizungumza na waandishi wanhabari kwenye banda la Mfuko huo, Mkuu wa Kitengo cha Usajili nwa Wanachama cha Mfuko huo, Bw. Msafiri S. Mugaka, alsiema, PSPF kupitia mpango wake wa PSS, imefanikiwa kusajili wanachama wapya kadhaa, ambayo ilikuwa ni moja ya huduma walizokuwa wakizitoa kwenye maonyesho hayo ya siku moja.

  "Pia wanachama wetu waliweza kuja na kupatiwa huduma za taarifa za michango yao, wanawezaji kufaidika na mafao mbalimbali ya yatolewayo na Mfuko kama vile fao la Elimu, Uzazi, mikopo kwa wafanyakazi wapya, na mafao mengine kadhaa,"alisema.

  Maonyesho hayo yalishirikisha makampuni kadhaa ya kibinafsi na taasisi za umma na yalilenga kuwakutanisha wateja wa Airtel, na taasisi hizo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe wa Airtel kutembelea taasisi hizo na kupatiwa huduma mbalimbali wakiwa hapo hapo kazini. 

  Mkuu wa kitengo cha kuandikisha wanachama cha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msafiri S. Mugaka, akiwapatia maelezo wanachama hawa wa PSPF, kuhusu mafao na faida nyingi ambazo mwanachama anaweza kupata ikiwa ni sehemu ya huduma zitolewazo na Mfuko.

  Elimu ikiendelea kutolewa kuhusu huduma za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo

  Penzila Kaisi (kulia), Afisa Matekelezo msaidizi wa PSPF, akimuelimisha mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua shughuli zake.

  Angelina akitoa somo kwa mwananchi huyu.

  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akimsikilzia kwa makini mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ambapo baadaye alijiunga baada ya kuelewa huduma za Mfuko huo.


  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mesigwa Baregu (kulia), akizungumza katika kongamano la Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha), ikiwa ni maadhimisho ya siku ya vijana duniani lililofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila.

  Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila akichangia mambo mbalimbali.
  Mada zikiendelea kutolewa.


  0 0

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewataka wakuu wa idara kwenye Halmashauri nchini kuacha kufanya kazi kimazoea kwa kuishia kukaa maofisini bila kwenda maeneo ya vijijini ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

  Jafo ametoa kauli hiyo ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi katika Halmashauri za Singida, Shinyanga, Uyui na Sikonge mkoani Tabora. Akizungumza na watumishi katika halmashauri hizo, Jafo amesema imekuwa ni mazoea kwa wakuu wa idara kujifungia maofisini bila kufika vijijini kukutana na wananchi ili waweze kutatua kero zao.

  Hata hivyo amewaonya baadhi ya wakuu wa idara wanaowanyanyasa watumishi wa kada za chini kwa kuwapendelea baadhi yao katika mchakato wa upandishaji wa madaraja. Amewaagiza wakurugenzi kupangiana malengo na wakuu wa idara kuwa ni kitu gani kila mmoja wao atakifanya ndani ya mwaka mmoja kwenye eneo lake la kazi.

  Aidha amesema na wakuu wa idara wafanye hivyo hivyo kwa watu wao wa chini ili kila mtu apimwe kiutendaji ndani ya mwaka mmoja. Jafo amekemea tabia ya wakurugenzi wa Halmashauri kupitisha malipo ya miradi ambayo inakuwa imejengwa chini ya kiwango na kwamba ni ubadhirifu wa fedha za wananchi kwa kuwa haifikii malengo yaliyokusudiwa.

  “Hali kama hii imejitokeza kule halmashauri ya kondoa mkoani Dodoma serikali imefanya uchunguzi na tayari hatua zimechukuliwa kwa watendaji 8 ambao wamesimamishwa kazi na wengine kufikishwa mahakamani kutokana na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo…Serikali itaendelea kuchukua hatua kwa yeyote atakayefanya vitendo kama hivi,”amesema Jafo

  Naibu Waziri huyo kwa takriban wiki mbili amefanikiwa kutembelea halmashauri 15 na kutembelea miradi 63 ikiwemo miradi ya hospitali, vituo cha afya na zahanati, miradi ya elimu, maji, na miundombinu ya barabara.

  Miongoni mwa Halmashauri alizozitembelea ni pamoja na Halmashauri ya Kilolo, Mufindi, Mafinga, Iringa, Chemba, Kibaha, Korogwe mji, Halmashauri ya Korogwe, Jiji Arusha, Kisarawe, Singida, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Uyui, na Sikonge .

  Jafo bado anaendelea na ziara yake katika mikoa ya Katavi na Rukwa kwa lengo kutimiza matakwa ya watanzania. 

  Naibu Waziri Jafo akiwa na Mbunge wa vitimaalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hamad walipotembelea mradi wa maji ulioanza kutoa maji katika kijiji cha Tinde Mkoa wa Shinyanga.
  Jafo akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Tinde Mkoa wa Shinyanga.
  Jafo akizungumza na wananchi na watumishi katika mradi wa maji kijijin cha Tinde.
  Naibu Waziri Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama wa Wilaya ya Shinyanga.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) unatarajiwa kuanza mwezi Desemba mwaka huu na kama ilivyo miradi mikubwa unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu na utajengwa kwa awamu nne ili kuharakisha kukamilika kwake.

  Waziri Prof. Mbarawa amesema Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo leo, wakati wa Mkutano wa Sita uliowakutanisha  Mawaziri wa Sekta ya Uchukuzi wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi, uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema lengo la mkutano huo ni kuangalia namna bora ya kupunguza vikwazo kwenye sekta hiyo baina ya nchi hizo.

  Amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi za Afrika Mashariki katika ujenzi wa reli hiyo utachochea kasi ya usafirishaji wa mizigo na shughuli za kibiashara na hivyo kuinua uchumi wa nchi hizo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya uchukuzi (hawapo pichani), katika Mkutano wa Sita wa Kamati ya Mawaziri wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi uliofanyika jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi wa Burundi Eng. Jeon Ntunzwenidana na kushoto ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi ya Tanzania Dkt. Leonard Chamuriho.

  “Kama mnavyojua Serikali imetenga kiasi cha shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo na wenzetu nao watatafuta fedha katika nchi zao ili kukamilisha ujenzi wake”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Aidha Prof. Mbarawa amebainisha kuwa kila nchi itatekeleza mradi wa kujenga reli ya kisasa kwa sehemu yake hivyo ni wajibu wa kila nchi kukamilisha mradi huo ili kuchochea maendeleo yanayotokana na Sekta ya Uchukuzi.

  Amesema kwa upande wa nchi ya Tanzania reli hiyo itaanza kujengwa kuanzia Dar es Salaam- Tabora-Isaka hadi Mwanza yenye urefu wa KM 1,219 ambayo ndiyo uti wa mgongo wa reli yenyewe. Sehemu nyingine ni kutoka Tabora-Mpanda- Kalemela; Tabora-Uvinza hadi Kigoma. Katika kuunganishwa na nchi ya Rwanda na Burundi, Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa reli hiyo itajengwa kuanzia Isaka-Rusumo mpaka Kigali na Keza mpaka Musongati.
  Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho akifafanua jambo kwa viongozi mbalimbali wa sekta ya uchukuzi (hawapo pichani), katika Mkutano wa Sita wa Kamati ya Mawaziri wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi uliofanyika jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.

  Naye Waziri wa Uchukuzi wa nchi ya Burundi Eng. Jeon Ntunzwenidana amefurahishwa na Serikali ya Tanzania katika jitihada zake za kuharakisha ujenzi wa reli hiyo na amesema Serikali ya Burundi itakamilisha ujenzi huo haraka ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na huduma za kibiashara baina ya nchi hizo.

  Waziri Prof. Mbarawa amesaini makubaliano ya uboreshwaji wa sekta ya mawasiliano, reli na barabara baina ya nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

  Zaidi ya trilioni 16 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa reli ya kisasa nchini Tanzania yenye takribani urefu wa KM 2,600.
  Viongozi wa Sekta ya Uchukuzi wakijadiliana kuhusu changamoto mbalimbali za sekta hiyo katika Mkutano wa Sita wa Kamati ya Mawaziri wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mkutano wa Sita wa Kamati ya Mawaziri wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) pamoja na mawaziri kutoka nchi shiriki wakisaini makubaliano ya uboreshwaji wa sekta ya mawasiliano, reli na barabara baina ya nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko, Simon Delens(wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa wiki iliyopita

  Na Mwandishi Weu, Dar es Salaam
  DROO ya mwisho ya Jijenge na Twiga Cement imefanyika leo huku mshindi wa mwisho huku mkazi wa Jiji la Mwanza Revocatus Mwombeki (32) akiibuka kuwa mshindi wa kwanza . Kutokana na ushindi huo Mwombeki ameshinda mifuko 600 ya Twiga Cement Extra ambaye ameshinda bada ya kucheza kwenye droo hiyo iliyoendeshwa kwa majuma manne.

  Katika droo hiyo nafasi ya pili ilikwenda kwa Sweya Bulaga (32) aliyepata zawadi ya mifuko 400 ya Cement huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Salum Ismail mkaazi wa Mkambalani Mkoani Morogoro ambaye amepata mifuko 200 ya Cement. Wakati huohuo Hamza Juma (29) Mkaazi wa Nkuhungu mkoani Dodoma aliibuka mshindi na kupata zawadi ya mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali kutoka Kiwanda cha Twiga Cement.

  Aidha washindi watatu katika droo hiyo waliopatikana wiki iliyopita wamekabidhiwa vyeti vyao vya ushindi ambao ni mshindi wa kwanza Maria Kalinga (35) kutoka Iringa amepata mifuko 600, Cassian Mihoza amejinyakulia mifuko 400 ya Cement , mkaazi wa Kunduchi Jijini Dar es Salaam na Kennedy Owili mkazi wa Jijini Mwanza ambaye amepata mifuko 200 ya Cement.

  Washindi hao wamepatikana katika droo iliyochezeshwa katika Kiwanda hicho cha Twiga Cement kilichopo Wazo Hill Jijini Dar es Salaam. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Ofisa Masoko Simon Delens amewashukuru wananchi wote ambao walijitokeza katika kucheza droo hiyo ambayo ilionekana kuwavutia wengi huku akisema kwamba Twiga Cement inawaandalia mambo mazuri zaidi wateja wake huku akisisitiza kuwa mambo mengi mazuri yatakuja ikiwa ni lengo la kuwafurahisha na kuwavutia wateja.
  Meneja Ukuzaji Biashara wa Twiga Cement, jamal Yahya akiongea na Revocatus Mwombeki (32) ambye ni mkazi wa Jiji la Mwanza aliyeibuka kuwa mshindi wa kwanza katika droo ya mwisho ya Jijenge na Twiga Cement Afisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hamed(wa pili kutoka kushoto) akifuatilia kwa makini huo katika droo hiyo.

  Mkuu wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Martha Haule akiongea na Salum Ismail mkazi wa Mkambalani Mkoani Morogoro ambaye ameibuka mshindi wa tatu na kujinyakulia mifuko 200 ya Cement.

  0 0

  Died 16th August 1986

  Dad, days come by sunrise and end by sunset. Indeed, days have today turned into 30 years since you answered God's call on that fateful morning of 16th August 1986 and yet it seems like it's only yesterday when we had you in our midst.  To others you are gone and forgotten but to us your legacy lives on.

  Dad, Many may think that after 30 years the wounds are completely healed.  But little do they know of the scars that lie in the hearts concealed. The memories you left are beautiful though the sorrow too great to be told to those who loved you.  The years may wipe out many things but the memory of you they will wipe out never!!!!. Dad, in our hearts you live still, and as we loved you, so we miss you.  You are not forgotten nor ever shall you be; as long as life and memory last we shall remember thee, our great mentor.

  As we fondly this day we celebrate years of life that was lived with grace, integrity, honour and humility. We miss you Dad.

  Fondly remembered by your beloved children Nelly, Gerald, Louisa, Alice, Susan, Andrew. Your son in laws Pascal, Rikard, Peter, Alvin, your grand children Jadden, Nelly, Andrew, Simon, Mercy and Michayla.

  0 0

  WANAWAKE wapata mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi pia wamehimizwa kutambua fursa za kiuchumi, kupambana na changamoto mbalimbali zinazomzunguka pamoja na kujihusisha katika shuguli za vikundi ili  kujiletea maendeleo na kupunguza umaskini.

  Hayo yamabainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena  wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha Wanawake Kiuchumi  lililofanyika leo kunduchi Mtongani jijini Dar es salaam leo. 

  Jukwaa hilo limewakutanisha Wanawake wapatao 150 likiwa na lengo la kuwapa elimu wezeshi Wanawake katika  harakati za  kutokomeza umaskini na kupambana na unyanyasaji wa aina zote ndani ya jamii zetu kwa kuendeleza elimu, haki na uhifadhi wa mazingira .

  Moses Emena  amesema “ Jukwaa hili limedhamiria kuleta mwamko na hamasa chanya kwa Wanawake wa eneo hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi.” ameongeza kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo, katika harakati za kupamba na umaskini.

  Emena  pia  amewashkuru wawezeshaji wa mafunzo hayo  Kampuni Trumark kwa kukubali kujitolea kutoa mwongozo wa maandalizi na kutoa elimu wezeshi kwa Wanawake na kushirikiana nasi bega kwa bega katika kufanikisha siku ya leo.

  Vile vile aliwashuru kwa dhati wadhamini na wadau wa maendeleo ya Wanawake Kampuni ya Vodacom Tanzania na Shirika la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kujitoa kwao kuwezesha,  bila kuwasahau wangeni waalikwa kutoka taasisi za fedha Akiba Commercial Bank, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, waandishi wa habari na wengine wote.

  Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi  ya MIBOSCO, Moses Emena na wafanyakazi wa Trumark Tanzania wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.
    Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba akizungumza na wanawake 150 katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililofanyika Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi wa Trumark, Agnes Mgongo akitoa somo la fursa kwa wanawake wapatao 150 waliohudhulia katika ufunguzi wa jukwaa la wanawake kuwezeshwa kiuchumi jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MIBOSCO, Moses Emena akizungumza na wanawake wapatao 150 kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) akiwa pamoja na wadau wengine wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuangalia Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria Sinza leo jijini Dar es salaam. Baadhi ya Wadau wa Mahakama waliotembelea Mahakama hiyo ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mawasiliano, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
  Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) akiwaelezea jambo baadhi ya Makatibu Wakuu na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ambao ni Wadau wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuwa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam. Anayetazamana na Kattanga ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) wakiwaonyesha jambo wadau wengine wa Mahakama walipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo jijini Dar esa salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (Kushoto) na Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi wakizungumza jambo walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya uanzishwaji wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akipita katika jengo la abiria wanaonkwenda Unguja wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam kukagua utendaji wa mashine za kukagua mizigo na abiria bandarini hapo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiongea na abiria wanaosafiri kuelekea Unguja wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam kukagua utendaji wa mashine za kukagua mizigo na abiria bandarini hapo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Uendeshaji Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Percoval Salama (wa kwanza kulia)  wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam.
  PICHA NA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (WUUM)

  0 0


  0 0


  SIMU.TV: Wakazi wa vijiji vinavyopakana na mto Kagera katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, wameiomba serikali kuingilia kati katika kutafuta amani ya wananchi wanaoishi kando ya mto huo; https://youtu.be/EQb4fNhWiWM

  SIMU.TV: Wakazi wa kijiji cha Chakama katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, wameelezea masikitiko yao ya kukosa huduma za kijamii toka kupatikana kwa uhuru;https://youtu.be/t1wBjZjHl7c

  SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema, serikali imedhamiria kuwapatia miradi mbalimbali wahandisi wazawa ili waweze kuendeleza ujuzi wao;https://youtu.be/IuXd2a6pvBo

  SIMU.TV: Waziri wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema, serikali inajitahidi kukarabati kwa uharaka kamera zilizoko eneo la ukaguzi ili kuimarisha usalama bandarini hapo; https://youtu.be/4aSXvNikE8k

  SIMU.TV: Serikali imeziagiza halmashauri za wilaya mkoani Ruvuma kuanzishwa kwa vikundi vya ushirika ili kurahisisha utoaji wa mikopo; https://youtu.be/71eCdfDNbsY

  SIMU.TV: Wizara ya ujenzi. mawasiliano na uchukuzi imesema, serikali ya Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa wataalamu hususani katika sekta ya usafirishaji;https://youtu.be/A-thZYVsv-g

  SIMU.TV: Kampuni za Bima nchini, zimetakiwa kuzingatia miongozo ya utendaji kazi wao ili kuepuka migogoro isiyokuwa na sababu za msingi; https://youtu.be/Alfu9IGcBck

  SIMU.TV: Naibu waziri wa mambo ya ndani nchini Hamad Msauni, amezindua rasmi mashindano ya mpinga cup yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya usalama barabarani; https://youtu.be/0QPbeE4Tc1U

  SIMU.TV: Wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa nchini timu ya soka ya Yanga, inatarajia kujitupa uwanjani siku ya kesho kurudiana na timu ya Mo Bejaia katika kombe la shirikisho barani Afrika; https://youtu.be/o-QRM_oqBcY

  SIMU.TV: Timu ya majeshi ya mchezo wa mikono ya Tanzania imefanikiwa kuifunga timu ya mchezo huo kutoka Uganda katika mashindano yanayoendelea nchini Rwanda;https://youtu.be/btI8ETVai-U

  0 0  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Nicodemus Thom Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa maofisa habari kutoka idara ya Habari. Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Nicodemus Thom Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa maofisa habari kutoka idara ya Habari. Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Nicodemus Thom Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa maofisa habari kutoka idara ya Habari. Mkutano wa waandishi wa habari na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ukiendelea. Kulia ni baadhi ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo.

  Na Mwandishi Wetu.
  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema ipo tayari kutoa huduma za Mawasiliano za kisasa kwa Taasisi za Umma zinazohamia mkoani Dodoma kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa taasisi hizo jijini Dar Es Salaam kuzisaidia kutekeleza majukumu yao. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Meneja Mawasiliano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelelezo) ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kwa Taasisi zake kuwasiliana na Umma na kutoa ufafanuzi wa hoja mbali mbali.

  “TTCL imejipanga vyema kufanikisha azma hii ya Serikali ya kuhamia Dodoma. Tupo tayari na tunao uwezo mkubwa wa Rasilimali watu, vifaa na utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za Mawasiliano.

  Tunawahakikishia wateja wetu wote kuwa, watakapochagua kuitumia TTCL, watakuwa wamefanya uchaguzi sahihi. Nitumie fursa hii kuziomba taasisi zote za Umma zinazohamia Dodoma na taasisi zote kwa ujumla kutumia huduma za TTCL ambazo siku zote zimethibitika kuwa ni huduma bora, za uhakika na zenye gharama nafuu,” alisema Bw. Thom Mushi. Akizungumzia kuhusu mipango ya Kampuni hiyo kuboresha huduma zake, Bw. Mushi alisema, kwa kutumia fursa iliyopo katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, TTCL inaendelea kutekeleza kwa vitendo wajibu wake kwa Umma kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunganisha Kampuni, Taasisi, Ofisi za Serikali, Mashirika ya Umma na binafsi wateja waliopo nchi jirani ili waweze kupata Mawasiliano ya uhakika wakati wote. 

  Kwa sasa tunao Mpango Mkakati wa Biashara wa miaka mitatu(Strategic Business Plan 2016-2018) unaolenga kuboresha na kuleta huduma mpya katika soko, kuongeza jita na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa Wateja wetu hasa tukizingatia kuwa, TTCL ni mhimili mkuu wa mawasiliano nchini Tanzania.

  Akifafanua kuhusu hatua muhimu zilizochukuliwa na TTCL hadi sasa kutekeleza mpango wa mabadiliko, alisema ni pamoja na kuboresha miundombinu ya mtandao wa Simu na Data, kuondoa mitambo chakavu, kuleta huduma bora na zenye kukidhi mahitaji. Aidha aliongeza kuwa TTCL imeboresha miundombinu ya simu za mezani na Mkononi kwa kuleta teknolojia ya GSM -2G, UMTS-3G na 4G LTE sokoni ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la mawasiliano. 

  Teknolojia hii itasaidia kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti yenye kasi zaidi. “…TTCL inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya Data nchi nzima (IP Core Network, IP transport Network, Metro Network). Hii itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu kama vile Wizara, Idara na Taasisi za Umma, Serikali za Mitaa, Taasisi za fedha, Kampuni za Umma na binafsi na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi. Kufanikiwa kwa mpango huu kutaleta mabadilko chanya katika huduma za kijamii kama vile Elimu, Afya, Biashara, Uwekezaji, Ujasiriamali, Kilimo, Ufugaji na huduma nyingine ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji mawasiliano ya uhakika ili kufanyika kwa ufanisi.” Wakati huo huo, kampuni ya TTCL imempongeza mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari (Maelezo) Mwanahabari Mwandamizi, Ndugu Hassan Abbas, kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo. 

  “Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kumpongeza Ndugu Hassan Abbas, kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.” “Wasifu wa Ndugu Abbas unatupa imani kubwa kwamba, chini ya uongozi wake, pamoja na utekelezaji wa Majukumu mengine, Idara ya Habari Maelezo itaendelea kutoa mwongozo thabiti kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali pamoja na kuhakikisha kuwa, Umma unapata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka kuhusu utendaji wa Serikali katika kuwatumikia,” alisema Bw. Thom Mushi.

  0 0


  Kutokana na sababu mbalimbali, Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imelazimika kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa michezo kadhaa ya mwanzo kama ifuatavyo.

  1. Mchezo Na. 2 – Kagera Sugar vs Mbeya City (20.08.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 21.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Sababu ni kuwa uwanja wa Kaitaba bado utakuwa kwenye matengenezo.

  2. Mchezo Na.4 – Toto African vs Mwadui FC (20.08.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 24.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za mabadiliko ni kuwa uwanja huo tarehe 20.08.2016 utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.

  3. Mchezo Na.13 – Kagera Sugar vs Stand United (27.08.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo huo ilikuwa ni Kagera Sugar, lakini kwa sasa timu mwenyeji atakuwa ni Stand United.


  4. Mchezo Na.55 – Toto vs Ndanda (02.10.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 03.10.2016 badala ya tarehe 02.10.2016

  5. Mchezo Na.80 – Mbao FC vs Ndanda fc (16.10.2016)
  Mchezo huo umerudishwa nyuma kutoka tarehe 16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni kuiwezesha timu ya Ndanda kucheza michezo miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza gharama.

  6. Mchezo Na.96 – Tanzania Prisons vs Mbao FC (22.10.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 23.10.2016 badala ya 22.10.2016 ili kuipa nafasi timu ya Mbao kupumzika na kusafiri. Tayari timu za Ligi Kuu ya Vodacom zimearifiwa na kuagizwa kuzingatia mabadiliko hayo.

  Source: tff.or.tz

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amezindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation 
  Mara baada ya uzinduzi huo Ulega aliwashukuru wafadhili hao nakuwaomba kuendelea kusaidia wilaya hiyo ili kukabiliana na uhaba wa Maji uliopo na kwamba Mkuranga ni moja ya maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya Maji....Pia aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia Maji  hayo vizuri ikiwa pamoja na kulinda miundombinu Yake ikiwamo solar na vinginevyo ili visiibiwe...ulega tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa jimbo hilo tayari ameshachimba visima katika vijiji zaidi ya vitano huku akisaidia kutatua mambo mbalimbali ambayo yamekuwa kero Kwa watu wake.
   Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Mwongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwalusembe   kweye hafla ya  uziduzi wa kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation mkoani Pwani.
  Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega  katika  kijiji cha Mwalusembe kwa ajili ya kuziduzi kisima cha Maji  ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo mkoani Mpwani. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

  Kundi la muziki la Wapancras linalojumuisha wasanii ndugu, Mecrass na Payus, la Jijini Mwanza, limeachia wimbo mpya uitwao "Nitunzie Siri", wakimshirikisha Abuu Mkali.

  Wimbo umetengenezwa pande za Vibe Nation & Quick Sound ikiwa ni mikono ya Producers, Aniwylee na Day Dream.
  Bonyeza HAPA Kusikiliza au bonyeza play hapo chini.
   Na BMG

  0 0

  Na Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba  Zanzibar inaendelea kufaidika kiuchumi na Maendeleo kutokana na kuungwa mkono kimisaada kutoka kwa mshirika wake mkubwa wa maendeleo Jamuhuri ya Watu wa China.
  Alisema China imekuwa mshirika wa karibu na Zanzibar hasa katika sekta ya Kilimo na Viwanda ulioanza mara baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambao umewezesha kufungua  milango ya ajira kwa Vijana waliowengi Visiwani Zanzibar.
  Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo  Zanzibar Bwana Xie Xiaolon aliyefika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambalisha rasmi kushika wadhifa wa mtangulizi wake Bwana  Xie Yunliang aliyemaliza muda wake.
  Alisema ujenzi wa utanuzi wa eneo la maegesho ya Ndege, Bandari ya Mpiga Duri Maruhubi, Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee Mkoani Pemba pamoja na uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya mtandao wa Mawasiliano { E. Government }ni miongoni mwa Miradi Minne mikubwa inayofadhiliwa na China kupitia Benki ya Kimataifa ya Exim.
  Balozi Seif  kupitia Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China na Benki hiyo kwa kuendelea kuiunga Mkono Zanzibar katika miradi  hiyo ya Maendeleo, Kiuchumi na Ustawi wa Jamii.
  Alisema hatua hiyo itazidi kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili uliodumu kwa takriban miaka 52 sasa ambao unazidi kukuwa kadri maisha ya Wananchi wa sehemu hizo yanavyoendelea kuingiliana Kibiashara na Kiutamaduni.
  Aidha Balozi Seif alifahamisha kwamba mabadiliko ya haraka ya kiuchumi yanayoendelea kufanywa na Taifa hilo kubwa la Bara la Asia yataendelea kutoa nafasi kubwa zaidi kwa  Nchi changa zinazoendelea hasa zile za Bara la Afrika kuiga mfano huo.
  Mapema akijitambulisha rasmi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha miradi iliyoanzishwa Zanzibar na kupata msukumo wa kiuwezeshaji kutoka Nchini Mwake inakamilika kwa wakati.
  Balozi Xie alielezea faraja yake kutokana na Uongozi wa  Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya ZTE yenye Makao Makuu yake  Nchini China uliofadhili mradi wa uwekaji  wa Taa za bara barani zinazotumia mwanga wa Jua kuanzisha mpango maalum wa kuzifanyia matengenezo taa hizo.
  Alisema zipo baadhi ya taa tayari zimeanza kuleta hitilafu zinazopelekea kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida za kutoa mwanga kwenye bara bara kutokana na uchakavu wa betri zake.
  Ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wake kwa kuendelea na harakati zao za kimaisha katika misingi ya amani na utulivu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
  Balozi Xie alieleza kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa Viongozi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla pamoja na Jamuhuri ya Watu wa China kuendelea kishirikiana kwa maslahi ya pande hizo mbili.
   Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar alipofika kujitambulisha rasmi kuanza kazi zake za Kidiplomasia hapa Zanzibar.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akizungumza na Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon aliyepo kati kati alipofika kujitambulisha rasmi. Wa kwanza kutoka kushoto ni msaidizi wa Balozi  Xie Xiaolon anayeshughulikia Utawala Bwana Wang Xingjun.
  Balozi Mdogo Mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

  0 0


  Wasalaam, 
  Ndugu zangu Waandishi wa Habari wa Hapa Makao Makuu ya Tanzania Yetu Dodoma.
    Lengo la Kuwaita Hapa Leo kwanza Kumpongeza Mwenyekiti Wetu wa CCM ambaye ni Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kuchaguliwa kwa Kura nyingi na Wajumbe wa Mkutano mkuu Kukiongoza Chama chetu  cha Mapinduzi, Pili Kuongoza Taifa letu Tanzania kwa kurudisha nidhamu kwa Watumishi wa Umma na Mali za Umma kutoshezewa ovyo, Ukusanyaji wa Mapato ya ndani, Elimu bure ambayo imeambatana na Kampeni iliyofanikiwa asilimia 97 ya Madawati, Kujali wanyonge katika kuendelea kuboresha huduma bora za Kijamii, Kushughulikia Kikamilifu suala la Rushwa na Ufisadi kwa kuunda Mahakama Maalumu ya Kushughulikia kesi za Mafisadi na Wahujumu Uchumi..

    Ndugu Waandishi wa Habari, Leo Ijumaa  wakati  wa Mapokezi ya Mwenyekiti Wetu Mh.Rais Dkt.Magufuli ameendelea kuonesha uchungu wake Juu ya Chama chetu kuhusu Mapato ya Jumuiya za ndani ya Chama ikiwa  mambo kadhaa ambayo baadhi ya Viongozi wamekua ni Miungu watu, wamekua wakitumia Mali za Chama na Jumuiya zake kwa maslahi yao Binafsi.

    Ndugu Wanahabari naomba sasa WANACCM nchi nzima tumsaidie Mwenyekiti Wetu kuwabainisha watu wenye dhamira ovu na Matendo yasiyofaa ndani ya Chama chetu ambao wanakiuka katiba,  taratibu na kanuni za Chama chetu cha Mapinduzi kuhusu Mali za Chama, Miradi ya Chama ambayo wamekua Wakiifanya kama sehemu yao ya Kujiingizia Kipato.
   Ndugu Wanahabari Namuomba Mwenyekiti Mh.Rais Dkt. Magufuli aunde Tume ya Uchunguzi wa Mali za Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwani Hali yake ni Mbaya Juu ya Mambo yafuatayo.

  1. Mapato ya Jengo na Juu ya Matumizi ya Fedha zinazopatikana na Mapato hayo ikiwa ni Mradi mkubwa wa Jumuiya ya Vijana(UVCCM ).

  2.Minada Holela ya Mali za Chama ikiwemo Magari n.k.ambayo imekua ikifanyika kinyume na Taratibu.

  3.Uuzwaji wa Viwanja(Mashamba) vya Jumuiya Mkoani Iringa.
  4.Kushughulikia Wasaliti ndani ya Chama na Jumuiya Yetu ya UVCCM ambao wamekua mchana CCM usiku vyama vya upinzani.

     Namuombea sana Mheshimiwa Rais Wetu ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kila siku ya Mungu kwani mambo anayofanya kwa Taifa kwa sisi wanyonge tupo Pamoja naye, lakini kuna baadhi ya waliozea njia za Ujanja Ujanja wanamuona kama adui. Endelea Mh.Mwenyekiti Dkt Magufuli  ambao tunakuamini tu Wengi, Tanzania Yetu kwa Muda mchache umeonesha Dhamira yako ya Kutufikisha Tanzania Mpya yenye Uchumi wa Viwanda, Kumiliki ndege zetu, Ukusanyaji madhubuti wa Mapato ya ndani, Kurudisha nidhamu serikalini kwa watumishi wa Umma, Mali za Umma kutoshezewa ovyo, Kufanikisha Elimu Bure, Kufanikisha uundwaji wa Mahakama Maalumu ya Kushughulikia Kesi za Mafisadi , wala Rushwa na Wahuhujumu Uchumi.
      Ndg. James Rock Mwakibinga,

     Kada CCM , mwanachama UVCCM.


            Dodoma, Tanzania

  0 0older | 1 | .... | 1317 | 1318 | (Page 1319) | 1320 | 1321 | .... | 3272 | newer