Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1315 | 1316 | (Page 1317) | 1318 | 1319 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Korea kusini nchini Tanzania Mhe. Song, Geum-Young alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo.
  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson akipokea jarida maalum kuhusu Korea kutoka kwa Balozi wa Korea kusini nchini Tanzania Mhe. Song, Geum-Young alipomtembelea Ofisini kwake ​Jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo jana. Picha na Bunge

  0 0

  Mfanyabiashara wa mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga, Joseph Machenja amekabidhi madawati 60 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani humo na kuwataka wananchi wote kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kutekeleza zoezi hilo.

  Akikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa wilaya hiyo Nyabaganga Taraba, Machenja alitoa mwito kwa wananchi kushirikiana na kuendelea kutengeneza madawati ili kuondoa kabisa uhaba.

  Alisema zoezi hilo ni endelevu na ndiyo maana ameonesha uzalendo kwa kuguswa na agizo la Rais la kuchangia madawati hayo katika wilaya hiyo japo anatoka Wilaya ya Kahama.

  “Nimeguswa na ndiyo maana nimechangia madawati haya ingawa sina mtoto anayesoma katika shule ya Kishapu na pia si lazima uwe mkazi wa hapa, hivyo nawaomba wananchi wachangie madawati,” alisema.

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya, Taraba alimshukuru kwa mchango wake ambapo alisema ni moyo wa kuigwa kwa wananchi wengine wa Kishapu japo anatoaka mbali.

  Aidha, aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kwa moyo wote waendelee kuchangia madawati kwani zimebaki siku chache kukamilisha zoezi hilo muhimu.

  Aliagiza madawati hayo yaende katika shule ya msingi Buduhe na kumkabidhi Mtendaji wa Kata ya Kishapu iliyopo shule hiyo, ambapo alisema yatasaidia wanafunzi 180.
  Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mfanyabishara Joseph Machenja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kama sehemu ya mchango wake katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga pamoja na mfanyabiashara aliyechangia madawati, Joseph Machenja katika viwanja vya ofisi ya halmashauri.
  Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakifutahia jambo wakati wa hafla fupi ya kupokea madawati katika viwanja vya ofisi ya halmashauri leo.
  Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Jumanne Chaula (kushoto) akimshukuru mfanyabiashara, Joseph Machenja baada ya kutoa msaada wa madawati katika halmashauri hiyo.

  0 0

  Na Zuena Msuya, Arusha 
  Wizara ya Nishati na Madini inafanya mnada wa Madini ya Tanzanite kwa mara ya kwanza yaliochimbwa kutoka migodi ya kampuni tano za wafanyabiasha wa madini hayo katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiko Mkoani Manyara. 
  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo wakati wa mchakato wa kupata wafanyabiashara watakaoshinda zabuni ya kununua madini hayo kutoka Mataifa mbalimbali Duniani wakiwemo watanzania. 
  Kalugendo alisema utaratibu wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei halisi inayoendana na soko la dunia. 
  Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao. Akizungumzia mnada huo, Kalugendo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO) pamoja Wizara ya Nishati na Madini, kwa lengo la kusimamia haki ya kila mhusika wa madini hayo. 
  " Madini ya Tanzanite yanathamani ya fedha nyingi sana,kwa usalama wa wanunuzi na wauzaji, Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hilo ili kujihadhari na watu wasio waaminifu," alisema Kalugendo.
   Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utaratibu huo ili uweze kuleta tija zaidi kwa Watanzania. Utaratibu huo ni wa kaiwaida kwa nchi zenye madini ya namna hii kama vile Zambia( emerald),Zimbabwe( Almasi) pamoja na Afrika kusini( almasi). 
  Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Agosti 12 mwaka mkoani Arusha.
  Mhandisi Juma Lunda( kulia) akimuelekeza mmoja wa wanunuzi wa madini ya Tanzanite kujaza fomu za kushiriki zabuni ya kununua madini hayo.

  Vifaa vinavyotumika kuhifadhia Madini ya Tanzanite.

  Sehemu inayotumiwa na wauzaji pamoja na wanunuzi kujiridhisha kwa kupima thamani ya madini ya Tanzanite kabla ya kufikia muafaka wa bei. 

   Mnunuzi wa madini ya Tanzanite Macmillan Njau( kulia) akijiridhisha kwa kupima thamani ya madini hayo kabla ya kununua akiwa na Mkurugenzi  wa Kampuni ya Franone Mining & Gem Company, Onesmo Mbise(katikati) ambaye ni muuzaji wa madini ya Tanzanite na Elia Benyamin( kushoto) Mnunuzi wa Madini.

  Mthaminishaji Madini ya Almasi wa Serikali Edward Rweyemamu (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau wa Madini ya Tanzanite( kushoto), Sekretari wa kituo cha Jimolojia ( TGC)Halima Hussein( wapili kulia) na Zainab Napacho (kulia)kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania( TMAA) 


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV. Misungwi wakati akielekea mkoani Mwanza. 
  PICHA NA IKULU.

  0 0  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa wataalam wa TEHAMA wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Arnold Mathoyo akieleza utaratibu wa mafunzo ya TEHAMA kwa washiriki wanaosimamia miradi ya TEHAMA chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.
  Washiriki wa mafunzo kuhusu TEHAMA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (hayupo pichani).
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi i akifungua mafunzo kwa wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

  Usimamizi na utekelezaji wa Serikali Mtandao unahitaji Rasilimaliwatu yenye weledi mkubwa wa kusimamia maeneo ya msingi.

  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi alisema hayo mkoani Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa miradi mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayotekelezwa chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania.

  “ Rasilimaliwatu katika eneo hili inahitaji kupewa mafunzo na kuendelezwa katika nyanja muhimu za usimamizi wa TEHAMA na pia kuwa na uwezo na uelewa wa mifumo na taratibu za utendaji kazi katika Taasisi za Umma” Bi. Mlawi alisema.

  Bi. Mlawi alifafanua kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la Serikali la kuwajengea uwezo wataalam wake ili kuboresha utekelezaji wa miradi ya Serikali Mtandao yenye lengo la kuziwezesha Taasisi za Umma kutoa huduma bora kwa Wananchi.

  Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yamelenga kuongeza uwezo kwa wataalam wa Serikali hususani katika Ununuzi na usimamizi wa utekelezaji wa mifumo na mitandao mbalimbali ya TEHAMA inayowekwa katika Taasisi za Serikali ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa Umma.

  Bi. Mlawi aliainisha kuwa uteuzi wa washiriki wa mafunzo hayo umezingatia ushiriki katika utekelezaji wa miradi ya RCIP na matokeo ya utafiti wa mahitaji ya mafunzo kwa maafisa TEHAMA wa Taasisi za Serikali, uliofanywa na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mwezi Septemba, 2015.

  Alisisitiza kuwa, kila mshiriki atajengewa uwezo wa kiufundi kulingana na mahitaji halisi katika eneo au maeneo ya kusimamia na kutengeneza mifumo ya TEHAMA.

  Naibu Katibu Mkuu huyo Bi. Mlawi, alielekeza washiriki wa mafunzo hayo wahakikishe ujuzi watakaoupata unawafikia wale ambao hawakubahatika kuchaguliwa kwa sababu idadi ya washiriki walioteuliwa kuhudhuria mafunzo ni ndogo ikilinganishwa ya idadi kubwa ya Maafisa TEHAMA waliopo katika Taasisi za Serikali ili kwa pamoja washirikiane kubuni mifumo ya TEHAMA yenye kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma.

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya RCIP eneo la Mifumo ya Serikali Mtandao “e-Government Applications” ambapo mifumo mbalimbali ya TEHAMA (ya Kimkakati na ya Kisekta) inaendelea kuwekwa na kutekelezwa katika Taasisi walizotoka washiriki wa mafunzo.

  Mifumo hiyo ni Mfumo wa Wakala ya Usajili, Vizazi na Vifo (Birth and Death Registration System) kupitia Wakala ya RITA; Mfumo wa Taarifa za Biashara (National Business Portal) kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu (Telemedicine system) kupitia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi (e- Procurement system) kupitia Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bohari ya Dawa (MSD), Mradi wa “electronic Records” kupitia Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na; Mradi wa “electronic Office” kupitia Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA).

  Mafunzo hayo yatatolewa kwa Maafisa, Wasimamizi wa miradi 62; Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA 15 na Maafisa Ugavi 50 kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali na yatafanyika kwa awamu 5 katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Dodoma.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi tiketi za ndege kwa waandishi wa habari wa watatu waliopata udhamini wa benki hiyo kwenda Nairobi Kenya kuhudhuria mafunzo ya biashara na masuala ya fedha. Waandishi waliopata ufadhili huo ni Finnigan Simbeye (The Guardian, Abduel Elinaza (Daily News) na Samuel Kamndaya (The Citizen). Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akuzungumza katika hafla hiyo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi Kenya, Mwandishi wa Habari wa gazeti la The Guardian Finnigan Simbeye.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi Kenya, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Daily News, Abduel Elinaza.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi Kenya, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Citizen, Samuel Kamndaya. 

  0 0

  Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kuhusu umuhimu wa Serikali kuwasiliana kimkakati na wananchi na namna bora ya kuwasilisha taarifa kwa jamii, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas akiongea na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi baina ya Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China Zhao Qizheng na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini. 
  Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

  0 0

  Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
  Na Jovina Bujulu-MAELEZO

  Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi ametoa wito kwa watanzania kuongeza juhudi katika kupiga vita dhidi ya ujangili nchini.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu cha “Tembo-Faru wana haki ya kuishi Tanzania” kilichoandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar  es salaam.

  Rais mstaafu huyo, amesema kumekuwa na tatizo la kutowalinda na kuwatunza wanyama hao kwani kuwauwa ni dhambi na kinyume na kusudio la Mungu kwa kuwa wanyama hao wana haki ya kuishi kama viumbe wengine.

  “ kumekuwa na matukio mengi ya uuaji wa wanyama wakiwemo tembo na faru na hivyo kupunguza rasilimali ya taifa kwa vizazi vijavyo na pia kitendo hicho ni kinyume na kusudio la Mungu hivyo ni vizuri kuwatunza, kuwapenda, kuwaendeleza na kuwalinda wanyama hao kwani ni moja ya vivutio vinavyochangia pato la Taifa” aliongeza Rais Mstaafu  Mwinyi.

  Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na mbuga nzuri duniani hivyo ni budi kushirikiana katika kupambana dhidi ya ujangili ndani ya nchi yetu.

  Ameongeza kuwa jumuiya ya ujangili ni kubwa ambayo inahusisha  mifumo mbalimbali ikiwemo watengenezaji wa silaha za kuua tembo, waagizaji wa meno ya tembo, wasambazaji na watu mashuhuri ambao wanatumia nyumba zao kuhifadhi meno ya tembo.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WILDAID  Peter Knights ambao ni wadhamini wa kitabu hicho, ameipongeza Serikali ya China kwa jitihada zake za kupiga marufuku biashara ya uuzaji wa meno ya Tembo hatua hiyo imesaidia kulinda wanyama hao. 
    
  Kitabu cha Tembo-Faru wana haki ya kuishi Tanzania kimetayarishwa na kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es salaam kikiwa na lengo la kudumisha amani kwa binadamu na Wanyama ili wasiweze kupoteza uhai wao.

  0 0

  Kutokana na sababu mbalimbali, Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imelazimika kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa michezo kadhaa ya mwanzo kama ifuatavyo.

  1. Mchezo Na. 2 - Kagera Sugar vs Mbeya City (20.08.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 21.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Sababu ni kuwa uwanja wa Kaitaba bado utakuwa kwenye matengenezo.

  2. Mchezo Na.4 - Toto African vs Mwadui FC (20.08.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 24.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za mabadiliko ni kuwa uwanja huo tarehe 20.08.2016 utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.

  3. Mchezo Na.13 - Kagera Sugar vs Stand United (27.08.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo huo ilikuwa ni Kagera Sugar, lakini kwa sasa timu mwenyeji atakuwa ni Stand United.

  4. Mchezo Na.55 - Toto vs Ndanda (02.10.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 03.10.2016 badala ya tarehe 02.10.2016

  5. Mchezo Na.80 - Mbao FC vs Ndanda fc (16.10.2016)
  Mchezo huo umerudishwa nyuma kutoka tarehe 16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni kuiwezesha timu ya Ndanda kucheza michezo miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza gharama.

  6. Mchezo Na.96 - Tanzania Prisons vs Mbao FC (22.10.2016)
  Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 23.10.2016 badala ya 22.10.2016 ili kuipa nafasi timu ya Mbao kupumzika na kusafiri. Tayari timu za Ligi Kuu ya Vodacom zimearifiwa na kuagizwa kuzingatia mabadiliko hayo.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
  Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake kupitia Sera zilizopo nchini humo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (kushoto) ambaye ni miongoni mwa wanawake viongozi wa Tanzania walionufaika na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa hafla fupi ya Tathmini ya Mafanikio ya Mfuko wa Hanns Seidel Foundation nchini Tanzania, jana usiku jijini Dar es salaam.
  Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko huo jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
  Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller (kulia) akifurahia picha ya kuchorwa aliyokabidhiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jana jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani.


  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wa pili kulia), akishirikiana na viongozi wengine akiwemo Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mheshimiwa Bonnah Kaluwa(wa kwanza kushoto),kuzindua ujenzi wa kituo cha polisi kinachojengwa katika Jimbo la Segerea ikiwa ni mkakati wa kupambana na uhalifu katika jimbo hilo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akishiriki ujenzi wa awali wa kituo cha polisi kinachojengwa katika Jimbo la Segerea ikiwa ni mkakati wa Mbunge wa jimbo hilo kupambana na vitendo ya uhalifu katika jimbo hilo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(suti nyeusi), akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi .Naibu Waziri huyo pia aliongoza Harambee ya Ujenzi wa kituo hicho ikiwa ni mkakati wa Mbunge wa Jimbo hilo Bonnah Kaluwa, kupambana na matukio ya uhalifu.Naibu Waziri huyo aliongoza.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi .Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mheshimiwa Bonnah Kaluwa. Ujenzi wa kituo hicho ni mkakati wa kupambana na matukio ya uhalifu yanayotokea katika jimbo hilo.
  Mbunge wa Jimbo la Segerea la Segerea, Bonnah Kaluwa, akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(suti nyeusi) na viongozi wengine kwenda kutembelea eneo ambapo ujenzi wa kituo cha polisi katika jimbo hilo umeanza ikiwa ni mkakati wa kupambana na matukio ya uhalifu jimboni hapo.
  Wananchi wa Jimbo la Segerea, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi ikiwa ni mkakati wa Mbunge wa Jimbo hilo, Bonnah Kaluwa, kupambana na matukio ya uhalifu katika jimbo hilo.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi mara baada ya kuwasili katikati ya jiji la Mwanza akitokea wilayani Sengerema Jumatano Agosti 10, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa furaha na mamia ya wananchi eneo la  Nyegezi stand jijini Mwanza wakati akitokea Wilayani Sengerema.  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa (kushoto) ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza masuala mbali mbali ya kisiasa na ya kijamii na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Msajili wa Vyama vya Siasa  nchini amekifuta katika orodha ya vyama vya siasa vyenye usajili wa muda Chama cha Maadili na Uwajibikaji        (CM-Tanzania) kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya usajili. Chama cha CM-Tanzania kilipata usajili wa muda tarehe 4 Februari, 2016.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 8(3) na (4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992, chama cha siasa chenye usajili wa muda ni lazima kiwasilishe maombi ya usajili wa kudumu ndani ya siku mia moja na themanini tangu tarehe ya kupata usajili wa muda. Aidha, uhai wa chama cha siasa chenye usajili wa muda unaisha baada ya siku mia moja na themanini (180) tangu kipate usajili wa muda .

  Hivyo, uhai wa cheti cha usajili wa muda wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-Tanzania) ulikwisha tarehe 2 Agosti, 2016, kwani waanzilishi wake walipaswa kuwasilisha maombi ya usajili wa kudumu siyo zaidi ya tarehe 02 Agosti, 2016.

  Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, waanzilishi na wanachama wote wa CM-Tanzania hawapaswi kufanya siasa au shughuli yoyote kwa jina la Chama cha Maadili na uwajibikaji, kwa sababu uhai wa cheti chake cha usajili wa muda umekwisha. Kufanya hivyo ni kukiuka Sheria za nchi.

  Kufutwa kwa Chama cha Maadili na Uwajibikaji  kunaifanya idadi ya  vyama vya siasa vyenye usajili wa muda  kuwa kimoja ambacho  ni  Chama cha Restoration of the Nation Party (RNP). Aidha, idadi ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni ishirini na mbili (22).

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za Feza, Habib Miradj akizungumza na waandishi wa habari juu kuhusiana na taarifa zinazozagaa za kufungwa kwa shule za Feza leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa shule wa Feza, kadri dalcicea.
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SHULE za Feza nchini hazitafungwa kutokana na shule hizo zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi hivyo ikibidi kufanya hivyo sheria zitatumika zilezizle zilizofanya shule hizo zisajiliwe.

  Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Bodi wa Shule za Feza, Habib Miradj wakati alipokutana na waandishi wa habari leo juu ya kuzagaa kwa taarifa katika mitandao si michuzi blog juu ya shule za fedha kufungwa, amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli na kuwataka wazazi kuendelea kuwaunga mkono katika kusukuma gurudumu la elimu.

  Amesema Feza imekuwa ikijulikana kimataifa kwa kufanya vizuri na kuweza kupata tuzo mbalimbali katika utoaji wa elimu ikiwa na wanafunzi wanaokwenda katika vyuo vya ndani ya nje wamekuwa wakipata ufaulu wa juu.

  Miradj amesema kuwa wakaguzi shule wamekuwa wakienda na kuwashauri vitu mbalimbali hivyo hata kufungwa kwa sheria zitatumika lakini  suala hilo halitegemei kutokea  katika shule zetu za feza kutokana na hadhi ambayo imefikia katika utoaji wa elimu.

  Aidha amesema kuwa Feza inazidi kujiimarisha katika utoaji wa elimu na kuongeza kuwa mpango wao kuhakikisha shule zinaongezeka katika baadhi ya maeneo kutokana na mahitaji ya elimu nchini.

  Amesema historia ya Feza imetokana na juhudi za serikali ya kutaka uwekezaji  wa shule ufanywe nchini baada kuonekana kufanya vizuri nchini Uturuki.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, lobu ya Jamii.
   SHAMBULIAJI Mkongwe na nahodha wa timu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi (Pichani)ametangaza rasmi kuachana na kusakata kabumbu na sasa anahamia upande wa benchi la ufundi, Mkongwe huyo amewahi tkucheza timu mbalimbali za ligi kuu kwa kujituma na kufikia malengo yake katika soka.

  Mkuu wa kitengo cha  Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara amethibitisha hilo na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kwa kimataifa utakaopigwa Jumapili ya Juma hili uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya URA ya Uganda.

  Manara amesema kuwa kwa sasa Mgosi atakuwa meneja wa timu na  aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa timu (Team Coordinator) huku kitambaa cha unahodha akikabidhiwa Jonas Gerald Mkude.

  Aidha kiungo wa klabu hiyo, Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea timu ya Mbeya City FC, ametolewa kwa mkopo African Lyoni liyopanda kucheza ligi Kuu msimu huu wa 2015/2016.

  Inaelezwa mechi ya Simba na  URA itakuwa ya mwisho ambapo Agosti 20 wekundu hao watashuka dimbani kukipiga na Ndanda  wakuchelechele katika uwanja wa Taifa.

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (kulia) akiwa katika kikao na Wawakilishi wa Wananchi watakaopitiwa na mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 kutoka Somanga Fungu hadi jijini Dar es Salaam utakaotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na watendaji kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na  Benki ya Maendeleo ya TIB.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (kulia) akisalimiana na Wawakilishi wa Wananchi watakaopitiwa na mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 kutoka Somanga Fungu hadi jijini Dar es Salaam utakaotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO. Wawakilishi hao walifika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo.  Kikao hicho pia kilihudhuriwa na watendaji kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na  Benki ya Maendeleo ya TIB.

  Na Teresia Mhagama, Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Benki ya Maendeleo ya TIB kuhakikisha kuwa kuanzia Septemba 17 mwaka huu, wanaendelea kuwalipa fidia wananchi watakaopitiwa na mradi wa usafirishaji umeme wa msongo wa kV 400 kutoka Somanga Fungu  wilayani Kilwa hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

  Naibu Waziri alitoa maagizo hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na Wawakilishi wa wananchi watakaopitiwa na mradi huo, Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Benki ya Maendeleo ya TIB.

  Kikao hicho kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini kililenga katika kuweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa fidia hiyo pamoja na kuunda Kamati itakayofuatilia utekelezaji wa malipo kwa wananchi watakaopitiwa na mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO. Hii ni baada ya kuonekana kuwa ulipaji wa malipo hayo ulikuwa ukisuasua na hivyo wananchi kuilalamikia Serikali.

  Naibu Waziri alisema kuwa jumla ya fedha inayopaswa kulipwa kwa wananchi hao katika wilaya za Temeke, Mkuranga, Kilwa,  Ilala na Kinondoni ni shilingi bilioni 79 na kwamba mpaka sasa Serikali imeshalipa shilingi bilioni 32.7 na kiasi kilichobaki ni shilingi 46.3.

  Hivyo katika kiasi hicho kilichobaki cha shilingi bilioni 46.3, Naibu Waziri aliziagiza TANESCO  na TIB kupunguza deni hilo kwa kuanza kuwalipa shilingi bilioni 7.3, Wananchi wa Kivule na Rufiji ambao watapitiwa na mradi  huo ambapo fedha zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 17 mwezi huu na ukomo wake ni tarehe 22 Septemba mwaka huu.

  " Hivyo nimewaelekeza TANESCO na TIB kuanza kulipa malipo hayo Tarehe 17 mwezi huu ambapo wataanza kulipa shilingi bilioni 1. 9, hilo ndio elekezo la kwanza na awamu ya kwanza," alisema Dkt. Kalemani.

  Alisema kuwa malipo mengine yatafanyika  tarehe 27 mwezi huu ambapo Taasisi hizo zitalipa shilingi bilioni 1.03 kwa wananchi, tarehe 8 mwezi wa 9 mwaka huu Taasisi hizo zitalipa shilingi  bilioni 1.60 na tarehe 15 mwezi wa Tisa zitalipa shilingi  bilioni 1.53 ambapo malipo ya mwisho kufanyika  ni tarehe 22 Septemba mwaka huu pale ambapo Taasisi hizo zitalipa shilingi bilioni 1.2  na hivyo watu wa Kivule na Rufiji watakuwa wamekamilika. 

  Dkt Kalemani aliongeza kuwa baada ya Awamu ya Kwanza ya malipo kukamilika mwezi Septemba mwaka huu,  malipo hayo ya fidia yataendelea kufanyika katika sehemu nyingine zenye madai hayo huku lengo likiwa ni kumaliza madai husika  mwezi Oktoba mwaka huu.

  Kuhusu uundaji wa Kamati ya kufuatilia malipo hayo ya fidia, Dkt. Kalemani alipendekeza Mwenyekiti wa Kamati hiyo atoke upande wa wananchi watakaopitiwa na mradi huo ili kufuatilia kwa karibu malipo hayo kwa wananchi, ambapo pendekezo hilo liliridhiwa na Wawakilishi  wa wananchi pamoja na Watendaji wa Serikali.

  Katika kikao hicho, Wawakilishi hao wa wananchi walimchagua Ndugu Josephat Haule kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo huku Katibu wa Kamati akitoka Wizara ya Nishati na Madini. Wajumbe wa Kamati hiyo wanatoka upande wa Wananchi, TANESCO, TIB na Wizara ya Nishati na Madini.
  Aidha, Naibu Waziri alitoa angalizo kuwa, mwananchi yeyote atakayewasilisha madai ya uongo au kuweka majina hewa ili alipwe fidia  atachukuliwa hatua kali za kisheria. 

  Aidha kwa nyakati tofauti Wawakilishi hao wa wananchi walimpongeza Naibu Waziri kwa kuamua kulivalia njuga suala hilo  ili kuwezesha mradi huo kutekelezeka kwa ufanisi na kuhakikisha wananchi wanapata haki yao.
  Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Innocent Luoga, alisema kuwa,  kukamilika kwa ulipaji wa fidia kwa wananchi hao kutawezesha kuanza kwa ujenzi wa njia hiyo ya kusafirisha umeme wa  msongo wa kV 400.

  Alisema kuwa umeme utakaosafirishwa  na miundombinu hiyo utatoka katika mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia itakayojengwa na kampuni ya Kilwa Energy katika eneo la Somanga wilayani Kilwa ambapo mitambo hiyo  itazalisha umeme wa kiasi cha megawati 320.
  Vilevile alisema kuwa Serikali ilichukua jukumu la kulipa fidia hiyo kwa wananchi mwaka 2015, hivyo  baada ya tathmini kukamilika,  fedha hizo zimeanza kulipwa na Serikali mwaka huu  kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB.

older | 1 | .... | 1315 | 1316 | (Page 1317) | 1318 | 1319 | .... | 3272 | newer