Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA SOKO LA MWANJELWA MKOANI MBEA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya Agost9, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili wenye soko kuu la kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya kulikagua
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 9, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kutembelea soko jipya la kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya, Agosti 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Uwajibikaji: JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

$
0
0
 Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane. Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau
Mkufunzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo 

akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.

Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura.
Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA ZIARANI MKOA WA KIGOMA

$
0
0
Na Abel Daud wa Globu ya Jamii, Kigoma

Waziri wa Mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba ameutaka Mkoa wa Kigoma kuendelea kukusanya silaha haramu zinazoingia nchini na kufanya shughuli za kihalifu.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma pamoja na maofisa mbalimbali wa Mkoani hapa katika ziara aliyoifanya hii leo ambayo inatarajiwa kumalizika hiyo kesho.
Akisoma taarifa kwa Waziri Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw.Samson Anga,amesema mwenendo wa uingiaji wa wakimbizi Mkoania hapa si mkubwa ukilinganisha na wastani wa wakimbizi 300 kwa siku waliokuwa wakiingia hapo awali mpaka kufikia wastani wa wakimbizi 220 wanaoingia hivi sasa kwa siku.
Anga ameendelea kusema kuwa kwa sasa kuna wakimbizi wapatao 23826 mkoni hapa,hata hivyo amesema ujio wa wakimbizi Mkoani hapa umekuwa ukiathiri mazingira kwa kiasi kikubwa hasa miti imekuwa ikikatwa ovyo kwa ajili ya matumizi ya kuni katka vijiji  jirani na kambi hizo.
Waziri Nchemba amesema taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ni Mkuu wa Wilayaa ya Kigoma Bw.Samson Anga jitihada zinazoendelea
kufanyika kukamata siraha haramu zinapaswa kuendelea kwa kuwa madhara yaletwayo na siraha hizo ni makubwa mno.

 Waziri Chemba akilakiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na baadhi ya maofisa
 Mh.Nchemba akisalimiana na Mkuu wa Takukuru mkoani Kigoma
 Maafisa wa polisi wakimsikiliza Waziri Nchemba
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kgoma Bw.Samson Anga akisoma taarifa fupi
Mhe. Nchemba Akizungumza na Kamati ya ulinzi na usala pamoja na maofisa wa serikali wa mkoa

Kennedy Uzoka Assumes Office as UBA GMD/CEO

$
0
0
Kennedy Uzoka has assumed as the Group Managing Director and CEO of pan-African banking group, United Bank for Africa (UBA) Plc.  
This follows the retirement of Phillips Oduoza as Group Managing Director and CEO of UBA Plc on July 31, 2016 after completing two terms of three years each.
Uzoka, the new GMD/CEO of UBA Plc, was until his appointment, the Deputy Managing Director, a position he has held in the last six years, working closely with the former GMD/CEO. His appointment as the new GMD is seen as a testimony to the strength of the bank’s succession planning process.
“Kennedy Uzoka’s is not only   very hard working, but he is also a man of impeccable integrity. He is passionate and committed to UBA. The board is confident that he will take the bank to the next level”   said Tony Elumelu, Chairman, UBA Plc.
Kennedy Uzoka comes well prepared for his new position. He has been leading the transformation agenda of the Bank, after returning from completing the Advanced Management Programme of Harvard Business School.
Uzoka has over two and a half decades of experience in commercial banking, strategy and business transformation. Prior to his sabbatical at Harvard, Uzoka served as Deputy Managing Director, UBA Group and was also the CEO of UBA Africa, responsible for the Group’s operations in 18 countries across Africa as well as business in New York and London.
“Uzoka brings an extremely strong skill set and a breadth of financial services experience that will help the bank execute the next phase of its growth strategy.” said Elumelu.
Speaking to staff in a video podcast after resuming on August 1, the new GMD/CEO, Uzoka who described UBA as a strong, recognizable and trusted brand across Africa, promised to build a bank based on a strong foundation of customer service.
“We will stay close to our customers and do everything possible to serve them properly. Our customers will be the beginning, the middle and the end of our strategy" he stated.
United Bank for Africa (UBA) Plc, is one of Africa's leading banking Groups with operations in 19 African countries and offices in three global financial centers: London, Paris and New York.
It is a publicly quoted company listed on the Nigerian Stock Exchange (NSE) and has a well diversified shareholder base. For more information visit www.ubagroup.com

Waziri mkuu Kassim Majaliwa azindua Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Mkoani Mbeya

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (kushoto) alipowasili katika banda la Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya. Katikati ni Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili
 Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (wapili kulia) akitambulisha baadhi ya wajumbe wa TAJATI kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alipowasili katika banda la Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale jana Jijini Mbeya kwa ajili ya kuzindua chama hicho
 Mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili (kushoto) akimuonyesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa picha yenye sura ya kufanana naye iliyochorwa na mmoja wa wanachama wa TAJATI baada ya kuzindua chama hicho jana Jijini Mbeya katika viwanja vya Nanenane John Mwakangale. Katikati ni mke wa Waziri Mkuu mama Mary Majaliwa. Picha zaidi BOFYAHAPA

MAKATIBU WAKUU WATEMBELEA KITUO MAHIRI CHA KUTUNZA KUMBUKUMBU (INTERNET DATA CENTRE) KIJITONYAMA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo akitoa maelezo ya kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (internet Data Centre) kwa Makatibu Wakuu hawapo pichani walipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Kijitonyama DSM. 
Afisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw. Suleimani Kagobe  akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu jinsi mfumo wa umeme unavyofanya kazi walipotembelea katika kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu kilichopo eneo la Kijitonyama DSM. 
Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila   katikati akitoa   maoni  yake kuhusu  kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu “ internet Data Centre”,  (wa kwanza kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri walipokitembelea kituo hicho eneo la Kijitonyama DSM. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano .

KUTOKA MAKTABA AUGUST 16, 2011: Muasisi wa Bongo Fleva Saleh Jabir

SERIKALI IMEJIPANGA KUONDOA MSONGAMANO KATIKATI YA JIJI -PROFESA MBARAWA

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mijini kwa Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa gari moshi litalofanya safari zake kuanzia Stesheni ya Dar es salaam hadi Pugu. Amessema kuwa kuanza kwa usafiri huo umepunguza daladala 45.
Amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha inapungaza kama sio kumaliza kabisa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. 

 Profesa Mbarawa amesema kuwa katika hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa njia ya boti katika baadhi ya maeneo na wataalam walishafanya kazi hiyo.
Aidha amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya na watakaofanya hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na kufisadi mali za reli.
Hata hivyo amesema waliojenga katika miundombinu ya reli wanatakiwa kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba hizo katika miundombinu hiyo ni kosa kisheria .Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es Salaam kuwa wataondokana na foleni kutokana na jitihada mbalimbali.
Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa malori ya mafuta ambapo mafuta yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Chalinze na kuanza kwa safari ya mikoani. Meya wa Jiji, Isaya Mwita amewataka wananchi kutumia usafiri huo kutokana na kutokwa na foleni na gharama yake kuwa nafuu.
Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kwa usafiri huo wameanza kutokana na nguvu ya serikali kuwa karibu katika utoaji wa huduma ya usafiri huo.

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipanda katika gari moshi ambalo safari zake zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari moshi uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Safari inaendelea.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).


YALIYOANDIKWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 10

SOMO LA SHERIA: MALI ILIYOPATIKANA KABLA YA NDOA

$
0
0
Na Bashir Yakub.

Mara kadhaa linapoibuka suala la kugawana mali pale ndoa inapohesabika kushindikana masuala kadhaa ya msingi na yanayohitaji uelewa huwa yanaibuka.

Moja ya suala kati ya masuala ambayo huibuka ni hili la kutenganisha na kufafanua hadhi ya mali za wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika kwa haki. Yawezekana mwanandoa akadhani ana haki katika mali fulani lakini kumbe kisheria hana haki hiyo ni mtazamo wake ndio unamsukuma kuamini hivyo.

Halikadhalika yawezekana mwanandoa kudhani hana haki katika mali fulani kumbe anayo haki. Ili kujua una haki ipi katika mali ipi na huna haki katika mali ipi yahitajika kujua misingi ya kisheria inayotumika kugawanya mali za wanandoa.

1.KUGAWANA MALI ZA WANANDOA.

Ieleweke kuwa tunapoongelea wanandoa kugawana mali tunaongelea talaka. Hakuna kugawana mali bila talaka. Na kisheria talaka inapotoka tu swali linalofuata ni habari ya mali na watoto kama wapo. Mali si lazima magari na manyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo vitanda, makabati, sahani n,k nazo ni mali kwa mujibu wa sheria. Navyo huhitaji mgao.

2. JE KUGAWANA MALI NI NUSU KWA NUSU ?.

Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika kugawa ni ule wa nusu kwa nusu. Jambo hili si kweli kwakuwa sheria ya ndoa 1971 iliyofanyiwa marekebisho 2002 haisemi kuwa utaratibu wa kugawana mali ni nusu kwa nusu. Sheria hii imeweka msingi mkuu wa kugawana mali ambao ndio hutumika katika mahakama zetu katika kutoa maagizo ya kugawa mali za wanandoa.

Msingi uliowekwa na sheria ni msingi wa kiwango cha mchango wa mwanandoa katika kupatikana kwa mali husika. Kiwango alichochangia mwanandoa katika kupatikana kwa mali hiyo ndicho kitakachokadiriwa na kiwango hicho ndicho atakachopewa.

Kwa hiyo kama ni nyumba ya vyumba sita mmoja anaweza kupata chumba kimoja na mwingine akapata vitano kutegemea na mchango wake. Na mchango hapa sio leta ni lete. Mchango sio hela tu hata kazi za nyumbani anazofanya mama wa nyumbani ambaye haleti hela nazo huitwa mchango ambapo hukadiriwa na kupata kile anachostahili.

3. MALI KABLA YA NDOA NA BAADA YA NDOA.

Katika kutenganisha mali za wanandoa huwa zinatenganishwa katika makundi makuu matatu. Kwanza kuna mali ambazo mtu alikuwa nazo kabla ya ndoa na wakati anaingia katika ndoa ameingia nazo. Kwa mfano mwanamke ameolewa akamkuta mwanaume tayari ana nyumba yake. Pili kuna mali ambazo zimepatikama wakati wawili wakiwa katika ndoa .

Kwa mfano ndoa imefungwa wawili wakaanza kuishi pamoja na taratibu wakaanza kujenga na kukamilisha. Na tatu ni mali ambazo zimepatikana katika ndoa lakini zikiwa hazina uhusiano wowote wa kindoa kwa mfano kurithi au kuzawadiwa mali. Tutaona hapa chini mazingatio ya sheria ya kila moja katika haya.

RC MASENZA AWAFARIJI YATIMA WA KITUO CHA FARAJA MGONGO KWA MISAADA YA MILIONI 7.2.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akimkabidhi msaada wa bati 100 pamoja na madawati 100 vyote vikiwa na thamani ya Tsh milioni 7.2 mkuu wa kituo cha Yatima cha Faraja Mgongo kata ya Nduli Manispaa ya Iringa Padri Franco Soloberi jana , mkuu huyo ametoa msaada huo kufuatia janga la moto lililoteketeza majengo ya kituo hicho mwezi uliopitaanayeshuhudia kushoto ni diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
Diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtoveakimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kutekeleza ahadi yake ya madawati na bati.
RC Iringa Amina Masenza akimkabidhi mkuu wa kituo cha yatima cha Faraja Mgogo Padri Franco Soloberi madawati 100 kulia ni diwani wa Nduli Bashir Mtove.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

GAZETI LA MSETO LAPEWA SIKU 7 KUMWOMBA RADHI NA KUMLIPA BILIONI MOJA NAIBU WAZIRI WA UJENZI.

$
0
0

Na Abushehe Nondo, Maelezo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Edwin Ngonyani amelitaka gazeti la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilingi bilioni moja kutokana na kuandika habari ya kumchafua.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake Waziri Ngonyani amesema kuwa Gazeti hilo la tarehe 4 Agosti 2016 liliandika habari yenye kichwa cha Habari “Waziri amchafua JPM” ikimuhusisha na upokeaji wa fedha kutoka moja ya Kampuni ya Madini wakati akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

“Nimewaandikia notisi ya siku saba ikiwataka waombe radhi na kunilipa fidia, na wasipofanya hivyo hatua stahiki kuwapeleka mahakamani akiwemo Mwandishi Josephat Isango, Mwanahalishi Publisher na Mchapaji wa gazeti hilo”. Alisema Mhandisi Ngonyani.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa habari hiyo siyo ya kweli na mwandishi ametumia nyaraka za kughushi ikiwemo barua iliyoandikwa tarehe 24 Julai  na kutiwa saini yake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO wakati ukweli ni kwamba tarehe hiyo yeye alikuwa ni Mkurugenzi kamili na siyo Kaimu kama barua hiyo inavyosomeka.

Ameongeza kuwa habari hiyo imewachafua watu wengi ikiwemo familia yake, wapiga kura wake wa jimbo la Namtumbo ambao walijitoa katika kumsaidia wakati wa kampeni na hali kadhalika zimemchafua Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumhusisha na fedha kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwaahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli alishasema kama kuna mfanyabiashara yeyote aliyechangia kuingia kwake ikulu ajitokeze na hakuna aliyefanya hivyo, Iweje leo mtu tu anaibuka na kuandika habari za kugushi? ”. Aliongeza.

Aidha Naibu Waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa waangalifu pindi wanapoandika habari za kutunga kwa kutotumia majina halisi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kanuni za uandishi wa hadithi (Habari za kutunga).

“Waandishi wa habari mnatakiwa kufuata maadili ya kazi yenu kwa kuandika habari zenye ukweli ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko na  migogoro isiyo ya lazima” Alisema Naibu waziri huyo.

DSTV WAZINDUA MSIMU MPYA WA SOKA BARANI ULAYA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande akimkabidhi mwandishi wa habari wa Kituo cha TBC Evance Mhando dekoda ya DSTV leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka barani Ulaya leo Jijini Dar es salaam, kulia ni Meneja Uendeshaji Ronald Baraka Shelukindo na kushoto ni Afisa Masoko Furaha Samalu.

Baadhi ya wadau wa michezo wakimsikiliza 
Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia kisimbuzi cha DSTV kimezindua msimu mpya wa soka barani Ulaya huku kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza ikitangazwa kwa lugha ya kiswahili. Msimu huo mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 13 unat anatarajiwa kuwa wa kipekee hasa baada ya kupunguza bei kwa watumiaji wapya ambapo watapata kwa dekoda kwa shilingi 79,000.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwaka mpya wa Soka, Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande amesema kuwa msimu huu mpya utakuwa ni wa kipekee sana kwani kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza itakuwa inatangazwa kwa kiswahili ambapo watanzania wataweza kuelewa vizuri sana na hii itakuwa ni muendelezo kama ilivyo ligi ya Hispania.

Chande amesema kuwa watu mwaka huu watapata na nafasi ya kuangalia burudani ya mpira na takribani mechi 300 zitakazonyeshwa moja kwa moja ambapo SuperSport wataonyesha kupifia chaneli za SS3, SS5, SS6, SS7 na SS11 kwa ligi kuu ya Uingereza huku ligi ya Hispania ikiwa ikionyeshwa kupitia kifurushi cha DSTV Compact.

Meneja Mauzo wa Multichoice, Baraka Shelukindo amesema kuwa mbali na kupungua kwa bei hiyo, channeli zimeingizwa katika kifurushi cha 84,000 na pia kwa sasa wapo kwenye mikakati ya kuandaa application mpya ya ya SuperSport ambazo zitakuwa na live Streaming pamoja na video zilizojiri za kuvutia.

Katika uzinduzi huo DSTV walichezesha droo na kuwapatia dekoda waandishi wanne wa habari.

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSHONA NGUO CHA TOOKU JIJINI DAR.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agosti 10, 2016.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Adelhem Meru na wapili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agosti 10, 2016.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Adelhem Meru na wapili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kutembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kushona nguo cha  Tooku kilichopo eneo la EPZ,Mabibo External jijini Dar es salaam baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza, Agosti 10,2016.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhem Meru na kulia kwake ni Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TANZIA: UPDATES ZA MSIBA WA MTANZANIA MWENZETU ALIYEFARIKI HUKO NCHINI DENMARK

$
0
0
Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli a.k.a Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +61283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze  kuhudhuria mazishi yake.

BREAKING NEWZZZZZZ.... NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA AMEMSIMAMISHA KAZI MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII MKOANI SIMIYU.

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bunamhala, Bw. Ramadhani Said kilichopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, kutokana na utendaji usioridhisha na kumteua Bi. Levina Mrema kushikilia wadhifa huo.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bi. Levina Mrema (kulia) aliyemteua wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja  Mkoani Simiyu.
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Bunamhala Ramadhani Saidi (Aliyesimama) akitoa maelezo juu ya chuo hicho kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (hayupo pichani) wakati wa ziara yake.

WAFANYABIASHARA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAWASILIANO NAFUU.

$
0
0
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu kushoto) akibofya kitufe cha kompyuta kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya kampuni ya Vodacom Tanzania, inayowezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) kupata huduma mbalimbali za bei nafuu za mawasiliano zilizounganishwa pamoja katika kurahisisha biashara ikiwemo huduma za data, huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu, simu za ofisini na huduma nyinginezo za mifumo ya usalama wa vifaa vya ofisi, akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kulia) Afisa Mkuu wa Idara ya Uendelezaji wa biashara kimtandao wa kampuni hiyo,Gregory Bond(wapili kushoto) na Mkuu wa kitengo cha wafanyabiashara wadogo na wakati wa kampuni hiyo,Aileena Meena. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa huduma mpya ya Vodacom Tanzania  inayowezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) kupata huduma mbalimbali za bei nafuu za mawasiliano zilizounganishwa pamoja katika kurahisisha biashara ikiwemo huduma za data ,huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu,simu za ofisini na huduma nyinginezo za mifumo ya usalama wa vifaa vya ofisi,Hafla hiyo amefanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (katikati)akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao (kulia) Afisa Mkuu wa Idara ya Uendelezaji wa biashara kimtandao wa kampuni hiyo,Gregory Bond (kushoto) baada ya kuzindua huduma mpya ya Vodacom Tanzania inayowezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) kupata huduma mbalimbali za bei nafuu za mawasiliano zilizounganishwa pamoja katika kurahisisha biashara ikiwemo huduma za data ,huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu,simu za ofisini na huduma nyinginezo za mifumo ya usalama wa vifaa vya ofisi.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Slaam leo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s)wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage(hayupo pichani)alipokuwa akizindua huduma mpya ya Vodacom Tanzania inayowezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) kupata huduma mbalimbali za bei nafuu za mawasiliano zilizounganishwa pamoja katika kurahisisha biashara ikiwemo huduma za data ,huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu,simu za ofisini na huduma nyinginezo za mifumo ya usalama wa vifaa vya ofisi.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Slaam leo.

MO BAJAIA WATUA, KUKIPIGA NA YANGA AGOSTI 13, 2016 UWANJA WA TAIFA

$
0
0
KIKOSI cha watu 35 ambao ni wachezaji na viongozi wa Timu ya MO Bajaia kutoka nchini Algeria, wametua Jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Agosti 9, 2016 na kufikia Hoteli ya Ledger Plaza, iliyoko Kunduchi Beach.

Timu hiyo imekuja kucheza na Young Africans ya Dar es Salaam, katika mchezo wa nne wa hatua ya Nane Bora kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaofanyika Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Licha ya kwamba Young Africans kuwa na pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi  A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja. Wakati Young Africans wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe.

Mchezo wa Young Africans dhidi ya Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.

Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11, 2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.

Kiingilio katika mchezo huo kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzungunguko kwa maana ya viti vya kijani, bluu na chungwa wakati Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu wa Waratibu wa Young Africans.

Kambi tiba ya GSM Foundation na MOI yazidi kuokoa maisha ya watoto

$
0
0
Jumla ya watoto 49 wameonwa na madaktari bingwa kutoka taasisi ya Mifupa, Ubongo na mishipa ya fahamu Muhimbili, wanaozunguka nchi nzima kutibu watoto waliozaliwa kwa tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi, katika kambi tiba inayodhaminiwa na GSM Foundation katika harakati za kuokoa maisha ya watoto hao, tatizo ambalo linasadikika kupoteza maisha ya watoto wengi zaidi nchini.

Kwa mujibu wa Kaimu kiongozi wa Kambi tiba hiyo ambayo leo imemaliza shughuli zake mkoani Ruvuma na sasa inaelekea Mkoani Mbeya, Dk Hamisi Shabani, kati ya watoto 49 walioingia maabara, ni wattoto 12 tu walioweza kufanyiwa upasuaji na hii inatokana na hali za kiafya walizokutwa nazo watoto hao.

Wataalam wanaoshiriki kambi tiba kutoka MOI na GSM Foundation wakiangalia picha za CT Scan kabla ya kuanza tiba mkoani Ruvuma.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002, jumla ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, lakini kati yao ni watoto 500 tu ndio wanaoweza kufika hospitalini na kupata tiba huku changamoto kubwa ikiwa ni hali ya kiuchumi na imani za kishirikina.

Utafiti unaeleza kwamba wazazi wengi wanaozaa watoto wenye vichwa vikubwa, huwaficha ndani au kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji wakiamini kwamba tatizo hilo ni la kishirikina,

Kiuhalisia, Tanzania ina madaktari bingwa 7 tu wenye uwezo wa kutibu watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, kati yao, sita wanafanya kazi Muhimbili Dar es Salaam, na mmoja anafanya kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bugando, jijini Mwanza.

Kambi tiba ya GSM inayojumuisha madaktari wanne, manesi wanne na mabwana usingizi wawili kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya Muhimbili Dar es Salaam.
Dk Mwanaabasi (Aliyeshika Daftari) akimruhusu Mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji Tausi Kambona baada kuonekana kama anaendelea vizuri.
Dk John Mtei akimuangalia mtoto Mariam Juma Said, ambaye alifanyiwa upasuaji baada ya jopo kujiridhisha kwamba yuko tayari kwa tiba.
Maandalizi ya upasuaji yakiendelea katika maabara ya Hospitali kuu ya mkoa wa Rvuma.

MAKONDA AMUAGIZA MKURUGEZI WA JIJI KUHAMISHA KITUO CHA MABASI UBUNGO KWENDA MBEZI MWISHO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaka Mkurugenzi wa jiji kuanza  mchakato wa kuhamisha kituo kikuu cha mabasi ya mkoani cha ubungo  kuhamia Mbezi mwisho 

Makonda ameyasema hayo leo wakati alipotembelea  kituo hicho leo, amesema kituo hicho kimeelemewa na idadi ya kubwa ya wasafiri huku miundombinu haiendani na utoaji wa huduma kwa wasafiri wanaotumia kituo hicho.


Makonda  amesema kuwa baada ya kituo hicho kuhama panatakiwa kufanyika  uwekezaji wa soko kubwa  ili kupunguza msongamano wa watu katika soko la Kariakoo.

Aidha Makonda amesema kuwa uamuzi huo umetokana na kuonekana kwa kituo hicho kuwa kidogo na kushindwa kutoa huduma ya usafirishaji ya abiria wanaoingia na kutoka katika mikoa mbalimbali.


Makonda ameutaka uongozi wa kituo hicho  kufunga taa maeneo yote kutokana na kutawala kwa giza nyakati za  usiku,ambapo ni  hatari kwa usalama wa abiria  wanaoshuka  nyakati hizo.

RC Makonda pia amepiga marufuku kukamata magari kwa kigezo cha maegesho, wakati hakuna alama zinazoonyesha sehemu ya kuegesha magari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akitembelea Kituo kikuu Ubungo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na sehemu ya Wananchi waliokuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Ubungo, Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasalimia wananchi.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images